Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

    Report Post
    Page 14 of 28 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast
    Results 261 to 280 of 544
    1. #1
      Mtoto wa Mkulima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2007
      Posts : 962
      Rep Power : 811
      Likes Received
      39
      Likes Given
      0

      Default Ni lake Nyasa au Lake Malawi?

      Wakubwa niwekeni sawa, nilikuwa nauliza Ziwa Nyasa ni Ziwa Nyasa au Ziwa Malawi? Na je, Kwanini Ziwa Victoria liendelee kuitwa Ziwa Victoria na si Ziwa Nyanza? Au ndio kuwaenzi watawala wetu wazungu?

      Lake Nyasa or Lake Malawi?
      The name of the lake itself is also disputed. Malawi claims the lake is named 'Lake Malawi' while international maps and other countries (most notably Tanzania) claim the name of the lake to be 'Lake Nyasa'. The origins of the dispute in the name have their background in geopolitical disputes that began prior to Malawi's independence in 1964, when it was previously known as Nyasaland.

      Further complications emerged for different political reasons in the 1960s, when the then President Banda (of Malawi) became the only African leader to establish diplomatic relations with white South Africa. This was fiercely repudiated by other African leaders, including the then President Nyerere (of Tanzania). The contrasting attitudes and policies gave further impetus to disputes between the two governments, on the name of the lake itself, and the boundary between the two countries.

      At present, the dispute between the two governments is largely dormant. Intergovernmental relations between Malawi and Tanzania are largely cordial.


      Tanzania-Malawi dispute
      The partition of the lake area between Malawi and Tanzania is disputed. Tanzania claims international borders through the lake along the lines of the borders between the German and British territories before 1914; Malawi, meanwhile, claims the whole non-Mozambican lake, including the waters next to the Tanzanian shore. The foundations of the dispute were set when the British colonial government, which had recently captured Tanganyika from Germany, put the water under the jurisdiction of Nyasaland without a separate administration for the Tanganyika portion. The dispute has led to conflicts in the past, though for several years Malawi has declined to enforce its claims to the disputed portion.

      Occasional flare-ups in in the 1990s and in recent times have impacted fishing rights, particularly of Tanzanian's who reside on the lake shore, who have occasionally been accused of fishing in Malawian waters.
      Quote By Mwawado
      Habari hiyo hata Mimi nimewahi kuisikia, hata ukiangalia Ramani ya ziwa hilo linaitwa Ziwa Malawi tofauti na hapo zamani tulipoliona kwenye ramani kama ziwa nyasa. Nashindwa kuelewa kwa dhati kama mpaka umegawanywa upya ama ndio yale yale ya kuambiwa kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.Inapaswa mipaka ya nchi yetu iwekwe wazi ili kutokuja kupoteza maeneo na Vivutio vyetu vya asili.

      Mpaka wa Tanzania na Malawi una matatizo ya muda mrefu, nakumbuka mwaka 1978 kulikuwa na kurushiana risasi kati ya Majeshi ya Tanzania na Malawi, kwa siku mbili mfululizo kulikuwa na amri ya kutokuwasha Taa katika Mji wa kyela mkoani Mbeya, Kipindi hicho nilikuwa Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa mbeya kwa Wakati Huo Mzee Richard Wambura alisema Mwl Nyerere ameamuru majeshi yetu yarudishe mapigo kama itaonekana Banda ataingiza majeshi Kyela. Serikali ya Banda ilikuwa inadai maeneo ya Matema Beach, Mto Songwe mpaka Ipinda yapo ndani ya Ardhi ya Malawi.

      Sasa inawezekana kabisa tumelitoa kwa hiyari ziwa liwe upande wa Malawi nasi tumebakiwa na Bandari tupu ya Itungi,ambayo sasa nafikiri haina hata meli moja baada ya TACOSHILI kufa.
      Quote By Gamba la Nyoka
      Kama serikali imelitoa hilo ziwa kwa Wamalawi pasipo kuhusisha maoni ya Watanzania, basi serikali inalo la kujibu. Huwezi kuwaambia wananchi waliokaa pale miaka nenda rudi eti, hayo maji usiyaguse ni ya wamalawi hayo.

      Hili suala ni lazima serikali ilitolee kauli haliwezi kuwa kimya kimya milele!
      Quote By Ruge Opinion
      Miaka ya 1970 Kamuzu Banda, rais wa Malawi, alitangaza kuwa lile ziwa lote ni la Malawi na akaanza kuwabugudhi Watanganyika waliokutwa kwenye ziwa. Nyerere akasogeza majeshi pale na kumtumia ujumbe Kamuzu aache uchokozi. Kamuzu akanywea.

      Tangu hapo hakujawahi kuwapo maelewano rasmi.

      Hilo ziwa lilikuwa linajulikana kama ziwa Nyasa kutokana na wenyeji pande zote mbili kuwa Wanyasa. Malawi vile vile ilikuwa inajulikana kama Nyasaland. Walipopata uhuru wakabadili jina na kujiita Malawi. Kwa hiyo na jina la ziwa wakalibadilisha bila makubaliano na sisi. Kwa hiyo kwao ni Ziwa Malawi na kwetu ni Ziwa Nyasa.
      Quote By kajembe
      Mgogoro huo ulianza enzi ya Kamuzu Banda alipokuwa raisi. miaka ya sitini Kamuzu alikuwa anazungumza kwenye redio yao, Malawi Broadcasting Corporation kutoka Blantyre, Malawi, na kusema ziwa lote ni la Malawi na pia wilaya ya Rungwe na hadi Mbeya ni sehemu ya Malawi.

