Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

    Report Post
    1. #1
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,418
      Rep Power : 10873
      Likes Received
      3798
      Likes Given
      426

      Default Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Zitto
      Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma ambayo imeunganishwa kwenye tuhuma hizo, Zitto Kabwe, alisema tuhuma hizo anazisikia, lakini anaziona kama siasa za majitaka kwa sababu zinarushwa bila ushahidi wowote.

      "Hakuna hata mbunge mmoja aliyesimama kusema nani amehongwa nini. Mimi binafsi sijahongwa na mtu yeyote wala mimi sijamtetea mtu isipokuwa natetea taratibu kufuatwa," alisema.

      Zitto alibainisha kuwa anaamini tuhuma hizo zimetokana na hasira za yeye kupinga posho za wabunge na sasa wameona hilo ndilo eneo la kumkomoa.

      "Kwa kuwa ‘my conscious is clear’, (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli. Hata hivyo, kwa kuwa tuhuma hizo zinasemwa juu juu tu, tutataka vyombo vya dola vichunguze na ikithibitika hatua zichukuliwe," alisema na kuongeza:

      "Kwangu mimi naona hizi ni siasa za urais na hasira za posho. Wenye kutaka urais wa vyama vyote na wapambe wao, wameungana kunichafulia heshima yangu. Wabunge wenye njaa ya posho, wameungana kunikomoa. Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa. Mwalimu Nyerere (Julius) alisema katika andiko lake la 'Tujisahihishe'.”

      Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini(Chadema) alishauri pia Spika wa Bunge kutumia Kamati ya Maadili kuchunguza tuhuma hizo kwa kuwa hazipaswi kuachwa zikapita hivihivi.


      Source: Mwananchi Jumapili.

    2. FemaTV & Radio

    3. #281
      sexon2000's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th April 2010
      Posts : 301
      Rep Power : 522
      Likes Received
      54
      Likes Given
      59

      Default Re: Hamaki ya Zitto inashangaza, hajatajwa jina lakini kang'aka...

      Quote By Crucifix
      Zitto hamaki ya nini kama huhusiki? Nani kasema mambo ya urais hapa. Kwani Jairo alikuwa anagombea urais alipolipuliwa last year. Mama Lwakatare nae anagombea urais?

      Tumekujua, una mikono michafu. Usicheze na sisi!
      ZITTO ana mikono michafu mno. Mwaka jana wafanyakazi wa PPF wanao changia hapa JF walijaribu kuonyesha alivyo mchafu kwa Rushwa za waziwazi, wakajiwa juu humu JF.

      Zitto amepokea mlungula toka uongozi wa PPF ili kuwasaidia soo la kujilipa miliono 220 kila mkurugenzi kinyume na taratibu. Alijitutumua mwaka jana mwezi wa nne, na kuagiza CAG akague, CAG akakagua na kuyaona madudu makubuwa PPF yakiwemo ya:

      1.Wakiwa wafanyakazi wa kudumu walitumia ujanja kubadili mikataba yao na kuwa wafanyakazi wa mikataba ili wawe wanalipwa GRATUITY ya 25% ya mishahara ya miaka 4 kila mwisho wa mkataba bila kibali cha hazina.

      2. Baada ya kumaliza miaka 4 March 2008, wakalipwa gratuity, lakini pia wakalipwa mafao ya wafanyakazi wa kudumu yaitwayo GROUP ENDOWMWNT. ZITTO katika kamati yake alikiri kuwa haya ni makosa lazima hatua zichukuliwe. CAG kampa ripoti yenye majibu haya, lakini kazibwa mdomo na rushwa toka uongozi wa PPF

      3. March 2011, wakalipwa tena Gratuity na Group endowment kinyume na sheria, maana mfanyakazi hustahili kimoja wapo sio vyote viwili kwa pamoja. CAG alimpa ripoti yenye haya yote, lakini Rushwa toka uongozi wa PPF imemnyamazisha

      4. Ilipofika May 2011, baada ya kiujilipa group endowment hadi maximum ya miaka 10, wakarudi kimya kimya na kuwa wafanyakazi wa kudumu, kwa kisingizio kuwa walikosea kujihamisha kuwa wa mkataba. Zitto kapewa ripoti ya huu ufisadi, lakini rushwa ya uongozi wa PPF imemfumba kinywa

      5. Mwezi August, 2011 kaamua kujiunga na mfuko wa PPF na kuwa mwanachama, na hili lilifanyika kwa mbwembwe nyingi na publicity kubwa, sasa hili si mgongano wa maslahi?

