Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

    Report Post
    Page 3 of 28 FirstFirst 1234513 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 547
    1. #1
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 812
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default Ni lake Nyasa au Lake Malawi?

      Wakubwa niwekeni sawa, nilikuwa nauliza Ziwa Nyasa ni Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi? Na je, Kwanini Ziwa Victoria liendelee kuitwa Ziwa Victoria na si Ziwa Nyanza? Au ndio kuwaenzi watawala wetu wazungu?

      Lake Nyasa or Lake Malawi?
      The name of the lake itself is also disputed. Malawi claims the lake is named 'Lake Malawi' while international maps and other countries (most notably Tanzania) claim the name of the lake to be 'Lake Nyasa'. The origins of the dispute in the name have their background in geopolitical disputes that began prior to Malawi's independence in 1964, when it was previously known as Nyasaland.

      Further complications emerged for different political reasons in the 1960s, when the then President Banda (of Malawi) became the only African leader to establish diplomatic relations with white South Africa. This was fiercely repudiated by other African leaders, including the then President Nyerere (of Tanzania). The contrasting attitudes and policies gave further impetus to disputes between the two governments, on the name of the lake itself, and the boundary between the two countries.

      At present, the dispute between the two governments is largely dormant. Intergovernmental relations between Malawi and Tanzania are largely cordial.


      Tanzania-Malawi dispute
      The partition of the lake area between Malawi and Tanzania is disputed. Tanzania claims international borders through the lake along the lines of the borders between the German and British territories before 1914; Malawi, meanwhile, claims the whole non-Mozambican lake, including the waters next to the Tanzanian shore. The foundations of the dispute were set when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, put the water under the jurisdiction of Nyasaland without a separate administration for the Tanganyika portion. The dispute has led to conflicts in the past, though for several years Malawi has declined to enforce its claims to the disputed portion.

      Occasional flare-ups in in the 1990s and in recent times have impacted fishing rights, particularly of Tanzanian's who reside on the lake shore, who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.
      Quote By Mwawado
      Habari hiyo hata Mimi nimewahi kuisikia, hata ukiangalia Ramani ya ziwa hilo linaitwa Ziwa Malawi tofauti na hapo zamani tulipoliona kwenye ramani kama ziwa nyasa. Nashindwa kuelewa kwa dhati kama mpaka umegawanywa upya ama ndio yale yale ya kuambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.Inapaswa mipaka ya nchi yetu iwekwe wazi ili kutokuja kupoteza maeneo na Vivutio vyetu vya asili.

      Mpaka wa Tanzania na Malawi una matatizo ya muda mrefu, nakumbuka mwaka 1978 kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi, kwa siku mbili mfululizo kulikuwa na amri ya kutokuwasha Taa katika Mji wa kyela mkoani Mbeya, Kipindi hicho nilikuwa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa Wakati Huo Mzee Richard Wambura alisema Mwl Nyerere ameamuru majeshi yetu yarudishe mapigo kama itaonekana Banda ataingiza majeshi Kyela. Serikali ya Banda ilikuwa inadai maeneo ya Matema Beach, Mto Songwe mpaka Ipinda yapo ndani ya Ardhi ya Malawi.

      Sasa inawezekana kabisa tumelitoa kwa hiyari ziwa liwe upande wa Malawi nasi tumebakiwa na Bandari tupu ya Itungi,ambayo sasa nafikiri haina hata meli moja baada ya TACOSHILI kufa.
      Quote By Gamba la Nyoka
      Kama serikali imelitoa hilo ziwa kwa Wamalawi pasipo kuhusisha maoni ya Watanzania, basi serikali inalo la kujibu. Huwezi kuwaambia wananchi waliokaa pale miaka nenda rudi eti, hayo maji usiyaguse ni ya wamalawi hayo.

      Hili suala ni lazima serikali ilitolee kauli haliwezi kuwa kimya kimya milele!
      Quote By Ruge Opinion
      Miaka ya 1970 Kamuzu Banda, rais wa Malawi, alitangaza kuwa lile ziwa lote ni la Malawi na akaanza kuwabugudhi Watanganyika waliokutwa kwenye ziwa. Nyerere akasogeza majeshi pale na kumtumia ujumbe Kamuzu aache uchokozi. Kamuzu akanywea.

      Tangu hapo hakujawahi kuwapo maelewano rasmi.

