Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

    Report Post
    Page 13 of 40 FirstFirst ... 3111213141523 ... LastLast
    Results 241 to 260 of 783
    1. #1
      Kyindokyakombe's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 97
      Rep Power : 375
      Likes Received
      95
      Likes Given
      2

      Default Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

      CHANZO: TBC1

      Quote By Profesy
      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

      TAMKO LA SERIKALI

      GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA


      Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

      Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

      Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

      Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

      Uamuzi wa Serikali
      Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.

      Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

      Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.

      Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.

      Imetolewa na

      OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
      30 Julai, 2012
      Committee to Protect Journalists (CPJ) Statement;

      Tanzanian authorities ban weekly indefinitely

      Nairobi, July 30, 2012--The Tanzanian government today banned indefinitely the critical Swahili-language weekly MwanaHalisi, accusing the paper of publishing seditious articles, according to local journalists and a statement by the information ministry.

      The ministry claimed that MwanaHalisi's four July editions contained seditious and false material but did not specify particular articles. Under the 1976 Newspaper Act, Tanzanian authorities can suspend a newspaper at will if they deem that it has "seditious intent," according to CPJ research. MwanaHalisi Chief Editor Jabir Idrissa told CPJ that the paper is considering filing an appeal.

      Idrissa and other local journalists said they suspect the ban is related to a series of articles in MwanaHalisiconcerning the kidnap and torture in late June of physician Steven Ulimboka. Unknown assailants kidnapped and beat Ulimboka on the outskirts of the main commercial city Dar es Salaam after he led a doctors' strike, according to news reports. MwanaHalisi's reports suggested involvement by authorities, citing phone records of an alleged security officer, Idrissa said. Tanzanian security services and President Jakaya Kikwete have denied government involvement, according to local and international reports.

      "Once again, Tanzanian authorities have wielded an archaic newspaper act and vague, unsupported accusations of sedition to censor reporting that is merely critical of the government," said CPJ East Africa Consultant Tom Rhodes. "Authorities should reverse this ban immediately and allow MwanaHalisi to report on the Ulimboka case without fear of reprisal."

      Over the past year, Tanzanian authorities have called MwanaHalisi's editors in for questioning every two or three weeks over their articles, Idrissa said.

      Tanzanian authorities used the Newspaper Act to suspend MwanaHalisi in October 2008 for three months for articles considered seditious and insulting to the president. During the 2010 election campaign, Sethi Kamuhanda, the permanent secretary of the ministry of information, visited print media houses to warn them that the government would close down any media that portrayed the government negatively, according to local journalists.



      For more data and analysis on Tanzania, visit CPJ's Tanzania page here.


      ###
      CPJ is a New York-based, independent, nonprofit organization
      that works to safeguard press freedom worldwide.
      Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

      Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.

    2. Miaka 50

    3. #241
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By thatha
      ok, lakini labda kuna jambo la msingi, unajua lile toleo liliingia ndani zaidi kiasi kwamba pengine hata kungetokea migongano kati ya vyombo vya dola, vyombo vya maamuzi na media. Nakumbuka hata baadhi ya taasisi za habari zilisema kuwa Mwanahalisi lilienda mbali zaidi.
      Ndugu hata sijui hayo...I just know one thing...acha liwalo na liwe, teh teh teh. Ukiona mtu anaandika vile unategemea nini?
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    4. #242
      pembejeo's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 5th July 2012
      Posts : 5
      Rep Power : 348
      Likes Received
      0
      Likes Given
      2

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      poleni kwa waliolifunga kwani upuuzi mlioufanya kwa ulimboka tumeshaujua subirini sasa 2015 muone

    5. #243
      Baba V's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Location : Buguruni Mnyamani
      Posts : 10,883
      Rep Power : 30218
      Likes Received
      4708
      Likes Given
      3477

      Default Re: Jf studio_Breaking News....Gazeti la Mwanahalisi lapata pigo...Nini Maoni yako....fuatilia

      Ni mwanzo mzuri kwa serikali, kesho waifungie na JF afu ndo waone tutakapokwenda kujadilia mambo yetu ikulu!

    6. #244
      Ng'wanangwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2010
      Posts : 5,989
      Rep Power : 1646
      Likes Received
      1136
      Likes Given
      414

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Ritz
      serikali imechelewa mno kulifungia.
      nimeipenda hiyo mkuu.

      sasa kulikuwa na haja gani ya kulifungia wakati washachelewa? scrappy government of msoga.
      CCM HAIKUBALIKI ...TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA...