      6. Sabasaba 2012, kajitangaza sana pale kwenye banda la PPF. Mbona hakuenda NSSF, PSPF, LAPF wala GEPF kwa mbwembwe na kupiga picha na kila mkurugenzi na meneja aliyekuwepo siku hiyo.

      Ripoti kafunika na kuwatetea akina William Erio Mkapa huku akijifanya ni mpambanaji wa ufisadi.

      Hili la TANESCO, asijitoe, ndiye wakwanza kutoa statement kuwa kusimamishwa kwa menejiment sio sahihi. Alikuwa na maslahi gani na MHANDO?

      Zitto ndugu yetu kijana, umepewa kuongoza kamati unajinufaisha, ukipewa nchi si utaiuza? Kwa kuwa huwa unasoma hapa JF, hebu jibu hizi tuhuma za PPF maana sisi wafanyakazi wa PPF tulikuamini mwanzoni lakini ulipojitumbukiza kwenye ufisadi wa DG wetu tumepoteza imani nawe kabisa.

    4. #282
      Zatara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2012
      Location : M/Nyamala
      Posts : 276
      Rep Power : 413
      Likes Received
      67
      Likes Given
      58

      Default Re: Wachaga wa chadema waungana na ccm kumdhiti zitto kabwe

      Quote By Kigogo
      yaani umejiunga specific kujibu hoja hii ama?ukibaraka huo..Zitto hata iweje hawezi kuwa rais ...tna uzoefu na dini anayotoka zitto kuwa haitoi viongozi makini..so aendelee tu na ubunge au awe rais wa kikundi cha wasaniii wa kigoma-leka tutigite
      Wewe na kina kaka? Ilikuwa ngumu kuamini kwamba haya mambo yana-udini ndani, na sitaki niamini hivyo. Ila unapoona tuna-base zaidi katika dini basi "something very serious is wrong in our mentality"

    5. #283
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,513
      Rep Power : 19750
      Likes Received
      5443
      Likes Given
      3640

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Rushwa bungeni moto
      • Mbatia sasa atishia kuwataja wakati wowote

