Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

    Report Post
    Page 11 of 40 FirstFirst ... 91011121321 ... LastLast
    Results 201 to 220 of 783
    1. #1
      Kyindokyakombe's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 97
      Rep Power : 375
      Likes Received
      95
      Likes Given
      2

      Default Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

      CHANZO: TBC1

      Quote By Profesy
      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

      TAMKO LA SERIKALI

      GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA


      Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

      Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

      Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

      Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

      Uamuzi wa Serikali
      Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.

      Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

      Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.

      Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.

      Imetolewa na

      OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
      WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
      30 Julai, 2012
      Committee to Protect Journalists (CPJ) Statement;

      Tanzanian authorities ban weekly indefinitely

      Nairobi, July 30, 2012--The Tanzanian government today banned indefinitely the critical Swahili-language weekly MwanaHalisi, accusing the paper of publishing seditious articles, according to local journalists and a statement by the information ministry.

      The ministry claimed that MwanaHalisi's four July editions contained seditious and false material but did not specify particular articles. Under the 1976 Newspaper Act, Tanzanian authorities can suspend a newspaper at will if they deem that it has "seditious intent," according to CPJ research. MwanaHalisi Chief Editor Jabir Idrissa told CPJ that the paper is considering filing an appeal.

      Idrissa and other local journalists said they suspect the ban is related to a series of articles in MwanaHalisiconcerning the kidnap and torture in late June of physician Steven Ulimboka. Unknown assailants kidnapped and beat Ulimboka on the outskirts of the main commercial city Dar es Salaam after he led a doctors' strike, according to news reports. MwanaHalisi's reports suggested involvement by authorities, citing phone records of an alleged security officer, Idrissa said. Tanzanian security services and President Jakaya Kikwete have denied government involvement, according to local and international reports.

      "Once again, Tanzanian authorities have wielded an archaic newspaper act and vague, unsupported accusations of sedition to censor reporting that is merely critical of the government," said CPJ East Africa Consultant Tom Rhodes. "Authorities should reverse this ban immediately and allow MwanaHalisi to report on the Ulimboka case without fear of reprisal."

      Over the past year, Tanzanian authorities have called MwanaHalisi's editors in for questioning every two or three weeks over their articles, Idrissa said.

      Tanzanian authorities used the Newspaper Act to suspend MwanaHalisi in October 2008 for three months for articles considered seditious and insulting to the president. During the 2010 election campaign, Sethi Kamuhanda, the permanent secretary of the ministry of information, visited print media houses to warn them that the government would close down any media that portrayed the government negatively, according to local journalists.



      For more data and analysis on Tanzania, visit CPJ's Tanzania page here.


      ###
      CPJ is a New York-based, independent, nonprofit organization
      that works to safeguard press freedom worldwide.
      Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

      Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.

    2. Miaka 50

    3. #201
      sweetlady's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 24th December 2010
      Location : Tanzania
      Posts : 15,335
      Rep Power : 36534
      Likes Received
      7487
      Likes Given
      4604

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By tanga kwetu
      nilitoa photocopy 25 hii habari ya kutekwa na kuteswa kwa Dr. Ulimboka na kuigawa kwa watu mbalimbali stendi ya mabasi juzi jumapili. kwa kulifungia, baadae naenda kutoa photocopy 40 zaidi na kuzisambaza.
      Hii mbinu yako nzuri nimeipenda mie pia hapa ofisini kuna mashine ya copy.....kuanzia leo natoa makopi yasiyokuwa na idadi na kuyasambaza kwa wana wa nchi hii huku nikiwaambia kuwa ukweli huo ndio umepelekea gazeti la mwanahalisi kufungiwa !
      Life without problems never make a strong and good person!

    4. #202
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,785
      Rep Power : 27113
      Likes Received
      10116
      Likes Given
      14055

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By sister
      duh basi hilo bandiko lilinipita iasee.
      mabandiko y usiku ni noma ila sasa huwaga hayakai sana manake mengi yanakuwaga ni threat
      Tangawizi likes this.
      "thought takes man out of servitude into freedom"
      'daima tudumu katika upendo'

    5. #203
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,057
      Rep Power : 0
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By ruttashobolwa
      Huo ni unafiki na fitina za serikali.
      ni unafiki,uchochezi na upandikizaji chuki wa kubenea na mabwana zake.

