JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

  Report Post
  Page 7 of 37 FirstFirst ... 56789 17 ... LastLast
  Results 121 to 140 of 721
  1. Mtoto wa Mkulima's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th April 2007
   Posts : 954
   Rep Power : 940
   Likes Received
   63
   Likes Given
   2

   Default Ni lake Nyasa au Lake Malawi?

   Wakubwa niwekeni sawa, nilikuwa nauliza Ziwa Nyasa ni Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi? Na je, Kwanini Ziwa Victoria liendelee kuitwa Ziwa Victoria na si Ziwa Nyanza? Au ndio kuwaenzi watawala wetu wazungu?

   Lake Nyasa or Lake Malawi?
   The name of the lake itself is also disputed. Malawi claims the lake is named 'Lake Malawi' while international maps and other countries (most notably Tanzania) claim the name of the lake to be 'Lake Nyasa'. The origins of the dispute in the name have their background in geopolitical disputes that began prior to Malawi's independence in 1964, when it was previously known as Nyasaland.

   Further complications emerged for different political reasons in the 1960s, when the then President Banda (of Malawi) became the only African leader to establish diplomatic relations with white South Africa. This was fiercely repudiated by other African leaders, including the then President Nyerere (of Tanzania). The contrasting attitudes and policies gave further impetus to disputes between the two governments, on the name of the lake itself, and the boundary between the two countries.

   At present, the dispute between the two governments is largely dormant. Intergovernmental relations between Malawi and Tanzania are largely cordial.


   Tanzania-Malawi dispute
   The partition of the lake area between Malawi and Tanzania is disputed. Tanzania claims international borders through the lake along the lines of the borders between the German and British territories before 1914; Malawi, meanwhile, claims the whole non-Mozambican lake, including the waters next to the Tanzanian shore. The foundations of the dispute were set when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, put the water under the jurisdiction of Nyasaland without a separate administration for the Tanganyika portion. The dispute has led to conflicts in the past, though for several years Malawi has declined to enforce its claims to the disputed portion.

   Occasional flare-ups in in the 1990s and in recent times have impacted fishing rights, particularly of Tanzanian's who reside on the lake shore, who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.
   Quote By Mwawado View Post
   Habari hiyo hata Mimi nimewahi kuisikia, hata ukiangalia Ramani ya ziwa hilo linaitwa Ziwa Malawi tofauti na hapo zamani tulipoliona kwenye ramani kama ziwa nyasa. Nashindwa kuelewa kwa dhati kama mpaka umegawanywa upya ama ndio yale yale ya kuambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.Inapaswa mipaka ya nchi yetu iwekwe wazi ili kutokuja kupoteza maeneo na Vivutio vyetu vya asili.

   Mpaka wa Tanzania na Malawi una matatizo ya muda mrefu, nakumbuka mwaka 1978 kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi, kwa siku mbili mfululizo kulikuwa na amri ya kutokuwasha Taa katika Mji wa kyela mkoani Mbeya, Kipindi hicho nilikuwa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa Wakati Huo Mzee Richard Wambura alisema Mwl Nyerere ameamuru majeshi yetu yarudishe mapigo kama itaonekana Banda ataingiza majeshi Kyela. Serikali ya Banda ilikuwa inadai maeneo ya Matema Beach, Mto Songwe mpaka Ipinda yapo ndani ya Ardhi ya Malawi.

   Sasa inawezekana kabisa tumelitoa kwa hiyari ziwa liwe upande wa Malawi nasi tumebakiwa na Bandari tupu ya Itungi,ambayo sasa nafikiri haina hata meli moja baada ya TACOSHILI kufa.
   Quote By Gamba la Nyoka View Post
   Kama serikali imelitoa hilo ziwa kwa Wamalawi pasipo kuhusisha maoni ya Watanzania, basi serikali inalo la kujibu. Huwezi kuwaambia wananchi waliokaa pale miaka nenda rudi eti, hayo maji usiyaguse ni ya wamalawi hayo.

   Hili suala ni lazima serikali ilitolee kauli haliwezi kuwa kimya kimya milele!
   Quote By Ruge Opinion View Post
   Miaka ya 1970 Kamuzu Banda, rais wa Malawi, alitangaza kuwa lile ziwa lote ni la Malawi na akaanza kuwabugudhi Watanganyika waliokutwa kwenye ziwa. Nyerere akasogeza majeshi pale na kumtumia ujumbe Kamuzu aache uchokozi. Kamuzu akanywea.

