Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tamko la Chama Cha Walimu(CWT)

    Report Post
    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast
    Results 101 to 120 of 149
    1. #1
      Olesambai's Avatar
      Member Array
      Join Date : 31st July 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 346
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Tamko la Chama Cha Walimu(CWT)

      Kufuatia hukumu iliyotolewa hapo jana na mahakama ya kazi ya kuwataka walimu kurejea kazini na kuwaamuru viongozi wa CWT kutangazia Umma kuwa mgomo umekwisha, Chama kimesema kitatoa tamko leo saa 4:00 asubuhi. Tamko hilo litaeleza kama chama kimeridhika na hukumu au wanakata rufaa. Taarifa hiyo haijaweka wazi kama walimu warejee kazini ama laa. Mtoa taarifa amewataka walimu kufuatilia vyombo vya habari saa 4 asubuhi. Nawaomba wadau mtakaopa updates mtuwekee humu. Karibuni.

      =============
      UPDATE
      =============
      Quote By tamuchungu


      Rais Chama cha Walimu nchini (CWT) Mwl. Gratian Mukoba akitoa taarifa ya chama hicho
      --
      UONGOZI wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), umesitisha mgomo uliokuwa unaendelea nchini, hivyo kuwataka walimu kurejea kazini.

      Rais wa chama hicho, Mukoba amesema wameamua kusitisha mgomo, baada ya kuingiwa na hofu ya viongozi wao wa juu kuhofiwa kukamatwa.
      Quote By Losambo
      Chama Cha Walimu Tanzania-CWT-kimetangaza kusitisha rasmi mgomo wa walimu na hivyo kuwataka walimu wote nchini kurejea kazini mara moja kuanzia leo ili kutekeleza majukumu yao ya kila siku kama kawaida.

      Akitoa tamko la CWT kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kukiagiza Chama hicho kitoe maelekezo kwa wanachama wake kurudi kazini, Rais wa Chama hicho GRATIAN MUKOBA amesema walimu wanarudi kazini wakiwa wamekata tamaa kutokana na hukumu hiyo.

      Amefafanua kuwa walimu wanaporudi kazini bila kuwa na mawazo yaliyotulia, utendaji wao utaathirika hivyo Chama kinatoa wito kwa Serikali kukutana na CWT kwa haraka ili kuendeleza majadiliano ya Madai mapya ya Walimu.

      Kuhusu kulipa fidia ya hasara waliyoipata wanafunzi, Chama hicho kimesema kinasubiri taarifa rasmi ya Serikali kuhusu hasara hiyo kwa kuwa hakina uwezo wa kufahamu hasara waliyoipata wanafunzi.

      Kwa mujibu wa Mwalimu MUKOBA wenye uwezo wa kuwasilisha hasara hiyo ni mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Serikali.

      Hapo jana Chama hicho kilipongeza kauli ya Rais JAKAYA KIKWETE yakusema Serikali inajali na kuthamini mchango wa Walimu nchini"

      Mytake:

      Mara kwa mara nimekuwa nikiwaona viongozi wa CWT ni wasaliti na katu hawatawatoa walimu katika lindi la matatizo yao ambayo ni ya msingi mkubwa. Naamini wanaendekeza njaa maana wanayofanya hayaingii akilini kabisa.
      Hebi jionee tamko lao baada ya mahakama kusitisha mgomo halafu utarajie serikali itasikiliza madai yao. Kama wangetaka suluhu kwa amani kusingekuwa na haja ya kugoma huko ni kama kumtishia nyau mkubwa.

      Walimu mna kazi kweli.

      Quote By nngu007
      JUMAMOSI, AGOSTI 04, 2012 05:38

      NA GABRIEL MUSHI


      *CWT yatangaza rasmi kurudi darasani
      *Yakusudia kukata rufaa ngazi za juu
      * Mukoba asisitiza madai yao yako palepale
      *Alia na polisi wanaotisha walimu waliogoma

      HATIMAYE Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimesalimu amri na kutangaza kusitisha mgomo wa walimu uliodumu kwa siku kadhaa nchi nzima.

      Kutokana na kauli hiyo, CWT imewataka walimu wote kurudi kazini ili kutekeleza agizo la Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, lililotolewa juzi mjini Dar es Salaam.

      Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema pamoja na mambo mengine, hukumu hiyo imewakatisha tamaa kwa kiasi kikubwa, hivyo wanajipanga kwa ajili ya kukata rufaa.

