Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

    Report Post
    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 82
    1. #1
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Utangulizi


      Mtafiti mmoja kutoka Argentina, Boaventura Santos de Sousa, aliwahi kuandika kwamba ‘mwandishi ingawa huandika kuhusu yaliyopita huwa anajaribu kueleza yaliyopo, siyo yaliyopita. Lakini, kwa kufanya hivyo, huwa pia anajiweka mbali na hali ya sasa na kwa hakika anaandika kwa ajili ya siku zijazo’.


      Muungano wa Zanzibar na Tanganyika umepita katika masaiba kadhaa tokea kuasisiwa kwake takriban miaka 45 iliyopita lakini mtikisiko ulioukumba katika siku za karibuni ni mkubwa sana. Ni mkubwa kwa sababu umegusa kiini cha Muungano huu ambapo suala linaloulizwa ni iwapo kwa kule kukubali kushirikiana katika baadhi ya mambo, je, Zanzibar na Tanganyika zimejifuta na hivyo kupoteza hadhi zake kama nchi? Hilo limekuwa ndiyo suala kubwa linaloulizwa na Wazanzibari hasa baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutamka Bungeni kwamba Zanzibar si nchi.


      Hakuna awezaye kubisha kwamba tokea kuasisiwa kwake, Muungano huu umejengeka kutokana na misingi ya khofu, kutiliana shaka na kutokuaminiana baina ya pande mbili zinazouunda, ambako wakati mwengine kumepelekea hata kutishia uhai wa Muungano wenyewe.


      Muungano umekuwa gumzo kuu katika takriban kila mjadala wa katiba na siasa katika nchi yetu. Umejitokeza na kujionyesha hivyo katika mwaka wa mwanzo wa Muungano kuhusiana na sakata la kuwa na Ubalozi wa iliyokuwa

      Ujerumani Magharibi kwa upande wa Tanganyika na Ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwa upande wa Zanzibar, kuhusiana na uwakilishi wa Zanzibar katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na uanzishwaji wa Benki

      Kuu ya Tanzania (BOT) mwaka 1964 – 1966, wakati wa kuunganisha vyama vya ASP na TANU kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977, katika mjadala wa marekebisho ya Katiba wa 1983/84 na hatimaye kujiuzulu kwa

      Rais wa pili wa Zanzibar Sheikh Aboud Jumbe, wakati wa kuondolewa katika Uwaziri Kiongozi kwa mwandishi wa makala haya na hatimaye kufukuzwa katika CCM na wenzake 6 mwaka 1988, katika harakati za madai ya kutaka

      kura ya maoni kuhusiana na Muungano huo mwaka 1989/90, wakati wa mjadala wa kuanzishwa vyama vingi mwaka 1991, katika sakata la Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) mwaka 1993, wakati wa mjadala wa

      G-55 kudai kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano mwaka 1994, katika mjadala wa marekebisho ya 11 na 14 ya Katiba ya Muungano mwaka 1994/95, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 1995 na ule wa 2000 na karibuni kabisa kuhusiana na suala la matarajio ya ugunduzi wa mafuta visiwani Zanzibar na harakati za kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki.


      Ukiondoa kuibuka kwake katika mijadala mikubwa ya kikatiba na kisiasa nchini, kwa upande mwengine katika uendeshaji wa shughuli za Serikali za kila siku, ‘matatizo na vikwazo kadhaa ya kiutawala na kiutendaji’ vimekuwa vikiripotiwa kila mara kwamba vinakwamisha uimarishaji wa Muungano.


      Tume na Kamati kadhaa zimeundwa kuainisha matatizo ya Muungano na kupendekeza njia za kuyatatua. Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeunda Tume na Kamati zifuatazo, miongoni mwa nyingi, kuhusiana na masuala haya:



      1. Kamati ya Mtei
      2. Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991)
      3. Kamati ya Shellukindo (1994)
      4. Kamati ya Shellukindo 2 ya kuandaa Muafaka juu ya Mambo ya Muungano baina ya SMZ na SMT.
      5. Kamati ya Jaji Mark Bomani (1995)
      6. Kamati ya Jaji Robert Kisanga (1998)
      7. Kamati ya 'Harmonization'
      8. Kamati ya Masuala ya Simu (Kamati ya Kusila)



      Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) nayo kwa upande wake iliunda Kamati zifuatazo kwa madhumuni hayo hayo:



      1. Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992
      2. Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamuhuna) ya 1997
      3. Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti ya Jaji Kisanga (Kamati ya Salim Juma Othman)
      4. Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya Kero za Muungano (Kamati ya Ramia) ya 2000
      5. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya Sera ya Mambo ya Nje
      6. Kamati ya Rais ya Wataalamu juu ya Kero za Muungano ya 2001
      7. Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
      8. Kamati ya Mafuta
      9. Kamati ya Madeni baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania
      10. Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ)
      11. Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu
      12. Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996 –1999)
      13. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya matatizo na kero za Muungano na taratibu za kuyaondoa (2004)



      Ukiacha Tume, Kamati na Ripoti hizo, kuanzia mwaka 1985 kulianzishwa utaratibu wa Kamati ya Pamoja ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Waziri Kiongozi wa Zanzibar pamoja na Mawaziri wa Serikali zetu mbili ambao ulitarajiwa uwe ndiyo jukwaa la kuzungumzia matatizo kutoka kwa washiriki wakuu wa Muungano huu na kuyapatia ufumbuzi unaofaa. Utaratibu huu uliachwa kwa muda mrefu lakini sasa umerejeshwa upya kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa katika mkutano na mawaziri na watendaji wakuu wa Serikali yake huko Ngurdoto, Arusha mwezi Februari, 2006.


      Mikutano, Makongamano, Semina na Warsha vimefanywa kujadili masuala haya na kupendekeza hatua za kuchukuliwa. Wasomi na wanafunzi wamefanya tafiti kadhaa na kujipatia shahada na stashahada hadi ngazi ya Ph.D juu ya Muungano lakini bado matatizo yako pale pale na yanaongezeka kila kukicha.


      Yanayoonekana na kuelezwa kama matatizo, mapungufu, dosari, kasoro na, kwa msamiati wa sasa, kero yamekuwa ndiyo yale kwa yale. Nini basi kiini cha haya? Na vipi tutayatatua?


      Mimi nimeamua kutoa changamoto kupitia waraka huu kwa kuitazama historia ya Muungano, jinsi ulivyoundwa, matatizo yanayoukabili, nafasi na hadhi ya Zanzibar katika Muungano na nini khatima ya Zanzibar na mustakbali wa Muungano huko tuendako. Nitakayoyaeleza yanaweza yakaonekana ni machungu kwa wakati huu wa sasa lakini kama asemavyo Santos de Sousa yanaweza yakawa ndiyo ufumbuzi kwa siku zijazo.




      Asili na Sababu za Muungano


      Maoni yanayotolewa kuhusu asili na sababu za Muungano yamekuwa yakitofautiana mno. Wapo wanaouleza Muungano huu kuwa ni wa pekee katika bara la Afrika, kwani ndiyo pekee ulioweza kudumu katika kutimiza azma na malengo ya kuleta umoja wa Afrika (Pan-Africanism),[2] na pia wapo wanauona kuwa ni ‘jaribio la kusisimia la ukoloni mdogo wa nchi moja ya Kiafrika kuiteka na kuitawala nchi nyengine ya Kiafrika.’[3]


      Kutokana na maelezo na hoja nyingi na zinazokinzana kuhusu asili na sababu za Muungano, si rahisi kusema moja kwa moja kuwa maelezo yepi au hoja ipi ni sahihi. Utangulizi (Preamble) wa Mkataba wa Muungano wenyewe unataja sababu kuu ya kuunganisha nchi za Zanzibar na Tanganyika kuwa ni ‘maingiliano ya muda mrefu ya watu wa nchi mbili hizi na mahusiano yao ya kidugu na kirafiki … na … kuendeleza umoja wa watu wa Afrika.’ Lakini miaka 45 sasa baada ya uzoefu wa Muungano huu, Wazanzibari wanajiuliza kweli haya ndiyo madhumuni ya Muungano huu?


      Wazo la kuungana linaweza kurudishwa nyuma tokea zama za harakati za ukombozi wa nchi za Afrika. Waasisi na wakuu wa harakati za kupigania Uhuru waliiona mipaka ya nchi zao iliyowekwa na wakoloni kuwa ni ‘mbinu za kibeberu’ zilizotekelezwa kwa ajili ya manufaa na maslahi yao. Kutokana na hisia hizo, mazungumzo ya kuanzisha aina fulani ya umoja miongoni mwa nchi huru za Afrika yalitawala duru za siasa katika miaka ya 5o na 60.


      Nadharia mbili zilijichomoza. Ya kwanza, ikishadidiwa na Kwame Nkrumah wa Ghana, ilikuwa ikitaka kuasisiwa kwa nchi moja tu ya Afrika nzima iliyoungana ikiwa na Serikali moja kwa bara zima. Nadharia hii ilipingwa na baadhi ya viongozi, wakiongozwa na Julius Nyerere waTanganyika, ambao walisisitiza haja ya kuanza na miungano ya maeneo (regional unions) chini ya mfumo wa Shirikisho badala ya kuwa na mpango wa Serikali moja.[4]


      Katika kulifikia lengo hilo, viongozi wa kisiasa wa nchi tatu za Afrika Mashariki – Kenya, Ugandana Tanganyika – walikuwa wakifanya mikutano ya mara kwa mara kipindi chote cha kati ya mwaka 1961 na 1963 kuona jinsi gani wanaweza kutimiza ndoto hiyo. Mfumo wa Muungano uliokuwa ukiandaliwa ulikuwa ni ule wa Shirikisho. Tamko la Pamoja la viongozi hao lilisema:


      “Sisi, viongozi wa wananchi na Serikali za nchi za Afrika Mashariki … tunayakinisha nia zetu kuhusu kuwepo kwa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki. Mkutano wetu wa leo unasukumwa na hisia za umoja wa Afrika (Pan-Africanism), na siyo tamaa za maslahi binafsi ya eneo hili. … Ijapokuwa Zanzibar haikuwakilishwa katika mkutano huu, tunapaaswa kuweka bayana kwamba nchi hiyo inakaribishwa kushiriki kikamilifu katika mikutano yetu kwa ajili ya uundwaji wa Shirikisho .”[5]


      Lakini Umoja wa Afrika (Pan-Africanism) hauonekani kuwa ndiyo dhamira pekee au kama ndiyo dhamira halisi ya Muungano. Wengi wanaamini, na mimi nikiwa mmoja wao, kwamba dhana hiyo ilitumiwa tu kuficha njama za muda mrefu za Nyerere kutaka kuimeza na kuitawalaZanzibar. Katika mwaka 1961, wakati Tanganyika inakaribia kupata Uhuru wake, Nyerere alinukuliwa akisema:


      “If I could tow that island [Zanzibar] out in the middle of the Indian Ocean, I would do it … I fear it will be a very big headache for me.”[6]


      Yaani, “Kama ningekuwa na uwezo wa kuvikokota visiwa vile [Zanzibar] na kuvitupa nje kabisa, katikati ya Bahari ya Hindi, basi ningefanya hivyo … Nakhofia vitakuja kuniumiza kichwa sana”.


