Heligoland-Zanzibar Treaty:The basis For Malawi Claims
Read this Heligoland treaty document between German & Great Britain which is the one of the documents used by the Malawi government to argue their case.
Re: Heligoland-Zanzibar Treaty:The basis For Malawi Claims
By HKigwangalla
Wewe haujausoma ule mkataba wa Heligoland treaty, na kama umeusoma basi umeupitia pita tu haukuuelewa, maana unachokisema wewe hapa na kilichoandikwa mule ni mbingu na ardhi...Waziri Membe leo amelifafanua hili vizuri sana na hata hiyo suggestion yako ya sisi kufungua kesi unayoisema ameipendekeza, ila kasema Malawi ni ndgu zetu na jirani zetu na tutalitatua hili kirafiki, kidemokrasia kabla hatujaamua kwenda kwenye mambo hayo ya mahakama na hata kufikia kwenye vita...
Kigwangalla,
Heligoland treaty nimeisoma yote. Pia nina utaalamu wa mambo ya ramani na ndiyo maana sikupata shida kuusoma. Imeandikwa kabla mimi sijazaliwa na hata kabla Nyerere hajazaliwa. Hivyo sihitaji kusomewa na Bernard Membe au na yeyote.
Hii comment yangu nimetoa kabla ya hotuba ya Membe. Nimesikiliza Membe yeye amejikita tu kwamba mpaka ni nusu ya Ziwa wakati hatoi tehcnical justification halafu unatakla nimuunge mkono.
Kama Membe ataenda na cooment alizokuaminisha jana Bungeni basi sahau kabisa kulikata hilo ziwa. Kama unaweza kumtetea basi sema justification yake aliyosema jana.
HUtetei kitu kwa misingi ya uzalendo. Unatetea kwa msingi ya ukweli. Idi Amini tulipompiga ni kwa sababu justification ya ukweli ilikuwepo, Kagera Salient ilikuwa ni yetu.
Mimi nawaonea huruma wote mnaodhani hayo mnayotuamishia sasa yatatufanya tuipate Lake Malawi.
.."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.
Re: Heligoland-Zanzibar Treaty:The basis For Malawi Claims
By Nikupateje
Richard,
Kigezo cha mipaka ni ramani iliyokuwa submitted huko United Nations. Wanaochora ramani hizikwenye GoogleEarth na GPS zote si wajinga. Ni ramani wanayotumia.
Narudia, haya mambo Tanzania ilitakiwa kuliwasilisha kwenye international community kuliko kudanganya kuwa inachukua hatua zingine ambazo sanasana zitailetea matatizo Tanzania.
Malawi wako correct.
Correct under what grounds? uhalisia ni kwamba watu walioishi karibu na ziwa hili tangu eanzi na enzi wana haki na ziwa hili bila kujali wanatoa nchi ipi. kwa hivo huwezi kusema wamalawi wana uhalai wa 100% wa ziwa lote na watanzania wanyimwe haki ambayo wanayo kabla hata ya kuja mkoloni. HUU SASA NDIO UKWELI. mpaka ni lazima uwe kati kwa kati
Follow Us Here