    6. #204
      Tangawizi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th June 2009
      Posts : 943
      Rep Power : 693
      Likes Received
      188
      Likes Given
      184

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By MAMA POROJO
      Kapigwa marufuku kuanzisha gazeti lingine.
      Kichwa chake nacho wameking'oa au bado anacho? Kwani uwezo wa mtu uko wapi, kwenye computer anayofanyia kazi au kichwani kwenye ubongo wake? Mbona kazi mnayo.
      "Carpe Diem...Seize the Day"

    7. #205
      themagainst's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 43
      Rep Power : 425
      Likes Received
      7
      Likes Given
      2

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      kubenea,my hero.never give up


    8. #206
      MLETAHOJA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 73
      Rep Power : 446
      Likes Received
      27
      Likes Given
      72

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Ritz
      Wewe ulitegemea kama nani jeshi la polisi alifanyi kazi kienyeji kuokota habari mitaani kwa waandishi makanjanja.
      Lakini kumwokota chizi na mwehu na kusingizia kuwa ni jasusi aliyekubuhu aliyemteka ulimboka kwa ushahidi uliorukwa na Mchungaji waliyemsingizia huo ndio umakini wa jeshi la Polisi unaotaka kutuaminisha. Jeshi lipi unalolizungumzia wewe hili la Kova au jingine. Waandishi wenye elimu kubwa ya uandishi hawawezi kuwa wachochezi maana wana matarajio ya kufanywa waandishi wa Ikulu. Umeziona taarifa zao wanazotoa kwa Press. Ni nafuu za huyo unayemuita Kanjanja ambaye kwa hatua hii Serikali imemuogopa na kumpandisha chati. Kidumu chama cha mapinduzi

    9. #207
      sweetlady's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 24th December 2010
      Location : Tanzania
      Posts : 15,335
      Rep Power : 36534
      Likes Received
      7487
      Likes Given
      4604

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Mvaa Tai
      Kwa taarifa yako Ulimboka akija hataruhusiwa kuzungumzia suala lake kwasababu lipo mahakamani kwani muhusika amekwishakamatwa.
      Hahahhaa muhusika ni yule kichaa au wamemkamata tena mwingine ?
      Life without problems never make a strong and good person!

    10. #208
      Tangawizi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th June 2009
      Posts : 943
      Rep Power : 693
      Likes Received
      188
      Likes Given
      184

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By gfsonwin
      mabandiko y usiku ni noma ila sasa huwaga hayakai sana manake mengi yanakuwaga ni threat
      gfsonwin, sasa huyo Rama mbona hawakuiacha picha yake tuione?
      "Carpe Diem...Seize the Day"

    11. #209
      Shardcole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,416
      Rep Power : 1289
      Likes Received
      1040
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By Dickson Ng'hily
      Hata kama gov ya Magamba imelifungia, still bado kuna njia nyingi za kufikisha taarifa kwa public na hebu tuzitumie hizo huku tukipambana kuhakikisha Mwanahalisi anafunguliwa...Na actually tutumie wakati huu wa mabadiliko ya katika kuhakikisha sheria kandamizi kama hizi zilizotumiwa na selikali dhaifu kulifungia Mwanahalisi na mengine mengi, hazina nafasi katika kizazi chetu na kile kijacho...
      Mkuu si uhamie CHADEMA basi kubwa tupambane vizuri na hii serkali dhalimu kwani unafaa sana ila tatizo umekula fungate na CCJ.

    12. #210
      Determine's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th April 2012
      Posts : 238
      Rep Power : 404
      Likes Received
      76
      Likes Given
      96

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By ritz
      kubenea nenda kaandikie tanzania daima.
      nenda wewe
      Kikwete ni Jasiri Sana

    13. #211
      artorius's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 529
      Rep Power : 478
      Likes Received
      100
      Likes Given
      0

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Hivi tumeshindwa kweli kuitoa hii serikali?

    14. #212
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,827
      Rep Power : 1148
      Likes Received
      188
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Magesi
      Kwa mara nyingine serikali dhaifu imeshindwa kujibu hoja ya kutaka kumshughulikia Dk.Ulimboka kwa kulifungia gazet la mwanahalisi lililomtaja mtuhumiwa bila uoga huu ni udhaifu mkubwa katika kuwajibika kwa wananchi
      Kubenea amejikaanga mwenyewe hakuna UHURU WA HABARI DUNIANI USIO NA MIPAKA , HAKUNA HAKUNA. NA UHURU USIO NA MIPAKA NI SAWA SAWA NA WENDA WAZIMU. Poleni sana ila Kubenea amelipwa kinacho stahiki na hana ushujaa wowote, mie nadhani badilisha heading isomer KUBENEA NA MWANAHALISI NI WASALITI NA WANAFIKI WA TAIFA.