      Imani hii inatiliwa nguvu na mahusiano ya karibu na ya muda mrefu yaliyokuwepo kati ya chama kilichokuwa kikitawala Tanganyika, TANU, na ASP ambacho kilishika hatamu za utawala baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964, mwezi mmoja tu baada ya Zanzibar kupata uhuru wake kutoka Uingereza hapo Desemba 10, 1963. Zilikuwepo taarifa tokea mwaka 1959 kwamba TANU na ASP zitakaposhika madaraka zitaziunganisha nchi mbili hizi kuwa Jamhuri moja.


      Wakati juhudi za kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki zikiwa zinafifia, Nyerere aliona fursaZanzibar ambayo hakutaka kuipoteza. Katika mazungumzo ya siri kati yake na Rais Abeid Amani Karume wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wakakubaliana kuziunganisha nchi mbili hizi. Hakukuwa na ushirikishwaji wa aina yoyote ule wa wananchi wa nchi hizi mbili katika maamuzi haya makubwa. Usiri uliogubika hatua hii kubwa unafichuliwa na si mwengine bali Nyerere mwenyewe pale aliposema:


      “[Tanganyika] tulipeleka polisi wetu Zanzibar. Baada ya kuyashinda matatizo kadhaa tukaungana. Sisi wenyewe kwa khiyari zetu tulikubaliana kuungana. Karume na mimi tulikutana. Peke yetu wawili tu tulikutana. Nilipomtajia wazo la Muungano, Karume hakufikiri hata mara mbili. Pale pale alinitaka kuita mkutano wa waandishi wa habari kutangaza azma yetu. Nilimshauri asubiri kidogo kwani ilikuwa bado ni mapema mno kuweza kuviarifu vyombo vya habari.”[7]


      Taarifa hizi ziliendelea kubaki kuwa siri hadi tarehe 26 Aprili, 1964 pale Redio ya Tanganyika ilipotangaza kwamba siku hiyo Marais wawili hao watakutana katika Bunge la Tanganyika kubadilishana Hati za Muungano ambazo zimeunganisha Zanzibar na Tanganyika kuwa Jamhuri moja. Hivyo inaonekana wazi kwamba tokea awali Muungano huu ulikosa ridhaa ya watu. Haukuwa Muungano wa watu, ulioundwa na watu, kwa maslahi ya watu. Bali ulikuwa na umeendelea kuwa ni Muungano uliosimamishwa kwa ridhaa ya watawala pekee.




      Kiini cha matatizo ya Muungano


      Ukitazama kwa jicho la sheria, kiini cha matatizo ya Muungano kinatokana na tafsiri ya Mkataba wa Muungano (Articles of Union) wa 1964. Hizi ndizo hati zinazounda, kupitia mkataba wa kimataifa, Jamhuri ya Muungano. Suala kubwa lililoumiza na linaloendelea kuumiza vichwa vya wengi na hivyo kuendelea kuulizwa ni mfumo gani wa Muungano ulikusudiwa kuwekwa na Mkataba huu? Ni muungano wa moja kwa moja (unitary) au wa shirikisho (federal)?


      Mfumo uliopo sasa ambao ulianza kutekelezwa 1964 ni ule wa serikali mbili – ile ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar. Tanganyika haikuwekewa serikali yake tofauti; madaraka yake kwa yale mambo yasiyo ya Muungano yalielezwa kwamba yatasimamiwa na kuendeshwa na Serikali hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, uhalali wa kisheria wa muundo huu umeendelea kuhojiwa na hata kupingwa kwamba hauwakilishi ipasavyo makusudio yaliyomo katika Mkataba ulioanzisha Muungano wenyewe.


      Mkataba wa Muungano wenyewe hauelezi bayana aina au mfumo wa muungano inaouanzisha lakini uko wazi kuhusiana na mgawanyo wa madaraka (distribution of power) inaouweka na idadi ya mamlaka (number of jurisdictions) zitakazokuwepo. Ibara ya (iii) (a) ya Mkataba huo inaanzisha ‘Bunge na Mamlaka ya Utendaji’ (Parliament and Executive) ndani ya na kwa ajili yaZanzibar ikiwa na mamlaka kamili kuhusiana na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwaZanzibar. Kwa upande mwengine, Ibara ya (iv) ya Mkataba huo inaanzisha ‘Bunge na Mamlaka ya Utendaji’ (Parliament and Executive) ya Jamhuri ya Muungano ikiwa na mamlaka kamili katika eneo lote la Jamhuri ya Muungano kuhusiana na mambo ya Muungano na, pia, ikiwa na mamlaka kamili ndani ya, na kwa ajili ya Tanganyika kuhusiana na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwa Tanganyika. Kwa hivyo, katika sehemu ya pili, mamlaka mbili tofauti zimechanganywa pamoja.


      Mjadala mkubwa na mkali umekuja kuhusiana na tafsiri ya Ibara hiyo ya (iv) na kule kuchanganya kwake mamlaka mbili hizo.


      Haya si masuala ya kisheria tu kama ambavyo baadhi yetu wanataka tuamini (ingawa nayo ni muhimu mno kama ilivyodhihirika hivi karibuni), bali pia ni masuala ya kisiasa kwa vile yanahusisha uwezo wa maamuzi, madaraka na mamlaka, na zaidi mchango wa gharama za uendeshaji na mgawanyo wa rasilimali na mapato kati ya wahusika wakuu. Mambo haya, katika uzoefu wa nchi za wenzetu, ndiyo yaliyopelekea kuvunjika kwa miungano yao kwani huzaa kutiliana shaka na kutokuaminiana. Kwa vile yanachukua sura ya kisiasa (kutokana na sababu nilizozitaja), haya hayana chama wala itikadi kama nitakavyoonyesha huko mbele. Kamaalivyowahi kusema Prof. Issa Shivji:


      “Ultimately, the question of the Union is primarily a political question and no amount of rhetoric about blood and cultural ties will matter when it comes to realpolitik.”[8]


      Yaani, “Mwisho wa yote, suala la Muungano linabakia kimsingi kuwa ni suala la kisiasa, na inapofikia kwenye siasa hasa, hotuba na kauli kali za jazba kuhusiana na mahusiano ya damu na ya kidugu, zote hazitafaa kitu.”


      Kwa hakika, kinyume na inavyojaribiwa kuonyeshwa na wengi kwamba Tanganyika imepoteza kila kitu katika muundo huu wakati Zanzibar imekabidhi sehemu tu ya madaraka yake, muundo wa Serikali mbili umepelekea wengi

      kuamini kwamba kilichofanyika ni kiini macho tu kwani ni Zanzibar iliyokabidhi sehemu muhimu ya mamlaka yake (mahusiano ya nchi za nje, ulinzi na usalama, uraia, kodi na ushuru, sarafu, nguvu kuu za kuendeshea uchumi na

      mengineyo) kwa Tanganyika na kisha Tanganyika ikajigeuza jina na kujiita Jamhuri ya Muungano. Na haya si maoni ya ngumbaru (kwa lugha ya Mwalimu Julius Nyerere) bali ni maoni ya watu wazito wakiwemo aliyekuwa Spika wa

      Bunge na ambaye sasa ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa ambaye alisema kwa jinsi mambo yalivyofanyika, Zanzibar inaonekana kama vile ni‘invited guest’ (mgeni aliyealikwa) katika Muungano.[9] Naye

      msomi mashuhuri ulimwenguni, Prof. Ali Mazrui alisema baada ya Muungano Zanzibar imepoteza kila kitu muhimu wakatiTanganyika imebadilika jina tu na kuwa Tanzania huku ikiwa na mamlaka zaidi lakini ikibaki na Rais wake, nembo yake ya Taifa, wimbo wake wa Taifa na hata kiti chake katika Umoja wa Mataifa.[10]




      Mkataba wa Muungano haujafuta Serikali ya Tanganyika


      Katika makubaliano ya kimataifa yaliyounda Muungano, ambayo hata hivyo katika muda wote wa uhai wa Muungano yamekuwa hayafuatwi, hakuna kifungu hata kimoja kilichotoa au kuagiza kwamba Serikali ya Tanganyika ifutwe kwa

      mujibu wa makubaliano hayo. Serikali ya Tanganyika, kama ilivyo ile ya Zanzibar, imelindwa na kifungu cha (v) kinachosomeka kwamba: “The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories”.Kinachosemwa hapa ni kwamba “Sheria zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kufanya kazi na kuwa na nguvu katika maeneo yao.”


      Wataalamu wa katiba na sheria wanafahamu kwamba katiba ndio sheria mama ya sheria zote za nchi. Hivyo Katiba ya Tanganyika imelindwa na inapaswa kuwepo na Serikali yake iwepo, pamoja na viongozi wake kuwepo na

      kusimamia mambo yasiyo ya Muungano. Katiba na sheria zaTanganyika ndizo zilizotakiwa zitumike katika eneo la Tanganyika kwa yale mambo yaliyokuwa hayamo kwenye Muungano kama ambavyo Katiba (au kabla ya hapo Matangazo ya Kikatiba –Constitutional Decrees) na sheria za Zanzibar zinavyotumika katika eneo la Zanzibar kwa yale mambo ambayo si ya Muungano. Hiyo ndio tafsiri ya ‘maeneo yao’.


      Wazanzibari wanafahamu kwamba Serikali ya Tanganyika imefutwa kwa makusudi na Bunge laTanganyika kinyume na Makubaliano ya Muungano ili kujipa nafasi kuitumia Serikali ya Muungano, kama kwamba ndio Serikali ya Tanganyika. Lengo ni hatimaye kuiuwa Serikali yaZanzibar na kufanya Tanganyika mpya ikiwa na jina jipya la Tanzania lenye mipaka mipya, yaani kuwa nchi moja yenye Serikali Moja.


      Hiyo ndio ghilba iliyofanywa na viongozi wa Tanganyika mara baada ya kuwekwa saini makubaliano. Kwa kusaidia kufichuwa ukweli wa hadaa hii, msomaji anashauriwa asome Sheria Na. 22 ya mwaka 1964 inayoitwa “Union of Tanganyika and Zanzibar Act, 1964.”


      Sheria hii ilipitishwa na Bunge la Tanganyika Aprili 25, 1964, siku moja kabla Muungano kuanza kufanya kazi. Ilikusudiwa kuthibisha kukubalika Muungano huo wa Tanganyika na Zanzibarupande wa Tanganyika (ratification). Kifungu cha (viii) cha Makubaliano ya Muunganokinaagiza ifanyike hivyo kwa pande zote mbili za Muungano.


      Inasikitisha kusoma katika kifungu Na. 2 cha sheria hiyo kwamba:


      “Existing law means the written and unwritten law as it exists immediately before Union Day but does not include the Constitution of Tanganyika in so far as it provides for the Government of the Republic of Tanganyika or any declaration or law or any provision which expires with effect from commencement of the Interim Constitution”.


      (“Sheria iliyopo maana yake ni sheria iliyoandikwa na isiyoandikwa kama ilivyo kabla tu ya siku ya Muungano lakini haijumuishi Katiba ya Tanganyika kwa mintaraf ya kuiweka kwake Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika au tamko, sheria au kifungu chochote ambacho kinafutika kwa kuanza kufanya kazi Katiba ya Muda (ya Muungano)).”


      Kwa hivyo, wakati Bunge la Tanganyika linapitisha sheria ya kuridhia, ratify, kuwepo kwa Muungano kwa upande wa Tanganyika, sheria hiyo ilianza kupinga vifungu vya makubaliano hayo. Mfano mwengine ni kifungu Na. 7 cha sheria hiyo kinachosema:


      “On the commencement of the Interim Constitution of the United Republic of Tanganyikaand Zanzibar, the Constitution of Tanganyika will cease to have effect for the Government of Tanganyika as a separate part of the United Republic”.


