Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

    Report Post
    Page 14 of 40 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast
    Results 261 to 280 of 783
    1. #1
      Kyindokyakombe's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 97
      Rep Power : 378
      Likes Received
      95
      Likes Given
      2

      Default Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

      CHANZO: TBC1

      Quote By Profesy
      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

      TAMKO LA SERIKALI

      GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA


      Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

      Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

      Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

      Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

      Uamuzi wa Serikali
      Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.

      Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

      Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.

      Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.

      Imetolewa na

      OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
      30 Julai, 2012
      Committee to Protect Journalists (CPJ) Statement;

      Tanzanian authorities ban weekly indefinitely

      Nairobi, July 30, 2012--The Tanzanian government today banned indefinitely the critical Swahili-language weekly MwanaHalisi, accusing the paper of publishing seditious articles, according to local journalists and a statement by the information ministry.

      The ministry claimed that MwanaHalisi's four July editions contained seditious and false material but did not specify particular articles. Under the 1976 Newspaper Act, Tanzanian authorities can suspend a newspaper at will if they deem that it has "seditious intent," according to CPJ research. MwanaHalisi Chief Editor Jabir Idrissa told CPJ that the paper is considering filing an appeal.

      Idrissa and other local journalists said they suspect the ban is related to a series of articles in MwanaHalisiconcerning the kidnap and torture in late June of physician Steven Ulimboka. Unknown assailants kidnapped and beat Ulimboka on the outskirts of the main commercial city Dar es Salaam after he led a doctors' strike, according to news reports. MwanaHalisi's reports suggested involvement by authorities, citing phone records of an alleged security officer, Idrissa said. Tanzanian security services and President Jakaya Kikwete have denied government involvement, according to local and international reports.

      "Once again, Tanzanian authorities have wielded an archaic newspaper act and vague, unsupported accusations of sedition to censor reporting that is merely critical of the government," said CPJ East Africa Consultant Tom Rhodes. "Authorities should reverse this ban immediately and allow MwanaHalisi to report on the Ulimboka case without fear of reprisal."

      Over the past year, Tanzanian authorities have called MwanaHalisi's editors in for questioning every two or three weeks over their articles, Idrissa said.

      Tanzanian authorities used the Newspaper Act to suspend MwanaHalisi in October 2008 for three months for articles considered seditious and insulting to the president. During the 2010 election campaign, Sethi Kamuhanda, the permanent secretary of the ministry of information, visited print media houses to warn them that the government would close down any media that portrayed the government negatively, according to local journalists.



      For more data and analysis on Tanzania, visit CPJ's Tanzania page here.


      ###
      CPJ is a New York-based, independent, nonprofit organization
      that works to safeguard press freedom worldwide.
      Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

      Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.


    2. #261
      kibol's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2012
      Location : dar es salaam
      Posts : 1,318
      Rep Power : 624
      Likes Received
      328
      Likes Given
      200

      Default

      Quote By Ndahani
      The way we see the problem is the problem. Yaani kuna watu wana vichwa bwana na wanafikiria utafikiri dunia inaishia leo. But all in all, I have kept the copy of that MwanaHalisi edition as a memory of the shit we have been making to ourselves by lack of critical thinking...it was one of the amazing investigative stories in our country.
      Pale waliwaacha utupu kabisa watawala wetu,cha ajabu ktk kufikiri kwao wakaona solution ni kulifungia mwanahalisi.shame on them

    3. #262
      Kichiringa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 12
      Rep Power : 366
      Likes Received
      2
      Likes Given
      1

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      aiseeeeee.....


      nadhani litakalofuata ni mwananchi then........uhuru litabaki milele.

    4. #263
      m4cjb's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd July 2012
      Posts : 96
      Rep Power : 367
      Likes Received
      4
      Likes Given
      5

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      kaka usife moyo tutafika tu.

    5. #264
      sembuli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Posts : 599
      Rep Power : 491
      Likes Received
      243
      Likes Given
      167

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By tamuchungu
      Mungu ibariki tanzania,mungu lisambaratishe mwanahalisi na wafuasi wake wanaopandikiza na kueneza chuki na uongo mioyoni mwa watanzania.aaaimen
      you again!!! kweli una haki ya kudai nyongeza ya posho ya propaganda from magamba, endelea kutumika hivyohivyo na kuweka utu wako rehani. shame on you

    6. #265
      Aristides Pastory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2012
      Posts : 347
      Rep Power : 440
      Likes Received
      58
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By MLETAHOJA
      Siyo kila unachokifahamu kinafaa kuandikwa. Unaandika yale yenye maslahi kwa taifa. Hilo aliloliandika lina maslahi kwa taifa maana jeshi letu la polisi limetuahidi kuwa linafanya kila jitihada kumbaini aliyemteka Ulimboka na mara zote polisi wamekuwa wakipongeza taarifa za uhalifu wanazopewa na raia wema kupitia kile wanachokiita ulinzi shirikishi. Kwa nini mara hii Mwanahalisi haipewi ushirikiano na jeshi la polisi badala yake linanyamazishwa? Hapo kuna kitu.
      Mbona KUBENEA hajaitwa kuhojiwa na jeshi la polisi.
      Kweli nimeamini nchi hii inawenyewe...


