Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

    Report Post
    Page 3 of 4 FirstFirst 1234 LastLast
    Results 41 to 60 of 62
    1. #1
      ukweli2's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th November 2011
      Posts : 50
      Rep Power : 389
      Likes Received
      39
      Likes Given
      11

      Default Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.Maoni yangu kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na mbunge:
      JOHN MNYIKA: Kufuatia uamuzi wa Spika wa Bunge jana jumamosi tarehe 28 Julai 2012 kukubali kuvunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini nimetakiwa kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi husika kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

      Sunday, July 29, 2012

      Kufuatia uamuzi wa Spika wa Bunge jana jumamosi tarehe 28 Julai 2012 kukubali kuvunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini nimetakiwa kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi husika kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na mbunge:

      Kwa maoni yangu uamuzi huo ni sahihi lakini umechelewa na pekee hauwezi kurejesha heshima ya bunge kwa ukamilifu wala hautaweza kushughulikia uzembe na udhaifu ulioko kwenye bunge na kwenye serikali ikiwa hautaambana na hatua nyingine za ziada na za haraka.Kwa upande mwingine, uamuzi huo umedhihirisha nilichokisema kwa nyakati mbalimbali kuhusu uzembe wa kibunge pamoja na udhaifu wa serikali.

      Ukiondoa tuhuma za wabunge wanaodaiwa kupokea rushwa ama kuwa na maslahi ya kifedha kwenye wizara, taasisi au mashirika wanayoyasimamia kwenye kamati mbalimbali, heshima ya bunge imeathiriwa vile vile na maamuzi mathalani uamuzi wa kuchaguliwa kwa mtuhumiwa wa ufisadi wa Rada Mbunge Andrew Chenge kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi.

      Hivyo hatua zaidi zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kuvunja na kamati zenye wajumbe waliotuhumiwa na pia kufanya mabadiliko makubwa kwenye wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu za bunge ili kupunguza maslahi ya kifedha ama tuhuma za rushwa miongoni mwa wajumbe wa kamati. Aidha Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imalize kazi yake kwa dharura ili majina ya wahusika yatajwe ndani ya bunge na bunge lijadili kupitisha maazimio ya hatua za ziada za kuchukuliwa na vyombo huru vya kiuchunguzi na hatimaye watakaothibitika kuvunja sheria wafikishwe mahakamani. Pamoja na hatua hizo, Kamati za Vyama nazo zichukue hatua kwa wabunge wake watakaotajwa ili kudumisha misingi ya uadilifu na uwajibikaji kwa maslahi ya umma.
      Hata baada ya hatua hizo, izingatiwe kuwa Bunge litaweza kujinasua kwenye uzembe ikiwa litatimiza kikamilifu wajibu wake wa kuisimamia serikali kwa mujibu wa ibara ya 63 kuondoa udhaifu wa serikali kwenye sekta ya nishati na sekta nyingine muhimu za taifa kwa kuhakikisha maazimio yote ya bunge yanatekelezwa kwa ukamilifu na kwa haraka kama nilivyoeleza kwenye maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni tarehe 15 Julai 2011 na tarehe 27 Julai 2012.

      Nilisema bungeni kwamba “Naamini iwapo maazimio ya Bunge juu ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC yangetekelezwa yote na kwa wakati toka mwaka 2008, maazimio ya bunge juu ya uendeshaji wa sekta ndogo ya gesi asili ya mwaka 2011 yangezingatiwa yote na kwa haraka, maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 yangechukuliwa kwa uzito unaostahili; taifa lingeepushwa kurudia mijadala ile ile kuhusu Wizara hii hii mara kwa mara”.

      Mathalani, Waziri wa Nishati na Madini ameeleza bungeni tarehe 28 Julai 2012 kuwa wapo wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara zenye kulihujumu Shirika la Umeme (TANESCO) na Spika wa Bunge akahitimisha kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itachunguza tuhuma husika na pia kwamba inakusudiwa kutungwa kwa Kanuni za Maadili (Code of Conduct) ili kudhibiti hali hiyo.

      Hata hivyo, Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kuwa mwaka 2008 baada ya Kashfa ya Richmond iliazimiwa katika Azimio Na. 11, kwamba “Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 (The Public Leadership Code of Ethics Act), ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa Viongozi Waandamizi wenye dhamana ya kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakani, jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya Bunge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.”

