Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

    Report Post
    Page 1 of 40 12311 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 783
    1. #1
      Kyindokyakombe's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 97
      Rep Power : 379
      Likes Received
      95
      Likes Given
      2

      Default Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

      CHANZO: TBC1

      Quote By Profesy View Post
      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

      TAMKO LA SERIKALI

      GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA


      Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

      Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

      Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

      Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

      Uamuzi wa Serikali
      Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.

      Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

      Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.

      Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.

      Imetolewa na

      OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
      30 Julai, 2012
      Committee to Protect Journalists (CPJ) Statement;

      Tanzanian authorities ban weekly indefinitely

      Nairobi, July 30, 2012--The Tanzanian government today banned indefinitely the critical Swahili-language weekly MwanaHalisi, accusing the paper of publishing seditious articles, according to local journalists and a statement by the information ministry.

      The ministry claimed that MwanaHalisi's four July editions contained seditious and false material but did not specify particular articles. Under the 1976 Newspaper Act, Tanzanian authorities can suspend a newspaper at will if they deem that it has "seditious intent," according to CPJ research. MwanaHalisi Chief Editor Jabir Idrissa told CPJ that the paper is considering filing an appeal.

      Idrissa and other local journalists said they suspect the ban is related to a series of articles in MwanaHalisiconcerning the kidnap and torture in late June of physician Steven Ulimboka. Unknown assailants kidnapped and beat Ulimboka on the outskirts of the main commercial city Dar es Salaam after he led a doctors' strike, according to news reports. MwanaHalisi's reports suggested involvement by authorities, citing phone records of an alleged security officer, Idrissa said. Tanzanian security services and President Jakaya Kikwete have denied government involvement, according to local and international reports.

      "Once again, Tanzanian authorities have wielded an archaic newspaper act and vague, unsupported accusations of sedition to censor reporting that is merely critical of the government," said CPJ East Africa Consultant Tom Rhodes. "Authorities should reverse this ban immediately and allow MwanaHalisi to report on the Ulimboka case without fear of reprisal."

      Over the past year, Tanzanian authorities have called MwanaHalisi's editors in for questioning every two or three weeks over their articles, Idrissa said.

      Tanzanian authorities used the Newspaper Act to suspend MwanaHalisi in October 2008 for three months for articles considered seditious and insulting to the president. During the 2010 election campaign, Sethi Kamuhanda, the permanent secretary of the ministry of information, visited print media houses to warn them that the government would close down any media that portrayed the government negatively, according to local journalists.



      For more data and analysis on Tanzania, visit CPJ's Tanzania page here.


      ###
      CPJ is a New York-based, independent, nonprofit organization
      that works to safeguard press freedom worldwide.
      Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

      Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.


    2. #2
      mamajack's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 1,153
      Rep Power : 587
      Likes Received
      275
      Likes Given
      71

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      duh,kweli tanzania tumethubutu tukashindwa,
      source ya ukweli ntapata wapi tena.
      terabojo, Jao, nsanu and 2 others like this.

    3. #3
      kamili's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th February 2011
      Posts : 246
      Rep Power : 472
      Likes Received
      59
      Likes Given
      181

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Fungia fungia vyombo vya habari, hii serikali kuna siku itakuta na wananchi wameifungia yenyewe.

    4. #4
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,660
      Rep Power : 4023
      Likes Received
      2944
      Likes Given
      5072

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Haaahaa! Ile dozi ya Kubenea ilikuwa kubwa kuliko. Maana imewaweka jamaa uchi bila kutegemea
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    5. #5
      ByaseL's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 1,795
      Rep Power : 950
      Likes Received
      94
      Likes Given
      11

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Waoga hao! Kwanza kulifungia ndio itazidisha uvumi kwamba serikali inahusika haswa. Pili kwani hata Ulimboka watanfunga mdomo akirudi?
      Ndahani, mizambwa, nsanu and 1 others like this.


    6. #6
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,921
      Rep Power : 1171
      Likes Received
      1058
      Likes Given
      804

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      mbona radio imani inayohubiri chuki za kidini kila siku haifungiwi?? kuna double standards kwenye media???
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    7. #7
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,687
      Rep Power : 1278
      Likes Received
      1318
      Likes Given
      1711

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      I saw this one coming.
      jamiif likes this.

