Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 29 of 29
    1. #1
      jamhuri ya zanzibar's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 44
      Rep Power : 352
      Likes Received
      9
      Likes Given
      3

      Default Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      Ni vyema kwanza ichukuliwe tahadhari kwamba uzalendo wa mtu kwa pahala alipo si kabila, rangi wala aina ya ngozi. Uzalendo pia haupimwi kwa kigezo cha ni nani aliyetangulia kufika pahala hapo kuliko wenzake, bali uzalendo ni pale mtu alipozaliwa kwa kuwa wazazi wake aliwakuta hapo, au ni pale mtu anapopenda, alipopachagua na kuwamua kua kwao kwa kuhamia, kukaa, kufia na kuzikwa. Kama uzalendo ni kufika mwanzo, basi kamwe wamarekani wasingejisifia uzalendo wao wa kimarekani, kwani wamarekani wa leo wanaofanya idadi kubwa ya wazalendo wa kimarekani ni wahamizi waliotokea Siberia na kuingia Alaska kiasi cha miaka 20 hadi 40 kabla ya Kristo (B.C), wakiwakuta huko wahindi wekundu (Red Indians) wakiwa tayari wameshafanya masikani yao kwa miaka mingi. Lakini hata hivyo mmarekani anabaki kuwa mmarekani tu, iwe anatokana na kizazi cha wahindi wekundu (Red Indians), awe ni mhamizi kutokea Siberia, au awe ni kizazi cha waafrika weusi walohamia huko wakati wa bishara ya utumwa.

      Wazanzibari na uarabu
      Baadhi ya wanahistoria wanadai wahamizi wa mwanzo walikuwa ni wageni kutoka bara la Asia waliokwenda huko kwa sababu za kibiashara. Inadaiwa watu hao walikuwa na asili za Yemen na Oman na walikuwa ni wafuasi wa dini ya kiislamu katika madhehebu ya sunni. Hii ilitokana na kutanda kwa utawala wa Yemen wa wakati huo ambapo hata Oman ilikuwa ni sehemu ya Yemen. Baada ya kuhamia kwao huko mwambaoni watu hao walimtambua mfalme wa Yemen kuwa ndie mtawala wao. Maneno haya yanathibitishwa na mwandishi wa kitabu maarufu na muhimu kinachoelezea safari ya udadisi na biashara katika mwambao wa Bahari ya Hindi, The periplus of erythrean sea, kitabu ambacho mwandishi mwenyewe Wilfred H. Schoff, mfanya biashara wa karne ya kwanza ndie aliefanya safari hiyo, safari ambayo ilimfikisha hadi katika mwambao wa Afrika mashariki. Wahamizi hao wa mwanzo katika mwambao walikuwa wakifanya biashara na wagiriki na warumi na baadae baada ya kuanguka kwa ufalme wa warumi, soko la bidhaa za biashara lilihamia China na India. Bidhaa kubwa kutoka Afrika Mashariki zilikuwa ni meno ya ndovu. Bidhaa zilizokuwa zikiletwa Afrika Mashariki zilikuwa ni silaha, vifaa vya chuma na vitu vya urembo.

      Hoja hii inadai mahusiano ya mapema sana kati ya mwambao wa Afrika ya mashariki na waarabu. Wilfred Schoff anasema katika kitabu chake, The periplus of the erythrean sea kuwa ameukuta mwambao wote wa Afrika mashariki wakati huo ukiwa umeshahamiwa na watu wa asili ya kiarabu tu, na wanamtambua mfalme wa Yemen kuwa ndiye mtawala wao. Schoff anasema kuwa watu aliowakuta wote ni wa asili za watu wasiokuwa waafrika, na hakukuwa na hata alama ya mtu mweusi kwa wakati huo. Kwa hakika Periplus, inayozungumzia mwambao wa Afrika ya mashariki na kuja chini kusini mpaka Zanzibar, haikuwataja kabisa watu weusi. Pia hoja hii inategemea sana maandishi yatokanayo na Giografia ya Ptolemy (mwanagiografia na mnujumu maarufu wa Alexandria). Giografia ya Ptolemy inawazungumzia (wabantu) na kuwepo kwao mwambaoni, lakini ni kusini kabisa ya eneo hilo ndiko wanakotokea, ambako bila shaka ni kusini ya kiasi cha Msumbiji ya sasa, ukija kwa juu kaskazini zaidi ya eneo hilo (la Afrika mashariki), watu waliokuwepo ni wasomali na wa-Ethiopia watupu (Oliver na Fage 1962: 98). Pia madai ya hoja hii yameegemezwa na wakati wa Ibn Batuta, msafiri na mwandishi mashuhuri. Katika maandishi yake Ibn Batuta anadai alipoutembelea mwambao wa Afrika mashariki katika karne ya 14 alishangazwa sana alipowaona waswahili kuwa ni watu waliokuwa na nyumba zao nzuri, waliokuwa wakijuwa kuvaa na kula kama walivyokuwa wazungu wa wakati huo.

      Kwa mujibu wa hoja hizo basi waarabu walikuwepo katika mwambao wa Afrika ya mashariki na Zanzibar kwa zaidi ya miaka 2000 nyuma. Msikiti wa kizimkazi, ni katika mabaki ya kihistoria yaliyo na umri mkubwa zaidi Zanzibar. Msikiti unakisiwa kuwepo hapo si chini ya miaka 900. Msikiti huu unaakisi ustaarabu wa waarabu au wapashia (wa-Iran) ambao walikuwa wameshafanya masikani yao Zanzibar karne nying huko nyuma. Kwenye ukuta wa mihrab wa msikiti huu pameandikwa hivi kwa Kipashia: “hii ni amri ya Kiongozi mtukukufu Sheikh Assayid Abu Imran Musa bin Alhassan bin Muhammad, Mungu ampe maisha marefu na awaangamize maadui wake”



      Kuhusu maneno hayo ya Kipashia katika mihraab kwa mujibu wa hoja hii ni kwamba waarabu hawa walipitia Pashia na kukaa muda mrefu kiasi cha kwamba utamaduni wao wa asili wa kiarabu uliathiriwa na ule wa kishirazi. Ndio maana maandishi ya kwenye mihraab yanaonekana kuwa ni ya mchanganyiko wa lugha mbili (maneno yameandikwa kwa lugha ya Kipashia lakini nambari zimeandikwa kwa kiarabu). Staili ya ujenzi wa msikiti huo pia haitofauiani na zile za misikikiti mengine iliyojengwa na waarabu.

