Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

    Report Post
    Page 1 of 30 12311 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 587
    1. #1
      raymg's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 643
      Rep Power : 475
      Likes Received
      143
      Likes Given
      15

      Default Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Sasa hivi wanafunzi kata ya ilemela mkoa wa mwanza wapo katika maandamano wakiwa na mabango tofauti yenye maandishi "tunataka haki zetu" wakielekea mahakama ya mwanzo wilaya ya ilemela kufungua kesi zidi ya waalimu kwa kukataa kuwafundisha...

      UPDATES:





      Wanafunzi wa shule za Msingi za Temeke wakiingia kwenye ofisi za Manispaa ya Temeke kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana na kuwasababishia kukosa masomo. Picha na Elizabeth Edward - Gazeti la Mwananchi

      - TBC1 imeripoti kuwa Ruvuma walimu wamegoma na imethibitisha vurugu kutokea mkoani Mbeya na kuwa nako walimu wamegoma.


      Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiandamana jana Jumatatu Julai 30, 2012, kupinga haki yao ya msingi ya kupata elimu kuvurugwa kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana. Wanafunzi hao waliandamana umbali wa kilomite 10 hadi ofisi za Afisa elimu wa manispaa hiyo na kueleza "kesi" yao ambapo wameitaka serikali kumalizana na walimu ili wao wasome.

      Quote By ugali wa asubuhi
      Rais wa chama cha walimu mkoani Mara ameonekana akitembea na silaha za jadi kama sime na mishale kwa ajiri ya kujihami akihofia kutekwa kama ilivyotokea kwa Dr Ulimboka.

      Source: Wapo Radio
      Quote By MASIKITIKO
      Singida:

      Wanafunzi wamekusanyika ofisi ya mkuu wa Mkoa muda huu mkoa wa Singida.
      Quote By agapetc
      Hayawi hayawi sasa yamekuwa, walimu wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Korogwe wamegoma kwenda shule kwa kuunga mkono viongozi wao walioutangaza.

      Shule nyingi zimeonekana walimu wakuu na wakuu wa shule tu ndiyo waliohudhuria maofisini, pia imebainika kuwa walimu wa sekondari wanaongoza kwa kutoenda kazini wakati shule za msingi imebainika walimu ktk shule chache wameenda kazini.
      Quote By Leonard Robert
      Huku Tanga wamefanya kweli, shule zilizonizunguka zote watoto wako wanacheza kaponda, hamna kinachoendelea, nimeongea na mwalimu mkuu mmoja hapa amesema kugoma kuko palepale na amesema leo hafungui hato ofisi..

      Kama nchi nzima ni hivi basi walimu wameamua
      Quote By Steve1
      Iringa Mjini nako kimenuka, ni walimu wakuu peke yao wapo vituo vya kazi.
      Quote By mtendaji wa kijiji
      Huku Wilaya ya Same nako kimenuka.

      Nimepita shule za Njoro, Ishinde, Majevu, Kisima, Makanya na Nkwini hakuna waalimu shuleni wanafunzi wametelekezwa
      Quote By Goldman
      Tunduma wanafunzi wakati wanaandamana, FFU wamewapiga bomu la machozi, sasa watu wakubwa wameingilia, gate la kwenda Zambia limefungwa kwa muda hakuna gari kuvuka!
      Quote By mpenda pombe
      Nipo huku Tabora, shule nyingi za mjini zimefungwa waalimu wamegoma, isipokua shule moja tu ya Msingi Mtendeni wapo waalimu wawili tu..

      Nitaendelea kuwajuza..
      Quote By Micro E coli
      Na huku Tegeta, Boko kimenuka. Mfano, Boko Secondary - hakuna walimu waliofika.
      Quote By Kiumbo
      Kibaha Mlandizi shule karibia zote msingi na sekondari hakuna walimu kabisa. Wanafunzi wamefurahi leo utawala binafsi kutoroka wakati wenzao wanaandamana.
      Eddy Kinawiro huku Kimara wanafunzi wa Shule ya Msing Kimara B wamerudi wote kutokana na kuwa shuleni hakuna walimu
      Quote By KIFUBA KYA ITAHWA
      Huku Bukoba nako kimenuka nipo Bukoba mjini hakuna walimu walioenda kazini na sekondari ndo kabisa hazina watu
      Quote By nolakinabo
      Katika mkoa wa Kilimanjaro:

      Katika shule za msingi walimu wakuu wameonekana wakiwahi shuleni huku wakiwa hawaelewi mgomo upo vipi "Mi siwezi kugoma nimebakiza mwaka mmoja kustaafu" mwalimu mkuu mmoja alisema.