      Hilo ziwa lilikuwa linajulikana kama ziwa Nyasa kutokana na wenyeji pande zote mbili kuwa Wanyasa. Malawi vile vile ilikuwa inajulikana kama Nyasaland. Walipopata uhuru wakabadili jina na kujiita Malawi. Kwa hiyo na jina la ziwa wakalibadilisha bila makubaliano na sisi. Kwa hiyo kwao ni Ziwa Malawi na kwetu ni Ziwa Nyasa.
      Quote By kajembe
      Mgogoro huo ulianza enzi ya Kamuzu Banda alipokuwa raisi. miaka ya sitini Kamuzu alikuwa anazungumza kwenye redio yao, Malawi Broadcasting Corporation kutoka Blantyre, Malawi, na kusema ziwa lote ni la Malawi na pia wilaya ya Rungwe na hadi Mbeya ni sehemu ya Malawi.

      Kuna siku mwezi wa September 1968 Nyerere alimwita Banda ni kichaa. Alikasirika sana kwa sababu ya madai ya Mzee Kamuzu kwamba sehemu za Tanzania ni za Malawi. Alidai hata Mbamba Bay na sehemu zingine mkoani Ruvuma karibu na Ziwa Nyasa kwamba ni za Malawi. Pia alidai jimbo lote, Eastern Province, la Zambia. Kaunda alimjibu Banda na kusema ni shauri yake akitaka kuanzisha vita.

      Kabla ya mgogoro huo, Banda alikuja Tanzania na kukutana na Nyerere mwaka 1962 na kumwambia hakuna nchi ya Mozambique. Alimwambia Nyerere wagawane nchi hiyo. Alimwambia Nyerere sehemu ya kaskazini ya Mozambique, sehemu ya Wamakonde jimbo la Cobo Delgado, "ni lako" Nyerere. Ni sehemu ya Tanzania. Sehemu za Mozambique zilizobaki ni za Malawi, Rhodesia na Swaziland. Nyerere alimpuuza tu.

      Baada ya miaka michache, 1968, Kamuzu akatangaza na kusema sehemu zetu za Tanzania nilizozitaja hapo juu ni sehemu za Malawi.

      Mzee Kamuzu alikuwa ni mkorofi sana.

      CHANZO CHA MGOGORO

      Mgogoro wa ziwa umetokana na uamuzi wa wakoloni wa Kiingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao wa Nyasaland wakati walipokuwa wanatawala nchi hiyo na ilipokuwa ni British Protectorate. Walifanya uamuzi huo baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu ya kwanza na Waingereza walipoichukua German East Afrika - iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika katika Kijerumani - na kuwa koloni yao ya Tanganyika. Kabla ya hapo, kutokana na makubaliano kati ya Waingereza waliokuwa watawala wa Nyasaland na Wajerumani waliokuwa watawala wa nchi yetu, mpaka wa ziwa ulikuwa kati ya ziwa. Na ndiyo mpaka huo tu ambao ni halali pamoja na jina kuitwa Nyasa, siyo Malawi.

      Uamuzi wa Waingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland haukubadilisha mpaka wa ziwa kihalali kwa sababu mipaka yote ya nchi zetu ilikubaliwa wakati bara letu lilipogawanywa na wakoloni. Ni mipaka hiyo ambayo hata sisi tuliikubali baada ya kupata uhuru na hakuna hata nchi moja ambayo ina haki peke yake ya kubadilisha mipaka hiyo. Hata Waingereza hawakuwa na haki ya kulikiweka Ziwa Nyasa chini ya ukoloni wao Nyasaland kwa sababu walivunja makubaliano yao na Wajerumani ambayo yalisema mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo: nusu ni sehemu ya Deutsch Ostafrika ambayo sasa ni Tanganyika, na nusu nyingine ni ya Nyasaland chini ya utawala wa Waingereza.

      Hata wilaya ya Rungwe ambayo ilijumuisha Kyela na Ileje ilikuwa inatawaliwa kutoka Nyasaland mara tu baada ya Wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza na Waingereza walipopewa madaraka ya kutawala nchi ambayo ilikuwa ni koloni ya Wajerumani; yaani nchi yetu ya Tanganyika.

      Deutsch Ostafrika - German East Africa - ilikuwa ni nchi tatu: Tanganyika, Ruanda na Urundi (nchi ambazo zilibadili majina na kuitwa Rwanda na Burundi mwaka 1962 baada ya kupata uhuru).

      League of Nations - jumuiya ya mataifa iliyoitangulia United Nations - iliwapa Wabeligiji Ruanda na Urundi. Koloni hizo mbili za Wabeligiji zilikuwa zinatawaliwa kutoka Leopoldville, mjii mkuu wa Belgian Congo, nchi ambayo pia ilikuwa inatawaliwa na Wabeligiji. Mpango huo ni kama vile wilaya ya Rungwe ilipowahi kutawaliwa kutoka Karonga na Waingereza waliokuwa wanatawala wa Nyasaland na baadaye kiuchukua nchi yetu ya Tanganyika kutoka kwa Wajerumani.

