Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

    Report Post
    Page 12 of 14 FirstFirst ... 21011121314 LastLast
    Results 221 to 240 of 279
    1. #1
      Mohamedi Mtoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Location : Lushoto - Kwemakame.
      Posts : 2,048
      Rep Power : 24548
      Likes Received
      3124
      Likes Given
      354

      Default Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Kauli hii iko kwenye ukurasa wake wa twitter.

      "Kwa masaa 3 nimejieleza mbele ya sekretariat ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa katibu Mkuu".

      Amekiomba chama kifanye uchunguzi juu yake na kuchukua hatua akibainika.
      Quote By Mdakuzi
      Kupitia akaunti yake ya Twitter, naibu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni ameweka wazi nia yake ya kuelezea kila kitu kuhusiana na tuhuma za rushwa dhidi yake, atakapofanya mkutano na waandishi wa habari kesho saa tano asubuhi kwenye ofisi za Bunge za jijini Dar.

      Zitto Kabwe: Kesho Nitazungumza na waandishi wa Habari ofisi za Bunge Dar Es Salaam kuanzia saa tano asubuhi. Kuendelea kukaa kimya ni silaha kwa adui.
      Updates toka magazetini July 31, 2012

      Mwananchi:

      Zitto ahojiwa kwa rushwa!

      SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.

      Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.

      Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.

      Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.

      Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.

      “Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Twitter.

      Lissu ataja wengine
      Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.

      Wabunge wengine watatu tumeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.

      Katika orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo kujinufaisha.

      “Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama hawahusiki,” alisema Lissu na kuendelea:

      “Ila uchunguzi wetu umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma.”

      Lissu alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo wana mgongano wa kimaslahi.

      Alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50.

      “Nasir Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta,” alisema na kuendelea;

      "....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo. Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini.”

      “Hawa ndiyo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi. Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi.”

      Lissu alisema kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na ni kinyume na maadili ya kibunge.

      Katika hatua nyingine Lissu amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema nazo zina madudu mengi.

      “Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe, uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili haki itendeke,” alisema.

      Alipoulizwa Chadema imefanya nini dhidi ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: “Nikiri kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo.”

      “Katika hili tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo.”

      Majibu ya tuhuma
      Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi.

      “Nimekuja bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (Chadema).”

      Kwa upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo.

      "Siyo kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla. Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10 kuhusu masuala hayo ya petroli,” alisema

      Aliishauri kambi hiyo ya upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

      Awali, Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu. Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki vituo vya mafuta.

      Kamata kwa upande wake alisema: “Kuna kamati maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli mtaujua, haraka ya nini?.

      Mjadala Bungeni
      Mjadala huo wa wabunge kuhusishwa na mgongano wa kimaslahi ulianza kulipuka bungeni jana asubuhi baada ya wabunge watatu; Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Salum Barwany (Lindi Mjini) na Mbunge wa Nkasi Kaskazni, Ali Kessy kutaka wabunge wanaotuhumiwa kwa ufisadi watajwe bungeni ili kuisafisha taasisi hiyo ya kutunga sheria.

      "Mheshimiwa Naibu Spika juma lililopita Mheshimwa (Vita) Kawawa alitoa hoja kutaka suala la ufisadi lishughulikiwe kwa kuvunjwa Kamati ya Madini na Spika akaridhia na kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Maadili. Kwa nini Kamati nyingine zilizohusishwa na ufisadi huo nazo zisivunjwe?” alihoji Nassari na kuendelea:

      “Kuna Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Mrema na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto. Kuna tabia ya wabunge kuzikimbia kamati zisizokuwa na mikataba kama Kamati ya Huduma za Jamii na wanazikimbilia kamati zenye mikataba.”

      Barwany alitaka Bunge litajiwe majina ya wabunge waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo mpaka wakapelekwa kwenye Kamati ya Maadili, akieleza kuwa hili litasaidia kulisafisha... “Tumeambiwa Kamati ya Maadili inajadili suala hilo, lakini hatujatajiwa ni wabunge gani waliopelekwa huko, tunaomba mtutajie ili Bunge lijisafishe.”

      “Mimi naungana na wazo la Barwany na Nassari. Majina yatajwe wabunge tunadhalilishwa na wananchi huko mitaani. tuwataje hadharani,’ alisema Kessy.

      Akitoa mwongozo wa hoja hiyo, Ndugai aliiagiza Kamati ya Uongozi ya Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge ili wakajadili suala hilo na baadaye apelekewe taarifa.

