Niko poor kweli kufumbua mafumbo Sungurampole, nisaidie basi eee ndugu.
Hapa nikimaanisha kama mahakama imeamua kurudisha watumishi kazin ahitoshi ili sisi tupate huduma inabidi pia wawaasimamie. nakosoa mtindo huu ambao tunahudumiwa na watumishi waliamrishwa na mahakama siyo sustainable na pia kazi hizi zinahitaji moyo ili tupate huduma stahili hivi ukimlazimisha daktari arudi kazini akimwona mgonjwa halafu akamwandikia asprin utalalamika ? kwani unajua ulistahili nini ukilalamika akiamua akuchome sindano ya maji isiyokuwa lazima utajua?
Tuombe Mungu mambo haya yaishe vizuri kutegemea mahakama ni short cu amabyo ukweli ni long and dangerous cut.
There is a higher court than courts of justice and that is court of conscience.
TWIZAMALLYA ninatamani kuendeleza malumbano na wewe, ila nimeogopa kitu kimoja tu: watu watashindwa kututofautisha! Lakini kwa kuwa kufundisha ni kazi yangu na ni taaluma ambayo mimi ni mgenzi kwayo, nitachukua muda mchache kukufundisha. Suala la kuamua kuyaelewa mafundisho yangu nitaliacha kwako binafsi kama ambavyo nimekuwa nikiwakokota mbuzi wangu hadi kwenye mto na kuwaachia maamuzi kamili juu ya kunywa maji. Wakaguzi wa Shule wapo katika ngazi tatu nchini mwetu. Wapo Wizarani, wapo katika kila Kanda na wengine wapo wilayani. Wale wa Kanda hufanya ukaguzi maalum mara moja moja hasa kwa shule za sekondari kwa kuwa raslimali wapewazo haziwapi uwezo wa kukagua mara nyingi kwa shule zote. Wale walioko wilayani wanawajibika kukagua shule za msingi katika wilaya husika lakini 'trend' inaonesha wakaguzi hawa hukaa tu ofisini mwao kama wanafunzi wa darasa lisilo na mwalimu na muda wa kazi uishapo hutawanyika hima. Hawana kazi ya kufanya kwa sababu hawana usafiri, viandikwa na viandikio, achilia mbali posho za kujikimu! Ikitokea mwanya fulani wakaguzi wa shule wakapewa fursa ya kubadilisha kitengo cha kufanyia kazi, nikudokeze tu, wote watakimbia fasta!! Kwa hiyo hoja uliyoitoa hapa kwamba wakaguzi wao ni 'full posho', siyo tu kwamba ni hoja mufilisi, bali ndiyo hoja imewasaidia wanajamvi kukujua jinsi ulivyo mbu mbu mbu wa kitengo hiki. Ila nakushauri usitahayari, maana ninaamini utanishukuru kwa kukuelimisha bila kukudai malipo yoyote. Karibu kwa maswali, mchango au nyongeza yoyote yenye tija, hasa kwa upande wako!
Ndio maana nilikuambia mwanzo mwl wa upe kuwa kwa vile nyinyi ni kunguru mnaogopa neno kufukuzwa kazi, basi ni rahisi kwa serikali kuboresha idara moja tu ya ukaguzi ili kuwaweka sawa waalimu wote.
No man can stand on top because he is put there. H.H. Vreeland
Follow Us Here