      Kuna siku mwezi wa September 1968 Nyerere alimwita Banda ni kichaa. Alikasirika sana kwa sababu ya madai ya Mzee Kamuzu kwamba sehemu za Tanzania ni za Malawi. Alidai hata Mbamba Bay na sehemu zingine mkoani Ruvuma karibu na Ziwa Nyasa kwamba ni za Malawi. Pia alidai jimbo lote, Eastern Province, la Zambia. Kaunda alimjibu Banda na kusema ni shauri yake akitaka kuanzisha vita.

      Kabla ya mgogoro huo, Banda alikuja Tanzania na kukutana na Nyerere mwaka 1962 na kumwambia hakuna nchi ya Mozambique. Alimwambia Nyerere wagawane nchi hiyo. Alimwambia Nyerere sehemu ya kaskazini ya Mozambique, sehemu ya Wamakonde jimbo la Cobo Delgado, "ni lako" Nyerere. Ni sehemu ya Tanzania. Sehemu za Mozambique zilizobaki ni za Malawi, Rhodesia na Swaziland. Nyerere alimpuuza tu.

      Baada ya miaka michache, 1968, Kamuzu akatangaza na kusema sehemu zetu za Tanzania nilizozitaja hapo juu ni sehemu za Malawi.

      Mzee Kamuzu alikuwa ni mkorofi sana.

      CHANZO CHA MGOGORO

      Mgogoro wa ziwa umetokana na uamuzi wa wakoloni wa Kiingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao wa Nyasaland wakati walipokuwa wanatawala nchi hiyo na ilipokuwa ni British Protectorate. Walifanya uamuzi huo baada ya Wajerumani kushindwa katika vita kuu ya kwanza na Waingereza walipoichukua German East Afrika - iliyokuwa inaitwa Deutsch Ostafrika katika Kijerumani - na kuwa koloni yao ya Tanganyika. Kabla ya hapo, kutokana na makubaliano kati ya Waingereza waliokuwa watawala wa Nyasaland na Wajerumani waliokuwa watawala wa nchi yetu, mpaka wa ziwa ulikuwa kati ya ziwa. Na ndiyo mpaka huo tu ambao ni halali pamoja na jina kuitwa Nyasa, siyo Malawi.

      Uamuzi wa Waingereza kuliweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland haukubadilisha mpaka wa ziwa kihalali kwa sababu mipaka yote ya nchi zetu ilikubaliwa wakati bara letu lilipogawanywa na wakoloni. Ni mipaka hiyo ambayo hata sisi tuliikubali baada ya kupata uhuru na hakuna hata nchi moja ambayo ina haki peke yake ya kubadilisha mipaka hiyo. Hata Waingereza hawakuwa na haki ya kulikiweka Ziwa Nyasa chini ya ukoloni wao Nyasaland kwa sababu walivunja makubaliano yao na Wajerumani ambayo yalisema mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo: nusu ni sehemu ya Deutsch Ostafrika ambayo sasa ni Tanganyika, na nusu nyingine ni ya Nyasaland chini ya utawala wa Waingereza.

      Hata wilaya ya Rungwe ambayo ilijumuisha Kyela na Ileje ilikuwa inatawaliwa kutoka Nyasaland mara tu baada ya Wajerumani kushindwa vita kuu ya kwanza na Waingereza walipopewa madaraka ya kutawala nchi ambayo ilikuwa ni koloni ya Wajerumani; yaani nchi yetu ya Tanganyika.

      Deutsch Ostafrika - German East Africa - ilikuwa ni nchi tatu: Tanganyika, Ruanda na Urundi (nchi ambazo zilibadili majina na kuitwa Rwanda na Burundi mwaka 1962 baada ya kupata uhuru).

      League of Nations - jumuiya ya mataifa iliyoitangulia United Nations - iliwapa Wabeligiji Ruanda na Urundi. Koloni hizo mbili za Wabeligiji zilikuwa zinatawaliwa kutoka Leopoldville, mjii mkuu wa Belgian Congo, nchi ambayo pia ilikuwa inatawaliwa na Wabeligiji. Mpango huo ni kama vile wilaya ya Rungwe ilipowahi kutawaliwa kutoka Karonga na Waingereza waliokuwa wanatawala wa Nyasaland na baadaye kiuchukua nchi yetu ya Tanganyika kutoka kwa Wajerumani.

      Baada ya vita kuu ya kwanza, na Wajerumani kushindwa vita hiyo, waziri mkuu wa Uingereza, Lloyd George, kwenye mkutano wa League of Nations alimwambia raisi wa USA, Woodrow Wilosn, kwamba aichukue German East Africa, yaani nchi yetu, na kuiweka chini ya utawala wa Merikani baada ya Wajerumani kuipoteza nchi hiyo katika vita kuu ya kwanza. Lakini President Wilson alikataa. Angekubali, nchi yetu ingetawaliwa na USA na tungekuwa koloni ya USA. Baada ya Rais Wilson kukataa kuichukua nchi yetu, Lloyd George akakubali na kusema ataichukua Tanganyika na kuiweka chini ya utawala wa nchi yake ya Uingereza. Tuliponea chupuchupu kuchukuliwa na Wamerika. Nchi yetu ingechukuliwa na Wamerika, labda tusingepata uhuru. Wamerika wangeing'ang'ania nchi yetu kama vile walivyo ng'ang'ania nchi zingine walizochukua bila kuzipa uhuru.