      “Naamini wenyeviti wote wa kamati mmo humu ndani, naomba sasa hivi mwende kwenye Ukumbi wa Spika mkajadili suala hilo halafu nipate majibu sasa hivi,” alisema.

      Baadaye jioni, Ndugai alisema kuwa Spika hawezi kuwataja kwa majina wabunge ambao wanajihusisha na rushwa kwa kuwa hawajui.

      Alisema Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana ilikubaliana kuwa ufanyike uchunguzi wa kina kwa ajili ya kuwabaini wale wanaoshukiwa na kwamba ikibainika Bunge litawaanika hadharani.

      “Kamati imerejea kumbukumbu za hansard ya Jumamosi kuwa ufanyike uchunguzi wa kina juu ya jambo hilo na wabunge mtaitwa kwa ajili ya kutoa ushirikiano, ikumbukwe kuwa mbunge akiitwa siyo kwamba ndiyo amekuwa mtuhumiwa, bali pale itakapothibitika majina yatawekwa hadharani,’’ alisema Ndugai.

      Naibu Spika alitahadharisha kuwa ndani ya Kamati hiyo utafanyika uchunguzi wa kutosha kubaini kama kuna mjumbe mwenye maslahi kwa wale wahusika basi ataondolewa ili kutoa nafasi kwa kamati kufanya kazi yake ipasavyo.

      Aliwatahadharisha wabunge kuwa Kamati hiyo haitaingilia utaratibu wa vyombo vya dola ambao wamekuwa wakiufanya ikiwemo wa Takukuru wa kuwahoji baadhi ya wabunge.

    2. Miaka 50

    3. #221
      Matola's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,465
      Rep Power : 0
      Likes Received
      5425
      Likes Given
      3612

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By Fmewa
      Sijui sana kuhusu mambo ya siasa but all I can say ni kuwa huyu kijana mwenzetu Zitto Kabwe anatakiwa atulie kwanza kwenye ubunge alionao kwa sasa....... hizi mbio za kufikiria urais zitamponza na ninaweza kuthubutu kusema kuwa zinaweza kuzima ndoto zake kisiasa na ndoto hizo zikawa kama historia tu. Kwa hiyo mimi nafikiri kwa kusoma alama za nyakati huu si wakati mwafaka kwa zitto kukimbizana na mambo ya Urais angejijenga kwanza, na ninanchohisi ni kuwa hata haya yanayomzonga hata kama ni ya kusingiziwa yanapozidi yatamwaribia image yake kisiasa (ni mtazamo wangu)
      Na kwa habari ya urais atakutana na vipingamizi sio Kutoka CCM tu bali hata katika chama chake.
      Lazima tujifunze kuyapa mambo muda ili yatokee.

      Caution: Niliyoyasema hapo juu ni mawazo na mtazamo wangu tu it may be right or wrong according to you.
      Thanks
      Kwa mtu yeyote makini na mwenye akili timamu ni lazima angeongea kama aliyoyasema. uko sahihi kwa 1000%
      SON OF DAVID likes this.

    4. #222
      FirstLady1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2009
      Location : Mama Mwenye Nyumba
      Posts : 14,946
      Rep Power : 3697
      Likes Received
      3572
      Likes Given
      5738

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By FREDOMFIGHTER
      Zitto ni kijana msomi mzuri tu na anafahamu anachokifanya, yeye yuko kwenye jukumu zito na ameapa kulitekeleza kwa uaminifu mkubwa kwa wanaomlipa, kazi hiyo si nyingine zaidi ya kuisambaratisha chadema, na malipo yake siyo fedha, hata hizo kelele za rushwa ni moshi tu umewekwa kuzuia watu wasione kilichomo ndani. Anavyosema anautaka urais ni kweli lakini siyo kupitia Chadema, huyu ndiye mteule wa baba Mwanaasha, au hamkumbuki kuwa mara mbili JK alisema anataka mrithi wake awe kijana, na mara ya mwisho alimpiga dongo EL kuwa wale wote wa umri kama wake (JK) ambao wana ndoto za kuwa rais wafute ndoto zao hizo, chezea JK wewe.
      Yaani umefanya niangue Kicheko wakati niko katika kipindi kigumu sana...
      Rushwa Bungeni
      Kufungiwa kwa Gazeti la Mwanahalisi
      Wizi wa mafao ya wafanya kazi...NSSF+ PPF
      No one is in charge of your happiness except you...
      God time is the best..