      na Edson Kamukara, Dodoma

      SAKATA la wabunge kuhongwa kwa nia ya kuyatetea makampuni ya mafuta na menejimenti ya Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) linazidi kuchukua sura mpya kadiri siku zinavyosonga mbele.
      Siku moja baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kuvurumisha makombora dhidi ya wabunge hao pasipo kuwataja kwa majina, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, ameibuka na jipya kuhusu sekeseke hilo.
      Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi amesema wakati wowote kuanzia sasa atawataja kwa majina wabunge wote waliopokea rushwa kwa lengo la kuwalinda viongozi wakuu wa TANESCO wanaokabiliwa na tuhuma za kulihujumu shirika hilo.
      Mbali ya hilo, Mbatia amemshutumu Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwa kuwalinda wabunge hao aliodai wamehongwa na mafisadi hao wa TANESCO.
      Kauli hiyo aliitoa jana mkoani hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Spika Makinda kuridhia kuivunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na kuiagiza Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.
      Mbatia alisema Spika anao ushahidi wa kutosha wa majina ya wabunge waliohongwa kwani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliliambia Bunge kuwa wana ushahidi wote.
      Alibainisha kuwa ushahidi huo ndiyo uliomfanya Spika Makinda akaridhia kuivunja kamati husika na kuipa kazi Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.
      Kiongozi huyo pia alisema hawana imani na kamati iliyopewa jukumu la kuwachunguza wabunge watuhumiwa wa rushwa kwa sababu inaundwa na baadhi ya watuhumiwa.
      “Tunamtaka Spika ajitakase kwanza kwa kuwaengua wajumbe ambao ni watuhumiwa, kinyume na hapo hatuna imani na kamati hiyo,” alisema.
      Alisema Bunge ni chombo kitukufu na ili utukufu huo uonekane ni lazima maamuzi yanayofanywa huko yaheshimiwe, hivyo akapendekeza kuwa mbali na Bunge kutumia kanuni zake kuwahukumu wabunge watuhumiwa au linaweza kuiga maamuzi ya baadhi ya mabunge ya Jumuiya ya Madola.
      Alitolea mfano mabunge ya Uingereza na India, ambapo Bunge la Uingereza limewahi kuwatimua na kuwavua ubunge wabunge 57 na India imefanya hivyo kwa wabunge 11 kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.
      “Hivyo basi tunatoa wito kuwa mbunge yeyote wa chama chochote anayeamini kwa dhamira yake kwamba ni mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na anafanya biashara na TANESCO kwa njia ya maslahi binafsi halafu anatumia rushwa kuwashawishi wabunge wengine au amepokea rushwa kutetea uovu ni bora akajiondoa mwenyewe kwenye ubunge kabla ya kuabishwa na Bunge,” alisema.
      Mbatia aliongeza kuwa wanamtaka Spika awe amewataja kwa majina wabunge waliopokea rushwa si zaidi ya wiki moja ili Bunge liwachukulie hatua, huku akiwaomba wabunge wenzake bila kujali itikadi za vyama vyao wafanye azimio la Bunge ili wahusika mbali na kuvuliwa ubunge wafungwe jela miaka mitano.
      “Kwa mujibu wa sheria namba 3 kifungu cha 32 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988, mbunge anakatazwa kuzungumza, kuhoji, kupiga kura au kutetea jambo lolote bungeni ambalo litakuwa na ushawishi wa maslahi yake binafsi kutoka nje na kwamba adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka mitano jela,” alisema Mbatia.
      Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na mbunge mwingine wa chama hicho wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alimtaka Spika kuzitaja kamati nyingine ambazo wajumbe wake wanatuhumiwa kwa rushwa.
      Mbali na Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, kamati nyingine zinazodaiwa baadhi ya wabunge wake kujihusisha na vitendo vya rushwa ni ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) chini ya Zitto Kabwe na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Augustine Mrema.
      Nyingine ni ya Miundombinu chini ya Peter Serukamba, Viwanda na Biashara ya Mahmoud Mgimwa na Ardhi, Maliasili na Mazingira chini ya James Lembeli.
      “Tatizo la nchi yetu ni kuchelewa kufanya maamuzi wakati muafaka. Tukilitakasa Bunge kwa kuwashughulikia wabunge waliokula rushwa ni wazi hata serikali itaanza kuwachukulia hatua wale ambao tumekuwa tukiwalalamikia kujihusisha na rushwa,”
      Mbatia aliwatahadharisha wabunge wa chama chake kuwa kama kuna yeyote aliyechukua rushwa katika sakata hilo, ajiengue mapema.
      Mbatia pia alitumia mwanya huo kuwatia matumaini wabunge waadilifu wenye misimamo mikali ya kuikosoa serikali kuwa wasiogopeshwe na sakata hilo ambalo alidai serikali italitumia kuwanyamazisha wabunge kwa vile walikuwa wakiikosoa.
      Ingawa Mbatia hakuwataja kwa majina wabunge hao, habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kuwa wabunge zaidi ya sita wanatajwa kuwa katika kundi la wale wanaotuhumiwa kuwatetea mafisadi wa TANESCO.
      Inadaiwa wabunge hao walipewa fedha na kampuni za mafuta ili washinikize kung’olewa kwa Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakim Maswi wanaodaiwa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kwa TANESCO kampuni ya Puma Energy.
      Habari zinaeleza kuwa, wabunge hao wako katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Viwanda na Biashara na Ardhi, Maliasili na Mazingira.
      Gazeti hili limedokezwa kwamba wabunge takriban wote isipokuwa mmoja tu, walioko katika orodha hiyo wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).



      Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.

    6. #284
      MDAU JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2011
      Posts : 322
      Rep Power : 479
      Likes Received
      40
      Likes Given
      25

      Default Re: Wachaga wa chadema waungana na ccm kumdhiti zitto kabwe

      Quote By Kigogo
      yaani umejiunga specific kujibu hoja hii ama?ukibaraka huo..Zitto hata iweje hawezi kuwa rais ...tna uzoefu na dini anayotoka zitto kuwa haitoi viongozi makini..so aendelee tu na ubunge au awe rais wa kikundi cha wasaniii wa kigoma-leka tutigite
      Dini gani ilitoa kiongozi aliye makini TZ? Na tumewahi kupata kiongozi makini lini?
      LAA ILAHA ILLALLAH MUHAMMADUR RASULULLAH

    7. #285
      kanewi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 52
      Rep Power : 360
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      sijaona tatizo la zzk kutangaza kuutaka uraisi ila ningependa kusema amekosea kutasmini mda wa wakujitokeza,.najua hawa wabunge wetu na watu wa makada mbalimbali wana washauri wao katika masuala ya msingi,mshauri wa zzk naona anataka kufanana na wa kikwete,hawatasmini mda wa kauli na nini cha kuzungumza wanaowashauri,.ningependa zzk asijitokeze tena kujibu mambo kwa pupa kwani ccm wapo kila mahara kama magaidi wa osama/alkaeda duniani,jambo zito alitupe humu jamvini tumshauri.

    8. Miaka 50

    9. #286
      BinMgen's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2008
      Posts : 1,484
      Rep Power : 853
      Likes Received
      110
      Likes Given
      229

      Default Re: Urais + ukabila,twaenda wapi

      Quote By Mrdash1
      umbo la mwili wake halimfai kuwa raisi wa nchi ni mfupi sana hana charisma ya uraisi, bola huyu tuliye naye aendelee kuliko mbilikimo. Mtu mfupi mawazo yake daima ni mafupi, hakuna kuona mbali ni ubinafsi tu na u mimi unatawala, hii ndo psychology ya mtu mfupi ya kujitutumua ili aonekane kwa vile anahisi inferior kutokana na udogo wa umbo lake. Watanzania watakuwa wajinga kama watafanya majaribio mengine kwa miaka mingine 10 ijayo.
      Dah! mkuu unanichekesha kweli hizo ndio sababu zako za kumpinga ZZK, Hebu tupeni sababu za msingi na ushahidi wa wazi zinazo wafanya mumkomalie ZZK kiasi hicho vinginevyo tutaamini yasemwayo ukavbila na udini tu unawasumbua.

      "Kwa kuwa ‘my conscious is clear’, (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli.by zitto
      Last edited by BinMgen; 30th July 2012 at 06:22.
      Life is too short don't wait



    10. #287
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Quote By Narubongo
      zitto ni kama mmiliki wa gazeti la mwananchi
      "Ni kama" labda but kiukweli ni mmiliki wa gazeti la Raia mwema na si mwananchi

    11. #288
      JIULIZE KWANZA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Posts : 1,586
      Rep Power : 750
      Likes Received
      248
      Likes Given
      675

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Nilikwambia zzk unaingia choo cha kike ndugu, haya ona Aibu hizi hata kujibu hoja huwezi unaanza kuropoka tunasubiria uanze kulia Kama mtoto wa mkulima Tehe Tehe Tehe mpaka 2015 hata ubunge utaukosa
      There shall be no peace without right for all...By Bob Marley.

    12. #289
      Filipo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : Kiding'a
      Posts : 6,349
      Rep Power : 18614
      Likes Received
      3508
      Likes Given
      1663

      Default

      Quote By Msiba
      Ktika hali isiyokuwa ya kawaida wachaga waliop chadema wameungana na wabunge wapenda posho wa ccm ili kumuadabisha Mh zuberi zitto,
      ukabila unawasumbua sana! Propaganda chafu kutoka Lumumba.