      Hali hii inaonekana kuwa mgomo huu hauna nguvu walimu wakuu wanawalazimisha walimu wao kufundisha..

      Nako mkoani Arusha hali ni tete, nikiwa Karatu Mjini shule nazo hazina walimu, wanafunzi; wapo walimu wakuu hasa wale wenye umri wamekuwa waoga kugoma
      Quote By MotoYaMbongo
      Urambo Mkoani Tabora, wanafunzi za sekondari wamesambaa mitaani, wa shule za msingi wametawanywa na walimu wakuu wao.
      Quote By nachid
      Iringa naona watoto wapo mtaani wanaserebuka
      Quote By Gwaje
      Nipo Igunga hapa mjini, kuna shule inaitwa Igunga Day nimeongea na walimu wamesema hawajaenda kazini ila kwa taarifa waliyonayo mkuu pekee ndie yuko kazini Safisana
      Quote By summa
      DODOMA
      walimu hawapo shuleni na baadhi ya shule wamerudi nyumbani kabisa
      Quote By Barnabas Shadrack
      Huku Mwanza kuna shule nyingi walimu wamehudhuria shuleni lakini wamekaa nje tu wakiwa wanaota jua.
      Quote By Bajabiri
      Rafiki yangu ni mwalimu wa Halmashauri ya CHUNYA ameni-sms kuwa WAO WAMEFUNGA SHULE
      Quote By Adolph
      Huku Kibaha napo kimenuka. Wanafunzi wamerudi majumbani kwao. Hakuna kinachoendelea!
      Quote By MotoYaMbongo
      Urambo Mkoani Tabora, wanafunzi za sekondari wamesambaa mitaani, wa shule za msingi wametawanywa na walimu wakuu wao.

      Mgomo umefanikiwa, walimu kaza uzi.
      Quote By nachid
      Iringa naona watoto wapo mtaani wanaserebuka
      Quote By Gwaje
      Nipo igunga hapa mjuni kuna shule inaitwa Igunga Day nimeongea na walimu wamesema hawajaenda kazini ila kwa taarifa waliyonayo mkuu pekee ndie yuko kazini Safisana
      Quote By summa
      DODOMA
      walimu hawapo shuleni na baadhi ya shule wamerudi nyumbani kabisa
      SOLIDARITY 4 EVER
      Quote By Barnabas Shadrack
      Huku Mwanza kuna shule nyingi walimu wamehudhuria shuleni lakini wamekaa nje tu wakiwa wanaota jua.
      Quote By Bajabiri
      Rafiki yangu ni mwalim wa halmashaur ya CHUNYA ameni-sms kuwa WAO WAMEFUNGA SHULE
      Quote By Adolph
      Huku kibaha napo kimenuka..wanafunzi wamerudi majumbani kwao..hakuna kinachoendelea!
      Quote By samilakadunda
      Taarifa toka mkoa wa Morogoro:

      Wanafunzi wanarudi nyumbani, secondary kwa Misinga wanafunzi wanazagaa mjini, hadi kieleweke, nimeongea na baadhi ya wanafunzi wanasema warudi nyumbani kwa kuwa waalimu hawapo mashuleni.
      Lucas Sabuni Baadhi ya S/M Nzega mjini wanafunzi wamerudi majumbani hakuna walimu mashuleni.
      Quote By Neiwa
      Upande wa Tunduma vurugu za wanafunzi zimetulia sasa (au niseme zimetulizwa); Hayo maandamano ya wanafunzi yalipelekea boarder ya upande wa Tunduma kusimamisha shuguli zake (sio kufungwa) kwa hofu ya usalama wa mali za wasafiri wanaotumia huo mpaka hasa magari ambayo huwa kwa wingi maeneo hayo.