      Bunge lilitaarifiwa Februari 2010 kuhusu utekelezaji wa Serikali kwamba kikundi kazi (Task Force) kiliundwa ambacho kiliandaa waraka wenye mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, (Sura 398) ambao ulikuwa katika ngazi ya kujadiliwa na Kamati ya Makatibu Wakuu (IMTC). Aidha, Bunge lilielezwa kuwa serikali ilitarajia kuwasilisha muswada husika katika mkutano wa kumi na tisa wa Bunge la tisa. Muswada huo haukupitishwa katika Bunge la tisa kama ilivyoshauriwa na kamati na mpaka kutokana na uzembe na udhaifu azimio hilo halijatekelezwa na tuhuma nyingine zimeendelea kuibuka.

      Aidha, kumetolewa madai ya baadhi ya wabunge kupokea ama kudai rushwa suala ambalo nalo Spika wa Bunge ametoa uamuzi kuwa litashughulikiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Lakini Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kwamba hii si mara ya kwanza kwa tuhuma za namna hiyo kutolewa juu ya baadhi ya wabunge wa kamati mbalimbali za bunge.

      Hata hivyo, kwa sababu ya kutochukua hatua kwa haraka na kwa ukamilifu tuhuma kama hizo zitaendelea kujirudia hata baada ya kuvunjwa kwa kamati ya bunge ya nishati na madini. Izingatiwe kwamba madai ya rushwa kutolewa kwa wabunge yaliwahi kujitokeza kuhusu Kamati ya Nishati na Madini na binafsi nilitoa ushuhuda kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mwaka 2011, na nikatoa ushuhuda tena kwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni mwaka 2011 kuwa yamekuwepo matukio ya kushawishi wabunge kwa rushwa hata hivyo hatua hazikuchukuliwa ama kuvunja kamati zilizotajwa au kuwachukulia hatua wahusika.

      Suala hili likatajwa tena na Mbunge wa Kigoma Kaskazini David Kafulila kuhusu Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na likatajwa tena na Kiongozi wa Upinzani Freeman Mbowe na Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe kuhusu uchaguzi wa Afrika Mashariki lakini hatua hazikuchukuliwa kuchunguza wabunge husika na kuchukua hatua. Iwapo maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 (Maarufu kama Sakata la Jairo), yangetekelezwa na wahusika wangechukuliwa hatua ingejenga nidhamu pia kwa watendaji wa wizara na mashirika ya umma kuhusu rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma yenye kulenga kuwaathiri wabunge kwa rushwa na maslahi mengine ya kifedha.

      Katika hali inayoonyeha kwamba Serikali bado haioni uharaka na ulazima wa kuchukua hatua, wakati bunge lilipokaa kama kamati tarehe 28 Julai 2012 kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini nilitaka ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo ambayo mpaka sasa hakuna taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa bungeni toka yapitishwe mwezi Novemba mwaka 2011; lakini Waziri akajibu tu kwamba hawezi kufanyia kazi taarifa za magazetini, bila kujali kwamba nilichouliza hakihusu taarifa za magazetini bali maazimio ya bunge baada ya kazi iliyofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ikarudiwa tena na Kamati Teule ya Bunge ambayo ilihoji wahusika na kupata pia vielelezo.

      Kwa hiyo, ni muhimu Serikali na Uongozi wa Bunge ukarejea kwenye Hotuba niliyowasilisha bungeni na kuchukua hatua kwa usimamizi wa Rais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge juu ya masuala yote niliyoyaeleza. Pamoja na kutaja ushawishi uliokuwa ukifanywa kwa wabunge kuhusu suala la ununuzi wa mafuta ya IPTL, na ufisadi ndani ya TANESCO nilieleza pia masuala mengine makubwa kwenye nishati na madini yenye kuhusu mabilioni ya shilingi kwenye mikataba mikubwa ya umeme, madini, mafuta na gesi asili pamoja na hatua za mabadiliko ya kimfumo zinazopaswa kuchukuliwa.

      Nimetoa maoni hayaleo jumapili tarehe 29 Julai 2012:


      John Mnyika (Mb)


      Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

      nawakilisha!!!

