Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

    Report Post
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 108
    1. #1
      Makutano Show's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd August 2012
      Location : Dar es Salaam, Tanzania
      Posts : 21
      Rep Power : 346
      Likes Received
      65
      Likes Given
      81

      Default Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe leo kuanzia saa tisa mchana atakuwa katika kipindi cha Makutano Magic FM kinachoendeshwa na Fina Mango ambapo atazungumzia na kutoa ufafanuzi kuhusu shutma za rushwa zilizolitikisa Bunge hivi karibuni ikiwa ni pamoja na yeye kudaiwa kuwa mmoja wa wabunge waliohongwa ili kutetea madudu ya Tanesco.

      Pia atazungumzia suala la mbio za Urais 2015 na posho kwa wabunge.

      Wana-JF mnaruhusiwa kuuliza maswali na kutoa maoni ambayo yatasomwa katika kipindi.

      Karibu.
      Quote By Kunta Kinte
      Amejibu ifuatavyo, kwa baadhi nitakayokumbuka

      - Urais, ni kweli ana nia ya kugombea pamoja na kwamba hajasema atagombea 2015,
      - Anashangaa katiba yetu kuweka umri wa mgombea urais uwe 40, wakati baadhi ya nchi jirani ni 35
      - Anapigania nyimbo za wasanii kwenye milio ya simu wapate 50% sasa hivi wanapata kiduchu - 7%?
      - Amekataa kujibu swali la posho na mishahara ya wabunge - kasema aulizwe spika
      - Kwa nini hayupo na wenzie kwenye operation sangara, kasemawamepeana ratiba na pia alikuwa ana ahadi ya kuhudhuria hicho kipindi cha Fina
      - Mwanasiasa ampendaye amesema Halima Mdee, Spokesperson - Bibi Titi Mohamed,

      Hayo ndio baadhi ya niyakumbukayo
      Quote By nngu007
      JUMAPILI, AGOSTI 05, 2012 | EVANS MAGEGE

      *Asema hajawahi kutangaza mwaka
      *Akiri ni vigumu bila baraka za chama
      *Aahidi kumuunga mkono atakayeteuliwa
      *Masha naye aibuka, autolea macho ubunge


      JINAMIZI la urais linaendelea kumwandama Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA).

      Hali hiyo imetokana na mwanasiasa huyo machachari kushindwa kuweka wazi mwaka wa uchaguzi ambao atagombea urais kama ambavyo amekwisha kutangaza.

      Zitto alipatwa na kigugumizi hicho jana alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Makutano kinachorushwa na radio ya Magic FM ya Dar es Salaam.

      Zitto alihojiwa kuhusu masuala mbalimbali na katika suala la urais aliendelea kusisitiza kuwa anautaka ingawa alishindwa kutaja mwaka ambao atatekeleza azma yake.

      Zitto alisema suala la kugombea urais ni azma yake kutoka moyoni na kueleza kuwa yeye ni tofauti na wanasiasa wengine ambao hulitaka jambo kwa kisingizio cha kutumwa na watu wengine.

      “Ni kweli nautaka urais jambo ambalo nataka Watanzania wajue, mimi sikusema ni lini lakini nia yangu ipo…iwe mwaka 2015, 2020 au 2025.

      “Dhamira yangu nataka siku moja kuliongoza taifa langu, kama mwanasiasa mkomavu huu ni uamuzi wangu kutoka moyoni, sijatumwa wala kuagizwa na mtu yeyote.

      “Siamini katika kauli za kutumwa, kuombwa wala kuagizwa ila kwa mwanasiasa anayejiamini katika uongozi lazima athubutu kuweka dhamira ya kweli katika kuongoza wananchi,”alisema Zitto.

      Hata hivyo, Zitto alisema pamoja na dhamira yake hiyo, ataendelea kufuata sheria na taratibu ambazo ni pamoja na kupata ridhaa ya chama chake cha CHADEMA.

      Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema hadi hivi sasa chama chake hakina mgombea urais na kueleza kuwa muda ukifika suala hilo litakuwa bayana.

