Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

    Report Post
    Page 18 of 29 FirstFirst ... 8161718192028 ... LastLast
    Results 341 to 360 of 573
    1. #1
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 815
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default Ni lake Nyasa au Lake Malawi?

      Wakubwa niwekeni sawa, nilikuwa nauliza Ziwa Nyasa ni Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi? Na je, Kwanini Ziwa Victoria liendelee kuitwa Ziwa Victoria na si Ziwa Nyanza? Au ndio kuwaenzi watawala wetu wazungu?

      Lake Nyasa or Lake Malawi?
      The name of the lake itself is also disputed. Malawi claims the lake is named 'Lake Malawi' while international maps and other countries (most notably Tanzania) claim the name of the lake to be 'Lake Nyasa'. The origins of the dispute in the name have their background in geopolitical disputes that began prior to Malawi's independence in 1964, when it was previously known as Nyasaland.

      Further complications emerged for different political reasons in the 1960s, when the then President Banda (of Malawi) became the only African leader to establish diplomatic relations with white South Africa. This was fiercely repudiated by other African leaders, including the then President Nyerere (of Tanzania). The contrasting attitudes and policies gave further impetus to disputes between the two governments, on the name of the lake itself, and the boundary between the two countries.

      At present, the dispute between the two governments is largely dormant. Intergovernmental relations between Malawi and Tanzania are largely cordial.


      Tanzania-Malawi dispute
      The partition of the lake area between Malawi and Tanzania is disputed. Tanzania claims international borders through the lake along the lines of the borders between the German and British territories before 1914; Malawi, meanwhile, claims the whole non-Mozambican lake, including the waters next to the Tanzanian shore. The foundations of the dispute were set when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, put the water under the jurisdiction of Nyasaland without a separate administration for the Tanganyika portion. The dispute has led to conflicts in the past, though for several years Malawi has declined to enforce its claims to the disputed portion.

      Occasional flare-ups in in the 1990s and in recent times have impacted fishing rights, particularly of Tanzanian's who reside on the lake shore, who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.
      Quote By Mwawado View Post
      Habari hiyo hata Mimi nimewahi kuisikia, hata ukiangalia Ramani ya ziwa hilo linaitwa Ziwa Malawi tofauti na hapo zamani tulipoliona kwenye ramani kama ziwa nyasa. Nashindwa kuelewa kwa dhati kama mpaka umegawanywa upya ama ndio yale yale ya kuambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.Inapaswa mipaka ya nchi yetu iwekwe wazi ili kutokuja kupoteza maeneo na Vivutio vyetu vya asili.

      Mpaka wa Tanzania na Malawi una matatizo ya muda mrefu, nakumbuka mwaka 1978 kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi, kwa siku mbili mfululizo kulikuwa na amri ya kutokuwasha Taa katika Mji wa kyela mkoani Mbeya, Kipindi hicho nilikuwa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa Wakati Huo Mzee Richard Wambura alisema Mwl Nyerere ameamuru majeshi yetu yarudishe mapigo kama itaonekana Banda ataingiza majeshi Kyela. Serikali ya Banda ilikuwa inadai maeneo ya Matema Beach, Mto Songwe mpaka Ipinda yapo ndani ya Ardhi ya Malawi.

      Sasa inawezekana kabisa tumelitoa kwa hiyari ziwa liwe upande wa Malawi nasi tumebakiwa na Bandari tupu ya Itungi,ambayo sasa nafikiri haina hata meli moja baada ya TACOSHILI kufa.
      Quote By Gamba la Nyoka View Post
      Kama serikali imelitoa hilo ziwa kwa Wamalawi pasipo kuhusisha maoni ya Watanzania, basi serikali inalo la kujibu. Huwezi kuwaambia wananchi waliokaa pale miaka nenda rudi eti, hayo maji usiyaguse ni ya wamalawi hayo.

      Hili suala ni lazima serikali ilitolee kauli haliwezi kuwa kimya kimya milele!
      Quote By Ruge Opinion View Post
      Miaka ya 1970 Kamuzu Banda, rais wa Malawi, alitangaza kuwa lile ziwa lote ni la Malawi na akaanza kuwabugudhi Watanganyika waliokutwa kwenye ziwa. Nyerere akasogeza majeshi pale na kumtumia ujumbe Kamuzu aache uchokozi. Kamuzu akanywea.

      Tangu hapo hakujawahi kuwapo maelewano rasmi.

