Na Salma Said,
Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, Mansour Yusuf Himidi, amesema atasimamia mtazamo wake kuhusu muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaofaa hata kama itapelekea kuvuliwa uwanachama.
Mwandishi wa DW Zanzibar, Salma Said, amefanya mahojiano na Mansour Yussuf Himidi, ambaye ni waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusiana na kauli za Katibu Mwenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, na wajumbe wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, kumtaka arudishe kadi ikiwa hakubaliani na sera ya sasa ya serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Habari hii kwa kirefu na audio clip, soma post HII
Kama CCM walishindwa kuvuana magamba basi hata hili litapita tu kama kawaida yao hivyo hapa hakuna jipya.
You can never have someone praise you,nor will anyone condemn you,never in the past,not at present and never will be in the future.
Vigogo wa wasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar sasa wasanifiwa na Nape mtu asaijuwa Zanzibar historia yake ndewe wala shikio Inaoneka na Muungano utamalizwa na kuvunjwa na wana wa Mapinduzi.
"Wallahi inanishangaza! wataka kutwambia 'platforms' zote alizotumia Mh Mansour kuelezea msimamo wake (na kwa kweli msimamo wa waZnz wengi wetu) ni kuropoka barabarani! ama kweli hizi ni dharau za mwisho! yaani pahala patakatifu kwenu nyie ccm ni huko dodoma tu? ..... nashangazwa na uoni wako hapa Mh. hivi hujui nani anaelazimisha huu muungano?? salaale! kwa uchache tu, hukumbuki 'hali ya hewa kuchafuka Znz, enzi za Mh Jumbe? ..... hukijui kipi kilowafukuzisha CCM maalim Seif na wenzake ..... hukumbuki vipi ajenda tu iloanzishwa bungeni ya G55, ile ya kudai Tanganyika? na mengineo mengi ....
Mh Muungano mnaulazimisha nyinyi viongozi wa CCM wa Tanganyika mkishirikiana na vibaraka wenu wachache waliopo hapa Znz, sisi tulio wengi hatuutaki huu muungano, na kwa kweli ushafika wakati hamna njia tena ya 'kuulinda kwa nguvu zenu zote' ..... hauishi tena katika nyoyo zetu, kama ni muungano uwe wa kimkataba, habari ndio hio.
Mtuwacheee Tupumueeeeeeeeeee! "
Simple life is healthier than egoism.
Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amesema potelea mbali kama ni kufukuzwa katika chama chake cha CCM lakini hatasita kuitetea Zanzibar
Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amesema yupo tayari kunyanganywa kadi ya chama hicho lakini hataregeza msimamo wake juu ya kuitetea Zanzibar katika Muungano. Kauli ya Mansoor imekuja siku chache baada ya chama hicho wilaya ya mjini kutoa maamuzi ya kuwataka viongozi wenye kupingana na msimamo wa chama kurejesha kadi za chama hicho au kuacha tabia hiyo mra moja.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Ujerumani (DW) jana Mansoor alisema kamwe hawezi kuogopa vitisho vinavyotolewa na watu wenye kujipa madaraka na udikteta ambao hawataki mabadiliko wala mawazo tofauti. Mansoor aliahidi kuendelea na msimamo wake katika kudai mabadiliko katika muundo wa Muungano na kusema kwamba msimamo wake hautabadilika licha ya vitisho vya baadhi ya Viongozi wa Chama hicho.
“Nimesema hayo tokea muda mrefu chama hiki kimetukuka na kina heshima na maadili yake ni baadhi ya watu wanataka kutuziba midomo lakini Mimi sijasema leo nimesema tokea 2008-2009 juu ya msimamo wangu juu ya mfumo wa muungano na leo naendelea kusema tena hata ikipidi kunyanynganywa kadi mimi narejea tena kuwa mfumo huu wa serikali mbili sikubaliani nao na nitaendelea kusema ahivyo hivyo siwezi kubadilisha maoni yangu leo baada ya kuwa na msimamo miaka yote hayo” alisisitiza Himid ambaye ni Mjumbe wa NEC.