    5. #223
      mtotowamjini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Location : None of Your Business
      Posts : 4,531
      Rep Power : 1262
      Likes Received
      1109
      Likes Given
      28

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      Mpaka jtano
      Every saint has a past, every sinner has a future' ...Oscar Wilde

      One man's good fortune is another man's misfortune


    6. #224
      Philipo Kidwanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2012
      Location : kusadikika
      Posts : 2,063
      Rep Power : 979
      Likes Received
      573
      Likes Given
      147

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By mamajack
      zito ni mbunge makini,the issue is anajichanganya sana na mambo mengi ya kipuuzi mara mafisadi,mara bongo movie,mara urais.i stated onde before,zito turudishie zitto wetu yule mzalendo mwenyekuweka maslai ya taifa mbele anayebeba sura ya tanzania yenye haki.please zitto what is happening,mbona kila siku wewe kwa mabaya tu??usiniambie ni wanakusingizia maana hata kipofu atakushangaa,actually ni lazima tusemwe ili tujue udhaifu wetu,lakini si kila linalisemwa ni kweli,but ni wajibu wetu kujichunguza na kubadilika.
      jitathimini brother!mchango wako unahitajika kuijenga nchi hii.
      nimekupata vizuri sana mama,hata kama mtu sio mbaya kadiri unavyokuwa karibu na ubaya ni rahisi kwa wakuonao kukuhusisha nao jitenge na uovu.
      LIMPETA

    7. #225
      commited's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2012
      Posts : 820
      Rep Power : 528
      Likes Received
      273
      Likes Given
      18

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      Quote By mtotowamjini
      Mpaka jtano

      asante kwa taarifa mkuu labda nilisikia vibaya mkuu nilijua ni leo.. asante sana. pamoja daima

    8. Study Abroad

    9. #226
      Jile79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2009
      Posts : 3,754
      Rep Power : 1262
      Likes Received
      210
      Likes Given
      8

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      Ataongea nini?....naomba waandishi wa habari wamzomee

    10. #227
      Nyangumi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th January 2007
      Posts : 593
      Rep Power : 751
      Likes Received
      5
      Likes Given
      1

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By REMSA
      Yawezekana kweli Zito hahusiki ktk hili,ila tatizo alilonalo anashindwa kusoma alama za nyakati.Zito amefikia
      mahali anjiona ni maarufu sana na muhimu sana ktk hili taifa,ndio maana anafanya mambo mengine bila kuangalia
      athali zake ni zipi hata kwa chama chake,watu wanaumiza vichwa wapate mbinu za kuimaliza CDM na hili Zito
      anajua lakini anawaza athari kwa chama chake haitamuathiri yeye.Jamaa wanajua wakimbabatiza Zito ktk hili
      automatic watakuwa wamepata la kusema kwa CDM,kuwa hata wabunge wake wanapokea rushwa
      .
      Tatizo alilofanya Zitto ni kuwa mtu wa maslahi yaliyojificha. Inawezekana kweli hakuchukua rushwa ili amtetee Mhando, ila alikuwa anamtetea kwa kuwa alikuwa anafaidika na biashara ya nguzo za Umeme toka Tanzania zinavushwa kwenda Kenya na kugongwa Mihuli kuwa zimetoka S.A. then zinarudishwa tene Bongo. Nchi hii tuanze kupiga risasi watu wanahujumu, au kuiba pesa za serikali au mashirika.

    11. #228
      commited's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2012
      Posts : 820
      Rep Power : 528
      Likes Received
      273
      Likes Given
      18

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      Quote By Jile79
      Ataongea nini?....naomba waandishi wa habari wamzomee

      huyu kijana zito binafsi nahisi kuna vitu vinaweza kumpoteza kabisa katika ramani ya siasa za nchi hiii.. hii spidi yake si salama sana

    12. #229
      Philipo Kidwanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2012
      Location : kusadikika
      Posts : 2,063
      Rep Power : 979
      Likes Received
      573
      Likes Given
      147

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      tatizo ni kwamba ukiwa na akili safi huruhusiwi kumuamini zito.
      LIMPETA

    13. #230
      Philipo Kidwanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2012
      Location : kusadikika
      Posts : 2,063
      Rep Power : 979
      Likes Received
      573
      Likes Given
      147

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      kuna watu wasipokufa tanzania haitakomboka asilani.
      LIMPETA

    14. #231
      Wayne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th May 2009
      Posts : 448
      Rep Power : 597
      Likes Received
      78
      Likes Given
      20

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By Jiwe Linaloishi
      hizi kashfa zinatuharibia safari yetu ya 2015 jamani tuwe makini ccm wanatafuta pa kushika....