    13. #290
      BinMgen's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2008
      Posts : 1,484
      Rep Power : 853
      Likes Received
      110
      Likes Given
      229

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Quote By JIULIZE KWANZA
      Nilikwambia zzk unaingia choo cha kike ndugu, haya ona Aibu hizi hata kujibu hoja huwezi unaanza kuropoka tunasubiria uanze kulia Kama mtoto wa mkulima Tehe Tehe Tehe mpaka 2015 hata ubunge utaukosa
      Mbona katulia! hebu angalia kauli yake hii "Kwa kuwa ‘my conscious is clear’, (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli.by zitto
      Life is too short don't wait



    14. #291
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,478
      Rep Power : 6168
      Likes Received
      3050
      Likes Given
      1017

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Quote By Mwita Maranya
      Kimbunga hayo ya kwamba mbunge wa Chadema alikueleza kwamba anamchukia zitto sababu ya kupinga posho hatuwezi kukuamini, uwezekano mkubwa unaweza kuwa umemlisha maneno, vinginevyo ungemtaja jina.
      Wapo baadhi ya wabunge toka Chadema wanaozitaka posho na wamezungumza hadharani; shibuda na Selasini kwa mfano. Sasa wewe unajitengenezea ushahidi fake ambao hatuwezi kuuthibitisha.
      Lakini pia ulitaja eti mbunge toka kaskazini ili upate kukamilisha agenda yako ya unafiki na kutekeleza mkakati wenu wa kuinadi cd ya ukanda ambayo watanzania wameendelea kuipuuza kama walivyopuuza na nyingine mlizotaka kuwagawia bure.
      Kwamba wabunge wa Chadema wanamchukia zitto ni umbea mwingine ambao huwezi kuuthibitisha. Nakushauri hizi siasa za kichovu waachie vijakazi wa nape wewe umevuka huko.
      Mkuu Mwita Maranya sifanyi siasa za kichovu ninachosema ni kweli na kweli tupu bila kumung'unya maneno. Mwita nakujua wewe ni CDM makini. Naomba uniambie msimamo wako binafsi na msimamo wa CDM kuhusu posho ambazo zilipigiwa kelele kwenye bunge la mwaka jana.
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    15. #292
      Khakha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2009
      Posts : 957
      Rep Power : 692
      Likes Received
      208
      Likes Given
      80

      Default

      Quote By Crucifix
      Zitto hamaki ya nini kama huhusiki? Nani kasema mambo ya urais hapa. Kwani Jairo alikuwa anagombea urais alipolipuliwa last year. Mama Lwakatare nae anagombea urais?

      Tumekujua, una mikono michafu. Usicheze na sisi!
      mkuu crucifix, kumbe zito kujifanya mzalendo kukataa posho za bungeni kumbe ana posho zake haramu tanesco anavuta kila mwezi. sina imani tena na dogo huyu.
      Crucifix likes this.

    16. #293
      Emashilla's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Location : Magadirisho, Usa-River
      Posts : 127
      Rep Power : 761
      Likes Received
      21
      Likes Given
      70

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Mleta hoja hii, una lako jambo! Kila mtu ana uhuru wa kusema au kuandika maoni yake,lakini hatima ya nchi hii haipo katika majungu ya vyama. Zitto Kabwe mnamfahamu vema.Yeye ameleta mwamko wa madai mengi sana na sikuzote mlimpuuza na Spika wenu kumfukuza bungeni na ninyi mliyaona na kuyaskia hayo. Leo mnatumia vifuli kuficha uozo wa baadhi ya watawala. TANESCO inatutesa au mnabisha? Nani dhaifu aliyempa Wiliam Mhando kuwa mkurugenzi wa Tanesco au ni Zitto mwenye Mazito juu ya rushwa za wakuu?