Aidha alisema Chama Cha Mapinduzi wilaya ya mjini hakina mamlaka ya kuitisha kikao na kutoa maamuzi kama hayo ambapo alisema ni watu wachache wenye nia ya kutaka kuwanyamazisha watu wenye maoni tofauti na wao. “CCM wilaya ya mjini hawana mamlaka hayo, lakini pia hawana uwezo wa kutunyamazisha kwani CCM haijakataza wanachama wake kuwa na mawazo tofauti sasa nashangaa hao wanaosema sisi tumekiuka msimamo wa Chama ni msimamo upi maana mchakato wa katiba upo huru na kila mtu anatakiwa kutoa maoni yake” Alisema Himid.
Katika kuonesha kukasirika kwake na uamuzi huo wa kutaka kuwanyanganya kazi, Muweka Hazina huyo wa CCM alisema kwamba ni jambo la aibu kwa CCM Wilaya ya Mjini kufanya vitendo vya kibaguzi na vya udikteta kutaka kuwafunga midomo watu wasitoe maoni yao. Alisema hakuna makosa kwa wana CCM kuwa na mawazo tofauti kwani kila mmoja ana haki ya kutoa maoni na kueleza msimamo wake na tabia ya kikundi cha watu kujiona wao ndio wenye mamlaka na wenye chama ni kosa na halipaswi kuachiwa.
“Hao ni ni wabaguzi hawataki watu waseme ukisema unaonekana msaliti, hao ni watu wenye mawazo mgando hawataki kusikiliza fikra nyengine wanataka wanachosema wao ndio kiwe hicho hicho hilo haliwezekani na hatutakubali” Alisisitiza.
Hata hivyo alisema zama za kusema tunakwenda na fikra za mwneyekiti umepitwa na wakati na sasa jamii kubwa inakwenda na vijana amabo wanataka mabadiliko nchini hivyo aliwashauri wana CCM kuwaachia watu watoe maoni yao kwa uhuru kwani katiba tayari imetoa uhuru huo hivyo CCM hawawezi kuwa juu ya sheria.
“Hii nchi sio ya CCM peke yake hapa kuna CUF kuna Chadema na pia kuna vyama vyengine lakini wengine hawana hata vyama sasa hatuwezi kuendelea na watu ambao hawataki kuwa na mabadiliko wenye mawazo mgando …zama hizo zimeshapitwa na wakati wakati wa kwenda na fikra za mwenyekiti umekwisha” alisema Mansoor ambaye ni Waziri aisye na wizara maalumu.
Mmweka Hazina huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, alisema kitendo kilichofanywa cha kutishiwa kunyanganywa kadi ya CCM na baadhi ya viongozi hao ni cha fedheha na kimekitia aibu Chama cha CCM mbele ya wana jamii.
Himid alisema yeye ametokana na mifupa ya Chama cha Afro Shiraz (ASP) hivyo suala la kuwepo kwa dhana ya wanachama wa madaraja ndani ya CCM halipo kwa kuwa Chama hicho kinaheshimu misingi ya haki za binadamu na kuwataka wenye kudhani kwamba wao ndio wana mamalaka zaidi kuliko wengine waache tabia hiyo.
Hivi karibuni chama cha mapinduzi CCM wilaya ya mjini kilitoa tamko la kuwataka wajumbe wa baraza la wawakilishi, akiwemo Muweka Hazina wa CCM Zanzibar, Mansoour na makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar kuacha mara moja kukiuka maadili ya chama chao kwa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya muungano. Jana akihojiwa na DW, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisikika akisema kwamba viongozi wanaokwenda kinyume na madili ya chama chao watatakiwa kwenda kujieleza katika vikao na iwapo watathibitika wamekwenda kinyume basi watanyanganywa kazi au kufukuzwa.
Nape alisema mwana yoyote CCM hawezi kwenda kinyume na maadili ya chama chake na iwapo atakuwa na msimamo mwengine usiokuwa wa chama hicho basi atatakiwa kuwasilisha maoni yake ndani ya vikao na iwapo maoni hayo wajumbe hawatayaridhia basi atalazimika kurejesha kazi ya chama hicho iwapo yeye hatokubaliana na msimamo wa kikao. Akijibu suala hilo Himid alisema kuwa Nape hawezi kugawa matabaka wanachama wa CCM, wale wa Tanzania Bara na Zanzibar kwani wote ni wanachama wanahaki sawa mbele ya sheria na katika CCM.
