Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

    Report Post
    Page 4 of 28 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 547
    1. #1
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 812
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default Ni lake Nyasa au Lake Malawi?

      Wakubwa niwekeni sawa, nilikuwa nauliza Ziwa Nyasa ni Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi? Na je, Kwanini Ziwa Victoria liendelee kuitwa Ziwa Victoria na si Ziwa Nyanza? Au ndio kuwaenzi watawala wetu wazungu?

      Lake Nyasa or Lake Malawi?
      The name of the lake itself is also disputed. Malawi claims the lake is named 'Lake Malawi' while international maps and other countries (most notably Tanzania) claim the name of the lake to be 'Lake Nyasa'. The origins of the dispute in the name have their background in geopolitical disputes that began prior to Malawi's independence in 1964, when it was previously known as Nyasaland.

      Further complications emerged for different political reasons in the 1960s, when the then President Banda (of Malawi) became the only African leader to establish diplomatic relations with white South Africa. This was fiercely repudiated by other African leaders, including the then President Nyerere (of Tanzania). The contrasting attitudes and policies gave further impetus to disputes between the two governments, on the name of the lake itself, and the boundary between the two countries.

      At present, the dispute between the two governments is largely dormant. Intergovernmental relations between Malawi and Tanzania are largely cordial.


      Tanzania-Malawi dispute
      The partition of the lake area between Malawi and Tanzania is disputed. Tanzania claims international borders through the lake along the lines of the borders between the German and British territories before 1914; Malawi, meanwhile, claims the whole non-Mozambican lake, including the waters next to the Tanzanian shore. The foundations of the dispute were set when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, put the water under the jurisdiction of Nyasaland without a separate administration for the Tanganyika portion. The dispute has led to conflicts in the past, though for several years Malawi has declined to enforce its claims to the disputed portion.

      Occasional flare-ups in in the 1990s and in recent times have impacted fishing rights, particularly of Tanzanian's who reside on the lake shore, who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.
      Quote By Mwawado
      Habari hiyo hata Mimi nimewahi kuisikia, hata ukiangalia Ramani ya ziwa hilo linaitwa Ziwa Malawi tofauti na hapo zamani tulipoliona kwenye ramani kama ziwa nyasa. Nashindwa kuelewa kwa dhati kama mpaka umegawanywa upya ama ndio yale yale ya kuambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.Inapaswa mipaka ya nchi yetu iwekwe wazi ili kutokuja kupoteza maeneo na Vivutio vyetu vya asili.

      Mpaka wa Tanzania na Malawi una matatizo ya muda mrefu, nakumbuka mwaka 1978 kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi, kwa siku mbili mfululizo kulikuwa na amri ya kutokuwasha Taa katika Mji wa kyela mkoani Mbeya, Kipindi hicho nilikuwa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa Wakati Huo Mzee Richard Wambura alisema Mwl Nyerere ameamuru majeshi yetu yarudishe mapigo kama itaonekana Banda ataingiza majeshi Kyela. Serikali ya Banda ilikuwa inadai maeneo ya Matema Beach, Mto Songwe mpaka Ipinda yapo ndani ya Ardhi ya Malawi.

      Sasa inawezekana kabisa tumelitoa kwa hiyari ziwa liwe upande wa Malawi nasi tumebakiwa na Bandari tupu ya Itungi,ambayo sasa nafikiri haina hata meli moja baada ya TACOSHILI kufa.
      Quote By Gamba la Nyoka
      Kama serikali imelitoa hilo ziwa kwa Wamalawi pasipo kuhusisha maoni ya Watanzania, basi serikali inalo la kujibu. Huwezi kuwaambia wananchi waliokaa pale miaka nenda rudi eti, hayo maji usiyaguse ni ya wamalawi hayo.

      Hili suala ni lazima serikali ilitolee kauli haliwezi kuwa kimya kimya milele!
      Quote By Ruge Opinion
      Miaka ya 1970 Kamuzu Banda, rais wa Malawi, alitangaza kuwa lile ziwa lote ni la Malawi na akaanza kuwabugudhi Watanganyika waliokutwa kwenye ziwa. Nyerere akasogeza majeshi pale na kumtumia ujumbe Kamuzu aache uchokozi. Kamuzu akanywea.

      Tangu hapo hakujawahi kuwapo maelewano rasmi.