      Zitto alisisitiza kuwa hana ubinafsi juu ya hoja hiyo na kusema kuwa mwanachama yeyote atakayeteuliwa kupeperusha bendera katika wadhifa huo yuko tayari kumuunga mkono.

      Akizungumzia suala la tuhuma za rushwa linalohusisha wabunge kuhongwa na kampuni na baadhi ya makampuni ya mafuta, Zitto alirejea msimamo wake wa kupinga kuhusika katika rushwa.

      Zitto alisema binafsi yake anaiamini tume iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda katika kushughulikia sakata hilo kwa kusema kuwa ripoti ya tume hiyo itabainisha ukweli iwapo anahusika au laa.

      “Kwa sasa tumekuwa katika taifa la majungu, uwongo, fitna na tuhuma zisizokuwa na maana na haya yamekuwa kama maisha ya kawaida ya wananchi.

      “Nadhani kwa hili tusiliongelee sana na tuiachie tume iliyoundwa kuchunguza jambo hili ifanye kazi kwa uhuru mkubwa..kwani inatakiwa kutoa majibu yake ndani ya siku 14…msihofu majibu yatatoka tu hivu karibuni,”alisema Zitto.

      Zitto pia alisisitiza kuwa yeye siyo mla rushwa na wala hajawahi kula rushwa.

      Mwanasiasa huyo kijana anadaiwa kuwa na utajiri mkubwa na baadhi ya mali anazodaiwa kuwa nazo ni pamoja na ujenzi wa kasri unaoendelea Mbezi Dar es Salaam na magari ya kifahari.

      Katika mahojiano hayo, Zitto alikanusha madai hayo akisema maneno yote hayo yaliyoibuka ni fikra hasi juu ya nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).

      “Dhamana niliyonayo katika POAC inawajenge watu sura tofauti ya labda najinufaisha na madaraka yangu katika kamati hiyo…nasimamia mashirika zaidi ya 290, kwa hiyo wanafikiri Zitto ni tajiri.

      “Na kama vile haitoshi ule msimamo wangu kupinga posho za ubunge nayo ilifanya wengi wachukie …lakini nitaendelea na msimamo wangu ule ule.

      “Kuhusina na mali zangu ..mimi si tajiri kama wengi wanavyodhani, sina Range Rover, Hammer au jumba la fahari kama watu wanavyozusha.

      “Mimi ninajenga Kigoma, Dar es Salaam sina nyumba, sina kiwanja achilia mbali kiwanja sijawahi kuomba kiwanja Dar es Salaam wala Dodoma, hilo kasri nitakuwanalo wapi?.

      “Nakumbuka siku hiyo mambo haya yaliibuka ilikuwa siku ambayo bajeti ya Nishati na Madini ilikuwa inawasilishwa ….na katika wakati mwengine siku hiyo hiyo, mishahara na posho mpya kwa wabunge zilianza kutoka, hivyo basi wabunge wengi walichangia jambo hilo hadi wengine wasiopenda kuzungumuza siku hiyo walizungumza,” alisema Zitto.

      Alipohojiwa juu ya kiasi kipya cha posho na mshahara Zitto alikataa katu katu kuzungumzia hoja hiyo na kusema kuwa mtu wa kuulizwa ni Spika wa Bunge, Anne Makinda.

      Wakati huohuo, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha alisema bado anayo dhamira ya kuwania tena ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza.

      Masha aliangushwa na mbunge wa sasa jimbo hilo, Ezekia Wenje wa Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2010 na hivyo kupoteza ubunge pamoja na uwaziri.

      Masha ambaye alikuwa akihojiwa katika kipindi hicho alisema bado anayo dhamira ya kugombea tena kiti hicho cha ubunge wa Nyamagana lakini hajaamua atafanya hivyo lini.

      Alisema kuwa hawezi kutangaza ni lini atafanya hivyo lakini iwapo wananchi wa jimbo hilo watamuhitaji kugombea uchaguzi ujao wa 2015 atafanya hivyo.

      “Nikigomea tena sitashindwa …suala la kutaka kugombea ni lazima lakini kwa sasa nafanya biashara zangu binafsi…najipanga nitarudi tena katika siasa,” alisema Masha.