      Baada ya vita kuu ya kwanza, na Wajerumani kushindwa vita hiyo, waziri mkuu wa Uingereza, Lloyd George, kwenye mkutano wa League of Nations alimwambia raisi wa USA, Woodrow Wilosn, kwamba aichukue German East Africa, yaani nchi yetu, na kuiweka chini ya utawala wa Merikani baada ya Wajerumani kuipoteza nchi hiyo katika vita kuu ya kwanza. Lakini President Wilson alikataa. Angekubali, nchi yetu ingetawaliwa na USA na tungekuwa koloni ya USA. Baada ya Rais Wilson kukataa kuichukua nchi yetu, Lloyd George akakubali na kusema ataichukua Tanganyika na kuiweka chini ya utawala wa nchi yake ya Uingereza. Tuliponea chupuchupu kuchukuliwa na Wamerika. Nchi yetu ingechukuliwa na Wamerika, labda tusingepata uhuru. Wamerika wangeing'ang'ania nchi yetu kama vile walivyo ng'ang'ania nchi zingine walizochukua bila kuzipa uhuru.

      Kuhusu Ziwa Nyasa, kwa kifupi ni kwamba mpaka halali uko kati ya Ziwa. Ni mpaka ambao Wajerumani na Waingereza walikubaliana kuzigawa koloni zao: Nyasaland kuwa ya Waingereza; nchi yetu, Deutsh Ostafrika, kuwa ni ya Wajerumani. Walikubaliana kwamba mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo. Upande mmoja tu, Waingereza, hawakuwa na haki ya kubadili mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland walipolikweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland.

      Nukuru kutoka kitabu cha Nyerere and Africa: End of an Era, ukurasa 484:

      "Dr. Banda also claimed substantial parts of Tanzania, including - Rungwe district - and the rest of Mbeya Region in southwestern Tanzania, as Malawian territory. He also claimed the entire Eastern Province of Zambia, provoking a curt response from Zambia’s president, Dr. Kenneth Kaunda, who challenged Banda to 'Go ahead and declare war on Zambia.'

      And President Nyerere dismissed Banda’s claim to large chunks of Tanzanian territory as 'expansionist outbursts, which do not scare us, and do not deserve my reply.' The outlandish claim also drew a sharp response from Nyerere who said Dr. Banda was 'insane.' But, he warned, 'Dr. Banda must not be ignored; the powers behind him are not insane.'"


      Akizungumza ktk chuo kikuu cha Dar es Salaam, November 1997, Mwalimu Nyerere alisema

      "In 1961 we became independent. In 1962, early 1962, I resigned as prime minister and then a few weeks later I received Dr. Banda. Mungu amuweke mahali pema (May God rest his soul in peace). I received Dr. Banda. We had just, FRELIMO had just been established here and we were now in the process of starting the armed struggle.

      So Banda comes to me with a big old book, with lots and lots of maps in it, and tells me, 'Mwalimu, what is this, what is Mozambique? There is no such thing as Mozambique.' I said, 'What do you mean there is no such thing as Mozambique?' So he showed me this map, and he said: 'That part is part of Nyasaland (it was still Nyasaland, not Malawi, at that time). That part is part of Southern Rhodesia, that part is Swaziland, and this part, which is the northern part, Makonde part, that is YOUR part.'

      So Banda disposed of Mozambique just like that. I ridiculed the idea, and Banda never liked anybody to ridicule his ideas.
      So he left and went to Lisbon to talk to Salazar about this wonderful idea. I don’t know what Salazar told him. That was ‘62."
      Quote By Simba mnyama
      Wana-JF,

      Mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa unaonesha ngoma bado mbichi kabisa. Hebu tusome hizi habari kutoka Malawi:

      Lake Malawi/Nyasa row: Time to show strong leadership
      By Cedrick Ngalande August 6, 2012
      At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times. During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time. Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now? Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

      Test for President Joyce Banda to diplomatically manage the dispute on the boundary You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts. Statesmanship is a game because image is everything in international politics.