   Tangu hapo hakujawahi kuwapo maelewano rasmi.

   Hilo ziwa lilikuwa linajulikana kama ziwa Nyasa kutokana na wenyeji pande zote mbili kuwa Wanyasa. Malawi vile vile ilikuwa inajulikana kama Nyasaland. Walipopata uhuru wakabadili jina na kujiita Malawi. Kwa hiyo na jina la ziwa wakalibadilisha bila makubaliano na sisi. Kwa hiyo kwao ni Ziwa Malawi na kwetu ni Ziwa Nyasa.
   Quote By kajembe View Post
   Mgogoro huo ulianza enzi ya Kamuzu Banda alipokuwa raisi. miaka ya sitini Kamuzu alikuwa anazungumza kwenye redio yao, Malawi Broadcasting Corporation kutoka Blantyre, Malawi, na kusema ziwa lote ni la Malawi na pia wilaya ya Rungwe na hadi Mbeya ni sehemu ya Malawi.

   Kuna siku mwezi wa September 1968 Nyerere alimwita Banda ni kichaa. Alikasirika sana kwa sababu ya madai ya Mzee Kamuzu kwamba sehemu za Tanzania ni za Malawi. Alidai hata Mbamba Bay na sehemu zingine mkoani Ruvuma karibu na Ziwa Nyasa kwamba ni za Malawi. Pia alidai jimbo lote, Eastern Province, la Zambia. Kaunda alimjibu Banda na kusema ni shauri yake akitaka kuanzisha vita.

   Kabla ya mgogoro huo, Banda alikuja Tanzania na kukutana na Nyerere mwaka 1962 na kumwambia hakuna nchi ya Mozambique. Alimwambia Nyerere wagawane nchi hiyo. Alimwambia Nyerere sehemu ya kaskazini ya Mozambique, sehemu ya Wamakonde jimbo la Cobo Delgado, "ni lako" Nyerere. Ni sehemu ya Tanzania. Sehemu za Mozambique zilizobaki ni za Malawi, Rhodesia na Swaziland. Nyerere alimpuuza tu.

   Baada ya miaka michache, 1968, Kamuzu akatangaza na kusema sehemu zetu za Tanzania nilizozitaja hapo juu ni sehemu za Malawi.

   Mzee Kamuzu alikuwa ni mkorofi sana.

   CHANZO CHA MGOGORO

   Mgogoro wa ziwa umetokana na uamuzi wa wakoloni wa Kiingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao wa Nyasaland wakati walipokuwa wanatawala nchi hiyo na ilipokuwa ni British Protectorate. Walifanya uamuzi huo baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu ya kwanza na Waingereza walipoichukua German East Afrika - iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika katika Kijerumani - na kuwa koloni yao ya Tanganyika. Kabla ya hapo, kutokana na makubaliano kati ya Waingereza waliokuwa watawala wa Nyasaland na Wajerumani waliokuwa watawala wa nchi yetu, mpaka wa ziwa ulikuwa kati ya ziwa. Na ndiyo mpaka huo tu ambao ni halali pamoja na jina kuitwa Nyasa, siyo Malawi.

   Uamuzi wa Waingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland haukubadilisha mpaka wa ziwa kihalali kwa sababu mipaka yote ya nchi zetu ilikubaliwa wakati bara letu lilipogawanywa na wakoloni. Ni mipaka hiyo ambayo hata sisi tuliikubali baada ya kupata uhuru na hakuna hata nchi moja ambayo ina haki peke yake ya kubadilisha mipaka hiyo. Hata Waingereza hawakuwa na haki ya kulikiweka Ziwa Nyasa chini ya ukoloni wao Nyasaland kwa sababu walivunja makubaliano yao na Wajerumani ambayo yalisema mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo: nusu ni sehemu ya Deutsch Ostafrika ambayo sasa ni Tanganyika, na nusu nyingine ni ya Nyasaland chini ya utawala wa Waingereza.