      Hilo ziwa lilikuwa linajulikana kama ziwa Nyasa kutokana na wenyeji pande zote mbili kuwa Wanyasa. Malawi vile vile ilikuwa inajulikana kama Nyasaland. Walipopata uhuru wakabadili jina na kujiita Malawi. Kwa hiyo na jina la ziwa wakalibadilisha bila makubaliano na sisi. Kwa hiyo kwao ni Ziwa Malawi na kwetu ni Ziwa Nyasa.
      Quote By kajembe View Post
      Mgogoro huo ulianza enzi ya Kamuzu Banda alipokuwa raisi. miaka ya sitini Kamuzu alikuwa anazungumza kwenye redio yao, Malawi Broadcasting Corporation kutoka Blantyre, Malawi, na kusema ziwa lote ni la Malawi na pia wilaya ya Rungwe na hadi Mbeya ni sehemu ya Malawi.

      Kuna siku mwezi wa September 1968 Nyerere alimwita Banda ni kichaa. Alikasirika sana kwa sababu ya madai ya Mzee Kamuzu kwamba sehemu za Tanzania ni za Malawi. Alidai hata Mbamba Bay na sehemu zingine mkoani Ruvuma karibu na Ziwa Nyasa kwamba ni za Malawi. Pia alidai jimbo lote, Eastern Province, la Zambia. Kaunda alimjibu Banda na kusema ni shauri yake akitaka kuanzisha vita.

      Kabla ya mgogoro huo, Banda alikuja Tanzania na kukutana na Nyerere mwaka 1962 na kumwambia hakuna nchi ya Mozambique. Alimwambia Nyerere wagawane nchi hiyo. Alimwambia Nyerere sehemu ya kaskazini ya Mozambique, sehemu ya Wamakonde jimbo la Cobo Delgado, "ni lako" Nyerere. Ni sehemu ya Tanzania. Sehemu za Mozambique zilizobaki ni za Malawi, Rhodesia na Swaziland. Nyerere alimpuuza tu.

      Baada ya miaka michache, 1968, Kamuzu akatangaza na kusema sehemu zetu za Tanzania nilizozitaja hapo juu ni sehemu za Malawi.

      Mzee Kamuzu alikuwa ni mkorofi sana.

      CHANZO CHA MGOGORO

      Mgogoro wa ziwa umetokana na uamuzi wa wakoloni wa Kiingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao wa Nyasaland wakati walipokuwa wanatawala nchi hiyo na ilipokuwa ni British Protectorate. Walifanya uamuzi huo baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu ya kwanza na Waingereza walipoichukua German East Afrika - iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika katika Kijerumani - na kuwa koloni yao ya Tanganyika. Kabla ya hapo, kutokana na makubaliano kati ya Waingereza waliokuwa watawala wa Nyasaland na Wajerumani waliokuwa watawala wa nchi yetu, mpaka wa ziwa ulikuwa kati ya ziwa. Na ndiyo mpaka huo tu ambao ni halali pamoja na jina kuitwa Nyasa, siyo Malawi.

      Uamuzi wa Waingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland haukubadilisha mpaka wa ziwa kihalali kwa sababu mipaka yote ya nchi zetu ilikubaliwa wakati bara letu lilipogawanywa na wakoloni. Ni mipaka hiyo ambayo hata sisi tuliikubali baada ya kupata uhuru na hakuna hata nchi moja ambayo ina haki peke yake ya kubadilisha mipaka hiyo. Hata Waingereza hawakuwa na haki ya kulikiweka Ziwa Nyasa chini ya ukoloni wao Nyasaland kwa sababu walivunja makubaliano yao na Wajerumani ambayo yalisema mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo: nusu ni sehemu ya Deutsch Ostafrika ambayo sasa ni Tanganyika, na nusu nyingine ni ya Nyasaland chini ya utawala wa Waingereza.

      Hata wilaya ya Rungwe ambayo ilijumuisha Kyela na Ileje ilikuwa inatawaliwa kutoka Nyasaland mara tu baada ya Wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza na Waingereza walipopewa madaraka ya kutawala nchi ambayo ilikuwa ni koloni ya Wajerumani; yaani nchi yetu ya Tanganyika.

      Deutsch Ostafrika - German East Africa - ilikuwa ni nchi tatu: Tanganyika, Ruanda na Urundi (nchi ambazo zilibadili majina na kuitwa Rwanda na Burundi mwaka 1962 baada ya kupata uhuru).