      Wazanzibari na ubantu
      Wanahistoria waounga mkono uarabu kama ndio athari ya mwanzo ya ustaarabu katika mwambao pia hawakuacha kuwazungumza wabantu, ujio wao na uhusiano wao na mwambao wa Afrika ya mashariki. Wabantu ni jamii za waafrika weusi wanaozungumza lugha za kikabila za kiafrika ambao wana asili zao kutokea Afrika ya kati na Afrika ya Kusni. Wanahistoria hawa wanakana kuwepo kwa tarehe rasmi ya uhakika ambapo wabantu walihamia mara ya kwanza Zanzibar, lakini wao wanadai kwamba mpaka mwishoni mwa mwaka wa 700 kabla ya kristo (B.C ) kwa yakini sio Zanzibar tu, bali Afrika mashariki yote kiujumla ilikuwa ishavumbuliwa na kuhamiwa na watu wasio na asili ya kiafrika. Wao wanasisitiza kwamba ni vigumu kukisia ni karne ngapi nyuma hasa wabantu walifika katika mwambao wa Afrika ya mashariki na hatimae wakafika Unguja na Pemba lakini wanachoweza kusema ni kwamba walifika huko baada ya mwambao kwisha kuvumbuliwa tayari na watu wa asili zisizokuwa za kiafrika. Mwambao wa Afrika mashariki kwa mujibu wa wanahistoria hawa ulikuwa unafahamika na wenyeji wa Arabuni katika karne ya 8 kabla ya Kristo. Kumbukumbu zao zinadai pia kwamba taifa la Kiarabu la Ausan ambalo lilisambaratika mwaka wa 700 Kabla ya Kristo, lilifanya biasharana na bila shaka lilimiliki sehemu ya mwambao (Gray 1962: 10-11).

      Utafiti wao unadai kwamba katika nyakati za karne ya 16 (16th century AD) ndani ya ukoloni wa kireno ndipo hasa mababu na mabibi wa wazanzibari wa asili za kibantu walipoanza kuingia katika visiwa vya Zanzibar, zaidi kwa kupitia biashara ya utumwa. Kutokea hapo sasa uingiaji wa wabantu kutoka Mrima kuingia Zanzibar ukawa ni wa kawaida na kwa wingi. Hata baharia, mpelelezi wa kireno, Vasco Dagama, aliekuwa akifanya upelelezi sehemu mbalimbali kwa lengo la kuweka ukoloni, mwishoni mwa karne ya 10 (10th century) aliyefika katika pwani ya Afrika ya mashariki na anakiri aliwakuta huko watu wa mwambao kuwa ni wale watu wenye ustaarabu wa jahazi (dhow civilization) tu, na akasisitiza kuwa watu hao walikuwa wanauwelewa vyema ustaarabu wa ubaharia wa jahazi kama alivyokuwa akiujua yeye (Issa 1999).

      Madai yao zaidi ni kwamba mara baada ya kuhamia wabantu wakitokea Mrima, walioana na wenyeji wale walioitwa wahadimu, wapemba, na watumbatu na kupatikana watoto machotara. Machotara hawa ndio wale waitwao waswahili. Wakijaribu kutoa uthibitisho wao wanadai hata Mwinyi mkuu wa Dunga anaonekana nae alihemkwa na mabibi wa kibantu na kuzaa watoto machotara. Ipo picha maarufu sana kwa kumbukumbu za kihistoria, inamuonyesha Mwinyi mkuu wa Dunga (ambae bado anatambuliwa kama Mshirazi), yeye amekozea maumbile ya kiarabu, akiwa na mtoto wake ambae ni chotara, ameshapoteza ule uarabu wa baba yake na amekozea zaidi ubantu wa mama yake.


      Hata hivyo Ipo mijadala mirefu miongoni mwa wanahistoria na wanasiasa wanaodai kwamba wenyeji wa mwanzo wa Zanzibar walikuwa wabantu kutokea bara hususan Tanganyika. Miongoni mwa wanahistoria hao ni Matokke na Mrina. Katika hoja hii panadaiwa kwamba wavuvi kutoka bara walifika na kuhamia sehemu mbali mbali za visiwani na matokeo yake sehemu hizi zikakuwa na kufanyika vijiji. Kutokana na upokeaji wa wageni zaidi, vijiji navyo vikakuwa zaidi na watu wakaendelea kuzaliana. Kwa ari ya kutaka kuyamudu mazingira yao, watu hawa waliweza kujipatia maarifa, ujuzi na uwezo wa kujenga vibanda vidogo vidogo na kuimarisha vitendea kazi vyao. Sambamba na hoja hiyo yapo pia madai kwamba wahamizi wa mwanzo wa Zanzibar waliingia sehemu ya kusini Unguja wakitokea katika sehemu nyegine za mwambao wa Afrika ya Mashariki. Baadhi ya masimulizi ya watu wa Muyuni yanadai watu wa mwanzo wa Muyuni walikuwa ni wagunya. Wagunya hawa walitokea katika mwambao wa Kenya ambao pi inasemekana walihamia na maeneo ya Bwejuu. Halkadhalika baadhi ya watu wa Paje na Jambiani inaaminika walitokea Pate na Rufiji ambapo hapo mwanzoni walikuwa ni wavuvi wa dago.

      Wazanzibari na ushirazi
      Kuna utata mwingi kuhusiana na historia ya washirazi na kuwepo kwao katika Zanzibar na Afrika ya Mashariki. Mengi yameandikwa na kusemwa kuhusiana na washirazi. Wako wanaosema washirazi na ujio wao sio kitu cha ukweli bali ni hadithi za kubuni. Kwa mujibu wa wanahistoria hawa neno ushirazi lilizushwa na kuungwa mkono na wakoloni ili kukidhi matakwa ya kurahisisha utawala kwa misingi ya ukabila. Miongoni mwa hoja wanazozitoa wanahistoria hawa akiwemo S. J. Kirkman ni vile kukosekana kwa athari za maingiliano ya kimila za kishirazi na waswahili pamoja na kukosekana kwa matumizi ya lugha ya kipashia katika utamaduni wa Kiswahili. Hata hivyo mwanahistoria B. Kurmm amegundua athari ya maneno 78 ya kipashia katika lugha ya Kiswahili.

      Pia mwanahistoria T. Spear anawaelezea washirazi kama sio kabila la watu bali ni kundi la watu wa tabaka la wafanyabiashara na matajiri. Bila shaka kundi hilo linatokana na maingiliano kati ya wenyeji wa sehemu za Afrika Mashariki na wageni. Kwa mujibu wa Spear kwa hivyo, neno shirazi linahusiana na tabaka la matajiri au watawala. Akifafanua Bwana Spear anasema washirazi sio wapashia bali ni waafrika au ni wafanyabiashara wenye asili ya kiarabu. Makabila ya watawala (mamwinyi) wa watu hao walioitwa washirazi yanatoa uthibitisho wa hoja ya Spear. Makabila ya mamwinyi wa washirazi ni kama vile Al-alawi, Al-bajuni, Al-addibawy, Al-bahasany, Al-ahdali, Al-attasi n.k, ambayo bila shaka ni makabila ya waarabu na sio waajemi (Issa 1999).

