Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha

    Report Post
    Page 3 of 3 FirstFirst 123
    Results 41 to 43 of 43
    1. #1
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha

      Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini nawawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwawatoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfanoninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio chawafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwana kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.

      Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedhakuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara nakulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwamfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani chafedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu patona matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyopicha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihalifamilia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidini pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanyakazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizokuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume nasheria.

      Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wamuafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedhazisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendovisivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa pichailihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwakazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalishakiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwakufukuzwa.

      Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchibila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume nasheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenyenafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungubasi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shuleimekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima nakutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maishakujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia sikuza mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuzasheria za nchi yetu Tanzania?

      Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumiziya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibukwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hatakufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa nikuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchiusiovumilika.

      Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimilimkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kamaawa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenyeshida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.

      Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu waowa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumiaviongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharauna kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyeshauzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kuteteasheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lughaya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa lakuongea kishahili na wanafunzi.

      Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
      Kwanza kupandisha mshahara na mazingira yakazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwani manyanyaso ya waajiri.
      Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali piamfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwabinafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni.

      Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wamapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shidaza watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watuwasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendowanaweza kuzifanya.

      Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchinikuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu zakitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwamanufaa ya Tanzania.

      Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi yakufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.

      Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kuteteanchi yangu Tanzania.

      Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga:+255 755 379 737

      Chanzo:HABARI NA MATUKIO: MWALIMU AFUKUZWA KAZI KWA KUONGEA "KISWAHILI" - ARUSHA
      Mkandara likes this.
      Nasema : CCM tunadhani adui yetu ni Chadema hapana ni Watendaji wetu katika Serikali ya CCM tukawabane hao - Livingstone Kibajaji Lusinde 2013 25 April at 11:54am.

    2. FemaTV & Radio

    3. #41
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,602
      Rep Power : 15259
      Likes Received
      3727
      Likes Given
      2861

      Default Re: Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha


      Mwalimu Daniel Urioh.

      Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737

      Tumesikia upande mmoja tu na tunajadili na kutoa kuuhukumu upande wa pili ambao hatujasikiliza hoja zao.
      • Kawaida ya waajiri hutoa onyo mtu anapofanya kosa, na inapotokea kurudiarudia hufukuzwa.
      • Walimu wengi wamepata ajira au elimu kwa ujanjaujanja, pengine hata darasani kiingereza haipandi, wataka shule iathirike?
      • Waendeshaji shule wa kutoka nje wamezoea kuwekeana mikataba na waajiriwa pamoja na masharti yake, kama ameyavunja wafanyeje?
      • Shule nyingine binafsi kama seminary wanachofanikiwa katika elimu ni kukazia uzungumzaji kiingereza ndani na nje ya darasa maana yake eneo lote la shule, iwe mwalimu au mwanafunzi, sasa kama mwalimu anapokuwa wa kwanza kuvunja utaratibu wa shule sasa uongozi wa shule ufanyeje?


      Binafsi sina maana ya kutetea uongozi wa shule, ila natetea ukweli huu kwamba kila shule ina malengo na mlengo wake katika utoaji wa elimu kuweka taratibu na sheria za shule kwa wanafunzi na staff. Kama mmoja wapo wa staff anakiuka taratibu na sheria za shule ambazo ndio njia ambayo uongozi wa shule unaona kuna umuhimu wa kukuza kiwango cha elimu kwa wanafunzi huyo anakosa na anastahili adhabu hiyo kama alionywa na hakujirekebisha.

      Watanzania tumezoea mno kulalamikia kila kitu kwa ajili ya kutetea udhaifu katika uwajibikaji na utendaji wetu wa kila siku katika ajira zatu. Hilo tuliangalie, na pengine mwajiri hakufahamu sana uwezo wa Mwalimu, amekuja kumshtukia alipogwaya katika utendaji wake akiwa ameshaajiriwa, napengine alimpa nafasi labda atajirekebisha lakini hakuna mafaniki.

    4. #42
      Masauni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th August 2010
      Posts : 377
      Rep Power : 519
      Likes Received
      48
      Likes Given
      0

      Default Re: Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha

      Quote By JokaKuu
      ..wa-Tz tuhakikishe tunajifunza Kiingereza kwa juhudi zote.

      ..Kiswahili hakiwezi kutufikisha mbali, that is the reality.
      Asante sana joka kuu. ebu waambie hao watanzania. ukiwa Tanzania unajifanya wa maana sana kuzungumza kiswahili ukitoka nje ya mipaka ya Tanzania hakuna kiswahili. kama hujui english macho yatakutoka utabaki kusema kila kitu YES YES. Tunashindwa kuutangaza utalii kwa sababu ya lugha tunalalamika.Tunaingia mikataba mibovu kwa sababu hatujui lugha ya kiingereza. Kiswahili sio dili ni upumbavu tu wa viongozi waliofanya tangu mwazo!! WATANZANIA MLIOKO HUKO TANZANIA JIFUNZENI KIINGEREZA KWA BIDII, WAFUNDISHE WATOTO WENU LUGHA YA KIINGEREZA. TUNA WASANII WAZURI SANA AMBAO WANGEKUWA NI WASANII WA KIMATAIFA LAKINI KWA SABABU YA LUGHA WANABAKI KUWA WASANII WA KIBONGO NA VIHELA KIDUCHU WANAJIONA WAMEFIKA. BILA KUJUA KIINGEREZA TUTAJITENGA NA KUWA KAMA KISIWA.
      JokaKuu likes this.

    5. #43
      dudus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,294
      Rep Power : 1004
      Likes Received
      1287
      Likes Given
      520

      Default Re: Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha

      Quote By Bornvilla
      Mnaabudu wazungu halafu mnakuja kulalamika hapa tuwasaidie nini? Endeleeni kuwaabudu!
      Lakini si kwa kiwango anachaobudiwa mwarabu kule Pemba.

    6. Miaka 50
    Page 3 of 3 FirstFirst 123

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...