      (“Itapoanza kufanya kazi Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika naZanzibar, Katiba ya Tanganyika itasita kuwa na maana kwa Serikali ya Tanganyika kamasehemu moja ya Jamhuri ya Muungano.”)


      Kwa maneno mengine, sheria ambazo zilitakiwa zitumike kwa Tanganyika kwa mambo ambayo si ya Muungano zilipewa maana mpya kwamba eti zisijumuishe Katiba ya Tanganyika.


      Jambo moja lililo wazi, pamoja na hatua hii ya kuifuta Katiba ya Tanganyika, ni kwamba kule kuendelea kutambua kuwepo kwa sheria nyengine za Tanganyika bado kunamaanisha kuwepo kwa mamlaka ya Tanganyika ambako sheria hizo kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano ziliendelea na zinaendelea kutumika hadi leo.


      Zaidi, inapaswa ifahamike kwamba kufuta Katiba ya Tanganyika kulikofanywa na vifungu vya sheria hii hakukubadilisha makubaliano yaliyokwishatiwa saini kati ya Serikali mbili zilizounda Muungano, yaliyosema kwamba sheria za nchi mbili hizi zitaendelea kutumika katika maeneoyao. Bunge la Tanganyika, na hata hili la Muungano, halikuwa na mamlaka kutafsiri vifungu vya Mkataba wa Muungano.


      Utaratibu wa kisheria ni kwamba kama Mkataba ulitakiwa kutafsiriwa basi ni walioandika rasimu ya mkataba huo ndio walipaswa kutoa tafsiri ya vifungu vyake, tafsiri ambayo ingepaswa iwe sehemu ya Mkataba huo. Na wala makubaliano yale hayakufuta wadhifa wa Rais wa Tanganyika. Si hivyo tu, bali pia Katiba ya Muungano ambayo ilitakiwa iwe ya muda tu kwa mwaka mmoja(interim) ilikuwa ni ile ya Tanganyika iliyofanyiwa marekebisho kwa ajili ya kutumika kwa Serikali ya Muungano.


      Haikuruhusiwa kutumika kuiongoza Tanganyika kwa sababu Tanganyika ilikuwa na Katiba yake na Rais wake. Mwalimu Nyerere alikuwa na vyeo viwili, Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano na Katiba ya Muungano na Rais wa Tanganyika kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika, kama alivyokuwa Mzee Karume ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano na Katiba ya Muungano na akaendelea kubaki kuwa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa Tangazo la Katiba ya Zanzibar (Constitutional Decrees).


      Hivyo ndivyo makubaliano yalivyo hadi hii leo. Waliobadilika ni watu tu. Kufanya vyenginevyo ni kinyume na makubaliano yale na ndio sababu ya migogoro ya Muungano. Yaliyofanyika ni ujanja uliokuwa hauna nia njema kwa Zanzibar kama alivyosema Prof. Issa Shivji, mtaalamu wa Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


      “Lakini yote ya kuepusha Serikali ya Tanganyika kuwepo yalifanywa kwa makusudi kabisa, ili itumike Serikali ya Muungano kama ndio Tanganyika. Katika Sheria ile Na. 22 ya 1964, Rais wa Tanganyika amejipa madaraka ya kutunga na kutoa maagizo yanayohusu Muungano kwa kutumia amri (decrees) za sheria ya Tanganyika.
      Siku ile inapopitishwa sheria ile zilipitishwa pia Decrees mbili zilizotokana na vifungu Na. 6 (3), cha 8 na cha 5 cha sheria hiyo Na. 22 ya 1964, yaani The Provisional Transitional Decree 1964, na ile ya Interim Constitution Decree 1964 ambazo zote hazikuwa halali maana ni Decrees zilizopitishwa na Bunge la Tanganyika zilizotokana na Sheria Na. 22 ya 1964 ya Tanganyika.”


      Miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha kuwa hakukuwa na nia njema katika Muungano huu tokea awali ni pale wafanyakazi wa Serikali ya Tanganyika wote walipopandishwa vyeo kwa pamoja na kuwa wafanyakazi wa Muungano kama kifungu cha 3 (1) cha Provisional Transitional Decree kinavyosema:


      “Every person who holds office in the service of the Republic of Tanganyika immediately before the Union Day, shall on Union Day be deemed to have been elected, appointed or otherwise selected to the corresponding office in the service of the United Republic.”


      Yaani kila mfanyakazi aliyekuwa wa Serikali ya Tanganyika mara kabla ya siku ya Muungano kufumba na kufumbuwa, pengine kwa uchawi wa kifimbo cha Mwalimu Nyerere, anakuwa mara moja mfanyakazi wa Serikali ya Muungano kuanzia siku ya Muungano. Huu tuuiteje kama si ujambazi wa kikatiba (constitutional banditry)?


      Vivyo hivyo, kifungu cha 6 (i) cha Decree kinasema mara tu baada kuanza Muungano, Mahkama ya Tanganyika na Majaji wake wote nao watakuwa ndio Mahkama na Majaji wa Jamhuri ya Muungano kinyume na Makubaliano ya Muungano. Mpaka leo Katiba zote mbili hazitambuwi Mahkama (ukiondoa Mahkama ya Rufaa) kama ni suala la Muungano. Nembo ya Tanganyikainatumika kama nembo ya Serikali ya Muungano na Idara ya Mwanasheria Mkuu wa Tanganyikainachukuliwa kama Idara ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano.


      Haya yote hayamo na ni kinyume na Makubaliano ya 1964. Yote haya na kile kifungu cha 7 cha Sheria Na. 22 ya 1964 kinachofuta kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika hayakubadilisha na wala hayana mahusiano na Makubaliano ya Muungano ya 1964. Yote haya yalifanywa na Bunge la Tanganyika kwa maslahi ya Tanganyika nje ya Makubaliano.


      Aliyekuwa Spika wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Pius Msekwa, analifahamu vyema suala hili. Katika waraka wake alioutoa kwenye Semina kuhusu Muungano hapo Hoteli ya Mkonge, Tanga tarehe 25—27 Februari 1994 anasema:


      “The Transitional Decree, 1964 published on 01/05/64, transferred persons who were holding office in the public service of the Republic of Tanganyika to the corresponding office in the public service of the United Republic of Tanzania. By the same decree the High Court of Tanganyika also became the High Court of UnitedRepublic of Tanzania and the public seal of Tanganyika became public seal of theUnited Republic.”


      Athari za hatua hizi kwa Zanzibar ziko wazi. Tanganyika imejigeuza Tanzania na imechukua mamlaka ya mambo muhimu ya Zanzibar huku ikijipa hadhi ya kuwa juu ya Serikali ya Zanzibarkinyume na Mkataba wa Muungano. Hii ndiyo siri ya viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kung’ang’ania mfumo wa Serikali mbili na kukataa kata kata mabadiliko yoyote ya mfumo huo kwani Tanganyika inanufaika nao kwa kuwa yenyewe ndiyo imekuwa ‘Muungano’. Kukubali muundo wa Serikali tatu ni kuzifanya Tanganyika na Zanzibar ziwe na hadhi na fursa sawa katika Muungano, jambo ambalo Tanganyika hailitaki maana kulikubali ni kukubali kupoteza fursa zote inazozipata hivi sasa kwa kujikweza kwake na kujifanya kuwa ndiyo ‘Muungano’.


      Ushahidi wa wazi wa hoja yangu hii ni kwamba mtu anapoangalia taasisi zote za Muungano zilizoundwa chini ya Katiba au sheria za Muungano ambazo zinazikutanisha Serikali mbili zilizopo sasa, ataona kuwa wajumbe wanaowakilisha upande wa Serikali ya Muungano wote ni kutoka Tanganyika. Hoja inayojitokeza ni kwamba Serikali ya Muungano ni ya shirika ambapoZanzibar ni sehemu ya ushirika huo, kwa nini basi wajumbe wanaowakilisha Serikali hiyo ya Muungano watoke upande wa Tanganyika peke yake? Jawabu ni rahisi. Serikali ya Muungano kwa hakika ni Serikali ya Tanganyika iliyojivika joho la Muungano.


      Rais Jakaya Kikwete amekaririwa hadharani akisema matatizo ya Muungano hayatokani na muundo bali yanasababishwa na viongozi. Hoja, maelezo na mifano niliyoitoa hapo juu inatosha kumuonyesha Rais kwamba kauli yake si sahihi. Vyote viwili – muundo na pia kukosekana kwa nia njema upande wa viongozi – ni sababu za kuwepo kwa matatizo yasiyokwisha ya Muungano.


      Sisi katika CUF tumesema wazi kwamba kuna haja ya kuuimarisha Muungano wetu kwa kurekebisha kasoro hii ya msingi. Njia ya kufanya hivyo ni kuzionyesha wazi wazi mamlaka zote tatu zilizomo katika Mkataba wa Muungano ili kuondosha khofu za kudhani mmoja anafaidika katika muundo huu na mwengine anakandamizwa. Serikali ya Zanzibar ionekane wazi wazi, Serikali ya Tanganyika ionekane wazi wazi, na Serikali ya Muungano ionekani wazi wazi. Hapo hapatakuwa na hofu ya mkubwa kummeza mdogo, wala mdogo kupendelewa na kupewa uwakilishi unaozidi kiwango chake.




      Uvunjwaji wa Mkataba wa Muungano


      Mbali na suala la muundo wa Muungano, maeneo mengine mengi yanayogusa msingi wa Mkataba wa Muungano yaliendelea kuvunjwa na Serikali ya Tanganyika ikivaa joho la Muungano.


      Kifungu cha (viii) cha Mkataba wa Muungano kinaweka sharti kwamba Mkataba huo hautokuwa halali hadi pale Bunge la Tangayika na Baraza la Mapinduzi likishirikiana na Baraza la Mawaziri la Zanzibar yatakapopitisha sheria za kuridhia Mkataba huo. Upo ushahidi wa kutosha kwamba Bunge la Tanganyika lilikutana na kuuridhia Mkataba huo tarehe 25 Aprili, 1964. Hakuna ushahidi wowote kwamba Baraza la Mapinduzi likishirikiana na Baraza la Mawaziri la Zanzibaryalikaa kuuridhia Mkataba huo. Kwa hakika ushahidi ulioibuliwa na Prof. Issa Shivji katika kitabu chake cha karibuni kabisa, Pan-Africanism or Pragmatism? Lesssons of Tanganyika-Zanzibar Union umeweka wazi pasina chembe ya wasiwasi kwamba Mkataba huo haujaridhiwa na upande wa Zanzibar hadi hii leo. Ndiyo kusema, Mkataba wa Muungano haujapata uhalali wa kisheria hadi leo.


      Kifungu cha (iii) cha Mkataba wa Muungano kiliorodhesha mambo 11 tu ambayo ndiyo yaliyokubaliwa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika kuwa mambo ya Muungano. Hata hivyo, kipindi cha miaka 45 ya Muungano kimeshuhudia mambo hayo yakiongezwa isivyo halali kwa kutumia chombo kisicho na mamlaka ya kufanya hivyo yaani Bunge la Muungano na sasa kufikia 23 lakini ukiyanyumbua yanafikia 35. Ikumbukwe kwamba kila hatua ya kuongeza mambo ya Muungano maana yake ni kuchukua mamlaka ya Zanzibar na kuyahaulisha kwa Serikali ya Muungano ambayo kama tulivyokwisha onyesha kwa hakika hasa ni Serikali ya Tanganyika.