      Pamoja na hoja hizo zinazoukataa ushirazi pia upo ushahidi wa kuthibitisha kuwepo kwa ushirazi. Moja ni matumizi ya kalenda kama zile wanazotumia washirazi. Sio Zanzibar tu bali hata maeneo mengine ya Afrika Masharika mpaka leo kuna watu wanaofuata kalenda zao za kinujumu mbali ya zile za kiislamu kwa mfano Nairuzi, yaani siku ya mwaka au mwaka kogwa. Siku hiyo ya mwanzo wa mwaka wa kishirazi hufuatana na tarehe 21 Machi ambapo urefu wa mchana na usiku hulingana. Sherehe za mwaka kogwa Unguja husherehekewa kwa kukoga baharini kama njia ya kujitoharisha mwili, kuzima moto wa wa zamani na kuwasha moto mpya kwa kutumia fimbo mambo ambayo yanalingana mno na sherehe za kishirazi. Msikiti wa kizimkazi unaokisiwa kuwa na miaka 900 tangu kujengwa kwake na maneno ya lugha ya kipashia katika mihraab yake unaakisi ujio wa washirazi mapema sana katika visiwa hivi.

      Uchambuzi wa takwimu za kuzaliwa zilizofanywa kuanzia mwaka 1953 hadi 1963 ambapo wazanzibari walitakiwa kuwaandikisha watoto wao kwa makabila yao halisi zinaonyesha wenyeji wa visiwani walijitambulisha miongoni mwa makabila matatu. Makabila yenyewe ni wahadimu, watumbatu na washirazi. Makabila ya wapemba na waswahili ambayo yalitumika kabla ya hapo hayakutambuliwa tena kama makabila. Thuluthi moja ya wenyeji wa Unguja na takriban nusu ya wapemba walijitambulisha kama washirazi. Ushirazi ulionekana kwa hivyo kushamiri zaidi na kuota mizizi katika kisiwa cha Pemba. Katika kipindi cha karne ya 8 hadi ya 15 ndipo washrazi wanapodhaniwa kuwa waliwasili. Washirazi ndio waliokuwa wafanya biashara wakubwa katika pwani nzima ya Afrika mashariki na visiwa vyake vya Unguja, Pemba na Mafia katika kipindi hicho jambo ambalo lilisababisha kukua sana kwa miji hiyo. Wahadimu, wapemba (wadiba) na watumbatu ndio hasa historia inaowaita washirazi wa Unguja na Pemba. Wahadimu walikuwepo katika maeneo ya Kaskazini ya kisiwa cha Unguja na walikuwa wakiishi kwa wingi katika maeneo ya Nungwi, Kijini, Muyuni, Pwani mchangani, Chwaka, Bwejuu, Makunduchi, Kizimkazi na Uzi. Mji mkuu, au mji muhimu wa wahadimu ulikuwa ni Dunga. Watumbatu walikuwa wakiishi katika maeneo ya kisiwa cha Tumbatu. Pia watumbatu walionekana kuishi maeneo kama vile Donge, Bumbwini na Mwanda (Ingrams 1962).

      Wadiba (wapemba) ambao ndio wenyeji wa kisiwa cha Pemba pia wananasibishwa na washirazi. Hata hivyo wadiba pia wananasibishwa na waarabu. Kwa mujibu wa wanahistoria hawa, wadiba ni watu walio na asili zao kutokea katika mji wa Diba. Diba ni mji ulioko baina ya Oman na Sharjah. Inasemekana kuwa uko mji mwengine unaoitwa Diba maeneo ya bara Hindi, lakini hiyo sio Diba ya asili. Kwa kutilia nguvu hoja yao hiyo ni mitindo yao ya misikiti na majengo waliojenga huko Pemba katika masikani yao katika miji kama vile Pujini na Kengeja ni sawa na ile ya Diba ya Uarabuni. Ushahidi wa mabaki ya majengo ya kale na vihame vya Mkamandume ndio wanaotumia kuyakinisha madai yao haya. Wanahistora hawa hawakanushi ushirazi bali wanadai kwamba mji wa Shirazi ulikuwa ni kituo chao walichopitia na kuishi hapo wakitokea bara arabu kabla ya safari yao ya kuja katika mwambao wa Afrika ya mashariki na visiwa vya Zanzibar.

      Watu hawa, yaani watumbatu, wahadimu, wapemba (wadiba) mwanzoni kabisa baada ya uhamiaji wao, walikuwa wakiishi kwa mifumo ya tawala za kienyeji za umwinyi mkuu. Waliishi katika tawala zao za kienyeji zinazojitegemea. Watumbatu walikuwa na Mwinyi mkuu wao, wahadimu walikuwa na Mwinyi mkuu wao na wapemba (wadiba) walikuwa na Mwinyi mkuu wao. Mwinyi mkuu wa mwanzo wa Dunga Hassan Bin Abdalla anadhaniwa kutawala katika karne ya 13 na Mwinyi mkuu wa mwisho Ahmed Bin Muhammed (angalia picha hapo chini), ambaye alikuwa mashuhuri zaidi na ambaye ndie aliyejenga kasri iliyopo Dunga anadhaniwa kutawala kuanzia mwaka 1728 hadi 1865. Mwinyi mkuu wa wapemba anaekumbukwa zaidi na historia ni Mkamandume. Baadhi ya wakati tawala hizi zilikuwa na masikizano na baadhi ya wakati zilikuwa na migogoro ya hapa na pale.

      Totauti kidogo na kisiwa cha Unguja ambacho kilikuwa chini ya tawala zaidi ya moja za kienyeji, Pemba yote kwa upande wake ilikuwa chini ya Mwinyi mkuu mmoja tu wa kishirazi. Taifa la kisiwa cha Pemba liliasisiwa mwaka 1550 chini ya utawala wa Mwinyi mkuu. Hichi ndio kipindi peke yake katika historia ambapo Pemba ilijitegemea yenyewe kiutawala. Mmmoja wa mamwinyi hao anaekumbukwa zaidi na historia ni Mwinyi mkuu wa Pujini Pemba, mtawala wa kienyeji wa washirazi. Huyu alikuwa akiitwa, Mohammed bin Abdulrahman Al-addibawy. Huyu ndiye yule aliyekuwa akijulikana kwa jina la umaarufu la “Mkamandume”. Kimakosa jina hili lilifahamika na kuelezwa vibaya na baadhi ya walioandika historia au pia inawezekana waliandika kwa makusudi kwa malengo yao binafsi. Wapotoshaji hawa wa historia wameandika kwamba aliitwa mkamandume kwa kuwa mtawala huyu akiwafanyia vibaya wanaume wenzake kwa kuwavuta uume wao kama anavyokamwa ng’ombe maziwa.. Huu ni upotoshaji wa historia na dharau kwa wahenga hawa wa wapemba. Vikongwe wengi wa kipemba wanakataa kabisa kupokea ngano hizo kutoka kwa mababu na mabibi zao. Kauli nzito ni kwamba neno “mkama” linatoka kwenye neno la kiarabu “maqaam” kwa maana ya nafasi ya cheo. Kwa mswahili wa kawida atakubaliana na mimi kwamba neno “Mkamandume” halina jengo la kiswahili kizuri (fasaha) bali neno “Makamo wa madume” amabalo ndio asili yake lina jingo la Kiswahili kizuri ambalo bila shaka ndio neno la awali na maana halisi iliyokusudiwa kwa mtawala huyu. Kwa hivyo neno Mkamandume lilikuwa na maana ya kuwa huyu bwana alikuwa juu zaidi kwa cheo na utukufu kuliko watu wote waliokuwa chini ya utawala wake. Kwa kiingereza ni kwamba alikuwa “above men’ na sio “milker of men”