   Hata wilaya ya Rungwe ambayo ilijumuisha Kyela na Ileje ilikuwa inatawaliwa kutoka Nyasaland mara tu baada ya Wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza na Waingereza walipopewa madaraka ya kutawala nchi ambayo ilikuwa ni koloni ya Wajerumani; yaani nchi yetu ya Tanganyika.

   Deutsch Ostafrika - German East Africa - ilikuwa ni nchi tatu: Tanganyika, Ruanda na Urundi (nchi ambazo zilibadili majina na kuitwa Rwanda na Burundi mwaka 1962 baada ya kupata uhuru).

   League of Nations - jumuiya ya mataifa iliyoitangulia United Nations - iliwapa Wabeligiji Ruanda na Urundi. Koloni hizo mbili za Wabeligiji zilikuwa zinatawaliwa kutoka Leopoldville, mjii mkuu wa Belgian Congo, nchi ambayo pia ilikuwa inatawaliwa na Wabeligiji. Mpango huo ni kama vile wilaya ya Rungwe ilipowahi kutawaliwa kutoka Karonga na Waingereza waliokuwa wanatawala wa Nyasaland na baadaye kiuchukua nchi yetu ya Tanganyika kutoka kwa Wajerumani.

   Baada ya vita kuu ya kwanza, na Wajerumani kushindwa vita hiyo, waziri mkuu wa Uingereza, Lloyd George, kwenye mkutano wa League of Nations alimwambia raisi wa USA, Woodrow Wilosn, kwamba aichukue German East Africa, yaani nchi yetu, na kuiweka chini ya utawala wa Merikani baada ya Wajerumani kuipoteza nchi hiyo katika vita kuu ya kwanza. Lakini President Wilson alikataa. Angekubali, nchi yetu ingetawaliwa na USA na tungekuwa koloni ya USA. Baada ya Rais Wilson kukataa kuichukua nchi yetu, Lloyd George akakubali na kusema ataichukua Tanganyika na kuiweka chini ya utawala wa nchi yake ya Uingereza. Tuliponea chupuchupu kuchukuliwa na Wamerika. Nchi yetu ingechukuliwa na Wamerika, labda tusingepata uhuru. Wamerika wangeing'ang'ania nchi yetu kama vile walivyo ng'ang'ania nchi zingine walizochukua bila kuzipa uhuru.

   Kuhusu Ziwa Nyasa, kwa kifupi ni kwamba mpaka halali uko kati ya Ziwa. Ni mpaka ambao Wajerumani na Waingereza walikubaliana kuzigawa koloni zao: Nyasaland kuwa ya Waingereza; nchi yetu, Deutsh Ostafrika, kuwa ni ya Wajerumani. Walikubaliana kwamba mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo. Upande mmoja tu, Waingereza, hawakuwa na haki ya kubadili mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland walipolikweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland.

   Nukuru kutoka kitabu cha Nyerere and Africa: End of an Era, ukurasa 484:

   "Dr. Banda also claimed substantial parts of Tanzania, including - Rungwe district - and the rest of Mbeya Region in southwestern Tanzania, as Malawian territory. He also claimed the entire Eastern Province of Zambia, provoking a curt response from Zambia’s president, Dr. Kenneth Kaunda, who challenged Banda to 'Go ahead and declare war on Zambia.'

   And President Nyerere dismissed Banda’s claim to large chunks of Tanzanian territory as 'expansionist outbursts, which do not scare us, and do not deserve my reply.' The outlandish claim also drew a sharp response from Nyerere who said Dr. Banda was 'insane.' But, he warned, 'Dr. Banda must not be ignored; the powers behind him are not insane.'"


   Akizungumza ktk chuo kikuu cha Dar es Salaam, November 1997, Mwalimu Nyerere alisema

   "In 1961 we became independent. In 1962, early 1962, I resigned as prime minister and then a few weeks later I received Dr. Banda. Mungu amuweke mahali pema (May God rest his soul in peace). I received Dr. Banda. We had just, FRELIMO had just been established here and we were now in the process of starting the armed struggle.

   So Banda comes to me with a big old book, with lots and lots of maps in it, and tells me, 'Mwalimu, what is this, what is Mozambique? There is no such thing as Mozambique.' I said, 'What do you mean there is no such thing as Mozambique?' So he showed me this map, and he said: 'That part is part of Nyasaland (it was still Nyasaland, not Malawi, at that time). That part is part of Southern Rhodesia, that part is Swaziland, and this part, which is the northern part, Makonde part, that is YOUR part.'

