Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

    Report Post
    Page 5 of 28 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 546
    1. #1
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 812
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default Ni lake Nyasa au Lake Malawi?

      Wakubwa niwekeni sawa, nilikuwa nauliza Ziwa Nyasa ni Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi? Na je, Kwanini Ziwa Victoria liendelee kuitwa Ziwa Victoria na si Ziwa Nyanza? Au ndio kuwaenzi watawala wetu wazungu?

      Lake Nyasa or Lake Malawi?
      The name of the lake itself is also disputed. Malawi claims the lake is named 'Lake Malawi' while international maps and other countries (most notably Tanzania) claim the name of the lake to be 'Lake Nyasa'. The origins of the dispute in the name have their background in geopolitical disputes that began prior to Malawi's independence in 1964, when it was previously known as Nyasaland.

      Further complications emerged for different political reasons in the 1960s, when the then President Banda (of Malawi) became the only African leader to establish diplomatic relations with white South Africa. This was fiercely repudiated by other African leaders, including the then President Nyerere (of Tanzania). The contrasting attitudes and policies gave further impetus to disputes between the two governments, on the name of the lake itself, and the boundary between the two countries.

      At present, the dispute between the two governments is largely dormant. Intergovernmental relations between Malawi and Tanzania are largely cordial.


      Tanzania-Malawi dispute
      The partition of the lake area between Malawi and Tanzania is disputed. Tanzania claims international borders through the lake along the lines of the borders between the German and British territories before 1914; Malawi, meanwhile, claims the whole non-Mozambican lake, including the waters next to the Tanzanian shore. The foundations of the dispute were set when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, put the water under the jurisdiction of Nyasaland without a separate administration for the Tanganyika portion. The dispute has led to conflicts in the past, though for several years Malawi has declined to enforce its claims to the disputed portion.

      Occasional flare-ups in in the 1990s and in recent times have impacted fishing rights, particularly of Tanzanian's who reside on the lake shore, who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.
      Quote By Mwawado
      Habari hiyo hata Mimi nimewahi kuisikia, hata ukiangalia Ramani ya ziwa hilo linaitwa Ziwa Malawi tofauti na hapo zamani tulipoliona kwenye ramani kama ziwa nyasa. Nashindwa kuelewa kwa dhati kama mpaka umegawanywa upya ama ndio yale yale ya kuambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.Inapaswa mipaka ya nchi yetu iwekwe wazi ili kutokuja kupoteza maeneo na Vivutio vyetu vya asili.

      Mpaka wa Tanzania na Malawi una matatizo ya muda mrefu, nakumbuka mwaka 1978 kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi, kwa siku mbili mfululizo kulikuwa na amri ya kutokuwasha Taa katika Mji wa kyela mkoani Mbeya, Kipindi hicho nilikuwa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa Wakati Huo Mzee Richard Wambura alisema Mwl Nyerere ameamuru majeshi yetu yarudishe mapigo kama itaonekana Banda ataingiza majeshi Kyela. Serikali ya Banda ilikuwa inadai maeneo ya Matema Beach, Mto Songwe mpaka Ipinda yapo ndani ya Ardhi ya Malawi.

      Sasa inawezekana kabisa tumelitoa kwa hiyari ziwa liwe upande wa Malawi nasi tumebakiwa na Bandari tupu ya Itungi,ambayo sasa nafikiri haina hata meli moja baada ya TACOSHILI kufa.
      Quote By Gamba la Nyoka
      Kama serikali imelitoa hilo ziwa kwa Wamalawi pasipo kuhusisha maoni ya Watanzania, basi serikali inalo la kujibu. Huwezi kuwaambia wananchi waliokaa pale miaka nenda rudi eti, hayo maji usiyaguse ni ya wamalawi hayo.

      Hili suala ni lazima serikali ilitolee kauli haliwezi kuwa kimya kimya milele!
      Quote By Ruge Opinion
      Miaka ya 1970 Kamuzu Banda, rais wa Malawi, alitangaza kuwa lile ziwa lote ni la Malawi na akaanza kuwabugudhi Watanganyika waliokutwa kwenye ziwa. Nyerere akasogeza majeshi pale na kumtumia ujumbe Kamuzu aache uchokozi. Kamuzu akanywea.

      Tangu hapo hakujawahi kuwapo maelewano rasmi.

