Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

    Report Post
    Page 19 of 28 FirstFirst ... 91718192021 ... LastLast
    Results 361 to 380 of 544
    1. #1
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 811
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default Ni lake Nyasa au Lake Malawi?

      Wakubwa niwekeni sawa, nilikuwa nauliza Ziwa Nyasa ni Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi? Na je, Kwanini Ziwa Victoria liendelee kuitwa Ziwa Victoria na si Ziwa Nyanza? Au ndio kuwaenzi watawala wetu wazungu?

      Lake Nyasa or Lake Malawi?
      The name of the lake itself is also disputed. Malawi claims the lake is named 'Lake Malawi' while international maps and other countries (most notably Tanzania) claim the name of the lake to be 'Lake Nyasa'. The origins of the dispute in the name have their background in geopolitical disputes that began prior to Malawi's independence in 1964, when it was previously known as Nyasaland.

      Further complications emerged for different political reasons in the 1960s, when the then President Banda (of Malawi) became the only African leader to establish diplomatic relations with white South Africa. This was fiercely repudiated by other African leaders, including the then President Nyerere (of Tanzania). The contrasting attitudes and policies gave further impetus to disputes between the two governments, on the name of the lake itself, and the boundary between the two countries.

      At present, the dispute between the two governments is largely dormant. Intergovernmental relations between Malawi and Tanzania are largely cordial.


      Tanzania-Malawi dispute
      The partition of the lake area between Malawi and Tanzania is disputed. Tanzania claims international borders through the lake along the lines of the borders between the German and British territories before 1914; Malawi, meanwhile, claims the whole non-Mozambican lake, including the waters next to the Tanzanian shore. The foundations of the dispute were set when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, put the water under the jurisdiction of Nyasaland without a separate administration for the Tanganyika portion. The dispute has led to conflicts in the past, though for several years Malawi has declined to enforce its claims to the disputed portion.

      Occasional flare-ups in in the 1990s and in recent times have impacted fishing rights, particularly of Tanzanian's who reside on the lake shore, who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.
      Quote By Mwawado
      Habari hiyo hata Mimi nimewahi kuisikia, hata ukiangalia Ramani ya ziwa hilo linaitwa Ziwa Malawi tofauti na hapo zamani tulipoliona kwenye ramani kama ziwa nyasa. Nashindwa kuelewa kwa dhati kama mpaka umegawanywa upya ama ndio yale yale ya kuambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.Inapaswa mipaka ya nchi yetu iwekwe wazi ili kutokuja kupoteza maeneo na Vivutio vyetu vya asili.

      Mpaka wa Tanzania na Malawi una matatizo ya muda mrefu, nakumbuka mwaka 1978 kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi, kwa siku mbili mfululizo kulikuwa na amri ya kutokuwasha Taa katika Mji wa kyela mkoani Mbeya, Kipindi hicho nilikuwa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa Wakati Huo Mzee Richard Wambura alisema Mwl Nyerere ameamuru majeshi yetu yarudishe mapigo kama itaonekana Banda ataingiza majeshi Kyela. Serikali ya Banda ilikuwa inadai maeneo ya Matema Beach, Mto Songwe mpaka Ipinda yapo ndani ya Ardhi ya Malawi.

      Sasa inawezekana kabisa tumelitoa kwa hiyari ziwa liwe upande wa Malawi nasi tumebakiwa na Bandari tupu ya Itungi,ambayo sasa nafikiri haina hata meli moja baada ya TACOSHILI kufa.
      Quote By Gamba la Nyoka
      Kama serikali imelitoa hilo ziwa kwa Wamalawi pasipo kuhusisha maoni ya Watanzania, basi serikali inalo la kujibu. Huwezi kuwaambia wananchi waliokaa pale miaka nenda rudi eti, hayo maji usiyaguse ni ya wamalawi hayo.

      Hili suala ni lazima serikali ilitolee kauli haliwezi kuwa kimya kimya milele!
      Quote By Ruge Opinion
      Miaka ya 1970 Kamuzu Banda, rais wa Malawi, alitangaza kuwa lile ziwa lote ni la Malawi na akaanza kuwabugudhi Watanganyika waliokutwa kwenye ziwa. Nyerere akasogeza majeshi pale na kumtumia ujumbe Kamuzu aache uchokozi. Kamuzu akanywea.

      Tangu hapo hakujawahi kuwapo maelewano rasmi.

      Hilo ziwa lilikuwa linajulikana kama ziwa Nyasa kutokana na wenyeji pande zote mbili kuwa Wanyasa. Malawi vile vile ilikuwa inajulikana kama Nyasaland. Walipopata uhuru wakabadili jina na kujiita Malawi. Kwa hiyo na jina la ziwa wakalibadilisha bila makubaliano na sisi. Kwa hiyo kwao ni Ziwa Malawi na kwetu ni Ziwa Nyasa.
      Quote By kajembe
      Mgogoro huo ulianza enzi ya Kamuzu Banda alipokuwa raisi. miaka ya sitini Kamuzu alikuwa anazungumza kwenye redio yao, Malawi Broadcasting Corporation kutoka Blantyre, Malawi, na kusema ziwa lote ni la Malawi na pia wilaya ya Rungwe na hadi Mbeya ni sehemu ya Malawi.