    2. Study Abroad

    3. #21
      maria pia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th July 2012
      Posts : 304
      Rep Power : 403
      Likes Received
      31
      Likes Given
      65

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Safi sana, tulio nje ya Dar es Salaam kwa muda huu mtakuwa mmetusaidia sana.......

    4. #22
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,435
      Rep Power : 19775
      Likes Received
      4277
      Likes Given
      906

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Asante fina kwa fursa ya kuuliza maswali.

      Swali kwa Zitto:

      Kwanini unaung'ang'nia huo uenyekiti? Kwanini usijiweke pembeni ili uchunguzi ufanyike vizuri?

      Kwanini amekuwa akijichanganya sana kwa matamko yake mara aseme tatizo ni urais, mara uenyekekiti, mara posho; naomba aseme lipi ni chanzo cha tuhuma!

    5. #23
      pembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 285
      Rep Power : 490
      Likes Received
      79
      Likes Given
      322

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Mh Zitto ueleze uma kwa nini una ndoto za kuwania urais? Nini unafikiri utafanya kitakachoinua hali ya mlalahoi? Mrema alijaribisha akiwa waziri wa Mambo ya Ndani wananchi wakaona na kutafakari. Usafi Dar uliimarika, migogoro ya kifamilia ilipunguka, magendo yalipungua etc. Mwaka 1995 akagombea urais akapata alichopata (satisfactory results).

      Wewe ni nini hasa utafanya ambacho kwa sasa umejaribu kukikemea kikashindikana?

    6. RR
      #24
      RR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2007
      Location : Close
      Posts : 5,599
      Rep Power : 1741
      Likes Received
      1016
      Likes Given
      481

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Ameshawahi, kwa wakati wowote kuwa na masilahi binafsi (yeye ama watu wake wa karibu) na TANESCO?
      Bunge: Upuuzi unaolindwa na sheria...kwa kutumia hela za Watz!

    7. #25
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3256
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Quote By Molemo
      Mkuu msemaji wa chama ni John Mnyika,inavyoonyesha hufuatilii mambo kwa sababu hayo yote unayozungumzia Mnyika ametoa kauli.
      Molemo Mkuu, asante sana kwa kunijulisha hivyo na kwa kweli nimefarijika kusikia kuwa hii figure ipo ndani ya chama
      chetu

      Nikiri kuwa mimi ni mgeni kidogo ingawa huwa ninajaribu kufatilia pale ninapoweza.
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Bitabo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2011
      Posts : 1,372
      Rep Power : 660
      Likes Received
      445
      Likes Given
      261

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Dada Fina nakushukuru sana kwa kuja JF ambayo watangazaji wengi wanaikimbia eti ni mtandao wa kizushi na wa 'ma-haters''. You proved them wrong. Asante kwa hilo

      Sasa hii show yako kwa sisi tulio mikoa ambayo Times FM haisikiki tunapataje hayo mahojiano?
      Uovu wa siku moja, unaondoa wema wa MWAKA MZIMA

    10. #27
      Companero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2008
      Posts : 4,752
      Rep Power : 6503
      Likes Received
      954
      Likes Given
      1105

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Mbona nasikia nyimbo tu kwenye FM 92.9?
      "Each generation must, out of relative obscurity, discover its mission, fulfil it, or betray it"/Kila kizazi, katika utata wa kipindi chake, lazima kiutambue wajibu wake na kiutekeleze au kiusaliti - Frantz Fanon

    11. #28
      jmushi1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2007
      Posts : 14,375
      Rep Power : 16492
      Likes Received
      4298
      Likes Given
      5491

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Quote By Companero
      Mbona nasikia nyimbo tu kwenye FM 92.9?
      Kaingia mitini?hawezi kujibu yale maswali uliyomwuliza yaliyotokana na "tamko" lake...Tusubiri tuone,sina haja ya kuongezea swali,yote yameshaulizwa.
      "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

    12. #29
      Kunta Kinte's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th May 2009
      Posts : 2,559
      Rep Power : 2532
      Likes Received
      595
      Likes Given
      759

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Kipindi kimefutwa? maana saa hizi nasikia wanaume TMK tu
      Have patience with all things, but chiefly have patience with yourself.- Saint Francis de Sales

    13. #30
      Zipuwawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2010
      Posts : 2,194
      Rep Power : 867
      Likes Received
      307
      Likes Given
      123

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Zitto kwanini hataki kujihusisha na M4c na kwenda kujikita na vituo vya radio kujishughulisha na mambo yake?
      Maisha yetu ni mafupi lazima tuyatete kwa namna yeyote ile!

