Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

    Report Post
    Page 14 of 30 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast
    Results 261 to 280 of 587
    1. #1
      raymg's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 644
      Rep Power : 475
      Likes Received
      144
      Likes Given
      15

      Default Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Sasa hivi wanafunzi kata ya ilemela mkoa wa mwanza wapo katika maandamano wakiwa na mabango tofauti yenye maandishi "tunataka haki zetu" wakielekea mahakama ya mwanzo wilaya ya ilemela kufungua kesi zidi ya waalimu kwa kukataa kuwafundisha...

      UPDATES:





      Wanafunzi wa shule za Msingi za Temeke wakiingia kwenye ofisi za Manispaa ya Temeke kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana na kuwasababishia kukosa masomo. Picha na Elizabeth Edward - Gazeti la Mwananchi

      - TBC1 imeripoti kuwa Ruvuma walimu wamegoma na imethibitisha vurugu kutokea mkoani Mbeya na kuwa nako walimu wamegoma.


      Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiandamana jana Jumatatu Julai 30, 2012, kupinga haki yao ya msingi ya kupata elimu kuvurugwa kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana. Wanafunzi hao waliandamana umbali wa kilomite 10 hadi ofisi za Afisa elimu wa manispaa hiyo na kueleza "kesi" yao ambapo wameitaka serikali kumalizana na walimu ili wao wasome.

      Quote By ugali wa asubuhi
      Rais wa chama cha walimu mkoani Mara ameonekana akitembea na silaha za jadi kama sime na mishale kwa ajiri ya kujihami akihofia kutekwa kama ilivyotokea kwa Dr Ulimboka.

      Source: Wapo Radio
      Quote By MASIKITIKO
      Singida:

      Wanafunzi wamekusanyika ofisi ya mkuu wa Mkoa muda huu mkoa wa Singida.
      Quote By agapetc
      Hayawi hayawi sasa yamekuwa, walimu wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Korogwe wamegoma kwenda shule kwa kuunga mkono viongozi wao walioutangaza.

      Shule nyingi zimeonekana walimu wakuu na wakuu wa shule tu ndiyo waliohudhuria maofisini, pia imebainika kuwa walimu wa sekondari wanaongoza kwa kutoenda kazini wakati shule za msingi imebainika walimu ktk shule chache wameenda kazini.
      Quote By Leonard Robert
      Huku Tanga wamefanya kweli, shule zilizonizunguka zote watoto wako wanacheza kaponda, hamna kinachoendelea, nimeongea na mwalimu mkuu mmoja hapa amesema kugoma kuko palepale na amesema leo hafungui hato ofisi..

      Kama nchi nzima ni hivi basi walimu wameamua
      Quote By Steve1
      Iringa Mjini nako kimenuka, ni walimu wakuu peke yao wapo vituo vya kazi.
      Quote By mtendaji wa kijiji
      Huku Wilaya ya Same nako kimenuka.

      Nimepita shule za Njoro, Ishinde, Majevu, Kisima, Makanya na Nkwini hakuna waalimu shuleni wanafunzi wametelekezwa
      Quote By Goldman
      Tunduma wanafunzi wakati wanaandamana, FFU wamewapiga bomu la machozi, sasa watu wakubwa wameingilia, gate la kwenda Zambia limefungwa kwa muda hakuna gari kuvuka!
      Quote By mpenda pombe
      Nipo huku Tabora, shule nyingi za mjini zimefungwa waalimu wamegoma, isipokua shule moja tu ya Msingi Mtendeni wapo waalimu wawili tu..