      Wazanzibari ni jamii ya asili na ustaarabu mseto (cosmopolitan society)
      Kabla ya kuja mkoloni wa kiingereza Zanzibar, wazanzibari wa asili mbali mbali kama walivyo hivi sasa walikuwa wakiishi kwa mapenzi makubwa bila ya chuki za ukabila na urangi, au kwa lugha nyengine, waliishi bila ya mimi ni nani na wewe na nani. Muengereza alikuja kuwaundia wazanzibari vyama vya kikabila na urangi. Vyama hivyo yaani jumuiya za kikabila ni kama vile Arab association, Shirazi association, African association, Indian association na jumuiya nyengine. Wazanzibari nao wakavishabikia vyama hivi vya kikabila na kila mmoja akawacha kupigania maslahi ya uzanzibari na akapigania maslahi ya kabila lake. Lakini hayo yalikuwa ni mafanikio makubwa kwa Muengereza, kwani ni sera yake muhimu ya ukoloni ya wagawe uwatawale (divide and rule).Kuanzia harakati za kutafuta uhuru chama cha ASP na viongozi wake akiwemo kiongozi mkuu Karume waliukejeli na kuupiga vita ukweli kwamba wazanzibari ni watu wa asili na ustaarabu mseto na kujaribu kuyatenga makundi yote ya kizanzibari yalio na asili zake kutoka nje ya bara la Afrika kama vile waarabu, wahindi, magoa nk. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hata washirazi wenye asili zao kutokea Iran ambao ndio wanaofanya asilimia kubwa ya wazanzibari nao walipigwa vita. Kama hilo halitoshi hata wakomoro wenye ngozi nyeupe lakini wenye asili zao kutokea katika bara la Afrika nao walikejeliwa na kukataliwa. Kwa viongozi wa ASP mzanzibari namba moja au mzanzibari asilia na mwenye hadhi kubwa ni lazima awe mwafrika mwenye ngozi nyeusi. ASP iliupigia kelele, kuunadi na kuutukuza uafrika pamoja na ngozi nyeusi na kuzidharau jamii zote za kizanzibari zilizobaki.

      Kabla ya mapinduzi ASP na viongozi wake walijaribu kuwaheshimu washirazi wakifahamu bila ya wao na wingi wao ushindi kwa ASP ingelikuwa ndoto. Mara tu baada ya mapinduzi na ASP kushika hatamu chuki dhidi ya ushirazi na washirazi zikadhihirika. Serikali ya Karume ilipambwa na viongozi wenye asili zao kutokea bara hususan Tanganyika. Hii inajionyesha hata kwa majemedari wa mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzo lilikuwa na watu wengi zaidi wenye asili zao kutokea bara. Hii iliwafanya wafikirie kwamba serikali ya mapinduzi ni ya wazanzibari wa asili za bara na waliobaki ni watu wa daraja la pili. Baada ya mapinduzi Karume aliwataka watu wote wenye asili ya kikomoro kuomba uzanzibari (Burgess 2009:204).

      Kwa kuwa Karume mwenyewe alikuwa na asili yake kutokea Malawi aliwaogopa sana washirazi. Katika akili yake Karume aliwaona washirazi ni watu wanaoringa na kujidai kama wazanzibari halisi. Hivyo basi aliwalazimisha washirazi nao kubadilisha makabila yao. Washirazi wengi walilikataa agizo hilo la Karume hususan wapemba. Wengi wa washirazi Pemba walisema wao hawana kabila jengine mbadala mpaka Karume atakapowapatia baba wengine. Hivyo basi hali halisi ya ugozi na ukabila ilipamba moto zaidi baada ya mapinduzi kuliko kabla. Wapigaji na wachezaji wa ngoma hiyo chafu ya ukabila baada ya mapinduzi walikuwa viongozi wa serikali ya mapinduzi na wajumbe wa baraza la mapinduzi la mwanzo kama vile Karume mwenyewe, Seif Bakari na Abdalla Said Natepe, Mungu awarehemu.
      Baada ya mapinduzi vitabu vyote vya historia vilivyofundisha ukweli kuhusu Zanzibar, maisha ya masultani, na urithi wa ustaarabu mseto vilichomwa moto (Burgess 2009). Tukio moja la uchomaji huo lilifanyika eneo la Lumumba Unguja mbele ya macho ya maelfu ya watu. Badala yake mwenyekiti wa Youth league, Seif Bakari aliandika kitabu kipya kilichokua kikisomeshewa watoto mashuleni. Katika kitabu chake hicho, Seif Bakari anadai kuwa yote yaliopita kabla ya mapinduzi yalikuwa si chochote bali ni dhiki na dhuluma. Katika kuzidi kuchonga chuki miongoni mwa wazanzibari weusi dhidi ya wenye ngozi nyeupe, Abdalla Said Natepe ambae ni mjumbe wa mwanzo wa baraza la mapinduzi na mjumbe wa kamati ya watu 14 alikuwa akifanya mikutano ya hadhara kuwaaambia watu hadithi za uzushi. Miongoni mwa hadithi hizo ni kuwa waarabu waliwalazimisha waafrika kupanda minazi kisha wakawa wanajifundishia shabaha kwa kuwatungua kwa risasi. Hadithi nyengine ni kuwa waarabu waliwalazimisha wanawake wa kiafrika kufyagia barabara kwa maziwa yao na waja wazito wa kiafrika walip[asuliwa ili bibi wa kiarabu ajue mtoto amekaaje tumboni. Mafundisho haya yamekuwa yakitolewa mashuleni kwa muda mrefu ili kutia sumu katika akili za watoto wa kishirazi na kifrika dhidi ya waarabu.