      League of Nations - jumuiya ya mataifa iliyoitangulia United Nations - iliwapa Wabeligiji Ruanda na Urundi. Koloni hizo mbili za Wabeligiji zilikuwa zinatawaliwa kutoka Leopoldville, mjii mkuu wa Belgian Congo, nchi ambayo pia ilikuwa inatawaliwa na Wabeligiji. Mpango huo ni kama vile wilaya ya Rungwe ilipowahi kutawaliwa kutoka Karonga na Waingereza waliokuwa wanatawala wa Nyasaland na baadaye kiuchukua nchi yetu ya Tanganyika kutoka kwa Wajerumani.

      Baada ya vita kuu ya kwanza, na Wajerumani kushindwa vita hiyo, waziri mkuu wa Uingereza, Lloyd George, kwenye mkutano wa League of Nations alimwambia raisi wa USA, Woodrow Wilosn, kwamba aichukue German East Africa, yaani nchi yetu, na kuiweka chini ya utawala wa Merikani baada ya Wajerumani kuipoteza nchi hiyo katika vita kuu ya kwanza. Lakini President Wilson alikataa. Angekubali, nchi yetu ingetawaliwa na USA na tungekuwa koloni ya USA. Baada ya Rais Wilson kukataa kuichukua nchi yetu, Lloyd George akakubali na kusema ataichukua Tanganyika na kuiweka chini ya utawala wa nchi yake ya Uingereza. Tuliponea chupuchupu kuchukuliwa na Wamerika. Nchi yetu ingechukuliwa na Wamerika, labda tusingepata uhuru. Wamerika wangeing'ang'ania nchi yetu kama vile walivyo ng'ang'ania nchi zingine walizochukua bila kuzipa uhuru.

      Kuhusu Ziwa Nyasa, kwa kifupi ni kwamba mpaka halali uko kati ya Ziwa. Ni mpaka ambao Wajerumani na Waingereza walikubaliana kuzigawa koloni zao: Nyasaland kuwa ya Waingereza; nchi yetu, Deutsh Ostafrika, kuwa ni ya Wajerumani. Walikubaliana kwamba mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo. Upande mmoja tu, Waingereza, hawakuwa na haki ya kubadili mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland walipolikweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland.

      Nukuru kutoka kitabu cha Nyerere and Africa: End of an Era, ukurasa 484:

      "Dr. Banda also claimed substantial parts of Tanzania, including - Rungwe district - and the rest of Mbeya Region in southwestern Tanzania, as Malawian territory. He also claimed the entire Eastern Province of Zambia, provoking a curt response from Zambia’s president, Dr. Kenneth Kaunda, who challenged Banda to 'Go ahead and declare war on Zambia.'

      And President Nyerere dismissed Banda’s claim to large chunks of Tanzanian territory as 'expansionist outbursts, which do not scare us, and do not deserve my reply.' The outlandish claim also drew a sharp response from Nyerere who said Dr. Banda was 'insane.' But, he warned, 'Dr. Banda must not be ignored; the powers behind him are not insane.'"


      Akizungumza ktk chuo kikuu cha Dar es Salaam, November 1997, Mwalimu Nyerere alisema

      "In 1961 we became independent. In 1962, early 1962, I resigned as prime minister and then a few weeks later I received Dr. Banda. Mungu amuweke mahali pema (May God rest his soul in peace). I received Dr. Banda. We had just, FRELIMO had just been established here and we were now in the process of starting the armed struggle.

      So Banda comes to me with a big old book, with lots and lots of maps in it, and tells me, 'Mwalimu, what is this, what is Mozambique? There is no such thing as Mozambique.' I said, 'What do you mean there is no such thing as Mozambique?' So he showed me this map, and he said: 'That part is part of Nyasaland (it was still Nyasaland, not Malawi, at that time). That part is part of Southern Rhodesia, that part is Swaziland, and this part, which is the northern part, Makonde part, that is YOUR part.'

      So Banda disposed of Mozambique just like that. I ridiculed the idea, and Banda never liked anybody to ridicule his ideas.
      So he left and went to Lisbon to talk to Salazar about this wonderful idea. I don’t know what Salazar told him. That was ‘62."
      Quote By Simba mnyama View Post
      Wana-JF,

      Mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa unaonesha ngoma bado mbichi kabisa. Hebu tusome hizi habari kutoka Malawi:

      Lake Malawi/Nyasa row: Time to show strong leadership
      By Cedrick Ngalande August 6, 2012
      At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times. During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time. Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now? Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

      Test for President Joyce Banda to diplomatically manage the dispute on the boundary You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts. Statesmanship is a game because image is everything in international politics.