      Alisema maagizo yaliyotolewa na mahakama yatekelezwa na CWT, baada ya kuipitia kwa umakini hukumu hiyo.

      “Leo (jana), nimewaita kwa ajili ya kutekeleza sehemu ya maagizo ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, yaliyotolewa na Jaji Sophia Wambura kwenye Shauri Na. 96 ya mwaka 2012. Katika hukumu hii, mahakama imeagiza chama kitoe maelekezo kwa wanachama wake kurudi kazini kuanzia leo (jana) Agosti 3, mwaka huu.

      “Kwa maelekezo hayo, chama kinawaagiza wanachama wake kurudi kazini kuanzia leo (jana) kutekeleza majukumu yao ya kila siku, maagizo mengine ya mahakama yatatolewa maelekezo, baada ya kupitia hukumu kwa makini na kupata ushauri wa wakili wetu na wanachama watajulishwa,” alisema.

      Alisema kuhusu kulipa fidia ya hasara waliyoipata wanafunzi, chama kinasubiri taarifa rasmi ya Serikali, kwa kuwa CWT haina uwezo wa kufahamu hasara waliyopata wanafunzi.

      Alisema mwenye uwezo wa kuwasilisha hasara hiyo, ni mlalamikaji katika kesi hiyo, ambaye ni Serikali.

      “Kwa kuwa hukumu hii, imewakatisha tamaa walimu wanarudi kazini, huku mwajiri wao akionyesha kutowajali kutokana na madai yao kutopewa kipaumbele katika kuboresha maslahi yao.

      “Walimu wanamwangalia mwajiri wao ambaye ni Serikali amewapuuza akifahamu kuwa kwa vyovyote vile atakimbilia mahakamani…hii haijafuta cheti cha kutopatikana kwa suluhu ya mgogoro wa Julai 25, mwaka huu, haiondoi ukweli kwamba maslahi ya walimu ni duni.

      “Pamoja na walimu kuendelea kupuuzwa na mwajiri wao kwa kuwapa maslahi duni, chama kitaendelea na majadiliano na Serikali kuhusu nyongeza ya mishahara na posho kama kilivyowasilisha. Chama kina imani hukumu hii imetoa somo kwa mwajiri ili atambue umuhimu wa kuzungumza na walimu wote nchini,” alisema.




      KUKATA RUFAA
      Kuhusu kukata rufaa, alisema chama hicho kinawasiliana na wakili wake ili kuona uwezekano wa kukata rufaa.

      “Baadhi ya vipengle vya hukumu, vinahitaji ufafanuzi wa Mahakama ya Rufaa ili kuondoa utata wa kisheria, wanachama wanaombwa kuwa wavumilivu wakati huu.

      “Kwa sababu mahakama, imetuonea kwa kipengele wanachodai tulitoa muda kwa Serikali kabla ya kuitisha mgomo katika siku za mapumziko, wakati wao wenyewe walishawahi kutoa saa 3:48 usiku,” alisema.



      WATAKA KULINDWA
      Kuhusu usalama wao, Mukoba alisema katika kipindi cha mgomo baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya, waliamuru wanachama wa CWT na viongozi wake kukamatwa bila na sababu za msingi.

      “Baadhi yao, wamefikishwa mahakamani kwa kuhamasisha mgomo wa walimu, chama kina wasiwasi kuhusu usalama wa viongozi na wanachama walioshiriki na kuhamasisha mgomo wa walimu.

      “Chama kinatoa rai, kwa Serikali na vyombo vya dola, wakiwamo maofisa usalama na makamanda wa polisi wa mikoa na wilaya, kuhakikisha viongozi wa chama na wanachama waliohamasisha mgomo wanakuwa salama bila kudhurika.



      MAZUNGUMZO NA SERIKALI
      Alisema walimu wanarudi kazini bila kuwa na mawazo yaliyotulia, juu ya utendaji wao wa kazi.

      “Chama kinatoa wito kwa Serikali, kukutana na CWT haraka kuendeleza majadiliano ya madai ya walimu, msimamo wetu tangu mwanzo ulikuwa ni kujadiliana na Serikali kupitia kwa msuluhishi, aliyeteuliwa na Tume ya usuluhishi na uamuzi.

