Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake...

    Report Post
    Page 3 of 3 FirstFirst 123
    Results 41 to 47 of 47
    1. #1
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 4,157
      Rep Power : 1847
      Likes Received
      1431
      Likes Given
      1539

      Default Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake...

      ....Katika kile kinachoonekana kama ni kuanza kwa mbio za uenyekiti wa UWT kati ya wagombea wakubwa wawili yaani Bi Anne Kilango na Bi Sophia Simba hali imeanza kuwa mbaya kwa Bi Anne Kilango. Taarifa zilizotoka leo zinadai kuwa Bi Anne Kilango amekusanya ameanza rafu kwa kukusanya pesa kiwango kikubwa kwa ajili ya kugawa takrima aka rushwa. Na fununu zinasema kuwa wanaume wengi wako nyuma yake kuliko hata wanawake na lengo ni kuhakikisha kuwa Bi Sophia Simba anang'olewa kwenye kiti kile.

      ....Itakumbukwa kuwa ugomvi na kusuguana kwa hawa wagombea wawili akujaanza leo wala jana, kumeanza tangu ambapo Bi Sophia Simba alipomtaja Bi Anne Kilango kama mchangiaji anayeropoka na anajifanya anatetea maslahi ya umma wakati harusi yake na Mzee Malecela ilichangiwa na mafisadi wakubwa. Hoja hii ilimfanya Mzee Malecela asimame na kuomba kuwa kuna wabunge wanapaswa wapelekwe mirembe akimlenge Bi Sophia Simba.

      Source: Magazeti ya leo.

      Habari zaidi:-

      Quote By nngu007
      JUMATATU, AGOSTI 06, 2012 05:48 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

      WAKATI mbio za kuwania nafasi mbalimbali zikiendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi, hali ya mambo imeanza kubadilika. Kubadilika huko, kumeibuka ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambapo mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango baada ya kudaiwa kupewa kitita cha fedha na kampuni moja ya Kichina (jina tunalo).

      Kampuni hiyo, ujenzi wa gati katika Bandari ya Dar es Salaam, inadaiwa kutoa kitita cha fedha, ili kuhakikisha Kilango, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge, anachaguliwa katika kwenye nafasi hiyo.

      Kilango, ambaye hivi sasa amechukua fomu ya kuwania nafasi kwa ajili ya kugombea nafasi ya uenyekiti UWT), anatarajiwa kupambana na mwenyekiti wa sasa, Sophia Simba.

      Kila mmoja wa wabunge ambao, wanasifika kwa kujipambanua kama wabunge wanapinga ufisadi ndani na nje ya Bunge.

      Habari za kuamini zilizoifikia MTANZANIA, zinasema Kilango alianza kazi ya kuwafikia baadhi ya makatibu wa mikoa wa UWT na kuanza kuwashawi, ili wamchague katika nafasi ya Uenyekiti kwa ahadi ya kuondoa ukomo kwa wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM.

      Chanzo hicho, kinasema baadhi ya makatibu wa mikoa ambao hakuwafikia alilazimika kuwapigia simu, ili wamuunge mkono, huku wale wote waliogoma kufanya hivyo, alitumia lugha kali.

      Baadhi ya makatibu hao, waliiambia MTANZANIA na walikiri kupokea fedha kutoka kwa mbunge huyo, kama njia ya ushawishi katika harakati za kuwania nafasi hiyo.

      Taarifa hizo, zinasema nguvu ya fedha ilianza kuonekana Machi 13-14 mkoani Dodoma, baada ya kuandaa semina kwa kukusanya wenyeviti wa wilaya na mikoa, waliokuwa wakihudhuria semina elekezi, kuelekea uchaguzi wa ndani na nafasi ya mwanamke katika kuwania uongozi.

      Katika semina hiyo, inadaiwa mbunge huyo, alitumia nafasi hiyo hasa muda wa jioni kufanya ushawishi kwa viongozi wa mikoa na kuwataka kumchagua.

      Viongozi hao, walisema wakati wa semina hiyo, Kilango alitumia nafasi hiyo na kueleza dhamira yake, huku akitoa vitisho hasa kwa watu wanaodaiwa kupewa Sh 30,000, kwa kila mmoja.

      “Nguvu, aliyonayo mama Kilango, hivi sasa naye ni mmoja wa watu waliopata fedha kutoka kwa kampuni ya Kichina na baada ya kupata alianza kufanya ushawishi kwa wanawake wa UWT, hasa makatibu wa mikoa, lakini hivi sasa tutaona mwisho wake nini.

      “Katika kikao cha Dodoma, nakumbuka tulikusanywa usiku na kupelekwa katika Hoteli ya Fity Six, iliyopo jirani na jengo la Bunge, na kuanza kutupatia kitu kidogo… baada ya hapo alituambia hela ya Mpare haiendi bure na kama ukiichukua na ukienda kinyume utakufa, tena akisema atatulisha yamini wote aliotupa fedha.

      “Alisema Sophia Simba, hatakiwi na wabunge wanawake wa CCM, viongozi wa taifa na hata Rais nae hamtaki, hivyo achaguliwe yeye, kwani ana ushawishi ndani ya Kamati Kuu ya CCM (CC), na amekuwa akiungwa mkono na viongozi wote wa taifa,” kilisema chanzo chetu.