    15. #213
      KASHOROBANA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th July 2011
      Posts : 1,476
      Rep Power : 691
      Likes Received
      235
      Likes Given
      86

      Default Re: Kubenea na mwanahalisi ni mashujaa wa taifa

      Sasa ndo washalifungia, inamaana wengine lazima waogope vinginevyo nao watafungiwa, serikali hii si dhaifu dhidi ya wanahabari

    16. #214
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1844
      Likes Received
      593
      Likes Given
      413

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Ndahani
      Ushawahi kuona mtu anawinda mende na bunduki?

      Nimeona mtu anayewinda sisimizi kwa kifaru.
      mwita ke mwita likes this.

    17. #215
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,057
      Rep Power : 0
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Ndahani
      thatha, hata mimi sijui wana sababu zipi. Labda ni kwasababu ya toleo lao la wiki iliyopita!
      ok, lakini labda kuna jambo la msingi, unajua lile toleo liliingia ndani zaidi kiasi kwamba pengine hata kungetokea migongano kati ya vyombo vya dola, vyombo vya maamuzi na media. Nakumbuka hata baadhi ya taasisi za habari zilisema kuwa Mwanahalisi lilienda mbali zaidi.
      Ndahani likes this.

    18. #216
      Richard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2006
      Location : LANGLEY
      Posts : 2,277
      Rep Power : 1099
      Likes Received
      492
      Likes Given
      1684

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Gagnija
      Najaribu tu kufikiria, hivi Mwanahalisi wakienda mahakamani kupinga kufungiwa huku, na mahakama ikaamuru kuwa kufungiwa huko ni batili na walipwe fidia kwa hasara itokanayo, huyo atakayekuwa ameamua wafungiwe na kusababisha hasara hiyo tumchukulie hatua gani?
      Ndugu,

      Hili suala ni zito sana, na Kubenea ninavyomuaminia anazo data zote na viambatanisho kama ambavo amekuwa akifanya katika kuleta habari zake.

      Nasema hivyo kwa kutumia mifano ya habari zake za kuhusu EPA na zingine nzito.

      Mwanahalisi inaweza kupima uzito wa kifungo hicho na kama ilivyokuwa mwaka 2009 ilipofungiwa wanaweza kwenda mahakamani ingawa hawatoweza kushinda kesi kutokana na mahakama hiyohiyo kuwa moja ya mihimili ya serikali.

      Lakini kwa kupitia baraza la habari ambalo nalo huchaguliwa na lipo kwenye payroll ya serikali pia suala hilo linaweza kuangaliwa ingawa waziri wa wizara husika ambae ndie alietoa agizo la kufungiwa nae amefuata uamuzi wa vikao vya dharura.

      Pia chanzo cha habari cha bwana Said Kubenea nacho kinaweza kuwa matatizoni kwa ama kuhatarisha maisha yake au ya Kubenea au wote wawili.

      Kwahio bado tunasubiri toleo la filamu ya Mabwepane and Wrath of the Pliers mwaka 2015, inshaalah!.
      Gagnija likes this.
      When thinking about my risk assessment, I always remember:
      HAZARD and the RISK .

    19. #217
      CHABURUMA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 26th June 2012
      Posts : 128
      Rep Power : 373
      Likes Received
      13
      Likes Given
      8

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Tuliyajua hayo kitambo kweli yametimia. Siku zenu za kukaa madarakani zinahesabika.

    20. #218
      Nicas Mtei's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st December 2010
      Location : Shamba
      Posts : 8,651
      Rep Power : 32147
      Likes Received
      5004
      Likes Given
      5177

      Default

      Quote By Shardcole
      Mkuu si uhamie CHADEMA basi kubwa tupambane vizuri na hii serkali dhalimu kwani unafaa sana ila tatizo umekula fungate na CCJ.
      Kwani yupo chama gani huyo? 2010 algombea ubunge Temeke kwa kuptia Chadema.

    21. #219
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,785
      Rep Power : 27113
      Likes Received
      10116
      Likes Given
      14055

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Quote By Tangawizi
      gfsonwin, sasa huyo Rama mbona hawakuiacha picha yake tuione?
      hebu nenda post 202 unaweza kumuona.
      "thought takes man out of servitude into freedom"
      'daima tudumu katika upendo'

    22. #220
      Tram Almasi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 26th February 2009
      Location : Marsabit
      Posts : 753
      Rep Power : 672
      Likes Received
      217
      Likes Given
      92

      Default Re: Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

      Mhh!Ukweli na Uwazi!Oh me Oh my!
      "YouR MoST UNhaPPy CuSToMers ArE YoUr GREateST SOurCE Of LEarNInG"- BiLL GaTEs

    Page 11 of 40 FirstFirst ... 91011121321 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...