“Sisi Watanzania hatuna uhuru, yeye amegawa kwa utabaka, sisi ni watu wazima tuna haki na uhuru, Nape hawezi kutwambia sisi watu wazima kwamba tukasema anayotaka yeye, ule wakati wa ndio Mwenyekiti haupo kila mtu ana haki yake kutoa maoni na hata Tume ya Jaji Warioba inasema hivyo” Alisema Himid. Na kuongeza kwamba. “Mimi naichukulia kuwa hii ni njama ya kutaka kuwaziba midomo Wazanzibari, hatujakiuka miongozo wala sheria tutaendelea kusema kutaka mabadiliko ya muundo wa Muungano, hii nchi asilimia kubwa ni vijana na vijana wanataka mabadiliko na hilo haliwezi kukwepwa” Aliongeza.
Licha ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa mbali ya kueleza msimamo wa Chama hicho, lakini amesema wanachama wake hawafungiki kuwa na maoni na mitazamo tofauti katika mchakato wa katiba mpya.
“Mie nadhani kuna baadhi ya watu wana fikra za udikteta, haiwezekani twende kwenye kutoa maoni tukasema tunataka Serikali mbili kama ilivyosema CCM sisi ni watu wazima tuna haki zetu na tusichaguliwe la kusema na kwa nini tuzibwe au tufungwe midogo?” Alihoji.
Mansoor amesema msimamo wake kuhusu mfumo wa muundo wa Muungano utabakia kama ulivyo kutaka kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika muundo huo kwani kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kutoka Zanzibar ambayo hayapatiwi ufumbuzi kutokana na kuwepo kwa muundo dhaifu wa Muungano. Alisema hakuna mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano, lakini ni lazima kukawepo kwa Muungano wenye maslahi ambayo hautakuwa na kero na ndio maana wamekuwa wakitoa maoni ya kutaka mabadiliko ya muundo na sio kuvunja.
“Mimi pia nakubali muungano una manufaa, lakini sikubaliani na mfumo wa Muungano na ndio maana tunasema kwa mfumo huu sebu(sitaki)” alisema Mweka Hazina wa CCM Zanzibar.
Tokea kuanza kwa machakato wa katiba wazanzibari wengin wamekuwa na maoni ya aina mbili tofauti ambapo wapo wengine wakitaka muungano kama ulivyo uendelee na wengine wakisema wanataka muungano wa serikali mbili zenye mamlaka kamili na zenye kuirejeshea Zanzibar ya kuingia mikataba na nchi za nje na baadae kuwe na mkataba.
Kwa kusikiliza mahojiano ya Mhe: Mansoor Bonyeza hapa.
Tuachiwe...tupumuwe
Hivi ninani akisema anaweza kusikilizwa kama si wananchi? Nape na kundi lake kutisha watu wenye mawazo tofauti na chama chao itakimaliza ccm kwa kasi ya ajabu, huu si wakati wa kutisha watu, Nampongeza waziri alie heshimu hisia zake mwenyewe,
Ashakum si matusi; Wanaopenda sana kuvunja muungano ni wenye asili ya uarabu na uarabu koko, hiyo wanafanya kwa maslahi mapana zaidi. Zaidi wengi wao wanatumika na zaidi wanawatumia nywele ngumu kuwa makuwadi wao hasa kwa kuangalia kipengele cha dini. Walio, na waliokuwa kwenye madaraka pia wana nia ya kuuvunja muungano.
Kwa kifupi, maslahi makubwa hasa kwa nchi za kiarabu ni ya kisiasa, magharibi kama ipo ni kiuchumi, na kwa wazanzibari wengi wanaotaka kuvunja hawajui lakini kwa tabaka la hapo juu ni uchumi uchwara, kiaiasa na kidini.
Historia ni mwalimu mzuri; ingefaa sana wazanzibari wakafundishwa historia yao ya ukweli na siyo ya kupotosha au kuipaka sukari. Tangu kabla ya mwarabu, baada ya mwarabu, kufika kwa wazungu na uhuru, mapinduzi na muungano.
Muungano ukivunjika kama alivyosema mzee kifimbo, wengi wa wazanzibari nyewele ngumu watakuwa watumwa, na watawatumikia waarabu na waarabu koko.
