Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

    Report Post
    Page 5 of 6 FirstFirst ... 3456 LastLast
    Results 81 to 100 of 111
    1. #1
      NasDaz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2009
      Location : Ushenzini
      Posts : 3,085
      Rep Power : 5351
      Likes Received
      1444
      Likes Given
      1668

      Default Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Wakati Wizara ya Nishati na Madini ikitarajiwa kuwasilisha bajeti yake kwa mwaka wa Fedha 2012/2013, mvutano miongoni mwa wabunge umezidi kutanuka kiasi cha kuhatarisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.

      Lakini wakati hali hiyo ya mvutano ikibainika miongoni mwa wabunge, kile kinachoelezwa kuwa ni mvutano kati ya viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa upande mmoja na viongozi wa TANESCO waliosimamishwa umechukuwa sura mpya, ikielezwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (aliyesimamishwa), William Mhando, ana maslahi katika zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi ya kampuni ya mkewe, Eva Mhando inayoitwa Santa Clara Supplies Co. Ltd.

      Kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Limited inadaiwa kupewa mkataba wa Sh.884,550,000 na TANESCO kwa ajili ya kusambaza vifaa hivyo.

      Lakini akizungumza ofisini kwa Raia Mweam jana Jumanne, Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe, Eva ambaye awali alikuwa akifanya kazi TANESCO ndiye ameajiriwa na kampuni hiyo.

      KAMPUNI KUPEWA ZABUNI:

      Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Mhando, akiwa Mkurugenzi wa TANESCO, bila kujali mgingano wa kimaslahi aliacha mchakato wa kuipa zabuni kampuni hiyo uendelee na hatimaye kampuni hiyo ikashinda zabuni hiyo ya kusambaza vifaa vya ofisi kwa TANESCO.

      Mhando anadaiwa kuipa kampuni hiyo iliyosajiliwa April 04, 2011, taarifa zaidi zikieleza kuwa, kampuni hiyo ilianza na mataji wa Sh. Miliomi kumi na wanahisa wake ni Fred Willliam, Veronica William na Steven William na kwa mujibu wa usajili wa kampuni hiyo, wanahisa hao pia ni makaimu wakurugenzi.

      Maelezo ya usajili wa kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Co. Ltd, ambayo Raia Mwema imefanikiwa kuyaona, yanaonyesha kuwa ipo katika kitalu namba 204, Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.

      Kwenye orodha ya wanahisa na makaimu wakurugenzi wa kampuni hiyo majina ya Fred na Veronica, yamebainika kuwa ni watoto wa Mhando.

      MAJIBU YA MHANDO.

      Katika kufafanua kuhusu suala hilo, Mhando alisema wakati akiwa TANESCO katika ngazi za chini alikuwa akifanya kazi katika shirika hiloo na mkewe, Eva.

      Hata hivyo kwa mujibu wa maelezo yake, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo pekee la kusambaza umeme nchini, Wizara ya Nishati na Madini, ilimwandikia barua ya kutaka mkewe aachishwe kazi ili kuepusha uwezekano wa kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi.

      “Mke wangu aliacha kazi, lakini tulikuwa na kampuni hiyo ya stationery Kariakoo na kwa sababu biashara haikuwa nzuri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, tuliuza kampuni hiyo mwaka jana.

      Mke wangu aliajiriwa tu katika kampuni hiyo baada ya kununuliwa ili waweze kutumia uzoefu wake katika kuiendesha.

      “Sasa kwa nafasi ya mke wangu, yeye ni Mtendaji wa hiyo kampuni lakini shughuli zote za kutafuta shughuli zote za kutafuta zabuni zinafanywa na wakurugenzi wa kampuni hiyo, si mke wangu.

      “Kwahiyo, walipoomba kazi TANESCO hatua zote zilifanyika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sharia na kampuni hiyo ilishandanishwa na kampuni nyingine na hatimaye ikashinda,” alisema Mhando.

      NB: KWA MAELEZO ZAIDI, UKITAKA KUFAHAMU SINTOFAHAMU YA BUNGE NA SAKATA LA MHANDO, SOMA SOURCE YA HABARI HII-GAZETI LA RAIA MWEMA, July 25,2012.

      MY TAKE:
      Wale wanaomtetea Fisadi Chipukizi William Mhando, jaribuni kutetea na uozo huu....!!
      The Boss, introvert, Uswe and 5 others like this.
      I am a free thinker! It's only my free thinking that leads me, to what am commenting. Thus, I've no doubt that today I can be your fellow but tomorrow your enemy, and the agent between us being my comments!! So, If today we agree with cheers, tomorrow we'd not disagree with jeers!