      “Tatizo lilikuwa ni serikali ambayo haikuwa tayari kuzungumza na CWT, ushahidi umeonekana kuwa muda wa siku 50 za mgogoro huu, hakuna mwakilishi wa Serikali aliona umuhimu wa kukutana na viongozi wa CWT kuzungumza nao, badala yake waliamua kutumia vyombo vya habari kukishambulia chama.

      “Chama kinashauri Serikali ichukue hatua za haraka kutibu majeraha ya walimu kwa kujadiliana na CWT kuhusu madai yao na kufuta barua zote zilizosambazwa kwa walimu kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu,” alisema.

      Julai 30, mwaka huu, CWT kiliitisha mgomo wa walimu nchi nzima ili kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao ambayo ni nyongeza ya mshahara kwa asilimia 100, posho ya walimu wanaofundisha masomo ya sayansi asilimia 55, walimu wa sanaa 50 na mazingira magumu 30. Lakini Rais Jakaya Kikwete akihutubia taifa katika utaratibu wake aliojipangia, alisema Serikali haina uwezo wa kulipa madai ya walimu kutokana na bajeti ndogo iliyopo
      .

    2. Miaka 50

    3. #101
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,057
      Rep Power : 0
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By Babuu Rogger
      Jamani Kuulimboka kuna tisha.
      kweli kabisa,ni vyema sana kwa watumishi wa umma kutumia zaidi majadiliano ya mezani kudai haki zetu,

    4. MI6
      #102
      MI6's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 19th July 2012
      Posts : 142
      Rep Power : 373
      Likes Received
      17
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By Crashwise
      Kumbuka pia kipato cha walimu ni kidogo sna na juzi walitishiwa hawatalipwa mishahara kama wataendelea na mgomo....lakini kama wangekuwa na kipato kizuri wakawa na akiba angalau miezi mitatu wangeliendeleza kwasasa acha waendelee na mgomo baridi mpaka mwaka 2015. waakuwa na mchango mkubwa sana kuiondoa serikali hii ya kibabe....
      Hii comment nimeipenda ki ukweli.sijui
      kama serikali inaplan B ya watu wa kusimamia uchaguzi 2015 au imeamua liwalo na liwe...

    5. #103
      masalu mhalagani's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th July 2012
      Posts : 11
      Rep Power : 345
      Likes Received
      0
      Likes Given
      26

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      Ee Mugu tusaidie!!zaidi ya 3/4 ya watz wana umaskini wa kipato(income poverty),kwa hy wengi wa watoto wa tz wanasoma kwenye public schools,bila elimu(c ile ya kwenye matokeo ya mitihani) watu hawa watakua watumwa either wa waafrika wenzao ama wa mataifa wengine e.g wacpojua jiografia vyema,hawatajua mipaka ya nchi hii wanamoishi,maliasili muhmu kama mafuta na inakoweza kupatikana nchini,etc!!mgomo baridi ni kusababisha kuperish kwa taifa letu cku ww ukiwa kaburini,vijana wachache wa cku izo watatulaum wote sio jk tu!!mi naona bora kufikiria kitu kingine ila co kufundisha uongo au kutofundisha kabsa,kama unaona huwz kuona njia mbadala ebu imiza wenzio labda kuna m2 anaweza akaja na mawazo mazuri!!MUNGU IBARIKI TANZANIA

    6. #104
      cjilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Behind you
      Posts : 391
      Rep Power : 468
      Likes Received
      119
      Likes Given
      157

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      ndo nini sasa umewapotezea wenzio muda mpaka wamekosa kazi ya sensa halafu unasitisha mgomo kirahisi namna hii, unafikiri siku nyingine watakuamini tena? Umeshapoteza imani kwao, ungejipanga mapema serikali imekushika sehemu ndogo sana, ungewauliza madaktari wakupe muelekeo kuwa wao kuwa walifanyeje?
      liwalo na liwe

    7. MI6
      #105
      MI6's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 19th July 2012
      Posts : 142
      Rep Power : 373
      Likes Received
      17
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By Kakalende
      Walimu waliunga mkono mgomo huu lakini viongozi wao wamewaangusha, tena wamechangia sana kufanya mgomo ushindwa. Siamini kama viongozi wa cww hawakujua taratibu za kufuata au walishirikiana na serikali kukiuka kanuni makusudi ili mgomo ushindwa. Si ajabu JK alivyoongelea suala lao juzi alikuwa mpole vile?