      Kuna siku mwezi wa September 1968 Nyerere alimwita Banda ni kichaa. Alikasirika sana kwa sababu ya madai ya Mzee Kamuzu kwamba sehemu za Tanzania ni za Malawi. Alidai hata Mbamba Bay na sehemu zingine mkoani Ruvuma karibu na Ziwa Nyasa kwamba ni za Malawi. Pia alidai jimbo lote, Eastern Province, la Zambia. Kaunda alimjibu Banda na kusema ni shauri yake akitaka kuanzisha vita.

      Kabla ya mgogoro huo, Banda alikuja Tanzania na kukutana na Nyerere mwaka 1962 na kumwambia hakuna nchi ya Mozambique. Alimwambia Nyerere wagawane nchi hiyo. Alimwambia Nyerere sehemu ya kaskazini ya Mozambique, sehemu ya Wamakonde jimbo la Cobo Delgado, "ni lako" Nyerere. Ni sehemu ya Tanzania. Sehemu za Mozambique zilizobaki ni za Malawi, Rhodesia na Swaziland. Nyerere alimpuuza tu.

      Baada ya miaka michache, 1968, Kamuzu akatangaza na kusema sehemu zetu za Tanzania nilizozitaja hapo juu ni sehemu za Malawi.

      Mzee Kamuzu alikuwa ni mkorofi sana.

      CHANZO CHA MGOGORO

      Mgogoro wa ziwa umetokana na uamuzi wa wakoloni wa Kiingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao wa Nyasaland wakati walipokuwa wanatawala nchi hiyo na ilipokuwa ni British Protectorate. Walifanya uamuzi huo baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu ya kwanza na Waingereza walipoichukua German East Afrika - iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika katika Kijerumani - na kuwa koloni yao ya Tanganyika. Kabla ya hapo, kutokana na makubaliano kati ya Waingereza waliokuwa watawala wa Nyasaland na Wajerumani waliokuwa watawala wa nchi yetu, mpaka wa ziwa ulikuwa kati ya ziwa. Na ndiyo mpaka huo tu ambao ni halali pamoja na jina kuitwa Nyasa, siyo Malawi.

      Uamuzi wa Waingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland haukubadilisha mpaka wa ziwa kihalali kwa sababu mipaka yote ya nchi zetu ilikubaliwa wakati bara letu lilipogawanywa na wakoloni. Ni mipaka hiyo ambayo hata sisi tuliikubali baada ya kupata uhuru na hakuna hata nchi moja ambayo ina haki peke yake ya kubadilisha mipaka hiyo. Hata Waingereza hawakuwa na haki ya kulikiweka Ziwa Nyasa chini ya ukoloni wao Nyasaland kwa sababu walivunja makubaliano yao na Wajerumani ambayo yalisema mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo: nusu ni sehemu ya Deutsch Ostafrika ambayo sasa ni Tanganyika, na nusu nyingine ni ya Nyasaland chini ya utawala wa Waingereza.

      Hata wilaya ya Rungwe ambayo ilijumuisha Kyela na Ileje ilikuwa inatawaliwa kutoka Nyasaland mara tu baada ya Wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza na Waingereza walipopewa madaraka ya kutawala nchi ambayo ilikuwa ni koloni ya Wajerumani; yaani nchi yetu ya Tanganyika.

      Deutsch Ostafrika - German East Africa - ilikuwa ni nchi tatu: Tanganyika, Ruanda na Urundi (nchi ambazo zilibadili majina na kuitwa Rwanda na Burundi mwaka 1962 baada ya kupata uhuru).

      League of Nations - jumuiya ya mataifa iliyoitangulia United Nations - iliwapa Wabeligiji Ruanda na Urundi. Koloni hizo mbili za Wabeligiji zilikuwa zinatawaliwa kutoka Leopoldville, mjii mkuu wa Belgian Congo, nchi ambayo pia ilikuwa inatawaliwa na Wabeligiji. Mpango huo ni kama vile wilaya ya Rungwe ilipowahi kutawaliwa kutoka Karonga na Waingereza waliokuwa wanatawala wa Nyasaland na baadaye kiuchukua nchi yetu ya Tanganyika kutoka kwa Wajerumani.

      Baada ya vita kuu ya kwanza, na Wajerumani kushindwa vita hiyo, waziri mkuu wa Uingereza, Lloyd George, kwenye mkutano wa League of Nations alimwambia raisi wa USA, Woodrow Wilosn, kwamba aichukue German East Africa, yaani nchi yetu, na kuiweka chini ya utawala wa Merikani baada ya Wajerumani kuipoteza nchi hiyo katika vita kuu ya kwanza. Lakini President Wilson alikataa. Angekubali, nchi yetu ingetawaliwa na USA na tungekuwa koloni ya USA. Baada ya Rais Wilson kukataa kuichukua nchi yetu, Lloyd George akakubali na kusema ataichukua Tanganyika na kuiweka chini ya utawala wa nchi yake ya Uingereza. Tuliponea chupuchupu kuchukuliwa na Wamerika. Nchi yetu ingechukuliwa na Wamerika, labda tusingepata uhuru. Wamerika wangeing'ang'ania nchi yetu kama vile walivyo ng'ang'ania nchi zingine walizochukua bila kuzipa uhuru.