      Nitaendelea kuwajuza..
      Quote By Micro E coli
      Na huku Tegeta, Boko kimenuka. Mfano, Boko Secondary - hakuna walimu waliofika.
      Quote By Kiumbo
      Kibaha Mlandizi shule karibia zote msingi na sekondari hakuna walimu kabisa. Wanafunzi wamefurahi leo utawala binafsi kutoroka wakati wenzao wanaandamana.
      Eddy Kinawiro huku Kimara wanafunzi wa Shule ya Msing Kimara B wamerudi wote kutokana na kuwa shuleni hakuna walimu
      Quote By KIFUBA KYA ITAHWA
      Huku Bukoba nako kimenuka nipo Bukoba mjini hakuna walimu walioenda kazini na sekondari ndo kabisa hazina watu
      Quote By nolakinabo
      Katika mkoa wa Kilimanjaro:

      Katika shule za msingi walimu wakuu wameonekana wakiwahi shuleni huku wakiwa hawaelewi mgomo upo vipi "Mi siwezi kugoma nimebakiza mwaka mmoja kustaafu" mwalimu mkuu mmoja alisema.

      Hali hii inaonekana kuwa mgomo huu hauna nguvu walimu wakuu wanawalazimisha walimu wao kufundisha..

      Nako mkoani Arusha hali ni tete, nikiwa Karatu Mjini shule nazo hazina walimu, wanafunzi; wapo walimu wakuu hasa wale wenye umri wamekuwa waoga kugoma
      Quote By MotoYaMbongo
      Urambo Mkoani Tabora, wanafunzi za sekondari wamesambaa mitaani, wa shule za msingi wametawanywa na walimu wakuu wao.
      Quote By nachid
      Iringa naona watoto wapo mtaani wanaserebuka
      Quote By Gwaje
      Nipo Igunga hapa mjini, kuna shule inaitwa Igunga Day nimeongea na walimu wamesema hawajaenda kazini ila kwa taarifa waliyonayo mkuu pekee ndie yuko kazini Safisana
      Quote By summa
      DODOMA
      walimu hawapo shuleni na baadhi ya shule wamerudi nyumbani kabisa
      Quote By Barnabas Shadrack
      Huku Mwanza kuna shule nyingi walimu wamehudhuria shuleni lakini wamekaa nje tu wakiwa wanaota jua.
      Quote By Bajabiri
      Rafiki yangu ni mwalimu wa Halmashauri ya CHUNYA ameni-sms kuwa WAO WAMEFUNGA SHULE
      Quote By Adolph
      Huku Kibaha napo kimenuka. Wanafunzi wamerudi majumbani kwao. Hakuna kinachoendelea!
      Quote By MotoYaMbongo
      Urambo Mkoani Tabora, wanafunzi za sekondari wamesambaa mitaani, wa shule za msingi wametawanywa na walimu wakuu wao.

      Mgomo umefanikiwa, walimu kaza uzi.
      Quote By nachid
      Iringa naona watoto wapo mtaani wanaserebuka
      Quote By Gwaje
      Nipo igunga hapa mjuni kuna shule inaitwa Igunga Day nimeongea na walimu wamesema hawajaenda kazini ila kwa taarifa waliyonayo mkuu pekee ndie yuko kazini Safisana
      Quote By summa
      DODOMA
      walimu hawapo shuleni na baadhi ya shule wamerudi nyumbani kabisa
      SOLIDARITY 4 EVER
      Quote By Barnabas Shadrack
      Huku Mwanza kuna shule nyingi walimu wamehudhuria shuleni lakini wamekaa nje tu wakiwa wanaota jua.
      Quote By Bajabiri
      Rafiki yangu ni mwalim wa halmashaur ya CHUNYA ameni-sms kuwa WAO WAMEFUNGA SHULE
      Quote By Adolph
      Huku kibaha napo kimenuka..wanafunzi wamerudi majumbani kwao..hakuna kinachoendelea!
      Quote By samilakadunda
      Taarifa toka mkoa wa Morogoro:

      Wanafunzi wanarudi nyumbani, secondary kwa Misinga wanafunzi wanazagaa mjini, hadi kieleweke, nimeongea na baadhi ya wanafunzi wanasema warudi nyumbani kwa kuwa waalimu hawapo mashuleni.
      Lucas Sabuni Baadhi ya S/M Nzega mjini wanafunzi wamerudi majumbani hakuna walimu mashuleni.
      Quote By Neiwa
      Upande wa Tunduma vurugu za wanafunzi zimetulia sasa (au niseme zimetulizwa); Hayo maandamano ya wanafunzi yalipelekea boarder ya upande wa Tunduma kusimamisha shuguli zake (sio kufungwa) kwa hofu ya usalama wa mali za wasafiri wanaotumia huo mpaka hasa magari ambayo huwa kwa wingi maeneo hayo.