    2. Miaka 50

    3. #81
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,672
      Rep Power : 977
      Likes Received
      584
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By Mkandara
      kuibeba Puma energy ni kwa maslahi ya Taifa? Mimi naweza jenga hoja ya maana kwa nini tunaihitaji IPTL
      au Dowans kwa manufaa ya Taifa..Nothing new mkuu wangu toka Maswi, mhando, waliopita hadi Ngereja na wengineo kote kumeoza .. wazungu wanasema kata mti panda mti...
      msuguano unaoendelea ni ulaji tu! jambo baya zaidi sidhani kama waziri yuko ktk control ya wizara yake!
      Mkandara likes this.

    4. #82
      OLESAIDIMU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2011
      Posts : 1,242
      Rep Power : 733
      Likes Received
      494
      Likes Given
      470

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Quote By Mkandara
      Lakini lazima uelewe kinahcofanyika mkuu wangu. Unamwondoa Mhando ili nimweke Mkandara ambaye nataka kumpa deal ndugu yangu ambaye anakubaliana/kutokubaliana na bajeti ya wizara ya nishati na madini ambayo kuna washikaji/ maadui fulani na fulani in the process of Ufisadism...

      Kwa hiyo wewe macho yako kwa Mhando na Tanesco, wenzako wanatazama vilivyomo ndani ya bajeti kuna ulaji gani, vizuizi gani, kina nani watakuwa wadeni wa Tanesco ktk tender, uzalishaji wa kampuni hii yenye matumizi kuliko mapato..Think large bro.. usipigwe changa la macho!
      Come what may si kuna taasisi maalum za kufanya vetting ya wateuliwa??????? Kama watapitisha mtu asiye muadilifu na akaangukia mikononi ma wananchi wenye hasira the results can easily be predicted....................a u??????

      We are now taking larger steps leaving aside the thinkimg large ability...............atleast by saying this is not rite, if one bullies arround ok but we consciously know and say that.....this is not wat we need for the time being
      Hegemony is unlikely ever to be complete (A. Gramsci)

    5. #83
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,246
      Rep Power : 3564
      Likes Received
      3070
      Likes Given
      463

      Default Bosi wa TANESCO amtetea mkewe; Mkewe adaiwa kupewa zabuni ya Sh. milioni 800

      Mwandishi Wetu

      Toleo la 251
      25 Jul 2012

      • Mkewe adaiwa kupewa zabuni ya Sh. milioni 800
      • Wabunge bado waendelea kuvutana

      WAKATI Wizara ya Nishati na Madini ikitarajiwa kuwasilisha bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013, mvutano miongoni mwa wabunge umezidi kutanuka kiasi cha kuhatarisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.

      Lakini wakati hali hiyo ya mvutano ikibainika miongoni mwa wabunge, kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni mvutano kati ya viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa upande mmoja na viongozi wa TANESCO waliosimamishwa umechukua sura mpya, ikielezwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (aliyesimamishwa), William Mhando, ana maslahi katika zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi ya kampuni ya mkewe, Eva Mhando, inayoitwa Santa Clara Supplies Co. Ltd.

      Kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Ltd inadaiwa kupewa mkataba wa Sh. 884,550,000 na TANESCO kwa ajili ya kusambaza vifaa hivyo.

      Lakini akizungumza ofisini kwa Raia Mwema jana Jumanne, Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo akidai ya kuwa kwa sasa, kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe, Eva ambaye awali alikuwa akifanya kazi TANESCO ndiye ameajiriwa na kampuni hiyo.

      Kampuni kupewa zabuni

      Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Mhando, akiwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, bila kujali mgongano wa kimaslahi aliacha mchakato wa kuipa zabuni kampuni hiyo uendelee na hatimaye kampuni ikashinda zabuni hiyo ya kusambaza vifaa vya ofisi kwa TANESCO.

      Mhando anadaiwa kuipa mkataba kampuni hiyo iliyosajiliwa Aprili 04, mwaka jana (2011), taarifa zaidi zikieleza kuwa, kampuni hiyo ilianza na mtaji wa hisa wa Sh. milioni kumi na wanahisa wake ni Fred William, Veronica William na Steven William na kwa mujibu wa usajili wa kampuni hiyo, wanahisa hao pia ni makaimu wakurugenzi.

      Maelezo ya usajili wa kampuni hiyo ya Santa Clara Supplies Co. Ltd, ambayo Raia Mwema imefanikiwa kuyaona, yanaonyesha kuwa ipo katika kitalu namba 204, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

      Kwenye orodha ya wanahisa na makaimu wakurugenzi wa kampuni hiyo majina ya Fred na Veronica, yamebainika kuwa ni watoto wa Mhando.

      Majibu ya Mhando

      Katika kufafanua kuhusu suala hilo, Mhando alisema wakati akiwa TANESCO katika ngazi za chini alikuwa akifanya kazi katika shirika hilo na mkewe, Eva.

      Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo yake, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo pekee la kusambaza umeme nchini, Wizara ya Nishati na Madini, ilimwandikia barua ya kutaka mkewe aachishwe kazi ili kuepusha uwezekano wa kuwapo kwa mgongano wa kimaslahi.

      “Mke wangu aliacha kazi, lakini tulikuwa na kampuni hiyo ya stationary Kariakoo na kwa sababu biashara haikuwa nzuri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, tuliuza kampuni hiyo mwaka jana. Mke wangu aliajiriwa tu katika kampuni hiyo baada ya kununuliwa ili waweze kutumia uzoefu wake katika kuiendesha.

      “Sasa kwa nafasi ya mke wangu, yeye ni mtendaji wa hiyo kampuni lakini shughuli zote za kutafuta zabuni zinafanywa na wakurugenzi wa kampuni hiyo, si mke wangu. Kwa hiyo, walipoomba kazi TANESCO hatua zote zilifanyika kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria na kampuni hiyo ilishindanishwa na kampuni nyingine na hatimaye kushinda,” alisema Mhando.

      Akizungumzia mkataba wa zaidi ya Sh milioni 884 kwa kampuni hiyo, Mhando alisema kiwango hicho cha fedha si lazima kitumike chote katika mahitaji ya kampuni na kwamba kutumika kwake kunategemea cash flow (mzunguko wa fedha).

      “Hiyo kampuni hadi sasa ni kama imepewa kazi ya milioni zisizozidi 15. Kwa hiyo si lazima fedha zote kwenye mkataba huo zitumike,” alisema Mhando.

      Mivutano kabla bajeti

      Tayari kuna mgawanyiko wa wazi miongoni mwa wabunge. Wabunge wengine wakiamini uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini unatimiza wajibu wake wa “kuinyoosha” wizara hiyo pamoja na mashirika yaliyoko chini yake likiwamo TANESCO.

      Lakini wakati baadhi ya wabunge wakiamini hivyo, wabunge wenzao wengine wameapa kushiriki mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati kwa kuwaandama viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, kuanzia Waziri, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi.

      Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekwishakuwa na mpasuko mkubwa, ambao msingi wake ni hatua ya kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, iliyochukuliwa na Bodi ya Shirika hilo.

      Hoja ya wabunge walioapa kuushambulia uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini ni pamoja na madai kuwa, Katibu Mkuu, Maswi aliipa zabuni ya kuuza mafuta mazito kampuni ya Puma Energy, ambayo inadaiwa kushindwa katika ushindani wa zabuni.

      Hata hivyo, wengine ambao wanaunga mkono uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wanahoji ujasiri wa wabunge hao kutetea kwamba mafuta mazito yanunuliwe na TANESCO kwa bei kubwa kutoka kwa kampuni zilizoshinda zabuni, badala ya kununua mafuta hayo kwa kampuni ya Puma ambayo ilikuwa ikiuza kwa bei nafuu zaidi.

      Wabunge ambao tayari wameweka misimamo yao wazi kumtetea Mhando ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka. Zitto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, wakati Sendeka ni mjumbe katika Kamati ya Nishati na Madini.

      Kutoka Wizara ya Nishati

      Lakini wakati hali ikiwa hivyo miongoni mwa wabunge, Maswi Jumatatu wiki hii alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akisema baadhi ya wamiliki wa/na kampuni ambazo zimekuwa zikiiuzia mafuta mazito TANESCO zimekuwa zikijihusisha na vitendo vya udanganyifu, ikiwa ni pamoja na kuuza mafuta hayo kwa bei ya juu zaidi.

      Kwa mujibu wa Maswi, baadhi ya kampuni hizo zimekuwa zikinunua mafuta kwa bei ya chini kutoka Kampuni ya Puma Energy na baadaye kuiuzia IPTL kwa bei ya juu.

      Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, Mwaswi alisema: “Kwa hiyo, haya mambo Watanzania wanapaswa kuyafahamu. Na ninyi waandishi msaidie kuandika mambo yenye maslahi kwa taifa. Mimi nitasimamia maslahi ya taifa, hatuwezi kuacha kununua mafuta kwa bei rahisi halafu tununue kwa bei ya juu. Shilingi moja tu kwa mfano, katika maisha ya Mtanzania ni kubwa. Si mnaona mkipandishiwa bei ya dizeli na petroli mnavyolalamika?”

    6. #84
      Lambardi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2008
      Location : KITAANI ZAIDI
      Posts : 4,525
      Rep Power : 1798
      Likes Received
      655
      Likes Given
      0

      Default Re: Bosi wa TANESCO amtetea mkewe; Mkewe adaiwa kupewa zabuni ya Sh. milioni 800

      Maswi ule uzalendo ule bado upooo??au umeenda na maji ya bahari??

