Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

    Report Post
    Page 8 of 9 FirstFirst ... 6789 LastLast
    Results 141 to 160 of 163
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16308
      Likes Given
      8393

      Default Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!


      Katika umaskini wetu tumejifunza kufurahia! MM

      Kumekuwa na tabia ya "kuumbuana" huko ndani ya chama tawala. Hili halikuanza leo Jumamosi. KUanzia wakati wa Mrema, Mzindikaya na wengine hakuna shaka hata kidogo kuwa wapo watendaji wa serikali ya CCM ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kujinufaisha. Richmond ilifunua hili, kashfa ya sukari ilifunua hili kama vile kashfa ya EPA ilivyolifunua. Hakuna geni!

      Kwamba leo kwenye wizara ile ile ambayo kila mwaka imekuwa ikikumbwa na kashfa inaibuliwa kashfa nyingine si jambo la kushangaza, na kwa hakika siyo jambo la kusema "siamini hili linawezekana". Mtu anayesema hivyo alikuwa wapi miaka mitano iliyopita? Ati leo Prof. Muhanga kusema kitu ambacho Mnyika naye alikisema jana imekuwa ni "hongera, kudos, jasiri!" wakati hapa hapa tulikuwa mwaka 2008 wakati watu walitajwa na Waziri Mkuu akajiuzulu! Wangekuwa wanajifunza yasingerudia tena!

      Ili kukamilisha onesho lao la mazingaombwe wanavunja kamati ya nishati na madini; ili kiwe nini? Wote waliokuwemo kwenye hiyo kamati bado wapo Bungeni. Hakuna mtu tuliyeona ametiwa pingu na kuondolewa Bungeni; hata TAKUKURU watakapotangaza kuwa wameanza uchunguzi (na watafanya hivyo sometime next week au mapema zaidi) watu wataanza kushangalia kuwa sasa TAKUKURU ifanye kazi yake!

      Kwamba Mhando (Mkurugenzi wa Tanesco) amejipa mkataba yeye na mke wake na kukiuka waziwazi sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya 1998 halina shaka. Lakini cha kushangaza ni kuwa ati Waziri anaenda kumlipua Bungeni badala ya aliyemteua kumfukuza kazi, kumtia pingu na kuhakikisha anaingia gerezani yeye na wote waliowezesha dili hilo.

      Siyo hivyo tu, kwamba Bungeni wabunge wanajuana nani anakula rushwa na wanazungumza wakisukumizwa siyo na uzalendo bali na vilivyomo "mfukoni" na Bunge lenyewe linashangilia kuwa "waambie hao!" halafu bado watu wanakaa kujadili bajeti hiyo hiyo. Tunajuaje hao wanaopiga kelele za "sema sema" na "waambie waambie" na wenyewe hawafanyi hivyo kwa nguvu ya mifuko mingine?! Tumeona Spika anavyoendesha Bunge tunajuaje kama naye haendeshi kwa sababu kuna mifuko kadhaa huko nyuma? Tunaona Mwendesha Mashtaka Mkuu na Mwanasheria Mkuu hawafanyi lolote kuonesha nchi yetu inasheria je yawezekana na wenyewe wamepewa "mlungula" (vijana wanaweza kuwa wamelisahau hilo neno).

      Tunaona Rais akiteua watu ambao wana mashaka na anawavumilia na kuchafua kabisa utumishi wa umma; na ukimya wake unapiga kelele? Je yawezekana na yeye yuko na huu mtindo wa kukaa pembeni kwa sababu naye anautumikia mfuko mwingine? Nani ni msafi basi kama waliozungumza na kudhaniwa wasafi kumbe na wao wamechafuka na wale ambao wanapiga kelele zaidi ya uchafu kumbe wenyewe pia ndio wachafuaji? Nani anaweza kuaminiwa? Rais haaminiwi, Waziri Mkuu haaminiwi, sasa Bunge nalo linaonekana haliwezi kuaminika. Tutaamini vipi tukiona mtu anazungumza kwa uchungu kumbe ni uchungu wa kuogopa kupoteza 'wema na fadhili'?

      Hakuna namna ya kusafisha hili isipokuwa kuvunja hili Bunge kwani limechafuka na kulichafua taifa. Sijui watalivunja vipi lakini wananchi wasiwe na imani nalo na hawapaswi kuwa na imani nalo hasa kama watuhumiwa ndani yake bado wapo. Kwani si tuliambiwa kuwa kuna wabunge walikatiwa kitu wakati wa sakata la Jairo? Wako wapi? Wametiwa pingu lini? Nyet! Halafu kweli sisi na akili zetu tukiwa wanafunzi wa zuri wa historia ya karibuni tunaweza hata kutoa pongezi? POngezi kwa kitu gani? kutaja majina? kutuambia kinachojulikana?