      Kuhusu Ziwa Nyasa, kwa kifupi ni kwamba mpaka halali uko kati ya Ziwa. Ni mpaka ambao Wajerumani na Waingereza walikubaliana kuzigawa koloni zao: Nyasaland kuwa ya Waingereza; nchi yetu, Deutsh Ostafrika, kuwa ni ya Wajerumani. Walikubaliana kwamba mpaka wa ziwa ni kati ya ziwa hilo. Upande mmoja tu, Waingereza, hawakuwa na haki ya kubadili mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland walipolikweka ziwa hilo chini ya utawala wao Nyasaland.

      Nukuru kutoka kitabu cha Nyerere and Africa: End of an Era, ukurasa 484:

      "Dr. Banda also claimed substantial parts of Tanzania, including - Rungwe district - and the rest of Mbeya Region in southwestern Tanzania, as Malawian territory. He also claimed the entire Eastern Province of Zambia, provoking a curt response from Zambia’s president, Dr. Kenneth Kaunda, who challenged Banda to 'Go ahead and declare war on Zambia.'

      And President Nyerere dismissed Banda’s claim to large chunks of Tanzanian territory as 'expansionist outbursts, which do not scare us, and do not deserve my reply.' The outlandish claim also drew a sharp response from Nyerere who said Dr. Banda was 'insane.' But, he warned, 'Dr. Banda must not be ignored; the powers behind him are not insane.'"


      Akizungumza ktk chuo kikuu cha Dar es Salaam, November 1997, Mwalimu Nyerere alisema

      "In 1961 we became independent. In 1962, early 1962, I resigned as prime minister and then a few weeks later I received Dr. Banda. Mungu amuweke mahali pema (May God rest his soul in peace). I received Dr. Banda. We had just, FRELIMO had just been established here and we were now in the process of starting the armed struggle.

      So Banda comes to me with a big old book, with lots and lots of maps in it, and tells me, 'Mwalimu, what is this, what is Mozambique? There is no such thing as Mozambique.' I said, 'What do you mean there is no such thing as Mozambique?' So he showed me this map, and he said: 'That part is part of Nyasaland (it was still Nyasaland, not Malawi, at that time). That part is part of Southern Rhodesia, that part is Swaziland, and this part, which is the northern part, Makonde part, that is YOUR part.'

      So Banda disposed of Mozambique just like that. I ridiculed the idea, and Banda never liked anybody to ridicule his ideas.
      So he left and went to Lisbon to talk to Salazar about this wonderful idea. I don’t know what Salazar told him. That was ‘62."
      Quote By Simba mnyama
      Wana-JF,

      Mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa unaonesha ngoma bado mbichi kabisa. Hebu tusome hizi habari kutoka Malawi:

      Lake Malawi/Nyasa row: Time to show strong leadership
      By Cedrick Ngalande August 6, 2012
      At around the time of independence quite a few people in Tanzania wanted to claim a huge part of Lake Malawi or Lake Nyasa . Cool heads eventually prevailed, as most Tanzanians, including the legendary President Julius Nyerere, understood the importance of respecting boundaries emanating from colonial times. During most of Dr Kamuzu Banda’s rule, Tanzania never really pushed this crazy idea of dividing up the lake. The issue was almost forgotten during the rule of Dr Bakili Muluzi and thereafter. In fact, Dr Bingu wa Mutharika commissioned a company to start exploring oil in the lake. Tanzania said nothing at that time. Now we have a new president and all of sudden the Tanzanians are demanding that our government stop all exploration activities in the lake until all border issues have been clarified. Why now? Folks, there is a reason why we have tradition. Tradition may appear useless and outdated but it is important because it usually become established after a long experience. In politics there is what is known as ‘presidential protocol’. These are small things which over the years have proven to be niceties a president must or must not do in order to represent his/her country correctly.

      Test for President Joyce Banda to diplomatically manage the dispute on the boundary You would think some of them are not important but they are. Here are a few of them – presidents never bow for other presidents in public; presidents never escort anybody to their car; presidents walk with their arms spread outwards apparently projecting power and being in control; presidents usually put on a solid color (one color) necktie because it portrays power; when two presidents greet each other while facing the camera, each of them jostle to be on the right side so that his palm will face the camera- another sign of power, apparently; when in company of other presidents, they try to be the last one to enter the door – a fatherly gesture; there is an interesting video clip of Chairman Yassier Arafat and PM Ehud Barak jostling to be the last one to enter a room at Camp David. The sight of President George W Bush gently pushing PM Gordon Brown into Number 10 Downing Street before himself angered some British political experts. Statesmanship is a game because image is everything in international politics.

      A country’s image depends a lot on the demeanor of its leader. President Barak Obama likes to pat other leaders on their back after greeting them; you thought that was an unplanned coincidence? Just remember, how your father used to pat you on the back when you were a good boy!
      It is said that Bill Clinton failed to get a good deal at his summit with Boris Yelsin in Moscow because President Clinton having sprained his ankle arrived in Moscow on a wheelchair. The sight of a sick American president is said to have psychologically emboldened Boris Yelsin. Ghana is said to have regained its respect in West Africa when President J.J. Rawlings arrived at the 25th Organization of African Unity meeting in Togo in July 2000 in a military uniform portraying a very youthful image. The presidency is acted on a world stage. What a president says and does is very important! When Joyce Banda took over the presidency, she made it appear like Malawi will now be doing everything the donor community tells her to do. In fact some British newspapers were so pleasantly surprised with this that they called us ‘a donor fearing nation’. President Joyce Banda went to London and even bowed before Queen Elizabeth, a very strange gesture considering that both are heads-of-state. Well, all these words and actions have now collectively given an image of a weak leadership in Malawi. The world has sensed blood. Now Tanzania has decided it is time to split up the lake. Notice that they did not bring up this crazy idea when Muluzi or Mutharika were in charge. If we dignify Tanzania’s unreasonable request, one wonders what the next thing will be. Are they now going to claim Chitipa? Will Mozambique now claim Mulanje Mountain?