    7. #266
      Getsemane's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 27
      Rep Power : 355
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Demokrasia kitanzini Tz.
      Utawala bora unachimbiwa kaburi wakati uwazi unapelekwa uhamishoni!!

    8. #267
      SASATELE's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th September 2011
      Posts : 150
      Rep Power : 423
      Likes Received
      81
      Likes Given
      22

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      duh. habari ya kufungiwa kwa Mwanahalisi imenisikitisha sana kwa sababu mbili:
      1. Serikali ilitakiwa ione mbele zaidi ya namna ilivyotumia mabavu kuzima taarifa za uchunguzi za gazeti moja ilhali kuna magazeti mengi yatakayoendelea kuandika habari za uchunguzi
      2. kufungiwa kwa gazeti hilo kutaiweka Tanzania katika list ya nchi zinazominya uhuru wa wananchi kupata habari
      3. Hata wale ambao hawakuisoma habari ile wataisoma sasa tena wakiwa na alama ya kujiuliza kichawani(!) dhidi ya serikali

      Hapa nasema serikali imekurupuka!!

    9. #268
      Dickson Ng'hily's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 22nd October 2010
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 326
      Rep Power : 504
      Likes Received
      189
      Likes Given
      182

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Shardcole
      Mkuu si uhamie CHADEMA basi kubwa tupambane vizuri na hii serkali dhalimu kwani unafaa sana ila tatizo umekula fungate na CCJ.
      Mkuu Shardcole, nakuomba uwe unafanya utafiti hata kidogo kabla ya kuandika...Hebu angalia profile pic yangu pia signature yangu bila shaka vyo kwa pamoja vyaweza kukupa tip ya kuwa mimi ni wa upande gani katika siasa za Tanzania...

      sweke34 likes this.
      'Ppooooz.......Pawaaaaa
      Hakuna Kulala.......Mpaka Kieleweke'
      0716/0765/0788-030030

    10. #269
      Mkirua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2010
      Posts : 3,548
      Rep Power : 1064
      Likes Received
      1285
      Likes Given
      619

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      There are currently 856 users browsing this thread. (186 members and 670 guests)
      The world suffers a lot. Not because of the violence of bad people, but because of the silence of good people!

    11. #270
      Nivea's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 5,980
      Rep Power : 16311
      Likes Received
      3393
      Likes Given
      4336

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By tamuchungu
      hapa tunashindana kwa hoja,sio muda wa kujiunga jf.mwanahalisi anafanyia uchunguzi wake kwenye daftari la wapiga kura halafu anakuja kutudanganya hapa kwa nini?hatudanganyiki.
      tamuchungu pole sana hufai hata kuwa mzazi hata wawatoto wa panya kwa akili uliyonayo utawakorogea sumu wafe ukijikinga na gharama za maisha
      Kosea njia utaelekezwa,lakini usikosee mtu wakuoa /kuolewa naye,vinginevyo majuto yatakuwa sehemu ya maisha yako.tuliza kichwa unapochagua mwenzi wa maisha.

    12. #271
      Mnyakatari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th October 2010
      Posts : 716
      Rep Power : 682
      Likes Received
      255
      Likes Given
      180

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Kulifungia gazeti hata kidogo hakuwezi kuzuia ukweli ama usijulikane au ule uliojulikana ufutike kwenye fikra za watanzania.Wengi wamesoma toleo hilo na mpaka sasa wamehifadhi wanaendelea kulisoma na wengine ambao hawakusoma.

      Hata wakitoa tangazo la kuwataka watu wenye gazeti hilo walisalimishe polisi kabla msako wa nyumba kwa nyumba haujapita bado hawawezi kufuta ukweli kuwa waliomteka,kumtesa vibaya na kujaribu kumuua dr.Ulimboka ni usalama wa taifa.

      Kwakuwa gazeti limefungiwa kwa muda usiojulika basi uongozi wa mwanahalisi ufanye mpango wa kuprint kopi nyingi za gazeti hilo lizidi kusambaa mpaka vijijini.

    13. #272
      LORDVILLE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Location : Imaginary island
      Posts : 1,433
      Rep Power : 641
      Likes Received
      127
      Likes Given
      150

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By tamuchungu
      hapa tunashindana kwa hoja,sio muda wa kujiunga jf.mwanahalisi anafanyia uchunguzi wake kwenye daftari la wapiga kura halafu anakuja kutudanganya hapa kwa nini?hatudanganyiki.
      mawazo mgando na membamba!!

