Re: Should CHADEMA Fire Zitto?
Issue ya rushwa ni ya kipuuzi kama uzinzi. Unaweza ona katoto kazuri kenye uzoefu katik mchezo ingawa ni kadogo kiumri, kimekula sana maisha waziwazi na wakubwa kuliko wewe, ila siku zinavyokwenda kinaanza kutega, kinakutafuta kama mshauri, halafu kinaamua weka wazi mambo kuwa kinakuzimia na kinavyokujua kinaamini kuwa kuwa nawe maisha yake yatabadilika sana.Ghafla akili inaanza kulainika na kuifikiri hiyo option, and then occassionally kinatokea kwa style ya kuhamasiza zaidi akili yako.Then unalegea, unajisikia kuhesabu 1, 2 , unastop, siku inapita.Then akili inakosa uvumilivu, halafu natokea mtu kukafukuzia mbele yako, unapata wivu bila kujijua, na hali ya kutaka wahi inaongezeka .Then mazingira yanakuja tena unaanza hesabu 1,2 unashangaa umepita 3.Unafanya zoezi rasmi.Katikati ya Tukio unashtushwa na kujilaumu kwa ulichofanya baada ya kuona mamlaka ikikutia hatia hatiani, marafiki wanakushangaa, watoto, na mchumba /mke wako anakushangaa anakuchukia, anakuona kuwa hata mwanao unaweza mnanii, na mwanao naye kama yupo naye anaanga kuogopa, ghalfa inakuwa habari ya nchi hata kama ulikuwa hujulikani hata ktk nyumba kumi za jirani.
Rushwa ina mbaya zaidi ilikunyemelea wakati una hitaji hela na watoa rushwa walikuwa na predatory strategies.Huna ujanja unakuwa prey within seconds, halfu unashindwa elewa kwanini watu wa karibu nao wanakuchukia wanakuacha pekee yako uilezee hiyo hali.Ni haki yao kwa vile hawakuwa nawe wakati ulikuwa unajenga mazingira ya kudakwa, wakati ukitoa utetezi kuwa hao wawindaji hawakuwezi kwani umeshakomaa na kuwajua vya kutosha.Pengine pia ukaongeze nyama kuwa hii ndio njia ya wewe kunasa mambo yao.
CIA huwa wakituma operative wao huwa wanatuma na mtu mwingine wa kumtazama, ili asijejikuta amekuwa addicted/au hata kuangukia katika mapenzi na tamaduni au hata uatartibu wa anayewindwa.Hata wagonjwa wa waganga hujikuta wakiolewa na waganga.
Kama mh atakuwa ameanguka kweli basi CDM watakuwa na kipindi kigumu sana:
-Kumtupa si vyema kwani pia alikuwa na mchango.
-Kumtunza bado ni shida kwani kam ni addict basi ,once occassionally atakuwa akienda onja unga kambi ya jirani.
-CDM kumtuza kuta compromise misingi yao, kwani watakuwa na double standard na baadaye CCM wakaamua tumia kama fimbo.Kwani hata suala la posho, CCM wamejitahidi kulalama kuwa CDM wanapokea.
-Kama ni kweli na Takukuru wakalivalia njuga, kupigana kumtoa ni kuingilia utawala wa sheria, na hata akitoka itabidi awe mjumbe wa halamshauri kwani public image itakuwa ni burdden.
ZItto ndiye anayejua ukweli hadi sasa,kabla hizo tuhuma hazijachukua sura mpya.Anapaswa kuwa na busara ,ajitahidi kuminimize impact na ajaribu kutokihusisha chama na mapungufu yake kwa kiasi awezacho.Awe kama marion Jones,yule dada mkimbiaji aliyekuja thibitika kutumia dawa, alikubali makosa yake, akawajibika kwa kulipa fine na kurudisha medali zote, na kupata kifungo ch amiezi kadhaa.sasa anaishi kwa furaha ana amani,sasa yupo kuru kushiriki ibada, kukaa na watu kwani keshatoa hatia.
Kama Zitto atakuwa amehusika basi atakuwa na test ingine katik nafsi yake ,kuukubali ukweli hata kama utakuwa umemaliza kabisa nguvu ya kutangaza nia.Atakuwa na test ya kulinda chama, na wengine ambao hawakuhusishwa.Atakuwa na Test ya kutoona matatizo yake yamesababishwa na wana CDM wengine.Kwani bado takukuru wanaweza anzisha upelelezi wa kuzuia suala kama sasa tunavyoambiwa kuwa suala lipo mahakamani, litakalomfanya apoteze nafasi ya CDM hata kama baadaye itagundulika otherwise.
Pia kama hana hatia pia inabidi awe na mpangilio mathubuti wa kujitoa na kuiaminisha jamiii kuhusu hilo na kuwafanya wenzie warudi katik hali ya kawaida na upendo kama zamani wakati cdm ikiwa just another party
SIMPLY THE RADICAL: I can`t wait to see the criminalization of CCM,UWT,Bunch of Policemen/women,and all wanafiki na wachumia tumbo.
Follow Us Here