      Hilo ziwa lilikuwa linajulikana kama ziwa Nyasa kutokana na wenyeji pande zote mbili kuwa Wanyasa. Malawi vile vile ilikuwa inajulikana kama Nyasaland. Walipopata uhuru wakabadili jina na kujiita Malawi. Kwa hiyo na jina la ziwa wakalibadilisha bila makubaliano na sisi. Kwa hiyo kwao ni Ziwa Malawi na kwetu ni Ziwa Nyasa.
      Quote By kajembe
      Mgogoro huo ulianza enzi ya Kamuzu Banda alipokuwa raisi. miaka ya sitini Kamuzu alikuwa anazungumza kwenye redio yao, Malawi Broadcasting Corporation kutoka Blantyre, Malawi, na kusema ziwa lote ni la Malawi na pia wilaya ya Rungwe na hadi Mbeya ni sehemu ya Malawi.

      Kuna siku mwezi wa September 1968 Nyerere alimwita Banda ni kichaa. Alikasirika sana kwa sababu ya madai ya Mzee Kamuzu kwamba sehemu za Tanzania ni za Malawi. Alidai hata Mbamba Bay na sehemu zingine mkoani Ruvuma karibu na Ziwa Nyasa kwamba ni za Malawi. Pia alidai jimbo lote, Eastern Province, la Zambia. Kaunda alimjibu Banda na kusema ni shauri yake akitaka kuanzisha vita.

      Kabla ya mgogoro huo, Banda alikuja Tanzania na kukutana na Nyerere mwaka 1962 na kumwambia hakuna nchi ya Mozambique. Alimwambia Nyerere wagawane nchi hiyo. Alimwambia Nyerere sehemu ya kaskazini ya Mozambique, sehemu ya Wamakonde jimbo la Cobo Delgado, "ni lako" Nyerere. Ni sehemu ya Tanzania. Sehemu za Mozambique zilizobaki ni za Malawi, Rhodesia na Swaziland. Nyerere alimpuuza tu.

      Baada ya miaka michache, 1968, Kamuzu akatangaza na kusema sehemu zetu za Tanzania nilizozitaja hapo juu ni sehemu za Malawi.

      Mzee Kamuzu alikuwa ni mkorofi sana.

      CHANZO CHA MGOGORO

      Mgogoro wa ziwa umetokana na uamuzi wa wakoloni wa Kiingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao wa Nyasaland wakati walipokuwa wanatawala nchi hiyo na ilipokuwa ni British Protectorate. Walifanya uamuzi huo baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu ya kwanza na Waingereza walipoichukua German East Afrika - iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika katika Kijerumani - na kuwa koloni yao ya Tanganyika. Kabla ya hapo, kutokana na makubaliano kati ya Waingereza waliokuwa watawala wa Nyasaland na Wajerumani waliokuwa watawala wa nchi yetu, mpaka wa ziwa ulikuwa kati ya ziwa. Na ndiyo mpaka huo tu ambao ni halali pamoja na jina kuitwa Nyasa, siyo Malawi.

      Uamuzi wa Waingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland haukubadilisha mpaka wa ziwa kihalali kwa sababu mipaka yote ya nchi zetu ilikubaliwa wakati bara letu lilipogawanywa na wakoloni. Ni mipaka hiyo ambayo hata sisi tuliikubali baada ya kupata uhuru na hakuna hata nchi moja ambayo ina haki peke yake ya kubadilisha mipaka hiyo. Hata Waingereza hawakuwa na haki ya kulikiweka Ziwa Nyasa chini ya ukoloni wao Nyasaland kwa sababu walivunja makubaliano yao na Wajerumani ambayo yalisema mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo: nusu ni sehemu ya Deutsch Ostafrika ambayo sasa ni Tanganyika, na nusu nyingine ni ya Nyasaland chini ya utawala wa Waingereza.

      Hata wilaya ya Rungwe ambayo ilijumuisha Kyela na Ileje ilikuwa inatawaliwa kutoka Nyasaland mara tu baada ya Wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza na Waingereza walipopewa madaraka ya kutawala nchi ambayo ilikuwa ni koloni ya Wajerumani; yaani nchi yetu ya Tanganyika.

      Deutsch Ostafrika - German East Africa - ilikuwa ni nchi tatu: Tanganyika, Ruanda na Urundi (nchi ambazo zilibadili majina na kuitwa Rwanda na Burundi mwaka 1962 baada ya kupata uhuru).

      League of Nations - jumuiya ya mataifa iliyoitangulia United Nations - iliwapa Wabeligiji Ruanda na Urundi. Koloni hizo mbili za Wabeligiji zilikuwa zinatawaliwa kutoka Leopoldville, mjii mkuu wa Belgian Congo, nchi ambayo pia ilikuwa inatawaliwa na Wabeligiji. Mpango huo ni kama vile wilaya ya Rungwe ilipowahi kutawaliwa kutoka Karonga na Waingereza waliokuwa wanatawala wa Nyasaland na baadaye kiuchukua nchi yetu ya Tanganyika kutoka kwa Wajerumani.