      A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!
      It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image. The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important! When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’. President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge. If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

      Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian. Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE


    2. #341
      robert josephat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 625
      Rep Power : 481
      Likes Received
      79
      Likes Given
      282

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      utumwa wa kifikra ni tatizo kubwa ktk nchi zetu za kiafrika sidhani eti kitu maji ambao ni uhai kwa binadamu na viumbe leo hii tunayagombea tena kwa kutishiana kijeshi si sawa kabisa.hapa wazungu wanataka kuyatumia maji kama silaha ya kutupiganisha sisi waafrika ili wao wafaudu na mbinu wanayotumia ni mafuta ambayo yako ndani ya maji.jamani tuwe makini kabisa kwani mbinu hii ya maji ndio ambao kinjekitile mgwale alioitumia kuwaangamiza wafrika wenzake dhidi ya risasi za moto za mjerumani.mungu ibariki tanzania,mungu ibariki afrika asanteni.

    3. #342
      robert josephat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 625
      Rep Power : 481
      Likes Received
      79
      Likes Given
      282

      Default Re: Ni kweli kuwa Tanzania haina haki na ziwa Nyasa?

      wazungu wao siku zote target zao ni 50-200yrs mbele na mara nyingi plans/target hizo uzibalidisha na kuwa ni missions kiukweli ebu tuyaangalie hata hayo makampuni ya explolation kwa upande ule wa malawi yanatoka wapi maana influence kubwa ni lazima itoke kwa wale walioprpopose hiyo mipaka awali.katika hili sishangai mlango wa kusini kuwa ndio mlango mkuu kwa tanzania yetu kuteleza ama kuteketea kiuchumi siku zijazo kama juhudi za makusudi hatachukuliwa kutatua maana kwa sasa tz ni mojawapo ya nchi pekee duniani ambao mali zake zingali mbichi na nyingi zimeiva hivyo kuwatoa udenda hata wale ambao ni majirani zake.kiukweli sisi tanzania ni wakarimu sana kwani hata kwenye wimbo wetu wa taifa tumemwoba mwenyezi mungu kuwabaliki waafrika/afrika lakini wao leo hii wao wanataka kutuvua nguo hadharani katika hili mwenyezi mungu atawaadhibu siku moja,lakini nasi tuwaombee maana hawajui watendalo.mungu ibariki tzn,mungu ibaliki afrika,asanteni.

    4. #343
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,692
      Rep Power : 3657
      Likes Received
      3211
      Likes Given
      473

      Default Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana 1/2

      Mgogoro wa Ziwa Nyasa na tamaa ya Malawi katika mafuta na gesi



      Wanafunzi wakivuka ziwa Nyasa kuelekea shule.


      SASA ieleweke wazi kwamba hali si shwari kati ya Tanzania na Malawi. Pengine ni vizuri kujiuliza leo ni kwa nini mtafuruku uchukue nafasi kubwa leo.

      Kivipi Mtanzania wa kawaida, aoneshwe kama ni jambo lililokuja ghafla? Kimsingi, mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi umekuwapo kwa zaidi ya nusu karne. Hivi sasa umechukua sura mpya baada ya nchi hiyo jirani kusema ndiyo inayomiliki sehemu yote ya ziwa hilo.



      Pengine kauli hiyo peke yake, isingeleta shari. Alama ya hatari imetokana na kauli ya vitisho, iliyotoka Serikali ya Malawi kwamba itafanya kila linalowezekana, ikiwamo kutumia nguvu za kijeshi kuhakikisha ziwa hilo linabaki kwenye himaya yao.

      Picha iliyopo ni kwamba Malawi wameshaona Watanzania ni wapole. Kwamba ni waoga wa kupitiliza, kwa hiyo wakiambiwa kuhusu nguvu ya kijeshi, watarudi nyuma. Sijui uthubutu huu wameupata wapi lakini ninachowaza ni kwamba viongozi wa Malawi, wanahisi sisi ni mazezeta. Vile ambavyo madai yao yalivyo hayana msingi na hayakubaliki hata kidogo, ndivyo ambavyo ukitafakari wanachokitaka kiwe, huku wakitoa vitisho vya kupigana vita, unaweza kujiuliza kuhusu wigo wa uelewa wao.

      Ni rahisi kuamini ndugu zetu hao wana dosari za kiufahamu. Kweli Ziwa Nyasa lote ni lao? Huo mpaka ni wa namna gani hasa, kiasi kwamba eti Mtanzania akikanyaga tu maji ya ziwa hilo, anakuwa yupo Malawi. Muda wa kutafuta maelewano hawataki, wanakimbilia kwenye vita.