      Hata hivo so far shughuli zinaendelea kama kawaida kwa sasa katika offisi hizo za Migration hapo mpakani.
      Quote By msweken
      Mgomo hadi shule za vijijini kabisa, wife anafundisha mpwapwa kanambia mkuu wa shule pekee ndiye aliyeenda kituo cha kazi, walimu wengine wote hakuna aliyejitingisha, wapo makwao wanafanya mambo yao..!!
      Quote By Getsemane
      Mbozi:
      Huku pia hapa Vwawa watoto wamegoma na wameandamana hadi kwenye ofisi za halmashauri(Bomani) ambapo pia ofisi za mkuu wa wilaya zipo. Mtaani pia watoto wamezagaa na wimbo wao ule ule "Tunataka haki zetu" wameongeza tena kuwa "Hatutaki kupewa rushwa"
      Quote By master gland
      Hapa mkoani Mtwara na wilaya zake zote ikiwemo Newala, Masasi, Tandahimba, Nanyumbu, Mtwara mjini hali ni tete hakuna walimu zaidi ya wakuu wa shule.

      MAAFISA ELIMU WANARANDARANDA MASHULENI NA FORM ZAO NA WANAKOSA WAKUMSAHINISHA HALI NI TETE
      Quote By Echolima
      Niko Kahama mjini Mgomo wa waalimu unaendelea kama kawaida
      Simon Mwangoka Mwasile Shule ya secondary Uyole na shule ya msingi Itezi zilizoko katika jiji la mbeya wamegoma 99% nimeshuhudia mwenyewe kwa kutembelea maeneo husika.
      Quote By Mikael P Aweda
      Kisarawe, karibu shule zote hakuna walimu. Wanafunzi wanacheza shuleni.

      Source: Mimi mwenyewe niko huku kikazi.
      Quote By Kengedume
      Nimezungu takribani shule kadhaa hapa ndani ya manispaa ya Shinyanga, mpaka dakika hii wanafunzi wametapakaa nje ya madarasa wanacheza tangu asubuhi! Shule ya msingi Ushirika, Bugoi, Chamaguha na n.k

      Kimenuka mbaya!
      Quote By Naytsory
      Hanang' shule ya sekondari Mahu wanafunzi wamefunga barabara ya kwenda Singida kwa kutumia madawati, hivi sasa polisi na ofisi ya elimu wamekwenda kule kutuliza hali.
      Walimu wameitikia mgomo kwa zaidi ya 90% kwani shuleni wapo wapo wakuu wa shule na walimu wa field na wale wa kujitolea, shule za msingi wapo walimu wakuu tu.

      Hivyo ndivyo hali ilivyo kwa Hanang' leo nilipofika hapa Katesh makao makuu ya wilaya.
      Quote By ukwelikitugani
      Mfa maji haachi kutapatapa,Wahenga walisema. Imekuwa kawaida kwa CCM, Bwana Kikwete na wana-Propaganda wake kutafuta mchawi wa migomo na migogoro mbalimbali badala ya kutafuta suluhisho la kudumu la ufumbuzi wake. Mtakumbuka matukio kadhaa yalitokea,mfano:

      1. Maandamano ya Wanavyuo,kudai mikopo na kuboreshwa mazingira.. Walijitokeza watetezi wengi na makada wa CCM kudai ati ni Chadema wanaohusika. (impact yake- ccm kupoteza kukubalika vyuoni).
      2. Ukaja mgomo wj madaktari na crucifiction ya bwana-Daktari Ulimboka. Hapa Kikwete, CCM yake na vibaraka wao TISS waliwatuhumu Chadema kuwa nyuma ya wadai haki zao (madaktari). (Impact yake- CCM kuonekana bulshit katika jamii ya madaktari)!
      3. Mgomo wa Walimu.. Hali inavyoelekea,si punde itatamkwa Chadema wapo nyuma ya wadai haki hawa. Natamani sana wataalam wa propaganda wa bwana JMK na chama lake wajitokeze na kuwakemea walim waache kutumiwa na CHADEMA..