      Government must make clear that no part of Malawi is up for discussion – full stop! It is time to show strength. Tell Tanzania that Lake Malawi was, is and will always be Malawian. Surprisingly, after all these arrogant statements by the Tanzania government, our government’s response is at best a whimper. The minister of foreign affairs has issued a statement saying the issue will be settled ‘amicably’. Really, Mr. Minister? What could be an amicable statement? Are you planning to even dignify Tanzania’s unreasonable demand? Do you plan to divide up the lake? How can you have an amicable settlement to an
      ONE OF THE STRONGEST WEAPONS IS DIALOGUE

    2. FemaTV & Radio

    3. #261
      MkamaP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2007
      Posts : 4,675
      Rep Power : 1569
      Likes Received
      310
      Likes Given
      93

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Kama vipi waachieni ziwa lao, hii yawezekana ni strategy ya wamagharibi wameona hawawezi coz chaos kwa njia ya ndani sasa wanatumia vibaraka.

      After all, hata tukiingia vita nao hiyo cost itakayotokea hapo ni kubwa mno kuja kurudishwa na ziwa nyasa tunayopigania itakuwa zaidi ya miaka 500. Uzuri hawawezi weka border yao ufukweni ni lazima waiweke majini, kwa hiyo kuchota maji na kuiba samaki tutaiba tu kama kawaida.

      Hii pia inaweza kuwa na choko choko kutoka kwa nchi jirani za east afrika, baada ya kukataa ile pact yao ya ulinzi sasa wamepitia kule ili waje kukuambieni si tulikwambia ukakataa packt yetu ya ulinzi. Kimsingi TZ ikipigana na malawi itakuwa inapigana na nchi karibu zote za afrika mashariki. Cha msingi viongozi kama hawana treaty ya karatasi ya ku-defend tunachohitaji basi wajifanye tu kusahau waipotelezee mbali hiyo issue.

    4. #262
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,836
      Rep Power : 3272
      Likes Received
      1314
      Likes Given
      916

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Quote By MkamaP
      Kama vipi waachieni ziwa lao, hii yawezekana ni strategy ya wamagharibi wameona hawawezi coz chaos kwa njia ya ndani sasa wanatumia vibaraka.

      After all, hata tukiingia vita nao hiyo cost itakayotokea hapo ni kubwa mno kuja kurudishwa na ziwa nyasa tunayopigania itakuwa zaidi ya miaka 500. Uzuri hawawezi weka border yao ufukweni ni lazima waiweke majini, kwa hiyo kuchota maji na kuiba samaki tutaiba tu kama kawaida.

      Hii pia inaweza kuwa na choko choko kutoka kwa nchi jirani za east afrika, baada ya kukataa ile pact yao ya ulinzi sasa wamepitia kule ili waje kukuambieni si tulikwambia ukakataa packt yetu ya ulinzi. Kimsingi TZ ikipigana na malawi itakuwa inapigana na nchi karibu zote za afrika mashariki. Cha msingi viongozi kama hawana treaty ya karatasi ya ku-defend tunachohitaji basi wajifanye tu kusahau waipotelezee mbali hiyo issue.
      Hiyo tabia ya watanzania kukubali yaishe ndiyo imefanya Tanzania isiendelee kwani viongozi wamekuwa wakiiba mali za umma au kuuza raslimali za nchi kwa kujua kuwa watu watapiga kelele kidogo tu na baadaye watakubali yaishe na kuniacha ninakula nilichoiba!!! Tulisikia kelele za Loliondo miaka ya tisini lakni leo takribani miaka 20 bado waarbu wanapakia Twiga kwenda uarabuni sisi tulishakubali yaishe.
      Mkandara likes this.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    5. #263
      Ndoano's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th August 2011
      Posts : 172
      Rep Power : 428
      Likes Received
      25
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By MkamaP
      Kama vipi waachieni ziwa lao, hii yawezekana ni strategy ya wamagharibi wameona hawawezi coz chaos kwa njia ya ndani sasa wanatumia vibaraka.

      After all, hata tukiingia vita nao hiyo cost itakayotokea hapo ni kubwa mno kuja kurudishwa na ziwa nyasa tunayopigania itakuwa zaidi ya miaka 500. Uzuri hawawezi weka border yao ufukweni ni lazima waiweke majini, kwa hiyo kuchota maji na kuiba samaki tutaiba tu kama kawaida.

      Hii pia inaweza kuwa na choko choko kutoka kwa nchi jirani za east afrika, baada ya kukataa ile pact yao ya ulinzi sasa wamepitia kule ili waje kukuambieni si tulikwambia ukakataa packt yetu ya ulinzi. Kimsingi TZ ikipigana na malawi itakuwa inapigana na nchi karibu zote za afrika mashariki. Cha msingi viongozi kama hawana treaty ya karatasi ya ku-defend tunachohitaji basi wajifanye tu kusahau waipotelezee mbali hiyo issue.
      nina wasiwasi na uraia wako.