    7. #85
      Marcus Aurelius's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st July 2012
      Posts : 49
      Rep Power : 353
      Likes Received
      18
      Likes Given
      47

      Default Re: Bosi wa TANESCO amtetea mkewe; Mkewe adaiwa kupewa zabuni ya Sh. milioni 800

      The saga goes on..

    8. RukaaJuu Final

    9. #86
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,837
      Rep Power : 2970
      Likes Received
      2450
      Likes Given
      3518

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      NasDaz
      ..what u didnt say ni kwamba, Puma walishindwa ktk tender kwasababu bei yao ilikuwa ya juu sana.

      ..sasa baadaye ndiyo wakaenda kuichongea kampuni iliyoshinda kwamba inanunua mafuta hayo toka kwa Puma na zaidi waka-negotiate ku-supply kwa bei ndogo zaidi.

      ..pia Katibu Mkuu hakufuata utaratibu ktk kusitisha tender ya kwanza na kuamua kuwapa tender Puma.

      ..mimi nadhani hawa waachwe walipuane kwanza halafu baadaye wote watimuliwe. nimeshangazwa sana na jinsi wanavyofanya kazi, mahusiano yao kazini, pamoja na matamshi yao ktk vyombo vya habari.

    10. #87
      Mbugi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Location : BOX 2063 MBEYA
      Posts : 818
      Rep Power : 587
      Likes Received
      83
      Likes Given
      13

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Quote By NasDaz
      Usemayo ni sahihi....hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba mara nyingi huwa stori za magazeti yetu huwa si za kuaminika; lakini ni ngumu sana kwa gazeti kama Raia Mwema lidai kwamba limeongea na Mhando wakati hawajaongea!! Si Raia Mwema.....hapa sina shaka yoyote kwamba ni kweli Raia Mwema limeongea na Mhando otherwise; tuhuma zilizotolewa na gazeti hilo ni nzito hivyo Mhando hana budi kukanusha suala la yeye kuongea na Raia Mwema!!...
      Hoja hapo naina inasound ni muhimu ajibu/akanushe/ lakini pia hii inaonyesha the way nchi yetu ilivyo very weak internal control hasa kwa vyombo vyetu vya usalama wa taifa, nalisemea hili kwa misingi kwamba transaction inayohusika hapo ni kubwa, na sioni ni kwanini iliweza mature.
      NasDaz likes this.

    11. #88
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,488
      Rep Power : 6171
      Likes Received
      3059
      Likes Given
      1020

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Duh Mhando amekamatwa chini ya mkanda, hatoki hapo. Utetezi mwingine bwana ati waliuza kampuni mke akawa mwajiriwa tu! Utadhani anaongea na watoto wa shule ya VIDUDU!
      NasDaz likes this.

    12. #89
      Osaka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Location : Morogoro
      Posts : 1,099
      Rep Power : 620
      Likes Received
      269
      Likes Given
      162

      Default

      Quote By Mkandara
      Sijui kama unazungumzia kipande hiki hapa au..

      Au kuna kipande kingine maana hapa naona kiapo tu cha hiyo evaluation committte na sii nani haruhusiwi kupewa kisheria..Hapa sioni kitu mkuu wangu tuna viapo toka kwa rais, bungeni, majaji sisi wenyewe tukisimamishwa kizimbani hii yote haina maana ikiwa kuna ruksa ktk kufanya jambo fulani maadam usikamatwe. Kuapa hakuna maana yoyote zaidi ya kumtakaza alokuwa ktk committee hii kuwa Yeye hana conflict of interest ndani ya kile kinachohitajika (procurement requirement). Wamesema specific member wa avaluation kutokuwa na conlfict of interest wapi...Nje ya hapo kama sina tugaje shi lolo ni mwendo mdundo..

      Kifupi mkuu wangu mimi simtetei Mhando kwa lolote ila naitetea Tanesco siku zote. Sina haja ya kujua kafanya nini sijui tenda ya mkewe wakati tunaliwa mabillioni na hawa viongozi wetu kwa kupitia wizara zao. Nachosema mimi madudu ya Tanzania ni mengi sana, imefikia huwezi kumchambua kuku ukamla..Viongozi wetu wanasiasa ndio chanzo cha migogoro yote ya Tanesco na hatutaweza kumpima kiongozi yeyote kwa makosa yalotokana na Siasa. Hata mimi ukiniweka Tanesco nitatafuta kujijenga tu maana najua huwezi kuliokoa shirika hilo..