      My take:- Ni uwezo mdogo wa kiuongozi na utawala alionao kikwete,kukimbilia visingizio kama chaka la kuficha udhaifu.
      :- Natoa wito kwa walim kwa kuwa wapo wengi,na wana mtandao mkubwa kila kona ya nchi, basi wawe mashuhuda wa kuwa CHADEMA ndio watetezi wa haki kwani hata CCM wanakiri hivyo,na kubwa zaidi thamani yenu mbele ya chama tawala ni ndogo mno.
      Quote By fmpiganaji
      Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mwanza, Thadaeus Ruwa'ichi ameonya kuwa taifa ambalo linachezea elimu halitathaminika popote huku akisema madai ya walimu ni ya msingi.
      ...
      Source: Mwananchi Alhamisi (Leo)
      Quote By harakat
      Kitendo cha baadhi ya waalimu kwenda shule na kuweka mgomo baridi kunywa chai na kuendelea kupiga soga
      kimezungumziwa na mukoba kwamba sio kizuri wote wakae makwao waendelee na shughuli nyingine ikiwemo mikakati ya kujiajiri
      "“Mgomo huu hauna ukomo, ni Serikali tu ndiyo itakayoamua uishe au uendelee. Tukipewa nyongeza tunazotaka utaisha lakini tusipopewa utaendelea milele,” alisema Mukoba. Jana ilikuwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa mgomo huo.

      Alisema mgomo huo ni wa mafanikio makubwa, kwa sababu unahusisha asilimia 95 ya walimu... “Walimu wachache wanaoendelea kwenda shuleni ni waoga, wanafiki wenye kujipendekeza ili wapate vyeo na wanasaliti wenzao wanaodai haki zao,” alisema.

      hapa naendelea kuungana nae moja kwa moja "solidarity 4reva"

    2. Miaka 50

    3. #261
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,777
      Rep Power : 27111
      Likes Received
      10114
      Likes Given
      14052

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      mbona na bado?????????? hapa hatukubali hadi kieleweke aisee tumechoka ile mbaya huko mlandizi ukionekana mwl unakwenda shule unapigwa kama mbwa mwizi chezeya waalim this time?
      Kyaiyembe likes this.
      "thought takes man out of servitude into freedom"
      'daima tudumu katika upendo'

    4. #262
      Paul Kijoka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th October 2010
      Location : KIMARA, DAR
      Posts : 1,337
      Rep Power : 702
      Likes Received
      226
      Likes Given
      172

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Vipi home Kagera kunajiri nini?

    5. #263
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,140
      Rep Power : 606
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Quote By gfsonwin
      mbona na bado?????????? hapa hatukubali hadi kieleweke aisee tumechoka ile mbaya huko mlandizi ukionekana mwl unakwenda shule unapigwa kama mbwa mwizi chezeya waalim this time?
      Nimetoka kuongea na dada yangu ni mwalimu kaniambia kuwa AMEGOMA.
      Huyu alikuwa akiwashangaa watu waliokuwa wakigoma kipindi kilichopita. Nilipomuuliza kuwa imekuwaje safari hii amegoma?
      Majibu yameniacha mdomo wazi maana kasema kuwa;
      "Nimekuwa nikifuatilia madai yangu kila wakati, lakini kila kukiwepo na matumaini kuwa sasa naweza kulipwa nitaambiwa kumbukumbu zimepitwa na wakati hivyo nipeleke viamabatanisho upya! huku bado naendelea kupunjika maana daraja langu nililonalo nitofauti na mshahara wangu, sasa nashindwa kujua nitadai mpaka lini?. NIMEAMUA NA MIMI KUGOMA"
      Elli and gfsonwin like this.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    6. #264
      Baba V's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Location : Buguruni Mnyamani
      Posts : 10,962
      Rep Power : 30234
      Likes Received
      4722
      Likes Given
      3477

      Default

      Quote By simplemind
      Msaada tafadhali maana ya boma.
      Ofisi ya halmashauri ndogo ya mji!