      Malawi wanahitaji kuwaheshimu Watanzania. Ni ukweli ulio wazi kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Malawi kutoa madai hayo, lakini ni mara yake ya kwanza kutumia kauli yenye vitisho vya kiwango hicho kinachoashiria vita kati ya Tanzania na wao. Madai hayo yalitolewa kwa mara ya kwanza na Rais wa Kwanza wa nchi hiyo, Dk. Kamuzu Banda.

      Madai hayohayo, yalirudiwa na wanasiasa mbalimbali, akiwemo mmoja wa viongozi wa vyama vya upinzani, Chakufya Chiana. Baadhi ya maswali yanayoulizwa ni haya yafuatayo;

      Je, ni mambo yapi yameshindikana kutatuliwa katika mgogoro huo kwa muda wote huo wakati kuna vyombo vya kimataifa vyenye uwezo na mamlaka za kusuluhisha migogoro kama hiyo? Pili, ni upande upi ambao umeonekana kukwamisha mazungumzo hayo? Kwa muda mrefu yamekuwapo mazungumzo kuhusu mgogoro wa mpaka huo, kupanuka kwa mgogoro huo hivi sasa kumechochewa na dalili za kuwapo kwa kiasi kikubwa cha gesi na mafuta katika ziwa hilo na hatua ya Malawi kuingia mkataba na kampuni ya Surestream Petroleum ya Uingereza.

      Kampuni hiyo, tayari imeanza utafiti na utafutaji wa nishati hiyo, ikiwamo sehemu za eneo la Tanzania katika ziwa hilo.

      Kauli ya shari ya Serikali ya Malawi ilitokana na hatua ya Serikali ya Tanzania kuitaka serikali hiyo kusitisha shughuli hizo hadi suala la mpaka litakapopatiwa ufumbuzi.

      Je, baadhi ya mambo kwenye mgogoro yamekuwa yakifanywa siri? Mbona sasa hali ya amani imehatarishwa hivi sasa? Ukweli ni kwamba Tanzania na Malawi, zimekuwa na uhusiano mzuri kiasi cha wananchi wa pande zote katika mpaka huo kutembeleana, kuoana, kufanya biashara na hata kupata huduma zote pasipo kujali uraia wao.

      Mtazamo wangu unanifikisha kwenye jawabu kwamba endapo wananchi wa pande zote mbili wangejua nani amekuwa kikwazo katika juhudi za kutatua mgogoro huo, wangeweka shinikizo kwa viongozi wa pande hizo mbili na hatimaye kupata suluhu ya mgogoro huo.

      Kwa kuangalia sura ya undugu uliopo kati ya Watanzania na Wamalawi, kwa hakika vita haitakiwi. Lakini tunafanyaje ikiwa ndugu zetu hao wanataka mapambano? Je, vita ni utashi wao au Malawi inatumiwa ili kutia dosari historia yetu nzuri, kwamba ni kisiwa cha amani? Muda utaeleza.

      Watanzania hatutakiwi kuombea vita kwa sababu hiyo siyo sherehe. Kwamba watu watakutana ukumbini, kucheza muziki, kula kuku, bata, kunywa supu na aina nyingine ya maakuli.

      Tukumbuke Vita ya Kagera iliyomwondoa Nduli Iddi Amin. Vita hiyo kama mfano hai kabla ya kuingia kwenye vita na Malawi, iliigharimu Tanzania maisha ya watu na kubwa zaidi ni mali. Tanzania ilipata hasara ya fedha za kigeni zaidi ya shilingi trilioni 5.

      Wananchi wa leo, waliokuwa na akili timamu kwa wakati huo, wanakumbuka madhara makubwa yaliyotokea. Kama ni ushauri, basi napendekeza kwamba mgogoro huo wa mpaka kati yetu na Malawi umalizike kwa pande zote mbili kufikia maridhiano badala ya vita.

      Lakini kama hawataki je? Na kwa nini watangulize kauli ya kutaka vita? Kama si tamaa ya mafuta na gesi, basi wametumwa kuvuruga amani yetu.

      Kwa upande mwingine, Malawi haiwezi kulaumiwa kwa sababu mgogoro huo ni pandikizi la ukoloni uliotokana na mkataba wa mwaka 1890 ambao ulielekeza kwamba sehemu yote ya ziwa hilo iwe upande wa Malawi.

      Hata hivyo, swali la kujiuliza ni hili;

      Je, viongozi wa Malawi, wao hawatumii akili? Kweli Ziwa Nyasa lote ni lao na Tanzania haina eneo kabisa? Tanzania inayo haki ya kumiliki nusu ya eneo la ziwa hilo kutokana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sheria ya Bahari ya mwaka 1982 inayotaka nchi zinazogawana eneo la bahari au ziwa zigawane eneo hilo nusu kwa nusu.