   So Banda disposed of Mozambique just like that. I ridiculed the idea, and Banda never liked anybody to ridicule his ideas.
   So he left and went to Lisbon to talk to Salazar about this wonderful idea. I don’t know what Salazar told him. That was ‘62."
   Quote By Simba mnyama View Post
   Wana-JF,

   Mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa unaonesha ngoma bado mbichi kabisa. Hebu tusome hizi habari kutoka Malawi:

   Lake Malawi/Nyasa row: Time to show strong leadership
   By Cedrick Ngalande August 6, 2012
   At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times. During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time. Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now? Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

   Test for President Joyce Banda to diplomatically manage the dispute on the boundary You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts. Statesmanship is a game because image is everything in international politics.

   A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!
   It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image. The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important! When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’. President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge. If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

   Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian. Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an
   ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE


  2. Kachanchabuseta's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th March 2010
   Posts : 7,303
   Rep Power : 2051
   Likes Received
   633
   Likes Given
   1457

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Jamaa yuko busy na misafara

  3. lutondwe's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 20th December 2010
   Posts : 146
   Rep Power : 587
   Likes Received
   72
   Likes Given
   24

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By Kakalende View Post
   Je, Mh. Membe aliliongelea hili kwenye mawasilisho yake Bungeni? au kama liliwahi kusemewa wadau tuleteeni hapa maelezo ya serikali yenu na hatua gani zimechukuliwa kurekebisha mpaka.
   Binafsi,nadhani kwa vyovyote vile,hakuna hata cm 1 ya kipande cha nchi hii kitatoweka.Lazima tuwe wachungu kama wayahudi vinginevyo watatuchezea.Natamani sisi ndiyo tuwe wa kwanza kuchukua maeneo ya nchi jirani kama vile Msumbiji,Kongo,Malawi na zambia kwani katika historia inaonyesha wakazi wa maeneo hayo yanakaliwa na watu wenye asili ya Tanganyika na waliowengi wanaongea Lugha ya Kibena.Tutarudisha nchi zetu kwa amani.Kwa kuanza tutaanza kuwa kuunganisha kama tulivyofanya upande wa kaskazini mwa nchi.

  4. r2ga's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th April 2012
   Posts : 94
   Rep Power : 508
   Likes Received
   22
   Likes Given
   35

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By TANMO View Post
   Hivi kuna faida gani kuingia vitani kugombania mipaka ilhali kwa kiasi kikubwa wakazi wa maeneo husika wanaingiliana kwenye shughuli zao za kila siku? Mmalawi akitaka mafuta ya taa anakuja Tanzania kuchukua, hivyo hivyo kwa mtanzania anayeishi mpakani. Hebu tujifunze kutumia Diplomasia jamani.

   Nguvu zenyewe za kupigana hatuna, mpaka leo tumeshindwa kupigana na maradhi, na umasikini. Adui ujinga ndiyo anatupiga kila kukicha, hadi Rais wa nchi naye ujinga umemshinda nguvu na sasa ndiyo unaomuongoza kwenye kila analofanya na kusema..

   I just want you to know that, when we talk about war, we're really talking about peace...,

  5. mzeelapa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th July 2010
   Posts : 928
   Rep Power : 766
   Likes Received
   201
   Likes Given
   227

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By rosemarie View Post
   mkuu download google earth utaona mipaka ya taifa
   Hiyo google earth mtu mjanja anaweza kuifanyia mabadiliko namna anavyotaka, na inawezekana hawa Wamalawi wamefanya hivyo hakafu sasa wanadai ziwa lote ni lao. Kujua mipaka lazima ifanyike phyisically achana na mambo ya Google. Hata kwenye atlas za kawaida mipaka inaonekana, lakini ni sahihi?

  6. Kichuguu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th October 2006
   Location : Popote Porini
   Posts : 8,015
   Rep Power : 9270302
   Likes Received
   2691
   Likes Given
   1707

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By Kakalende View Post
   Mwaka jana kuna chi 2 za Amerika Kusini; Nicaragua/Honduras, nusura waingie vitani baada ya mojawapo kufuata ramani ya Google na kutangaza kuwa ndio mpaka wao rasmi.