      Halafu hii ni committe nzima haina mtu mmoja hivyo maadam tender sii yake yeye mtu mtu anaweza kukwepa kama Mkapa alivyokwepa uwajibikaji kwa sababu iliyosajiliwa ni Kampuni sio jina lake..Kampuni becomes a legal entity na pia yeye hakuwa ktk evaluation committe...Huu ujanja ujana wa Azimio la Zanzibar ndio nisoupenda. tupige marufuku kisheria kwa kuweka miiko na maadili wazi kwa kila mtu kufuata na sio kuweka vikao vya tume na kuwapa viapo wakati wanazidi kutumaliza... SHERIA ichukue mkondo wake.
      I like this!

    13. #90
      Mokerema's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th November 2011
      Posts : 236
      Rep Power : 427
      Likes Received
      117
      Likes Given
      84

      Default

      Quote By Osaka
      I like this!
      Osaka!
      Wewe na Mkandara acheni kudandia mambo msiyoyafahamu. CEO au MD wa Tanesco ndiye anayeteua Chairman wa Tender Board na Mkuu wa Kitengo cha Procurement. Pia huteua wajumbe wote wa Tender Board. Hata hivyo akiwa ndiye accounting officer anateua wajumbe au members of evaluation Committee. Kwa hiyo kuna uwezekano akiwa Corrupt anakuwa na nguvu kubwa za kuamua hatima ya machakato wa Tender yoyote! Hata hivyo anakuwa ni signatory wa Mikataba yote. He has nowhere to hide kama hakuwawajibisha waliomwingiza choo cha kike.

      Taking that on board anawajibika na what ever miscarriage that happens. Kwa kuipatia zabuni kampuni ambayo Mke wake ni employee without declaring interest it unlawful and he just has to dance to the msic . No wonder they are booking him for abuse of power. The subject under discussion ni irrespective of the outcome of the IDO tender , Katibu Mkuu is inclined to get value for money . Hayo makampuni au Kampuni whether Oryx, au Total or whatever they could have gone back to PPA or PPRA for appeal mbona tunayasemea? The bottom line of Public procurement is getting value for money.

      Huwezi lipa a lot of money just lying under the umbrella of following procedures. Tuache CAG afanyie kazi the ToR let us not jump into concllusion .
      Whatever the outcome has to be respected na anayepaswa kuwajibishwa atafahamika.
      NasDaz likes this.

    14. #91
      Bwana Mapesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th April 2011
      Posts : 466
      Rep Power : 502
      Likes Received
      83
      Likes Given
      212

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Directors....F...William...... ..ve william..........ste William....duh hawa ndo waliouziwa hiyo kampuni...na Mh. anaitwa William Mhando........kweli Maskini halali Mchanaa...
      NasDaz likes this.

    15. #92
      NasDaz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2009
      Location : Ushenzini
      Posts : 3,085
      Rep Power : 5351
      Likes Received
      1444
      Likes Given
      1668

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Quote By Kimbunga
      Duh Mhando amekamatwa chini ya mkanda, hatoki hapo. Utetezi mwingine bwana ati waliuza kampuni mke akawa mwajiriwa tu! Utadhani anaongea na watoto wa shule ya VIDUDU!
      Mkuu wangu Kimbunga,
      Huyu Injinia mie kanikosha hapa "Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo akidai ya kuwa kwa sasa, kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe!"
      I am a free thinker! It's only my free thinking that leads me, to what am commenting. Thus, I've no doubt that today I can be your fellow but tomorrow your enemy, and the agent between us being my comments!! So, If today we agree with cheers, tomorrow we'd not disagree with jeers!

    16. #93
      NasDaz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2009
      Location : Ushenzini
      Posts : 3,085
      Rep Power : 5351
      Likes Received
      1444
      Likes Given
      1668

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Quote By Mokerema
      Osaka!
      Wewe na Mkandara acheni kudandia mambo msiyoyafahamu. CEO au MD wa Tanesco ndiye anayeteua Chairman wa Tender Board na Mkuu wa Kitengo cha Procurement. Pia huteua wajumbe wote wa Tender Board. Hata hivyo akiwa ndiye accounting officer anateua wajumbe au members of evaluation Committee. Kwa hiyo kuna uwezekano akiwa Corrupt anakuwa na nguvu kubwa za kuamua hatima ya machakato wa Tender yoyote! Hata hivyo anakuwa ni signatory wa Mikataba yote. He has nowhere to hide kama hakuwawajibisha waliomwingiza choo cha kike.

      Taking that on board anawajibika na what ever miscarriage that happens. Kwa kuipatia zabuni kampuni ambayo Mke wake ni employee without declaring interest it unlawful and he just has to dance to the msic . No wonder they are booking him for abuse of power. The subject under discussion ni irrespective of the outcome of the IDO tender , Katibu Mkuu is inclined to get value for money . Hayo makampuni au Kampuni whether Oryx, au Total or whatever they could have gone back to PPA or PPRA for appeal mbona tunayasemea? The bottom line of Public procurement is getting value for money.