    14. #31
      jmushi1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2007
      Posts : 14,375
      Rep Power : 16492
      Likes Received
      4298
      Likes Given
      5491

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Hawezi kujibu maswali ya hapa,kuna anayebisha hilo?
      "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

    15. #32
      Bams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Posts : 829
      Rep Power : 600
      Likes Received
      333
      Likes Given
      9

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Licha ya kuonesha uwezo katika maeneo kadhaa, watu wengi wana mashaka juu ya uadilifu wako, utashi, hekima, busara na mshikamano wako na viongozi wenzio na chama. Je katika matukio yafuatayo yaliyotia shaka juu ya uadilifu na dhamira yako, unayatolea maelezo gani:

      1) Wakati wa kampeni za uchaguzi za 2010 wakati viongozi wenzio wa CHADEMA wakiwa wanahangaika kutafuta kura, wewe ulionekana maeneo kadhaa ukifanya mikutano ya siri na RA. Mikutano hiyo iliyokuwa na manufaa kwa chama, Taifa au kwako binafsi? Ilikuwa na faida kwa kiasi gani, na mlikuwa mkiongelea nini?

      2) Wakati viongozi wenzio wa CHADEMA mwaka 2010 wakisulibiwa na jeshi la polisi na TISS, wewe ulithibitika wakati wote ukiwa na mawasiliano ya karibu na viongozi wa juu wa TISS. Mawasiliano yako ya daima na viongozi wa TISS, yalikuwa ni kwaajili ya manufaa ya Taifa, yako binafsi, wapiga kura wako au viongozi wenzako wa CHADEMA? Na kwa nini wewe pekee yako ndani ya CHADEMA, unaonekana kutopata misukosuko yoyote kutoka polisi? Nini uhusiano wako na TISS na viongozi wake?

      3) Kwa nini mwaka 2010 uliamua kumpigia kampeni JK badala ya mgombea wa chama chako Dr. Slaa?

      4) Kwa nini kila mara umeonekana kutaka madaraka ya kila nafasi inapopatikana?

      5) Kwa kujitathmini mwenyewe unadhani ni nini mapungufu yako (ambayo ni lazima uyafanyie kazi) na nini nguvu zako? i.e. your strengths and weaknesses.

      6) Kila mara umezungumzia nafasi ya vijana katika uongozi wa Taifa, je, unazungumzia vipi mchango wa ujana katika uongozi bora? Unazungumzia vipi utendaji mbovu wa mawaziri vijana walioteuliwa na JK katika serikali yake (ref. Ngeleja, Maige na Malima) hata kulazimika kuwateua wazee (ref. Prof. Muhongo & Mgimwa) ili kuokoa jahazi lililowashinda vijana? Je, ujana ni sifa inayoweza kuliokoa Taifa au zaidi ni moral satifaction kuliko faida tunayoweza kuipata?
      Quote By Makutano Show
      Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe leo kuanzia saa tisa mchana atakuwa katika kipindi cha Makutano Magic FM kinachoendeshwa na Fina Mango ambapo atazungumzia na kutoa ufafanuzi kuhusu shutma za rushwa zilizolitikisa Bunge hivi karibuni ikiwa ni pamoja na yeye kudaiwa kuwa mmoja wa wabunge waliohongwa ili kutetea madudu ya Tanesco.

      Pia atazungumzia suala la mbio za Urais 2015 na posho kwa wabunge.

      Wana-JF mnaruhusiwa kuuliza maswali na kutoa maoni ambayo yatasomwa katika kipindi.

      Karibu.
      NG'ONGOVE likes this.