      As a matter of fact...ZINASAFISHA NJIA....Wale wote wasiofaa .....tutawatambua kwa matendo yao...come 2015 watakosa pakushika.....I LOVE NATURE
      ALL TEMPTATIONS ARE FOUND EITHER IN HOPE OR FEAR

    15. #232
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      press ni kesho Dodoma, saa tano. Sio leo. Sio Dar. Dodoma ni mahala mwafaka kujibu tuhuma hizi za kijinga kabisa...by Zitto
      I'm Naturaly Evasive..

    16. #233
      Ronal Reagan's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 2,627
      Rep Power : 958
      Likes Received
      615
      Likes Given
      256

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      Quote By commited
      asante kwa taarifa mkuu labda nilisikia vibaya mkuu nilijua ni leo.. asante sana. pamoja daima
      Hata mimi nilisikia jana kuwa kesho (leo jumanne), Zitto atafanya press conference. Kama kaihirisha asante kwa taarifa.

    17. #234
      Zemu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2008
      Posts : 422
      Rep Power : 643
      Likes Received
      45
      Likes Given
      18

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      Kaupeleka Jumatano Dodoma sio Dar tena.

    18. #235
      commited's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2012
      Posts : 820
      Rep Power : 528
      Likes Received
      273
      Likes Given
      18

      Default Re: Vip kuhusu mkutano wa zito na waandishi wa habari leo???

      Quote By Edson
      press ni kesho Dodoma, saa tano. Sio leo. Sio Dar. Dodoma ni mahala mwafaka kujibu tuhuma hizi za kijinga kabisa...by Zitto
      daah huyu ndugu na haya maneno yake.. haya,... Ngoja tuombe uzima kesho si mbali

    19. #236
      Wayne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th May 2009
      Posts : 448
      Rep Power : 597
      Likes Received
      78
      Likes Given
      20

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Quote By mtotowamjini
      labda huyu wa sasa hivi ndio the REAL zitto yule wa mwanzo was a fake one alikua anapretend...jus a suggestion msinitukane humu
      Tupo pamoja kiongozi
      ALL TEMPTATIONS ARE FOUND EITHER IN HOPE OR FEAR

    20. #237
      Muarubaini's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 223
      Rep Power : 403
      Likes Received
      47
      Likes Given
      0

      Default Chadema huu ni muda muafaka wa kumfukuza Zitto, mna umma unawasapoti, ataishia kama Mrema

      Huu ni muda mzuri wa kumfukuza huya msaliti ambae kila cku anakisumbua chama. Na safari hii akifukuzwa hana pa kukimbilia, utakuwa mwisho wake kama ilivyo kuwa Mrema baada ya kutoka Nccr. Mkimuacha safari hii kuna cku atakivunja chama vipandevipande

    21. #238
      KANA KA NSUNGU J's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th July 2012
      Posts : 23
      Rep Power : 348
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default Re: Chadema huu ni muda muafaka wa kumfukuza Zitto, mna umma unawasapoti, ataishia kama Mrema

      Naunga mkono hoja ila kwa asilimia 40 tu.Najua CDM hawakurupuku, wanajua jinsi ya kum handle huyu kopo na makopo mengine ndani ya chama kama akina shibuda.Muda ukifika kwa njia sahihi ataondolewa tu.Haijalishi sasa au baadae

    22. #239
      Nduka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2008
      Posts : 5,562
      Rep Power : 1629
      Likes Received
      379
      Likes Given
      552

      Default

      Quote By Jile79
      Ataongea nini?....naomba waandishi wa habari wamzomee
      Labda wale wa gazeti la mchaga TZ Daima.

    23. #240
      hasan124's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 2nd January 2012
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 656
      Rep Power : 503
      Likes Received
      120
      Likes Given
      104

      Default Re: Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

      Hivi ni Zito Kabwe AMA Kabwela? Tusihukumu, Tusubiri na tutajua mbivu na Mbichi. Urais mchezo?
      FirstLady1 likes this.
      ADC - DIRA YA MABADILIKO : ADC - TUMAINI LA MTANZANIA.

    24. FemaTV & Radio
    Page 12 of 14 FirstFirst ... 21011121314 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...