    17. #294
      Kichiringa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 12
      Rep Power : 362
      Likes Received
      2
      Likes Given
      1

      Default Re: Wachaga wa chadema waungana na ccm kumdhiti zitto kabwe

      Quote By Msiba
      Ktika hali isiyokuwa ya kawaida wachaga waliop chadema wameungana na wabunge wapenda posho wa ccm ili kumuadabisha Mh zuberi zitto, yote hayao yametokana na mambo makuu mawili;

      1.Zitto kukataa posho na kuendelea kutozichukua mpka leo, wahafdhina ndani ya chadema wameona wanaaibika hasa baada ya mbungewa iramba mwigulu kuwachana ukweli, kma hiyo hitoshi wabunge wengi wa chadema ambao ni wa kaskazini waliingia kwenye chama na lengo lake likiwa ni kupata pesa , walitumia mbinu nyingi sana kumharibia zitto reputation yake ndani ya jamii na nje ya siasa ili aonekane yeye amehongwa au alikuwa na ubia na mhando wa tanesco.

      2.Kitendo cha zitto kutangaza kugombea urais 2015 kiliwastua sana wachaga kiasi cha kutengengeneza mkakati wa kummaliza kwenye medani za siasa kwa kushirikiana na ccm, ikumbukwe kwenye maswala ya ukabila wachaga huweka nje itikadi zao, na hiyo kazi alipewa selasin amabaye uhusiano wake na wachaga wenzio haupo na alizungumza vitu vingi sana
      Kama CHADEMA wataendelea na huu ujinga 2015 chma hakifiki na hata kikifika ccm wameshajuwa mahali pa kuwamamlizia ni juu ya urais na posho pekee yake.

      Mnyika ambaye yeye daiama ni mnafiki huwa anazungumzia hilo chini ya meza na maelezo yake niliyoyapata kwa njia ya kiintelejensia nitayaweka very soon baada ya secretary wangu kumalaiza kuyatype. Kafulila alisema CHADEMA ni ya wachaga na wewe ukijifanya ni yako wako tayari kukuharibia kwa gharama yoyote ile

      Msiba,

      kweli nimeamini una Msiba. Ukiisha huo msiba tujuze.......

    18. #295
      Kilbark's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Mbekenyera
      Posts : 483
      Rep Power : 670
      Likes Received
      24
      Likes Given
      20

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Zitto (sorry to mention his name) is just a proxy of the current ruling system.
      MASHOGA, WASAGAJI, MAMENDE WAUAWE. HAWANA TOFAUTI NA WAUAJI WA MA ALBINO.

    19. #296
      Tumaini Makene's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2012
      Posts : 1,062
      Rep Power : 8907
      Likes Received
      2231
      Likes Given
      768

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Quote By Kimbunga
      Mkuu Mwita Maranya sifanyi siasa za kichovu ninachosema ni kweli na kweli tupu bila kumung'unya maneno. Mwita nakujua wewe ni CDM makini. Naomba uniambie msimamo wako binafsi na msimamo wa CDM kuhusu posho ambazo zilipigiwa kelele kwenye bunge la mwaka jana.

      Kimbunga


      Mwita Maranya kakwambia nusu ya ukweli unaopaswa kuambiwa, kutokana na namna unavyojenga hoja zako hapa mara kwa mara. Unataka kujua msimamo wa chama juu ya ufisadi wenu wa kitaasisi (institutionalized fraud) kupitia mfumo wa posho? Usisumbuke mkuu, pata nakala ya ilani ya CHADEMA!

      Kupinga mfumo wa posho na badala yake kuhitaji uhuisho wa mishahara kwa watumishi wa kada zote, ni kwa CHADEMA ni suala la kisera mkuu. Hivyo kama Mwita Maranya ni mwanachama/mpenzi makini kama ulivyokiri wewe hapa, basi tayari msimamo wake unaujua kupitia msimamo wa chama katika suala hili.