      Huwezi lipa a lot of money just lying under the umbrella of following procedures. Tuache CAG afanyie kazi the ToR let us not jump into concllusion .
      Whatever the outcome has to be respected na anayepaswa kuwajibishwa atafahamika.
      Kwavile Mods wanatulazimisha tutoe "Like" moja tu, zingine hizi hapa:
      You like this. You like this. You like this. You like this.
      I am a free thinker! It's only my free thinking that leads me, to what am commenting. Thus, I've no doubt that today I can be your fellow but tomorrow your enemy, and the agent between us being my comments!! So, If today we agree with cheers, tomorrow we'd not disagree with jeers!

    17. #94
      NasDaz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2009
      Location : Ushenzini
      Posts : 3,085
      Rep Power : 5351
      Likes Received
      1444
      Likes Given
      1668

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      JokaKuu It's Ok,

      Nakuomba uvae viatu vya Katibu Mkuu Maswi at least kwa muda!! Unaingia ofisini, unakuta Tanesco wananunua lita moja ya mafuta mazito kwa sh.2000/= toka JokaKuu Petroleum Ltd. Mara, anakujia MD wa NasDaz Petroleum Products anakupa umbeya (ukitaka, unaweza ita hata fitina) kwamba, hao JokaKuu Petroleum Products lazima wawauzie mafuta kwa bei ya juu kwakuwa huwa hawaagizi wenyewe moja kwa moja bali wananunua kwetu kwa sh.1,500/=!! Nawe kama Katibu Mkuu unamuuliza MD wa NasDaz, ni kwanini hamuuzi wenyewe hayo mafuta moja kwa moja kwa TANESCO ili wawe wananunua kwa hiyo bei ya Sh. 1,500/=! MD huyu anakujibu kwamba wanashindwa kuuza kwa TANESCO kwavile wao hawakushinda tenda hiyo!

      Tell me SIR, as a Permanent Secretary of Ministry Of Energy; baada ya kusikia hayo utachukua hatua gani?! Will you go on relying on procedures which suck every coin available in the hands of TANESCO au utakiuka procedures provided u're sure it will help TANESCO to minimize operative cost?!

      Now let's be back to the common sense!! Kwamba, Puma Energy walitoa bei ya juu sana kiasi kwamba wakakosa hiyo tender. Kama kigezo ni bei, ina maana huyo ambae alishinda tenda yeye alitoa bei ya chini kuliko Puma Energy! Na kwenye zabuni yoyote; it's all about business war among competing companies! So, unachotaka kuniambia mkuu wangu JokaKuu ni kwamba, hiyo kampuni baada ya kushinda tenda na Puma kushindwa; bado Puma wakakata shauri la kuwauzia hao rivals wao mafuta kwa bei ya chini iliyowawezesha kuuza kwa TANESCO kama ambavyo mkataba wao ulivyotaka?! Yaani walikata shauri la kuwauzia mafuta rivals wao kwa bei ya chini ili baadae wakapige majungu kwa katibu mkuu!!! Does it bring any sense! Ungeniambia kwamba Puma walipandisha mafuta yao ili rivals wao wasiweze kununua na hivyo kushindwa ku-fullfil terms walizokubaliana na TANESCO, hapo at least ingeingia akilini na kinyume chake inaonesha ni ama kutapatapa kwa kambi ya Mhando au bado hawajawa wajuvi wa kujitetea kama ambavyo Mhando tayari amethibitiha....si unaona hapa mkuu wangu..." Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo akidai ya kuwa kwa sasa, kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe, Eva..." Jibu hilo la Mhando lina maana kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria!! Hapa inaonesha wazi kwamba Mhando amebananishwa kwenye kona! Mtu wa aina hii, huwa hana tena ujasiri; si wa mwili tu, bali hadi akili! Network huwa inakata, tangu kwenye ubongo, hadi joints za mwili! Ni kama mtu aliyefumaniwa na mke wa mtu!! Mzee wa miaka 60 aliyefumaniwa, anaweza kujikuta anatoa shikamoo kwa kijana wa miaka 30, aliyemfumania! Si kwa lengo la kumlainisha, la hasha.....!!!
      JokaKuu likes this.
      I am a free thinker! It's only my free thinking that leads me, to what am commenting. Thus, I've no doubt that today I can be your fellow but tomorrow your enemy, and the agent between us being my comments!! So, If today we agree with cheers, tomorrow we'd not disagree with jeers!