      Hilo ziwa lilikuwa linajulikana kama ziwa Nyasa kutokana na wenyeji pande zote mbili kuwa Wanyasa. Malawi vile vile ilikuwa inajulikana kama Nyasaland. Walipopata uhuru wakabadili jina na kujiita Malawi. Kwa hiyo na jina la ziwa wakalibadilisha bila makubaliano na sisi. Kwa hiyo kwao ni Ziwa Malawi na kwetu ni Ziwa Nyasa.
      Quote By kajembe
      Mgogoro huo ulianza enzi ya Kamuzu Banda alipokuwa raisi. miaka ya sitini Kamuzu alikuwa anazungumza kwenye redio yao, Malawi Broadcasting Corporation kutoka Blantyre, Malawi, na kusema ziwa lote ni la Malawi na pia wilaya ya Rungwe na hadi Mbeya ni sehemu ya Malawi.

      Kuna siku mwezi wa September 1968 Nyerere alimwita Banda ni kichaa. Alikasirika sana kwa sababu ya madai ya Mzee Kamuzu kwamba sehemu za Tanzania ni za Malawi. Alidai hata Mbamba Bay na sehemu zingine mkoani Ruvuma karibu na Ziwa Nyasa kwamba ni za Malawi. Pia alidai jimbo lote, Eastern Province, la Zambia. Kaunda alimjibu Banda na kusema ni shauri yake akitaka kuanzisha vita.

      Kabla ya mgogoro huo, Banda alikuja Tanzania na kukutana na Nyerere mwaka 1962 na kumwambia hakuna nchi ya Mozambique. Alimwambia Nyerere wagawane nchi hiyo. Alimwambia Nyerere sehemu ya kaskazini ya Mozambique, sehemu ya Wamakonde jimbo la Cobo Delgado, "ni lako" Nyerere. Ni sehemu ya Tanzania. Sehemu za Mozambique zilizobaki ni za Malawi, Rhodesia na Swaziland. Nyerere alimpuuza tu.

      Baada ya miaka michache, 1968, Kamuzu akatangaza na kusema sehemu zetu za Tanzania nilizozitaja hapo juu ni sehemu za Malawi.

      Mzee Kamuzu alikuwa ni mkorofi sana.

      CHANZO CHA MGOGORO

      Mgogoro wa ziwa umetokana na uamuzi wa wakoloni wa Kiingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao wa Nyasaland wakati walipokuwa wanatawala nchi hiyo na ilipokuwa ni British Protectorate. Walifanya uamuzi huo baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu ya kwanza na Waingereza walipoichukua German East Afrika - iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika katika Kijerumani - na kuwa koloni yao ya Tanganyika. Kabla ya hapo, kutokana na makubaliano kati ya Waingereza waliokuwa watawala wa Nyasaland na Wajerumani waliokuwa watawala wa nchi yetu, mpaka wa ziwa ulikuwa kati ya ziwa. Na ndiyo mpaka huo tu ambao ni halali pamoja na jina kuitwa Nyasa, siyo Malawi.

      Uamuzi wa Waingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland haukubadilisha mpaka wa ziwa kihalali kwa sababu mipaka yote ya nchi zetu ilikubaliwa wakati bara letu lilipogawanywa na wakoloni. Ni mipaka hiyo ambayo hata sisi tuliikubali baada ya kupata uhuru na hakuna hata nchi moja ambayo ina haki peke yake ya kubadilisha mipaka hiyo. Hata Waingereza hawakuwa na haki ya kulikiweka Ziwa Nyasa chini ya ukoloni wao Nyasaland kwa sababu walivunja makubaliano yao na Wajerumani ambayo yalisema mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo: nusu ni sehemu ya Deutsch Ostafrika ambayo sasa ni Tanganyika, na nusu nyingine ni ya Nyasaland chini ya utawala wa Waingereza.

      Hata wilaya ya Rungwe ambayo ilijumuisha Kyela na Ileje ilikuwa inatawaliwa kutoka Nyasaland mara tu baada ya Wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza na Waingereza walipopewa madaraka ya kutawala nchi ambayo ilikuwa ni koloni ya Wajerumani; yaani nchi yetu ya Tanganyika.

      Deutsch Ostafrika - German East Africa - ilikuwa ni nchi tatu: Tanganyika, Ruanda na Urundi (nchi ambazo zilibadili majina na kuitwa Rwanda na Burundi mwaka 1962 baada ya kupata uhuru).