   Hawa jamaa wa Google, msitari wa mpaka wamechora na rangi nyekundu kisha wanaonyesha LAke Nyasa yote imebaki Malawi, hii imekaaje? Nadhani hili la ugomvi wa mpaka halina itikadi, nakumbuka miaka ya nyuma enzi za Hayati Mwalimu nusura tuzipige na Malawi wakati wa Dr. Banda kwa ajili ya mpaka huu.
   .........Ni kweli, mwaka 1970 tulitwangana kwa siku kama mbili hivi na Malawi kwa sababu ya mpaka huo huo, ambapo Dr. Banda alikuwa akitumia na ureno kusudi wachukua sea advantage dhidi ya Tanzania. Tlimtwanga kwa nguvu sana kwa siku moja tu ikabidi afyate mkia na mpaka ukabaki ule wa mjerumani hadi miaka ya hivi karibuni ndipo tumezan akusikia tatizo hili tena.

   Kulegalega kwa nguvu zetu za kijeshi kutokana na kuendesha nchi bila sera za utaifa bali sera za uwekezaji za IMF basi tutajikuta tunanyang'anywa sehemu kubwa za mipaka yetu na majirani zetu. Mwishoni utasikia Kenya nao wanadai kuwa mlima Kilimanjaro ugawanywe katikati kusudi nusu iwe kenya na ile nusu nyingine iwe Tanzania kwa vile hakuna mantiki mpaka kupinda in favor of Tanzania. M7 naye anaweza kudai kuwa ile sehemu ya Kagera iliyotufanya tutwangane mwaka 1979 nayo......... Hatari zadi ni pale Rwanda itakapodai sehemu kubwa ya Ngara kwa vile ina asili ya rwanda zaidi, na Burundi nayo kudai sehemu kubwa ya Kibondo kwa vile nayo ina asili ya Burundi.................

   Sababu kubwa ya nchi kuwa na majeshi ya ulinzi ni kulinda mipaka yake; sasa sisi tunaposhindwa kulinda mipaka yetu ni dhahiri kuwa jeshi letu haliwezi tena kufanya kazi hiyo. Mipaka ya nchi yoyote yenye jeshi imara la ulinzi huwa inaogopwa na kuheshimiwa sana na majirani zake. Iwapo Tanzania ingetanza kuwa Malawi imeingilia territory yetu na hivyo imetangaza vita dhidi Tanzania; kwa hiyo Tanzania italazimikai kutumia nguvu kulinda mipaka yake, ungeona Malawi wanajirudi tena kwa kuomba suluhu haraka sana. Juzi nilizoma wakiwa wanajibu kwa kejeli kwa vile wanajua kuwa hatuwezi kuwafanya lolote.
   Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo


  7. sembuli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2012
   Posts : 746
   Rep Power : 648
   Likes Received
   351
   Likes Given
   257

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By pumbatupu View Post
   Itakuwa vizuri waki'declare' hivyo ili tupigane manake yale mabomu ya mbagala na g'mboto hayana pa kutumika..nadhani itakuwa muafaka kuanza kuyatumia sasa kuliko hivi yanavyotuua wenyewe..
   pumbatupu: umenichekesha sana,ila kweli wanajeshi wetu wamekaa muda sana bila zoezi kama juzi mwanajeshi kazirai kwa mshituko baada ya gurudumu la basi kupasuka jirani yake, 'hajasikia milipuko muda mrufu'

  8. Juaangavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd November 2009
   Posts : 867
   Rep Power : 790
   Likes Received
   88
   Likes Given
   22

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Nshimbo tell us something on this issue!

  9. Abunwasi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th June 2009
   Location : Urbanite
   Posts : 1,415
   Rep Power : 12179087
   Likes Received
   259
   Likes Given
   498

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By Kakalende View Post
   Mwaka jana kuna chi 2 za Amerika Kusini; Nicaragua/Honduras, nusura waingie vitani baada ya mojawapo kufuata ramani ya Google na kutangaza kuwa ndio mpaka wao rasmi.

   Hawa jamaa wa Google, msitari wa mpaka wamechora na rangi nyekundu kisha wanaonyesha LAke Nyasa yote imebaki Malawi, hii imekaaje? Nadhani hili la ugomvi wa mpaka halina itikadi, nakumbuka miaka ya nyuma enzi za Hayati Mwalimu nusura tuzipige na Malawi wakati wa Dr. Banda kwa ajili ya mpaka huu.