      Kuhusu Ziwa Nyasa, kwa kifupi ni kwamba mpaka halali uko kati ya Ziwa. Ni mpaka ambao Wajerumani na Waingereza walikubaliana kuzigawa koloni zao: Nyasaland kuwa ya Waingereza; nchi yetu, Deutsh Ostafrika, kuwa ni ya Wajerumani. Walikubaliana kwamba mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo. Upande mmoja tu, Waingereza, hawakuwa na haki ya kubadili mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland walipolikweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland.

      Nukuru kutoka kitabu cha Nyerere and Africa: End of an Era, ukurasa 484:

      "Dr. Banda also claimed substantial parts of Tanzania, including - Rungwe district - and the rest of Mbeya Region in southwestern Tanzania, as Malawian territory. He also claimed the entire Eastern Province of Zambia, provoking a curt response from Zambia’s president, Dr. Kenneth Kaunda, who challenged Banda to 'Go ahead and declare war on Zambia.'

      And President Nyerere dismissed Banda’s claim to large chunks of Tanzanian territory as 'expansionist outbursts, which do not scare us, and do not deserve my reply.' The outlandish claim also drew a sharp response from Nyerere who said Dr. Banda was 'insane.' But, he warned, 'Dr. Banda must not be ignored; the powers behind him are not insane.'"


      Akizungumza ktk chuo kikuu cha Dar es Salaam, November 1997, Mwalimu Nyerere alisema

      "In 1961 we became independent. In 1962, early 1962, I resigned as prime minister and then a few weeks later I received Dr. Banda. Mungu amuweke mahali pema (May God rest his soul in peace). I received Dr. Banda. We had just, FRELIMO had just been established here and we were now in the process of starting the armed struggle.

      So Banda comes to me with a big old book, with lots and lots of maps in it, and tells me, 'Mwalimu, what is this, what is Mozambique? There is no such thing as Mozambique.' I said, 'What do you mean there is no such thing as Mozambique?' So he showed me this map, and he said: 'That part is part of Nyasaland (it was still Nyasaland, not Malawi, at that time). That part is part of Southern Rhodesia, that part is Swaziland, and this part, which is the northern part, Makonde part, that is YOUR part.'

      So Banda disposed of Mozambique just like that. I ridiculed the idea, and Banda never liked anybody to ridicule his ideas.
      So he left and went to Lisbon to talk to Salazar about this wonderful idea. I don’t know what Salazar told him. That was ‘62."
      Quote By Simba mnyama
      Wana-JF,

      Mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa unaonesha ngoma bado mbichi kabisa. Hebu tusome hizi habari kutoka Malawi:

      Lake Malawi/Nyasa row: Time to show strong leadership
      By Cedrick Ngalande August 6, 2012
      At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times. During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time. Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now? Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

      Test for President Joyce Banda to diplomatically manage the dispute on the boundary You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts. Statesmanship is a game because image is everything in international politics.

      A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!
      It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image. The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important! When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’. President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge. If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

      Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian. Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    2. Miaka 50

    3. #361
      Mlamba Ndimu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th August 2012
      Location : Kusadikika
      Posts : 10
      Rep Power : 342
      Likes Received
      1
      Likes Given
      3

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Quote By Augustine Moshi
      It does not make sense for one country to have its border on the beach in another country. Such a border cannot be defended.

      Ni kichekesho kwamba unaweza ukae kwenye ufukwe wa ziwa na kila unapoogelea uanaingia nchi nyingine. We should not accept that.

      Kweli ni kichekesho. Hata Wamalawi wanajua ndio maana miaka yote hiyo walikaa kimya labda tu kutikisa kiberiti hapa na pale. Yaani hata kama ziwa lote ni la kwao hata kama walipewa kihalali sisi tunawezaje kudefend border? Lazima tugawane nusu kwa nusu. Tutumie diplomatic channels zote, ikishindikana ndio hivyo tena.....

    4. #362
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,141
      Rep Power : 41573
      Likes Received
      6044
      Likes Given
      1056

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Quote By Augustine Moshi
      Mpaka tuliokuwa nao wakati wa kupata uhuru ndio ulitambuliwa na OAU, na ndio unatambuliwa na AU. Mpaka huo uko katikati ya ziwa. It does not make sense for one country to have its border on the beach in another country. Such a border cannot be defended.

      Wakati Kamuzu Banda alipotingisha kiberiti alikuta kimejaa; na ndugu zetu wa Malawi wakaacha hiyo ishu. Sasa wametingisha tena. Je, kiberiti bado kimejaa? wakidhani hakijajaa hawataacha kung'ang'aniza.

      Tumeshatoa tamko rasmi kwamba hakuna kufanya utafiti wowote wa mafuta na gesi sehemu ambayo sisi tunajua ni yetu; na badala yake tujadiliane kwanza. Malawi imekataa rasmi kusimamisha shughuli hiyo. What is our plan B? Lazima tulipanga tutafanyaje kama wasipositisha. Sio kupigana, bali inabidi kuweka wazi kwamba ndege yote itakayoingia anga la Tanzania bila kibali itakamatwa au kutunguliwa. Tukiwa wazi kwenye hilo basi hakuna ndege itathubutu kuingia.