      Baada ya vita kuu ya kwanza, na Wajerumani kushindwa vita hiyo, waziri mkuu wa Uingereza, Lloyd George, kwenye mkutano wa League of Nations alimwambia raisi wa USA, Woodrow Wilosn, kwamba aichukue German East Africa, yaani nchi yetu, na kuiweka chini ya utawala wa Merikani baada ya Wajerumani kuipoteza nchi hiyo katika vita kuu ya kwanza. Lakini President Wilson alikataa. Angekubali, nchi yetu ingetawaliwa na USA na tungekuwa koloni ya USA. Baada ya Rais Wilson kukataa kuichukua nchi yetu, Lloyd George akakubali na kusema ataichukua Tanganyika na kuiweka chini ya utawala wa nchi yake ya Uingereza. Tuliponea chupuchupu kuchukuliwa na Wamerika. Nchi yetu ingechukuliwa na Wamerika, labda tusingepata uhuru. Wamerika wangeing'ang'ania nchi yetu kama vile walivyo ng'ang'ania nchi zingine walizochukua bila kuzipa uhuru.

      Kuhusu Ziwa Nyasa, kwa kifupi ni kwamba mpaka halali uko kati ya Ziwa. Ni mpaka ambao Wajerumani na Waingereza walikubaliana kuzigawa koloni zao: Nyasaland kuwa ya Waingereza; nchi yetu, Deutsh Ostafrika, kuwa ni ya Wajerumani. Walikubaliana kwamba mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo. Upande mmoja tu, Waingereza, hawakuwa na haki ya kubadili mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland walipolikweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland.

      Nukuru kutoka kitabu cha Nyerere and Africa: End of an Era, ukurasa 484:

      "Dr. Banda also claimed substantial parts of Tanzania, including - Rungwe district - and the rest of Mbeya Region in southwestern Tanzania, as Malawian territory. He also claimed the entire Eastern Province of Zambia, provoking a curt response from Zambia’s president, Dr. Kenneth Kaunda, who challenged Banda to 'Go ahead and declare war on Zambia.'

      And President Nyerere dismissed Banda’s claim to large chunks of Tanzanian territory as 'expansionist outbursts, which do not scare us, and do not deserve my reply.' The outlandish claim also drew a sharp response from Nyerere who said Dr. Banda was 'insane.' But, he warned, 'Dr. Banda must not be ignored; the powers behind him are not insane.'"


      Akizungumza ktk chuo kikuu cha Dar es Salaam, November 1997, Mwalimu Nyerere alisema

      "In 1961 we became independent. In 1962, early 1962, I resigned as prime minister and then a few weeks later I received Dr. Banda. Mungu amuweke mahali pema (May God rest his soul in peace). I received Dr. Banda. We had just, FRELIMO had just been established here and we were now in the process of starting the armed struggle.

      So Banda comes to me with a big old book, with lots and lots of maps in it, and tells me, 'Mwalimu, what is this, what is Mozambique? There is no such thing as Mozambique.' I said, 'What do you mean there is no such thing as Mozambique?' So he showed me this map, and he said: 'That part is part of Nyasaland (it was still Nyasaland, not Malawi, at that time). That part is part of Southern Rhodesia, that part is Swaziland, and this part, which is the northern part, Makonde part, that is YOUR part.'

      So Banda disposed of Mozambique just like that. I ridiculed the idea, and Banda never liked anybody to ridicule his ideas.
      So he left and went to Lisbon to talk to Salazar about this wonderful idea. I don’t know what Salazar told him. That was ‘62."
      Quote By Simba mnyama
      Wana-JF,

      Mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa unaonesha ngoma bado mbichi kabisa. Hebu tusome hizi habari kutoka Malawi:

      Lake Malawi/Nyasa row: Time to show strong leadership
      By Cedrick Ngalande August 6, 2012
      At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times. During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time. Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now? Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

      Test for President Joyce Banda to diplomatically manage the dispute on the boundary You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts. Statesmanship is a game because image is everything in international politics.