      Chanzo: GPL














    5. #344
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,692
      Rep Power : 3657
      Likes Received
      3211
      Likes Given
      473

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana


      Kwahiyo labda tunaweza kushinda na hii sheria ya UN ya Mwaka 1982 kuhusu Bahari na Maziwa...

      Kama ni Maziwa kama ni nchi Mbili lazima wagawane nusu kwa nusu...

      Sijui kwanini Waziri wetu wa Nje hakulijua hili; Wangemuuliza Salim A. Salim au Benjamin Mkapa wengeweza kumsaidia

      Lakini anaonekana kichwa ngumu... na akalidanganya BUNGE!! chombo cha kutunga sheria...

    6. #345
      Hute's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 1,424
      Rep Power : 718
      Likes Received
      358
      Likes Given
      23

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      cha muhimu ni kwamba, mgogoro huu ulikuwepo muda mrefu na haujawahi kutatuliwa, hivyo ni muda muafaka sasaivi kwasababu tayari umeshaibuka usitulie hadi utatuliwe kieleweke...la sivyo, tutakuja tuchapane siku moja.
      Tanzania ni tajiri,tena tajiri sanaaaa, lakini dah we acha tu! sijui kwanini watu wake masikini?


    7. #346
      Manyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Posts : 1,929
      Rep Power : 766
      Likes Received
      309
      Likes Given
      294

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      Huu ndo muda muafaka wa kushughulikia huu mgogoro moja kwa moja, na siyo kubakisha tena viporo vitakavyoleta shida baadae!

    8. #347
      Lu-ma-ga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 1,922
      Rep Power : 832
      Likes Received
      541
      Likes Given
      8

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      Ziwa wameuza wakubwa wa nchi wala mama banda hana kosa ni mkataba wa siri msitafute mchawi subirini mtakuja shangaaa.

    9. #348
      livingafrican's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th June 2009
      Posts : 20
      Rep Power : 514
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Wakuu,ukweli uko wazi kwamba ziwa lote ni la Malawi

    10. #349
      dudus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,339
      Rep Power : 1018
      Likes Received
      1323
      Likes Given
      531

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      Quote By nngu007 View Post
      ...
      Hata hivyo, swali la kujiuliza ni hili;

      Je, viongozi wa Malawi, wao hawatumii akili?
      Kweli Ziwa Nyasa lote ni lao na Tanzania haina eneo kabisa? Tanzania inayo haki ya kumiliki nusu ya eneo la ziwa hilo kutokana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sheria ya Bahari ya mwaka 1982 inayotaka nchi zinazogawana eneo la bahari au ziwa zigawane eneo hilo nusu kwa nusu.


      Chanzo: GPL

      Wakuu naomba kufahamishwa:-

      (i) Kabla ya ukoloni; wakazi waliokuwa wakiishi upande wa Tanganyika walikuwa wanalitumia hilo ziwa kwa shughuli mbali mbali toka vizazi na vizazi.

      (ii) Ingelikuwa mkataba wa kulitoa ziwa lote kwa Malawi ni kwa manufaa ya Tanganyika pia au mabadilishano ambayo Tanganyika ingenufaika kwa namna fulani (kama Russia ilivyoiuzia Marekani eneo la Alaska) angalau ingeleta sense. Lakini haiingii akilini kuinyang'anya Tanganyika hususan wananchi wanaozunguka ziwa ili wao warudishiane visiwa (Heligoland) walivyodhulumiana huko Ulaya ni zaidi ya ukatili kwa watu wetu. Hii haikubaliki popote na kwa hali yoyote.

      (iii) Hivi ni kila mkataba ulioingiwa na serikali za kikoloni ni binding hadi leo? Hata kama huu wa Ziwa Nyasa uliowadhalilisha wananchi wetu kwa kiwango cha kutisha? Uliowanyangánya watu wetu rasilimali waliyopewa na Mungu tangu kuwepo kwa dunia hii? Kwa udhalilishaji huu na hofu waliyoishi nayo wakazi wa eneo husika kwa miaka yote tangu 1890 hadi leo wanastahili kudai na kulipwa fidia kwa athari walizozipata.

      (iv) Mikataba ya kimataifa leo hii inasemaje?

    11. #350
      Zanta's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th April 2011
      Posts : 1,329
      Rep Power : 757
      Likes Received
      434
      Likes Given
      368

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      Quote By nngu007 View Post

      Kwahiyo labda tunaweza kushinda na hii sheria ya UN ya Mwaka 1982 kuhusu Bahari na Maziwa...