Mungu isaidie Zanzibar
Mimi huwa nadhania ndiyo sina maslahi na Muungano, kumbe ni wengi wanamtazao kama wangu, to me hata Muungano ukifa kesho sina cha kupoteza wala cha kuongeza. Nijuavyo mimi hata wanaotaka muungano usife hawataki tuu kwamba Historia iandikwe kwamba muungano ulikufa wakiwa wao madarakani lakini in reality hakuna Mtu mwenye shida na Muungano.
Mnang'oa meno ya Tembo ili mukayauze, mnang'oa meno na Kucha za Watanzania wasio na hatia ili iweje?
Well Said Nnauye Jr lakini katiba ya Jamhuri Muungano wa Tanzania haimzuii raia yeyote kutoa maoni ama fikra zake ikiwa TU hayo maoni yake ama hizo fikra zake hazivunji sheria za nchi ama haki za mtu mwingine. Kwa nini viongozi wengi wanaogopa kuujadili muungano hata kwa constructive way?
Deo Mimi ni mfuasi mzuri wa Muungano, ila hayo mawazo yako yamekaa kibaguzi sana, ungetumia njia nyingine kuwasilisha mawazo yako natumai hadhira ingekuelewa vizuri. Ni dhambi kubwa kujaribu kuulazimisha ulimwengu kuwa wanaopinga muungano ni waarabu.
Nashukuru, Kijana Msomali, kwa kweli siyo niayangu kuweka mawazo yangu katika taswira ya kibaguzi, lakini nimeandika hivyo kwa kutazama namna mambo yanavyokwenda.
Pia ninajua historia kamili ya Zanzibar, hivyo natambua nani youpo kazini na tangu lini. Ina uma sana pale ambapo watu wengi wanaingizwa kwenye mkumbo kwa kutokufahamu kwao na kwa makusudi, na hasa viongozi wao wanapo fanya shughuli zao kwa maslahi binafsi.
Kumbuka historia ya Zanzibar imepotoshwa kwa makusudi.
Utawala wa Mkapa ulimaliza masomo yanayoweza vijana kujua historia yao, na kuwajengea uzalendo na hii ilifanywa kwa makusudi, na lengo nikutufanya watumwa kwenye nchi yetu. Na ndivyo ilivyo sasa hapa Tanzania.
Kwa kila Mzalendo lazima atapenda sana Muungano.
Labda asielewe manufaa yake
ni vema tu bwana Mzenji73, ninacho shindwa kuelewa ni kuwa wazenj wengi ukiwemo wewe mna amini kuwa wa bara tunafaidi sana huu muungano na tunaishi kwa jasho la watu wachache wa zenj (about 3million with over 35million!). cha kujiuliza ni je zanzibar kuna nini? Mzee Nyerere mnatakiwa nyie wazenj mheshimu sana kwa mengi aliyowafanyia kwa huo muda aliokuwa madarakani maana nina amini bila yeye kufanikisha muungano mnaouponda sasa hivi mngelikuwa mmechinjana vyakutosha na bara tungelikua na wakimbizi chungu mbovu kutoka visiwa hivyo! anyway ni muda muafaka kwenu sasa kuchagua kwenda Oman au kuendelea na udugu uliojengeka (japo nyie mwajiita wakaazi na kubagua wabara huko visiwani),
bado kuna watu wana mawazo ya kale..wanafikiri huu muungano hauwezi kujadiliwa...wanafanya kama ni biblia ama quraan...
Ccm kuweka sera ya muungano isiyo taka mabadiliko ndio imezaa uamsho, na ndio iliyo zaa g55 ya kina kiseka na marmo.
Mansour ana yo haki ya kujadili na kukosoa ikiwa sera ya chama chake haindani na wakati wa sasa na matazamio ya wengi..
Wahafidhina wasio taka mabadiliko ndani ya ccm ..na watu kama kina nape ni watu ambao ukiwatoa katika siasa basi hawawezi kufanya kazi aina nyengine..watu kama hawa ni wachumia tumbo kwa kutumia siasa
siasa sio dini..na muungano sio dini unaweza kujadiliwa...na kinyume chake utavunjika tu....hata kama dola itatumika.lakini watu wataukataa mpaka kitaeleweka
kwa watu makini kuna haja ya kuujadili muungano ili uwe wa usawa na wenye misingi imara..