      Je, walimu bado mna imani na viongozi wa ccw katika kutetea maslahi yaenu? Mkoba anasema mgomo umefanikiwa; je, walimu wamepata yale waliyokuwa wanapigania au mmeishia kuwakosesha masomo watoto wetu?

      Mkoba inabidi ataueleze iwapo walimu waendelee kumwamini kuandaa mgomo mwingine!
      UKITAKA KUELEWA ANACHOSEMA MKOBA.
      kaa mwezi 1 fanya kama unatembelea shule yoyote ya serikali jirani nawe ndo utajua nini mkoba anamaanisha.
      Siku mwl akiacha kugoma utajua tu ila kwa sasa mwl amegoma na ataendelea kugoma mpaka watu mtamuelewa mwl akigoma ni madhara gani yanayojitokeza...


    8. #106
      Peter Kabelelo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th August 2009
      Posts : 13
      Rep Power : 500
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      Quote By ruttashobolwa
      Duuuuuuh! Kweli uoga ni kitu kibaya!
      Ndo hivyo! taifa la wananchi kama kondoo husababisha serikali kuwa umbwa mwitu! ni principle

    9. #107
      Jiwe Linaloishi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th May 2008
      Location : Mlimani
      Posts : 3,109
      Rep Power : 17239
      Likes Received
      1624
      Likes Given
      1125

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      tunarudi kwasababu tumelazimishwa na mahakama lakini msitegemee tutafundisha... subirini division Omari... tu
      SEMA UKWELI UMWAIBISHE SHETANI

    10. #108
      TEMILUGODA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2012
      Posts : 954
      Rep Power : 558
      Likes Received
      134
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By master gland
      That`s what expected, For now retreat is the only solution, ili tujipange upya na shule zikifunguliwa tunarudi kudai chetu hadi kielewekeHatuwezi kukubali katika familia moja ya baba na mama mmoja watoto wanapata distingushed service lazima kitaeleweka

      TUNAFIKIRI PART 1 IMESHASOMEKA LENGO LILIKUWA NI KUWA ALERT KUWA SISI WALIMU TUKIAMUA TUTANAWEZA NA HAKUNA WA KUTUZUIA SASA BASI HII PART 2 ITAKAYOFIKA BAADA YA KUFUNGUA SHULE HAKUNA KINACHOWEZA KUTUSTOPISHA KWANI HATA HUKO WANAKOTEGEMEA KUKIMBILIA TUTAKUWA TAYARI KWA LOLOTE.

      MY FELLOW TEACHERS THIS IS JUST A BEGNING THE REALLY PICTURE IS SOON TO COME NO BODY CAN STOP ITBIG UP MUKOBA WE WILL FIGHT TOGETHER UNTIL THEN
      Causation zipo3,1ni necessary cause eg.meza ya mazungumzo[tayari],2ni emmediate cause eg.mgomo[tayari] na tatu ni ultimate cause eg.maandamano[yatafuata tu]baada ya hapo kitaeleweka2.

    11. #109
      Meshack G's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th December 2011
      Posts : 34
      Rep Power : 381
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Ng`wanakidiku
      Nimeipenda hii. Hawana dili hawa waalimu. Kwanza ni watu ambao serikali haiwapendi kabisa na inaweza kuwafukuza any time!!
      Acheni dharau na kejeli, hasa mtu anapodai haki kwa mwajili wake. Ninyi mpo hapa na unaandika na kuchangia leo kwenye hii JF, Mwalimu ndiye aliyekusaidia. Laana itakuwa juu yenu kwa kumtukana mwalimu. Shiiittt!!!

    12. #110
      j joni's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 49
      Rep Power : 369
      Likes Received
      10
      Likes Given
      15

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      Maneno yako aliwahi kuyasema Mwl. E. Kezilahabi. soma shairi lake.
      Sikilizeni wimbo huu:
      Nilipokuwa mtoto niliitwa Chacha
      Kwa matamshi yangu ya sasa
      Nilipokuwa kijana niliitwa Chaupele
      Nilipokuwa mtu mzima niliitwa Manywele
      Nilipokuwa Mwalimu nikaitwa Bure.

      Huu utakuwa wimbo wako
      Utakapostaafu urudipo nyumbani
      Umelewa kangara na nyayo zako
      Zikishindwa kulenga njia nyembamba vijijini.
      Utakuwa kichekesho cha watoto
      Watakaokuita, Ticha! Popote upitapo.