      Kama ni Maziwa kama ni nchi Mbili lazima wagawane nusu kwa nusu...

      Sijui kwanini Waziri wetu wa Nje hakulijua hili; Wangemuuliza Salim A. Salim au Benjamin Mkapa wengeweza kumsaidia

      Lakini anaonekana kichwa ngumu... na akalidanganya BUNGE!! chombo cha kutunga sheria...
      hebu soma kipengele hapo kwenye red ndio wamalawi wana base.
      Where the coasts of two States are opposite or adjacent to each other, neither of the two States is entitled, failing agreement between them to the contrary, to extend its territorial sea beyond the median line every point of which is equidistant from the nearest points on the baselines from which the breadth of the territorial seas of each of the two States is measured. The above provision does not apply, however, where it is necessary by reason of historic title or other special circumstances to delimit the territorial seas of the two States in a way which is at variance therewith
      hiii ndio point ya wamalawi wao wanasema kuna Treaty ya 1890 kwa hiyo hiyo UN convection ya 1982 hai apply hapa
      Better to have a Good Dictatorship than Bad Democracy !!!!

    12. #351
      Bra-joe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 596
      Rep Power : 483
      Likes Received
      184
      Likes Given
      0

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      Mimi ningeishauri serikali iache kubishana na wa Malawi, iende katikati ya ziwa hilo na kuulinda mpaka wetu tu, kama inavyolindwa mipaka mingine, atakaevuka bila ruhusa basi ashughulikiwe ipasavyo. Hapo wa Malawi watatia akili.

    13. #352
      Who Cares?'s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Location : JUPITER PLANET
      Posts : 1,390
      Rep Power : 840
      Likes Received
      570
      Likes Given
      279

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      Quote By bra-joe View Post
      mimi ningeishauri serikali iache kubishana na wa malawi, iende katikati ya ziwa hilo na kuulinda mpaka wetu tu, kama inavyolindwa mipaka mingine, atakaevuka bila ruhusa basi ashughulikiwe ipasavyo. Hapo wa malawi watatia akili.
      nakuunga mkono mia kwa miaaa...

      I like these germany shephered spicies of dogs...hawana makelele wala nini..just vitendo..they says actions speaks louder than words... Weka soldiers mpakani hawaongei na mtu na hakuna mtu kuingia na sio tu katika maji mpaka nchi kavu..

      Wanawake hao wa malawi wanaweza kudai na kyela ni yao...na hao mabosi wao ni marufuku kupima mafuta hata diseli achilia mbali oxygen na methane...

      Akivuka mtu kuja kwetu risasi...kamata weka ndani mpaka atuonyeshe hiyo visa inayomruhusu kuja kwetu.
      if we die the next generation will fight them too..and the one after them untill the victory is on our side

    14. #353
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,692
      Rep Power : 3657
      Likes Received
      3211
      Likes Given
      473

      Default Re: Malawi tamaa ya Mafuta na Gesi; Sheria ya 1982 ya UN ya Bahari na Maziwa inazitaka nchi kugawana

      Quote By Zanta View Post
      hebu soma kipengele hapo kwenye red ndio wamalawi wana base.

      hiii ndio point ya wamalawi wao wanasema kuna Treaty ya 1890 kwa hiyo hiyo UN convection ya 1982 hai apply hapa

      Lakini Hiyo Treaty ya 1890 ilifanyika kwa Manufaa ya Nchi Mbili ambazo hazikujali Manufaa ya nchi zingine Mbili...

      Wakati Malawi inapewa ziwa lote; Hawakujali Manufaa ya Ziwa hilo kwa Tanganyika... Nchi hizo ziliinyima Uhuru wa

      kulitumia ziwa hilo na wananchi wake... nadhani litaweza kujadiliwa UN na hiyo ya 1982...
      Zanta likes this.

    15. #354
      misha's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th November 2010
      Posts : 31
      Rep Power : 441
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Madai ya Hayati Kamuzu Banda, yalizimwa pale alipofahamishwa kuwa ndani ya nchi yake kulikuwa na sehemu ambazo zilikuwa zikikaliwa na wenyeji wa Tanzania-kwa maana kuwa Machifu wa Tanzania walipewa eneo kama sehemu yao.

      Kwa mfano Wnyanyembe walipewa sehemu kama hizo nao wakabaki Itetemia, kuna uwezekano mkubwa Hayati Karume alikuwa na asili ya Tanzania tangu awali.

