
By
Mrimi
Kwanza nikiri kwamba kukosoa ni utamaduni wa kujenga, hapo hakuna shaka.
Umeanza vizuri kabisa mkuu, ila mimi napingana na wewe kidogo hapo kwenye red. Sishangai kwani unapokuwa vitani huchagui silaha. Na hii imekuwa silaha ambayo wapinzani wa CDM wamekuwa wakiitumia kwa muda mrefu sasa, inagawa binafsi naona kama kwa sasa haina nguvu sana ktk vita hii.
Kitu ambacho watu wengi sasa, ama kwa makusudi au kwa kutokujua, mfumo wa kisiasa wa sasa sio kama ule wa kumwondoa mkoloni. Kipindi cha uhuru, adui alikuwa mkoloni, kwa hiyo vuguvugu la mageuzi lilijumuisha jamii zote za kitanzania. Ila kwa sasa ni tofauti, vuguvugu la mageuzi linahusu jamii moja, yaani familia moja(Tanzania). Kwa maana kwamba unapambana na adui ambaye ni ndugu yako, ili upate support itategemea jinsi gani utawashawishi wanafamilia wenzako kukuunga mkono.
Kwa maana hii mwanzo wa mageuzi lazima utaanza na mtu mmoja, kisha wawili, theni watatu, wanne, watano.... nk. Kwa vyoyote huwezi kuanza na kupata wafuasi wengi kwa mara moja. Hilo sijui kama unalitambua au la, ila kumbuka unapokuwa unaanza vuguvugu kama hili adui yako naye hajalala. Lazima na yeye anatafuta mbinu za kukudhoofisha, ndio maana hapa hata wewe unatumika kuwadhoofisha wapinzani. Hii ni haki yako kabisa, maana haya ni mapambano.
Kwa issue ya ukanda au ukabila/familia halina tofauti na maelezo yangu ya hapo juu. Siku zote vuguvugu la mageuzi huanza na watu wenye mawazo na itikadi inayofanana. Hii haimfungi mtu kuanza na jamaa zake, wafanyakazi wenzake, marafiki zake kwa sababu unapoanza kunadi sera zako ni lazima utaanza na watu walio karibu yako. Na hii ina sababu nyingi tu, maana pengine ndio watu unaowaamini, mimi sioni kama hilo ni tatizo. Hata wewe kesho ukifikiria kuanzisha taasisi fulani, watu wa kwanza kuwaona lazima ni watu wako wa karibu unaodhani unawaamini.
Kuhusu kuenea sehemu mbalimbali nchini, hii iko wazi. Moto siku zote utaanza na majani makavu point A kisha utaenea hadi point B, C, D....nk. Namaanisha kwamba kuenea kwa CDM sehemu mbalimbali nchini kutategemea uwezo na kasi yake ya kujinadi, ambayo hata hivyo lazima ku'overcome resistance kutoka kwa wapinzani wake wanaozidi kila kukicha. Lakini hata hivyo wanajitahidi, maana hata wewe umekiri kwamba uchaguzi uliopita wamepata mafanikio fulani. Huu kwao ni mwanzo mzuri.
Kuhusu mgogoro wa uongozi ndani ya chama, mimi huwa sipendi kuishi kwa hisia. Maana mambo mengi yamekuwa yakichukuliwa kwa
'hear said' tuuu, lakini ukijakufuatilia unakuta ni mbinu tu za kuwombea adui yako njaa. Lakini ukweli unabaki kwamba muda huo ukifika kila kitu kitakuwa wazi, tutajua nani ndiye nani.
Ninachosisitiza ni kwamba,sio tu CDM, bali hata vyama vingine vilivyopo na vitakavyoanzishwa, visinyimwe fursa ya kujieneza kwa sababu nyepesi nyepesi kama hizi ulizotoa hapa. Waachwe watanzania wachague vyama na viongozi wanaowataka.
Nadhani nimeeleweka mkuu.
Follow Us Here