      Hata hivo so far shughuli zinaendelea kama kawaida kwa sasa katika offisi hizo za Migration hapo mpakani.
      Quote By msweken
      Mgomo hadi shule za vijijini kabisa, wife anafundisha mpwapwa kanambia mkuu wa shule pekee ndiye aliyeenda kituo cha kazi, walimu wengine wote hakuna aliyejitingisha, wapo makwao wanafanya mambo yao..!!
      Quote By Getsemane
      Mbozi:
      Huku pia hapa Vwawa watoto wamegoma na wameandamana hadi kwenye ofisi za halmashauri(Bomani) ambapo pia ofisi za mkuu wa wilaya zipo. Mtaani pia watoto wamezagaa na wimbo wao ule ule "Tunataka haki zetu" wameongeza tena kuwa "Hatutaki kupewa rushwa"
      Quote By master gland
      Hapa mkoani Mtwara na wilaya zake zote ikiwemo Newala, Masasi, Tandahimba, Nanyumbu, Mtwara mjini hali ni tete hakuna walimu zaidi ya wakuu wa shule.

      MAAFISA ELIMU WANARANDARANDA MASHULENI NA FORM ZAO NA WANAKOSA WAKUMSAHINISHA HALI NI TETE
      Quote By Echolima
      Niko Kahama mjini Mgomo wa waalimu unaendelea kama kawaida
      Simon Mwangoka Mwasile Shule ya secondary Uyole na shule ya msingi Itezi zilizoko katika jiji la mbeya wamegoma 99% nimeshuhudia mwenyewe kwa kutembelea maeneo husika.
      Quote By Mikael P Aweda
      Kisarawe, karibu shule zote hakuna walimu. Wanafunzi wanacheza shuleni.

      Source: Mimi mwenyewe niko huku kikazi.
      Quote By Kengedume
      Nimezungu takribani shule kadhaa hapa ndani ya manispaa ya Shinyanga, mpaka dakika hii wanafunzi wametapakaa nje ya madarasa wanacheza tangu asubuhi! Shule ya msingi Ushirika, Bugoi, Chamaguha na n.k

      Kimenuka mbaya!
      Quote By Naytsory
      Hanang' shule ya sekondari Mahu wanafunzi wamefunga barabara ya kwenda Singida kwa kutumia madawati, hivi sasa polisi na ofisi ya elimu wamekwenda kule kutuliza hali.
      Walimu wameitikia mgomo kwa zaidi ya 90% kwani shuleni wapo wapo wakuu wa shule na walimu wa field na wale wa kujitolea, shule za msingi wapo walimu wakuu tu.

      Hivyo ndivyo hali ilivyo kwa Hanang' leo nilipofika hapa Katesh makao makuu ya wilaya.
      Quote By ukwelikitugani
      Mfa maji haachi kutapatapa,Wahenga walisema. Imekuwa kawaida kwa CCM, Bwana Kikwete na wana-Propaganda wake kutafuta mchawi wa migomo na migogoro mbalimbali badala ya kutafuta suluhisho la kudumu la ufumbuzi wake. Mtakumbuka matukio kadhaa yalitokea,mfano:

      1. Maandamano ya Wanavyuo,kudai mikopo na kuboreshwa mazingira.. Walijitokeza watetezi wengi na makada wa CCM kudai ati ni Chadema wanaohusika. (impact yake- ccm kupoteza kukubalika vyuoni).
      2. Ukaja mgomo wj madaktari na crucifiction ya bwana-Daktari Ulimboka. Hapa Kikwete, CCM yake na vibaraka wao TISS waliwatuhumu Chadema kuwa nyuma ya wadai haki zao (madaktari). (Impact yake- CCM kuonekana bulshit katika jamii ya madaktari)!
      3. Mgomo wa Walimu.. Hali inavyoelekea,si punde itatamkwa Chadema wapo nyuma ya wadai haki hawa. Natamani sana wataalam wa propaganda wa bwana JMK na chama lake wajitokeze na kuwakemea walim waache kutumiwa na CHADEMA..