      League of Nations - jumuiya ya mataifa iliyoitangulia United Nations - iliwapa Wabeligiji Ruanda na Urundi. Koloni hizo mbili za Wabeligiji zilikuwa zinatawaliwa kutoka Leopoldville, mjii mkuu wa Belgian Congo, nchi ambayo pia ilikuwa inatawaliwa na Wabeligiji. Mpango huo ni kama vile wilaya ya Rungwe ilipowahi kutawaliwa kutoka Karonga na Waingereza waliokuwa wanatawala wa Nyasaland na baadaye kiuchukua nchi yetu ya Tanganyika kutoka kwa Wajerumani.

      Baada ya vita kuu ya kwanza, na Wajerumani kushindwa vita hiyo, waziri mkuu wa Uingereza, Lloyd George, kwenye mkutano wa League of Nations alimwambia raisi wa USA, Woodrow Wilosn, kwamba aichukue German East Africa, yaani nchi yetu, na kuiweka chini ya utawala wa Merikani baada ya Wajerumani kuipoteza nchi hiyo katika vita kuu ya kwanza. Lakini President Wilson alikataa. Angekubali, nchi yetu ingetawaliwa na USA na tungekuwa koloni ya USA. Baada ya Rais Wilson kukataa kuichukua nchi yetu, Lloyd George akakubali na kusema ataichukua Tanganyika na kuiweka chini ya utawala wa nchi yake ya Uingereza. Tuliponea chupuchupu kuchukuliwa na Wamerika. Nchi yetu ingechukuliwa na Wamerika, labda tusingepata uhuru. Wamerika wangeing'ang'ania nchi yetu kama vile walivyo ng'ang'ania nchi zingine walizochukua bila kuzipa uhuru.

      Kuhusu Ziwa Nyasa, kwa kifupi ni kwamba mpaka halali uko kati ya Ziwa. Ni mpaka ambao Wajerumani na Waingereza walikubaliana kuzigawa koloni zao: Nyasaland kuwa ya Waingereza; nchi yetu, Deutsh Ostafrika, kuwa ni ya Wajerumani. Walikubaliana kwamba mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo. Upande mmoja tu, Waingereza, hawakuwa na haki ya kubadili mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland walipolikweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland.

      Nukuru kutoka kitabu cha Nyerere and Africa: End of an Era, ukurasa 484:

      "Dr. Banda also claimed substantial parts of Tanzania, including - Rungwe district - and the rest of Mbeya Region in southwestern Tanzania, as Malawian territory. He also claimed the entire Eastern Province of Zambia, provoking a curt response from Zambia’s president, Dr. Kenneth Kaunda, who challenged Banda to 'Go ahead and declare war on Zambia.'

      And President Nyerere dismissed Banda’s claim to large chunks of Tanzanian territory as 'expansionist outbursts, which do not scare us, and do not deserve my reply.' The outlandish claim also drew a sharp response from Nyerere who said Dr. Banda was 'insane.' But, he warned, 'Dr. Banda must not be ignored; the powers behind him are not insane.'"


      Akizungumza ktk chuo kikuu cha Dar es Salaam, November 1997, Mwalimu Nyerere alisema

      "In 1961 we became independent. In 1962, early 1962, I resigned as prime minister and then a few weeks later I received Dr. Banda. Mungu amuweke mahali pema (May God rest his soul in peace). I received Dr. Banda. We had just, FRELIMO had just been established here and we were now in the process of starting the armed struggle.

      So Banda comes to me with a big old book, with lots and lots of maps in it, and tells me, 'Mwalimu, what is this, what is Mozambique? There is no such thing as Mozambique.' I said, 'What do you mean there is no such thing as Mozambique?' So he showed me this map, and he said: 'That part is part of Nyasaland (it was still Nyasaland, not Malawi, at that time). That part is part of Southern Rhodesia, that part is Swaziland, and this part, which is the northern part, Makonde part, that is YOUR part.'

      So Banda disposed of Mozambique just like that. I ridiculed the idea, and Banda never liked anybody to ridicule his ideas.
      So he left and went to Lisbon to talk to Salazar about this wonderful idea. I don’t know what Salazar told him. That was ‘62."
      Quote By Simba mnyama
      Wana-JF,

      Mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa unaonesha ngoma bado mbichi kabisa. Hebu tusome hizi habari kutoka Malawi:

      Lake Malawi/Nyasa row: Time to show strong leadership
      By Cedrick Ngalande August 6, 2012
      At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times. During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time. Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now? Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

      Test for President Joyce Banda to diplomatically manage the dispute on the boundary You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts. Statesmanship is a game because image is everything in international politics.