   Guys, dont you find it strange that to the south the border btn malawi and msumbiji goes right in the middle lakini to the north iwe tofauti?????? wanatania hao

  10. Makala Jr's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2011
   Location : Africa
   Posts : 3,396
   Rep Power : 14548
   Likes Received
   1077
   Likes Given
   1

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Mi naona kauli ya serikali kwamba tuko tayari kujibu chokochoko zozote zitakazo oneshwa na Malawi haitoshi.Kama serikali ya Malawi haionyeshi mkakati wa wazi kuhusu ziwa Nyasa basi tuanze sisi.

   Ni lazima tutambue kwamba nchi za magharibi kupitia makampuni yao ya utafiti na biashara ndiyo wanayofanya kazi malawi.Endapo kesho Malawi itatangaza machimbo ya madini ziwani...basi Nchi za ulaya na Marekani wataingia ubia kisha watashirikiana na Malawi kuweka Kambi za majeshi ya majini.

   Hata tukiingia vitani Malawi watasaidiwa hata kwa njia ya siri ili kuidhoofisha Tanzania. Baadaye nchi hizo bepari zitakuwa tayari kutoa mkopo kwa nchi hizi mbili ili kuinua uchumi kwa masharti ya kufungua milango ya uwekezaji kwenye madini na ardhi haswa Tanzania kwa kudai punguzo la kodi ama kulipa madini kwa miaka kadhaa.

   Kwani Reli ya mjerumani tumelipa kwa gharama gani? J.K fungua njia ya Mazungumzo,usisubiri uchokozwe!

  11. Nsabhi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd February 2011
   Posts : 1,063
   Rep Power : 761
   Likes Received
   156
   Likes Given
   167

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Tanzania Tanzania nakulilia Tanzania nani atakulinda? Wale tuliowakabidhi madaraka ya kukulinda wanakuacha ukimrgwa kidokidogo mwishoni si utaisha na kupotea kabisa kwenye ramani ya dunia? Uzalendo uko wapi? Nyerere upo wapi? Njoo ututetee! Hakuna mtetezo aliyebaki. Waliopo ni waoga na kila wao ni michakato tu. Nchi yetu inavamiwa na Wamalawi na Warundi hakuna wa kuitetea!
   Quote By LordJustice1 View Post
   Wewe kichwa chako kibovu sana! Tukiwa wajinga wataendelea kumega mipaka kama akina Iddi Amini alivyodai kwamba Kagera Salient iko Uganda! Sasa hivi nako Warundi wameumega mpaka wetu! Kamuzu Banda naye aliwahi kudai kuwa Wilaya yote ya Kyela iko Malawi! Kwa hiyo wewe kwa akili yako finyu tukae kimya tu ili "kuogopa malumbano na vita?" Open your mind please!

  12. Nsabhi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd February 2011
   Posts : 1,063
   Rep Power : 761
   Likes Received
   156
   Likes Given
   167

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Wewe huna hata chembe ya uzalendo. Hapa tunachosema na kwamba ziwa Nyasa ni letu pia
   Quote By Mzee Kijana View Post
   Ukweli ni kwamba kwa mujibu wa mkataba wa kikoloni wa Heligoland (Heligoland Treaty of 1890) ziwa lote ni sehemu ya Malawi. Tanzania haina nguvu yoyote ya kisheria inayoweza kufanya ishinde kesi kama itapelekwa mahakama ya dunia. Tunachofanya kwa sasa ni ubabe tu. Malawi wana haki kutokana na mikataba ya mipaka tuliyorithi kutoka kwa wakoloni ambayo kila nchi inapaswa kuiheshimu. Vipi nao Wakenya wakidai mlima Kilimanjaro ambao ulikuwa kwao kabla ya kuhamishiwa kwetu? Kama Wamalawi wana haki wapewe ziwa lao.