    18. #95
      MchunguZI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th June 2008
      Posts : 1,308
      Rep Power : 819
      Likes Received
      216
      Likes Given
      76

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Quote By Lu-ma-ga
      Sisi tulishajua UDHAIFU wa kamati ya Zitto, kuna vitu wanajaribu kutetea lakini they are real unprofessional, haiwezekani leo mtumishi kasimamishwa halafu POAC wakuja na hoja nyepesi eti hawajaridhishwa na mchakato wa kumsimamisha mhando, this is outright ridiculous.Mh zitto naamini ata turn around to the original status he used to be ,other wise he gonna let down himself
      Tatizo la Zitto ni kulewa sifa. Alishaambiwa enzi zile aliposhabikia magenereta ya TANESCO. Ni wazi amekuwa ni mtu asiyeeleweka ingawa huko aendako sioni mwisho wake. Binafsi nimeuliza mara nyingi hapa JF nielezwe ni lipi Zitto ametufanyia wa-Tz kiasi tumukubuke. Mi namkumbuka kwa sifa ya kufukuzwa Bungeni TU!

      Sasa anaanza kutamani Urais, lakini kule Kigoma wanafahamu yeye si m-TZ wa kigoma. Ni m-TZ wa Kongo. Zitto siyo Muha!
      The educated differ from the uneducated as much as the living from the dead --Aristotle

    19. #96
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,837
      Rep Power : 2970
      Likes Received
      2450
      Likes Given
      3518

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Quote By NasDaz
      JokaKuu It's Ok,

      Nakuomba uvae viatu vya Katibu Mkuu Maswi at least kwa muda!! Unaingia ofisini, unakuta Tanesco wananunua lita moja ya mafuta mazito kwa sh.2000/= toka JokaKuu Petroleum Ltd. Mara, anakujia MD wa NasDaz Petroleum Products anakupa umbeya (ukitaka, unaweza ita hata fitina) kwamba, hao JokaKuu Petroleum Products lazima wawauzie mafuta kwa bei ya juu kwakuwa huwa hawaagizi wenyewe moja kwa moja bali wananunua kwetu kwa sh.1,500/=!! Nawe kama Katibu Mkuu unamuuliza MD wa NasDaz, ni kwanini hamuuzi wenyewe hayo mafuta moja kwa moja kwa TANESCO ili wawe wananunua kwa hiyo bei ya Sh. 1,500/=! MD huyu anakujibu kwamba wanashindwa kuuza kwa TANESCO kwavile wao hawakushinda tenda hiyo!

      Tell me SIR, as a Permanent Secretary of Ministry Of Energy; baada ya kusikia hayo utachukua hatua gani?! Will you go on relying on procedures which suck every coin available in the hands of TANESCO au utakiuka procedures provided u're sure it will help TANESCO to minimize operative cost?!

      Now let's be back to the common sense!! Kwamba, Puma Energy walitoa bei ya juu sana kiasi kwamba wakakosa hiyo tender. Kama kigezo ni bei, ina maana huyo ambae alishinda tenda yeye alitoa bei ya chini kuliko Puma Energy! Na kwenye zabuni yoyote; it's all about business war among competing companies! So, unachotaka kuniambia mkuu wangu JokaKuu ni kwamba, hiyo kampuni baada ya kushinda tenda na Puma kushindwa; bado Puma wakakata shauri la kuwauzia hao rivals wao mafuta kwa bei ya chini iliyowawezesha kuuza kwa TANESCO kama ambavyo mkataba wao ulivyotaka?! Yaani walikata shauri la kuwauzia mafuta rivals wao kwa bei ya chini ili baadae wakapige majungu kwa katibu mkuu!!! Does it bring any sense! Ungeniambia kwamba Puma walipandisha mafuta yao ili rivals wao wasiweze kununua na hivyo kushindwa ku-fullfil terms walizokubaliana na TANESCO, hapo at least ingeingia akilini na kinyume chake inaonesha ni ama kutapatapa kwa kambi ya Mhando au bado hawajawa wajuvi wa kujitetea kama ambavyo Mhando tayari amethibitiha....si unaona hapa mkuu wangu..." Mhando alikiri kuitambua kampuni hiyo akidai ya kuwa kwa sasa, kampuni hiyo si mali ya familia yake bali mkewe, Eva..." Jibu hilo la Mhando lina maana kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria!! Hapa inaonesha wazi kwamba Mhando amebananishwa kwenye kona! Mtu wa aina hii, huwa hana tena ujasiri; si wa mwili tu, bali hadi akili! Network huwa inakata, tangu kwenye ubongo, hadi joints za mwili! Ni kama mtu aliyefumaniwa na mke wa mtu!! Mzee wa miaka 60 aliyefumaniwa, anaweza kujikuta anatoa shikamoo kwa kijana wa miaka 30, aliyemfumania! Si kwa lengo la kumlainisha, la hasha.....!!!
      NasDaz,

      ..I have seen a picture like this before.

      ..I dont trust both of them, Mhando, and Maswi.

      ..kwenye hiyo scenario uliyotuletea umesahau kitu kimoja kwamba Puma walijaribu kuwalangua Tanesco lakini wakashindwa ujanja na walanguzi wenzao.