      Kama ni kugawana basi Tanzania itamega eneo kubwa la Malawi. Kun'gang'ania Ziwa Nyasa na kukaidi kusititisha uchunguzi wa gesi ni kitendo kinachohalalisha vita moja kwa moja.

    16. #355
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 4,085
      Rep Power : 1237
      Likes Received
      988
      Likes Given
      247

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi



      watukutu wote hugongwa makonzi, hiyo ramani inaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa, tutambue kuwa ramani hiyo haikuchorwa miaka ya 1800 mnayo-refer kuwepo treaty, hapo kwa ramani hiyo, treaty imekuwa doomed down to a pont of not existing. AKOLEWE KONZI ASOTAKA KUJUA HILI.
      Ni rahisi zaidi popo kuwa ndege, kuliko ndizi kuwa tunda

    17. #356
      Kyakukanwa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th September 2010
      Posts : 10
      Rep Power : 446
      Likes Received
      1
      Likes Given
      4

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania na sehemu yetu yote ndani ya ziwa Nyasa..!

    18. #357
      Kyakukanwa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th September 2010
      Posts : 10
      Rep Power : 446
      Likes Received
      1
      Likes Given
      4

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Mungu ibariki Africa Mungu ibariki Tanzania na sehemu yetu yote ndani ya ziwa Nyasa..!

    19. #358
      Reginald12's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th August 2012
      Posts : 166
      Rep Power : 452
      Likes Received
      65
      Likes Given
      197

      Default Re: Ni kweli kuwa Tanzania haina haki na ziwa Nyasa?

      Quote By Gamba la Nyoka View Post
      katika pekua pekua yangu nimepata kuona mahali kwamba Tanzania haina haki na ziwa Nyasa, tofauti na ziwa Tanganyika ama ziwa Victoria ambazo tunagawana maji na nchi kadhaa, lakini inasemekana kwamba Wamalawi wanadai kuwa Ziwa nyasa ambalo wao wanaliita ziwa malawi ni mali yao na mpaka halali ni ukingo wa ziwa na si ndani ya maji. je wana JF mnalionaje suala hili?

      Kuna taarifa za kusisimua humu, msimamo wa Mwalimu na Kawawa miaka ya 60. Google hiyo document.

      'The Malawi-Tanzania Boundary Dispute
      Author(s): James Mayall Reviewed work(s):Source: The Journal of Modern African Studies, Vol. 11, No. 4 (Dec., 1973), pp. 611-628Published by: Cambridge University Press

    20. #359
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Mpaka tuliokuwa nao wakati wa kupata uhuru ndio ulitambuliwa na OAU, na ndio unatambuliwa na AU. Mpaka huo uko katikati ya ziwa. It does not make sense for one country to have its border on the beach in another country. Such a border cannot be defended.

      Wakati Kamuzu Banda alipotingisha kiberiti alikuta kimejaa; na ndugu zetu wa Malawi wakaacha hiyo ishu. Sasa wametingisha tena. Je, kiberiti bado kimejaa? wakidhani hakijajaa hawataacha kung'ang'aniza.

      Tumeshatoa tamko rasmi kwamba hakuna kufanya utafiti wowote wa mafuta na gesi sehemu ambayo sisi tunajua ni yetu; na badala yake tujadiliane kwanza. Malawi imekataa rasmi kusimamisha shughuli hiyo. What is our plan B? Lazima tulipanga tutafanyaje kama wasipositisha. Sio kupigana, bali inabidi kuweka wazi kwamba ndege yote itakayoingia anga la Tanzania bila kibali itakamatwa au kutunguliwa. Tukiwa wazi kwenye hilo basi hakuna ndege itathubutu kuingia.

      Ni kichekesho kwamba unaweza ukae kwenye ufukwe wa ziwa na kila unapoogelea uanaingia nchi nyingine. We should not accept that.

      Sheria au mkataba uisiokuwa wa haki hauna nguvu. Ni kama mikataba ya 3% ya dhahabu yetu; kwa vile siyo ya haki tumedai ijadiliwe upya. Ni kama Group Areas Act za South Africa na Rhodesia zilivyokuwa hazikubaliki pamoja na kwamba zilikuwa sheria. Mikataba kati ya wakoloni ambayo sio ya haki haina nguvu. Hatuhitaji kuikubali.
      Last edited by Augustine Moshi; 20th August 2012 at 01:52.
      Kiranga likes this.
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    21. #360
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,553
      Rep Power : 5114
      Likes Received
      2603
      Likes Given
      2287

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Ziwa ni pasu kwa pasu fullstop...
      "To greed, all nature is insufficient"

    Page 18 of 29 FirstFirst ... 8161718192028 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...