      Nyimbo za uafrika dhidi ya asili nyengine zote ziliendelea kuimbwa ndani serikali ya mapinduzi kupitia warithi wake wenye misimamo mikali ya uhafidhina wa ugozi na umapinduzi kwa lengo la kulinda malengo na uhalali wa mapinduzi hayo. Kuthibitisha kasi na nguvu za uhafidhina huu na chuki dhidi ya watu wasiokuwa na asili ya kiafrika ndani ya Zanzibar ni maneno ya Omar Ramadhani Mapuri, ambae yeye mwenyewe ana asili yake kutoka Tanzania bara, aliyekuwa Waziri wa elimu na Naibu waziri kiongozi katika awamu ya nne ya Rais Salmin Amour. Kupitia kitabu chake, Zanzibar Revolution, Achievements and Prospects, kitabu ambacho kinazungumzia kiwango cha juu cha ukabila katika enzi za ustaarabu duniani, Mapuri ameweka wazi hisia zake kali dhidi ya watu wasiokua waafrika ndani ya Zanzibar. Lengo kuu la Mapuri katika kitabu chake ni kuwataka wazanzibari wenye asili za kiafrika kuungana dhidi ya kile anachokiita chokochoko na uchokozi wa nchi za magharibi na waarabu ambao chini kwa chini kwa mujibu wa Mapuri wanataka kurudisha tena ushawishi wao Zanzibar kama ilivyokuwa kabla ya mapinduzi. Umoja huu ambao Mapuri anawaasa wazanzibari ndio ule ule uliotumika katika harakati za uhuru na mapinduizi ya 1964.Katika kitabu chake pia Mapuri anakana kwa nguvu zote mauwaji yaliyofanywa na mapinduzi ya 1964 na kwa mujibu wa mawazo yake yale yanayoripotiwa kuwa ni upotezaji wa roho za watu kwa mgongo wa mapinduzi ya 1964 ni uongo mtupu na kusisitiza kwamba watu waliokufa kutokana na mapinduzi hayo ni wachache mno. Hata hivyo katika kitabu chake anadai kuwepo kwa nyaraka zinazobainisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani iliyopinduliwa ya kutaka kuuwa raia wengi wa kiafrika kama ni kulipiza kisasi kwa mauwaji ya waarabu waliouliwa kufuatia uchaguzi wa juni 1961 ijapokuwa hakubainisha katika kitabu chake nyaraka hizo zilipo. Mapuri anadai nyaraka hizo zinathibitisha kwamba serikali ilipanga kuuwa waafrika sitini (60) kwa kila mwarabu mmoja aliyeuliwa Juni 1961.

      Mapuri pia anadai nyaraka hizo zinathitisha azma ya serikali ya Shamte na Sultani kuzitaifisha mali zote za waafrika wasio na asili za kizanzibari. Hakumalizia hapo Mapuri pia ameandika kwamba Serikali ya Shamte ilikuwa na lengo la kuwafanya watumwa wazanzibari wote wenye asili ya kiafrika na hatimae Zanzibar kutangazwa kama ardhi ya waarabu. Kikubwa zaidi ambacho pia Mapuri amewatanabahisha wazanzibari katika kitabu chake ni azma ya Serikali ya Shamte iliyopinduliwa kuwauwa watoto wote wa asili ya kiafrika na wanawake wenye asili ya kiafrika kulazimishwa kuolewa na waarabu kwa malengo ya kutokomeza ngozi nyeusi Zanzibar. Alichokifanya Mapuri bila shaka lilikuwa si jambo geni katika historia ya Zanzibar. Ni marudio tu ya yale yalioanzia miaka ya 1960 ya mapambano ya makabila katika kugombania kumezwa, kufunikwa au kutokomezwa na makabila mengine.
      Ni jambo la kushangaza mno kwa enzi ambayo vuguvugu la kihistoria la ukabila na uasili tayari limeshasahaulika, kiongozi wa ngazi za juu katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anapika upya migawanyiko ya wazanzibari kwa misingi ya rangi, ngozi na wanakotokea mababu zao. Kiongozi kama huyu bila shaka ana dhima kubwa ya kuwaunganisha wazanzibari walio na asili na utamaduni wa kila namna karibu kutoka pembe zote za dunia lakini badala yake anashajihisha na kuhimiza umoja na muungano wa baadhi ya wazanzibari dhidi ya wenzao. Hata hivyo sio Mapuri peke yake katika viongozi wa leo wanaopiga kelele za ukabila na uasili ndani ya Zanzibar ya kisasa. Wapo wenzake Mapuri ambao wao wamefika mbali zaidi kwa kudai kwamba vijukuu na vinying’inya vya waarabu hawapaswi kupewa madaraka ya Zanzibar kwa kunasibika kwao na kabila la wapinga mapinduzi ya 1964. Katika kitabu chake, Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru, Harith Ghassany analizungumzia hivi suala hili.

      Fikra ya uzalendo ya Pan-Africanism ambayo ilikuwa ikipigiwa kelele na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilikuwa na misingi kwamba kila asiye “Muafrika” ni mgeni (wakuja) Afrika na kwa maana hiyo pia ni mgeni Zanzibar hata kama alizaliwa na alikuwa na mizizi mirefu na mipana ndani ya Zanzibar. Kinyume chake kila aliyekuwa ana asili ya Kiafrika (kibantu) na hata kama hakuzaliwa na wala hana mizizi mirefu ndani ya Zanzibar basi ana haki zaidi juu ya kuweza kutawala kwa sababu tu ni “Muafrika.” Hapa sharti ifahamike kwanza kuwa neno “Afrika” linatokana na neno Ifriqiya, ambayo wanahistoria wanathibitisha ilikuwa ni jimbo la Kaskazini ya Afrika katika nchi ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la Tunisia. Ibn Khaldun, mwanafalsafa wa historia maarufu duniani na baba wa sayansi ya jamii (sociologist) aliyeishi miaka 676 nyuma, amemzungumza katika kitabu chake Mfalme wa zamani wa Yemen Afriqus Bin Qays Bin Sayfi. Kwa mujibu wa Ibn Khaldum Mfalme huyu aliishi wakati wa Nabii Musa au labda kidogo kabla yake. Ibn Khaldum anathibitisha kuwepo kwa mfalme huyo kutoka Yemen ambaye jina lake hilo inawezekana sana likawa moja wapo wa asili ya jina “Afrika”. Mawazo yaliyoenezwa kila upande ni kwamba Zanzibar ni ya Muafrika mweusi mwenye asili ya bara peke yake kuliko Muafrika mwingine yeyote hata kama amezalika huko Zanzibar kwa dahari nyingi. Mawazo haya yanatokana na fikra kuwa “Bara la Waafrika” ni Bara la watu weusi tu. Watu weusi hao tena ni wale wanaotokana na asili ya Kibantu na Wabantu hao bila shaka wawe hawana kabisa asili au uhusiano wowote na Waarabu. Wenye mawazo haya bila shaka walisahau kuwa wanalitenga kundi kubwa la Waafrika wa Kaskazani katika nchi za Ethiopia, Somalia, Djibouti, Eritrea na Mauritius. Halkadhalika mawazo hayo yamewatenga wazungu wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Kenya. Pia mawazo hayo yamewatenga Mayahudi na Wahindi wazalendo wa Afrika, na makabila yote ya watu ambayo yana chimbuko lake katika bara hili” (Gassany 2010).

      Wazanzibari ni watu walio na asili zao nyingi na ustaarabu mchanganyiko ulizoanzia mbali. Asili za kiarabu, ki-pashia, kihindi, kitanganyika, kiganda, kikenya, kimsumbiji, kikomoro, kinyasa, kisumeri, kiassiri, kisomali, kiabisini, kifoniki, kidiba, kidebule, kireno, kibaluchi, kikurdi, kijojia, kichina, kisrilanka nk Wengi wao ni machotara, hakuna awezae kukaza mdomo akamtukana mbantu, akija akitanabahi kumbe kamtukana babu yake, au akakaza mdomo akamtukana mwarabu, akitanabahi kamtukana mama yake. Uarabu, ubantu, uhindi, na asili nyengine zote za wazanzibari zilizopo kamwe hazibandukani na uzanzibari na bila ya kundi moja tu katika hayo ni sawa na mwanadamu asivyokamilika akikosa baadhi ya viungo vyake.
      Last edited by jamhuri ya zanzibar; 5th August 2012 at 19:14.
      MziziMkavu likes this.