    8. #8
      Mamndenyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 13,507
      Rep Power : 35830
      Likes Received
      6907
      Likes Given
      21146

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      watafungia vingapi, aibu yao.
      mapungo likes this.
      SIYO WOTE WANAOTANGATANGA WAMEPOTEA

    9. #9
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 19,212
      Rep Power : 12771
      Likes Received
      6440
      Likes Given
      999

      Default re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Safi sana gazeti la udaku na majungu na kufitinisha watu hata hivyo serikali imechelewa mno kulifungia.
      MAMA POROJO and kilam like this.

    10. #10
      semtawa's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 25th July 2012
      Posts : 5
      Rep Power : 349
      Likes Received
      4
      Likes Given
      1

      Default Tetesi: MWANAHALISI imefungiwa

      Baada ya kufungiwa MWANAHALISI gazeti jingine la MWANAHABARI limepewa onyo kali.

    11. #11
      Ringo Edmund's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2010
      Location : MDAWI
      Posts : 3,673
      Rep Power : 1365
      Likes Received
      886
      Likes Given
      586

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Kubenea karibu huku na ikiwezekana anzisheni jingine,tupo pa1.
      Mboko and Gajunga like this.

    12. #12
      Ndibalema's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th April 2008
      Location : Mbagala
      Posts : 6,729
      Rep Power : 2030
      Likes Received
      1697
      Likes Given
      1697

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Serikali ime'prove failure.
      "Makalio ya sufuria hayaogopi moto"

    13. #13
      wasipemba's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Posts : 79
      Rep Power : 396
      Likes Received
      20
      Likes Given
      5

      Default Re: Tetesi: MWANAHALISI imefungiwa

      Quote By semtawa View Post
      Baada ya kufungiwa MWANAHALISI gazeti jingine la MWANAHABARI limepewa onyo kali.

      sio tetesi ni kweli limefungiwa kwa muda usiojulikana....
      semtawa likes this.

    14. #14
      ERIC JOSEPH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2011
      Location : MBEYA TANZANIA
      Posts : 340
      Rep Power : 466
      Likes Received
      34
      Likes Given
      2

      Default Re: MwanaHalisi Kwishney!

      mbona hakuna maelezo mkuu
      E.joseph

    15. #15
      Bornvilla's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2011
      Posts : 639
      Rep Power : 549
      Likes Received
      141
      Likes Given
      0

      Default Breaking News:MwanaHalisi lapigwa ban.

      Gazeti la mwanahalisi limefungiwa kwa muda usiojulikana kutokana na makala za uchochezi.
      source:TBC1 dira ya mchana.

    16. #16
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 551
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By ByaseL View Post
      Waoga hao! Kwanza kulifungia ndio itazidisha uvumi kwamba serikali inahusika haswa. Pili kwani hata Ulimboka watanfunga mdomo akirudi?
      mkuu! sisi hatuhitaji tu ishu ya dr! bali mambo mengi! sasa kulifungia hili, washayaficha mengi sana aisee! la dr lishakuwa wazi

    17. #17
      Ston Merchant's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st August 2011
      Location : Samunge
      Posts : 255
      Rep Power : 450
      Likes Received
      41
      Likes Given
      29

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Ritz View Post
      Safi sana gazeti la udaku na majungu na kufitinisha watu hata hivyo serikali imechelewa mno kulifungia.
      porojo.....
      " Umeme hauna kiuno lakini Unakatika. "

    18. #18
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 12,391
      Rep Power : 5160
      Likes Received
      3344
      Likes Given
      2738

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Imbombo ngafu,kubenea umetisha na Huyu ndie aliyemteka Dr ulimboka!
      FuturePresident likes this.

    19. #19
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,699
      Rep Power : 2911
      Likes Received
      3892
      Likes Given
      12472

      Default Re: Breaking News:MwanaHalisi lapigwa ban.

      Can they do that? Wamechochea nini? Mbona sijaona vurugu zozote zilizosababishwa na gazeti?
      Duduwasha, Sangarara and madame like this.

    20. #20
      matumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th July 2011
      Posts : 2,431
      Rep Power : 1468
      Likes Received
      716
      Likes Given
      679

      Default

      Quote By Ritz View Post
      Safi sana gazeti la udaku na majungu na kufitinisha watu hata hivyo serikali imechelewa mno kulifungia.
      vipi kuhusu Radio Imani?

    Page 1 of 40 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...