      MTANZANI ilipomtafuta Kilango, ili kupata ukweli juu ya tuhuma hizo, alimtaka mwandishi wa habari hizi kuandika chochote anachokijua dhidi yake.

      Mahojiano kati ya MTANZANIA na mbunge Kilango, yalikuwa kama ifuatavyo;

      MTANZANIA: Habari mama Kilango na pole na majukumu.

      Kilango: asante na nani mwenzangu.

      MTANZANI: ninaitwa …. kubwa nilitaka kufahamu ukweli juu ya tuhuma zinazokukabili kuhusu madai ya kupewa hongo na kampuni moja ya Kichina (jina tunalo), je suala hili lina ukweli wowote?

      Kilango: kijana nasema hivi, andika habari zote kama ulivyosikia, ili Watanzania wajue uchafu wangu,” alisema Kilango na kukata simu.


      snowhite likes this.
      "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"
      "Matatizo hayawezi kutatuliwa na uwezo ule ule mdogo wa watawala wa CCM walioyasababisha"




    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      TUNTEMEKE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2009
      Location : Mombasa
      Posts : 4,504
      Rep Power : 11337
      Likes Received
      323
      Likes Given
      236

      Default

      Quote By andishile
      nimemtaja simba au kilango?nimesema whanawake ambao tayari wana madaraka makubwa na mengi wasigombee!kama unadhani utawashawishi watu kwa kutufanya watoto humu,sahau!
      Sahau wewe NA ushamba wako ....

    4. #42
      andishile's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2012
      Posts : 608
      Rep Power : 481
      Likes Received
      151
      Likes Given
      314

      Default Re: Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake...

      Quote By MWAMI MSIMBI
      Sahau wewe NA ushamba wako ....
      hahahaaa!kazi unayo,usitake kutubebesha msalaba tusioweza kuuubeba!kwa hiyo asiyekubaliana na unayemuombea kura humu JF ni mshamba?

    5. #43
      maria pia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th July 2012
      Posts : 304
      Rep Power : 404
      Likes Received
      31
      Likes Given
      65

      Default

      Quote By Mjomba wa taifa
      CCM inakwenda katika uchaguzi wa viongozi ngazi zote za chama. Tayari warm matches zimeshaanza. Tumemuona Anna Kilango kishavaa Bukta anatroti kuchukua nafasi ya Sophia Simba.

      Hivi CCM wamechekecha akiba zao zote na kuona hao ndio silaha zao? kweli R.I.P CCM 05TH FEBRUARY 1977 - 29TH OCTOBER, 2015 bwana alitoa na bwana anatwaa jina lake lihimidiwe.
      Kudos......nimeipenda hii mkuu,ulikuwa una wazo km langu

    6. #44
      Lokissa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Location : Goba
      Posts : 4,092
      Rep Power : 5807
      Likes Received
      1026
      Likes Given
      2876

      Default Re: Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake...

      ukweli unauma sana
      UWT ilikuwa zamani sio sasa imeshapoteza mwelekeo
      kati ya sophia na kilango hakuna msafi wa kuiongoza UWT
      kwa ufupi sina chama na pia chadema sio chama cha kikanda labda utuambie zito, bob makani na wengineo ni wa kaskazini
      naona huna sera ya maana labda ukaimbe taarabu TOT.
      Quote By MWAMI MSIMBI
      Sio kila Sehemu unaweza kuwataja hao majambazi wenu chanyema.....hapa
      You may know me but you have no Idea who I am !

    7. #45
      maria pia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th July 2012
      Posts : 304
      Rep Power : 404
      Likes Received
      31
      Likes Given
      65

      Default

      Quote By MWAMI MSIMBI
      Mungu atakulaani kufananisha ccm na chama cha mkoa wa kaskazini ....ccm ni chama kubwa bana .....chadema ndio nini maana yake! ...
      Ww acha ujinga wako hapa,do u think Mungu anadhihakiwa kipumbavu!?,kajipange,cdm inaingiaje hapa!pu..afu

    8. Miaka 50

    9. #46
      Mo-TOWN's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2010
      Posts : 1,139
      Rep Power : 5162
      Likes Received
      222
      Likes Given
      84

      Default Re: Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake...

      Hii ndio shida ya siasa za TZ. Mtu ni mbunge bado anawania nafasi zingine. Binafsi napata shida kuamini kama ni kweli kuwa lengo ni kuwatunimikia wananchi.
      IT CAN BE DONE - PLAY YOUR PART!!

    10. #47
      mmwaisoba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th May 2012
      Posts : 430
      Rep Power : 226
      Likes Received
      22
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake...

      mfamaji haishi kutapatapa. Anne Kilango ndiye mwenyekiti mpya wa UWT. Ana watia kiwewe mavuvuzera makuhadi wa Conservative Union. Hapo mjiandae. Nashangaa hii Jamii Forum huwani wana Chadema. Pale wanapozungumzia saana mambo ya CCM ujue wamehisi kuna zahama linakuja dhidi yao. Kama baba paroko alivyozimwa kuwa anawaogopa LOWASA na CHENGE maana hawa ni majabali. Mara wakakurupuka kumpa tafu Sumaye yoote ni kifo cha CHADEMA ndo hofu yao. Subirini uchaguzi wa ndani Chadema mtabaki walewale ZITO HUYOOO ANAPETA NA WATU WAKE.

    Page 3 of 3 FirstFirst 123

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...