      A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!
      It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image. The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important! When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’. President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge. If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

      Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian. Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      LordJustice1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Posts : 2,069
      Rep Power : 2301
      Likes Received
      409
      Likes Given
      36

      Default

      Quote By TANMO
      Hivi kuna faida gani kuingia vitani kugombania mipaka ilhali kwa kiasi kikubwa wakazi wa maeneo husika wanaingiliana kwenye shughuli zao za kila siku? Mmalawi akitaka mafuta ya taa anakuja Tanzania kuchukua, hivyo hivyo kwa mtanzania anayeishi mpakani. Hebu tujifunze kutumia Diplomasia jamani. Nguvu zenyewe za kupigana hatuna, mpaka leo tumeshindwa kupigana na maradhi, na umasikini. Adui ujinga ndiyo anatupiga kila kukicha, hadi Rais wa nchi naye ujinga umemshinda nguvu na sasa ndiyo unaomuongoza kwenye kila analofanya na kusema..
      Wewe kichwa chako kibovu sana! Tukiwa wajinga wataendelea kumega mipaka kama akina Iddi Amini alivyodai kwamba Kagera Salient iko Uganda! Sasa hivi nako Warundi wameumega mpaka wetu! Kamuzu Banda naye aliwahi kudai kuwa Wilaya yote ya Kyela iko Malawi! Kwa hiyo wewe kwa akili yako finyu tukae kimya tu ili "kuogopa malumbano na vita?" Open your mind please!

    4. #42
      LordJustice1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Posts : 2,069
      Rep Power : 2301
      Likes Received
      409
      Likes Given
      36

      Default

      Quote By Njowepo
      Hao google wana yao uku mambo shwari wamalawi wanakwao nasi kwetu.Uku ritui,mbambabay,manda na itungi operation zaendelea hawa jamaa hatuna kwele nao kabisa.Kwanza karonga yote wanaoishi apo ni watz so suala la mpka kwao sio issue kabsaaa
      Hapa sio suala la kuingiliana, ni suala la mipaka yetu! Hao Watz wanaokaa Karonga wanalipa kodi wapi?

    5. #43
      Zinedine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2011
      Posts : 496
      Rep Power : 510
      Likes Received
      179
      Likes Given
      236

      Default

      Quote By LordJustice1
      Jana Membe amedai eti kuna kamati imeteuliwa kuhusu suala hilo! Pinda pia aliwahi kudai eti kuna timu ya wataalamu imepelekwa kukutana na wenzao wa Malawi! Hata hivyo niliwahi kusoma kitabu kimoja kilichoandikwa "Boundaries of East Africa" mwandishi aliandika ku-suggest kwamba kisheria Tanzania haina hata tone la la maji Ziwa Nyasa (wamalawi huliita Lake Malawi)! Wamalawi wamekuwa wajanja sana kusambaza Ramani hapa nchini zinazoonesha upuuzi kama huo! Mimi nionavyo, hakuna haja ya kujadiliana na wamalawi, ni vema tukakaa kwenye "state of conflict" tukawa na sehemu ya Ziwa kuliko tukaingia kwenye mjadala na kulikosa kabisa lile Ziwa!
      Fact ni kwamba ktk ramani ya tanganyika tulyopeleka un wakati uleeee, hilo ziwa lote lipo malawi-who to be blamed, hatuna ziwa hapo wazee tuwe wapole tu. By ze way Tngnyika haina haja ya kupigania raslmali kwani proved hata tukipewa raslimali zote duniani still hazitosaidia watz chini ya system hii ya magamba, in fact natamani kwa sasa hii nchi isiwe hata na raslimali moja kwa sasa ili kuepusha hizi intervention za majizungu wanaowapa sifa za kiongo magamba ili wazidi kuchota raslmali zetu. Let kwanza tuondoe magamba then tuta-accumulate resource zetu ikiwa pamoja na huko mpakani kwa ajil ya ziwa nyasa kwa faida ya wote! Ok

    6. #44
      Mpui Lyazumbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2010
      Location : Matemanga to Tunduru
      Posts : 1,364
      Rep Power : 719
      Likes Received
      156
      Likes Given
      67

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Sawa basi, wamalawi chukueni ziwa lenu! Lakini kumbukeni tutawa-charge kila wakati wimbi likipiga na kumega ardhi yetu. Let say 1ml usd kwa sqm 1.

    7. #45
      Masuke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2008
      Posts : 2,185
      Rep Power : 1011
      Likes Received
      385
      Likes Given
      82

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Mkuu huo mpaka ndo ulivyo sio kwenye google earth tu hata ukiangalia kwenye ramani zetu wenyewe ziwa lote liko malawi ingawa watanzania wanafanya shughuli zao mule, sijui kama ndo mpaka unavyotakiwa kuwa au ni makosa ya kiuchoraji.