      Ni kichekesho kwamba unaweza ukae kwenye ufukwe wa ziwa na kila unapoogelea uanaingia nchi nyingine. We should not accept that.

      Sheria au mkataba uisiokuwa wa haki hauna nguvu. Ni kama mikataba ya 3% ya dhahabu yetu; kwa vile siyo ya haki tumedai ijadiliwe upya. Ni kama Group Areas Act za South Africa na Rhodesia zilivyokuwa hazikubaliki pamoja na kwamba zilikuwa sheria. Mikataba kati ya wakoloni ambayo sio ya haki haina nguvu. Hatuhitaji kuikubali.
      Kaka usipotee namna hivi basi, kule kwenye deep theology na logic ukikosa sana upande wako maji ya idiocracy yanajaa.

      Hiyo point ya absurdity ya mpaka kuwa determined na a shifting shoreline aliisema Mwalimu Nyerere, succinctly.
      JokaKuu likes this.
      Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.


    5. #363
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By Kiranga
      Kaka usipotee namna hivi basi, kule kwenye deep theology na logic ukikosa sana upande wako maji ya idiocracy yanajaa.

      Hiyo point ya absurdity ya mpaka kuwa determined na a shifting shoreline aliisema Mwalimu Nyerere, succinctly.
      Naomba upunguze mabombastic kama ya wale waliosoma seminari enzi za Kilatini, naomba utufafanulie haya baadhi ya maneno sie wengine tulisoma enzi za walimu wa UPE ili kutunusuru kuisoma jf na dikshenari pembeni!.
      Idiocracy!
      Absurdity!
      Succinctly!, etc
      Last edited by Pasco; 20th August 2012 at 09:17.

    6. #364
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 855
      Rep Power : 966
      Likes Received
      544
      Likes Given
      601

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Quote By Pasco
      Naomba upunguze mabombastic kama ya wale waliosoma seminari enzi za Kilatini, naomba utufafanulie haya baadhi ya maneno sie wengine tulisoma enzi za walimu wa UPE ili kutunusuru kuisoma jf na dikshenari pembeni!.
      Idiocracy!
      Absurdity!
      Succintcly!, etc
      Pasco, ina maana ni kweli hujawahi kukutana na maneno kama haya maishani mwako?
      Mbona hata process ya kufungua computer yako au ku-browse hata website yoyote hayo unayoita bombastics huwezi kuyaepuka.

      hebu na wewe nieleza maana ya maneno yafuatayo ambayo uswahilini yanatumika sana:
      mdada
      mkaka
      tigo
      kunji
      vagi
      mlokole


      na mengine tele!
      Pasco likes this.
      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    7. #365
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 855
      Rep Power : 966
      Likes Received
      544
      Likes Given
      601

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Asante kwa THANKS yako PASCO kwenye post yangu hii namba 364. Ndicho ninachokupendea na naamini wengi wana cha kujifunza kwako.

      Ingekuwa mwingine nilivyojibu humu angeporomosha matusi.

      Keep it up Pascal. JF ni mahala pa kuelimishana ingawa bado kuna kazi kufika huko!
      Kiranga likes this.
      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    8. FemaTV & Radio

    9. #366
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,141
      Rep Power : 41573
      Likes Received
      6044
      Likes Given
      1056

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Quote By Pasco
      Naomba upunguze mabombastic kama ya wale waliosoma seminari enzi za Kilatini, naomba utufafanulie haya baadhi ya maneno sie wengine tulisoma enzi za walimu wa UPE ili kutunusuru kuisoma jf na dikshenari pembeni!.
      Idiocracy!
      Absurdity!
      Succinctly!, etc
      Check out www.dictionary.com
      Pasco likes this.
      Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.


    10. #367
      MtuKwao's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th October 2006
      Posts : 175
      Rep Power : 681
      Likes Received
      7
      Likes Given
      11

      Default Re: Mpaka wa Tanzania na Malawi ni katikati ya Ziwa Nyasa

      Quote By Mzuvendi
      Any county is entitled to print its own maps. However, international maps I have seen show that Lake Nyasa is in Malawi. The British administrators allocated the section of the lake that was under German East Africa to Malawi. I don't why they did it. But I guess they thought they will be in Africa forever. They didn't and they left Africans with tones of problems to solve.
      Tanganyika was then a protectorate under Britain! May be they did what would best serve their interest then, shift the whole lake to Malawi, their colony!!

    11. #368
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 855
      Rep Power : 966
      Likes Received
      544
      Likes Given
      601

      Default Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi? Tuliacha wavitumie...

      Kisiwa cha Ngkuyo kiko kilometa 11.1 kutoka bandari ya Mbamba_Bay. Kisiwa cha Lundu kiko kilomita 13.6 kutoka hapohapo Mbamba_Bay.

      Wakati pwani ya karibu kwa upande wa Malawi ni kwamba Ngkuyo kiko kilometa 45.9 na kile cha Lundu kiko kilomita 41.7.