      REST IN PEACE, DR.D.D. HAULE...Wema hawana Maisha

    7. #245
      m4cjb's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd July 2012
      Posts : 96
      Rep Power : 363
      Likes Received
      4
      Likes Given
      5

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By artorius
      Unajidhalilisha kwa njaa zako,bora ukae kimya
      umetumwa?mungu atatafuta njia nyingine ya kutupa hahari watz?mawazo yako na ya mchawi hayana tofauti.

    8. RukaaJuu Final

    9. #246
      GRILL's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th November 2007
      Posts : 101
      Rep Power : 606
      Likes Received
      11
      Likes Given
      2

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By sweetlady
      Hii mbinu yako nzuri nimeipenda mie pia hapa ofisini kuna mashine ya copy.....kuanzia leo natoa makopi yasiyokuwa na idadi na kuyasambaza kwa wana wa nchi hii huku nikiwaambia kuwa ukweli huo ndio umepelekea gazeti la mwanahalisi kufungiwa !
      Nakushauri kuwa makini usije na wewe kufungiwa lakini. Chezea serikali wewe!!

    10. #247
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,484
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4303
      Likes Given
      1248

      Default Re: Jf studio_Breaking News....Gazeti la Mwanahalisi lapata pigo...Nini Maoni yako....fuatilia

      Sasa hapa ndipo watu waamini yaliyo kuwa yanasemwa kila siku hii ni serikali dhaifu yenye maamuzi dhaifu. Hivi ni visasi na havito ishia hapa tutarajie kushangazwa zaidi.

    11. #248
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,039
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By sembuli
      karibu wote wanaounga mkono serikali kwa ujinga na aibu hii wamejiunga JF leo kama wewe!! Nahisi wewe ni mmoja wa wale wanaodai nyongeza ya posho za propaganda pale lumumba kwa kuunga mkono magamba na maamuzi yao ya kiimla.
      hapa tunashindana kwa hoja,sio muda wa kujiunga jf.mwanahalisi anafanyia uchunguzi wake kwenye daftari la wapiga kura halafu anakuja kutudanganya hapa kwa nini?hatudanganyiki.

    12. #249
      denoo49's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th March 2011
      Location : Kijijini
      Posts : 739
      Rep Power : 756
      Likes Received
      138
      Likes Given
      20

      Default

      Quote By Ndahani
      The way we see the problem is the problem. Yaani kuna watu wana vichwa bwana na wanafikiria utafikiri dunia inaishia leo. But all in all, I have kept the copy of that MwanaHalisi edition as a memory of the shit we have been making to ourselves by lack of critical thinking...it was one of the amazing investigative stories in our country.
      mkuu kama kunauwezekano wa kuiiatach naomba, uitupie humu tena maana mi nilii save lakini kila napojaribu kuifungua nakuta na pingamizi la akina mods

    13. #250
      FirstLady1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2009
      Location : Mama Mwenye Nyumba
      Posts : 14,976
      Rep Power : 3704
      Likes Received
      3581
      Likes Given
      5771

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Wajinga kabisa hawa wanashindwa kutetea hoja na kuamua kufungia gazeti
      Mwisho wao uko karibu sana.....
      wasidhani tunawaangalia tu
      Tanzania ya sasa sio Tanzania ya miaka 40 iliyopita
      mambo yao machafu yako wazi hivo hakuna wanachofanya....
      Ndahani and LORDVILLE like this.
      No one is in charge of your happiness except you...
      God time is the best..

    14. #251
      mang'ang'a's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 316
      Rep Power : 499
      Likes Received
      64
      Likes Given
      9

      Default Gazeti pendwa mwanahalisi lafungiwa

      Hii nimeisoma kutoka Michuzi blogspot, kwa sababu ya habari zinazo chochea wananchi.

      Sheria za nchii hii haziruhusu habari za kiuchunguzi? manake nionavyo mimi, wangeshtakiwa mahakamani wakishindwa kuthibitisha walicho toa gazetini ndio hatua zifuate.!!!!!!!!!!!!!!!!

    15. #252
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By denoo49
      mkuu kama kunauwezekano wa kuiiatach naomba, uitupie humu tena maana mi nilii save lakini kila napojaribu kuifungua nakuta na pingamizi la akina mods
      Soma mabandiko ya nyuma watu wame attach hiyo copy
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    16. #253
      MLETAHOJA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 73
      Rep Power : 446
      Likes Received
      27
      Likes Given
      72

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Dumela Mbegu
      Kubenea ni mnafiki na mpenda sifa hana lolote, Mbona ULIMBOKA ALIFANYIWA MCHEZO WA SODOMA NA GOMOLA hakuandika habari hizi na iko wazi ?
      Siyo kila unachokifahamu kinafaa kuandikwa. Unaandika yale yenye maslahi kwa taifa. Hilo aliloliandika lina maslahi kwa taifa maana jeshi letu la polisi limetuahidi kuwa linafanya kila jitihada kumbaini aliyemteka Ulimboka na mara zote polisi wamekuwa wakipongeza taarifa za uhalifu wanazopewa na raia wema kupitia kile wanachokiita ulinzi shirikishi. Kwa nini mara hii Mwanahalisi haipewi ushirikiano na jeshi la polisi badala yake linanyamazishwa? Hapo kuna kitu.