    8. Miaka 50

    9. #46
      Buchanan's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 19th May 2009
      Location : Somewhere!
      Posts : 9,253
      Rep Power : 8972
      Likes Received
      803
      Likes Given
      340

      Default

      Quote By Zinedine
      Fact ni kwamba ktk ramani ya tanganyika tulyopeleka un wakati uleeee, hilo ziwa lote lipo malawi-who to be blamed, hatuna ziwa hapo wazee tuwe wapole tu. By ze way Tngnyika haina haja ya kupigania raslmali kwani proved hata tukipewa raslimali zote duniani still hazitosaidia watz chini ya system hii ya magamba, in fact natamani kwa sasa hii nchi isiwe hata na raslimali moja kwa sasa ili kuepusha hizi intervention za majizungu wanaowapa sifa za kiongo magamba ili wazidi kuchota raslmali zetu. Let kwanza tuondoe magamba then tuta-accumulate resource zetu ikiwa pamoja na huko mpakani kwa ajil ya ziwa nyasa kwa faida ya wote! Ok
      Watu wa Mbinga, Ludewa na Kyela wanafaidi sana hili Ziwa kwa upande wa usafiri, shughuli za uvuvi na recreation (km Beach iliyopo Matema)! Sasa wewe unavyodai tu-accumulate resources unamaanisha nini, unataka tuwe na "Time Machine" ili kurudisha muda nyuma?

    10. #47
      Buchanan's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 19th May 2009
      Location : Somewhere!
      Posts : 9,253
      Rep Power : 8972
      Likes Received
      803
      Likes Given
      340

      Default

      Quote By masuke
      Mkuu huo mpaka ndo ulivyo sio kwenye google earth tu hata ukiangalia kwenye ramani zetu wenyewe ziwa lote liko malawi ingawa watanzania wanafanya shughuli zao mule, sijui kama ndo mpaka unavyotakiwa kuwa au ni makosa ya kiuchoraji.
      Hizo Ramani nasikia zimesambazwa na Wamalawi wenyewe hapa nchini!

    11. #48
      tindikalikali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 3,082
      Rep Power : 1215
      Likes Received
      392
      Likes Given
      89

      Default

      Quote By TANMO
      Hivi kuna faida gani kuingia vitani kugombania mipaka ilhali kwa kiasi kikubwa wakazi wa maeneo husika wanaingiliana kwenye shughuli zao za kila siku? Mmalawi akitaka mafuta ya taa anakuja Tanzania kuchukua, hivyo hivyo kwa mtanzania anayeishi mpakani. Hebu tujifunze kutumia Diplomasia jamani. Nguvu zenyewe za kupigana hatuna, mpaka leo tumeshindwa kupigana na maradhi, na umasikini. Adui ujinga ndiyo anatupiga kila kukicha, hadi Rais wa nchi naye ujinga umemshinda nguvu na sasa ndiyo unaomuongoza kwenye kila analofanya na kusema..
      Nashukuru kwa mchango wako, maisha yanaendelea tu huko. Mfano kyl, shughuli za uvuvi usio na tija zinaendelea.

    12. #49
      Zinedine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2011
      Posts : 496
      Rep Power : 510
      Likes Received
      179
      Likes Given
      236

      Default

      Quote By Buchanan
      Watu wa Mbinga, Ludewa na Kyela wanafaidi sana hili Ziwa kwa upande wa usafiri, shughuli za uvuvi na recreation (km Beach iliyopo Matema)! Sasa wewe unavyodai tu-accumulate resources unamaanisha nini, unataka tuwe na "Time Machine" ili kurudisha muda nyuma?
      Wazungu wanafaidi sana beach zetu,je ni za kwao? Plz soma post yangu ili upate ujumbe wangu-uspige meza tu ikiwa umetoka "kutafakari"

    13. #50
      ndetichia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Mwime - Buswangili
      Posts : 18,238
      Rep Power : 5109
      Likes Received
      2789
      Likes Given
      231

      Default

      Quote By Jackbauer
      Waziri muhusika hana habari,mbunge hajui na mkuu wa mkoa ana majukumu mengi!
      kwani waswahili wote wanajua mambo ya google earth kama rahisi mwenyewe ndo aliifahamu google earth baada ya kuzulu ofisi za microsoft..kwa hiyo sasa hata hizo habari sijui kama waziri atazijua..