      My take:- Ni uwezo mdogo wa kiuongozi na utawala alionao kikwete,kukimbilia visingizio kama chaka la kuficha udhaifu.
      :- Natoa wito kwa walim kwa kuwa wapo wengi,na wana mtandao mkubwa kila kona ya nchi, basi wawe mashuhuda wa kuwa CHADEMA ndio watetezi wa haki kwani hata CCM wanakiri hivyo,na kubwa zaidi thamani yenu mbele ya chama tawala ni ndogo mno.
      Quote By fmpiganaji
      Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mwanza, Thadaeus Ruwa'ichi ameonya kuwa taifa ambalo linachezea elimu halitathaminika popote huku akisema madai ya walimu ni ya msingi.
      ...
      Source: Mwananchi Alhamisi (Leo)
      Quote By harakat
      Kitendo cha baadhi ya waalimu kwenda shule na kuweka mgomo baridi kunywa chai na kuendelea kupiga soga
      kimezungumziwa na mukoba kwamba sio kizuri wote wakae makwao waendelee na shughuli nyingine ikiwemo mikakati ya kujiajiri
      "“Mgomo huu hauna ukomo, ni Serikali tu ndiyo itakayoamua uishe au uendelee. Tukipewa nyongeza tunazotaka utaisha lakini tusipopewa utaendelea milele,” alisema Mukoba. Jana ilikuwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa mgomo huo.

      Alisema mgomo huo ni wa mafanikio makubwa, kwa sababu unahusisha asilimia 95 ya walimu... “Walimu wachache wanaoendelea kwenda shuleni ni waoga, wanafiki wenye kujipendekeza ili wapate vyeo na wanasaliti wenzao wanaodai haki zao,” alisema.

      hapa naendelea kuungana nae moja kwa moja "solidarity 4reva"

    2. Miaka 50

    3. #2
      Gedeli's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th March 2012
      Posts : 187
      Rep Power : 399
      Likes Received
      47
      Likes Given
      114

      Default re: Wanafunzi shule ya msingi Ilemela waandamana kupinga mgomo wa walimu

      wanaongozwa na nani si rahisi wanafunzi wa shule ya msingi kujikusanya na kufanya kitu kama hicho
      mkada likes this.

    4. #3
      Msalagambwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2012
      Posts : 535
      Rep Power : 452
      Likes Received
      177
      Likes Given
      527

      Default re: Wanafunzi shule ya msingi Ilemela waandamana kupinga mgomo wa walimu

      Mahakama ya mwanzo?

    5. #4
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,417
      Rep Power : 5038
      Likes Received
      782
      Likes Given
      1785

      Default re: Wanafunzi shule ya msingi Ilemela waandamana kupinga mgomo wa walimu

      Ambatanisha na picha mkuu!!
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    6. #5
      MASIKITIKO's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th December 2011
      Posts : 205
      Rep Power : 478
      Likes Received
      28
      Likes Given
      2

      Default Mgomo wa walimu wanafunzi wakusanyika ofisi ya mkuu wa mkoa singida

      Singida:

      Wanafunzi wamekusanyika ofisi ya mkuu wa Mkoa muda huu mkoa wa Singida.
      CHANGER likes this.

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      agapetc's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st July 2012
      Posts : 29
      Rep Power : 349
      Likes Received
      4
      Likes Given
      20

      Default korogwe mgomo wa waalimu umetekelezwa

      Hayawi hayawi sasa yamekuwa, walimu wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Korogwe wamegoma kwenda shule kwa kuunga mkono viongozi wao walioutangaza.

      Shule nyingi zimeonekana walimu wakuu na wakuu wa shule tu ndiyo waliohudhuria maofisini, pia imebainika kuwa walimu wa sekondari wanaongoza kwa kutoenda kazini wakati shule za msingi imebainika walimu ktk shule chache wameenda kazini.

      Migomo kila kukicha inaashiria nini ktk nchi hii?
      KOKUTONA likes this.

    9. #7
      Kiumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 463
      Likes Received
      71
      Likes Given
      0

      Default re: Wanafunzi shule ya msingi Ilemela waandamana kupinga mgomo wa walimu

      Wanaongoza na nani. Eti mabango na huku hawajui kusoma na kuandika. Magamba kazini. Hawatuwezi tumechoka ngoja niendelee kulala.

