Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini nawawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwawatoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfanoninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio chawafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwana kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.
Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedhakuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara nakulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwamfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani chafedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu patona matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyopicha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihalifamilia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidini pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanyakazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizokuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume nasheria.
Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wamuafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedhazisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendovisivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa pichailihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwakazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalishakiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwakufukuzwa.
Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchibila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume nasheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenyenafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungubasi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shuleimekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima nakutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maishakujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia sikuza mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuzasheria za nchi yetu Tanzania?
Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumiziya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibukwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hatakufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa nikuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchiusiovumilika.
Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimilimkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kamaawa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenyeshida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.
Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu waowa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumiaviongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharauna kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyeshauzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kuteteasheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lughaya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa lakuongea kishahili na wanafunzi.
Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
Kwanza kupandisha mshahara na mazingira yakazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwani manyanyaso ya waajiri.
Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali piamfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwabinafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni.
Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wamapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shidaza watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watuwasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendowanaweza kuzifanya.
Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchinikuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu zakitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwamanufaa ya Tanzania.
Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi yakufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.
Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kuteteanchi yangu Tanzania.
Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga:+255 755 379 737
Chanzo:HABARI NA MATUKIO: MWALIMU AFUKUZWA KAZI KWA KUONGEA "KISWAHILI" - ARUSHA

Reply With Quote



Follow Us Here