      A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!
      It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image. The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important! When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’. President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge. If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

      Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian. Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    2. Miaka 50

    3. EMT
      #81
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 8,918
      Rep Power : 61730
      Likes Received
      7219
      Likes Given
      6455

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Hili ni tatizo la kihistoria na inaonekana halifuatiliwi tena tokea Nyerere aondoke madarani. Kwanza kuna tatizo kuhusu jina la ziwa. Malawi wanasema ziwa linaitwa "Lake Malawi wakati sisi tunadai ni "Lake Nyasa". Nchi nyingine na ramani za kimataifa zinalitambua jina la Lake Nyasa. Tatizo lilizanza baada ya Malawi kupata uhuru wake mwaka 1964. Kwa wale waliosoma historia watakumbuka kuwa kabla ya uhuru wake, Malawi ilikuwa ikiitwa Nyasaland. Walipopata uhuru na kubadilisha jina, walitaka pia kubadilisha jina la ziwa kutoka ziwa Nyasa kwenda Ziwa Malawi.

      Kitu kingine kilichochangia huu mgogoro ni Banda kuanzisha uhusiano wa kibalozi na serikali ya makaburu Afrika Kusini miaka ya 1960s. Viongozi wengi wa Kiafrika akiwemo Nyerere alipinga sana hili. Hii iliongeza chachu ya mgogoro juu ya jina na ramani ya ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi. Kwa sasa mgogoro juu ya jina la ziwa ni dormant.

      Ukija kwenye ramani, Tanzania inadai mpaka unapita katikati ya ziwa. Huu ni mpaka uliowekwa kati ya Uingereza na Ujerumani wakati wa Berlin Conference juu ya kuigawa Afrika katika makoloni. Malawi wanadai ziwa lote liko Malawi ispokuwa ile sehemu ya chini iliyo Msumbiji. Tatizo ni pale Ujerumani iliponyang'anywa makoloni yake baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, ambapo Tanganyika iliwekwa chini ya Uningereza. Kitu ambacho serikali ya kikoloni ya Uingereza ilifanya ni kuweka maeneo yote ya maji ya Ziwa Nyasa chini ya mamlaka ya Malawi (wakati huo Nyasaland) ikiwemo pia ile sehemu ya maji iliyokuwa upande wa Tanganyika. Hiki ndicho kiini cha tatizo kwa sababu baada ya Malawi kupata uhuru, automatically walidhani maji yote ya Ziwa Nyasa yako kwao kwa sababu yaliwekwa chini ya mamlaka yao tokea ukoloni.

      Japokuwa kumekuwa na migogoro ya hapa na pale, Malawi imekataa kusema wazi kuwa ziwa ni lao. Kulikuwa na mgogoro miaka ya 1990s na miaka ya 2000s lakini haukufika mahali. Hata hiyo imeadhiri kwa kiasi kikubwa haki za wavuvi hasa wale wa upande wa Tanzania wanaoishi kando kando ya ziwa. Mara nyingi wamekuwa wakilaumiwa na wenza wa Malawi kuwa wanavua kwenye maji ya Malawi.

      Serikali ya pande zote husika zinabidi kulichukulia hili suala kwa uzito zaidi. Vingenevyo ukitokea mgogoro wa wananchi wa pande zote husika hapa, itakuwa ngumu kusuluhisha. Haya mambo sijui ya kuunda tume, yatachukuwa miaka na miaka kutatua hili tatizo. Resources are very scarce. Siku ikugundulika kuna madini ndani ya ziwa itakuwa ni balaa.

      Chini hapo ramani ya Google inaonyesha Ziwa Malawi halipo Tanzania. Serikali ilishawahi hata kuwaandikia Google kujua ni vigezo gani walivyotumia kuchora hii ramani?




      Attached Thumbnails  
      Last edited by EMT; 23rd July 2011 at 18:03.
      Kakalende, King of Kings and Mwali like this.
      “Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.

    4. #82
      MdogoWenu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd December 2009
      Posts : 54
      Rep Power : 489
      Likes Received
      7
      Likes Given
      6

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Au ndio sababu kuna wakati ikalewta hoja kwamba Oscar Kambona hakuwa mtanzania na kwa muda wakamnyang'ana passport, hadi na yeye aliposema hata Nyerere baba yake alitokea karibu na Rwanda.

