Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani?

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 24 of 24
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,523
      Rep Power : 46715
      Likes Received
      16444
      Likes Given
      8471

      Default Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani?

      Nimeeleza kwenye ile mada nyingine kuwa haya yote ni mazingaombwe. Bado naamini hivyo. Ninaamini mazingaombwe haya ni kamili (complete illusion) kwa sababu kamati teule iliyoundwa na Spika Makinda kuchunguza tuhuma hii kimsingi imepewa jukumu lisilowezekana. Kamati hii inaongozwa na Hassan Ngwilizi (CCM) na wajumbe wake wengine wakiwa ni: John Chiligati (CCM), Said Arfi (CHADEMA), Riziki Omar Juma (CUF), na Gosbert Blandes (CCM).

      Nani aliomba rushwa na aliombaje?
      Kazi kubwa ya kuweza kuthibitisha hili inaanzia hapa. KT inapaswa kupata ushahidi usiokinzana wa kuonesha nani aliomba rushwa TANESCO na aliomba rushwa hiyo vipi. Ni rahisi - kwa kiasi - kuweza kutaja majina ya walioomba rushwa lakini kuweza kuonesha waliomba "vipi" rushwa hiyo ikawa ni kazi. Kama mbunge aliomba rushwa kwa mtendaji wa TANESCO na wakati anafanya hivyo walikuwa wawili tu ni kwa kiasi gani maneno ya mtendaji wa TANESCO yataweza kuaminika bila ya ushahidi mwingine wowote wa nje (mawasiliaoni ya simu, email, video au vimemo)?

      Kumbe haitoshi kusema tu "fulani aliomba rushwa" kwani hilo peke yake bila ushahidi wa nje wa uombaji huo ni maneno dhidi ya maneno.

      Nani alipokea rushwa?
      Sasa inawezekana kuwa ni vigumu kuonesha ni vipi rushwa iliombwa; lakini ni rahisi kwa kiasi chake kuonesha kama rushwa ilipokelewa. Kama rushwa haikutolewa na hakuna ushahidi wa kuonesha kuwa rushwa imepokelewa madai kuwa kuna mtu aliomba rushwa yanaweza kuonekana ni masimulizi tu. Kama rushwa ilipokelewa ni wazi basi kuna mtu aliitoa. Huyu aliyetoa ni nani? na kama alitoa ni kwanini alitoa bila kujaribu kuwasiliana na TAKUKURU kuwanasisha wataka rushwa hawa?

      Hili linatudokeza lile la kwangu la "mazingaombwe". Kama mtu alitoa rushwa bila kushirikisha vyombo vya usalama ili kumnasa mtoa rushwa mtu huyo naye anashtakika kwa mashtaka ya kutoa rushwa! Ikumbukwe katika sheria yetu mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanashtakika! Ushahidi wa kuwa mtu kapokea rushwa ni pamoja na kukutwa na rushwa. Ina maana akaunti za wabunge WOTE wanaotuhumiwa kupokea rushwa (siyo kuomba tu) ni LAZIMA zipitiwe na kamati teule na pamoja na akaunti hizo ni zile za JAMAA NA NDUGU WA KARIBU na kulinganisha mtiririko (flow) ya fedha katika siku ambazo viongozi wanadaiwa kuomba rushwa.

      Uchunguzi huu hauwezi kukamilika bila kueleza wazi kuwa akaunti za wabunge watuhumiwa na jamaa zao wa karibu zilikuwa au hazikukutwa na kiasi cha fedha kinachodaiwa kutolewa. Naamini wataangalia pia 'movement' ya fedha kutoka akaunti hizo baada ya tarehe ya sakata kulipuka bungeni.

      Itakuwaje kama hakuna ushahidi wa kiforensiki wa rushwa?
      Sasa, swali hili liko katika kiini cha nani anasema kweli. Kama hakuna ushahidi wa rushwa kutolewa au kupokelewa na wala hakuna ushahidi wa rushwa kuombwa ni kwa vipi watu waliweza kusimama BUNGENI na kudai kuwa kulikuwa na rushwa? Je tunakumbuka (au tumesahau) jinsi sakata la Jairo lilivyodai kuwa kuna "rushwa" ilitolewa kwa wabunge na wengine tulipinga vile vile kwani hakukuwa na ushahidi? Na ni kweli walipochunguza "hawakukuta" rushwa hiyo? Sasa kama hakuna ushahidi wowote kuonesha kama rushwa iliombwa, ilitolewa au ilipokelewa hawa wabunge wanaosimama kudai kuna rushwa wanapata wapi taarifa hizo?

      Lakini kama wapo wabunge wanaopokea rushwa (wakiomba au wasipoomba) na wanaweza kuficha rushwa hiyo kiasi kwamba haiwezi kuonekana kwa vyombo vya usalama je hii ina maana gani? Je tuna uhakika gani kuwa kila wanapoulizwa "wale wanaokubali waseme ndiyo" wanasema ndiyo na "wale wanaokataa waseme hapana" halafu "waliosema ndio wameshinda" wanafanya hivyo wakiwa na mulungula mfukoni au kwenye vyungu vyao? Lakini, kama ni kweli wabunge wanaweza kuhongwa kwa ajili ya kufanya mambo fulani Bungeni na hakuna mtu ambaye ameweza kuwanasa ina maana kuwa tuna mfumo mbovu kabisa wa kupigana na rushwa? siyo?