      Visiwa vyote hivi hasa Ngkuyo ni miliki ya Malawi enzi na enzi. Kisiwa hiki Ngkuyo ni maarufu kwa utalii na hujulikana kama Ngkuyo Island Rocks. Hiki Ngkuyo Island kinatangazwa sana duniani kama diving centre (Click here).

      Ukitaka kuona zaidi watalii wanavyokaribishwa kuona aina ya samaki wa kisiwa hiki ambacho sehemu kubwa ni mawe angalia video hii.

      Kwa nini nimeleta thread hii kwa suala lilelile la Malawi. Ni kweli ni suala lilelile lakini kwa context nyingine ili tupate kushirikiana kimawazo, ugumu ninaouona kila mara tunavyozidi kupekua suala hili.

      Kwa kilomita nilizoweka hapo, kwa hali ya kawaida ni kwamba visiwa hivi viko kilomita chache sana kutoka pwani ya Tanzania kuliko pwani ya Malawi. Kilomita 11.1 za kutoka Ngkuyo Island ni sawa na jijini Mwanza kutoka Usagara kwenda Kigongo_Ferry.

      Maana yake ni kwamba ukiwa Mbamba_Bay unakiona kisiwa hiki vizuri tu kwa macho. Lakini kutoka kisiwa hiki kwenda Malawi yaani kilomita 45.9 ni umbali wa kuzidi Mwanza hadi Ukerewe kwani kutoka Kayenze hadi Nansio pale Ukerewe ni kilomita 30.5 tu.

      Sasa, tunapofikiri kwamba tunaweza kupata mpaka ukawa nusu kwa nusu, basi maana yake Malawi iache kabisa kuvitumia visiwa hivi kwa shughuli yoyote bila ruhusa yetu hata kama tangu kuja kwa wakoloni walivitumia kama vya Malawi na dunia nzima ikafahamu hivyo!

      Je, watakubali kiasi hicho. Ndiyo tuone ugumu wa suala hili. Ugumu ambao kitabu hiki kilishauzungumza kwenye ukurasa wa 249 {Click here}.

      Ukisoma hapo utaona kwamba mimi nimetaja visiwa hivi viwili lakini yeye kavitaja vitatu yaani Ngkuyo, Lundu na Papia.

      Binafsi, hapa ndipo nadhani hata mawaziri wote wameshaeleza kwamba suala hili ni gumu na inaweza likafikisha International Coast of Justice.

      Visiwa ni sehemu muhimu sana. Kisiwa cha Bongoyo kiko kilometa 5.2 kutoka Msasani_slipway. Kisiwa cha Saa Nane hakizidi kilomita mbili kutoka Tilapia Hotel pale Mwanza.

      Lakini leo useme unachukua kisiwa cha Bongoyo au ufanye lolote kwa kisiwa cha Saa Nane hakika hapo unakaribisha mengine tu.

      Ndiyo na wamalawi wanavyoviona visiwa hivi ambavyo havijawahi kuwa vya nchi nyingine japo tumeona kwamba viko jirani zaidi na Tanzania. Lakini tunaposema mpaka uwe nusu kwa nusu basi fikiri mara mbili maana kuna baadhi humu walidhani ni maji tu hakuna masuala kama haya.

      Na kama ndege zilizotua majini zilifukuzwa sasa sijui kwa nini matumizi ya utalii kwa visiwa hivi hayakukatazwa tangu kale? Je, kama kweli ndege zilizuiwa je, visiwa hivi vimehamishwa visiwe karibu na Tanzania. hapana haiwezekani. Je, shughuli za utalii za Malawi zimesimamishwa? Binafsi sijasikia labda nyinyi wenzangu.

      Kama ni hivyo, basi nina haki ya kusema na sisiti kusema kukataza ndege zisitue majini ni sawa kabisa na kusema shughuli yoyote ya ziwani mle maadamu iko kwenye ile nusu inayoelekea Tanzania isiendelee.

      Hivyo, sisiti kusema kusimamisha utafiti wa zile ndege kwenye nusu hii na kuacha shughuli za utalii ni unafiki usioweza kutetewa kwa njia yoyote.

      Ukweli ni kwamba shughuli za utalii na kila kitu kwa visiwa hivyo zinaendelea. Tuachane na hayo turudi kwenye kujiuliza. Kama tutabahatika kushinda na nusu ikawa kwetu, je umiliki wa visiwa hivi utakuwaje?

      Ni rahisi sana kukurupuka na kusema vitakuwa vyetu. Si rahisi kiasi hicho. Hapa ndipo inabidi tuangalie nini kilitokea kwenye ziwa hilohilo kwa upande wa Mozambique. Ukweli ni kwamba mpango mzima wa kwanza ilikuwa ziwa lile mipaka ipite ukingo wa mashariki kama ilivyofanyika Tanzania. Lakini Portugal ikaingia mkataba walau kupata sehemu ya ziwa hilo.

      Mkataba ulipoingia Nyasaland wakapewa milima kadhaa na Mozambique ikapewa portion ya Ziwa na ndiyo sababu kuna sehemu kule mpaka wa Mozambique unaingia ziwani.

