Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
Habari za j2 wadau
Kutoka kwa John Mnyika>>>>>....Leo saa saba hadi tisa alasiri,mkutano wa mtandaoni kutoa maoni juu ya suala la SSRA na NSSF! Mjadala utakuwa ktk: mnyika.blogspot.com!
Mnyika: Nalazimika kukusanya maoni kwa hatua ya sasa kupitia njia ya mtandao kutokana na udharula wa hoja husika
re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
Hivi ni kweli kifungu cha mafao ya kujitoa kilichomekewa alafu naona wabunge kama wameipozea sana hii ishu au kwa vile wao hawamo hawaoni ni kwamba watu wengi watakufa haraka kwa sababu ya pressure ya hili jambo.
Maoni yangu ni kwamba yaani kama ikishindakana kabisa basi angalau iwe mtu pale unapochukua mkopo nusu ya pesa yako iliyopo ndo ihesabibike kama umesha jiunga na huo mpango wao manake hiyo mikopo wanasema tu hawatoa hao na hili jambo kama litashindikana huko BUNGENI tunaomba tumjue mbunge mmoja mmoja nani kasema sheria hii iendelee na nani alikua anataka itolewe MANAANAKE HAPA NAPUMULIA JUU JUU IKIPITISWA TU MAUTI YAMENIKUTA
Muache kujipa majina hayo maana inaonyesha udhaifu wa kufikiria na kuamua wakati polisi hawapo hivyo bali wao wanapokea amri kwa wanao waongoza,umeonyesha udhaifu mkubwa sana kwa kuuliza ilo swali.futa ilo jina
Re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
Hivi hiyo sheria ilipitishwa na nanai? Siyo wabunge wetu akiwemo Mnyika? Hivi utaratibu wa kupitisha sheria ukoje?
Hawakuona hayo mapungufu au walipitisha bila kusoma wakikimbilia posho? Kwa mtindo huu ni sheria ngapi za kikansamizi zinapitishwa na wabunge wetu kwa kuwa inaonekana huwa hata hawazisomi hadi tunaowakilishwa tunakuja kugundua kwamba wawakilishi wetu wametupeleka kusiko!
Kama ni hivyo wao wanawakilisha nini sasa halafu wanakuja kujifanya ati wanawasilisha hoja kwa hati ya dharura. Wabunge wetu wanakosa utukufu na sipendi tena kusikia ati Bunge letu Tukufu; hakuna utukufu hapo.
sasa kaka watu 300 wanasema YES, sasa mtu mmpja ukisema NO atakuelewa nani? haiitaj degree kuelewa jambo kama hili!!!
Yeye alisemaje? Huwa namuamini sana kwa hoja hata kama haikupita lakini angesema tungemuelewa badala ya kuwa miongoni mwa waliopitisha anagutuka baada ya wawakilishwa kugundua udhaifu wa sheria.
Re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
By Polisi
Atueleze kwanza wakati hii sheria inafanyiwa marekebisho bungeni mwezi Aprili alikuwa wapi? Kwanini hakuiinga kipindi hicho?
Naomba kumjibu mtoa maoni wa saa 3:56 swali lake: ‘mlikuwa wapi wakati haya yanapitishwa? Sio wapinzani, sio chama tawala... wote mlishiriki kutukandamiza.”, kwa kurejea taarifa yangu ya tarehe 3 Agosti 2012 kwa umma kuwa:
“Ikumbukwe kwamba kifungu cha kufuta mafao ya kujitoa kilichozua mgogoro hakikuwepo wakati muswada uliposomwa kwa mara ya kwanza bungeni tarehe 1 Februari 2012 bali kiliwasilishwa kupitia jedwali la marekebisho ya Wizara lililowasilishwa tarehe 13 Aprili 2012 bila malengo na madhumuni yake kuelezwa kwa ukamilifu.
Kupitishwa kwa kifungu hicho kumethibitisha maneno niliyoyatoa bungeni kuwa tumefika hapa tulipo kutokana na ‘uzembe wa bunge na wabunge’ na kwa hili pamoja na mchango nilioutoa bungeni kwa maandishi siku hiyo juu ya haja ya kuwa mfumo mpana zaidi wa pensheni na hifadhi ya jamii (universal pension and social security) pamoja na kuwa sikuunga mkono kifungu husika kilichoingizwa kinyemela naomba radhi kwa wananchi wa Ubungo na wafanyakazi kwa kutokuwasilisha jedwali la marekebisho kupinga kifungu hicho kuingizwa.
Izingatiwe kuwa ili kurekebisha hali hiyo tarehe 27 Julai 2012 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali itoe maelezo maelezo kuhusu taarifa zilizotolewa bungeni tarehe 13 Aprili 2012 kuwa wafanyakazi ikiwemo wa migodini kupitia vyama vyao walihusishwa kutoa maoni yaliyopelekea kufutwa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits); suala ambalo Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO) kililikanusha.