      ..ningekuwa Maswi ningefanya uchunguzi, na kutafuta kampuni nyingine tofauti na Puma, itakayoweza ku-supply kwa bei sawa, au ndogo zaidi ya inayopendekezwa na Puma. Vilevile, ningehakikisha zoezi hilo linafuata TARATIBU za manunuzi na mikataba.

      ..mwisho, Maswi anajitetea kwamba ameamua kupindisha taratibu ili kuokoa fedha, na wewe unamuunga mkono. Je, Mhando naye akisema amempa mke wake tender, kutokana na uzalendo, na nia njema ya kuokoa fedha za shirika, what r u going to say??

      ..naendelea kusisitiza kwamba TARATIBU na SHERIA zifuatwe wakati wote.

    20. #97
      Hebron Caleb's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 171
      Rep Power : 384
      Likes Received
      43
      Likes Given
      3

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Halafu Viongozi wetu wanaenda USA na FRANCE eti kuangalia mitambo ya kuzalisha umeme na hawakuipata ni kweli pamoja na maendeleo yote ya IT bado kuna watu wanafanya manunuzi kwa njia hiyo?????????????????????????? ??? Yaani ni kama wanaenda kununua viazi ulaya pale Kariakoo shimoni?????????????????Tanzan ia we are finished. Nilisema hata kama hamtaniunga mkono kuna siku nitaandamana peke yangu and will deliver the message. Mungu atusaidie.

    21. #98
      Mokerema's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th November 2011
      Posts : 236
      Rep Power : 427
      Likes Received
      117
      Likes Given
      84

      Default

      Quote By JokaKuu
      NasDaz,

      ..I have seen a picture like this before.

      ..I dont trust both of them, Mhando, and Maswi.

      ..kwenye hiyo scenario uliyotuletea umesahau kitu kimoja kwamba Puma walijaribu kuwalangua Tanesco lakini wakashindwa ujanja na walanguzi wenzao.

      ..ningekuwa Maswi ningefanya uchunguzi, na kutafuta kampuni nyingine tofauti na Puma, itakayoweza ku-supply kwa bei sawa, au ndogo zaidi ya inayopendekezwa na Puma. Vilevile, ningehakikisha zoezi hilo linafuata TARATIBU za manunuzi na mikataba.

      ..mwisho, Maswi anajitetea kwamba ameamua kupindisha taratibu ili kuokoa fedha, na wewe unamuunga mkono. Je, Mhando naye akisema amempa mke wake tender, kutokana na uzalendo, na nia njema ya kuokoa fedha za shirika, what r u going to say??

      ..naendelea kusisitiza kwamba TARATIBU na SHERIA zifuatwe wakati wote.
      JokaKuu,

      Acha kungangania ya kale hapa Jamvini kumewekwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani ina details za kutosha kuhusu swali la mafuta.

      Acha uvivu hivi unajua sheria za manunuzi? Huyo unayemtetea aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco William Mhando ni kihiyo mwenye elimu ya kuungaunga aliyoipata Huko Cuba katika Hali ya kutatanisha. Alifuta Zabuni nyingi kwa visingizio vya hovyo na kuwapatia mafisadi wake wakiongozwa na Rostam Aziz, Yusuf Manji na hayo makampuni ya kichina kununua Vifaa vyenye Kiwango cha chini na kujipatia mabilioni ya fedha na management yake Makao Makuu na Mikoani. Hata nguzo za miradi ya REA zinakaguliwa na Wapambe wa Mhando ni fake na umri wake hazitakaa zaidi ya miaka mitano. JokaKuu soma ,
      JokaKuu and NasDaz like this.

    22. #99
      OPTIMUS TZ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th January 2012
      Posts : 390
      Rep Power : 447
      Likes Received
      60
      Likes Given
      1

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Mimi nafikiri huyu mtu akapimwe akili huo Uhandisi ali upata vipi? hata akili ya kufanya ufisadi hana sasa yeye ni msemaji wa mke wake au hicho kikampuni au ni msemaji wa wote; jamani wizi waachieni wachaga na wahindi.........nyie wabantu mtaishia jela ohoooooo .....ona Liumba,Mahalu,Jairo, sasa huyu msambaa..Muhando.............. ..mue mnaconsult wezi wazoefu ndugu zangu kabla ya kukurupuka kutafuta utajiri wa haraka haraka.........VERY STUPID

    23. #100
      Arvin sloane's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2011
      Posts : 885
      Rep Power : 574
      Likes Received
      130
      Likes Given
      40

      Default Re: Madudu mengine ya William Mhando wa TANESCO!

      Kumbe zitto naye ni wa kutilia mashaka kwa nini? anamtetea fisadi huyu?

    Page 5 of 6 FirstFirst ... 3456 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...