      Lakini badi hiyo haikutosha. Wakati wanagawa hivi, ikaja kesi ya visiwa kadhaa kikiwemo kisiwa cha Lukoma. Ile nusu waliyopewa Mozambique ikawa inakimeza kisiwa hiki Lukoma. Lakini makubaliano yale ya Portugal na Britain yaliweka wazi kwamba Lukoma Island kweli iingie ndani ya Mozambique territory lakini ibaki kwenye ownership ya Nyasaland!

      Hivyo, ukiiangalia Lukoma kwenye ramani unaweza kukurupuka na kusema ni sehemu ya Mozambique. Na wala si kukurupuka tu, kama huijui histiry hii kama wengi wasivyijua kuhusu mipaka hii na wakawa hawajaka notekey yoyote basi hakika utasema Lukoma ni sehemu ya Mozambique wakati ukweli ni sehemu ya Malawi.

      Hali hii ya Lukoma yaani eneo fulani la Malawi kuwa ndani ya eneo la nchi nyingine huitwa exclave. Ni tofauti na Britani kuwa na Falkland au USA kuwa na Alaska na Hawaii kwa sababu hayo hayajazunukwa na nchi nyingine.

      Hivyo, tunapojadili hili suala la Malawi, tu-explore possibilities zote ambazo tunaweza kuziona ngeni na tukaishia kupiga kelele kwa sababu tu ya kutokujua.

      Binafsi, bado sijawa na hakika kama tutapata ziwa hili kama tunavyolihitaji. Lakini tukilipata basi tusisahau kwamba kesi ys Lukoma kule Mozambique inaweza kuwa imeweka precedent kiasi kwamba visiwa hivi tunaweza tusivipate hata kama tunaweza kupata nusu ya ziwa.

      Jadili kwa kuongeza elimu
      Jasusi, JokaKuu, Kichuguu and 3 others like this.
      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    12. #369
      amkawewe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th December 2011
      Posts : 747
      Rep Power : 525
      Likes Received
      119
      Likes Given
      534

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Duh shule mpya kwa tusiojua haya mambo.

    13. #370
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 3,992
      Rep Power : 1214
      Likes Received
      973
      Likes Given
      247

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi.

      Wasomaji, huyu Nikupateje ana kazi maalum humu jamvini.

      Nikuambie kitu kimoja ewe Nikupateje;
      kipindi kabla ya utafiti wa mafuta na gesi ziwani TULIKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA lakini kwa sasa, HATUKUBALINI KUTOKUBALIANA, na hatimaye mmoja lazima adundwe ndiyo akubali matakwa ya mwenziye. Tutaipigaje malawi!!!!!
      Ni rahisi zaidi popo kuwa ndege, kuliko ndizi kuwa tunda

    14. #371
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,623
      Rep Power : 2892
      Likes Received
      3838
      Likes Given
      12231

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Nikupateje,
      Weka picha au ramani hapa mkuu, ili tuone hivyo visiwa viko upande gani.
      Nikupateje likes this.

    15. #372
      TAYADI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th July 2012
      Posts : 1,315
      Rep Power : 608
      Likes Received
      209
      Likes Given
      253

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Hivi ni wajerumani na waingereza waliokuwa watu wa kwanza kuishi kando ya ziwa?... Hivi kabla ya Anglo-German agreement ya mwaka 1890 - Ziwa hili lilikuwa la nani?......

      Ni watu gani walikuwa wakiishi kando ya ziwa upande wa Tanzania?...... Waliishije?.... Waliliitaje ziwa hili?..... Utamaduni wao ulikuwaje?.... Hawa Wapangwa, Wakisi, Wanyakyusa, n.k. Ziwa hili walilitumiaje?. Mgawanyo huu ulipofanyika wadanganyika hawa walikuwa wanaelewa nini kuhusu makubaliano haya?

      ...Ni karibu miaka 122 tu imepita sasa - tangu hawa jamaa kutoka ulaya wakubaliane kunyang'anya mali ya WADANGANYIKA!!!,..... Je, vizazi vyote enzi za mkoloni vilichukuliaje shughuli za uchumi zilizokuwa zikifanyika upande wa DANGANYIKA?.. Ni wangapi wamewahi kukamatwa na kushitakiwa kwa kuiba samaki au maji Ziwani?.... Kwa nini wadanganyika miaka yote hiyo wameachiwa kutumia ziwa hilo bila kikwazo chochote?..... "WENYE MALI" ....hawajawahi kufanya doria au nao waliamini kila mmoja anahaki ya kumiliki?. AU?...

      KYALA KUMWANYA UKO ULIKO?............ PAKUPYUTAA?...
      Mantaleka, Nikupateje and isoko like this.

    16. #373
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,744
      Rep Power : 1162
      Likes Received
      251
      Likes Given
      2511

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      sasa wewe mwenyewe umeongelea mfano wa visiwa vya lukoki vilivyo ndani ya mipaka ya msumbiji, sasa unaona ugumu gani kwa suala hili kuwa solved kama la msumbiji? kwamba eneo letu ni mpaka km kadha ndani ya kisiwa lakini hivyo visiwa tuna mwachia dada yetu afanyie biashara, sema mafuta au gesi ikipatikana ni yetu. upo?

