Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

    Report Post
    Page 2 of 14 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 279
    1. #1
      Mohamedi Mtoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Location : Lushoto - Kwemakame.
      Posts : 2,209
      Rep Power : 24584
      Likes Received
      3374
      Likes Given
      367

      Default Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Kauli hii iko kwenye ukurasa wake wa twitter.

      "Kwa masaa 3 nimejieleza mbele ya sekretariat ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa katibu Mkuu".

      Amekiomba chama kifanye uchunguzi juu yake na kuchukua hatua akibainika.
      Quote By Mdakuzi
      Kupitia akaunti yake ya Twitter, naibu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni ameweka wazi nia yake ya kuelezea kila kitu kuhusiana na tuhuma za rushwa dhidi yake, atakapofanya mkutano na waandishi wa habari kesho saa tano asubuhi kwenye ofisi za Bunge za jijini Dar.

      Zitto Kabwe: Kesho Nitazungumza na waandishi wa Habari ofisi za Bunge Dar Es Salaam kuanzia saa tano asubuhi. Kuendelea kukaa kimya ni silaha kwa adui.
      Updates toka magazetini July 31, 2012

      Mwananchi:

      Zitto ahojiwa kwa rushwa!

      SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.

      Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.

      Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.

      Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.

      Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.

      “Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Twitter.

      Lissu ataja wengine
      Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.

      Wabunge wengine watatu tumeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.

      Katika orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo kujinufaisha.

      “Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama hawahusiki,” alisema Lissu na kuendelea:

      “Ila uchunguzi wetu umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma.”

      Lissu alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo wana mgongano wa kimaslahi.

      Alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50.

      “Nasir Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta,” alisema na kuendelea;

      "....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo. Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini.”

      “Hawa ndiyo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi. Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi.”

      Lissu alisema kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na ni kinyume na maadili ya kibunge.

      Katika hatua nyingine Lissu amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema nazo zina madudu mengi.

      “Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe, uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili haki itendeke,” alisema.

      Alipoulizwa Chadema imefanya nini dhidi ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: “Nikiri kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo.”

      “Katika hili tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo.”

      Majibu ya tuhuma
      Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi.

      “Nimekuja bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (Chadema).”

      Kwa upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo.

      "Siyo kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla. Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10 kuhusu masuala hayo ya petroli,” alisema

      Aliishauri kambi hiyo ya upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

      Awali, Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu. Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki vituo vya mafuta.

      Kamata kwa upande wake alisema: “Kuna kamati maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli mtaujua, haraka ya nini?.

      Mjadala Bungeni
      Mjadala huo wa wabunge kuhusishwa na mgongano wa kimaslahi ulianza kulipuka bungeni jana asubuhi baada ya wabunge watatu; Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Salum Barwany (Lindi Mjini) na Mbunge wa Nkasi Kaskazni, Ali Kessy kutaka wabunge wanaotuhumiwa kwa ufisadi watajwe bungeni ili kuisafisha taasisi hiyo ya kutunga sheria.

      "Mheshimiwa Naibu Spika juma lililopita Mheshimwa (Vita) Kawawa alitoa hoja kutaka suala la ufisadi lishughulikiwe kwa kuvunjwa Kamati ya Madini na Spika akaridhia na kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Maadili. Kwa nini Kamati nyingine zilizohusishwa na ufisadi huo nazo zisivunjwe?” alihoji Nassari na kuendelea:

      “Kuna Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Mrema na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto. Kuna tabia ya wabunge kuzikimbia kamati zisizokuwa na mikataba kama Kamati ya Huduma za Jamii na wanazikimbilia kamati zenye mikataba.”

      Barwany alitaka Bunge litajiwe majina ya wabunge waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo mpaka wakapelekwa kwenye Kamati ya Maadili, akieleza kuwa hili litasaidia kulisafisha... “Tumeambiwa Kamati ya Maadili inajadili suala hilo, lakini hatujatajiwa ni wabunge gani waliopelekwa huko, tunaomba mtutajie ili Bunge lijisafishe.”

      “Mimi naungana na wazo la Barwany na Nassari. Majina yatajwe wabunge tunadhalilishwa na wananchi huko mitaani. tuwataje hadharani,’ alisema Kessy.

      Akitoa mwongozo wa hoja hiyo, Ndugai aliiagiza Kamati ya Uongozi ya Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge ili wakajadili suala hilo na baadaye apelekewe taarifa.

      “Naamini wenyeviti wote wa kamati mmo humu ndani, naomba sasa hivi mwende kwenye Ukumbi wa Spika mkajadili suala hilo halafu nipate majibu sasa hivi,” alisema.

      Baadaye jioni, Ndugai alisema kuwa Spika hawezi kuwataja kwa majina wabunge ambao wanajihusisha na rushwa kwa kuwa hawajui.