      Nani hajui watumishi wanavyojipa miradi wao wenyewe kwa wenyewe au kupitia jamaa zao? kwani ripoti ya CAG ya karibuni haikuonesha hili kwenye halmashauri mbalimbali ambapo madiwani kadhaa wamejigawia tenda? Kwani ni mara ya kwanza kuona mtu anauzia serikali kitu kwa bei tofauti (marked up) huku akijua kabisa kuwa bei halisi ni ya chini? Kwani ni mara ya kwanza kuona mtu anapodai mafao yake ili yafanyiwe uzuri uzuri anaweza kuongeza kidogo ili aweze kumkatia chochote mtumishi wa utumishi ili mambo yaende vizuri?

      Watanzania tunapenda sana drama! Tunakuwa kama tunasikiliza "Penzi Kitovu cha Uzembe" au "Aliyejuu". Tunasubiri wiki baada ya wiki kuangala kuna nini kipya. Wapo kweli kabisa ambao wamekaa kwenye viti vyao wanacheka kweli na kusifia kuwa "bunge letu kali sana" au "waziri huyo bomba sana". Really? Kwa lipi? Ni kipi ambacho kimesemwa leo ambacho hakijawahi kusemwa huko nyuma? Ni madai yapi ambayo yametolewa leo ambayo yanashangaza kweli kuwa yanawezekana? Kwa vile katajwa mchungaji? Mbona wengine tulishamtaja huyu na kuandika hapa achunguzwe leo watu wanashtuka?

      Tutafungukaje kama tunashangilia mazingaombwe na kupongeza viini macho? Tumeharibiwa na kitu gani kiasi kwamba tunaridhishwa na vitu vidogo kama watoto wanapopewa chuchu za plastiki kunyonya ili waache kulia! Tunapewa hizi pacifiers za maneno na tunajisahau na kuanza kuimba "Kidumu, kidumu"? Mbona hakuna jipya? Mbona ni yale yale. Shilingi ukigeuza upande wa pili haibadiliki thamani! Kinyonga akijigeuza rangi bado hubaki kinyonga! Wizara ya nishati na madini imekuwa ni kitovu cha kashfa nyingi tu lakini leo ndio watu wanataka tushtuke kuwa kuna ufisadi? Really?

      Ukiwaambia hili watakimbilia "tatizo siyo sera ni watu"! Na wapo wanaoamini hivyo kabisa. Kwamba wakibadilisha watu sera zitatekelezeka! Miaka 50 wamebadilisha watu wangapi!?

      Mojawapo ya falsafa za uongo (deceptive philosophy) zinazonezwa sana ili kuzuia watawala kuwajibishwa ni hii ya "kuona mazuri vile vile". Kwamba, wananchi wanatakiwa waone mazuri ya kuyasifia ili watawala wajisikie vizuri. Ni falsafa ya uongo kwa sababu serikali kufanya mazuri siyo hisani na wala siyo 'optional'! Ni wajibu wa serikali kufanya mazuri na haiitaji kusifiwa kufanya mazuri.

      Kwamba, serikali ikijenga barabara kwa kodi za wananchi isifiwe? Kwamba ikijenga hospitali - hata kama hazina madaktari, nyenzo au madawa ya kutosha- bado isifiwe kwa sababu ni jambo "zuri"? Kwanini umsifie Waziri kwa kufichua ufisadi? alkuwa na option ya kutofichua!? Polisi akikamata mwizi asifiwe kwa kukamata mwizi? alikuwa na option ya kutomkamata?

      Watawala wanaotumia kodi ya wananchi kuleta maendeleo na watu hao waliomba kibali kuwaongoza wananchi hawana sababu ya kusubiri wananchi kuwasifia "kwa mazuri" wanayoyafanya? Jukumu la wananchi kuangalia mabaya yanayofanywa na kuimbia serikali kwamba haya ni mabaya! Kwa sababu siyo jukumu wala sababu ya serikali kufanya madudu!