      Kumbuka Mwalimu utakapostaafu.
      Mijusi watataga mayai ndani ya viatu
      Vyako vilivyokwisha visigino
      Na ndani ya sidiria chakavu
      Zilizoshikizwa kamba kwa pini.
      Mende watazaliana ndani ya chupa tupu
      Za marashi na za bia.

      Na manyigu yatajenga ndani ya kofia
      Zilizosahaulika kutani.
      Utakapokufa nge watazaliana
      Chini ya jiwe juu ya kaburi lako,
      Na mlevi fulani (isome fisadi) akipita atapenga
      Na kupangusa vidole kwenye jiwe pweke.
      Mwanzo na mwisho wako ndio huo.

      Lakini wakati ungali hai
      Unaweza kubadilisha mkondo wa maji.
      Lakini kwanza tuzungumze. Wewe na mimi.
      Acha mioyo yetu izungumze.
      Baada ya kunyanyaswa
      Na kisha nusu mshahara.

    13. #111
      mwita ke mwita's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th August 2010
      Posts : 671
      Rep Power : 0
      Likes Received
      59
      Likes Given
      112

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      afadhali they have done something

    14. #112
      Duduwasha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 2,620
      Rep Power : 6249
      Likes Received
      523
      Likes Given
      418

      Default Walimu na Mgomo Baridi Wasema Mpaka Kieleweke

      Hi Picha nimeiona Sehemu nina ipa Like kwa Machungu... Sijui nilie!!!Liwalo na Liwe... kama Kiwete anasema haina uwezo wa Kuwalipa mimi napoana watoke Madarakani wapishe wanaoweza Kuendesha Nchi .. huyu jamaa tukimuacha atatuachia nchi yenye Wajinga wengi... Dawa ya Jeuri ni Kusudi ila Watakao umia ni Wananchi...

    15. #113
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 548
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      jaguar- KIGEUGEU! watz vigeugeu.
      MZUNGU AKIJICHUBUA HUJUE MOYONI ANA UAFRICA!.by stamina

    16. #114
      coil's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th July 2012
      Posts : 19
      Rep Power : 346
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Jiwe Linaloishi
      tunarudi kwasababu tumelazimishwa na mahakama lakini msitegemee tutafundisha... subirini division Omari... tu
      Sasa mkisha fika shule si mfundishe tu hao watoto,kama mliamua kugoma mngejipanga mfanye mgomo wa ukweli au huo wa awamu ya pili mgome mgomo wa kutikisa serikali ila kwa sasa muwafundishe tu.

    17. #115
      Manager's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st April 2011
      Posts : 453
      Rep Power : 500
      Likes Received
      61
      Likes Given
      363

      Default Re: CWT chasitisha mgomo rasmi

      Quote By ruttashobolwa
      Duuuuuuh! Kweli uoga ni kitu kibaya!
      At least they have tried. A message has been delivered to the masses ready for 2015 election. Heri mwoga anayejaribu kuliko shujaa aliye nyuma ya screen ya computer

    18. #116
      lugisi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 20
      Rep Power : 349
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Walimu na Mgomo Baridi Wasema Mpaka Kieleweke

      Ni matatizo makubwa sasa hakuna elimu

    19. #117
      lugisi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 20
      Rep Power : 349
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Walimu na Mgomo Baridi Wasema Mpaka Kieleweke

      vyema kuiondoa serikali ya ccm tu madarakani

    20. #118
      African teacher's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st August 2012
      Posts : 24
      Rep Power : 347
      Likes Received
      2
      Likes Given
      1

      Default Re: Walimu na Mgomo Baridi Wasema Mpaka Kieleweke

      Tuiondoeni mapema hyo kitu kabla ya 2015,mbegu chafu sana Kikwenga

    21. #119
      lugisi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 20
      Rep Power : 349
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Walimu na Mgomo Baridi Wasema Mpaka Kieleweke

      tusiseme tu uamuzi tunao sisi

    22. #120
      Fredrick Sanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2011
      Location : Kijitonyama
      Posts : 2,982
      Rep Power : 2590
      Likes Received
      637
      Likes Given
      776

      Default Re: Walimu na Mgomo Baridi Wasema Mpaka Kieleweke

      Duhhhhh.
      We shall overcome, righteousness shall always prevail.

    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...