    7. #265
      Wa kaa's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 30th July 2012
      Posts : 6
      Rep Power : 344
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Hapa Mwanga kilimanjaro, asilimia 99 ya walimu wamegoma isipokuwa wasaliti wachache wa smt ya kifaru ndo wapo kazi. Na pia walimu wanatishwa na afisa elimu kwa niaba ya ded. Hivyo wanahitaji msaada wa kisheria haraka.

    8. RukaaJuu Final

    9. #266
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,140
      Rep Power : 606
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Nina imani humu walimu nao wamo maana hawajaenda kazini. sasa je nini kinafuata.
      There are currently 852 users browsing this thread. (154 members and 698 guests)

      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    10. #267
      Baba V's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Location : Buguruni Mnyamani
      Posts : 10,962
      Rep Power : 30234
      Likes Received
      4722
      Likes Given
      3477

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Nani kawaona Zomba,Ritz,Rejao,MAMAPOROJO,Bu rn Karudi, tume ya katiba, na tamuchungu,watupe maelezo ya upande wa pili, because wao ni kurugenzi ya mawasiliano kivuli!

    11. #268
      Elli's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Kijito-Upele
      Posts : 8,584
      Rep Power : 2553
      Likes Received
      2143
      Likes Given
      1862

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Kha!! si walitangaza hakuna mgomo? bado sijaskia toka jijini Dar mambo yakoje huko jamani
      ...but what MAN is entirely without Evil intent in the Silence of his Soul???

    12. #269
      Baba V's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Location : Buguruni Mnyamani
      Posts : 10,962
      Rep Power : 30234
      Likes Received
      4722
      Likes Given
      3477

      Default

      Quote By Kyaiyembe
      Nina imani humu walimu nao wamo maana hawajaenda kazini. sasa je nini kinafuata.
      There are currently 852 users browsing this thread. (154 members and 698 guests)
      Pokea LIKE ya buku mkuu!

    13. #270
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,140
      Rep Power : 606
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Quote By Pombekali
      Nani kawaona Zomba,Ritz,Rejao,MAMAPOROJO,Bu rn Karudi, tume ya katiba, na tamuchungu,watupe maelezo ya upande wa pili, because wao ni kurugenzi ya mawasiliano kivuli!
      Kwa vile umewataja watajitokeza.
      Labda walikuwa hawajapewa madesa ya kuandika hivyo wanasubiri kutoka kwa N. Nauyo. na Vasco.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    14. #271
      Wizzo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2010
      Location : Arusha
      Posts : 432
      Rep Power : 516
      Likes Received
      79
      Likes Given
      34

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      sekondari ya mkombozi hedaru walimu wote wapo kazini,sijui wao wamelidhika na mshahara?

    15. #272
      OMEGA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2011
      Posts : 392
      Rep Power : 476
      Likes Received
      111
      Likes Given
      51

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Hao waheshimiwa nadhani wanafikiri kwa kutumia...huu haukuwa wakati muafaka wa kutangaza nyongeza ya mishahara ya hadi kufikia millioni 11 kama ni kweli,wasingetangaza leo,nadhani na hiyo imechangia hasira za waalimu na kuongeza hamasa ya mgomo,anyway najua serikali itawafikiria na kutatua tatizo kabla ya sensa,otherwise itakuwa aibu kwani na sensa bila waalimu ni ngumu kidogo.Bunge itisheni kikao cha dharula mjadili suala ili kabla hali haijawa tense.
      NEGLIGIBLE likes this.

