Nimefuatilia sana hoja za wabunge na waziri na naibu wake juu ya TANESCO, ninaona siasa zaidi kuliko hali halisi, hapo ndipo naungana na Zitto kabwe. Sakata la Jairo lilipita bila kutajwa wabunge walio hongwa watanzania tukafurahi sana kwa sababu mtu mmoja kasimamishwa kazi kwa taratibu zilizokuwa zinafanywa na wizara zote huko nyuma.
Waziri pamoja na katibu wake walifanya lobbying kwa wabunge wasimamie hoja za kijinga ili budget yao mbaya ipite, Kwa sababu tuna wabunge wajinga na wapenda sifa kila mmoja alisimamia wala rushwa, hapo ndipo prof alishinda; ukitaka kumshinda mjinga hapo ndipo panafaa; Mjinga yeyote anasimamia sehemu nyepesi iliaonekane ana uchungu.
Kwa jicho langu la Mbali muheshimiwa Lowassa kawashinda wote washindani wake na kwa hili anasitahili kupewa uwaziri Mkuu walio mpokonya. Kwa sababu inaonekana ni hawa wabunge wala rushwa ndio walitunga ule uongo. Katika hili wengi wataingia hata ambao hatuzanii kama Mwakyembe, Makamba junior etc.
Kibaya zaidi wanasema wabunge, hawasemi Fulani na Fulani mbona Kafulila alisema kipindi kile Zambi, na yule aliyekamatwa na Rushwa wamefanya abc, lakini leo hatuambiwi majina; Wabunge wa CCM ukiona wamesimama hivyo amini usiamini wamekomaa wakiamini Zitto kala hizo pesa, lakini kwa Siasa za Zitto naamini hawezi fanya ujinga kama huo.
Siku si nyingi tutaanza mgao wa Umeme, ndipo uongo na Ukweli wa Waziri wetu tutaujua.
Naomba niishie hapa

Reply With Quote

Follow Us Here