Sera ya ccm ya serikali 2 ni kioja kwa wenye kufikiri
ila ni nzuri kwa wenye maslahi binafsi
mungu isaidie zanzibar ili watu kama hawa wanao fananisha kila kitu cha zanziabar ni warabu( japo ndani ya nyoyo zao wanamaanisha waislam)wasipate lengo la kuwagawa wazanzibari..
Sasa tatizo la muungano sio la kundi moja tu hata ccm nao wamechoka...
Wanaotaka mabadiliko ni wazenji wote...na wale ambao hawataki ni wale ambao wanafaidi kwa posho za muungano..hawa ndio wanao penda hali ya sasa isibadilike.
Hakuna mwarabu wala mzungu kuna wazanzibari tu
tukubali sasa upepo umebadilika...sababu zilizokuwapo nyuma ya pazia la muungano halipo tena
ni nyerere kutumiwa na mabeberu kuzuia zanzibar kuwa 'cuba' hii ndio sababu ya muungano huu.
Nyerere hakua na haja ya kuungana kwani alishawahi kutamka kwamba angekua na uwezo basi angevisokomeza visiwa hivi baharini
kauli hizo zipo..na vijana wanazijua ...sio warabu ama nani siasa hizo zimeshashindwa
Tatizo linabaki pale pale. Wzba ukisoma hoja zao hawana kitu unachoweza kusema wanakijua na wanakisimamia.
Kuna mtu kaandika hapo juu mwisho wa serikali 2 Chumbe. Hajasema serikali 3 au mkataba mwisho Chumbe. Sasa hapa najiuliza hivi wenzetu wanataka muungano uvunjike au wanadai kitu kingine?
Lakini pia soma hoja za WZNZ hawana mbadala au hatima kuhusu suala hili. Wao wamebaki kulalamika ili hali wanakila uwezo wa kumaliza kadhia ya muungano. Ni wao kuamua tu hata leo, wanakila silaha ya kisheria. Hawataki!
Wanasema mwisho chumbe! hawasemi pesa za bure asilimia 7 mwisho chumbe, hawasemi ajira na fursa za biashara mwisho chumbe, hawasemi nyaya za umeme mwisho chumbe, hawasemi elimu ya bure mwisho chumbe.
Lakini basi hata kama mwisho ni chumbe wanauwezo wa kuzuia hilo? Maana jeshi linalomlinda rais wa Zbar limevuka Chumbe, mishahara ya BLW imevuka Chumbe!!!!
Tunasubiri kidogo tu, makontena ya ZNZ kuja bara mwisho Chumbe, Ajira za ZNZ bara mwisho Chumbe nk. Ni suala la muda tu mtaonja machungu ya Tanganyika! Mtazamia Tanganyika kama mnavyozamia Ulaya.
Mtabaki kusafisha baraza za Waarabu na wajomba zao! Angalia orodha ya akina Kussa nk. na jiulize wewe nywele za kipili pili una ZNZ?
Anyway mimi bado namuomba Nape anijibu maswali niliyomuuliza.
LET ZNZ GO!
Je ni nini nafasi ya Shirazi kama taifa, Oman, wale waOman waliotangaza uhuru na wakati wa mapinduzi (matukufu) walikimbia na mpaka leo wanajitambua kama waZanzibari? Nini nafasi ya Iran? Libya ilikuwa na interest ambayo Gadafi amekufa nayo. Bado mataifa mengi ya kiarabu yana interest na roots zao hapo, hawa vipi?
Usisahau mabepari uchwara wanaotaka kulichuuza nchi yenu ambao wao ni wazanzibari?
Ni matajiri wangapi duniani wanaona fursa ya kujiendeleza hapo Zanzibar tena kwa kusaidiwa na mataifa yao?
Hawa wote wana mawakala wao hapo.
Ni muhimu sana kujua historia kama nilivyosema hapo juu na Nyerere anajua historia hiyo. Ndio maana walioendesha mauaji ya halaiki siku ya mapinduzi (yanayosemekana ni matukufu) walilenga kundi fulani la watu kwa sababu fulani. Kwa nini mpaka leo hamtukuzi uhuru uliotangazwa na Sultani mwaka 1963?
Follow Us Here