    14. #51
      Tuyuku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Posts : 658
      Rep Power : 560
      Likes Received
      139
      Likes Given
      16

      Default

      Quote By LordJustice1
      Jana Membe amedai eti kuna kamati imeteuliwa kuhusu suala hilo! Pinda pia aliwahi kudai eti kuna timu ya wataalamu imepelekwa kukutana na wenzao wa Malawi! Hata hivyo niliwahi kusoma kitabu kimoja kilichoandikwa "Boundaries of East Africa" mwandishi aliandika ku-suggest kwamba kisheria Tanzania haina hata tone la la maji Ziwa Nyasa (wamalawi huliita Lake Malawi)! Wamalawi wamekuwa wajanja sana kusambaza Ramani hapa nchini zinazoonesha upuuzi kama huo! Mimi nionavyo, hakuna haja ya kujadiliana na wamalawi, ni vema tukakaa kwenye "state of conflict" tukawa na sehemu ya Ziwa kuliko tukaingia kwenye mjadala na kulikosa kabisa lile Ziwa!
      Mwandishi huyo alikuwa sahihi. Suala la mpaka wa Malawi na Tanzania, Wamalawi wapo sahihi kisheria. Ingawa sheria za kimataifa zinasema mahali penye maji kama maziwa na bahari mpaka ni katikati ya maji hayo hali ni tofauti kwa Malawi na Tanzania. Kwa mujibu wa mkataba baina ya Tanzania na Malawi uliosainiwa wakati wa ukoloni (kumbuka kote Tanganyika na Malawi mkoloni alikuwa Mwingereza) mpaka ni kingo za ziwa Malawi kwa upande wa Tanzania. Na huo ni mkataba rasmi nashangaa tu serikali inapiga porojo haitaki kusema ukweli. Isipokuwa kuna mazungumzo yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu sasa ili kuondoa utata uliopo juu ya mkataba huo.
      Kakalende likes this.

    15. #52
      MAHENDEKA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th July 2010
      Location : behind you
      Posts : 104
      Rep Power : 471
      Likes Received
      19
      Likes Given
      60

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Zinedine
      Fact ni kwamba ktk ramani ya tanganyika tulyopeleka un wakati uleeee, hilo ziwa lote lipo malawi-who to be blamed, hatuna ziwa hapo wazee tuwe wapole tu. By ze way Tngnyika haina haja ya kupigania raslmali kwani proved hata tukipewa raslimali zote duniani still hazitosaidia watz chini ya system hii ya magamba, in fact natamani kwa sasa hii nchi isiwe hata na raslimali moja kwa sasa ili kuepusha hizi intervention za majizungu wanaowapa sifa za kiongo magamba ili wazidi kuchota raslmali zetu. Let kwanza tuondoe magamba then tuta-accumulate resource zetu ikiwa pamoja na huko mpakani kwa ajil ya ziwa nyasa kwa faida ya wote! Ok
      sentensi yako ya kwanza hapo juu sijaielewa ,ramani ya Tanganyika tuliipeleka UN ili iweje? mipaka iliyopo leo nchi za kiafrika ziliamua kuirithi kama ilivyo toka kwa wakoloni mwaka 1884 huko Berlin ujerumani

      sasa Google inahusikaje kufanya hayo?

      Italeta fujo sana endapo kila nchi itajiamulia mambo kienyeji-enyeji kama Malawi inavyotaka kufanya,vita vya Uganda vilipiganwa kwa mambo kama haya
      Blinds leaders of blinds all finally fall into a ditch

    16. #53
      VoiceOfReason's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Everywhere
      Posts : 5,239
      Rep Power : 1895
      Likes Received
      1152
      Likes Given
      603

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By LordJustice1
      Wewe kichwa chako kibovu sana! Tukiwa wajinga wataendelea kumega mipaka kama akina Iddi Amini alivyodai kwamba Kagera Salient iko Uganda! Sasa hivi nako Warundi wameumega mpaka wetu! Kamuzu Banda naye aliwahi kudai kuwa Wilaya yote ya Kyela iko Malawi! Kwa hiyo wewe kwa akili yako finyu tukae kimya tu ili "kuogopa malumbano na vita?" Open your mind please!
      Mkuu labda hao kina Idd Amini ndio wajinga, labda binadamu wote ni wajinga.., hivi unajua ni pesa kiasi gani inatumika kwenye majeshi dunia yote?, hivi unajua ni madhara kiasi gani yanatokana na vita, na ni nini hasa huwa sababu ya kugombana zaidi ya tamaa na upuuzi wa mtu mmoja ?

      Hivi unajua binadamu tungekuwa na busara, upendo na sio ubinafsi na tamaa tungeweza kutumia malighafi za dunia yote tukala na kusaza na kila mtu akawa na maisha mazuri...