    14. #273
      Baba V's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Location : Planet Nibiru
      Posts : 11,528
      Rep Power : 42519
      Likes Received
      5073
      Likes Given
      4242

      Default

      Quote By OSOKONI
      mbona radio imani inayohubiri chuki za kidini kila siku haifungiwi?? kuna double standards kwenye media???
      Was,,,ng,, hawa, hawana maana yoyote, na wamekuq,upuka, this is gonna cost them very much!

    15. #274
      Nicas Mtei's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : Shamba
      Posts : 8,660
      Rep Power : 32152
      Likes Received
      5007
      Likes Given
      5203

      Default

      Quote By Dickson Ng'hily
      Mkuu Shardcole, nakuomba uwe unafanya utafiti hata kidogo kabla ya kuandika...Hebu angalia profile pic yangu pia signature yangu bila shaka vyo kwa pamoja vyaweza kukupa tip ya kuwa mimi ni wa upande gani katika siasa za Tanzania...

      Alikurupuka bila kujua.

    16. #275
      andybird314's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd January 2012
      Location : Tanzania
      Posts : 2,787
      Rep Power : 993
      Likes Received
      578
      Likes Given
      297

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      huu ndio uzuri wa Tanzania yaani ukiongea sana au kudai unajua lazima wakufanyie kitu ambacho hutasahau. Wanao elewa lazima wajue kuwa hiyo ni kuwafunga wasiseme uozo wa serikali yetu dhaifu
      Kweli kuishi Tanzania kuona mengi

    17. #276
      Getsemane's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 27
      Rep Power : 355
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default

      Demokrasia kitanzini Tz.Utawala bora umechimbiwa kaburi wakati uwazi umepelekwa uhamishoni!!

    18. #277
      kibol's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2012
      Location : dar es salaam
      Posts : 1,318
      Rep Power : 624
      Likes Received
      328
      Likes Given
      200

      Default

      Quote By FJM
      Kwa hili serikali haiwezi tena kudai kuwa inafuata utawala wa demokrasia na sheria. Kama wana-dispute habari yoyote iliyoandikwa kwenye gazeti la mwanahalisi kwa nini wasiende mahakamani? Ni nani anayeamua habari fulani ni ya uchochezi au la? Nini maana ya uchochezi? Na watanzania wana akili na utashi wa kujua uchochezi au mpaka serikali iwatafunie habari? Hii inaharibu credibility ya serikali.
      Sheria moja kandamizi sana kwa vyombo vya habari ndio imewapa hayo mamlaka,kwamba waziri habari,utamaduni na michezo anaweza akaamka asubuhi kwasababu anazozijua yeye akaamua kulifungia gazeti lolote lile.wako sahihi kwasababu tunafuata utawala wa sheria na sio utawala bora,unaweza kuua na ukawa sahihi tu maadam sheria inakuruhusu kufanya hivyo.

    19. #278
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1258
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      By Ritz

      Wewe ulitegemea kama nani jeshi la polisi alifanyi kazi kienyeji kuokota habari mitaani kwa waandishi makanjanja.
      Ukiambiwa una akili fupi unakataa sijui kwanini...huyo Deo hapo chini ndiyo angekuwa mtu wa kwanza kuhojiwa hata kama jeshi la polisi lingekuwa dhaifu kiasi gani. Tuambie jeshi la polisi linatoa wapi ushahidi kwenye uchunguzi wao unaoendelea wakati mtu aliyekuwepo kwenye tukio mpaka sasa hivi hajahojiwa.
      Taarifa za kuaminika zinasema, polisi hawajawahi kuwahoji Dk. Deogratias Michael aliyeshuhudia Dk. Ulimboka akitekwa; Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) Hellen Kijo-Bisimba wala Onesmo ole Ngurumwa, mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini waliokwenda kumchukua polisi Bunju.

    20. #279
      oxlade's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th July 2012
      Posts : 236
      Rep Power : 397
      Likes Received
      10
      Likes Given
      12

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      no more udaku.........lol

    21. #280
      Dickson Ng'hily's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 22nd October 2010
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 326
      Rep Power : 504
      Likes Received
      189
      Likes Given
      182

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Nicas Mtei
      Alikurupuka bila kujua.
      Hahahaha...Umeona eeeh...Kamanda upo lakini! Niko Tabora but in 3days nitakuwa on ma way back home...@ Nicas Mtei
      'Ppooooz.......Pawaaaaa
      Hakuna Kulala.......Mpaka Kieleweke'
      0716/0765/0788-030030

    Page 14 of 40 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...