      Alisema Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana ilikubaliana kuwa ufanyike uchunguzi wa kina kwa ajili ya kuwabaini wale wanaoshukiwa na kwamba ikibainika Bunge litawaanika hadharani.

      “Kamati imerejea kumbukumbu za hansard ya Jumamosi kuwa ufanyike uchunguzi wa kina juu ya jambo hilo na wabunge mtaitwa kwa ajili ya kutoa ushirikiano, ikumbukwe kuwa mbunge akiitwa siyo kwamba ndiyo amekuwa mtuhumiwa, bali pale itakapothibitika majina yatawekwa hadharani,’’ alisema Ndugai.

      Naibu Spika alitahadharisha kuwa ndani ya Kamati hiyo utafanyika uchunguzi wa kutosha kubaini kama kuna mjumbe mwenye maslahi kwa wale wahusika basi ataondolewa ili kutoa nafasi kwa kamati kufanya kazi yake ipasavyo.

      Aliwatahadharisha wabunge kuwa Kamati hiyo haitaingilia utaratibu wa vyombo vya dola ambao wamekuwa wakiufanya ikiwemo wa Takukuru wa kuwahoji baadhi ya wabunge.


    2. #21
      Tata's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2009
      Posts : 2,369
      Rep Power : 958
      Likes Received
      521
      Likes Given
      333

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Zitto is innocent until proved guilty.
      LORDVILLE likes this.

    3. #22
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 4,061
      Rep Power : 1239
      Likes Received
      257
      Likes Given
      41

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Zitto anatisha moja wa vijana mwenye kusimamia anachokiamini na kinachomtesa Sasa ni hiyo misimamo Yake believe me

    4. #23
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,714
      Rep Power : 988
      Likes Received
      598
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By Father of All
      Kwa tabia yake ya undumila kuwili Zitto hawezi kuponyoka. Kama kweli anamilki Hummer na magari mengine kama ilivowahi kuripotiwa kuwa alimsadia magari Kafulila kwenye kampeni, Zitto ni fisadi hakuna shaka. Kinachofurahisha kwenye mchezo huu wa kuvuana nguo, hakuna fisi atayenusurika kutokana na ukweli kuwa hata hao wanaowashutumu wenzao hawafanyi hivyo kwa uzalendo bali visasi vya kuzuiwa kuliibia shirika la Umeme. Mhando si wa kwanza. Dr Idris Rashid aliiba sana ukiachia mbali familia na shemeji za Mkapa waliotumia Net Group Problems kulimaliza kabisa shirika letu.Bado serikali ambayo huwa halipii umeme inaotumia. Msururu ni mrefu kama uchunguzi wa kina utafanyika.
      mkuu kwa hiyo mafisi yanagombea mzoga?

    5. #24
      Jile79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2009
      Posts : 3,848
      Rep Power : 1285
      Likes Received
      227
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By narubongo
      dr slaa ni mmoja wa wanaosemekana kuusaka urais 2015
      je zitto ana imani dr slaa kuongoza sekretarieti? Ukizingatia wanaomchafua zitto ni wabunge wapenda posho na wasaka urais kutoka vyama vyote
      kwani yeye zitto atake posho za nini wkt mafisadi wamemuwezesha?....tuulize sisi tunaomjua zitto in and out sio nyie mnaomuona mbele ya vyombo vya habari...zitto is a dangerous person bora hata kikwete

    6. #25
      Muggssy's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th August 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 70
      Rep Power : 516
      Likes Received
      10
      Likes Given
      18

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By measkron
      Aeleze na Ndege ya TANAPA yeye huwa anaitumia kama nani na kwa mamlaka yapi? Kama mwenyekiti Wa kamati ya Bunge ya Mahesabu ya mashirika ya umma ataweza kukagua TANAPA kwa haki? Zitto ni fisadi, aeleze Gari aliyopewa na Nimrod Mkono na huo mshahara anaolopwa na Rostam Azizi ni kwa kazi ipi.
      Tukubali tukatae zitto anatumika ku distabilise Chadema kumbuka wakati wa kampeini kule Arumeru watu wako kwenye battle field dakika za lalasalama nakumbuka zilikua zimebaki siku mbili tuu anaibuka na hoja ya kugombea uraisi ili ahamishe ajenda kuu ya kampeini thank God kwa busara ya Dr. Slaa alivo uliza juu ya kauli ile ya Zitto alisema hawezi kuzungumzia upuzi maana ajenda iliyopo ni Nasari kuingia bungeni. Ila kwa hili kapatikana na mengine yatafumuka hata mama yake mzazi aliwahi kukiri hadharani kwamba mwanae anatumiwa