    16. #273
      NEGLIGIBLE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2011
      Location : TANZANIA
      Posts : 277
      Rep Power : 476
      Likes Received
      50
      Likes Given
      120

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Mimi wasi wasi wangu mkubwa ni hasara ambayo serikali inaweza kupata iwapo haitakuwa makini kuushughulikia mgomo huu.................mara nyingi sensa na chaguzi nyingi zimekuwa zikisimamiwa na walimu kwa umakini,iwapo walim watatoswa kushirikishwa kwenye sensa nina uhakika sensa haitafanikiwa kwa sababu ya umakini wa walimu hauwezi kufikiwa na makundi mengine mengi ambayo yanaweza kutumiwa(kwa sababu ya kukosekana kwa accountability,nidhamu waliyonayo waalim wengi).................lakini pia kuwashirikisha ni risk,unampa kazi mtu ambaye una mgogoro naye,..............lakini pia madai ya kundi fulani la waislam kutokushiriki sensa hayapaswi kupuuzwa.

    17. #274
      Masanilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2007
      Location : Swat valley, Keta Keta
      Posts : 19,127
      Rep Power : 5481
      Likes Received
      3530
      Likes Given
      1950

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Hatupendi kusikia Kiongozi wa Chama cha Waalimu atekwe na Ramadhani Ighondu yule Mfanyakazi wa Ikulu na apatikane Msitu wa Pande akiwa ameng'olewa meno na kucha. Dawa ni kukaa chini mjadiliane si kufungia magazeti. Serikali ya makenge hii

      Kindness is the language which the deaf can hear and the blind can see - Mark Twain
      CCM is enemy of GOD

    18. #275
      Nzowa Godat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2011
      Posts : 1,384
      Rep Power : 678
      Likes Received
      229
      Likes Given
      12

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Nasikia walimu wamepania kuhujumu zoezi zima la SENSA. Serikali iwe macho. Ikiwezekana msiwapange kwenye zoezi hili.

    19. #276
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,140
      Rep Power : 606
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Quote By Wizzo
      sekondari ya mkombozi hedaru walimu wote wapo kazini,sijui wao wamelidhika na mshahara?
      Zifuatazo zaweza kuwa sababu za wao kuwepo kazi;
      1. Hawana mawasiliano mavuri na maeneo mengine ya ncho.
      2. Hawajiamini hivyo hicho kibarua chao wanakilinda hata kwa MKOPO mshahara.
      3. Wanaweza kuwa wana matatizo ya qualification.
      4. Wameanza ajira juzi juzi.
      Kwa vyovyote vile wamejisaliti na kuwasaliti wenzao maana kama hawajaungana kutetea maslai yao pamoja na waoo wataumia huko mbele ya safari.
      Wizzo likes this.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    20. #277
      augustino ameri's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th July 2012
      Posts : 163
      Rep Power : 379
      Likes Received
      21
      Likes Given
      0

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Hao maofisa elimu wanaozunguka na form za kusainisha walimu waliogoma wao hawanamadai,au wao ni sawa na mnyampala gerezani.?

    21. #278
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,140
      Rep Power : 606
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Quote By augustino ameri
      Hao maofisa elimu wanaozunguka na form za kusainisha walimu waliogoma wao hawanamadai,au wao ni sawa na mnyampala gerezani.?
      Kama walimu watajitokeza imekula kwao maana ukigoma mwajiri wako utamwona wapi wakati hauko kazini?. wanatakiwa kukaa nyumbani mpaka watakapotangaziwa vinginevyo.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    22. #279
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,425
      Rep Power : 5041
      Likes Received
      786
      Likes Given
      1804

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Kuna mikoa kama Morogoro, Mtwara, Lindi na Mara hatujapata updates! kulikoni , huko hatuna members wa JF wakatupa hali halisi?
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    23. #280
      Masanilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2007
      Location : Swat valley, Keta Keta
      Posts : 19,127
      Rep Power : 5481
      Likes Received
      3530
      Likes Given
      1950

      Default Re: Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

      Bila shaka CHADEMA wanahusika na migomo hii!

      Kindness is the language which the deaf can hear and the blind can see - Mark Twain
      CCM is enemy of GOD

    Page 14 of 30 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...