      Jifunze kuitafuta na kuisema kweli tupu. Fanyia kazi ushauri wa Mwita Maranya.
      nsanu likes this.
      "Nothing in the world is more dangerous than sincere ignorance and conscientious stupidity." Martin Luther King

    20. #297
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,513
      Rep Power : 19750
      Likes Received
      5443
      Likes Given
      3640

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Quote By BinMgen
      Mbona katulia! hebu angalia kauli yake hii "Kwa kuwa ‘my conscious is clear’, (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli.by zitto
      Nilikuwa sijui kama na wewe ni Mc wa Kigoma All Stars, naona umekariri kama kasuku huo msemo.
      Kwakuwa una mahaba na Zitto mfikishie ujumbe huu, mwambie kama shida yake ni Urais basi anaweza kuwa Rais wa TFF au Rais wa THT au hata Miss Tanzania.
      Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.

    21. #298
      ruzinga's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th February 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 371
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Wachaga wa chadema waungana na ccm kumdhiti zitto kabwe

      mambo ya dini yametoka wapi tena! hao wezako mliopo ktk dini moja ndo wameimaliza nchi kwa wageni mbona husemi, acha udini mkubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    22. #299
      Chiya Chibi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2011
      Location : Penye Oxygen
      Posts : 441
      Rep Power : 486
      Likes Received
      102
      Likes Given
      12

      Default Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

      Kama katiba ingeruhusu na Nchi ingekuwa na pesa, ningeshaul bunge livunjwe il tuanze upya, ninavyoona uchafu ni mwingi, kamati zote zimeoza, maswal ya rushwa kwa wabunge we2 ni meng kuliko majibu, naona 2015 ni mbal kufanya maamuz mazito na kadri tunavyozidi kuwaacha ndivyo nchi inavyozid kuliwa. CHADEMA mjipange tu, kama Zito, Mnyika na wengineo ni wachafu, bas muwamwage tu kama wale madiwan wa Arusha.

    23. #300
      Sisomeki's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th March 2012
      Posts : 86
      Rep Power : 381
      Likes Received
      21
      Likes Given
      27

      Default Re: Wachaga wa chadema waungana na ccm kumdhiti zitto kabwe

      Quote By Msiba
      Ktika hali isiyokuwa ya kawaida wachaga waliop chadema wameungana na wabunge wapenda posho wa ccm ili kumuadabisha Mh zuberi zitto, yote hayao yametokana na mambo makuu mawili;

      1.Zitto kukataa posho na kuendelea kutozichukua mpka leo, wahafdhina ndani ya chadema wameona wanaaibika hasa baada ya mbungewa iramba mwigulu kuwachana ukweli, kma hiyo hitoshi wabunge wengi wa chadema ambao ni wa kaskazini waliingia kwenye chama na lengo lake likiwa ni kupata pesa , walitumia mbinu nyingi sana kumharibia zitto reputation yake ndani ya jamii na nje ya siasa ili aonekane yeye amehongwa au alikuwa na ubia na mhando wa tanesco.

      2.Kitendo cha zitto kutangaza kugombea urais 2015 kiliwastua sana wachaga kiasi cha kutengengeneza mkakati wa kummaliza kwenye medani za siasa kwa kushirikiana na ccm, ikumbukwe kwenye maswala ya ukabila wachaga huweka nje itikadi zao, na hiyo kazi alipewa selasin amabaye uhusiano wake na wachaga wenzio haupo na alizungumza vitu vingi sana
      Kama CHADEMA wataendelea na huu ujinga 2015 chma hakifiki na hata kikifika ccm wameshajuwa mahali pa kuwamamlizia ni juu ya urais na posho pekee yake.

      Mnyika ambaye yeye daiama ni mnafiki huwa anazungumzia hilo chini ya meza na maelezo yake niliyoyapata kwa njia ya kiintelejensia nitayaweka very soon baada ya secretary wangu kumalaiza kuyatype. Kafulila alisema CHADEMA ni ya wachaga na wewe ukijifanya ni yako wako tayari kukuharibia kwa gharama yoyote ile
      akili yako imewaza na hapo ndio mwisho? your so useless

    Page 15 of 18 FirstFirst ... 51314151617 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...