      A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!
      It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image. The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important! When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’. President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge. If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

      Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian. Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    2. Miaka 50

    3. #61
      Feedback's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 4,095
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      2066
      Likes Given
      1125

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By LordJustice1
      Wewe kichwa chako kibovu sana! Tukiwa wajinga wataendelea kumega mipaka kama akina Iddi Amini alivyodai kwamba Kagera Salient iko Uganda! Sasa hivi nako Warundi wameumega mpaka wetu! Kamuzu Banda naye aliwahi kudai kuwa Wilaya yote ya Kyela iko Malawi! Kwa hiyo wewe kwa akili yako finyu tukae kimya tu ili "kuogopa malumbano na vita?" Open your mind please!
      Mimi nimemshangaa sana TANMO eti anasema haina haja kugombea mipaka kwa vile tuna mambo mengi ya kushughulikia, tukiwa na viongozi watano tu wenye kichwa kama chake nafikiri Mwanza, Shinyanga Kagera zote zingekuwa sehemu ya Uganda, Kilimanjaro, Arusha, Mara zingekuwa za Kenya, Kigoma na Rukwa zingekuwa za Burundi, Mbeya yote wangekuwa wamewapa Malawi kwa huruma yao, Dar, Pwani, Mtwara na Tanga zingekuwa za Zanzibar. Labda Dodoma na Tabora tu ndizo zingebaki.
      Only in Tanzania

    4. #62
      LordJustice1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Posts : 2,069
      Rep Power : 2301
      Likes Received
      409
      Likes Given
      36

      Default

      Quote By VoiceOfReason
      Mkuu labda hao kina Idd Amini ndio wajinga, labda binadamu wote ni wajinga.., hivi unajua ni pesa kiasi gani inatumika kwenye majeshi dunia yote?, hivi unajua ni madhara kiasi gani yanatokana na vita, na ni nini hasa huwa sababu ya kugombana zaidi ya tamaa na upuuzi wa mtu mmoja ?Hivi unajua binadamu tungekuwa na busara, upendo na sio ubinafsi na tamaa tungeweza kutumia malighafi za dunia yote tukala na kusaza na kila mtu akawa na maisha mazuri...Najua sometimes jeshi ni la muhimu ili kuweka amani na kuepukana na vichaa, lakini kama binadamu tungekuwa na busara labda kungekuwa na Jeshi kubwa la dunia (United Nations) ambalo lingekuwa kama kiranja wa dunia kwa kumfunza adabu yeyote anaekiuka maadili... au maybe LOVE ndio njia pekee ya kuepuka vitaMaybe dunia nzima na watu wote ni wajinga na tunafight the wrong war between people badala ya kufight against the environment and betternment ya kila mtu hivi hii mipaka ni nani aliyoiweka na kwanini mtu yoyote asiweze kwenda popote pale kutafuta maisha so long wenyeji wa hapo wanamkaribisha.
      Tatizo lako unaongelea vitu vya kufikirika ndio maana unadai eti "kungekuwa na ..........! Hizo ndoto zako hazitatimia milele na tangu dunia hii iumbwe imekuwa na migogoro mfululizo! As long as resources za dunia zitaendelea kuwa depleted conflicts zitazidi kuibuka, esp kuhusu mipaka! Just imagine suala ambalo halina ubishi katika mpaka wa TZ/Burundi, jamaa wanazidi kujisogeza tu! Kwa hiyo sio kwamba watu wanataka migogoro ila uhaba wa resources ndio tatizo! Na hiyo UN unayoiamini na yenyewe inaongozwa na watu wenye kuwakilisha maslahi yao binafsi!Kwa ujumla mlinzi wa mipaka yetu ni sisi wenyewe, hakuna mtu atakayetuwezesha kuilinda mipaka hiyo!
      Feedback likes this.

    5. #63
      VoiceOfReason's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Everywhere
      Posts : 5,239
      Rep Power : 1895
      Likes Received
      1152
      Likes Given
      603

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Feedback
      Naona hata aibu ku argue na mtu kama wewe usiyejua maana ya mipaka ya nchi, taifa na utaifa
      siku moja utasema haina maana kugombea mlima kilimanjaro tuwaachie kenya si limlima tu watalipeleka wapi hata ukiwa Moshi mjini unauona, pole sana.
      Je na mimi kwenye post yangu No.25...?, Sababu mimi nilivyomuelewa the all notion ya kupigana vita kwa kugombania vitu ni ujinga na ubinafsi na upuuzi wa binadamu ambapo huenda wote tungeweza kushare resources za dunia bila matatizo... (Binadamu ndio adui mkubwa wa dunia, ndio destroyer mkubwa).., After all hii mipaka yote ni man made (MAN THE DESTROYER..)
      Even a Genius Asks Questions....

    6. #64
      Feedback's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 4,095
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      2066
      Likes Given
      1125

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By VoiceOfReason
      Mkuu labda hao kina Idd Amini ndio wajinga, labda binadamu wote ni wajinga.., hivi unajua ni pesa kiasi gani inatumika kwenye majeshi dunia yote?, hivi unajua ni madhara kiasi gani yanatokana na vita, na ni nini hasa huwa sababu ya kugombana zaidi ya tamaa na upuuzi wa mtu mmoja ?

      Hivi unajua binadamu tungekuwa na busara, upendo na sio ubinafsi na tamaa tungeweza kutumia malighafi za dunia yote tukala na kusaza na kila mtu akawa na maisha mazuri...

