Takashi,
..sidhani kama Nyerere alihusika na kifo cha Karume.
..Wanamapinduzi walianza kumalizana wenyewe kwa wenyewe na ninaamini hicho ndicho kilichopelekea Karume kuuwawa.
..Nakuomba uwe mkweli, na utueleze ni Mzanzibari gani ameuawa ktk ardhi ya Tanganyika wakati Nyerere akiwa madarakani.
..Pia kabla ya kifo cha Karume kulikuwa na majaribio 14 ya kujaribu kumuondoa madarakani. Bila muungano, au bila Nyerere, uwezekano mkubwa kungetokea mapinduzi mengine Zanzibar.
..Kuhusu OIC, na manung'uniko yenu, naomba kukumbusha kwamba Tanganyika tulivunja uhusiano wetu na Ujerumani Magharibi pale walipojaribu kutulazimisha tuvunje uhusiano wetu na Ujerumani Mashariki. Kumbuka kwamba Zanzibar ndiyo waliokuwa wa kwanza kuwa na mahusiano na Ujerumani Mashariki.
..Sasa huwezi kusikia Tanganyika tunawalaani Wazanzibari kwa kukosa misaada ya Ujerumani Magharibi. Katika muungano wowote lazima kuwa na spirit ya "nipe-nikupe."
..Suala la OIC sidhani kama kuna ulazima wa kuliangalia kama kero na kusema ndiyo sababu ya kuvunja muungano. After all tuna mashirikiano[kidiplomasia, kibiashara,kiutamaduni] na nchi nyingi zilizoko ktk jumuiya ya OIC. Katika mazingira hayo sidhani kama kujiunga na OIC kutaleta mabadiliko makubwa ktk hali ya uchumi ya Zanzibar au Tanganyika.
..Tatizo lingine ni kwamba hamuutendei haki muungano, and in the process u put yourself down. Mfano mzuri ni madai yako kwamba Zanzibar haiwezi kuwa na mashirikiano ya kimataifa bila kupata kibali cha Membe. Unasahau kwamba wizara hiyo ni yetu sote, na kuna wakati iliongozwa na Salim Ahmed Salim, na Ahmed Hassa Diria, wote ni Wazanzibari. Hata sasa hivi Naibu waziri wa mambo ya nje anatokea Zanzibar.
..Kwa mtizamo wangu Zanzibar haijabanwa na Tanganyika. Labda utueleze, other than OIC, ni chombo gani ambacho ZNZ ilipenda kuwa na mahusiano nacho lakini imekwamishwa na muungano.
..Suala la kukopa nje sina utaalamu nalo, lakini I am tempted to speculate kwamba ZNZ inakopesheka zaidi ikiwa imefungamana na Tanganyika kuliko ikiwa yenyewe. Mtakapogundua mafuta hali hiyo itabadilika lakini in the mean time nadhani kuna advantage mnazopata kwenye muungano.
..Mwisho, ni hatua gani za kiuchumi ambazo ZNZ ingependa kuchukua lakini mkazuiwa na muungano au Tanganyika? Je, muungano ndiyo umeangusha zao la karafuu ambalo ndiyo lilikuwa mhimili wa uchumi wa ZNZ? Je, muungano umewazuia wa-ZNZ kuwa sekta mbadala ya uchumi zaidi ya karafuu? Je, utalii umeshindwa ZNZ kutokana na muungano? Kwanini ZNZ na Tanganyika zinashindwa na Seychelles,Mauritius,Kenya,Egy pt,Afrika Kusini, ktk kuvutia watalii?
..Kwa maoni yangu wa-ZNZ mnaburuzana,hamko honest with each other, ktk hizi harakati za kuvunja muungano. Sababu hiyo ndiyo inayopelekea kuibuka kwa mawazo ya ajabu-ajabu kama vile "muungano wa mkataba", au "muungano wa Swiss", au hata serikali 3. Kama muungano ni mbaya kiasi hicho basi kungekuwa hakuna kumung'unya maneno ktk harakati za kuuvunja.
Follow Us Here