Ndio maana mkuu wanngu nilitaka watu warudi nyuma kufikiria kwanza tumefika fikaje hapa?..Ukisha jua tulikotoka haya yanayotokea leo hii majibu yake ni rahisi kabisa..Hakuna mtu hapa asiyejua kwamba hii mitambo yote inayotumaliza leo hii ni mitambo iliyotokana na swala la DHARURA..
Sawa ulazima wa wakati ule kuwanunulia mafuta ulionekana kwa sababu sisi ndio tulitaka umeme haraka kuziba pengo lilokuwepo hadi pale tutakapo kuwa tayari wakapiga mahesabu na kusema miaka miwili. Na ndio maana mikataba ya mwanzo ilikuwa ya muda mfupi.. Mara ghafla wajanja wakaingia, Tukapigwa na changa la IPTL, hatujakaa sawa Richmond hizi zote japokuwa ziliingia bado ktk mikataba ya dharura lakini dharura isokwisha.. Imeendelkezwa mpaka leo makusudi kabisa..Tunaendelea kuwalipia mafuta na kwa ujinga wetu tunatazama mafuta na ughali wake kumbe kinachofanyika hapa ni kuhakikisha hatuwezi kuenga miradi yetu wenyewe kuhakikisha tunafuta mikataba ya dharura..
Chief katoa mfano wa usafiri wa kwenda Morogoro na bus la Aboud unamnunulia mafuta halafu ukisha fika Morogoro anakutoza Nauli...Chief mimi nasema sii afadhali hiyo maana ni gharama ya siku moja tu. Kilichofanyika ni sawa na kwamba wewe uliharibikiwa usafiri wako njiani, ukawaomba Aboud wakufiishe Morogoro mkakubaliana utanunua mafuta halafu utalipa nauli.. Kwa sababu ulikuwa na shida ukakubali matumizi makubwa ya siku moja tu... Ukalipa na kupewa ride hadi Moro, deal limekwisha..
Tatizo la Tanesco sasa ni kwamba lile deal la dharura watu (viongozi wa serikali) wakalichezea mchezo sasa likawa ndio mpango mzima - ndio usafiri wako kwa sababu kwanza sii hela unazotoa hazitoki mfukoni mwako halafu pili kumbe Aboud ni bus la mjomba..Kwa hiyo unaweka mkataba kuwa ni lazima usafiri uwe Aboud kila siku, lijazwe mafuta halafu tulipie kodi ya siku kama vile vile unavyokodisha Limo, usafiri usisafiri tozo la siku halishuki iwe umeenda Moro au hapana, kapanda mtu au hukupanda. IPTL ni Limousine tulokodisha kwa msiba usokuwepo..
Halafu mashirika mengine pia yanavutwa ktk kukodisha kwa safari za Mwanza, Mbeya, Arusha wote wanaahidiwa kupewa mafuta na wakati mwingine vipuli wakikwama kabisa halafu bado tunawalipa wote sii nauli bali kukodisha kwa siku nzima...Kama mnakumbuka vizuri tunavyofanya ktk maharusi au misiba huwa tunakodisha Costa kwa siku na huwa tulinalipia mafuta, dereva na cha juu kwa uukodishaji wa siku nzima au safari yenyewe.
Na tukisha maliza msiba ama shughuli za Harusi deal linakufa mwenye Costa anaendelea na biashara zake nasi tutarudi ktk usafiri wetu wa kila siku.. Tatizo la Tanesco huku kukodisha kwa dharura ya msiba huu msiba haiuishi kila siku tunamuua ndugu ili bus likodishwe..Sasa ni kiasi gani kinalipwa kwenye kukodisha bus sio tatizo mama, Tatizo lipo ktk mfumo huu wa kukodisha magari na kuendelea kuua ndugu zetu wakati hakuna msiba wowote..Hizo Costa zimekuwa sasa ndio usafiri wetu wa kudumu, tukiwanunulia mafuta na vipuli halafu sasa imefikia tunawavutia kabisa bomba la gas toka Kusini.
Halafu tunasema Kwa nini Tanesco wanashindwa kujiendesha. aaah kwa sababu mafuta yamenunuliwa ghali wangefanya hivi ama vile kwa nini hawakununua ya rahisi - guyz sisi hatukutakiwa kuwa ktk mpango huu hata kidogo..Mimi nasema hivi kwa nini bado tunakodisha hii mitambo? ilikuwa ya dharura hii dharura itakwisha lini..Hutapata jibu kwa sababu hii kitambo au hizi Costa ni za Viongozi wenyewe..Nchi haina Umeme lakini viongozi wetu wamenunua mashangingi Ma VX kila mmoja wao watu zaidi ya 500.. nina hakika wangechukua gari za thamani chini ya Usd 50,000 tu tungekuwa na mtambo mmoja mkubwa sana wa kutosheleza Dar na vitongoji vyake..
Follow Us Here