      Najua sometimes jeshi ni la muhimu ili kuweka amani na kuepukana na vichaa, lakini kama binadamu tungekuwa na busara labda kungekuwa na Jeshi kubwa la dunia (United Nations) ambalo lingekuwa kama kiranja wa dunia kwa kumfunza adabu yeyote anaekiuka maadili... au maybe LOVE ndio njia pekee ya kuepuka vita

      Maybe dunia nzima na watu wote ni wajinga na tunafight the wrong war between people badala ya kufight against the environment and betternment ya kila mtu hivi hii mipaka ni nani aliyoiweka na kwanini mtu yoyote asiweze kwenda popote pale kutafuta maisha so long wenyeji wa hapo wanamkaribisha.
      Even a Genius Asks Questions....

    17. #54
      Mwita25's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th April 2011
      Posts : 3,852
      Rep Power : 1318
      Likes Received
      1119
      Likes Given
      43

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Hako kaziwa NYASA kenyewe hakana faida yoyote ya kiuchumi kwa taifa letu zaidi ya kutujazia nafasi tu. Waache wamalawi walichukue tu, sisi tuna fursa nyingi sana za kiuchumi mfano Ziwa Victoria, Mlima Kilimanjaro, Serengeti n.k. Tusijaribu kushawishi jeshi kuingia vitani, lina kazi nyingi nyingine za kufanya kwa taifa letu.

    18. #55
      kajembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 419
      Rep Power : 516
      Likes Received
      101
      Likes Given
      116

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Wakati wa Banda alidai eneo lote la Mkoa wa Mbeya ni sehemu ya Malawi!na kuna chama kimoja siku za miaka ya Mwinyi bado walidai sehemu hiyo ya Tanzania ni ya malawi na hata hivyo wanyakyusa na watu wa Kalonga malawi wote wanaongea lugha moja na ni ndugu na ndiyo maana kunakuwa natuhuma watu wengine wanadhaniwa ni wamalawi sio watanzania,kuna Mtanzania amewahi kuchukua madaraka makubwa ktk serikali ya malawi wakati alikuwa ni Mtanzania, Hapa ndipo inapokuja umuhimu wa vitambulisho vya kitaifa,watu wamekuwa wakiangalia zaidi mikoa ya kagera ktk tatizo hilo lakini wamesahau Mbeya na Ruvuma! Hata zambia nani anajua kwamba Mwanawasa alikuwa ana asili ya Tanzania? kwa taarifa yenu Baba yake alikuwa ni Mnyakyusa wa TZ, Zambia nako lipo hilo Tatizo hasa kwa Watanzania wengi ambao wameshika madara zambia,wabunge,mawaziri na wafanya biashara wengi tu.Kuna wimbi kubwa sana la watanzania waliohamia zambia wakati wa uchumi ulioshamili wa shaba na sasa wengine watoto wao wanarudi Tz na ni wengi sana.kuna mmoja aliwahikuniambia Baba yao aliwaambia kabla hajafa hapa TZ kwamba ikiwa siku moja wakiona maisha magumu TZ wanaweza kurudi kuishi zambia maana wana uraia wa kuzaliwa Zambia na wana vyeti vya kule vya kuzaliwa,Tatizo kubwa hapa kwa utafiti mdogo niliofanya wengi wana uzalendo wa Tanzania waliko toka wazazi wao na hapo najifunza jambo kuhusu Wanyarwanda wa kitusi kwanini wanakuwa na uzalendo sana wa Rwanda kwao.

      Kitu cha muhimu nikuwa makini sana na mambo kama haya maana yanaweza kuleta matatizo makubwa sana kati ya nchi na nchi,kumbuka kuna watanzania wengi sana malawi na kama walivyo wamalawi kwa hiyo busala nikuwa na maelewano, wazungu walitugawa tu kama mbuzi huku wakigawa ndugu upande huu wengine upande mwingine,ktk malawi wilaya ya karonga wale ni wanyakyusa kule wanaitwa Wangonde na wanyakyusa wa Kyela ni wangonde pia,wale wa Rungwe ni wanselya,wengine ni wandali wa ileje na wakinga lakini hayo majina yametokana na maeneo woote hao ni kabila moja na utamaduni mmoja. Wakinga wanakuwa na tofauti kidogo zaidi sababu ya kuingiliana na wabena lakini ukiwasikiliza wanaongea lugha moja na makundi mengine haya.

      Mwisho swala la ziwa inabidi serikali kulitatua mapema tusije kuingia kwenye vita,uchumi utaharibika kama vita ya Uganda ilivyo tuhalibia ingawaje sio sababu ya kuwa masikini mpaka sasa maana rwanda wamepigana miaka yote na sasa wanatuacha mbali kabisa.