      Najua sometimes jeshi ni la muhimu ili kuweka amani na kuepukana na vichaa, lakini kama binadamu tungekuwa na busara labda kungekuwa na Jeshi kubwa la dunia (United Nations) ambalo lingekuwa kama kiranja wa dunia kwa kumfunza adabu yeyote anaekiuka maadili... au maybe LOVE ndio njia pekee ya kuepuka vita

      Maybe dunia nzima na watu wote ni wajinga na tunafight the wrong war between people badala ya kufight against the environment and betternment ya kila mtu hivi hii mipaka ni nani aliyoiweka na kwanini mtu yoyote asiweze kwenda popote pale kutafuta maisha so long wenyeji wa hapo wanamkaribisha.
      Maelezo yako yote yanaonyesha tatizo lako ni kuogopa vita tu lets say wamalawi wakupe bure utakubali.
      Only in Tanzania

    7. #65
      VoiceOfReason's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Everywhere
      Posts : 5,239
      Rep Power : 1895
      Likes Received
      1152
      Likes Given
      603

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By LordJustice1
      Tatizo lako unaongelea vitu vya kufikirika ndio maana unadai eti "kungekuwa na , Hizo ndoto zako hazitatimia milele na tangu dunia hii iumbwe imekuwa na migogoro mfululizo! ..........!
      Kufikirika or not does not change the fact of the matter..., wala mimi sioti mkuu ninajua kabisa kwamba duniani conflicts hazitaisha ila ukweli unabaki kuwa kwamba sababu ya tamaa za binadamu wote me included kungekuwa na better way of sharing resources, sababu dunia ina resources za kutosha na huwezi wewe peke yako ukawa nacho ukategemea mtu ambae hana atakuangalia tu.., bali atakuja na kujinyakulia... Therefore mkuu the best alternative sio walionacho kungangania na kulinda, bali ni kuhakikisha ambao hawana nao wanachukua piece of the cake (though I know that will never happen sababu ya ubinafsi)

      And Mkuu mark my words.. Vita kubwa itakayokuja Africa ni ya kugombania maji (sidhani kama Egypt na Sudan) watakubali wafe kwa kukosa maji au ukame just because Tanzania wanafanya Irrigation kwa kutumia ziwa Victoria.. Kwahiyo mkuu the better way kuepuka hii potential conflict maybe ni kuangalia environmental impacts au kuanza (rain harvesting), Sababu Mkuu kama ni choice ya kufa kwa ukame hakuna vifaru vitakaomzuia mtu wa Somalia, au Sudan au Egpyt kuja kunywa maji ya ziwa victoria
      Even a Genius Asks Questions....

    8. RukaaJuu Final

    9. #66
      Feedback's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 4,095
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      2066
      Likes Given
      1125

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Mwita25
      Hako kaziwa NYASA kenyewe hakana faida yoyote ya kiuchumi kwa taifa letu zaidi ya kutujazia nafasi tu. Waache wamalawi walichukue tu, sisi tuna fursa nyingi sana za kiuchumi mfano Ziwa Victoria, Mlima Kilimanjaro, Serengeti n.k. Tusijaribu kushawishi jeshi kuingia vitani, lina kazi nyingi nyingine za kufanya kwa taifa letu.
      Kwani kazi kuu ya jeshi ni nini kuzalisha mboga mboga.
      Robato likes this.
      Only in Tanzania

    10. #67
      VoiceOfReason's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Everywhere
      Posts : 5,239
      Rep Power : 1895
      Likes Received
      1152
      Likes Given
      603

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Feedback
      Maelezo yako yote yanaonyesha tatizo lako ni kuogopa vita tu lets say wamalawi wakupe bure utakubali.
      Mkuu you dont get my point kabisa, mimi sisemi kwamba self defense ni ujinga wala sisemi kwamba Wamalawi wapo sawa? Hapana hata mtu akija nyumbani kwako lazima ujitetee na kulinda mali na uzima wako..., Lakini point yangu ni kwamba Ubinafsi na kutokuweza kwa Binadamu kuishi pamoja ndio sababu ya haya matatizo yote hata wadudu sisimizi wanaweza kuishi pamoja na kufight against the common enemy and maybe sisi binadamu tungekuwa better off badala ya kupigana na binadamu mwenzetu tungekuwa tunapigana na mazingira ili tuweze ku-better off maisha yetu
      Last edited by VoiceOfReason; 23rd July 2011 at 14:10.
      Even a Genius Asks Questions....