      Kifungu cha (vii) cha Mkataba huo kinataka Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mashauriano na makubaliano na Makamu wa Rais ambaye pia ni Rais wa Zanzibar kuunda Tume ya Katiba kwa lengo la kutayarisha rasimu ya Katiba ya Kudumu ya Muungano na baadaye kuifikisha rasimu hiyo mbele ya Bunge la Katiba (Constituent Assembly) litakalokuwa na wajumbe idadi sawa kati ya Zanzibar na Tanganyika kama watavyokubaliana viongozi hao wawili. Hatua hii muhimu sanakikatiba ilitakiwa itekelezwe ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tokea tarehe ya Muungano. Hadi hii leo hakuna Tume ya Katiba iliyoundwa wala Bunge la Katiba lililoundwa na kuitishwa kwa madhumuni ya kupitisha Katiba ya Kudumu ya Muungano. Kilichofanyika ni kuwa siku moja kabla ya kumalizika mwaka mmoja uliotakiwa, Bunge la Muungano lilitakiwa kupitisha sheria ya kuahirisha kwa muda usiojulikana tarehe ya kutekelezwa kwa hatua hii na hadi leo imesahaulika kabisa.


      Lakini mbali na dhoruba hizo dhidi ya Mkataba wa Muungano, rungu kubwa zaidi ambalo ndilo lililotumika kuimaliza Zanzibar lilikuwa ni kule kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM huku ikijipa madaraka juu ya vyombo vyengine vyote vya maamuzi katika nchi ikiwemo Serikali na Bunge na Baraza la Wawakilishi. Chini ya dhana ya Chama kushika hatamu(Party Supremacy) iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa lengo la kujilimbikizia madaraka yeye na Chama alichokuwa akikiongoza kama milki yake binafsi, CCM iliweza kutoa maagizo na maamuru mazito bila ya kujali madaraka ya Serikali ya Zanzibar yaliyotolewa kupitia Mkataba wa Muungano na hivyo kujinyakulia uwezo wote wa kuitawala Zanzibar ipendavyo huku viongozi wa Zanzibar wanaohoji wakituhumiwa kwamba wanapinga nidhamu ya Chama.




      Matatizo yatokanayo na kiini cha tatizo


      Kiini cha tatizo la msingi la Muungano ambalo kwa mtazamo wa CUF ni muundo wake unaotokana na tafsiri potofu ya Mkataba wa Muungano (Articles of Union) ndicho kimepelekea kujitokeza kwa matatizo mengine katika miaka 45 hii na ambayo yanaongezeka kila uchao.


      Mtu anapoangalia matatizo au hizi zinazoitwa kero atagundua kuwa karibu yote yanatokana ama na mshirika mmoja (mara nyingi Zanzibar) kutokuuamini au kuutilia shaka upande mwengine, au mshirika wa pili (mara nyingi Tanganyika ikivaa joho la Muungano) kuamini kwamba ina haki ya moja kwa moja kuamua na kutekeleza mambo fulani bila ya kulazimika kupata ridhaa ya upande wa pili ambao inahisi kama imeubeba tu. Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa tatizo linarudi kwenye muundo. Zanzibar haifahamu mamlaka ya Muungano katika Serikali ya Muungano yanaishia wapi ambapo mamlaka kwa mambo yasiyo ya Muungano kwa ajili yaTanganyika yanaanza. Tanganyika nayo kwa ‘kuwemo’ kwake katika Serikali ya Muungano kunaifanya ‘ishindwe kufahamu’ ni vipi na wapi Zanzibar inapata mamlaka ya kuhoji mambo ambayo ‘yameshatamkwa’ kwamba ni ya Muungano hata kama hayakuwemo katika Mkataba wa asili wa Muungano. Hali hii inaonekana katika kila kile kinachoitwa ‘kero’ za Muungano.


      Mifano inaweza kutolewa kwa takriban mambo yote, lakini kwa madhumuni ya waraka huu tuchukue mifano ya mambo matatu yafuatayo yanayozusha malalamiko:



      1. Umilikaji wa Mafuta na Gesi asilia.




      1. Uchangiaji katika gharama za Muungano na mgawanyo wa mapato yanayotokana na Muungano.




      1. Uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge la Muungano.



      Umilikaji wa Mafuta na Gesi asilia


      Kwanza, kuingizwa kwake katika orodha ya mambo ya Muungano (kama ilivyo kwa mambo mengi yaliyoongezwa baadaye) hakukufuata taratibu za Serikali ya Muungano (ambayo pia ni Serikali ya Tanganyika kwa mambo yasiyo ya Muungano) kuishauri na kupata ridhaa ya Zanzibar. Pili, Zanzibar inataka kujua ikiwa mafuta yanapaswa kuwa suala la Muungano na hivyo mapato yatakayopatikana yanufaishe pande zote mbili, kwa nini madini mengine yanayopatikana Bara kama vile dhahabu, almasi au tanzanite hayakufanywa pia kuwa ya Muungano na hivyo kunufaisha pande mbili pia? Kwa hivi sasa, ambapo si mambo ya Muungano, mapato yake yanaponufaisha Tanganyika peke yake, yanaingia katika mfuko (account) upi wa matumizi? Tatu, ikiwa mapato yatakayopatikana kutokana na mafuta yataingia katika mfuko wa Muungano, kuna uhakika gani wa kutumika kwa shughuli za Muungano tu wakati hakuna mifuko tofauti ya fedha kwa shughuli za Muungano na zile za Tanganyika zisizo za Muungano?


      Uchangiaji katika gharama za Muungano na mgawanyo wa mapato yanayotokana na Muungano


      Je, mtu anaposema Zanzibar haichangii gharama za uendeshaji wa vyombo na taasisi za Muungano kwa sababu tu Serikali ya Zanzibar haitoi fungu la fedha na kuliingiza katika Serikali ya Muungano, Tanganyika ambayo hata

      Serikali haina inachangia vipi na kiasi gani? Ikiwa mchango wake unatolewa na Serikali ya Muungano, kwani hii siyo serikali ya shirika ambapoZanzibar ni mbia? Vipi basi Zanzibar itakiwe ichangie mara mbili kwa kutumia hadhi mbili

      tofauti? Na ikichangia (iwapo itachangia), ina uhakika upi kwamba itakachotoa hakitatumiwa na Serikali ya Muungano kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano ikitumia mamlaka yake kwa madhumuni hayo? Vivyo

      hivyo kwa mapato yatokanayo na vyombo na taasisi za Muungano, tunajua Zanzibar inapata mgao wake na kiasi chake kimewekwa wazi (ingawa hakikubaliki kwa Wazanzibari). Masuala yanakuja: Yale mapato yanayobaki katika

      Serikali ya Muungano, kuna kipi cha kuonyesha mpaka wa matumizi yake kwa Muungano na kwa shughuli za Tanganyikazisizo za Muungano? Uadilifu na uwajibikaji wa matumizi yatokanayo na mgao huu wa mapato utaonekana vipi?


      Uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge la Muungano

      Wananchi wengi wa Tanganyika wanahoji vipi Zanzibar iliyo ndogo na ambayo ina watu wasiozidi milioni moja inawakilishwa na wabunge wa kuchaguliwa 50 wakati Dar es Salaam yenye wananchi wengi zaidi ina wabunge wa kuchaguliwa 7 tu? Wabunge hawa

      wanashiriki mijadala yote ya Bunge ikiwemo ya mambo yasiyo ya Muungano (ambayo kwa usahihi yatakuwa ni mamlaka ya Tanganyika kwa mambo yasiyo ya Muungano yanayosimamiwa na Serikali ya Muungano). Wanapata wapi uhalali wa kufanya hivyo

      wakati Wazanzibari hawapangiwi shughuli hizo (kwa mfano elimu, afya, kilimo, maji, umeme, habari, michezo, biashara, viwanda,

      serikali za mitaa n.k.) na Serikali ya Muungano wala hawasimamiwi katika mambo hayo na Bunge la Muungano? Uko wapi mpaka wa mamlaka ya Wazanzibari katika ushiriki wa Bunge hilowakati wao wana Serikali yao inayopanga na Baraza la Wawakilishi lao linalosimamia mamboyao kama hayo yasiyo ya Muungano?


      Mifano hii inatosha kuonyesha kwamba karibu matatizo yote, kama si yote, yanatokana na mkanganyiko na mgongano wa maslahi kati ya pande mbili ambao nao unasababishwa na mfumo usio wazi kuhusiana na mgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka tatu za Muungano zinazotambuliwa katika Mkataba wa Muungano.


      http://mfumokristo.blogspot.com/2012...akbali-wa.html
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    2. FemaTV & Radio

    3. #21
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By MziziMkavu
      Maswala yanayohusu serikali ya Mapinduzi Zanzibar Serikali ya muungano inayaingilia kati yapo mengi tu mojawapo ni hii hapa : Membe akalia 200bn za Zanzibar Bonyerza hapa http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...-zanzibar.html Mkuu Mkandara
      Dah ama kweli wewe mgumu sana kuelewa mapana ya Muungano..Yaani wewe na mkeo akipewa fedha toka nje azilete tu ndani ya nyumba na halali yake?. Ebu kwa kiola unapofikiria jambo iweke ndoa yako na mkeo halafu ndio ujue yapi na mke na yapi na ya ndoa ruksa.. Na labda nikuulize MEMBE Ni nani? anaiwakilisha serikali ya bara au ya Muungano? iweje swala hili liwe na Zanzibar ikiwa wawekezaji wote nchini wanapitia njia hiyo hiyo. Nini azma yao na deni hili litawahusu kina nani ikiwa Zanzibar inajulikana sio Nchi nje ya Muungano wetu. Mwinyi alipowauzia Saidia Loliondo ilikuwa kaingilia maswala ya bara?..Hivi rais akitokea Zanzibar hawezi kuweka ama kukataa misaada na mikataba inayohusu Bara!..

      labda nikwambie hivi hata Marekani kwenyewe walioanza kabla yetu Sii Senator, Governor wala Member wa Congress anaweza kwenda nje na kuweka mikataba ya aina yoyote wala kupokea misaada toka nje pasipo kupitishwa na serikali kuu. Mkuu mahusiano yoyote ya kimataifa ni lazima yapitie Ofisi wa Membe maana ndiye mwakilishi wetu sote. Mama Clinton majuzi alikuwa Malawi anawakilisha Marekani na hadi zozote anazozitoa zitawahusu Wamarekani wote..

      Hivi kuna tatizo gani kwa Zanzibar kupitia serikali ya Jamhuri ya muungano kuwawakilisha ktk mikataba yake nje ua mpaka awepo Mzanzibar ndio mnaiona haki..Rais kachaguliwa na sisi wote iweje nyie mjiweke kimbelembele kwenda kuweka mikataba ambayo inahusu zaidi mahusiano yetu KITAIFA. nani huko anaijua Bendera ya Zanzibar au Tanganyika!

      Hawa walioleta hiyo misaada walielewa vizuri sheria na walijua ktk kutaka kugombanisha serikali hizi mbili ni kuonyesha lengo la kutoa fedha kwa serikali ya Zanzibar wakati wanajua fika haiwezekani huu sio Utawala wa Kisultan ambao Sultan wa UAE anaweza kuweka mikataba pasipo Sultan wa Dubai au Sharja kuhusika. Hii ni serikali ya JAMHURI babuu mbona hamuelewi.