    5. #83
      MdogoWenu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd December 2009
      Posts : 54
      Rep Power : 489
      Likes Received
      7
      Likes Given
      6

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Mnaukumbuka huu wimbo:
      Bandaaa wa Malawi, umetuvalia ngozi ya Simba
      Kututishia watanzania, hatujali, hatujali.

    6. #84
      LordJustice1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Posts : 2,069
      Rep Power : 2301
      Likes Received
      409
      Likes Given
      36

      Default

      Quote By Feedback
      Wamalawi wanatumia hiyo picha ya google ku justify madai yao wewe utatumia ramani ipi wakati hata uliyopeleka UN inaonyesha ziwa liko upande wa Malawi.
      Uliipeleka wewe UN?

    7. #85
      Mwakifulefule's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 24th November 2010
      Posts : 6
      Rep Power : 432
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Ntafurah sana Kama Kyela itakuwa upande wa Malawi kwani Malawi hawana Tatizo la umeme kama huu na hata Viongozi wakituletea longolongo tutakuwa tunaandamana na kudai haki yetu...

    8. RukaaJuu Final

    9. #86
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 856
      Rep Power : 966
      Likes Received
      544
      Likes Given
      601

      Default Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Inapatikana pia kwenye Hansard ya July 30, 2007 ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    10. #87
      ndomyana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 1,826
      Rep Power : 735
      Likes Received
      179
      Likes Given
      0

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Mpaka wake ni mto songwe kwa upande wa wilaya ya kyela na upande mwingine ni ziwa nyasa

    11. #88
      Mzuvendi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th April 2009
      Posts : 202
      Rep Power : 553
      Likes Received
      64
      Likes Given
      14

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Any county is entitled to print its own maps. However, international maps I have seen show that Lake Nyasa is in Malawi. The British administrators allocated the section of the lake that was under German East Africa to Malawi. I don't why they did it. But I guess they thought they will be in Africa forever. They didn't and they left Africans with tones of problems to solve.
      Kimbunga and Butola like this.
      My English is raw, so bear with me.

    12. #89
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,484
      Rep Power : 6170
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      1020

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Quote By ndomyana
      Mpaka wake ni mto songwe kwa upande wa wilaya ya kyela na upande mwingine ni ziwa nyasa
      Mkuu mpaka huu umekuwa na utata kwa miaka mingi. Kwa upande wa Tanzania tunasema mpaka upo katikati ya ziwa Nyasa lakini Wamalawi wao wanasema Mpka ni mto Songwe na ufukwe wa Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania. Hii imekuwa ni ero ya miaka mingi sana. Kumbukumbu zinaonyesha kwamba kwenye miaka ya tisini kuna ramani ziliingizwa hapa nchini zikionyesha kwamba mpaka ni ufukwe wa Ziwa Nyasa, serikali ikazipiga marufuku.
      mfianchi likes this.
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    13. #90
      ndomyana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 1,826
      Rep Power : 735
      Likes Received
      179
      Likes Given
      0

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Kunakisa niliskia malawi wakadai ziwa nyasa lote lao., ko watanzania mnatakiwa kulipia kwa matumizi yoyote ya ziwa. Nyerere akakubali na akasema kama ufukwe ndo mpaka basi kila wimbi linalopiga ufukwe wetu mtaulipia tsh1. Wamalawi wakanyosa mikono juu.
      Njowepo and mfianchi like this.

    14. EMT
      #91
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 8,918
      Rep Power : 61730
      Likes Received
      7219
      Likes Given
      6455

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      “Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.

    15. #92
      Gurta's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th September 2010
      Location : Mang'ola
      Posts : 1,943
      Rep Power : 906
      Likes Received
      374
      Likes Given
      483

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Lilw ni ziwa Nyasa au ziwa Malawi? School texts za Kenya hazifahamu kuhusu uwepo wa ziwa Nyasa, kwa mfano.

    16. #93
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,227
      Rep Power : 908
      Likes Received
      283
      Likes Given
      60

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      kwa sasa ukiangalai gooogle earth, mipaka inaonesha lote liko malawi, nadhani kuna haja ya kukumbushana

      Quote By Jasusi
      mbona sisi tuliosoma enzi za ukoloni tunalijua hilo?