    7. #26
      busar's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2011
      Posts : 353
      Rep Power : 448
      Likes Received
      40
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By mamajack
      zito ni mbunge makini,the issue is anajichanganya sana na mambo mengi ya kipuuzi mara mafisadi,mara bongo movie,mara urais.i stated onde before,zito turudishie zitto wetu yule mzalendo mwenyekuweka maslai ya taifa mbele anayebeba sura ya tanzania yenye haki.please zitto what is happening,mbona kila siku wewe kwa mabaya tu??usiniambie ni wanakusingizia maana hata kipofu atakushangaa,actually ni lazima tusemwe ili tujue udhaifu wetu,lakini si kila linalisemwa ni kweli,but ni wajibu wetu kujichunguza na kubadilika.
      jitathimini brother!mchango wako unahitajika kuijenga nchi hii.
      Duh, unamahaba ya that na mpiganaji Zito Z. Kabwe

    8. #27
      Nyakageni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2011
      Posts : 5,543
      Rep Power : 1603
      Likes Received
      816
      Likes Given
      52

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      God bless Chadema!

    9. #28
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Game Reserve
      Posts : 8,318
      Rep Power : 12079
      Likes Received
      5545
      Likes Given
      5385

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By Mohamedi Mtoi
      Kauli hii iko kwenye ukurasa wake wa twitter.

      "Kwa masaa 3 nimejieleza mbele ya sekretariat ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa katibu Mkuu".

      Amekiomba chama kifanye uchunguzi juu yake na kuchukua hatua akibainika.
      Nadhani huu ni uamuzi wa busara sana badala ya kusubiri maneno yazidi kukua ni vizuri kumaliza udhia mapema.
      Nadhani sasa sekretariati imepata mengi kutoka kwake na hivyo kuinufaisha sana kamati kuu itakapokutana kwa ajili ya kutafakari tuhuma hizo dhidi yake.

      Narudia tena kumshauri kamanda Zitto ajiepushe na tabia ya kupenda kuwa msemaji wa kila kitu kinachojitokeza mbele yake, afanye hivyo pale anapolazimika tu. Kama anajitambua kwamba yeye ni "presidential hopeful" lazima ajilinde kwa kauli na matendo yake. Hii vita baridi ccm wanayopigana nae yeye hajaijua kwakuwa wamekuwa wakimpamba na yeye akaanza kujisahau kumbe walikuwa wanamlia timing wammalize.
      Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

    10. #29
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,448
      Rep Power : 2485
      Likes Received
      970
      Likes Given
      385

      Default

      Quote By Alfred Daud Pigangoma
      Kilaza wa jimbo la Tabora, Rage mzee wa bastora ameomba muongozo wa spika kuwa kwa nini Mh. Tundu Lissu kataja majina ya wabunge wala rushwa wa CCM pekee na ameacha wa CHADEMA. Sasa anataka muongozo ili na Zitto atajwe.
      Nae si ataje kama anakithibitisho kama Lisu?

    11. #30
      mgashi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 227
      Rep Power : 408
      Likes Received
      61
      Likes Given
      3

      Default

      Quote By mamajack
      zito ni mbunge makini,the issue is anajichanganya sana na mambo mengi ya kipuuzi mara mafisadi,mara bongo movie,mara urais.i stated onde before,zito turudishie zitto wetu yule mzalendo mwenyekuweka maslai ya taifa mbele anayebeba sura ya tanzania yenye haki.please zitto what is happening,mbona kila siku wewe kwa mabaya tu??usiniambie ni wanakusingizia maana hata kipofu atakushangaa,actually ni lazima tusemwe ili tujue udhaifu wetu,lakini si kila linalisemwa ni kweli,but ni wajibu wetu kujichunguza na kubadilika.
      jitathimini brother!mchango wako unahitajika kuijenga nchi hii.
      Kama kukusikia amekusikia abakize utekelezaji tu, namuomba zitto baada ya hii inshu kupita ajirekebishe kuna kitu atakuwa amejifunza kwani bado tunamuhitaji sana kwa ukombozi wa taifa letu. Rudi kundini kaka anza kusambaza M4C kama zamani.

    12. #31
      Mdakuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 286
      Rep Power : 420
      Likes Received
      54
      Likes Given
      12

      Default Zitto Kabwe aamua kuvunja ukimya juu ya Tuhuma za Rushwa dhidi yake!

      Kupitia akaunti yake ya Twitter, naibu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni ameweka wazi nia yake ya kuelezea kila kitu kuhusiana na tuhuma za rushwa dhidi yake, atakapofanya mkutano na waandishi wa habari kesho saa tano asubuhi kwenye ofisi za Bunge za jijini Dar.

      Zitto Kabwe: Kesho Nitazungumza na waandishi wa Habari ofisi za Bunge Dar Es Salaam kuanzia saa tano asubuhi. Kuendelea kukaa kimya ni silaha kwa adui.
      Kagalala likes this.