    6. #264
      Lawrence Luanda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th November 2011
      Posts : 604
      Rep Power : 499
      Likes Received
      51
      Likes Given
      0

      Default Re: Ni kweli kuwa Tanzania haina haki na ziwa Nyasa?

      Quote By Mtanzania
      Hakuna mgogoro wa mpaka Tanzania na Malawi-Serikali

      Na Mwandishi Wetu,Dodoma

      NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rita Mlaki, aliliambia Bunge jana kuwa hakuna mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi unaosababishwa na Ziwa Nyasa.

      Alisema wameshakaa vikao mara mbili na viongozi wa serikali ya Malawi kuzungumzia kuhusu mipaka na kuridhika kuwa hakuna tatizo hilo kati ya nchi hizo.

      Waziri Mlaki alisema wanatarajia kukaa kikao cha tatu ili kupata tafsiri ya namna mipaka inavyogawanywa katika maeneo ya ziwa na bahari.

      Alikuwa kijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mkwajuni (CCM), Mzee Ngwali Zuberi, aliyetaka kujua lini serikali za Tanzania na Malawi zitakaa kutatua tatizo la mipaka kati ya nchi hizo.

      Swali hilo lilitokana na swali la msingi la Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kwa Waziri wa Maji, aliyetaka kujua serikali imeshindwaje kunadi jina la Ziwa Nyasa ili kuondoa utata wa Malawi inayodai kuwa ziwa hilo lote ndani ya nchi yao.

      Naibu Waziri wa Maji, Shamsa Mwangunga akijibu swali la Mbunge Nyalandu alisema Tanzania ina uhusiano mzuri na Malawi kwa muda mrefu na kwamba ahaina mgogoro kuhusu ziwa hilo.

      Hata hivyo, alikiri kuwa sheria za wakati wa wakoloni ndiyo chimbuko la Ziwa Nyasa na kwamba mkataba wa Anglo German ulibainisha kwamba ziwa hilo ni milki ya Malawi kinyume na taratibu za sasa za mipaka inayopita majini, inayotoa fursa sawa kwa nchi zinazotenganishwa kwa ziwa au bahari, kwamba mpaka upitie katikati ya ziwa au bahari husika.

      Alisema Tanzania na Malawi zinaendelea kutumia ziwa hilo kwa shughuli za kila siku bila ya mgogoro wa aina yoyote na pia zinaendelea kubuni miradi ya pamoja ya kuendeleza Bonde la Ziwa Nyasa.
      Utamaduni wa kujibu maswali kwa mazoea unaletaga mkanganyiko kama huu........haiitaji uwe profesor kujua kuna mgogoro wa mipaka kati yetu na Malawi. kipi ni kipi kati ya Membe anayesema Taifa liko tayari kwa vita au hawa mawaziri........


    7. #265
      MkamaP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2007
      Posts : 4,675
      Rep Power : 1569
      Likes Received
      310
      Likes Given
      93

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Quote By Kichuguu
      Hiyo tabia ya watanzania kukubali yaishe ndiyo imefanya Tanzania isiendelee kwani viongozi wamekuwa wakiiba mali za umma au kuuza raslimali za nchi kwa kujua kuwa watu watapiga kelele kidogo tu na baadaye watakubali yaishe na kuniacha ninakula nilichoiba!!! Tulisikia kelele za Loliondo miaka ya tisini lakni leo takribani miaka 20 bado waarbu wanapakia Twiga kwenda uarabuni sisi tulishakubali yaishe.
      Hiyo unayoongelea ni tofauti kidogo, kama umenisoma vizuri tangu mwanzo, ni kuwa tuchukue facts zetu tusonge mahakamani tukishindwa huko, basi issue tuipotezee kupigana vita saizi sio viable soln. Hilo ziwa, halina thamani kama thamani tutakayopoteza kwa vita hiyo.

      Kuna mataifa yanaipigia jaramba TZ kuhakikisha wanachukua mali bure kabisa ama wanawakalia kwa mabavu. Ama kwa namna nyingine wanarudisha ukoloni kwa mabavu angalia walivyofanya Libya, Iraq, afghan, na sasa Syria wanaunga kwa nguvu zote wahasi tena hadharani.

      Angalieni DRC Congo jinsi ka-nchi kadogo kama Rwada kalivyo i-distablize Congo. Ile vita ya Rwanda na Burundi was very well calculated. MAlengo yalikuwa congo, sema wanyarwanda na warundi wakaingia mkenge wakalianzisha wao kwa wao, lengo lilikuwa tu kuipindua hizo serikali harafu hao puppeti wao wai-vamie congo. Unafikiri rwanda kama rwanda wangeisumbua DRC mpaka leo? kuna vigogo wanaochota uranium kule.

      Mkipigana vita, mkashindwa anayeshinda anawakalia kwa mabavu, labda awe na roho njema kama ya Nyerere kuwaachia. Na ni just rule of thumb, ya kwamba tikipigana mataifa makubwa yote na jirani wote watai-support Malawi ili malawi washinde waje wachote mali zenu kwa nguvu na kuwakalia kwa mabavu maana ni TZ kuna mali nyingi sana.

      Ni rule of thumb hiyohiyo, tukipigana na malawi hakuna taifa litakalo i-support TZ kwa sababu ya uki apply ile hesabu ya differential equations unaona dhairi ya kwamba mataifa ya ki-support Tanzania na wakaishinda malawi kule malawi wataenda kuchuma nini?
      Kuweni makini ndugu zangu, heri nusu shari kuliko shari kamili.
      Last edited by MkamaP; 8th August 2012 at 13:02.