    17. #374
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,836
      Rep Power : 3272
      Likes Received
      1314
      Likes Given
      916

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Ni bahati mbaya kuwa mkataba wa Berlin kuhusu maji haukuwa umezungumza lolote kuhusu visiwa vilivyoko ndani ya maji yale; kwa hiyo inawezekana visiwa vikawa vya Malawi (ingawa sivijui) lakini maji yakiwa ya Tanzania.

      Tatizo kubwa sasa hivi ni kuwa mkataba wa Heligo uliandikwa kwa kutumia background ya mkataba wa Berlini kuhusu maji ya bonde la Kongo, ambapo maji yale yalikuwa ya wote.

      Background hiyo ndiyo inayofanya sheria za leo za kimataifa kuhusu maji ziwe halali kuwa mpaka halisi utapita katikati ya maji hayo. Swaziland zimezungukwa na Afrika ya Kusini lakini bado siyo sehemu ya Afrika ya Kusini.
      JokaKuu likes this.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    18. #375
      TAYADI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th July 2012
      Posts : 1,315
      Rep Power : 608
      Likes Received
      209
      Likes Given
      253

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      NAJIULIZA MASWALI MENGI ....!... Ni nani mwenye mamlaka ya kugawa mipaka ya ziwa au maeneo ya kiutawala?.... Je, Ni mikataba ya kikoloni tu iliyo valid?.... Je, sisi (Waafrika hatuwezi kufanya makubaliano ya msingi mpaka mzungu aseme?........... .........Hivi ni wajerumani na waingereza waliokuwa watu wa kwanza kuishi kando ya ziwa?... Hivi kabla ya Anglo-German agreement ya mwaka 1890 - Ziwa hili lilikuwa la nani?...... Ni watu gani walikuwa wakiishi kando ya ziwa upande wa Tanzania kabla ya mkataba huu?...... Walilitambua ziwa hili kuwa ni la nani?........... Waliishije?.... Waliliitaje ziwa hili?..... Utamaduni wao ulikuwaje?........ Hawa Wapangwa, Wakisi, Wanyakyusa, n.k. Ziwa hili walilitumiaje?. Mgawanyo huu ulipofanyika wadanganyika hawa walikuwa wanaelewa nini kuhusu makubaliano haya? ....Ni karibu miaka 122 tu imepita sasa - tangu hawa jamaa kutoka ulaya wakubaliane kunyang'anya mali ya WADANGANYIKA!!!,..... Je, vizazi vyote enzi za mkoloni vilichukuliaje shughuli za uchumi zilizokuwa zikifanyika upande wa DANGANYIKA?.. Ni wangapi wamewahi kukamatwa na kushitakiwa kwa kuiba samaki au maji Ziwani?.... Kwa nini wadanganyika miaka yote hiyo wameachiwa kutumia ziwa hilo bila kikwazo chochote?..... "WENYE MALI" ....hawajawahi kufanya doria au nao waliamini kila mmoja anahaki ya kumiliki?. AU?... ........................... Acha ninyamaze mwisho watasema hata hewa hii ninayovuta ni ya Malawi!.... .... GWE KYALA, KUMWANYA UKO ULIKO?............ PAKUPYUTAA?...

    19. #376
      JamboJema's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 14th June 2011
      Location : Mwanza
      Posts : 746
      Rep Power : 551
      Likes Received
      77
      Likes Given
      216

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Unafahamu kisiwa kilichopo ziwa victoria kilicholeta kelele kati ya Uganda na Kenya? Unajua kulitamkwa nn juu ya 'mmiliki wa maji' na 'mmiliki wa kisiwa'? Mie sio msomi kama wewe unavyojinasibu. Tafiti utupatie jibu.
      Uchakavu wa Mahakama si nafuu ya hukumu!

    20. #377
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 855
      Rep Power : 966
      Likes Received
      544
      Likes Given
      601

      Default Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Quote By Kichuguu
      Ni bahati mbaya kuwa mkataba wa Berlin kuhusu maji haukuwa umezungumza lolote kuhusu visiwa vilivyoko ndani ya maji yale; kwa hiyo inawezekana visiwa vikawa vya Malawi (ingawa sivijui) lakini maji yakiwa ya Tanzania.

      Tatizo kubwa sasa hivi ni kuwa mkataba wa Heligo uliandikwa kwa kutumia background ya mkataba wa Berlini kuhusu maji ya bonde la Kongo, ambapo maji yale yalikuwa ya wote.

      Background hiyo ndiyo inayofanya sheria za leo za kimataifa kuhusu maji ziwe halali kuwa mpaka halisi utapita katikati ya maji hayo. Swaziland zimezungukwa na Afrika ya Kusini lakini bado siyo sehemu ya Afrika ya Kusini.

      Kichuguu

      Kwanza najua kupata LIKE kutoka kwako ni ngumu mno. Asante kwa LIKE yako. Sikutaka kutaja mfano wa Swaziland lakini nimejikita zaidi kwenye exclave kama visiwa hivi vya Malawi wakati Swaziland unayosema ni enclave kama ilivyo Vatican nchini Italy au Mnaco nchini Ufaransa.