    2. Study Abroad

    3. #21
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3256
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      Kwanza nina ushauri wa bure tu, ukiona vyema chukua, hutaki wacha: Wakati wa ku"google" jaribu kusoma kile unachokikopi na kupaste. Hebu angalia hii:
      Wahadimu walikuwepo katika maeneo ya Kaskazini ya kisiwa cha Unguja na walikuwa wakiishi kwa wingi katika maeneo ya Nungwi, Kijini, Muyuni, Pwani mchangani, Chwaka,Bwejuu, Makunduchi, Kizimkazi na Uzi.

      Hapa inaonesha mwandishi haijui Unguja hata iko wapi sikwambii kujua kusini kaskazini.

      La pili, kwa kutumia logic tu, iweje kuwa rahisi kwa Wapashia au Waomani kuweza kufika Kizimkazi kwanza (fikiria masafa na mazingira ya bahari) kabla mtu anayetoka Bagamoyo? Pia angalia umbali wa Wagunya kutoka Pate/Lamu vs Wamanyema kutoka Mrima, ni nani yupo karibu kijiografia?

      Tatu, kwa mawazo yangu, longolongo zote hizi ni historia za kupikwa na kama ilivyo kawaida ya historia, haiachi kuwa na maslahi ndani iwe hasi au chanya. Kwangu mimi Wilfred H. Schoff na T.Spear hawana tafauti na Mapuri, wote waliandika kwa maslahi yao.

      Mwisho (satirically), niliposoma hilo la "Milker of men" ndio nimetanabahi kuwa kumbe "uCameroon" haukuanza leo.
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    4. #22
      njiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Location : ax^2+bx+c=0
      Posts : 4,942
      Rep Power : 2365
      Likes Received
      950
      Likes Given
      171

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      Quote By Nicholas
      Mwandishi kajitahidi kuandika vizuri na reference za kuvutia ila shida hakutaka kuwa honest baadhi ya maeneo.Miaka haya yakitokea si Ukristu au islam ulikuwa na nafasi .Ila zohorostan ,Uhindu na uyahudi ambao haukusambaa walakutajwa sana katika biashara nje ya mashariki ya Kati.

      Greece na Rome Hazikutawala kwa kipindi kimoja Greece ilipoanguka ndipo rome ikaingia na by that time hapakuwa na Uislam katika bara Arabia.Persian na Walebanon wa mwanzo au phoenian ndio walikuwa wajuzi wa baharini.So suala la SUNNI na SHIA halikuwepo.Hata ukristu wenyewe haukuwa umefika hapo ulipo ingawa baadhi ya persian walishakuwa wakristu wengine walikuwa na dini ya asili ya Iran.

      Sababu ya msingi ya kuinuka kwa biashara ya uchina,india ilikuwa kwa vile kulishakuwa na biashara kati ya Hizo nchi na Africa mashariki ,na baadaye watu wa ulaya wakawa wakienda kule wakidhani kuwa dhahabu,chuma, na vitu vingine vilikuwa vikipatika kule bila kujua walikuwa madalali au waongeza dhamani tuu.

      Na kuna historia inayotia mashaka si tuu wahindi hata wachina , mtu mweusi alishawahi kushika himaya katika bara hindi na uchina.Ila baada ya kuibuka kwa utumwa ndipo vizazi vyao vikaanza banwa na kupotea.


      Ningependa tumi alogic zaidi hapa kuliko quote ili kuweka sawa tfsiri za huyu mwandishi, mahiri ila pia nayependa tumia keyboard yake kuanza pindihs historia na baadaye tupotee kabisa.Miaka 200 nyuma hata ukihesabu tokea sasa hapakuwa na Ukristu nje ya mashariki ya kati na Maghreb.mwandishi anazo data ila anatafsiri kwa malengo yake.

      Ukisoma Quran tukufu , hadith na Sira pamoja na maandiko mengine ya Kiarabu utaona ya Kuwa utumwa ulianza kabla hata Muhamad hajazaliwa.Na hivyo kufanya ushahidi kuwa Utumwa haukuanzishwa na Uislam, ingawa Baadaye waislam waliokuja baadaye hawakufanya juhudi kubwa kuuzimisha.Ndio maana hiyo miaka 900 unayoinyesha ya msikiti ni matokeo ya vizazi vilivyokuja vikiwa na waislam baada ya uislam kuanza na kuenea hadi uajemi na sehemu nyingie zilizokuwa na ustaarabu wa kikristu ,kiyahudi na Zohor.Na hivyo waajemi wote na walebanon waliokuja walikuja kama waislam na hivyo kukawa na mabadiliko katika tamaduni zao ambazo zlianza kuwa na influence za kairabu kwa kiasi kikubwa.

      There is doubt wewe umegeuza logic hapa, waarabu walikuwa superior na ndio walifanya persian wawe waislam na watanze tumia kiarabu.So huo mchanganyiko ni wazi kuwa waajemi ndio walistruggle katika kiarabu.Na hii hadi eo inaoneka katika nchi nyingi zenye waislam huwa machanganyiko wa kiarabu na lugha nyingine ni mkubwa ila katika nchi za kiarabu kiarabu ndicho hutawala.

      Historia ya watu wasio wabantu kuingia Africa mashariki haionyeshi wao kuingia mwambao wa afrika mashriki kwa umbali unafikia palipo dar ya Leo achilia mbali Tanga,Jamii za kimasai, mbulu etc hawkaufika huko.Ila wabantu walikuwepo pwani kwa miaka immomerable na hakuna ushahidi kuwa miaka 700BC palikuwa na ukoloni ukanda wa Africa mashariki,kwani wageni wote waliokuja walikuwa wakifanya biashara na aliyeondoka na mtu mweusi alikuwa ma akipewa na chief kama wasaidizi.

      Ndugu yangu nakukumbusha tena Vitabu vya kiislam vinaonyesha utumwa ulikuwepo kabla ya Uislam,sasa karne ya 1600.Wareno wakija tayari utumwa ulikuwa na umri mkubwa.Na ushuhuda wa wasomi wa kiislam kuwa walikuwa waafrica wakiwa na ustaarabu kama wa wazungu ni ushuhuda tosha kuwa Si wazungu tuu, na waarabu pia walishngaa maendeleo.Na huo ni ushuhuda kuwa watu hawa hawakuwa wa kwanza toka nje kuwa na mahusiano na watu wa pwani.Na hawa ni wachina, wahindi, phoenisians ambao tayari walikuwa na ustaabu mkubwa katika nguo na walikuwa kama daraja la ustaarabu wa magharibi ya iliyokuwa katik ustraabu wa wagiriki na Warumi.