    8. Miaka 50

    9. #266
      Byendangwero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 832
      Rep Power : 601
      Likes Received
      28
      Likes Given
      0

      Default Utatuzi wa mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tz huko mikononi mwa watawala wetu

      Kumekuwepo na kauli nyingi juu ya namna nzuri ya kushughulikia mgogoro wa mpaka unaofukuta hivi sasa, kati ya Tanzania na Malawi. Kwa maoni yangu, mgogoro wa mpaka kati ya nchi hizi mbili hauwezi kutatuliwa bila ya kushirikisha watawala wa zamani wa nchi hizi mbili: Ikumbukwe kulingana na msimamo wa umoja wa Afrika, nchi zote za Afrika zinatakiwa kuendelea kuheshimu mipaka zilizoridhishwa kutoka kwa wokoloni. Kama hivyo ndivyo, ni nchi ya uingereza tu ambayo ndiyo yenye turufu katika kuupatia ufumbuzi mgogoro huu. Swali la kujiuliza ni kwanini watawala wetu wa sasa badala ya kutumia njia hiyo kutatua mgogoro huo haraka, wamekuwa wakijikita katika kutoa kauli zenye mahudhui ya kuukuza mgogoro wenyewe. Baadhi ya wachambuzi wa siasa wanaelezea hali hiyo kuwa inatokana na mifarakano iliyopo sasa hapa nchini mwetu; Kwa mujibu wa wachambuzi hao, kuibuka kwa mgogoro huo wa mpaka kati ya malawi na Tanzania, kumewapa fursa watawala wetu ya kuwalaghai wananchi kusahau tofauti zao, na badala yake kuungana pamoja kutetea mipaka ya nchi yao; katika hali hiyo, wanasiasa hao watafanya kila linalowezekana kuhakikisha mgogoro huo haupatiwi ufumbuzi wa haraka.

    10. #267
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,836
      Rep Power : 3272
      Likes Received
      1314
      Likes Given
      916

      Default Re: Ni kweli kuwa Tanzania haina haki na ziwa Nyasa?

      Quote By Mtanzania
      Hakuna mgogoro wa mpaka Tanzania na Malawi-Serikali

      Na Mwandishi Wetu,Dodoma

      NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rita Mlaki, aliliambia Bunge jana kuwa hakuna mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi unaosababishwa na Ziwa Nyasa.

      Alisema wameshakaa vikao mara mbili na viongozi wa serikali ya Malawi kuzungumzia kuhusu mipaka na kuridhika kuwa hakuna tatizo hilo kati ya nchi hizo.

      Waziri Mlaki alisema wanatarajia kukaa kikao cha tatu ili kupata tafsiri ya namna mipaka inavyogawanywa katika maeneo ya ziwa na bahari.

      Alikuwa kijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mkwajuni (CCM), Mzee Ngwali Zuberi, aliyetaka kujua lini serikali za Tanzania na Malawi zitakaa kutatua tatizo la mipaka kati ya nchi hizo.

      Swali hilo lilitokana na swali la msingi la Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kwa Waziri wa Maji, aliyetaka kujua serikali imeshindwaje kunadi jina la Ziwa Nyasa ili kuondoa utata wa Malawi inayodai kuwa ziwa hilo lote ndani ya nchi yao.

      Naibu Waziri wa Maji, Shamsa Mwangunga akijibu swali la Mbunge Nyalandu alisema Tanzania ina uhusiano mzuri na Malawi kwa muda mrefu na kwamba ahaina mgogoro kuhusu ziwa hilo.

      Hata hivyo, alikiri kuwa sheria za wakati wa wakoloni ndiyo chimbuko la Ziwa Nyasa na kwamba mkataba wa Anglo German ulibainisha kwamba ziwa hilo ni milki ya Malawi kinyume na taratibu za sasa za mipaka inayopita majini, inayotoa fursa sawa kwa nchi zinazotenganishwa kwa ziwa au bahari, kwamba mpaka upitie katikati ya ziwa au bahari husika.

      Alisema Tanzania na Malawi zinaendelea kutumia ziwa hilo kwa shughuli za kila siku bila ya mgogoro wa aina yoyote na pia zinaendelea kubuni miradi ya pamoja ya kuendeleza Bonde la Ziwa Nyasa.
      Mawaziri wetu nao ni bure kabisa, na nina wasiwasi kuwa hawa watashindwa kujenda hoja kuhusu maji yale.

      Nimeshaandika hapa mara nyingi sana kuwa katika mkutano wa berlini; Ziwa Nyasa lilikuwa ni sehemu ya eneo huru la kibiashara ikiwa ni pamoja na mito mikubwa yote iliyoko kwenye eneo la bonde la kongo, na mto Zambezi. Mkataba huo wa Heligo haukubadilisha article ya kwanza ya mkutano wa Berlin kuhusu hiyo free zone. Mkataba ulibainisha kuwa Ujerumani itaishia Mashariki mwa Ziwa, lakini haukusema kuwa ziwa lile litakuwa chini ya Uingereza. Hata wakati mfalme wa uingereza alipotuma gavana wake wa kwanza kwenda Malawi, alimpa order kuwa eno lake ni lile lililoko magharibi mwa ziwa Nyasa hakusema kuwa ni Ziwa Nyasa pamoja na eneo lote liliko magharibi yake.