  13. OPTIMUS TZ's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th January 2012
   Posts : 391
   Rep Power : 578
   Likes Received
   60
   Likes Given
   1

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Nafikiri kuna wakati tutaambiwa hilimjambo liko mahakamani kwasababu ubavu wa vita hatuna jeshi la majini hata kuokoa maiti haliwezi na huko ziwa nyasa sijui hata kama wana mtubwi....................nchi imekuwa dhaifu sana

  14. OPTIMUS TZ's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th January 2012
   Posts : 391
   Rep Power : 578
   Likes Received
   60
   Likes Given
   1

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Hivi tuna hata mtubwi wa jeshi huko nyasa?

  15. OPTIMUS TZ's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th January 2012
   Posts : 391
   Rep Power : 578
   Likes Received
   60
   Likes Given
   1

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By Nationalist View Post
   Doesn't make sense to deprive people living on the shores of lake Nyasa the right to enjoy its resources. To some of us, the lake has been and will always be the only natural and customary source of life. Any act purporting to rob us of this prerogative is in deed an explicit violation of fundamental human rights. Our Commander in Chief needs to assure us that our armed forces will stand shoulder to shoulder with us and preserve our rightful use of the lake. Any acts of aggression by the neighbor should be met with decisive and commensurate response. We have full faith in our Government that it will take the right course of action in the course of this crisis. God bless the United Republic of Tanzania, God bles our men and women in uniform.
   Your commander in chief is fasting and not interested in defending the nation his policy for now is LIWALO NA LIWE, be prepare to fight the Malawi by yourself the dam lake is gone for good ........malafyale!

  16. Columbus's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Location : Bongoland
   Posts : 1,998
   Rep Power : 963
   Likes Received
   598
   Likes Given
   139

   Default TZ/ Malawi:Ufanyike uchunguzi kwanza

   Naanza kuwa na wasiwasi ni kwa namna ambavyo suala la mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi unavyochukuliwa,hivi mathalani umeanika shati lako kwenye kamba halafu anakuja mtu analichukua halafu wewe badala ya kulipokonya unaanza kumbembeleza akurudishie! hii inakuwaje!! wasi wasi wangu usije ukakuta huyu Joyce ameshahakikishiwa na mafisadi wa TZ atangaze umiliki wa eneo letu la ziwa, mafisadi sio watu jamani yawezekana wameshafanya mipango yao na ndio maana huyu Joyce anakuwa na jeuri kiasi hiki.

  17. Straight's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th December 2010
   Posts : 346
   Rep Power : 626
   Likes Received
   42
   Likes Given
   13

   Default Lake malawi or nyasa

   Currently conflicts btn the bounderies of Lake Nyasa arise again.. Let see who is correct.

   Introduction
   Lake Malawi mostly known as Lake Nyasa is an african Great lake and southernmost Lake in the East African Rift System. this lake, the third largest in Africa and the eighth largest lake in the world, is located between Malawi, Mozambique, and Tanzania. Its the second deepest lake in Africa.

   Geography
   Lake Malawi or lake Nyanza is btn 560 and 580km long and about 75km wide at its widest point. this Total surface of the lake is about 29,600km.

   Is it Lake Nyasa or Lake Malawi..?
   The
   Geographic name of the lake is disputed. Malawi claims that it is named Lake Malawi whereas most other countries amd international made maps state that the name is Lake Nyasa. The Origin of the dispute over the name has its background in geopolitical disputes that began before the independence of Malawi was achieved in 1964, the territory had been known as ''Nyasaland''
   Further complications emerged for political reasons during the 1960s, when President Hastings Banda of Malawi became the only African leader to establish diplomatic relations with the white-ruled country of South Africa. This recognition of the South African regime was fiercely repudiated by almost all other African leaders, including President Julius Nyerere of Tanzania. This contrasting in policies toward South Africa gave some more impetus to disputes between Malawi and Tanzania, especially concerning the name of the lake itself — the water boundary between the two countries.

   For this same lake, the name "Lac Maravi" had been used on the map of "Afrique sud" by J.B.B. d'Anville, which was published in France in 1749. David Livingstone's name for the lake was based on his colleague's misunderstanding of African languages of the area. When Livingstone asked his staff members, who were not from the area of the lake, to state its name for him, they said the word "nyasa", not realizing that this was the local word for any large body of water (such as a lake). In effect, "Lake Nyasa" literally means "Lake Lake". This name could also be spelled "niassa", "nyanja", or "nyanza", based on the other languages of the region.
   Presently, the dispute between the two governments over the lake's name is mostly dormant. Diplomatic relations between Malawi and Tanzania, and the relationships between their wildlife police forces and other associations, are largely cordial.