    13. #32
      LORDVILLE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Location : Imaginary island
      Posts : 1,433
      Rep Power : 641
      Likes Received
      127
      Likes Given
      150

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      i shocked!! siamin...ila acha wafanye uchunguz kwanza bado sija muhukum!!!! ana nafas bado....

    14. #33
      Kagalala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Posts : 1,308
      Rep Power : 699
      Likes Received
      396
      Likes Given
      155

      Default Re: Zitto Kabwe aamua kuvunja ukimya juu ya Tuhuma za Rushwa dhidi yake!

      Labda anataka kujiuzulu Ubunge na Nyazifa zake zote ndani ya Chama. I like Zitto lkn kama hii ya Rushwa ni kweli basi siasa ni mchezo mbaya sana.
      Our biggest Enemy is not to try what others have done.

    15. #34
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,448
      Rep Power : 2485
      Likes Received
      970
      Likes Given
      385

      Default

      Quote By Narubongo
      dr slaa ni mmoja wa wanaosemekana kuusaka urais 2015
      je zitto ana imani dr slaa kuongoza sekretarieti? ukizingatia wanaomchafua zitto ni wabunge wapenda posho na wasaka urais kutoka vyama vyote
      Nadhani si kumchafua kwani najua lisemwalo lipo na kama halipo laja, kwa uande wangu sina imani na zito kwani ukiangalia dhahiri zito wa miaka iliyopita bungeni siyo huyu wa leo yaani sijaona uzalendo wake wa awali

    16. #35
      Jile79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2009
      Posts : 3,848
      Rep Power : 1285
      Likes Received
      227
      Likes Given
      9

      Default Re: Zitto Kabwe aamua kuvunja ukimya juu ya Tuhuma za Rushwa dhidi yake!

      Hawezi kukwepa mtego huu alioandaliwa na mafisadi....lazima ang'oke tu hana jipya zaidi ya kutaka misifa

    17. #36
      yaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2011
      Posts : 690
      Rep Power : 541
      Likes Received
      216
      Likes Given
      67

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By Narubongo
      dr slaa ni mmoja wa wanaosemekana kuusaka urais 2015
      je zitto ana imani dr slaa kuongoza sekretarieti? ukizingatia wanaomchafua zitto ni wabunge wapenda posho na wasaka urais kutoka vyama vyote
      Mkuu, hivi unajua kwamba Dr Slaa aliombwa kukubali kugombea urais kupitia chama chake CDM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010?
      Hakuwahi kusema hata mara moja hadharani, kwamba anataka kugombea urais.

      Kwa sababu hiyo hana sababu ya kumfitini Mhe. Zito, kwa sababu hakuna anayejua nani ataombwa tena kugombea Urais kupitia CDM japo intuitively watu wanahisi kwamba atakuwa ni Dr. tena.

    18. #37
      kibai's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Posts : 160
      Rep Power : 405
      Likes Received
      34
      Likes Given
      27

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Zottophobiasis, that is what you can easily say! kuna mambo mengi sana juu ya Zitto. Nigekuwa mshauri wake wa karibu ningemshauri akanushe kuwatetea TANESCO na kwamba hakujua kama wako hivyo, siyo mungu yeye akajua kila kitu lakini Zitto hakuchukua rushwa hata kidogo, mi naamini kabisa.
      Quote By King Kong III
      Zitto zitto!! What more can I say???

    19. #38
      Stanleyabra's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th July 2012
      Posts : 12
      Rep Power : 351
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto Kabwe aamua kuvunja ukimya juu ya Tuhuma za Rushwa dhidi yake!

      Tusubili hiyo kesho lkn kaa mkijua kuwa alikuwa akiwindwa mda mlefu na hizo ni mbinu za kumwua kisiasa.

    20. #39
      moto2012's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd July 2012
      Posts : 973
      Rep Power : 8547
      Likes Received
      561
      Likes Given
      214

      Default re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      pole bro Zitto! mi ni mmoja ambaye na admire misimamo yako juu ya unayoyaamini! But be careful na hao magamba, they are very tricky?

    21. #40
      Kagalala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Posts : 1,308
      Rep Power : 699
      Likes Received
      396
      Likes Given
      155

      Default Re: Zitto Kabwe aamua kuvunja ukimya juu ya Tuhuma za Rushwa dhidi yake!

      Quote By Stanleyabra
      Tusubili hiyo kesho lkn kaa mkijua kuwa alikuwa akiwindwa mda mlefu na hizo ni mbinu za kumwua kisiasa.
      Sasa hapa ndo inabidi aonyeshe umaili wake wa kupangua mambo magumu.
      Our biggest Enemy is not to try what others have done.

    Page 2 of 14 FirstFirst 123412 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...