    17. #254
      Aristides Pastory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2012
      Posts : 347
      Rep Power : 437
      Likes Received
      58
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By artorius
      Walipofikia walimu na madaktari,tupaendeleze,hii ndo chance ya kujikomboa
      Maandamano makubwa yanakuja.... waiting a sit!

    18. #255
      LORDVILLE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Location : Imaginary island
      Posts : 1,323
      Rep Power : 615
      Likes Received
      117
      Likes Given
      141

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Kyindokyakombe
      Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

      CHANZO: TBC1

      Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

      Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.
      kama gazet limefungiwa ili kuficha uovu wao basi waamie humu JF watupashe!! nahisi kuna mwingine wata muulimboka haya tungoje!!!

    19. #256
      Sooth's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th April 2009
      Posts : 922
      Rep Power : 697
      Likes Received
      313
      Likes Given
      200

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      .... Walipokuja na sinema za Mkenya kwa Gwajima, werevu tukajua serikali haitaki kujikamata kwa kumteka na kumtesa Ulimboka. Ktk dunia ya leo na ktk mazingira ambayo Ulimboka alikuwa akiwasiliana kwa simu na watu mbalimbali kuhusiana na mgomo, haiingii akilini kwamba vyombo vyetu vya usalama havikufikiria ku-track simu zote zilizo wasiliana na Ulimboka. Jamani hawa polisi hata ukimtukana mtu kwa njia ya msg, watakushtaki au kukukamata, sembuse kwa hili ambapo mtu alitekwa na kuteswa nusura kufa?

      Kinachoonekana hapa ni kwamba serikali haitaki watu wazungumzie suala la Ulimboka kwa sababu linaiacha uchi. Pia wanajua kwamba watanzania ni wasahaulifu-suala lisipoongelewa kwa muda wanasahau. Ktk nchi makini, suala la ulimboka na sinema zinazoendelea, zingetosha kuiyumbisha serikali, lakin si hapa bongo.

      Nimalizie kwa kuwapa moyo Mwanahalisi: "You have a very good number of royal readers, including myself. We buy your paper every week, and we are willing and able to follow you anywhere!". Waiting to hear from you with regard to directions for the future....
      LORDVILLE likes this.
      "There is a very thin line between inflation and extortion."-Sooth.

    20. #257
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,484
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4303
      Likes Given
      1248

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Kubenea juu! Serikali dhaifu.

    21. #258
      MtamaMchungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 1,541
      Rep Power : 807
      Likes Received
      710
      Likes Given
      64

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Moto wa wiki iliyopita ulikuwa mkali, anyway tutafika tu.

    22. #259
      mizambwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2008
      Posts : 1,439
      Rep Power : 975
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1811

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Wajameni tunaomba mwenye nakala ya makala ya hilo Gazeti atuwekee hapa hewani.

      Tunashindwa kuelewa kwani tupo gizani wengine hatukuliona hilo gazeti la siku hiyo.

      Tuwekeeni hapa nasi tufumbue macho nimejaribu website yao, kweli inaonyesha hiyo makala ilikuwepo katika website lakini uki - click inaonyesha Website imefungiwa pia.

      Bila shaka Serikali wameifungia na Website pia kwa muda usiojulikana.



      MIZAMBWA
      INANIUMA SANA!!!
      SASA NIMEAMINI KUWA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!!!!, TUANDAE KABURI LA KUIZIKA MWAKA 2015

    23. #260
      m4cjb's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd July 2012
      Posts : 96
      Rep Power : 363
      Likes Received
      4
      Likes Given
      5

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By tusichoke
      Sijakuelewa kwamba unashabikia kufungiwa kwa gazeti au kunyimwa uhuru wa kupata taarifa za kweli? Mbona UWT hawajakanusha iwapo waliotajwa sio watumishi wao, kesho akiteswa ndugu yako utakuwa happy km gazeti likisema watu waliomtesa likifugiwa?
      hili ni dume la jike

    Page 13 of 40 FirstFirst ... 3111213141523 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...