      Wakati wa vita waingereza walilitumia ziwa lile kuwashambulia wajerumani na kuanzia hapo wakaanza kulimiliki na kuhamishia mpaka wao hadi upande wa mashariki mwa ziwa kinyume cha makubaliano yote ya nyuma kuhusu uhuru wa kutumia ziwa hilo na ile mito ya ya kwenye bonde la Kongo. Iwapo mpaka huo ungehamishwa kwenye nchi kavu (kama ambavyo rwanda na Burundi zilivyoondeolewa kwenye Germani East Africa, kusingekuwa na tatizo kabisa leo, lakini kuhamisha mpaka kwenda kwenye ufukwe wa ziwa ni kinyume cha sheria zote zinazohuzu maji ya asili; Tanzania wana haki zote katika swala hili.

      Inabidi viongozi wetu wawe na akili ya kusoma na kuelewa mikataba kwa makini. Swala hili siyo la kusema tuongee waturuhusu tutumie maji yale; kunataka wasiingie kwenye kipande chetu cha halali.
      Mkandara likes this.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    11. #268
      chambilino's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 3rd July 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      2

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      I believe that every creature in this mother world likes to live,peacefully and with hope. We African Brothers (Malawi & Tanzania) in a number of years we have common understanding and good relationship,why becoming eager to fight?? Is this a real solution to solve the problem raised over Lake Nyasa a.k.a Lake Malawi?? I do wonder some Malawians and my fellow Tanzanians are commenting here and being happy if war against each other is breaking!! This is non sense from senseless people..!! None of you who can real tell the truth who will benefit from this war…we have to think of the poor ..women..children..etc. If things become worse in one side(it can be TZ or MLW),JB or JK will flee to the foreign country.…leaving the poor ones suffering from this tragedy.It is true that most of African leaders nowadays are doing things for their own benefits,we TZnians and MLWians we have to think thrice who will benefit from the Lake Resources….obvious those who will have positions and close look on Production and sales…the poors will have a very very small parcentages you can’t tell. Most of those who comments here am sure are those who are falling in the group of the marginalised..the poors,those who do not have a chance of smelling of our nations’ cakes(Wealth). I Suggests that we Tanzanians and Malawians if the War breakes over this issues Let us demonstrate to Stop it..!! Guys in LLW and DAR we can do this… Also as some one commented we can not loose if we share the benefit of the lake together,we as brothers. The Wazungus have already confused us with their Treaties,most of them for their own benefits and not for ours. I am also disappointed with the Journalists and news reporters over this issue..they are also “Fans” of war. Some are telling us that TZ has already sent troops to the border…this is intimidating people they must be sure of what they are writing…I hope our leaders will compromise on the issue wisely. GOD Bless Africa

    12. #269
      Kituko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th January 2009
      Posts : 3,706
      Rep Power : 1286
      Likes Received
      489
      Likes Given
      173

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Great Thinker nngu007....................... .. shukrani sana,.....................hilo kalablasha umelipata wapi tena?......................... .............kaaazi kwelikweli,

    13. #270
      MkamaP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2007
      Posts : 4,675
      Rep Power : 1569
      Likes Received
      310
      Likes Given
      93

      Default Re: Ni kweli kuwa Tanzania haina haki na ziwa Nyasa?

      Quote By Kichuguu
      Mawaziri wetu nao ni bure kabisa, na nina wasiwasi kuwa hawa watashindwa kujenda hoja kuhusu maji yale.

      Nimeshaandika hapa mara nyingi sana kuwa katika mkutano wa berlini; Ziwa Nyasa lilikuwa ni sehemu ya eneo huru la kibiashara ikiwa ni pamoja na mito mikubwa yote iliyoko kwenye eneo la bonde la kongo, na mto Zambezi. Mkataba huo wa Heligo haukubadilisha article ya kwanza ya mkutano wa Berlin kuhusu hiyo free zone. Mkataba ulibainisha kuwa Ujerumani itaishia Mashariki mwa Ziwa, lakini haukusema kuwa ziwa lile litakuwa chini ya Uingereza. Hata wakati mfalme wa uingereza alipotuma gavana wake wa kwanza kwenda Malawi, alimpa order kuwa eno lake ni lile lililoko magharibi mwa ziwa Nyasa hakusema kuwa ni Ziwa Nyasa pamoja na eneo lote liliko magharibi yake.

      Wakati wa vita waingereza walilitumia ziwa lile kuwashambulia wajerumani na kuanzia hapo wakaanza kulimiliki na kuhamishia mpaka wao hadi upande wa mashariki mwa ziwa kinyume cha makubaliano yote ya nyuma kuhusu uhuru wa kutumia ziwa hilo na ile mito ya ya kwenye bonde la Kongo. Iwapo mpaka huo ungehamishwa kwenye nchi kavu (kama ambavyo rwanda na Burundi zilivyoondeolewa kwenye Germani East Africa, kusingekuwa na tatizo kabisa leo, lakini kuhamisha mpaka kwenda kwenye ufukwe wa ziwa ni kinyume cha sheria zote zinazohuzu maji ya asili; Tanzania wana haki zote katika swala hili.

      Inabidi viongozi wetu wawe na akili ya kusoma na kuelewa mikataba kwa makini. Swala hili siyo la kusema tuongee waturuhusu tutumie maji yale; kunataka wasiingie kwenye kipande chetu cha halali.
      Mkuu
      Umeongea vizuri, lakini ktk hii issue hatuishii kuongea vizuri tu, bali na kwa kuweka fact. Wengine hapa hatuna ujuzi wa historia ama sheria bali tuna emulate kitu kilichowekwa mezani. Kuna wadau hapa wameshatuwekea sijui treaty ya mwaka 1891 na inasema tanganyika inaishia kwa ufukwe wa ziwa. Sasa ingekuwa nyema kama waweza utuwekee hiyo docs inayosema na malawi nayo inaishia kwa ufukwe.