      Ndio maana nimesema hapo juu wale wanaoona kuona "upande wa pili" unaostahili sifa wafanye hivyo! Inapokuja serikali haisifiwi kwa kufanya mazuri, kwa kusimamia sheria au kwa kutumiza wajibu alioapa kuutumiza. Sasa Prof. Muhongo anasifiwa kwanini hasa? Ndio maana utaona miye SISIFII KABISA nikisikia mbunge kasema vizuri Bungeni au sijui katetea jambo gani bungeni! Ni WAJIBU WAKE! Kama anataka kusifiwa akichambua hoja au akipinga hoja atoke aje huku nje tumsifie! Aliomba kura kwenda Bungeni kuwatumikia wananchi; yeye anahitaji kutusifia sisi wananchi kwa kumtuma kufanya kazi. Yaani tumuajiri, tumlipe, tumpe marupurupu lukuki halatu tukae pembeni tuanze kumsifia kwa kuzungumza?

      Tuna matatizo gani sisi?

      Watu pekee wanaostahili sifa ni wale wanaofanya vitu kwa kujitolea na kujituma wenyewe si kwa sababu wanalipwa au wameajiriwa. WAkitaka kupongezwa vyama vyao viwaandalie sherehe ya kuzungumza vizuri Bungeni na za kufichua ufisadi. Kwa sisi wananchi hatutaki kuona ufisadi it is simple as that. Kama hawawezi kufanya kazi au kutimiza wajibu wao bila kusifiwa waache!!!

      Kwani nani kasema Tanzania kuna tatizo la umeme?

      Hadi watu watakapojua kuwa tatizo la Tanzania ni CCM na sera zake zilizoshindwa wataendelea kutumainia mabadiliko chini ya CCM kama vile watu wanaokinga mikono yao jangwani wakiombea mvua inye! Kinachoniudhi mimi zaidi na kwa kweli naanza kufikia ukomo wa kuvumilia ni hizi hotuba za wapinzani ambazo nazo zimejaa maneno ya kutarajia serikali ibadilike kiasi kwamba wanasahau kilichotufikisha hapa ni sera zilizoshindwa za CCM. Siyo udhaifu tu wa Kikwete, siyo tu ulegelege wa Bunge na uzembe wa CCM - ni sera mbovu ambazo zimekuwa na matokeo mabovu kwenye kila sekta - angalia afya, angalia Elimu, angalia Elimu ya Juu, angalia Nishati na Madini, angalia usalama. Ni ubovu ubovu ubovu tu. Halafu leo tunaambiwa juu ya ubovu zaidi tunaanza kushangilia!

      Kama kujua ubovu ni fahari basi tutengeneze mnara wa kumbukumbu za kashfa mbalimbali za ufisadi. Tuchonge sanamu za wahusika wa ufisadi huo na majina yao tuyachirize kwenye mnada huo. Kila mwaka tutenge siku ya kuwakumbuka mafisadi wetu na tuweke shada la maua. Iweje tushangilia kujua ubovu na kuambiwa ubovu ambao tayari tunaujua. Kwanini tusishangilie tukisikia Waziri afungwa miaka 400 jela; au Mbunge ahukumiwa miaka 30 jela kwa ufujaji? Kila mtu anajua hili haliwezi kutokea. Tutapewa "kesi mahakamani" tutafanyiwa mazingaombwe isipokuwa kupewa kitu halisi!

      Nasubiri kitu halisi nami nitashangilia, haya mazingaombwe yenu chezeni nyinyi na watoto wenu na mje kuwarithisha wajukuu wenu na vitukuu vyenu pamoja na vilembwe vya vilembwe vyenu! Watawasifia kwa jinsi mlivyofurahisha macho yetu!

      MMM
      Last edited by Mzee Mwanakijiji; 30th July 2012 at 07:16.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. Study Abroad

    3. #141
      Chapakazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2009
      Location : Kathmandu
      Posts : 2,910
      Rep Power : 1095
      Likes Received
      256
      Likes Given
      272

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      umeyasema yaliyo moyoni mwa wengi!
      Change begins with YOU

    4. #142
      mangikule's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 907
      Rep Power : 530
      Likes Received
      174
      Likes Given
      235

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Wapi Rostam!! mnakamata dagaa mnaacha papa!! tusidanganyane

    5. #143
      Arushaone's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st March 2012
      Location : Arusha
      Posts : 6,351
      Rep Power : 40133
      Likes Received
      5014
      Likes Given
      16211

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Mzee mwanakijiji una hekima sana.. I can say it openly. But tatizo hapa na ambalo everyone should understand ni hili; tanzania ni zaidi ya vile tuijuavyo. Same fisadis, same system, same country, never expect positive outcome out of it.