    2. Miaka 50

    3. #41
      nahavache's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd April 2009
      Posts : 466
      Rep Power : 609
      Likes Received
      130
      Likes Given
      277

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Kweli Mnyika umenena, waanze kwanza na mzee wa vijisent kama kweli wana nia ya dhati

    4. #42
      PROFESA KYANDO's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th July 2012
      Posts : 83
      Rep Power : 359
      Likes Received
      6
      Likes Given
      5

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      mnyika safi sana.. Bwana mdogo.. Endelea kupambana.. Haina kurudi nyuma

    5. #43
      akilipana's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th October 2009
      Posts : 57
      Rep Power : 497
      Likes Received
      3
      Likes Given
      10

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Atoe majina siyo kutoa hotuba general. Mbona Mwembe yanga majina yalitoka sasa kigugumizi cha nini?

    6. #44
      MVUMBUZI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th January 2011
      Posts : 2,583
      Rep Power : 1088
      Likes Received
      682
      Likes Given
      374

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Quote By Kiona
      Bwana Mdogo Mnyika umeshasema uamuzi wa Bi kiroboto ni sahihi na hiyo inatosha haina haja ya kueleza sana. Chadema sisi ni wepesi wa kuchanganua na kupambanua mambo. Yuko wapi January Makamba? kelele zake kumbe alikuwa anamuwinda Msukuma wa sengerema
      HIZI KWENYE red NDIZO SIASA Chakavu na za kujaza matumbo. Hasikii wala haoni baada ya kutimiza ndoto zake za kupata ulaji na huo ndio mwisho wake.

    7. #45
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 3,973
      Rep Power : 1217
      Likes Received
      247
      Likes Given
      41

      Default Mnyika na madudu ya tanesco

      Embu tueleze wewe Mnyika kwamba madudu haya yaliyotokea kwenye kamati yako mpaka kuvunjwa ulikuwa hujui au ulikuwa unasikilizia upepo upite.Kwa akili ya kawaida Mnyika mtu kama wewe Watu lazima wanajua ungechukulia ujiko wa kuripua maufisadi yaliyomo.Sasa kukaa kwako kimya ni dhahiri Unajua kinachoendelea kwenye hiyo kamati yenu iliyovunjwa.

    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      Shardcole's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,393
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1032
      Likes Given
      4

      Default Re: Mnyika na madudu ya tanesco

      Pumbaf na uwendawazimu @work

    10. #47
      Mtumpole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2010
      Location : Dreamland
      Posts : 519
      Rep Power : 546
      Likes Received
      93
      Likes Given
      327

      Default Re: Mnyika na madudu ya tanesco

      Quote By Mzinga
      Embu tueleze wewe Mnyika kwamba madudu haya yaliyotokea kwenye kamati yako mpaka kuvunjwa ulikuwa hujui au ulikuwa unasikilizia upepo .......
      Mzinga, ficha UPUMBAVU wako!
      Mwenye dhambi hana raha

    11. #48
      Asa79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2012
      Posts : 591
      Rep Power : 462
      Likes Received
      162
      Likes Given
      10

      Default Re: Mnyika na madudu ya tanesco

      Walimficha na walikuwa wanamzunguka walijua tu angelipuka fasta....na ameshalipuka sasa hizi blabla zingine ni utoto tu naamini ukikua utaacha labda km umetumwa na zitto

    12. #49
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,809
      Rep Power : 1143
      Likes Received
      187
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mzinga
      Embu tueleze wewe Mnyika kwamba madudu haya yaliyotokea kwenye kamati yako mpaka kuvunjwa ulikuwa hujui au ulikuwa unasikilizia upepo upite.Kwa akili ya kawaida Mnyika mtu kama wewe Watu lazima wanajua ungechukulia ujiko wa kuripua maufisadi yaliyomo.Sasa kukaa kwako kimya ni dhahiri Unajua kinachoendelea kwenye hiyo kamati yenu iliyovunjwa.
      Mnyika ni mla rushwa mzuri tu na hukuwahi hata siku moja kumsikia akiishutumu TANESCO. Na hata kwenye hotuba yake ya kambi ya upinzani ukiisoma kinaga ubaga utaona mnyika ana nufaika na huu mchezo wa Muhando, iko wazi wala haihitaji digrii ya chuo kikuu ili ujue mkuu

    13. #50
      POMPO's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 2,955
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1090
      Likes Given
      625

      Default Re: Mnyika na madudu ya tanesco

      hii nayo thread?

