NILIANDIKA hapa jana juu ya mada hapa juu. Nilisema najua baadhi ya watu watakuwa wamepongeza uteuzi wa Mwambene kuwa mkurugenzi wa MAELEZO kwa kuzingatia kuwa ni kijana na labda ataleta mabadiliko fulani kwenye tasnia ya habari.
Lakini nataka nitoe angalizo dogo ili muweze kufahamu kinundani kilichosababisha Mwambene kuteuliwa na Rais Kikwete kushika nafasi hiyo.
Uteuzi wa Mwambene unatokana na ile habari ya Membe na ufungiwaji MwanaHalisi. Membe ndiyo kiini cha kufungiwa MwanaHalisi kwa sababu ya kulinda maslahi yake binafsi kwa ZOKA. Membe na Zoka ni pacha na kidole, na kwamba ndiyo tegemeo la Membe la kufikishwa Ikulu ndani ya Usalama wa taifa.
Mnakumbuka jinsi stori za kutekwa kwa Dk. Ulimboka zilivyokuwa zinamuingiza moja kwa moja ZOKA katika mpango mzima. Kwa kuona hivyo, Membe akaamua kutumia njia za panya ikiwa ni pamoja na kumshawishi mkuu wa nchi kuagiza MwanaHalisi kufungwa.
Naye Mwambene, licha ya kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, ni mtu wa karibu sana na Membe. Infact, pale wizarani watu wakiwa wanamsema vibaya Membe halafu ghafla Mwambene akitokea, wote wananyamaza kimya! Uteuzi wake ni sehemu ya majadiliano aliyofanya Membe siku ile anajadiliana na JK kuhusu MwanaHalisi. Hii sehemu ya strategies zake kuelekea 2015. Kwa sisi tunaojua nini kinaendelea kwenye teuzi hizi, tunasema ngoja tusubiri tuone.....





Follow Us Here