      Kwamba wabunge wenyewe wanajuana nani mpokea rushwa na nani anapenda kuomba omba rushwa lakini wabunge hawa walioapa kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna hata mmoja wao ambaye ameweza kusaidia vyombo vya dala kuwanasa wenzie wala rushwa?


      Lakini swali la ugomvi ni kuwa: KAMA kweli Bungeni wala rushwa wapo, wanajuana na kulindana na wakikasirikiana wanatajana ni kwa kiasi gani tunaweza kuamini wanavyozungumza kwa jazba, kumwaga data na hata kuonekana ni wazalendo? Na kama wabunge wala rushwa hawawezi kupatikana tunaweza vipi kuliamini Bunge hili lote?

      Swali zaidi ambalo sitaki kufikiria maana yake ni kuwa ITAKUWAJE KAMA KAMATI TEULE ITAKUTA KUWA NI KWELI WAPO WABUNGE WAMEKULA RUSHWA? Ikumbukwe agizo la Spika Makinda ni kuwa wakimaliza kina Ngwilizi wamshauri nini cha kufanya! Hakuwapa agizo la kusoma ripoti yao BUNGENI. Kwanini wabunge wasimtake Spika kutaka Kamati Teule isome ripoti yake Bungeni moja kwa moja ILI BUNGE LIAMUE NINI CHA KUFANYA BADALA YA YEYE MTU MMOJA?
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    2. Miaka 50

    3. #21
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,523
      Rep Power : 46715
      Likes Received
      16444
      Likes Given
      8471

      Default Re: Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani?

      Quote By HIMO ONE
      Mwana kijiji bana yaani yuko kama housegirly wa zitto kumtetea tuu kwa kila namna

      duh.. mbona mna kazi sana? Ukiulizwa ni kauli gani inamtetea Zitto nina uhakika hutoweza kuonesha hata moja ila mwenyewe unaamini umesema kitu 'deep'!
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    4. #22
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,442
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      4805
      Likes Given
      2871

      Default Re: Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani?

      Tukiiangalia kamati iliyoundwa wajumbe wake ni wale wa kamati ya haki, maadili ya bunge isipokuwa mmoja tu,kamati ambayo nayo pia ilisemwa ivunjwe kwa kushindwa kazi.

      Wakati huo huo PCCB iliyopoteza imani na mvuto kwa jamii nayo inachunguza. Sasa hatujui ni uchunguzi gani utakaokuwa halali. Kwa jinsi ilivyo sidhani kuna matokeo yoyote ya maana zaidi ya kile MM anachokiita mazingaombwe.

      Tuhuma za rushwa zilitolewa mara nyingi sana na mbunge kafulila alifikia hata mahali pa kuwataja wahusika. Yote yakawekwa chini ya kapeti. Hivi kwanini hili linaonekana kuwa kubwa sana. Je, si kweli anatafutwa mtu kwa uchawi hapo na je wapinzani watapata hukumu sawa ikiwa Spika ni wa CCM na kamati inaundwa na Wana CCM wengi hata kwa kura tu wanashinda!

      Hivi kweli kwa akili zetu tunategemea Makinda aseme wabunge wa CCM wamepokea rushwa.
      Lakini pia tujiulize ukiacha kamati ya Mwakyembe ipi ingine iliyowahi kuweka uchunguzi wake hadharani.

      Mapendekezo ya bunge kuhusu Jairo na Luhanjo yamewekwa kapuni, tutarajie nini kipya ambacho Spika Makinda kama Spika anaweza kukifanya endapo mhimili mmoja unadharau maamuzi ya mhimili mwingine?

      Viongozi wa nchi yetu wametugeuza ndondocha, likitokea jambo kama si kisingizio cha mahakama, basi itaundwa kamati feki kupoteza mada husika.

      Viongozi hawataacha kutudharau hadi pale sisi wenyewe tutakapoacha kujidharau. Tutaacha kujidharau tutakapowawajibisha kwa kwa lazima.

      Hili halina itikadi ya kisiasa maana linagusa chombo cha kutunga sheria kwa wezi wa kuku na kujiundia kamati wanaponyoshewa kidole. Limegusa sehemu ya wananchi.

      Hivi kwanini Makinda asiondoke kwanza ili kulisafisha bunge na tuhuma hizi? Siyo kwamba anahusika lakini ameshindwa kusimamia bunge kiasi kwamba sasa ni chaka la maovu. Ni genge la wahuni wanaoleta mgao wa umeme kwa manufaa ya matumbo yao. Ni kongamano la wehu wasiojua kwanini wapo Dodoma.

      Makinda aondoke kwanza! vinginevyo kumkabidhi taarifa ya uchunguzi ni sawa na kumkabidhi fisi alinde bucha yako ya nyama.

      Makinda must go first!

    5. #23
      andrews's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th March 2012
      Posts : 1,683
      Rep Power : 0
      Likes Received
      142
      Likes Given
      76

      Default Re: Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani?

      CHAMA LEGELEGE HUZAA SERIKALI KAMA YA JAKAYA

    6. #24
      sesy nzenga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th June 2012
      Posts : 118
      Rep Power : 373
      Likes Received
      11
      Likes Given
      94

      Default Re: Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani?

      tusitegemehe sana mambo makubwa hakuna kamati ambayo iliundwa ccm ikatimiza haja za watanzania labda ya mwakyembe kidogo na yenyewe kuna mambo ilificha mpaka leo hii

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...