   Tanzania–Malawi dispute
   The partition of Lake Nyasa's surface area between Malawi and Tanzania is under dispute. Tanzania claims that the international border runs through the middle of the lake.This is along the lines of the border that were set out between the German and British territories before 1914. On the other hand, Malawi claims the whole of the surface of this lake that is not in Mozambique, including the waters that are next to the shoreline of Tanzania. The foundations of this dispute were laid when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, placed all of the water under the jurisdiction of the territory of Nyasaland, without a separate administration for the Tanganyikan portion of the surface. This dispute has led to conflicts in the past, though in recent years, Malawi has declined to attempt to enforce any claims to the disputed portion.
   Occasional flare-ups of conflict during the 1990s, and also sometimes in the 21st Century, have impacted fishing rights, particularly those of Tanzanian fishermen who reside on the lakeshore, and who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.

   Source:
   Wikepedia.

   Let us contribute.....

  18. JF-MBUNGE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st May 2012
   Posts : 422
   Rep Power : 571
   Likes Received
   158
   Likes Given
   221

   Default Re: TZ/ Malawi:Ufanyike uchunguzi kwanza

   Quote By distazo View Post
   Naanza kuwa na wasiwasi ni kwa namna ambavyo suala la mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi unavyochukuliwa,hivi mathalani umeanika shati lako kwenye kamba halafu anakuja mtu analichukua halafu wewe badala ya kulipokonya unaanza kumbembeleza akurudishie! hii inakuwaje!! wasi wasi wangu usije ukakuta huyu Joyce ameshahakikishiwa na mafisadi wa TZ atangaze umiliki wa eneo letu la ziwa, mafisadi sio watu jamani yawezekana wameshafanya mipango yao na ndio maana huyu Joyce anakuwa na jeuri kiasi hiki.
   Afadhali we umefikiria mbali kama mie....nashangaa viongozi wa CCM wanavyoropoka eti hata vita wapo tayari lkn mpaka usichukuliwe...Intelejensia ipo wapi sijui...mie pia nimefikiri isije ikawa mataifa makubwa yanaitumia tuu malawi alafu tuje tupigwee na ndio uwe mwisho wa CCM...Tufikiri sn na intelejensia inatakiwa kutusaidia sn kuchukuza hili ...ili nchi yetu ibaki salama.

   Ila napo tukiachia mpaka itakuwa sisi serikali ya watanzania woga naungana na wewe ni bora tuli malize hili swala kwa mazungumzo

  19. PhD's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th July 2009
   Location : houston texas
   Posts : 3,320
   Rep Power : 1866
   Likes Received
   1069
   Likes Given
   232

   Default Re: TZ/ Malawi:Ufanyike uchunguzi kwanza

   Acheni mambo yenu ya ovyo Huyu mama ni kipenzi cha marekani na ulaya mchokozeni muone cha moto

  20. kiplagati26's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 25th July 2012
   Location : Nanchang
   Posts : 241
   Rep Power : 523
   Likes Received
   69
   Likes Given
   92

   Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   Quote By yutong View Post
   Hii Migogoro lazima kuna watu wanacreate kwa maslahi yao binafsi. Mwaka jana tu Kenya na Uganda waligombea kisiwa, China, Japan, Philipenes nao wanagombania visiwa huko na sasa tanzania na malawi. Basi nao msumbiji karibuni watasema mto ruvuma ni wao na kenya watasema Mlima Kilimanjaro ni wao. Na viongozi wetu hawatoi tamko lolote ama ndo muendelezo wa udhaifu? Namkumbuka Mkapa waburundi walikohoa tu kabla hawajatema kohozi vifaru vilikuwa tayari mpakani.
   mkuu ulinzi na usalama wa mipaka yetu uko salama ni vyema kuelekea Ludewa,kyela,mbinga, ukajionee kwanza na sio kutoa lawama kwa serikali kwani serikali yetu hiko makini sana.


  21. muwanga's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 12th February 2012
   Posts : 9
   Rep Power : 499
   Likes Received
   0
   Likes Given
   3

   Post Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

   haya haya nimeingia kwa mara yatena


  Page 7 of 37 FirstFirst ... 56789 17 ... LastLast

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...