    11. #68
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,723
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Arafat
      Labda wanalindwa na hawa hapa:

      Ruhanjo , Ex-TISS Bosi Mr. EM, Waziri Mkulo ............!
      Vipi Chief haya mambo unahadidhiwa au umo...mbona unatoa reference ya ex.spy late E.Mzenna ...huyu alishakufa na kusahauliwa zamani....alikuwa chief miaka ya mwanzoni kabisa baada ya uhuru akafuatiwa na kina Marehemu Gama,ndio wakaja hawa kina Hassy Kitine ..marehemu Kombe Imran....ndio unakuja wa enzi za sasa kina Cornel Apson M,...na wa sasa......
      Enzi ya Imran na miaka miwili ya mwanzo ya Apson ..kabla ya sheria mpya ya usalama wa Taifa.......wote walikuwa wana operate undercover na ilikuwa mwiko kujulikana na hata uteuzi wa viongozi wao hakuwa for public consumption....hata wakiwa kwenye hafla walikuwa hawatajwi..tofauti na sasa ambako sioo ajabu hata wameaanza kuongea na vyombo vya habari ..wanapigwa picha na kuwekewa captions....

    12. #69
      rosemarie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 4,732
      Rep Power : 1366
      Likes Received
      280
      Likes Given
      142

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By LordJustice1
      Tatizo lako unaongelea vitu vya kufikirika ndio maana unadai eti "kungekuwa na ..........! Hizo ndoto zako hazitatimia milele na tangu dunia hii iumbwe imekuwa na migogoro mfululizo! As long as resources za dunia zitaendelea kuwa depleted conflicts zitazidi kuibuka, esp kuhusu mipaka! Just imagine suala ambalo halina ubishi katika mpaka wa TZ/Burundi, jamaa wanazidi kujisogeza tu! Kwa hiyo sio kwamba watu wanataka migogoro ila uhaba wa resources ndio tatizo! Na hiyo UN unayoiamini na yenyewe inaongozwa na watu wenye kuwakilisha maslahi yao binafsi!Kwa ujumla mlinzi wa mipaka yetu ni sisi wenyewe, hakuna mtu atakayetuwezesha kuilinda mipaka hiyo!

      wamalawi wamepania kuchukua lake nyasa
      sasa kwa taarifa zao wajue wanacheza na moto
      hawatujui watanzania tulivyo wabaya tukichokozwa
      ebu tuwaache tuone wanataka nini,kwa vyovyote ipo siku wataivamia kyela,mtaona wenyewe!

    13. #70
      Feedback's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 4,095
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      2066
      Likes Given
      1125

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By VoiceOfReason
      Mkuu you dont get my point kabisa, mimi sisemi kwamba self defense ni ujinga wala sisemi kwamba Wamalawi wapo sawa? Hapana hata mtu akija nyumbani kwako lazima ujitetee na kulinda mali na uzima wako..., Lakini point yangu ni kwamba Ubinafsi na kutokuweza kwa Binadamu kuishi pamoja ndio sababu ya haya matatizo yote hata wadudu sisimizi wanaweza kuishi pamoja na kufight against the common enemy and maybe sisi binadamu tungekuwa better off badala ya kupigana na binadamu mwenzetu tungekuwa tunapigana na mazingira ili tuweze ku-better off maisha yetu
      Unajua unatoa maelezo ya jumla mno kuhusu conflics za dunia ambazo zipo na hazitakwisha hata kama dunia nzima itakuwa na jeshi moja, jaribu ku site mfano wa ziwa Nyasa tunaloliongelea tufanye nini tuache tu wamalawi wali hodhi kwa vile watu wa sehemu hizo wanaishi vizuri. Conflicts zinatofautiana sources zake na hata kuzi solve kunatofautiana.
      Last edited by Feedback; 23rd July 2011 at 14:28.
      Only in Tanzania

    14. #71
      Jenerali QoyoJB's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 13th August 2009
      Posts : 139
      Rep Power : 525
      Likes Received
      22
      Likes Given
      3

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Tuwekee hiyo ramani hapa tuone kama vipi tumjulishe Jakaya awasiliane na Jenerali Devis Mamunyange aandae vijana

    15. #72
      rosemarie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 4,732
      Rep Power : 1366
      Likes Received
      280
      Likes Given
      142

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Jenerali QoyoJB
      Tuwekee hiyo ramani hapa tuone kama vipi tumjulishe Jakaya awasiliane na Jenerali Devis Mamunyange aandae vijana

      mkuu download google earth utaona mipaka ya taifa

    16. #73
      Buchanan's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 19th May 2009
      Location : Somewhere!
      Posts : 9,252
      Rep Power : 8972
      Likes Received
      803
      Likes Given
      340

      Default

      Quote By Feedback
      Unajua unatoa maelezo ya jumla mno kuhusu conflics za dunia ambazo zipo na hazitakwisha hata kama dunia nzima itakuwa na jeshi moja, jaribu ku site mfano wa ziwa Nyasa tunaloliongelea tufanye nini tuache tu wamalawi wali hodhi kwa vile watu wa sehemu hizo wanaishi vizuri.
      Hivi suala la "kuishi vizuri" linaingiaje linaingiaje kuhusu mpaka? Kwani Iddi Amini alipoanzisha vita tulikuwa tunaishi na Waganda vibaya? Huu mpaka kati ya Tz vs Malawi umekuwa siku zote katikati ya maji, hakuna haja ya kuendeleza chokochoko zisizo na msingi!