    16. #33
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,435
      Rep Power : 19775
      Likes Received
      4277
      Likes Given
      906

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Vipi mbona sioni updates? Jamaa kaingia mitini?

    17. #34
      Kunta Kinte's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th May 2009
      Posts : 2,559
      Rep Power : 2532
      Likes Received
      595
      Likes Given
      759

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Fina at least kuwa muungwana uje utueleze ni nini kimetokea, watu tuliacha shughuli zingine ili tuweze kufuatilia kipindi hiki!!
      Have patience with all things, but chiefly have patience with yourself.- Saint Francis de Sales

    18. #35
      JF-MBUNGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 356
      Rep Power : 426
      Likes Received
      121
      Likes Given
      198

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Quote By jmushi1
      Hawezi kujibu maswali ya hapa,kuna anayebisha hilo?
      Nilimshauri kupitia post hii asiongee ongee sana na media watu watamzoea na kumuona hana jipya nafikiri kachukuaushauri wangu....hilo litamsaidia

    19. #36
      Kunta Kinte's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th May 2009
      Posts : 2,559
      Rep Power : 2532
      Likes Received
      595
      Likes Given
      759

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      At last ameanza kuzungumza na amesema suala la rushwa kwa wabunge lisizungumzwe kwa sababu kuna tume inalifanyia kazi
      Have patience with all things, but chiefly have patience with yourself.- Saint Francis de Sales

    20. #37
      Kunta Kinte's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th May 2009
      Posts : 2,559
      Rep Power : 2532
      Likes Received
      595
      Likes Given
      759

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Quote By sembuli
      Mh. Zitto jamii imeshtushwa na utajiri wako wa ghafla ambapo inasemekana unajenga kasri Mbezi, pia unamiliki Range Rover 'Vogue' na hammer (magari ya kifahari);

      Swali 1: Je, Mh. Zitto upo tayari kupitia kipindi hiki cha radio kulitangazia taifa/kutaja MALI UNAZOMILIKI?

      Swali 2: Je, ukwasi ulio nao kwa kipindi hiki kifupi tangu uwe kiongozi (ubunge+ POAC) unaakisi vipi tumaini la vijana ?
      Anasema hana Vogue, hana Hammer na wala hajengi Dar.
      Have patience with all things, but chiefly have patience with yourself.- Saint Francis de Sales

    21. #38
      Invisible's Avatar
      Robot Array
      Join Date : 11th February 2006
      Location : Here...!
      Posts : 9,326
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      4881
      Likes Given
      5599

      Default Re: Zitto Kabwe on Magic FM: Tuhuma za Rushwa, Posho za wabunge na Mbio za Urais 2015

      Kunta Kinte,

      Amemaliza mkuu? Kajibu yepi? Kivipi?

    22. #39
      mndwadage's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2012
      Posts : 346
      Rep Power : 413
      Likes Received
      67
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Kunta Kinte
      At last ameanza kuzungumza na amesema suala la rushwa kwa wabunge lisizungumzwe kwa sababu kuna tume inalifanyia kazi
      mkuu tufafanulie basi amejibu nini huyo ndugu katika maswali ya wadau.?

    23. #40
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,140
      Rep Power : 12552
      Likes Received
      5720
      Likes Given
      739

      Default

      Quote By Molemo
      Mosi; Viongozi wote wa chama wako kanda ya Kati kuongoza operesheni Sangara. Yeye amesusia kushiriki na wenzake, Kwa hilo tu yeye hajioni ana agenda ya siri dhidi ya chama?

      Pili anasemaje kuhusu yeye kuwashambulia wabunge wa chama chake Nassari na Mdee pale walipokana habari za uongo za gazeti Mwananchi kwamba wamemtangaza yeye ni mgombea urais wa CHADEMA? Alikuwa na maslahi gani na habari ile?
      Mkuu mbona uwa umpendi mwanachadema mwenzako Zitto Kabwe, unataka kutuambia hiyo oparation sangara wapo wabunge wote wa Chadema kasoro ZZK.
      Lokissa likes this.

    24. Miaka 50
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...