      Wewe hapo ulipo unaweza kabisa kupinga mkopo wowote unaotolewa ama kupokelewa kutoka nchi ambazo zinalenga kuharibu mahusiano ya muungano wetu...Hao Oman watoe misaada kwetu wakati maisha yao wenyewe yanawashinda, Oman wana struggle kiuchumi hizi sadaka zimetokea wapi. Wazanzibar waliohamia huko tu wanabaguliwa na hata kupewa Soweto yao leo wawe na huruma sana kwa Zanzibar....
      Last edited by Mkandara; 7th August 2012 at 19:10.
      Exploration of reality

    4. #22
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mkandara
      Dah ama kweli wewe mgumu sana kuelewa mapana ya Muungano..Yaani wewe na mkeo akipewa fedha toka nje azilete tu ndani ya nyumba na halali yake?..Na labda nikuulize MEMBE Ni nani? anaiwakilisha seriikali ya bara au ya Muungano? iweje swala hili liwe na Zanzibar ikiwa wawekezaji wote wanapitia njia hiyo hiyo. Mwinyi alipowauzia Saidia Loliondo ilikuwa kaingilia maswala ya bara?..Hivi rais akitokea Zanzibar hawezi kuweka kuweka mikataba inayohusu Bara!..

      labda nikwambie hivi hata Marekani kwenyewe walioanza kabla yetu hawezi Senator, Governor wala Member wa Congress anaweza kwenda nje na kuweka mikataba ya aina yoyote wala kupokea misaada toka nje pasipo kupitishwa na serikali kuu. Mahusiano yoyote ya kimataifa ni lazima yapitie Ofisi wa Membe maana ndiye mwakilishi wetu sote.

      Hivi kuna tatizo gani kwa Zanzibar kupitia serikali ya Jamhuri ya muungano kuwakilisha ktk mikataba yake nje..rais kachaguliwa na sisi wote iweje nyie mjiweke kimbelembele kwenda kuweka mikataba ambayo inahusu zaidi mahusiano yetu KITAIFA.

      Hawa walioleta hiyo misaada walielewa vizuri sheria na walijua ktk kutaka kugombanisha serikali hizi mbili ni kuonyesha lengo la kutoa fedha kwa serikali ya Zanzibar wakati wanajua fika haiwezekani huu sio Utawala wa Kisultan mabo Sultan wa UAE anaweza kuweka mikataba pasipo Sultan wa Dubai au Sharja kuipitisha. Hii ni serikali ya JAMHURI babuu mbona hamuelewi.

      Wewe hapo ulipo unaweza kabisa kupinga mkopo wowote unaotolewa ama kupokelewa kutoka nchi ambazo zinalenga kuharibu mahusiano ya muungano wetu...Hao Oman watoe mkopo kwetu wanakati maisha yao wenyewe yanawashinda, Wazanzibar waliohamia huko tu wanabaguliwa na hata kupewa Soweto yao leo wawe na huruma sana kwa Zanzibar....
      Nakuacha kwa leo najiandaa kula Futari Nalog Off inaonyesha ukishindwa malumbano ya Siasa unaleta maneno ya matusi wewe Mkandara Masuala ya mke na mume yamehusiana na nini na mambo ya kisiasa?Tangu mwanzo nilikwambia usilete maneno ya Pumba lakini hujasikia nakuacha kwa leo usiniharibie saumu yangu baadae kwa sasa nalog off mkuu Mkandara
      Mkandara, Ibambasi and takashi like this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    5. #23
      Wachovu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th June 2012
      Posts : 223
      Rep Power : 1112
      Likes Received
      44
      Likes Given
      0

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Mie naona Wazanzibar wanatubore sana kila kukicha ni malalamiko kibao.Nionavyo mimi kitu cha msingi ni kkukubali au kukataa kuwepo na Muungano. Kama wanaona muungano hawautaki ni bora tukaachana nao. Wengi hawajui athari za kuuvunja bado wanadhani itakuwa bizness as usual ? Kutengena kwa kulazimishana ni kubaya zaidi kwa mtizamo wangu.
      Litatoka wimbi la timua timua hiyo mkae nyinyi wazanzibar mkijua hilo. Wenye mnakumbuka baada ya kuvunjika kwa afrika mashariki sijui wengine hamkuona kilichotokea ? wanadamu ni wanyama ndugu zangu kama ni mpemba utachukuliwa juu juu bila kurudi nymbani , mimi tafrani hiyo naiona inanyelea nchi hii. Watu wamekata tamaa kwa sasa , matatizo ni mengi sasa mkitaka kuanza varangati la watu kurudi kwao itakuwaje ? Maana tunaishi kwa kujuana waunguja na wapemba wametapakaa nchi nzima na wanajulikana ikitokea mshike mshike kuna madhara mengi . TUTAFAKARI
      MziziMkavu likes this.

    6. #24
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Hata tuyazime, maswali yale yale kuhusu Muungano yanaturejea



      HUKO nyuma nimeeleza kwamba haiwezekani kuijadili Tanzania pasipo kuujadili Muungano, na kwamba dalili za makundi ya watu kuhoji Muungano wetu kama ulivyo leo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
      Fursa tuliyo nayo hivi sasa ya kujadili na kuandika katiba mpya ni fursa adhimu tunayoipata kuujadili Muungano kwa kina na kuupatia ufumbuzi utakaotupeleka masafa marefu kidogo.

      Ye yote anayetaka kujua jinsi masuala ya Muungano yalivyotusumbua katika historia yetu ya takriban nusu karne atakumbuka mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na tume na kamati mbalimbali zilizoundwa katika jitihada za kujaribu kurekebisha baadhi ya masuala yaliyoonekana kukera makundi ndani ya nchi, na jinsi ambavyo jitihada hizo zote na kamati na tume hizo hazikufanikiwa kuondoa malalamiko kuhusu Muungano.

      Sasa itakuwa ni jambo la ajabu iwapo, wakati tunasema tunataka kuandika katiba mpya, tutajinyima wasaa wa kuujadili Muungano kwa kuwauliza wananchi wa pande mbili (Tanganyika na Zanzibar) ni nini wanachotaka, iwapo wanataka Muungano au hawautaki.
      Swali hilo la msingi likiiisha kupatikana, na jibu likawa kwamba wanautaka Muungano, ndipo sasa itawezekana kuangalia kwa undani ni mambo gani ndani ya mfumo na taratibu za Muungano yafanyiwe marekebisho ili kuyaweka sawa na kukidhi matarajio ya pande mbili zilizoungana.

      Binafsi nakataa dhana ya kuwaambia watu kwamba kuujadili Muungano ni sharti tujadili namna ya kuuboresha. Mtu huboresha jambo analotaka kuendelea nalo, na kama hataki kundelea nalo ni upuuzi kuanza kuliboresha. Haina maana hata kidogo. Na si kweli kwamba hatujasikia sauti za watu wanosema kwamba hawautaki Muungano, na wala pia si kweli kwamba hawana haki ya kuwa na mawazo kama hayo.

      Njia pekee kwa wale wanaopenda Muungano uendelee kuwapo (pamoja na marekebisho yatakayokubaliwa) ni kuwaacha wana-Muungano wenyewe waseme kwamba wanataka kuuendeleza kwa kuuboresha. Iwapo watasema kwamba hawautaki, na tujue kwamba hiyo ndiyo kauli yao, huo ndio utashi wao. Kujidai kwamba tutauendeleza Muungano bila ridhaa ya Watanganyika na Wazanzibari ni ndoto za Alinacha.

      Katika historia yetu tumekuwa na matukio kadhaa yaliyoutikisha Muungano lakini ikawezekana kuyazima kwa njia moja au nyingine. Tutakumbuka sakata la “kuchafuka kwa hali ya hewa” Visiwani mwaka 1983-84, iliyosababisha kuondolewa madarakani aliyekuwa rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi.
      Kimsingi alichokuwa akisema Jumbe ni kwamba Muungano ulihitaji marekebisho katika muundo wake ili uweze kukidhi mahitaji ya Wazanzibari.

      Tukumbuke pia kwamba wakati Jumbe akichukua hatua za kufanya mapendekezo ya kuuboresha Muungano kadri alivyoona inafaa, alikuwa ni kipenzi cha Mwalimu Nyerere, ambaye alijiona raha kufanya kazi na ‘msomi’ mwenzake baada ya kusumbuana sana na Abeid Karume, muasisi mwenzake wa Muungano, Karume akiwa ni mtu asiyetabirika, na mwenye maamuzi yaliyotatanisha.

      Inawezekana kwamba usiri wa hatua alizokuwa akitaka kuzichukua Jumbe ndio uliomuudhi Nyerere hata akaamua kumwadhibu Jumbe. Hata hivyo, haijulikani msimmao wa Mwalimu ungekuwa upi iwapo Jumbe angepeleka mapendekezo yake mbele ya kikao rasmi cha CCM au serikali na kuomba ridhaa juu ya mawazo yake ya kuboresha Muungano.

      Tofauti na hii leo, ambapo majadiliano ndani ya NEC ya chama-tawala yanajulikana Kariakoo na Manzese kabla kikao hakijafungwa, wakati ule wa sakata la Jumbe kikao cha siri maana yake ilikuwa ni kikao cha siri. Kikao hicho hakina hata ‘hansard’. Ndiyo maana itakuwa vigumu kujadili kwa undani maudhui ya mjadala uliofanyika ndani ya kikao kilichohitimishwa kwa kumvua Jumbe nyadhifa zake zote na kumpeleka ‘uhamishoni’ Mji Mwema.

      Muongo mmoja baadaye kundi la wabunge wa CCM lililojulikana kama G-55 (jina lilinuniwa na Issa Shivji) likaibuka na kudai marekebisho katika muundo wa Muungano kwa kuasisi serikali ya Tangayika na kuwa na muundo wa Shirikisho.
      Hoja iliyopelekwa bungeni na kundi hili iliungwa mkono kwa nguvu kubwa na watu wengi na hatimaye serikai ikaridhia hoja hiyo na kukubali marekebisho hayo yafanyike.

      Kwa mara nyingine tena ilikuwa ni Mwalimu Nyerere aliyesimama na kuipinga hoja hiyo, ikiwa tayari imekwisha kupitishwa na Bunge, na hatimaye juhudi zake zikafanikiwa kuitengua hoja hiyo.
      Ikumbukwe kwamba Mwalimu wakati huo hakuwa rais wala mwenyekiti wa chama chake, lakini kwa ushawishi aliokuwa nao aliweza kufanya alivyofanya.

      Nakumbuka, nikiwa mmoja wa kundi la G-55, tulikuwa na mabishano mengi na Mwalimu nyumbani kwake Msasani katika kipindi hicho, na nakumbuka kwamba Mwalimu alishikilia msimamo wake bila kutetereka, ingawaje baadhi yetu hatukuona mantiki ya kile alichokuwa akikitetea.

      Kimsingi, msimamo wake ulikuwa kwamba muundo wa serikali tatu ungevunja Muungano. Sisi tulikuwa na mawazo tofauti, kimsingi, kwa sababu tulikuwa hatuoni matiki ya kuwa na serikali mbili, moja ikiwa ni ya Zanzibar na ya pili ikiwa ni ya Zanzibar na Tanganyika.
      Hiyo ni historia. Lakini sasa zimejitokeza sauti zinazotoa mwangwi wa haya ninayoyasimulia, kwa mara nyingine zikidai muundo wa serikali tatu. Hizi ziko pande mbili za Muungano, nazo zinadhihirisha ukweli kwamba jambo hili halijaondoka; lipo na linahitaji mjadala wa kina ndipo lipatiwe ufumbuzi. Kulizimazima hakutasaidia sana.