    17. #74
      Buchanan's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 19th May 2009
      Location : Somewhere!
      Posts : 9,252
      Rep Power : 8972
      Likes Received
      803
      Likes Given
      340

      Default

      Quote By thabo mbeki
      mkuu download google earth utaona mipaka ya taifa
      GE haina mipaka halisi ya nchi yoyote!

    18. #75
      VoiceOfReason's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Everywhere
      Posts : 5,239
      Rep Power : 1895
      Likes Received
      1152
      Likes Given
      603

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Feedback
      Unajua unatoa maelezo ya jumla mno kuhusu conflics za dunia ambazo zipo na hazitakwisha hata kama dunia nzima itakuwa na jeshi moja, jaribu ku site mfano wa ziwa Nyasa tunaloliongelea tufanye nini tuache tu wamalawi wali hodhi kwa vile watu wa sehemu hizo wanaishi vizuri. Conflicts zinatofautiana sources zake na hata kuzi solve kunatofautiana.
      Kuhusu suala la Malawi hatuna jinsi wakituvamia lazima tupigane kujilinda sisi na mali yetu wala mimi hilo sibishi, ninachoongela mimi ni kuhusu maisha ya binadamu na kama vita ndio njia nzuri ya kusolve matatizo yetu, na kama binadamu wote ni wajinga badala ya kuungana na kupigana na mazingira tunapigana wenyewe kwa wenyewe.. na hili ni kuanzia enzi za kina Hitler mpaka hapo watakapokuja wajukuu zetu, itakuwa ni same story.

      Hivyo basi vichaa kama kina Hitler wapo miaka yote na inabidi tujilinde na hao wapuuzi je sio efficient kama tungekuwa na jeshi moja kubwa la dunia (lika-act kama peace keepers) kuliko hizi pesa nyingi zinazotumika kwenye majeshi, ya kila nchi? (They have got Money for War but they cant Feed the Poor - Tu Pac)..

      Tena mkuu hiki kipindi cha Nuclear Age.., ambapo vita vinaweza kupiganwa kwa technology na makombora ya mbali mwisho wa siku kwenye vita hakuna mshindi bali loosers, ni ukweli usiopingika shida nyingi za hii dunia zinaletwa na upumbavu wa mwanadamu
      Even a Genius Asks Questions....

    19. #76
      Feedback's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 4,095
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      2066
      Likes Given
      1125

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By VoiceOfReason
      Kuhusu suala la Malawi hatuna jinsi wakituvamia lazima tupigane kujilinda sisi na mali yetu wala mimi hilo sibishi, ninachoongela mimi ni kuhusu maisha ya binadamu na kama vita ndio njia nzuri ya kusolve matatizo yetu, na kama binadamu wote ni wajinga badala ya kuungana na kupigana na mazingira tunapigana wenyewe kwa wenyewe.. na hili ni kuanzia enzi za kina Hitler mpaka hapo watakapokuja wajukuu zetu, itakuwa ni same story.

      Hivyo basi vichaa kama kina Hitler wapo miaka yote na inabidi tujilinde na hao wapuuzi je sio efficient kama tungekuwa na jeshi moja kubwa la dunia (lika-act kama peace keepers) kuliko hizi pesa nyingi zinazotumika kwenye majeshi, ya kila nchi? (They have got Money for War but they cant Feed the Poor - Tu Pac)..

