Hali ya nchi imekuwa tete,kila idara ya utumishi wa umma imeingia kwenye mgomo,kinacho lalamikiwa ni madai ya msingi ya haki za watumishi,alkini serikali inayachukulia madai haya kama kero na kelele za mpangaji hazimzui mwenye nyumba kukosa usingizi.Tumeona mgomo wa madaktari na sasa mgomo wa waalimu.
Imekuwa ni kawaida sasa kwa serikali yetu sikivu kushindwa kutumia usikivu wake kukaa meza moja na watumishi wake ili kupata suluhisho la madai yao.Suluhisho limekuwa ni mahakama huku serikali ikitumika kutoa kauli ambazo mwisho wa siku mhimili wa mahakama uhitimisha kwa hukumu iliyo kwisha kutamkwa na serikali. Nini hatari yake,hatari yake ni mgongano wa madaraka na kuingilia uhuru wa mahakama.
Sisi sote ni mashahidi,tumeona serikali sikivu mara zote ikishindwa na kukimbilia mahakamani wakati huo huo kesi haijatajwa wao hukimbilia kwenye media na kutangaza migomo hiyo ni batili.Kuna haja gani basi ya kukimbilia mahakamani ikiwa tayari imeshatekeleza hukumu itakayo tolewa na mahakama? Hali kama hii athari yake kubwa ni uvunjivu wa amani tuliyo jivunia kwa miongo zaidi ya mitano.Ifike wakati kila mhimili mmoja uheshimu mhimili mwingine ili kulinda mgongano wa kimadaraka unao fanywa na serikali yetu sikivu.
Serikali hiyo hiyo sikivu kupitia kiongozi wa mhimili wa bunge imekuwa ikitumia rungu lake ipasavyo kuhakikisha hoja zote zinazo husiana na migogoro ya watumishi na serikali haijadiliwi bungeni kwa kigezo cha hoja hiyo iko mahakamani ilihali serikali ikitoa hukumu nje ya mahakama.Naomba wakuu wa JF tuliangalie hili kwa umakini ili kunusuru uchafuzi huu wa hali ya hewa kwa mgongano wa madarakaw unao fanywa makusudi na serikali yetu sikivu kwa mustakabali wa amnai ya nchi yetu.
Naomba kuwakilisha.

Reply With Quote


Follow Us Here