      I stand to be challenged!
      Last edited by kajembe; 23rd July 2011 at 12:57.

    19. #56
      Tusker Bariiiidi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2007
      Location : Sinza Dar es Salaam.
      Posts : 3,234
      Rep Power : 1254
      Likes Received
      376
      Likes Given
      51

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI! Ileje wilaya iliyopakana na Malawi kila kitu wanategemea Malawi kuanzia Radio zote ni za Malawi,sukari,Chumvi na comodities zote zinatoka Malawi tuwape hiyo wilaya kwani wakazi wake woote ni maskini sana...

    20. #57
      Ngongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th September 2008
      Location : Mlima Meru
      Posts : 4,877
      Rep Power : 1978
      Likes Received
      2356
      Likes Given
      3047

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Ziwa Nyasa ni mali ya Tanzania na Malawi mpaka ni katikati ya ziwa full stop.

    21. #58
      Vonix's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2011
      Posts : 564
      Rep Power : 521
      Likes Received
      73
      Likes Given
      109

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Google earth!!!!kwa hiyo tuufuate huo!kasema nani,ni ziwa lao kwa maana ya jina lakini kama ni kulitumia kwa shughuli za maendeleo mbona hiyo ni toka enzi ya banda samaki zinavuliwa humu na usafiri pia kama kawaida,kyela hadi mbambabei maana halisi ya kuwa lakwao watu wangezuiwa kuvua samaki na meli zingekatiza hilo ziwa kwa kuomba kibali malawi kitu ambacho hakipo na hakijawahi kuwa.nijuavyo mimi dai kuu la malawi kwa tz wala halikuwa ziwa ila wilaya nzima ya kyela miaka hiyo ya sabini mwishoni lakini toka tz ishinde vita ya uganda banda aliufyata.wacha walianzishe maana kuna mtafaruku wa kimaisha huko nina hakika karonga yote siku moja itakuwa mali yetu sema wanajeshi wetu wa sasa aaaaaaaaahh!!sijui kwa vile hatuna vita wanapiga raia wakubwa zao nao shimbo wamekuwa wafanya biashara ya zana za kilimo MBOMBO NGAFU.

    22. #59
      Feedback's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Posts : 4,096
      Rep Power : 1247
      Likes Received
      2066
      Likes Given
      1126

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By TANMO
      Hivi kuna faida gani kuingia vitani kugombania mipaka ilhali kwa kiasi kikubwa wakazi wa maeneo husika wanaingiliana kwenye shughuli zao za kila siku? Mmalawi akitaka mafuta ya taa anakuja Tanzania kuchukua, hivyo hivyo kwa mtanzania anayeishi mpakani. Hebu tujifunze kutumia Diplomasia jamani.

      Nguvu zenyewe za kupigana hatuna, mpaka leo tumeshindwa kupigana na maradhi, na umasikini. Adui ujinga ndiyo anatupiga kila kukicha, hadi Rais wa nchi naye ujinga umemshinda nguvu na sasa ndiyo unaomuongoza kwenye kila analofanya na kusema..
      Naona hata aibu ku argue na mtu kama wewe usiyejua maana ya mipaka ya nchi, taifa na utaifa
      siku moja utasema haina maana kugombea mlima kilimanjaro tuwaachie kenya si limlima tu watalipeleka wapi hata ukiwa Moshi mjini unauona, pole sana.
      Only in Tanzania

    23. #60
      Fidel80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 19,067
      Rep Power : 9501
      Likes Received
      3186
      Likes Given
      1237

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi - Google Earth

      Quote By Kakalende
      Mwaka jana kuna chi 2 za Amerika Kusini; Nicaragua/Honduras, nusura waingie vitani baada ya mojawapo kufuata ramani ya Google na kutangaza kuwa ndio mpaka wao rasmi.

      Hawa jamaa wa Google, msitari wa mpaka wamechora na rangi nyekundu kisha wanaonyesha LAke Nyasa yote imebaki Malawi, hii imekaaje? Nadhani hili la ugomvi wa mpaka halina itikadi, nakumbuka miaka ya nyuma enzi za Hayati Mwalimu nusura tuzipige na Malawi wakati wa Dr. Banda kwa ajili ya mpaka huu.
      Unashangaa hilo

      Mbona waKenya wanasema mlima Kilimanjaro upo kwao waziri mhusika yupo kimyaa anavimbiwa posho tu hata kulisemea anashindwa kwa vile kavimbiwa posho
      **^^+..Ukiuza Utumbo usiogope nzi..+^^**
      Chuda Raha
      Email: [email protected]

    Page 3 of 28 FirstFirst 1234513 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...