    10. #8
      Kiumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 463
      Likes Received
      71
      Likes Given
      0

      Default Re: korogwe mgomo wa waalimu umetekelezwa

      Mapinduzi daima.

    11. #9
      manucho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Posts : 561
      Rep Power : 469
      Likes Received
      79
      Likes Given
      0

      Default re: Wanafunzi shule ya msingi Ilemela waandamana kupinga mgomo wa walimu

      Ni wa shule ya msingi sekondari au chekechea wanaelekea mahakamani kwenda kufungua kesi

    12. #10
      Kiumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 463
      Likes Received
      71
      Likes Given
      0

      Default Re: Mgomo wa walimu wanafunzi wakusanyika ofisi ya mkuu wa mkoa singida

      Mapinduzi daima.

    13. #11
      Leonard Robert's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2011
      Posts : 4,247
      Rep Power : 1262
      Likes Received
      522
      Likes Given
      175

      Default Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Huku Tanga wamefanya kweli, shule zilizonizunguka zote watoto wako wanacheza kaponda, hamna kinachoendelea, nimeongea na mwalimu mkuu mmoja hapa amesema kugoma kuko palepale na amesema leo hafungui hato ofisi..

      Kama nchi nzima ni hivi basi walimu wameamua

    14. #12
      Leonard Robert's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2011
      Posts : 4,247
      Rep Power : 1262
      Likes Received
      522
      Likes Given
      175

      Default re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      huko kwingine vipi wadau?

    15. #13
      Msalagambwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2012
      Posts : 535
      Rep Power : 452
      Likes Received
      177
      Likes Given
      527

      Default Re: Mgomo wa walimu wanafunzi wakusanyika ofisi ya mkuu wa mkoa singida

      Kufanya nini kwa mkuu wa mkoa?

    16. #14
      LiverpoolFC's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2011
      Posts : 6,658
      Rep Power : 11273
      Likes Received
      1468
      Likes Given
      570

      Default Re: Wanafunzi shule ya msingi Ilemela waandamana kupinga mgomo wa walimu

      Hebu funguka vema Mkubwa!

      Wanafunzi wamefika leo shuleni wakauta walimu hawapo ama?

      Au wamefika wakashauriwa na walimu waandamane!

    17. #15
      zubedayo_mchuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2011
      Posts : 3,343
      Rep Power : 1058
      Likes Received
      588
      Likes Given
      43

      Default

      Quote By Msalagambwe
      Kufanya nini kwa mkuu wa mkoa?
      Kuchukua kwizi ya Uraia na kiswahl

    18. #16
      Gilo24's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 557
      Rep Power : 490
      Likes Received
      132
      Likes Given
      538

      Default Re: Mgomo wa walimu wanafunzi wakusanyika ofisi ya mkuu wa mkoa singida

      more updates tafadhali

    19. #17
      Mpita Njia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 6,698
      Rep Power : 3254
      Likes Received
      979
      Likes Given
      753

      Default Re: Mgomo wa walimu wanafunzi wakusanyika ofisi ya mkuu wa mkoa singida

      Quote By MASIKITIKO
      Wanafunzi wamekusanyika ofisi ya mkuu wa Mkoa muda huu.
      wanataka nini hapo?
      I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.

    20. #18
      Mpita Njia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 6,698
      Rep Power : 3254
      Likes Received
      979
      Likes Given
      753

      Default Re: Wanafunzi shule ya msingi Ilemela waandamana kupinga mgomo wa walimu

      tutasikia mengi leo
      I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.

    21. #19
      zubedayo_mchuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2011
      Posts : 3,343
      Rep Power : 1058
      Likes Received
      588
      Likes Given
      43

      Default

      Quote By Kiumbo
      Wanaongoza na nani. Eti mabango na huku hawajui kusoma na kuandika. Magamba kazini. Hawatuwezi tumechoka ngoja niendelee kulala.
      Wanaenda kufungua kesi juu wenzao walio maliza mwaka jana.wakafaulu lakini hawajui kusoma...

    22. #20
      Steve1's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 26th August 2011
      Posts : 7
      Rep Power : 392
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Gilo24
      more updates tafadhali
      iringa wanafunz wanajpgia misele mtaan.

    Page 1 of 30 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...