      Nafikiri utakuwa umesaidia zaidi, tusisubiri viongozi, mara nyingi sisi tusio viongozi tuna uelewa wa mambo zaidi ya viongozi, maana hawa viongozi wamepeana kifisadi. Wasaidia kwa hiyo doc ili wamalawi wakifuata doc zao uingereza sie tufuate docs ujerumani.

    14. #271
      luogajunior's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 5th August 2012
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      1

      Default Re: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

      Jamani watanzania wenzangu tusifanye mchezo na hili suala la mipaka muhimu ya inchi yetu..tukumbuke matatizo yanayowapata wenzetu wa israel na palestina ni mambo haya haya ya nani anastahili kupata nini..tuchukue muda wa kutosha kupata ukweli wa hili jambo na hasa wenzetu mliobobea kwenye haya mambo mtupe mwongozo basi.

    15. #272
      Jose M's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd February 2011
      Posts : 23
      Rep Power : 424
      Likes Received
      3
      Likes Given
      4

      Default Re: Ni kweli kuwa Tanzania haina haki na ziwa Nyasa?

      Sio kweli, hakuna vimisaada hata chembe. mbona CCM government inapewa misaada?

    16. #273
      PISTO LERO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2011
      Posts : 829
      Rep Power : 0
      Likes Received
      132
      Likes Given
      1

      Default Hii ndiyo mipaka ya ziwa Nyasa (tuijadili kwa manufaa ya taifa)

      Ramani hizi ni kabla ya mwaka 1993

      kwa mawazo yangu ziwa hili lipo malawi watanzania tuache ubabe.hii vita inayo lazimishwa ni kwa maslahi ya watu flani watanzania tuamke tusikabithi akili zetu kwa benard membe na lowasa hawa wanajua watakachokipata katika vita hii ndiyo maana wanaikazania.
      Attached Thumbnails      
      Last edited by PISTO LERO; 8th August 2012 at 17:29.
      Nikupateje likes this.

    17. #274
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,417
      Rep Power : 5038
      Likes Received
      782
      Likes Given
      1788

      Default re: Hii ndiyo mipaka ya ziwa Nyasa (tuijadili kwa manufaa ya taifa)

      Ikague tena thread yako mkuu!!
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    18. #275
      mosagane's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th July 2012
      Posts : 120
      Rep Power : 368
      Likes Received
      24
      Likes Given
      3

      Default re: Hii ndiyo mipaka ya ziwa Nyasa (tuijadili kwa manufaa ya taifa)

      hii thread hapo ndo imekamilika au mimi ndo siielewi?

    19. #276
      Polisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,529
      Rep Power : 736
      Likes Received
      357
      Likes Given
      233

      Default re: Hii ndiyo mipaka ya ziwa Nyasa (tuijadili kwa manufaa ya taifa)

      Mkuu, mimi nimeliona hili. Hii ni strategy ya watu wanaotafuta urais. Vita inaunganisha sana watu. Kwa hiyo atakayekuwa mstari wa mbele, ataonekana kama mtu mzalendo sana. Nadhani utakuwa umeshaona upepo tayari sasa hivi
      Nikupateje likes this.

    20. #277
      PISTO LERO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2011
      Posts : 829
      Rep Power : 0
      Likes Received
      132
      Likes Given
      1

      Default re: Hii ndiyo mipaka ya ziwa Nyasa (tuijadili kwa manufaa ya taifa)

      Hii diyo mppaka yenyewe samahanini kwa usumbufu
      Attached Thumbnails    

    21. #278
      mkataba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 147
      Rep Power : 375
      Likes Received
      35
      Likes Given
      4

      Default re: Hii ndiyo mipaka ya ziwa Nyasa (tuijadili kwa manufaa ya taifa)

      iko wapi iyo mipaka .......????????/

    22. #279
      mkataba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 147
      Rep Power : 375
      Likes Received
      35
      Likes Given
      4

      Default re: Hii ndiyo mipaka ya ziwa Nyasa (tuijadili kwa manufaa ya taifa)

      Quote By T.2015.CDM
      Hii diyo mppaka yenyewe samahanini kwa usumbufu
      Hawa akina Lowasa wanajitafutia umaarufu kwa karamu ya watu only, sasa hata hio Tanganyika apo wanatafuta nini zaidi ya ugomvi na Malawi. Waambie wakimaliza kuuwaa watu wa Malawi tunawasubiri huko The Heig.
      Nikupateje likes this.

    23. #280
      Sheba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 199
      Rep Power : 553
      Likes Received
      83
      Likes Given
      34

      Default

      Quote By T.2015.CDM
      Ramani hizi ni kabla ya mwaka 1993

      kwa mawazo yangu ziwa hili lip0 malawi watanzania tuache ubabe.hii vita inayo lazimishwa ni kwa maslahi ya watu flani watanzania tuamke tusikabithi akili zetu kwa benard membe na lowasa hawa wanajua watakachokipata katika vita hii ndiyo maana wanaikazania.
      Nashauri msubiri CHADEMA iingie madarakani ndio mkubali mpaka wa pwani.

    Page 14 of 28 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...