    6. #144
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16308
      Likes Given
      8393

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Najua watu wengi mmeangalia picha hiyo na kuangalia hao wanaosoma magazeti hapo kijiweni. Usipoaiangalia hiyo picha vizuri unaweza kukosa kuona watu wengine ambao wanatuma ujumbe mzito zaidi kuliko hao waliosimama hapo kudoea magazeti.
      Mkandara likes this.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    7. #145
      M-mbabe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2009
      Location : here n' there
      Posts : 1,297
      Rep Power : 745
      Likes Received
      326
      Likes Given
      352

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      ....................
      Tuna matatizo gani sisi?

      ..........................
      a million dollar question...that one.
      If you're not ready to die for it, put the word 'freedom' out of your vocabulary (Malcolm X)

    8. FemaTV & Radio

    9. #146
      Kisoda2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th May 2008
      Posts : 841
      Rep Power : 728
      Likes Received
      42
      Likes Given
      253

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Quote By Mr Rocky
      Nafikiri mkuu Kisoda2 haya mambo ya kusema kesi iko mahakamani haifai kuhojiwa yafikie mwisho wake tuone kile kinachotokana na hizo kesi mahakamani
      Maana inawezekana kesi mahakamani then mshatakiwa anakuja kuachiliwa kwa kukosa ushahidi au kutokuwa na kesi ya kujibu na hapo moto wa ile kitu unakuwa umeisha kabisa
      Tufikie mahali tuhoji haya mambo tuone wahusika wanapelekwa kweli mahakamani na kesi yao inaamuliwa kwa kipindi kifupi na tunaona uwajibikaji au wa kurudisha kile kilichopotea au kufilisiwa
      Kesi za akina Mramba na Yona mpaka leo ni danadana hatuoni maemdeleo na itafika 2015 tutadanganywa kuwa tumewafikishamafisadi mahakamani na si mnaona akina fulani na kura tutawapa tena
      haya ndio yanayotumpumbaza wananchi tuache kuhoji mambo ya maana tuwasikilize uwongo wanaotulisha



      Mkuu Sangarara nakubaliana na wewe kabisa
      Kuna sehemu wamekaa watu wanaanzisha zengwe wananchi wajadili kwa hasira na pupa wakiona single yao inaanza kuchuja wanalianzisha tena jingine ili wananchi wasahau lile la kwanza zito waanze kujadili jepesi
      yaani hizi single zao hazikao sokoni kabisa yaani zinatolewa mara kw amara wanapoona kuna haja ya kutoa single kuwasahaulisha wananchi na yale yaliyopita
      Wasahau mpaka shida zao waanze kujadili lile tukio
      Mkuu, hii kitu ipo long time kitambo ndani ya sisi mwizi. ndo maana wa kitengo cha propaganda. kila siku kazi yao ni kufikiria namna gani ya kutuhamisha toka topiki hii kwenda nyingine!
      na hili wana lijua kuwa wengi wet tu wavivu wa kuchambua(tunapenda rahisi rahisi) na hatuna utamaduduni wa kuhoji tukio la kwanza limeishia wapi, basi kwao inakuwa nyepesiiiii kutuinmgizia single mpya na kuisahaulisha ya kwanza.
      Tuamke/tuamshane!!
      " Masikini haishiwi NDOTO !!! "

    10. #147
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16308
      Likes Given
      8393

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      sasa viko wapi?
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    11. #148
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7367
      Likes Received
      6150
      Likes Given
      22265

      Default

      Quote By Maundumula
      Mzee Mwanakijiji,

      Hii nchi ina sheria na taratibu zake, huwezi kukurupuka tu kumtia mtu pingu na kumtupa lupango bila kufuata hatua stahili. ....usikurupuke tu kutaka kuona watu wanatiwa pingu mwishowe yanakuwa yale yale

      Msipende kuhadaa wananchi...
      Mkuu Maundumula, hapa unamaanisha nini?!. Unamaana kuna watu humu jf wanakurupuka?!. Yaani kuna watu humu jf wanapenda kuhadaa wananchi?!. Ni wakurupukaji wepi unaomaanisha wewe na ni hadaa zipi hizo hao wakurupukaji hupenda kuwaahadaa wananchi?.

