Kama tatizo ni masaa 48 waliyotoa, nashauri walimu wayatoe Jumatatu wagome Jumatano
Kwa uzoefu wangu nchii hii bila migomo hakuna haki, madai kalibu yote ya walimu mshahara 100% posho ya mazingira magumu 30% na posho maalumu ya kufundisha 50% HAYAJATIMIZWA. Ushauri wangu kwa CWT kama hawakuwa wanatuzuga watekeleze hayo matakwa ya mahakama waite upya mgomo. Natoa hoja!
Re: Kama tatizo ni masaa 48 waliyotoa, nashauri walimu wayatoe Jumatatu wagome Jumatano
Tatizo walimu wakianza kufuata utaratibu wa mgomo ili uwe halali serikali itakimbilia mahakamani na kuwabana tena kwamba mgomo wao batili coz kesi ipo mahakaman.
Re: Kama tatizo ni masaa 48 waliyotoa, nashauri walimu wayatoe Jumatatu wagome Jumatano
Kwa sasa atakuwa halali koz ile tume ya usuruhishi tayari imeundwa kwa mujibu wa kawambwa na hata kama wakienda mahakamani kama wamefuata stage zote likiwepo hilo la 48hrs notes tunategemea utakuwa halali.
Re: Kama tatizo ni masaa 48 waliyotoa, nashauri walimu wayatoe Jumatatu wagome Jumatano
Walimu cha kwanza wanachotakiwa kufanya ni kuwawajibisha viongozi wa CWT kwa uzembe wa kutokuandaa mgomo kwa umakini. Mgomo huo umewagharimu CWT zaidi ya sh. milioni 200 kuuandaa. Unapoandaa kitu cha gharama kubwa namna hiyo ni lazima uwe makini. Kutozingatia kifungu kidogo kama masaa hayahesabiwi weekend ni uzembe. Uwajibikaji uanzie CWT. Kwa aina hiyo ya viongozi wasitegemee kupata utatuzi wa matatizo yao, kwa sababu inaonyesha hayo matatizo ndio yanawapa viongozi sababu za kuchomoa pesa za CWT.
Re: Kama tatizo ni masaa 48 waliyotoa, nashauri walimu wayatoe Jumatatu wagome Jumatano
CWT walijua na hilo lilikua changa la macho wanasema serikali haiwathani walimu ila wao naona wanawadharau walimu coz hili ni zaidi ya changa la macho, siwalaumu walimu ila kwa viongozi wao huu ni Muda wa kuonyesha jamii kuwa ile ilikuwa ni mistake wairekebishe warudi barabarani, kututoa mawazo kuwa bado wao na serikali ni mabest hawawezi wagomea!
Re: Kama tatizo ni masaa 48 waliyotoa, nashauri walimu wayatoe Jumatatu wagome Jumatano
Selikali ya kihuni, mara kadhaa tumeishuhudia ikienda mahakamani usiku ili kuweka pingamizi la migomo. Je, mahakama gani inayofanya kazi usiku hata ishindwe kufanya kazi wekeend?
Re: Kama tatizo ni masaa 48 waliyotoa, nashauri walimu wayatoe Jumatatu wagome Jumatano
hakuna mgomo au maandamano duniani kote yaliyowahi kuruhusiwa kisheria watu wakiamua kuingia front wanaingia front tuu huu mlolongo wa mahakama ni kujidanganya na kupoteza muda! jaji mkuu na majaji wote wanateuliwa na rais mahakimu wanaajiriwa na kulipwa na serikali unategemea waende kinyume na maboss wao? Wafanyakazi tuungane tupige mgomo mmoja mzito sana bila cha mahakama tuone kama watatufukuza wote na kuleta wengine!hii kufuata utaratibu wa mahakama ni upuuzi na kiini macho!1
Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!
Follow Us Here