    17. #94
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,227
      Rep Power : 908
      Likes Received
      283
      Likes Given
      60

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      na ile sheria ya UN Convention on law of the Sea huko haitumia, au ni kwa jusa tu

    18. #95
      Ikwanja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2011
      Posts : 553
      Rep Power : 508
      Likes Received
      106
      Likes Given
      48

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      duh! hi kweli inachanganya sana, ukiwa malawi wao hawana ziwa nyasa, ila wana ziwa Malawi na ndo maana lote linaonekana kuwa la kwao

    19. #96
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,227
      Rep Power : 908
      Likes Received
      283
      Likes Given
      60

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Jamani jiografia nmejifunzia wapi? tuna bandari pale kyela na mbambabay sasa hizo meli zenafloot eneo lka wamalawi? haiwezekani zima tumepakana nalo kwa mikoa mitatu, yaani mbeya, iringa(sasa Njombe) an Ruvuma alufu liwe ilanamilikiwa kwa 100% na jirani yako, ina maana angeweka wanajeshi wake mpaka kwetu! huo mto songwe uko chini sana, lakini kuna matema beach ambay iko mbali sana , kwa hiyo mto songwe sio mpaka sahii, mkuu wa majeshi wa sasa anavuka mto songwe kwenda kijiji kwao na yuko ziwani kabisa, na hapo sio mwishi kuna watanzania wengine wakwenda mbali zaidi toka alipo yeye

      Quote By ndomyana
      Mpaka wake ni mto songwe kwa upande wa wilaya ya kyela na upande mwingine ni ziwa nyasa

    20. #97
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,227
      Rep Power : 908
      Likes Received
      283
      Likes Given
      60

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Mawawi zamani walikuwa wanajulikana kama Nyasa land, hii historia ndio inawafanya wafikilie wanyasa wote hata wale wa rudewa ni wamalawi

      Quote By Ikwanja
      duh! hi kweli inachanganya sana, ukiwa malawi wao hawana ziwa nyasa, ila wana ziwa Malawi na ndo maana lote linaonekana kuwa la kwao

    21. #98
      MESTOD's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2010
      Posts : 2,573
      Rep Power : 946
      Likes Received
      691
      Likes Given
      131

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Kuna haja ya kutangaza kabisa ziwa nyasa kuwa linaitwa ziwa nyasa. Niliona kipindi fulani cha e-tv ya s.a wakisema lake malawi ni moja maziwa nafuu zaidi duniani kutumia maji yake. Nikastuka sana.

      Anyway inaonekana nchi yetu ni kubwa sana ndo maana hata tunatangaza sehemu moja tu ya tanzania na kusahau sehemu nyingine.

    22. #99
      Butola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2010
      Posts : 1,520
      Rep Power : 783
      Likes Received
      266
      Likes Given
      647

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Quote By Gurta
      Lilw ni ziwa Nyasa au ziwa Malawi? School texts za Kenya hazifahamu kuhusu uwepo wa ziwa Nyasa, kwa mfano.

      ...Malawi aka Nyasa-land, so yote yana maana moja...

      Angalia ramani ya Malawi hapa, zingatia mpaka wake na Tanzania, http://www.nationsonline.org/oneworl...malawi_map.htm
      Last edited by Butola; 3rd February 2012 at 07:55.

    23. #100
      ndomyana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 1,826
      Rep Power : 735
      Likes Received
      179
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By andrewk
      Jamani jiografia nmejifunzia wapi? tuna bandari pale kyela na mbambabay sasa hizo meli zenafloot eneo lka wamalawi? haiwezekani zima tumepakana nalo kwa mikoa mitatu, yaani mbeya, iringa(sasa Njombe) an Ruvuma alufu liwe ilanamilikiwa kwa 100% na jirani yako, ina maana angeweka wanajeshi wake mpaka kwetu! huo mto songwe uko chini sana, lakini kuna matema beach ambay iko mbali sana , kwa hiyo mto songwe sio mpaka sahii, mkuu wa majeshi wa sasa anavuka mto songwe kwenda kijiji kwao na yuko ziwani kabisa, na hapo sio mwishi kuna watanzania wengine wakwenda mbali zaidi toka alipo yeye
      kaka usibishe vitu vingine usivojua. Mimi ni mwanakijiji mwenzake unaemsema mku wa majeshi, na mwakyembe wote wanatoka kijiji kimoja.. We mto unaousema ni kiwira ndo unavuka unenda kina mwamunyange. Ila songwe ni mpaka toka uku kasumulu hadi katumba songwe. Na huwaga mto huu songwe unamatatizo ya kuhamahama na kuingia tz zaidi pind yatokeapo mafuriko. Nafkiri umenipata ee..

    Page 5 of 28 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...