    14. #51
      POMPO's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 2,955
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1090
      Likes Given
      625

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Quote By Dumela Mbegu
      Mnyika ni mla rushwa mzuri tu na hukuwahi hata siku moja kumsikia akiishutumu TANESCO. Na hata kwenye hotuba yake ya kambi ya upinzani ukiisoma kinaga ubaga utaona mnyika ana nufaika na huu mchezo wa Muhando, iko wazi wala haihitaji digrii ya chuo kikuu ili ujue mkuu
      Aamewashika vibaya eh kwenye 0713... na bado mtaeleweka tu.

    15. #52
      beyanga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 184
      Rep Power : 380
      Likes Received
      21
      Likes Given
      53

      Default Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      kubenafrank likes this.

    16. #53
      Henge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 5,440
      Rep Power : 1674
      Likes Received
      918
      Likes Given
      1673

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Huyu mnyika asipozimwa mapema anaweza kuwatishio kwenye uraisi wangu huko mbeleni!
      Tutakupoteza mkuu!
      TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA by PINDA

    17. #54
      Makala Jr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th August 2011
      Posts : 1,582
      Rep Power : 707
      Likes Received
      325
      Likes Given
      0

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Nikuelewa kamanda Mnyika...japokuwa kuna mpuuzi humu kadai eti CHADEMA tunadandia hoja kwani ninyi magamba tangu lini mlikuwa na hoja ya kupinga ufisadi? Pia hata sisi ni watz na tuna haki ya kutoa maoni juu ya mambo yanayotumbisha kama taifa nadhani mnajisahau kisa mmeunda serikali na magamba yenu kwamba mtatupangia ya kuongea. Acheni upuuzi wana-ccm nchi inaenda mrama kaeni chini na mjue la kumshauri J.K tena ikiwezekana ahakikishe vikosi vya usalama vinafanya kazi 24.Sasa sisi CHADEMA hatupendi namna nchi inavyoendeshwa kijinga!

    18. #55
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 547
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Quote By Msalagambwe
      Jembe asilia hili.
      kweli jamaa ni jembe! ila hata zito tulikuwa tukimkubali jembe asili ivi ivi miaka michache iliyopita, ila katuangusha mbaya! ngoja tumuone huyu jembe naye!

    19. #56
      schwester's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 66
      Rep Power : 372
      Likes Received
      10
      Likes Given
      4

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Quote By kijiichake
      Ee Mungu nalia mbele yako, Taifa langu Tanzania kila kukuchapo leo afadhali na jana. Taifa langu hii limekuwa kiwanja cha mpira wa wahuni hakuna jipya humu nimiendelezo ya kutufilisi. Ifike wakatati Ee Mungu wetu ututete na kuwalipizia kisasi wale wanaofanya ufedhuli huu. Uyafute majina yao katika vitabu vyako vya rehema na kuyaandika majina yao, katika vitabu vya hukumu ya jehanum wasione raha wao wala watoto wao. Uwalipizie mara elfu matendo yao maovu juu ya Taifa hii. Tumelia hawakuona huruma, tumeteta hawakusikia wala kututizama, Taifa limevamiwa na viwavi jeshi, kila kitu kinatafunwa, hakuna vinavyo sazwa hata kwa ajili ya vizazi vijavyo, Ee Mungu tukomboe macho yetu tunayaelekeza kwako.

      Mpendwa maombi ya visasi Mungu hapatilizi, pia angalia sana unalaani hata kizazi cha hao wala rushwa hawana hatia na hata kama wanazo hakuna Mtanzania atakayepona. Hata wewe ni mwizi sijui kama unajua sasa ANGALIA HII LAANA SI KWA VIONGOZI HATA WEWE; Hapo ndipo ninapompenda MUNGU.

    20. #57
      Mdakuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 267
      Rep Power : 412
      Likes Received
      48
      Likes Given
      11

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Safi sana kamanda, tutaifikia tu nchi ya ahadi.... Nadhani tutaongea mengi kwenye Sangara inayokuja!
      Ame likes this.