      Kupotea kwa Ushirazi na historia ya kiajemi kulitoka na Nguvu ya Uislam.Uislam kwani baaday akuukubali uislam tayari ilibidi wapoteze kila kitu chao na kukumbatia utamaudi wa kiislam ambao ndio ulikuwa maisha ya kawaid akwa mwarabu.Na hii ilipelekea nao kufuta mambo mengi yasiendana na uislam

      Mwandishi hajwa honest kwani mbali kugombea uzanzibari ambao ni haki yake, pia anajaribu ku eneza Arabism.Mwandishi anawaweka waarbu kileleni pamoja na WaSunni, anwaacha waajemi/washirazi na wengine ambao historia liyoiweka inawadhihirisha zaidi.Mwandishi anafanya makosa ya kuufanya uislam ndio ulioanzisha utumwa, wakati utumwa ulikuwepo kabla ya uislam.Mwandishi hana nia ya kuwaunganisha wazanzibar pamoja na kuwapa elimu sahihi juu ya historia yao.Pamoja na kuondoa umiliki wa kisiwa kwa tabaka fulani.Kwani kihasilia wazawa wa Kule wanahaki ya kuishi na kuonyesha uzalendo.Zanzibar kama sehemu nyingine za Africa zimekuwa na uhamaji na uhamiaji kutoka na mabadiliko tofauti.
      Nicholas nimeipenda analysis yako! BRAVO
      Pure Matrimony >> Purity starts here (Quran 24:26)
      My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective" Njiwa"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯


    5. #23
      njiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Location : ax^2+bx+c=0
      Posts : 4,942
      Rep Power : 2365
      Likes Received
      950
      Likes Given
      171

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao



      Quote By Jasusi
      Nimeshindwa kumaliza makala yote. Lakini ukweli usioweza kupingika ni kwamba Waarabu, Waajemi, Wayunani, wote walikuwa ni wageni waliokuja kwenye ufukwe wa Afrika mashariki. Kuna umbali gani kutoka Zanzibar hadi Tanga kwa kulinganishwa na Oman hadi Zanzibar? Wenyeji asili wa Zanzibar ni Wabantu na hili halisutiki na halifutiki.
      Wallahi hili swali huwa ndio nawauliza kule kwenye facebook na majibu hawana... mimi ni mtu wa tanga & mombasa nimechanganya family yetu imechanganya damu but since baba ni watanga mbantu na sisi waislam tunafata kwa baba so mimi ni mtu wa tanga kuna kijiji kipo karibu na mombasa bahati nzuri kijiji chetu kipo ukanda wa bahari ... pemba unaiona ilee! na wapemba wengi wameingia na kuoa! ndani ya kijiji kwetu wala hatuhitaji boat kufika pemba.. mashua za kuvulia samaki watu wenda na kurudi mi ninavyodhani kabla hawajaja hawa waarabu na kulikuwa na jamii ya wabantu nao ni kutoka tanga .. it doesnt make any sense mtu kusema kwamba muarabu ndio alikuwa wa kwanza kufika pale na kukuta ardhi yoooote tupu hakuna hata mtu mmoja!..
      Jasusi likes this.
      Pure Matrimony >> Purity starts here (Quran 24:26)
      My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective" Njiwa"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯


    6. #24
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,410
      Rep Power : 2881
      Likes Received
      4755
      Likes Given
      2822

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      Harakati zote ni za kujenga uhalali kuwa waarabu ni wazalendo. Ukisoma vizuri ni wazi kuwa kuna mataifa mengine yalikuwepo tangu enzi na enzi,hao hawasemwi kama wazalendo bali wazalendo ni waarabu.

      Kuna mtu kauliza hivi Tanga na Pemba au Pemba na Oman wapi karibu? Haaaiinii akilini kuwa uvuvi umekuwepo miaka nenda rudi na hakuna mwafrika aliyewahi kwenda visiwani?

      Jambo la kushangaza sana, waafrika watumwa hawatajwi kama wazlendo bali wananasibishwa na Tanganyika.
      Utumwa wa kimazwazo unawamaliza wazanzibar kifikra. Kila uchao wao wanaota kuwa sehemu ya Uarabu. Wana imnai kabisa uarabau ndiyo race bora dunia. Hata kama umasikini utawamaliza midhali wao wana unasaba na waarabu, poa tu

      Ikifika hapo ndipo naona hatari kubwa sana kwa wenye nywele za kipili pili. Masikini nao wao wanaimba nyimbo bila kujua kuwa tungo nzima, kuanzia vina na mizani zote zimesheheni Uarabu.

      Umasikini wa kujitambua ni mbaya sana kuliko umasiikini wa mali.

    7. #25
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,719
      Rep Power : 1592
      Likes Received
      908
      Likes Given
      29

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      Quote By nngu007

      That's Too Much Complications... Just to disassociate with Tanganyika and to be closer to OMAN... Hakuna

      Mtanganyika yoyote anayetaka wewe uukatae UBANTU... lakini RAIS MWINYI generation yake inapatikana bara

      Tabora... Shamsi Vuai Nahodha anapatikana ... Tanga bila hata kuchanganya hayo makabila... even Alhaji Jumbe

      just to name the few... sio wote mama zao ni waarabu au wahindi hata kidogo; wengi weusiiii wachache sana ni

      Kama Salim Ahmed Salim; na Nyie wenyewe hamumpendi Nyerere alitaka awe Rais wa Zanzibar woote Nyie Mligoma

      Bara kuna Wabantu Wanaojiita Wazanzibari 300,000; Zanzibar Wabantu hao ni 430,000 sasa angalia wengi wako

      Wapi.....
      Salim Ahmed Salim ....wajomba zake wapo Tabora....Mzee Mwinyi ni Mkuranga ...kazikwa babu yake ...na wakati mmoja mwanaye Hussein kawa mbunge pale..

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      mwakaboko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th September 2010
      Posts : 633
      Rep Power : 566
      Likes Received
      140
      Likes Given
      858

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      kazi ipo, kwa upotoshaji huu. JZ anadai eti arabs ndiyo wenyeji zaidi kule ZENJ, basi kazi ipo kuelimisha jiografia
      Jasusi likes this.

    10. #27
      jamhuri ya zanzibar's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 44
      Rep Power : 352
      Likes Received
      9
      Likes Given
      3

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      Pinga hoja kwa hoja (weka references kama zangu) sio porojo. Weka japo references za Mrina na Matoke walimu wa Itikadi ya ubaguzi ya CCM. Wekeni pia japo references za Nyerere aliyewachukia wazanzibari hadi kufikia kusema "ningekua na uwezo ningevitumbukiza visiwa hivi vya Zanzibar katika bahari ya hindi". Sisi wazanzibari Zanzibar si ya mweusi wala mweupe, mbantu wala mwarabu sote tumezaliana wenyewe kwa wenyewe. Wageni wachache ndio wanaoretain asili yao na makabila yao. Wenyeji wenye mizizi mirefu hapa Zanzibar lazima kuna damu ya kichotara katika ukoo wake. Hatutukuzi mwarabu wale mtu mweusi wote ndio sisi. Nyinyi endeleeni kuabudu makabila ndio maana mpaka leo kuna vyama vya wachaga na wasokuwa wachaga. Sisi ni wazanzibari. Mlitugombanisha kwa fitna za Nyerere sasa tumeshtuka, tumeungana kudai nchi yetu.

      Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwnza.a

    11. #28
      Kingcobra's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Posts : 713
      Rep Power : 563
      Likes Received
      128
      Likes Given
      14

      Default

      Quote By jamhuri ya zanzibar
      Umekosea sana kuguess mleta uzi ni chotara la kibantu na mwarabu. Baba yake ni wa asili wa kipare ulioingia Zanzibar kiasi generations 6 nyuma. Hata hivyo kaelewa vyema historia ya nchi yake na njama za makafir walioiparaganya kwa malengo yao.

      Napinga sijatoa hitimisho la ni watu gani walifika mwanzo na kuwakuta wenzao wakiwa wameshahamia mwambaoni na Zanzibar lakini nimezidurusu hoja nyingi ninazozifahamu hata hiyo hoja unayoiunga mkono wewe kuwa wabantu ndio wa mwanzo kufika mwambaoni japo kuwa huna sitations za karibuni wala za kale ambazo ziko free fro conflict of interest.

      Wazanzibari hatukani ubantu maana ni wetu, hatukani, uarabu maana ni wetu, hatukani na nasaba zetu zote maana ni zetu. Yalitendeka hayo huko nyuma kuwapa kipaumbele watu fulani kuliko watu fualani ili kurahisisha mkakati wa kuitawala Zanzibar amabo ulifanikiwa hadi leo.

      Sasa wazanzibari sote tunaonana ni kitu kimoja pamoja na kila mtu na anavyoamini na hatugawiki tena. Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
      .
      Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni ndoto za alinacha tena za mchana. Endelea kusema makafir na kulialia kama kifaranga kilichoachwa na mama yake lakini hiyo mnayoiita jamhuri ya zanzibar hamuipati ng'ooooooo. It is too late to get it back. Tambua kuwa wanazibar weusi wengi wao wana undugu wa damu na wabara. Hawawezi kufanya upuuuzi wa kuwaacha wenzao kwa hila za waarabukoko kama wewe. Unachotakiwa ufahamu, whether you like or not ni kwamba Jamhuri ya Muungano ni chombo cha kudumu ambacho kilikuwepo mioyoni kwanza kabla ya kuundwa kwake na kutambulika kisheria, kipo na kitaendelea kuwepo milele na milele hata ukamilifu wa dahari bila kujali chochoko zenu zinazosukumwa na waarabu kupitia vibaraka njaa kama wewe. Idumu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
      Last edited by Kingcobra; 7th August 2012 at 04:07.

    12. #29
      Nicholas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 4,885
      Rep Power : 3594
      Likes Received
      1244
      Likes Given
      2108

      Default Re: Makuraish (wazalendo) wa kizanzibari na nasaba zao

      Quote By jamhuri ya zanzibar
      ..........
      Wazanzibari hatukani ubantu maana ni wetu, hatukani, uarabu maana ni wetu, hatukani na nasaba zetu zote maana ni zetu. Yalitendeka hayo huko nyuma kuwapa kipaumbele watu fulani kuliko watu fualani ili kurahisisha mkakati wa kuitawala Zanzibar amabo ulifanikiwa hadi leo.

      Sasa wazanzibari sote tunaonana ni kitu kimoja pamoja na kila mtu na anavyoamini na hatugawiki tena. Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwanza
      .
      teh teh..Haiwekekani kwa pamoja mkajiita waarabu, na baaday wabantu, na baadaye washirazi etc..Mtajiita wazanzibari,ila kitu mtu atajitambulishwa kwa kabila la babake.Hiyo na kujiita race zote kwa vile wazazi walijichanganya si sahihi sana.

      kwa kila kizazi mtu anajinasibu kwa chimbuko la baba.Ila waarabu huwa wanapenda sana kueneza uarabu kwa kujaribu jifanya kuwa sehemu ya waafrica, na dini yake kuitangaza kwa gia kuwa race zingine zina asili yake.Ila wakiwa na wengine Quraysh hawababaiki kusema kuwa wao ndio choosen.Ndio waislam wana support ya muarabu nje ya nchi za kiarau kuliko wakiwa kwa waarabu.Waarabu wana superiority complex inayofanya wasiheshimu race zingine kabisa, na kuwaona kuwa wapochini na walistahili kuwafanyia kazi.Hii spirit nayoimewaingia wazanzibar ndio maan ahawana roho yakuridhika katika mambo mengi ya Muungano ingawa wanadekezwa zaidi.

      Hapa hata post yako imeonyesha mkanganyiko kwa kuwapa uzito Quraysh wakati ulicho quote kinaonyesha kuwa Washiraji ndio walikuwa wengi kati ya waliotoka Asia na mashariki ya kati.Nami nikakuonyesha kuwa Waajemi na makabila yao walikuja kama wao.Ila baada ya kuukumbatia uislam uvu ya kubadilisha vitu vingi katika ustaarabu wa waajemi ndipo walipoteza mengi yao kadiri siku zilipokwenda.So bado ushahidi wa Misikiti si mkubwa kuonyesha kuwa Quraysh(Waarabu ndio walikuwa wengi),Ila washirazi walifanana zaidi na waarabu.Kuna sehemu umejaribu taka eleze mchanganyiko wa kiarabu na Lugha za kiajemi kuwa ni waarabu walikaa kule.Ila hujaonyesha nini kilikuwa kinaashiria kutoandikwa na mwanafunzi?Kiarabu au kiajemi?Bado Mwarabu na ubabe wake asingeona haja ya kuandika lugha ya kikafiri katika nchi isiyo ya kafiri.Na mara Zote si Kiarabu au hata uislam unaadapt bali wengine wana adapt kiarabu.

      Hii nortion ya Quraysh kuwa superior ni hatari sana kwa wazanzibar kwan soon itaanza watenganisha Wenye asili ya persia/Iran na hivyo kujenga mazingira ya USHIA na USUNNI ambao tayari pia na wewe umeutaja hapa.

      Na hapa piga ua Waarabu wa sehemu tofauti watapigana vikumbo wenyewe wa wenyewe kutoka na makabila ya vinchi vyao Yemeni watakuwa sana ethiopia na somalia, oman na wengine watakuja Zenj, pia watakuwa na vikumbo na Iran ambao watakuja jenga ushia kupitia watu wenye asili ya kwao.

      Hii thread nia ashirio kuwa mambo hayatokuwa shwari zenj na wabantu watakuwa tena sacrifice wa kwa vita za hizo kambi.
      Last edited by Nicholas; 7th August 2012 at 04:13.
      SIMPLY THE RADICAL: I can`t wait to see the criminalization of CCM,UWT,Bunch of Policemen/women,and all wanafiki na wachumia tumbo.

    13. Miaka 50
    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...