      Nimekuwa nikikagua kumbukumbu ili kujua kama Mwalimu Nyerere aliwahi kupiga marufuku mjadala kuhusu Muungano. Sikumbuki. Alimtoa Jumbe madarakani. Aliizima hoja ya G-55. Lakini sikumbuki hata mara moja akisema kwamba ni marufuku kuujadili Muunagno. Aliwaachia waliomzunguka waelewe kwamba kwake Muungano ulikuwa kitu azizi kwake na hapendi kichezewe, lakini hakusema kinagaubaga kwamba ni marufuku kuujadili.

      Ninaweza kwenda mbali zaidi na kusema kwamba, hata kama Mwalimu angekuwa amesema waziwazi kwamba ni marufuku kuujadili Muungano, bado tungeweza, katika mazingira ya leo, tukasema kwamba pamoja na heshima yetu kubwa kwake, lakini Muungano unajadilika. Mambo yamebadilika, na dunia inasonga mbele, na alichokiamini baba yako sicho unachotakiwa lazima ukiamini leo.

      Kama hivyo ndivyo, hakuna sababu yo yote ya kuweka makatazo katika majadala kuhusu Muungano. Acheni ujadiliwe kwa uwazi mkubwa kiasi kinachowezekana, mawazo yanayokinzana yashindanishwe na mumo tupate elimu ya kuuboresha Muungano.
      Mimi binafsi ni muumini mkubwa wa mamlaka ya watu ndani ya sehemu wanamoishi, kwa sababu mamlaka hayo ndicho kielelezo thabiti cha dhana ya kujitawala.

      Hatua yo yote inayopunguza uwezo wa wananchi wa sehemu fulani kujiendeshea shughuli zao kwa uhuru mpana kiasi kinachowezekana ndani ya umoja wa jumla, ni kitendo kinachokinzana na maendeleo.
      Wako Wazanzibari wanaosema uhuru wao wa kuendesha mambo yao umebinywa mno; wako Watanganyika wanaodhani kwamba katika

      Muunago huu Wazanzibari wanapewa nafasi ambazo si zao, na kwa hiyo wanawanyima nafasi Watanganyika. Hususan, dhana ya u-Zanzibari imekuzwa mno hadi inaamsha jawabu la u-Tanganyika.
      Shetani naye amejiingiza. Waziri wa zamani wa mafuta nchini Venezuela aliwahi kusema kwamba mafuta ya peteroli ni kinyesi cha Shetani nasi sote tunaogelea ndani yake.

      Inaelekea Shetani ametutembelea hivi karibuni, na tunasikia kelele za “Yangu! Yangu!” Baadhi ya Wazanzibari wameanza kuogelea mumo kabla hata Shetani hajaenda msalani.

      Bila shaka viyu kama hivyo (mafuta, gesi asilia, ardhi, misitu, rasilimali-bahari na kadhalika) vitakuja kutusumbua huko tuendako. Na tutakumbana na ile dhana ya mzandiki anayesema, “Chako chetu, changu changu.” Njia pekee ya kuondokana na uzandiki huo ni kuwa na mjadala mpana, wa wazi, na wa kituo.
      Chanzo: Raia Mwema
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    7. #25
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By MziziMkavu
      Nakuacha kwa leo najiandaa kula Futari Nalog Off inaonyesha ukishindwa malumbano ya Siasa unaleta maneno ya matusi wewe Mkandara Masuala ya mke na mume yamehusiana na nini na mambo ya kisiasa?Tangu mwanzo nilikwambia usilete maneno ya Pumba lakini hujasikia nakuacha kwa leo usiniharibie saumu yangu baadae kwa sasa nalog off mkuu Mkandara
      Alaaa hata mfano basi au naposema mke wewe unachukulia nawatukana kwa sababu uwezo wa mwanamke ni hafifu kwenu hivyo ni matusi?.. Wahi futur isifanye kufur, mimi bado hadi saa tatu usiku. Ukirudi utayakuta yamejaa tele kama pichi..

      Haya niseme mke wangu miye sio wako, hawezi kuleta fedha alizoahidiwa na mwanamme ndani ya nyumba pasipo kushauriana nami. Na usichukulie naposema Mke ukaona nawadhalilisha nyie maana kwangu mke mume sote ni wamoja, uwezo sawa na nafasi sawa ndani ya ndoa tena mwanamke ana mamlaka zaidi. Ningekuwa mwanamke ningesema Mume wangu hawezi kuleta hela alizoahidiwa nje na mwanamke kuziingiza nyumbani. Halafu Hivi ni nani naibu waziri wa Membe vile?..
      Ibambasi and MziziMkavu like this.
      Exploration of reality

    8. Miaka 50

    9. #26
      mkataba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 147
      Rep Power : 375
      Likes Received
      35
      Likes Given
      4

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Wachovu
      Mie naona Wazanzibar wanatubore sana kila kukicha ni malalamiko kibao.Nionavyo mimi kitu cha msingi ni kkukubali au kukataa kuwepo na Muungano. Kama wanaona muungano hawautaki ni bora tukaachana nao. Wengi hawajui athari za kuuvunja bado wanadhani itakuwa bizness as usual ? Kutengena kwa kulazimishana ni kubaya zaidi kwa mtizamo wangu.
      Litatoka wimbi la timua timua hiyo mkae nyinyi wazanzibar mkijua hilo. Wenye mnakumbuka baada ya kuvunjika kwa afrika mashariki sijui wengine hamkuona kilichotokea ? wanadamu ni wanyama ndugu zangu kama ni mpemba utachukuliwa juu juu bila kurudi nymbani , mimi tafrani hiyo naiona inanyelea nchi hii. Watu wamekata tamaa kwa sasa , matatizo ni mengi sasa mkitaka kuanza varangati la watu kurudi kwao itakuwaje ? Maana tunaishi kwa kujuana waunguja na wapemba wametapakaa nchi nzima na wanajulikana ikitokea mshike mshike kuna madhara mengi . TUTAFAKARI


      Wacha kuwatisha Wazanzibari, wao wameshapaangalia hapo ndio maana wadai nchi yao haijalishi, kwani huko Syria, Libya, Misri, Yemen, Tunisia ndio hivohivo baada ya mda si wametulia, basi na Zenji wala hawatafikia kama hivo tunavofikiria.

      Mimi nawajua Wazanzibari wakiona tu kuna harufu ya kufukuzwa Tanganyika wataondoka kabla ya kufukuzwa na wala hamtawaona hata watakapopita na mtawatafuta kwa udi na uvumba.

      Na wala kwa hilo tusitishane tugawane mbao tuuuuuuuuuuuuuuu.
      Ibambasi and MziziMkavu like this.

    10. #27
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mkandara
      Alaaa hata mfano basi au naposema mke wewe unachukulia nawatukana kwa sababu uwezo wa mwanamke ni hafifu kwenu hivyo ni matusi?.. Wahi futur isifanye kufur, mimi bado hadi saa tatu usiku. Ukirudi utayakuta yamejaa tele kama pichi..

      Haya niseme mke wangu miye sio wako, hawezi kuleta fedha alizoahidiwa na mwanamme ndani ya nyumba pasipo kushauriana nami. Na usichukulie naposema Mke ukaona nawadhalilisha nyie maana kwangu mke mume sote ni wamoja, uwezo sawa na nafasi sawa ndani ya ndoa tena mwanamke ana mamlaka zaidi. Ningekuwa mwanamke ningesema Mume wangu hawezi kuleta hela alizoahidiwa nje na mwanamke kuziingiza nyumbani. Halafu Hivi ni nani naibu waziri wa Membe vile?..
      Mkuu Mkandara tuchukulie huo mfano wako mbovu uliotoa wa kuhusu Mke na Mume ninavyojuwa mimi kati ya Mke na Mume wakiishi sana kwenye Ndoa yao inafika wakati Mmoja kati ya hao wawili anamchoka mwenzie kitabia ? au wote wawili wanachokana kitabia ?Na ikifika

      hatua ya Mmoja kumchoka mwenzie inakuwa Ndoa yao kati ya hao wawili Mume na Mke haidumu wanatengana na hivyo hivyo Muungano wa Miaka 48 wa Tanganyika na Zanzibar umefika kikomo ndugu zetu wa Zanzibar Wamesha choka na Kero ya

      huo Muungano wanachohitaji watengane kwa salama an Amani Wa Zanzibar hawautaki Muungano tena imekuwa ni basi tena inatosha miaka 48. Na kama ilivyo kwenye ndoa ya Miaka 48 kwa mfano wewe na mke wako mupo pamoja katika Ndoa yenu ya muda wa miaka 48 itakuwa wewe ndie wa kwanza Kumchoka Mke wako au Mke wako atakuchoka wewe kitabia na itakuwa ndio mwisho wa hiyo ndoa yenu ni kuachana sasa wewe unasemaje huo mfano wangu mkuu Mkandara?
      Ibambasi likes this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    11. #28
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By MziziMkavu
      Mkuu Mkandara tuchukulie huo mfano wako mbovu uliotoa wa kuhusu Mke na Mume ninavyojuwa mimi kati ya Mke na Mume wakiishi sana kwenye Ndoa yao inafika wakati Mmoja kati ya hao wawili anamchoka mwenzie kitabia ? au wote wawili wanachokana kitabia ?Na ikifika

      hatua ya Mmoja kumchoka mwenzie inakuwa Ndoa yao kati ya hao wawili Mume na Mke haidumu wanatengana na hivyo hivyo Muungano wa Miaka 48 wa Tanganyika na Zanzibar umefika kikomo ndugu zetu wa Zanzibar Wamesha choka na Kero ya

      huo Muungano wanachohitaji watengane kwa salama an Amani Wa Zanzibar hawautaki Muungano tena imekuwa ni basi tena inatosha miaka 48. Na kama ilivyo kwenye ndoa ya Miaka 48 kwa mfano wewe na mke wako mupo pamoja katika Ndoa yenu ya muda wa miaka 48 itakuwa wewe ndie wa kwanza Kumchoka Mke wako au Mke wako atakuchoka wewe kitabia na itakuwa ndio mwisho wa hiyo ndoa yenu ni kuachana sasa wewe unasemaje huo mfano wangu mkuu Mkandara?
      Sasa haya maneno..nashiukuru umerudi kuwa mdogo kidogo tulingane. basi kama ungesema toka zamani tumechokana au Wazanzibar wameichoka ndoa wala tusingefika huku. Sii kuweka visingizio wakati tumeishi pamoja ktk ndoa kwa miaka 48 sasa ati abuse zote ndio zinasemwa leo na iwe sababu ya kutalakiana.. I mean kwa mwenye kuelewa mtu anayekuwa Abused hahitaji miaka 40 ndani ya ndoa, unless wewe mwenyewe una matatizo binafsi.

      Sasa hata ktk hili la kuchoshwa, maajabu wa Wazanzibar hawataki talaka bali talaka rejea... wanachotaka tutalakiane lakini relationship yetu iendelee kwa sababu gani sijui.. nasi Bara tunasema kama waitaka talaka tusijuane maana ndio maana ya talaka. Wazanzibar wanasema hapana tume na makubaliano mpya lakini tusiwe wanandoa kila mtu awe na uhuru wa kufanya takavyo mbona kuna watu wanaishi kama wapenzi na wanatambuliwa kishieria(common in law). Mapenzi haya ndio bara hatuyataki...tunachowaambiamak e up your mind, kila mlichokitaka ktk miaka 48 tumeenda kwa kadhi na kuyarekebisha, mkadai mengi na mengine..