Hata hivyo, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya Hotuba yake tarehe 28 Julai 2012 hakutoa majibu yoyote bungeni kuhusu suala hilo hali ambayo imesababisha migongano kuendelea katika migodi mbalimbali kuhusu madai hayo hali ambayo kwa taarifa nilizozipata tarehe 1 na 2 Agosti 2012 inaweza kusababisha migomo migodini. Kufutwa kwa fao la kujitoa kumelalamikiwa pia na wafanyakazi na wadau wa hifadhi ya jamii katika Jimbo la Ubungo na katika taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, suala hili na tukio husika litumike kama rejea ya bunge na wabunge kuikatalia Serikali kuwasilisha marekebisho yenye athari kubwa kipindi cha mwisho na hivyo wabunge kukosa fursa ya kupata maoni ya wananchi na pia Serikali itakiwe kuomba radhi kufuatia kulipotosha bunge kuwa wadau wa hifadhi ya jamii hususan wafanyakazi na vyama vyao walishirikishwa na kuridhia wakati ambapo wamejitokeza na kukanusha madai hayo yaliyotolewa na Wizara bungeni.
Kwa upande mwingine kufutwa kwa mafao ya kujitoa msingi wake haupo kwenye marekebisho ya sheria yaliyofanyika tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali ni udhaifu katika mfumo mzima wa kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii nchini hali ambayo inahitaji wadau kutaka mabadiliko makubwa.”
Tuendelee na mkutano.
John Mnyika
For the Holy Quran says in Sura 42, verse 41: 'All those who fight when oppressed incur no guilt, but Allah shall punish the oppressor, Come the day.
Re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
By king kong iii
mnyika yupo jf aje na huku achukue maoni.
1.fao la kujitoa liwepo kwa sababu mifuko ya hifadhi za jamii ya tz haifanyi kazi kama huko usa wanapotaka kufatisha hyo sheria ya kuzuia kuchukua fao la kujitoa....wao social security inawalinda incase ukipoteza ajira unakuwa unalipwa
2.mifuko ya hifadhi za jamii iwe inawapa bonus ya faida wanayopata kwenye uwekezaji.
3.katika kipindi ambacho mtu anafanya kazi aruhusiwe kukopa fedha zake kwa riba nafuu (5%) @lst nusu na awe anakatwa kila mwisho wa mwezi.
4.serikali isiwe na mamlaka ya kuiingilia hyo mifuko kwani ssra ipo,na hao wakurugenzi wapunguziwe mishaara na posho!! Haiwezekani mkurugenzi analipwa mil25 p.m na posho hadi 1.5m kwa siku,come on!!!
pia mazingira ya tanzania ni tofauti na ulaya hivyo anytime hata hao waliopo kwenye ajira ya kudumu kuna kipindi huwa kuna ridandansi
Mie mwenyewe mhanga wa hili ukitaka kitu chako kipite ukiweke kwenye m issue jedwali ambayo mengi hayasomwi kwa kuwa watz wengi hawapendi namba hivyo wanasoma NARRATIVE tu ikifika kwenye majedwali ni wabunge wenyewe ndio wanaibua hivyo kwa kuwa wengi si wasomaji wakiambiwa JEDWALI na 1 mnasemaje wao wanaitikia IMEPITA na mwisho wa siku wanapitisha
Dah kweli siasa imetukaa vibaya au watu hatufuatilii bunge, mimi ninachojua mnyika na wenzake wachache wako makini ktk kila hoja na huwa hawaungi mkono kirais,tatizo kila wanapoonyesha kutetea wananchi kuna wabunge wanasema wanatafuta umaarufu sasa leo mnyika unamlaumu kwa kosa gani, kijana yupo smart ktk hoja nyingi na anasimamia anachokiamini siku zote
Re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
By tusichoke
Dah kweli siasa imetukaa vibaya au watu hatufuatilii bunge, mimi ninachojua mnyika na wenzake wachache wako makini ktk kila hoja na huwa hawaungi mkono kirais,tatizo kila wanapoonyesha kutetea wananchi kuna wabunge wanasema wanatafuta umaarufu sasa leo mnyika unamlaumu kwa kosa gani, kijana yupo smart ktk hoja nyingi na anasimamia anachokiamini siku zote
Mkuu mimi najua Mnyika yupo smart katika masuala mbalimbali lakini kwa hili wala. Nakumbuka CDM walikuwa makini kwenye suala la sheria ya mchakato wa katiba na wakatoka nje kuonyesha hasira zao. Mwishowe Rais alikubali na sheria ikafanyiwa marekebisho.
Lakini katika hili mimi sikuwasikia hata kidogo. Nimemsikia Mnyika baada ya wawakilishwa kulalama. Ladda walisoma lakini wakawa na kiwi ya macho hawakuona madhara ya hii sheria kwa jamii.
CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.
Re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
Suala hili ni muhimu kujadiliwa kwa manufaa ya wanachama, go Mnyika mtafute na JAFU kwani tayari amepita migodini kukusanya maoni hili ni kwa ajili ya wanachama wa mifuko hii na wala sio la kisiasa kama wengine wanavyotaka kupotosha hapa jamvini
Re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
Watanzania kwa lawama ndo wenyewe. Hata kama Mnyika alikuwepo wakati inapitishwa na yeye alipitiwa kwa mfano haimaanishi kwamba ndo akae kimya. Kagundua kosa,amejipanga kupambana upya na huo ndo ujasiri tunaohitaji. kila la heri Mnyika
Re: Mnyika na Mkutano wa mtandao kutoa maoni juu ya SSRA na NSSF
By Asha Abdala
We Polisi, si uende huku ulipoelekezwa kwenye mkutano ukamuulize hilo swali akujibu? Ndio nyinyi mnaalikwa kutoa maoni mnakacha mikutano halafu wengine wakifanya maamuzi kwa niaba yenu mnalalamika na kupinga baadaye.
Follow Us Here