    21. Ame
      #58
      Ame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Location : Global Citizen
      Posts : 1,513
      Rep Power : 1184
      Likes Received
      650
      Likes Given
      2615

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Quote By KipimaPembe
      Credibility ya bunge ilisambaratika siku ile CCM walipoamua kuteua spika kwa kuangalia jinsia; "sasa ni zamu ya wanawake!!"
      • Bunge linaakisi kinachoendelea ndani ya serikali; wabunge wengi wametoka kwenye nafasi mbali mbali za utendaji serikalini ndo wakaingia bungeni! Yale waliyokuwa wakiyatenda huko serikalini, wanaendelea kuyatenda hata wakishakuwa wabunge.
      • Inaaminika kuwa "motive" kubwa ya watu wengi kuingia Bungeni ni ili waweze kushiriki kwenye "bonanza" ya rushwa; wakiwa wamechoka kuwa watazamaji wanapokuwa watendaji huko serikalini.
      • Bunge limepitisha sheria nyingi kwa kuhongwa hasa wajanja wakichomekea vipengele wanavyojua jinsi watakavyovitumia. Wabunge wakikaribishwa vikao vya ndani vyenye maposho manene manene na "kueleweshwa" sheria zinazotarajiwa kutungwa.
      • Hivi karibuni SSRA, Serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii wamekaa na kutunga sheria ambayo inahakikisha fedha mifuko ya jamii zinakuwa kichaka cha serikali kuchezea "mdako" wa kuchota fedha za watu bila kujali; huku SSRA wakidai lengo ni kuboresha mafao; Bunge lilipitisha bila kuhoji hadi hapo wanaharakati walipowafungua macho wananchi.

      Bunge hili sasa hivi ni muhuri tu, linaweza kutumiwa na yeyote mwenye maslahi yake bila kujali. Halina heshima yoyote mbele ya macho ya wananchi.
      Above all they should know kwamba mwisho wa ubaya ni aibu! No stone will be left unturned....Ufisadi unahesabu muda wa maisha yake hapa Tanzania...Its so sad hata wale ambao walitakiwa kujilinda nafsi zao wakati huu tulipo jangwani kuelekea kanani hawataiona nchi ya ahadi kwakukumbuka masufuria ya nyama ya wamisri....

      When it comes to ufisadi sina chama dini kabila rangi ama race kila nafsi itendayo ufisadi lazima ife....Ame the preacher still preaching the gospel kama hamuamini maneno yake basi aminini matukio!

      Mnyika you are full protected hakuna atakaye kugusa na atakayejaribu atakutana na nguvu ambayo hajawahi kupata kuiona tangu ajitambue kuwepo kwenye hii dunia! Thanks for walking the talk!

    22. #59
      schwester's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 66
      Rep Power : 372
      Likes Received
      10
      Likes Given
      4

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Mara nyingi watu hupenda kutumia huu msemo wa ukiongea na kichaa nawe unakuwa kichaa tena Mshenzi. Sasa wananchi ifike mahali muelewe si kila hoja kujibu au kuongea, hata ukikaa kimya nayo ni majibu. Tumieni uwezo wenu kuimarisha chama na kuwaelimisha wananchi vilvyonyuma ya PAZIA na si kuhangaika na wale washenzi .

    23. #60
      schwester's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 66
      Rep Power : 372
      Likes Received
      10
      Likes Given
      4

      Default Re: Maoni ya John Mnyika juu ya Kuvunjwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini

      Pia ikumbukwe siku zote simba mwenda Pole ndiye mla nyama. Na debe tupu haliachi kuvuma. Tujipange Watz kutoka katika hawa wachache ambao wanasahau Yote yana mwisho. Pia Tuombeni Toba kwa ajili ya hili Taifa na wananchi, Pia tumwombe Mungu atuongoze tuombe vipi kwa Taifa hili na si kulalamika na kulaani TUNAJILAAAANI WENYEWE. Hakuna hata mmoja aliyesimama kwenye kinachomstahili wale wanaojitahidi wanauwawa je kwa Damu hiyo tutapona WAPI?

    Page 3 of 4 FirstFirst 1234 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...