      Lakini tukiingia ndani kwenye majibu yako sikubishii sana na kwa kiasi fulani yanaweza kuwa na ukweli. Lakini unaposema kwamba Heligoland ilitegemea precedence iliyowekwa na Berlin Conference kulingana na Congo Basin terms kwamba waterbodies ziwe free zone mimi hapo siwezi kukubishia sana.

      Kwa maana yako hii na ya wengi tu ni kwamba Lake Malawi si letu wala la Tanzania. Hata ikiwa hivi basi hakuna humu anayweweza kubisha kwamba Malawi hawajawahi kutukataza kufanya shughuli zetu humo. Kwa maana nyingine ni kwamba wale wanaosema kwa nini hawajaweka immigration controll office umeshawajibu kwamba huwezi kuweka office hiyo kwenye free zone unatakiwa kuiweka free zone inapoishia!

      Sasa kama ni hivyo, ni nini sababu ya Tanzania kuwaambia Malawi wasitafiti na ikibidi mafuta kwenye free zone?

      Tatizo jingine Kichuguu ni kwamba hizi sababu mnazoleta humu mitandaoani haielekei kama maafisa wa serikali wanazitumia hizo. Angalia majibu yao wote tangu jambo limeibuka.

      Hoja yangu niliyoleta sasa huwezi kuijibu kwa majibu mepesi kuwa water bodies zilikuwa free. Sasa kama zilikuwa free na Lake Malawi ikawa free kwa nini visiwa vyote vilivyomo humo ziwani ni vya Malawi bila kujali viko pwani yao au 0.25 miles kutoka Pwani yetu!

      Hebu tutafakari hili jambo na kuukubali ukweli wake. Tuache tabia zile za kuona wazi umeugua ugonjwa ambao hauponi halafu na dalili zote ni kufa halafu tunajiridhisha kwamba utapona tu. Ni bora hata ugonjwa maana huwa kuna tumaini la miujiza kuliko kuleta vigezo ambavyo kila vikijadiliwa kwa kina unaona wazi hapa hakuna kitu.
      Last edited by Nikupateje; 22nd August 2012 at 09:04.
      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    21. #378
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 855
      Rep Power : 966
      Likes Received
      544
      Likes Given
      601

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Quote By JamboJema
      Unafahamu kisiwa kilichopo ziwa victoria kilicholeta kelele kati ya Uganda na Kenya? Unajua kulitamkwa nn juu ya 'mmiliki wa maji' na 'mmiliki wa kisiwa'? Mie sio msomi kama wewe unavyojinasibu. Tafiti utupatie jibu.
      Wewe unaleta hoja nusunusu halafu unataka uletewe majibu, sasa unakuja humu kufanya nini bila kutuambia wewe ulipotafiti ulipata majibu gani!

      Sisi tumetafiti haya tumekuja na hoja iliyopo mezani. Uvivu wa kutafiti umekutawala unaishia kutaja unayoyataja tena nusunusu.

      Kajipange kwanza ukija na utafiti wenye majibu mambovu utajibiwa tu humu.

      Jibu hoja zangu wakati uanrudi kutafiti huko ulipopataja
      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    22. #379
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,226
      Rep Power : 908
      Likes Received
      283
      Likes Given
      59

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi? Tuliacha wavitumi

      walizi wa mipaka yetu wako wapi?

    23. #380
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 855
      Rep Power : 966
      Likes Received
      544
      Likes Given
      601

      Default Re: Mbona Tanzania hatukuwahi kudai visiwa vya Ngkuyo na Lundu kuwa si vya Malawi. Tuliacha wavitumi

      Quote By August
      sasa wewe mwenyewe umeongelea mfano wa visiwa vya lukoki vilivyo ndani ya mipaka ya msumbiji, sasa unaona ugumu gani kwa suala hili kuwa solved kama la msumbiji? kwamba eneo letu ni mpaka km kadha ndani ya kisiwa lakini hivyo visiwa tuna mwachia dada yetu afanyie biashara, sema mafuta au gesi ikipatikana ni yetu. upo?
      Unawaona walikuonea kwa suala la Malawi ndiyo haohao walioli-solve suala la Msumbiji, yaani wakoloni Portugese na Britons.

      Usingekuwa mvivu kusoma hata hii post yangu ungegundua kwamba wakoloni wa Mozambique walilisolve hili kwa kukaa mezani na kuandika mkataba mpya wa mpaka kupita katikati ya Ziwa.

      Lakini unatakiwa kujua kuwa Nyasaland haikupoteza nusu hiyo bure. Mkataba uliitaka Mozambique kutoa sehemu fulani ya nchi kavu yenye milima kadhaa kwa Nyasaland (Malawi).

      Sasa, maadam si mimi ila wewe mwenyewe umetaka nipende ya Mozambiqueyafanyike hapa Tanzania basi maana yake na sisi tutoe sehemu ya nchi kavu tuwape Malawi ili tupate kisehemu cha ziwa kama walivyopewa Mozambique.
      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    Page 19 of 28 FirstFirst ... 91718192021 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...