      Hii picha ndio haijengi mantiki kwetu sisi, maadam tulishafunga ndoa tukiachana tuachane hakua mtu kumtegemea mwingine wala habari za kujuana tena. lakini kinachowapa shida Zanzibar ni kwamba watoto wake wengi wanaishi na mama custudy tunayo sisi bara. na kama itafanyika referendum wazanzibar wanahofia watoto hawa Wazanzibara kupinga kuvunjika kwa ndoa..Well, sasa amueni basi mnataka kubakia ktk ndoa au.. Oooh Bara tuwapeni talaka, alaah! kwani kadhi nani, mlete kadhji tumalize maneno. Hivi kweli mnanataka kuondoka au miyeyusho tuongeze dau la kuwapa matumizi kila siku?.

      Majuzi tu mliposikia YAWEZEKANA kuna mafuta Pemba mtumee! mnataka tuwekeane mipaka ijulikane wapi mwisho wa Zanzibar utadhani mmeshinda lotto tayari.. hamna tofauti na huyu Mama Banda alosikia kuna uwezekano wa mafuta North ya lake Malawi basi anaweka madai ziwa lote ni la Malawi na kuonyesha hati za Mkoloni zinazoonyesha nchi inayoitwa NYASALAND..Haya Mafuta tu yamewatoa roho watu na Inslaallah naomba sana Mwenyezi Mungu hayo mafuta yasipatikane Pemba wala lake Malawi tuyapate Tanga na na dryland Mbeya halafu tutawaona mtabadilisha vipi tamaa hizi..
      JokaKuu, Mndamba and Ibambasi like this.
      Exploration of reality

    12. #29
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mkandara
      Sasa haya maneno..nashiukuru umerudi kuwa mdogo kidogo tulingane. basi kama ungesema toka zamani tumechokana au Wazanzibar wameichoka ndoa wala tusingefika huku. Sii kuweka visingizio wakati tumeishi pamoja ktk ndoa kwa miaka 48 sasa ati abuse zote ndio zinasemwa leo na iwe sababu ya kutalakiana.. I mean kwa mwenye kuelewa mtu anayekuwa Abused hahitaji miaka 40 ndani ya ndoa, unless wewe mwenyewe una matatizo binafsi.

      Sasa hata ktk hili la kuchoshwa, maajabu wa Wazanzibar hawataki talaka bali talaka rejea... wanachotaka tutalakiane lakini relationship yetu iendelee kwa sababu gani sijui.. nasi Bara tunasema kama waitaka talaka tusijuane maana ndio maana ya talaka. Wazanzibar wanasema hapana tume na makubaliano mpya lakini tusiwe wanandoa kila mtu awe na uhuru wa kufanya takavyo mbona kuna watu wanaishi kama wapenzi na wanatambuliwa kishieria(common in law). Mapenzi haya ndio bara hatuyataki...tunachowaambiamak e up your mind, kila mlichokitaka ktk miaka 48 tumeenda kwa kadhi na kuyarekebisha, mkadai mengi na mengine..

      Hii picha ndio haijengi mantiki kwetu sisi, maadam tulishafunga ndoa tukiachana tuachane hakua mtu kumtegemea mwingine wala habari za kujuana tena. lakini kinachowapa shida Zanzibar ni kwamba watoto wake wengi wanaishi na mama custudy tunayo sisi bara. na kama itafanyika referendum wazanzibar wanahofia watoto hawa Wazanzibara kupinga kuvunjika kwa ndoa..Well, sasa amueni basi mnataka kubakia ktk ndoa au.. Oooh Bara tuwapeni talaka, alaah! kwani kadhi nani, mlete kadhji tumalize maneno. Hivi kweli mnanataka kuondoka au miyeyusho tuongeze dau la kuwapa matumizi kila siku?.

      Majuzi tu mliposikia YAWEZEKANA kuna mafuta Pemba mtumee! mnataka tuwekeane mipaka ijulikane wapi mwisho wa Zanzibar utadhani mmeshinda lotto tayari.. hamna tofauti na huyu Mama Banda alosikia kuna uwezekano wa mafuta North ya lake Malawi basi anaweka madai ziwa lote ni la Malawi na kuonyesha hati za Mkoloni zinazoonyesha nchi inayoitwa NYASALAND..Haya Mafuta tu yamewatoa roho watu na Inslaallah naomba sana Mwenyezi Mungu hayo mafuta yasipatikane Pemba wala lake Malawi tuyapate Tanga na na dryland Mbeya halafu tutawaona mtabadilisha vipi tamaa hizi..
      Kwani wewe ukiachana na Mke wako ambaye Mumezaa watoto basi kutakuwa na uaduwi wowote? Marehemu baba yangu aliishi

      na Marehemu Mama yangu zaidi ya miaka 32 na waliachana mwaka 1980 mbona walikuwa wanaonana uso kwa uso na baba aliowa Mwanamke Mwengine wa kingoni. kuchana au kutengana sio ndio sababu ya kuweka uaduwi kati yetu sisi Wa

      Tanganyika na ndugu zetu wa Ki Zanzibar ? Tumeowana tumezaana tuko kitu kimoja ila Wenzetu WaZanzibar wamechoka na huo Umoja wetu Muungano wenu sasa kama mwenzako amechoka wewe bado unangojea nini tena kitokee Vita? Mauaji?

      uaduwi? Wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba Havizidi zaidi ya Watu Millioni 2 sasa kwanini tuumize vichwa kwa Watu ambao hawazidi zaidi ya Millioni 2? Mkuu Mkandara Wa Zanzibar hawataki Muungano wetu Tuwaache kama walivyo unaonaje mkuu?
      Ibambasi likes this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    13. #30
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By MziziMkavu
      Kwani wewe ukiachana na Mke wako ambaye Mumezaa watoto basi kutakuwa na uaduwi wowote? Marehemu baba yangu aliishi

      na Marehemu Mama yangu zaidi ya miaka 32 na waliachana mwaka 1980 mbona walikuwa wanaonana uso kwa uso na baba aliowa Mwanamke Mwengine wa kingoni. kuchana au kutengana sio ndio sababu ya kuweka uaduwi kati yetu sisi Wa

      Tanganyika na ndugu zetu wa Ki Zanzibar ? Tumeowana tumezaana tuko kitu kimoja ila Wenzetu WaZanzibar wamechoka na huo Umoja wetu Muungano wenu sasa kama mwenzako amechoka wewe bado unangojea nini tena kitokee Vita? Mauaji?

      uaduwi? Wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba Havizidi zaidi ya Watu Millioni 2 sasa kwanini tuumize vichwa kwa Watu ambao hawazidi zaidi ya Millioni 2? Mkuu Mkandara Wa Zanzibar hawataki Muungano wetu Tuwaache kama walivyo unaonaje mkuu?
      Kuonana uso kwa uso, sii hata Kenya tunaonana, Uganda tunaonana tena rais wetu mzuri sana anapenda viwanja atakuja sana Zanzibar lakini msimpe mke tu ili kusiwepo na mahusiano ya kimwili maana ndicho mkitakacho kuendeleza zinaa..

      Kama tunavunja muungano tukubaliane maana tunajua mnaye mke mwingine akilini naye ni mwarabu mweupe wa rangi, mwenye pua ya Upanga, mtoto nywele za singa hadi mgongoni halafu ukoo wa mfalme, na ndio anawatoa roho kiasi kwamba umenipa mfano wa hizo bil 200.

      Alaa wauze vichwa vipi wakati ndio wanaopata kuchagua wake/waume wengi kutoka kwetu bara?.. Sisi wabara tutaweza vipi kuingiliana na watu millio 2 au advantage ni yao kuweza kuuza mali zao kwa watu millini 40. Sisi hatuoni soko Zanzibar zaidi ya kutalii beach...Fikirieni kiuchumi na sio idadi ya kumezwa kwani sisi tumekuwa chewa!
      Last edited by Mkandara; 8th August 2012 at 02:30.
      JokaKuu and Ibambasi like this.
      Exploration of reality

    14. #31
      bagamoyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2010
      Posts : 1,308
      Rep Power : 1097
      Likes Received
      300
      Likes Given
      358

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Mh. Tundu Lissu akitoa hotuba Mbadala ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara inayohusu maswala ya Muungano.

      Kambi rasmi ya upinzani inasema baada ya katiba ya Muungano kuchakachuliwa na kuwekewa viraka vingi kinyume na makubaliano ya kuundwa kwa Muungano ya mwaka 1964, hivi sasa kuna nchi mbili ndani ya muungano yaani Tanganyika na Zanzibar.


      Video kwa hisani ya chadematv ya youtube.
      MziziMkavu likes this.

    15. #32
      Mzenji73's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th January 2009
      Posts : 203
      Rep Power : 823
      Likes Received
      33
      Likes Given
      53

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mkandara
      Hiyo serikali ya Muungano ni serikali ya kina nani?.. Si Wanzanzibar na Wabara ndio wameunda muungano huo ama? Mkuu wangu unajua hasa maana ya muungano au unazungumza tu vitu visivyojulikana mkidhani muungano ni sawa na JUMUIYA. Uliona wapi Federal Government haihusiki na maswala yanayohusu Muungano?. Hivi unataka kunambia Obama ni rais wa Illinois hawezi kuingilia maswala ya state nyingine ktk muungano wao. Ni yapi hayo ya serikali ya mapinduzi ambayo mliyakubali kikatiba leo yawe ya Zanzibar? na yapi ni ya bara. Haya nambie wakati Mwinyi alipokuwa rais alikuwa akiingilia maswala ya bara au... Mbona nyie mnaingilia kila siku ya bara kwa kutumia kiti cha muungano na hatusemi..
      " naam kwa mujibu wa makubaliano, serikali ya muungano ni yetu sote kwa yale yanayohusu muungano, matatizo ni kwamba hata kayo mambo yasiyo ya muungano SMT inatuingilia kwa kutuamulia, lakini vile vile kuna uhalali gani kwa yale yasiyo ya muungano upande wa tanganyika kuhudumiwa na SMT kwa jina la tanzania? "
      MziziMkavu likes this.

    16. #33
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mzenji73
      " naam kwa mujibu wa makubaliano, serikali ya muungano ni yetu sote kwa yale yanayohusu muungano, matatizo ni kwamba hata kayo mambo yasiyo ya muungano SMT inatuingilia kwa kutuamulia, lakini vile vile kuna uhalali gani kwa yale yasiyo ya muungano upande wa tanganyika kuhudumiwa na SMT kwa jina la tanzania? "
      Unadhani Wazanzibar wanaliona hili?..Vikao vyote vya bunge Dodoma wawakilishi wa Zanzibar wapo toka kinafunguliwa hadi kinafungwa na wanachangia ktk maswala yote. Wapo katika mabaraza yote ya bara na serikali ya muungano, toka vikao vya vyama hadi taifalakini hawaoni kama wameingia kila sehemu bara..Na Wabara hawaruhusiwi kuingia ktk Bunge lao, wizara zao, hata kupiga kura za ucguzi mkuu wa Taifa hawatakiwi japokuwa ni wakazi wa Zanzibar ama wanafanya kazi za jamhuri ya muungano.