      Tena mkuu hiki kipindi cha Nuclear Age.., ambapo vita vinaweza kupiganwa kwa technology na makombora ya mbali mwisho wa siku kwenye vita hakuna mshindi bali loosers, ni ukweli usiopingika shida nyingi za hii dunia zinaletwa na upumbavu wa mwanadamu
      Nchi za NATO zina jeshi lao la kujihami lakini sidhani kama ndio suluhisho.
      Sidhani kama kuna mtu anapenda vita, vita haiji in a single night inatokea pale njia za kidiplomasia zinaposhindikana, nafikiri hadi sasa kwa suala hili hizo njia zingine hazijashindikana ila kama zikishindikana hapo ndipo uwezekano wa kutokea vita unapokuja na huwezi kuikimbia vinginevyo urudi tena kwenye mazungumzo au ukubali yaishe kama wengine wanavyo suggest eti kaziwa kenyewe hakazalishi kitu(sizitaki mbichi hizi).
      Only in Tanzania

    20. #77
      Feedback's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 4,095
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      2066
      Likes Given
      1125

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Buchanan
      GE haina mipaka halisi ya nchi yoyote!
      Wamalawi wanatumia hiyo picha ya google ku justify madai yao wewe utatumia ramani ipi wakati hata uliyopeleka UN inaonyesha ziwa liko upande wa Malawi.
      Only in Tanzania

    21. #78
      VoiceOfReason's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Everywhere
      Posts : 5,239
      Rep Power : 1895
      Likes Received
      1152
      Likes Given
      603

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Feedback
      Nchi za NATO zina jeshi lao la kujihami lakini sidhani kama ndio suluhisho.
      Sidhani kama kuna mtu anapenda vita, vita haiji in a single night inatokea pale njia za kidiplomasia zinaposhindikana, nafikiri hadi sasa kwa suala hili hizo njia zingine hazijashindikana ila kama zikishindikana hapo ndipo uwezekano wa kutokea vita unapokuja na huwezi kuikimbia vinginevyo urudi tena kwenye mazungumzo au ukubali yaishe kama wengine wanavyo suggest eti kaziwa kenyewe hakazalishi kitu(sizitaki mbichi hizi).
      Kubali yaishe sio suluhisho, na hawa watu vichaa wakidhani kwamba wewe ni weak wanaweza wakachukua kila kitu, kwahiyo kujilinda na kupigania chako ni muhimu sana..

      Issue nyingine NATO; AU na UNITED NATIONS zote hazina meno na zinaendeshwa kisiasa na zinaendeshwa na wachache badili ya kuwa mtetezi wa haki na wanyonge wewe mpaka watu wanauana Rwanda Yogoslavia hawa jamaa walikuwa wapi.., ingebidi wawe kama fimbo ya dunia chokochoko yoyote wawe tayari kuingilia na kuisimamisha...

      Vita vingi Africa ni vya tamaa (Congo, Sierra Leone, Angola n.k.) na hivi vya mipaka mfano kipindi iraq ilivyotaka kuichukua Kuwait inabidi mkono wa Dunia uingilie kati (ingawa kipindi kile nadhani America iliingia sababu ya kimaslahi zaidi). Na tukija kwenye suala la resources inabidi watu tuwe pro-active hususan sa hizi haya mambo ya ukame na mazingira sababu nchi jirani pakiwa na ukame na njaa na wewe umebarikiwa na maji ya kumwaga believe me haitakuwa Nyasa pekee huenda hata Sudan akadai ana hisa kwenye lake Victoria... Kwahiyo mkuu sio kwamba nabisha vita visipiganwe lakini point yangu hulka ya binadamu ndio inapelekea matatizo mengine yatafutiwe dawa ngumu.., kwenye kila tatizo kuna uzembe au uchizi wa binadamu fulani uliopelekea huo upuuzi
      Even a Genius Asks Questions....

    22. #79
      Saint Ivuga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Posts : 20,732
      Rep Power : 10179
      Likes Received
      5675
      Likes Given
      12666

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Feedback
      Mimi nimemshangaa sana TANMO eti anasema haina haja kugombea mipaka kwa vile tuna mambo mengi ya kushughulikia, tukiwa na viongozi watano tu wenye kichwa kama chake nafikiri Mwanza, Shinyanga Kagera zote zingekuwa sehemu ya Uganda, Kilimanjaro, Arusha, Mara zingekuwa za Kenya, Kigoma na Rukwa zingekuwa za Burundi, Mbeya yote wangekuwa wamewapa Malawi kwa huruma yao, Dar, Pwani, Mtwara na Tanga zingekuwa za Zanzibar. Labda Dodoma na Tabora tu ndizo zingebaki.
      huyu dogo ni kilaza sana
      JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.

    23. #80
      Hute's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 1,410
      Rep Power : 713
      Likes Received
      354
      Likes Given
      23

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      kuingia vitani hata kwa ekari moja ni muhimu kabisa hata mimi nitachukua mtutu na kwenda vitani. ile bandari ya mbambabay kule mbinga inafanya nini kama ziwa lile ni la wamalawi? na nasikia membe aliongea kule malawi kuwa ziwa lile ni la wamalawi....membe ameuza nchi wajameni...
      Kama huna meno,usile bisi, kula Bwimbwi yaani kimbugi. Uongozi ukikushinda waachie wanaoweza!

    Page 4 of 28 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...