    12. #149
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Najua watu wengi mmeangalia picha hiyo na kuangalia hao wanaosoma magazeti hapo kijiweni. Usipoaiangalia hiyo picha vizuri unaweza kukosa kuona watu wengine ambao wanatuma ujumbe mzito zaidi kuliko hao waliosimama hapo kudoea magazeti.
      Duh yaani umeenda hadi kwa mama ntilie wanavyosumbuka na maisha wakati mabillioni yanaibiwa mkuu wangu - well life goes on!
      Mzee Mwanakijiji likes this.
      Exploration of reality

    13. #150
      Adharusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd January 2012
      Location : Mtwara
      Posts : 466
      Rep Power : 462
      Likes Received
      62
      Likes Given
      295

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Nilini tutakua na ujasiri Watanganyika...yale tunayo yaandika tukaweka katika vitendo
      'Vox populi,Vox dei"

    14. #151
      Nguto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 598
      Rep Power : 529
      Likes Received
      80
      Likes Given
      3

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Kweli mkuu, siasa nzuri ni ya "kutafuta hele kihalali!!"
      Quote By The Boss
      kufuatilia siasa za nchi ni 'hatari kwa afya yako'

    15. #152
      Gang Chomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th February 2008
      Location : hell
      Posts : 5,015
      Rep Power : 1719
      Likes Received
      961
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Gang Chomba
      Sasa hivi asilimia 70 ya watanzania wameshasahau sakata la Dr Ulimboka...
      Woooote wako kwenye sakata la wizara ya Nishati na Madini...

      THE SAGGA CONTINUA...
      65% ya watanzania kwa sasa hawafuatilii sakata la Dokta Ulimboka, hawafuatilii mgomo wa walimu wala Madaktari, hawafuatilii sakata la wizara ya nishati na madini......wooote akili zao kwa sasa zipo ktk msuguano wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
      BADILI TABIA likes this.

    16. #153
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,547
      Rep Power : 5611
      Likes Received
      6208
      Likes Given
      2281

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Gang Chomba,

      akili za watu sasa hivi zipo ziwa nyasa.....watanzania watu wa matukio sana loh..



      Quote By Gang Chomba
      BADILI TABIA

      Sasa hivi asilimia 70 ya watanzania wameshasahau sakata la Dr Ulimboka...

      Woooote wako kwenye sakata la wizara ya Nishati na Madini...
      "Behind every great fortune there is a crime."
      - Honore de Balzac (1799-1850)

    17. #154
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16308
      Likes Given
      8393

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Tuliposema watu wanashangilia mazingaombwe... na viinimacho...
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    18. #155
      zeus's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 13th August 2009
      Location : near
      Posts : 207
      Rep Power : 538
      Likes Received
      40
      Likes Given
      32

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      This is a thoughtful post. Nilipost hapa juzi kwamba we do not reforms as such, we need an immediate and complete overhaul of the system. Sasa napata impression kwamba opposition wanatuangusha kwa kutoshindilia moja kwa moja msumari wa mwisho kuitisha wananchi wote ku-overhaul huu mfumo wa umaskini. Main oppoistion are becoming merely predatory, going to the edge and back, instead of pursuing one and the decisive measure. au nao ni walewale nini?
      Last edited by zeus; 23rd November 2012 at 22:50.

    19. #156
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16308
      Likes Given
      8393

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Tukiuliza kiko wapi sasa... I hope we are wrong..
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    20. #157
      mpalu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th September 2010
      Location : MZINGIZINGI
      Posts : 1,537
      Rep Power : 747
      Likes Received
      405
      Likes Given
      359

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Quote By The Boss
      kufuatilia siasa za nchi ni 'hatari kwa afya yako'
      fuatilia lakini for your own risky
      When a person suffers from a delusion it is called insanity; when many people suffer from a delusion it is called religion.

    21. #158
      juju man's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th August 2012
      Posts : 27
      Rep Power : 346
      Likes Received
      4
      Likes Given
      10

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      mwisho wao umekaribia.....nahuzunishwa sana na fikra zao mgando....zinazojali maendeleo ya vitu na kuwaweka watu pembbeni....bila elimu na afya bora taifa litaangamia.

    22. #159
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16308
      Likes Given
      8393

      Default Re: Wanashangilia mazingaombwe na wanasifia viini macho! ... Silly People!

      Ile furaha ya hotuba motomoto, na kutajana majina na kuumbuana imeishia wapi? Watanzania tuanze kukataa mazingaombwe!!!
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    23. #160
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,662
      Rep Power : 974
      Likes Received
      576
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Ile furaha ya hotuba motomoto, na kutajana majina na kuumbuana imeishia wapi? Watanzania tuanze kukataa mazingaombwe!!!
      bado hawaamini kwamba yale yalikuwa maigizo!

    24. Miaka 50
    Page 8 of 9 FirstFirst ... 6789 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...