      Imefikia hadi wakati wa uchaguzi mkuu, wabara wanatakiwa warudi Bara japokuwa hawapigi kura za kumchagua mwakilishi wa serikali ya Mapinduzi ila ya Muungano. Kwa ujinga wao husimama ktk vituo vya kura na kuwaondoa Wabara ambao wanaishi Zanzibar wasipige kura kumchagua rais wa Jamhuri ya Tanzania.. Can U imagine that!..
      Haya hakuna Mbara ktk mabaraza yote la Wawakilishi ama la Mapinduzi japokuwa Wabara walishiriki ktk Mapinduzi hayo, huku bara wanataka wawe sehemu zote kwa sababu ni serikali ya muungano....Yaani hawaeleweki watu hawa kabisa halafu wanajiita wao sii wabaguzi walilelewa vizuri kupenda watu wote pasipo kuwabagua kwa trangi zao, dini, zao ama jinsia zao...
      Last edited by Mkandara; 8th August 2012 at 16:57.
      Ibambasi and MziziMkavu like this.
      Exploration of reality

    17. #34
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mkandara
      Kuonana uso kwa uso, sii hata Kenya tunaonana, Uganda tunaonana tena rais wetu mzuri sana anapenda viwanja atakuja sana Zanzibar lakini msimpe mke tu ili kusiwepo na mahusiano ya kimwili maana ndicho mkitakacho kuendeleza zinaa..

      Kama tunavunja muungano tukubaliane maana tunajua mnaye mke mwingine akilini naye ni mwarabu mweupe wa rangi, mwenye pua ya Upanga, mtoto nywele za singa hadi mgongoni halafu ukoo wa mfalme, na ndio anawatoa roho kiasi kwamba umenipa mfano wa hizo bil 200.

      Alaa wauze vichwa vipi wakati ndio wanaopata kuchagua wake/waume wengi kutoka kwetu bara?.. Sisi wabara tutaweza vipi kuingiliana na watu millio 2 au advantage ni yao kuweza kuuza mali zao kwa watu millini 40. Sisi hatuoni soko Zanzibar zaidi ya kutalii beach...Fikirieni kiuchumi na sio idadi ya kumezwa kwani sisi tumekuwa chewa!
      Unazungumza wewe Maneno ya Porojo hakuna Maneno yoyote yale ya msingi wowote ule unao zungumza wewe. Muhimu kuwa WaZanzibar hawautaki huo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanachotaka WaZanzibari Muungano uvunjike wanataka wawe huru kujiamulia mambo yao yenyewe acha porojo zako. mkuu Mkandara
      Ibambasi likes this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    18. #35
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By bagamoyo
      Mh. Tundu Lissu akitoa hotuba Mbadala ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara inayohusu maswala ya Muungano.

      Kambi rasmi ya upinzani inasema baada ya katiba ya Muungano kuchakachuliwa na kuwekewa viraka vingi kinyume na makubaliano ya kuundwa kwa Muungano ya mwaka 1964, hivi sasa kuna nchi mbili ndani ya muungano yaani Tanganyika na Zanzibar.


      Video kwa hisani ya chadematv ya youtube.
      Mkuu bagamoyo Kurudi kwa Tanganyika itarudi kwa njia nyepesi tu nayo ni moja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uvunjike ndio itarudi hiyo Tanganyika pasipo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuvunjika Tanganyika haiwezi kurudi hilo ndilo jibu kwa chama cha Chadema.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    19. #36
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By MziziMkavu
      Unazungumza wewe Maneno ya Porojo hakuna Maneno yoyote yale ya msingi wowote ule unao zungumza wewe. Muhimu kuwa WaZanzibar hawautaki huo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanachotaka WaZanzibari Muungano uvunjike wanataka wawe huru kujiamulia mambo yao yenyewe acha porojo zako. mkuu Mkandara
      Sawa wewe chukulia porojo lakini ndio facts.. watu mil 2 wanaweza sana ku benefit kwa soko la watu mil 40 kuuza mali zao bila ushuru wa kuingiza mali, lakini Bara hawahitaji soko la Zanzibar, think about that jinsi gani tunavyowapa taabu wakenya na Waganda. Tuvunje muungano mjifungie wenyewe halafu tutaona huo mzunguko ndani kama utaweza kuwasaidia kiuchumi.

      Haya nambie ni kiongozi gani anayetaka muungano uvunjike lakini pasiwepo na mkataba mwingine...Maana bara hatutaki mkataba wowote na Zanzibar zaidi ya muungano au tuvunje muungano.. wape mtihani huu viongozi wa Zanzibar halafu waje na jibu.. Nakuapia hutalipata.

      Wewe mwambie kiongozi yeyote wa Zanzibar:-
      1. Tuvunje muungano na hakuna ushirika wowote isipokuwa ule wa EA
      2. Tuendelee na Muungano uliopo turekebishe tu kuwa na serikali tatu kila upande ujitegemee. This is what Mainland offer hakuna zaidi wala pungufu.
      Ibambasi and Nguruvi3 like this.
      Exploration of reality

    20. #37
      Dezo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th July 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 346
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Wewe ni aibu hata kukujibu lakini wacha nikujibu tu. Wewe kenge unatoka mkowa gani wa hiyo Bongo chafu na jee mkowa wako una haya yafuatayo. Serikali kamili, Mawaziri, Wimbo wa Taifa, Jumba la Bunge, Raisi, Mahakama kuu na mipaka, Na jee hicho kakimkowa wako kishawahi kuwa na kiti Umoja wa Mataifa. Ndomaana nikasema aibu hata kukujibu wewe Sofulo.

    21. #38
      Nonda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th November 2010
      Location : Gongo La Mboto
      Posts : 5,816
      Rep Power : 1863
      Likes Received
      937
      Likes Given
      367

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mkandara
      Hiyo serikali ya Muungano ni serikali ya kina nani?.. Si Wanzanzibar na Wabara ndio wameunda muungano huo ama? Mkuu wangu unajua hasa maana ya muungano au unazungumza tu vitu visivyojulikana mkidhani muungano ni sawa na JUMUIYA. Uliona wapi Federal Government haihusiki na maswala yanayohusu Muungano?. Hivi unataka kunambia Obama ni rais wa Illinois hawezi kuingilia maswala ya state nyingine ktk muungano wao. Ni yapi hayo ya serikali ya mapinduzi ambayo mliyakubali kikatiba leo yawe ya Zanzibar? na yapi ni ya bara. Haya nambie wakati Mwinyi alipokuwa rais alikuwa akiingilia maswala ya bara au... Mbona nyie mnaingilia kila siku ya bara kwa kutumia kiti cha muungano na hatusemi..
      Mkuu Mkandara
      Tanzania ina states ngapi? nitajie kwa majina.

      Muungano wa Tanzania una wanachama wangapi? Nitajie kwa majina.
      Je unaona usanii wa muungano wetu?

      US ni muungano wa states ngapi? Zinaeleweka kwa majina?
      UK ni muungano wa nchi/ states ngapi? Zinajulikana kwa majina?

      Je Kiini macho cha Tanzania kimeundwa na nchi/ states ngapi?

      Dhana ya serikali kuu kwa Tanzania. Ifafanue.

      Serikali ya Muungano ina mamlaka yake?
      Serikali ya Tanganyika ina mamlaka yake?
      Serikali ya Zanzibar ina mamlaka yake?

      Je umewahi kusikia kuwa Tanzania ina mamlaka tatu za kisheria?
      Hint, mambo ya Muungano, Mambo ya bara(Tanganyika) mambo ya Zanzibar.

      Je hutaki kukubali kuwa Muungano huu wa Tz ni mazingaombwe?

      Mkuu Mkandara huu mfano wa mke na mume / baba na mama unaupenda sana unapozungumzia Muungano.
      Je EAC nayo ni ndoa nyengine? Unaelewa kuwa hatimae lengo ni kuunda shirikisho la Afrika ya Mashariki. Huku pia utatumia lugha ya mke na mume?

      Halafu mkuu, ni lazima mtu anayeelezea mizengwe ya Muungano awe Mzanzibari? Muomani au mwarabu,sultani?
      Ona tayari unamwita MziziMkavu, ninyi wazanzibari, mta....

      Prof Shivji au Lissu wanapoonesha dosari za muungano huwa wanabadilika na kuwa wazanzibari?
      Mkandara and MziziMkavu like this.

    22. #39
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Mkandara
      Sawa wewe chukulia porojo lakini ndio facts.. watu mil 2 wanaweza sana ku benefit kwa soko la watu mil 40 kuuza mali zao bila ushuru wa kuingiza mali, lakini Bara hawahitaji soko la Zanzibar, think about that jinsi gani tunavyowapa taabu wakenya na Waganda. Tuvunje muungano mjifungie wenyewe halafu tutaona huo mzunguko ndani kama utaweza kuwasaidia kiuchumi.

      Haya nambie ni kiongozi gani anayetaka muungano uvunjike lakini pasiwepo na mkataba mwingine...Maana bara hatutaki mkataba wowote na Zanzibar zaidi ya muungano au tuvunje muungano.. wape mtihani huu viongozi wa Zanzibar halafu waje na jibu.. Nakuapia hutalipata.

      Wewe mwambie kiongozi yeyote wa Zanzibar:-
      1. Tuvunje muungano na hakuna ushirika wowote isipokuwa ule wa EA
      2. Tuendelee na Muungano uliopo turekebishe tu kuwa na serikali tatu kila upande ujitegemee. This is what Mainland offer hakuna zaidi wala pungufu.
      Hakuna Kiongozi wa Serikali iliyopo Madarakani anaye zungumzia Kuvunjika kwa Muungano mpaka sasa mkuu Mkandara. Wanaye Zungumzia Suala la Kuvunja Muungano ni wananchi walala hoi Masikini

      Wazawa wa KiZanzibar ndio wanaotaka huo Muungano uvunjike wananchi wamechoshwa na Kero za Muungano mimi niliwahi kuwauliza Wa Zanzibar munachotaka kitu gani wakasema hatutaki Muungano tunachotaka tuwe huru wa kujiamuliwa mambo

      yetu wenyewe nikasema lakini nyinyi mupo wachache mpaka suala hilo walikubali Wenzenu wa Tanganyika walinirukia kiasi cha kutaka kunipiga na kusema kwenda zako wewe na hao Wa Tanganyika sisi tumesha choka na huo Muungano wenu

      tunachotaka tuwe huru Hatuutaki huo Muungano sasa Mkuu ikiwa kama ni wewe uliye wahoji hao Wa Zanzibar na hawautaki huo muungano utasema kitu gani Mkuu Mkandara
      Mkandara and Ibambasi like this.
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    23. #40
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8144
      Likes Given
      26620

      Default Re: Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

      Quote By Dezo
      Wewe ni aibu hata kukujibu lakini wacha nikujibu tu. Wewe kenge unatoka mkowa gani wa hiyo Bongo chafu na jee mkowa wako una haya yafuatayo. Serikali kamili, Mawaziri, Wimbo wa Taifa, Jumba la Bunge, Raisi, Mahakama kuu na mipaka, Na jee hicho kakimkowa wako kishawahi kuwa na kiti Umoja wa Mataifa. Ndomaana nikasema aibu hata kukujibu wewe Sofulo.
      Mkuu acha Matusi hapa hatuzungumzi mambo ya matusi tunashauriana kuhusu suala la Muungano na hatima yake kama wewe huwezi malumbano ya siasa nenda kalumbane mambo ya Simba na Yanga nani ni Kiboko yake. Jibu kwa heshima na tadhima usijibu kwa kuleta chuki zako utakula BAN Mkuu jiheshimu utaheshimiwa usilete maneno ya Pumba hapa mkuu Dezo
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...