The topic speaks for itself.
The main thread can be found here: http://www.jamiiforums.com/great-thi...05-2012-a.html
Update:
Update Muhimu sana:Tumepigiwa sim na Matola, anaomba mjadala uendelee kesho. Alijitolea kwa kuchangia katika mjadala huu kupitia internet cafe kwa muda wa masaa sita, ila sasa anaona it's getting too late. Kesho asubuhi nitarudi kuwajulisheni muda kamili wa kuendelea mjadala. In the mean time tuendelee kukusanya comment na masuali ya members wote katika thread ya "side comments"
Jamani wana JF kuna mambo ni personal zaidi, lakini hili lililonipata naona ni janga, mama yangu mzazi amefail step na alikuwa amefanyiwa oparesheni ya neuron surgeon sasa ametonenesha ile sehemu aliyofanyiwa oparesheni, nimeshinda MOI leo na sikuweza kufanya chochote, Nampenda Mama yangu siwezi kumteleza.
Natumia fursa hii kuwaomba radhi wana JF kwamba wanisamehe kwa kutokupatikana leo, nadhani kwa waelewa wanajuwa vyema uchungu wa Mama. Roulette mimi ndio nimerudi nyumbani sasa hivi wakati waliofunga wanajiandaa kupata daku. tusameheehane ndugu zangu, nina majonzi.
UPDATES - QUESTIONS FROM MEMBERS;
Kuongeza fedha katika Mfuko wa Uwezeshaji Kiuchumi wa wajasiriamali wadogo (Mfuko wa JK) kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB. ilitoa kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB (Shilingi bilioni 5.25) na CRDB (Shilingi bilioni 5.25). Kiasi hiki kiliwezesha kutolewa kwa mikopo ya Shilingi bilioni 37.17 ikiwa in asilimia 118 ya Shilingi 31.5 zilizotengwa kutolewa na benk hizo mbili.
Qn;
Zomba tueleze nani alipata hizi bilions ulizotaja katika aya yako hii Sio kusifia tuu na kusema kuwa mkopo huu ulisaidia nani alizipata na zimesaidia nini na kwa nini hadi sasa hata marejesho hayaonekani Mikopo hii ililengwa kuwasaidia wale wajasiriamali wadogo klujikwamua na kufanya biashara katika hali nzuri ila zilitolewa na kuishia kwenye mikono ya watu ambao mnawajua ninyi ila mmekaa kimya wala hamtaki kutujuza ni akina nani. Na wala hamjasema lolote kuhusu kurejeshwa kwa mkopo huo ili uwasaidie wengine ambao wanauhitaji.
Qn;
Kuhusu sheria na utawala, kwa mara ya kwanza Tanzania tumeona ingezeko la mahakimu, majaji, na kupunguwa kwa kesi kwa kiasi kikubwa sana mahakamani.
Je ongezeko hilo linareflect hali halisi ya mahamaka zetu na mlundikano wa kesi? je hao mahakimu na majaji walioongezeka kuna vitendea kazi kuwawezesha kuhimili hali ya nchi yetu? Maana kuna wilaya ambhazo hazina mahakama za mwanzo au hata majengo kuendeshea kesi mbalimbali. Au inabidi hakimu aendeshee kesi zake kwenye ghala (refer Magu)?
Je budget ya kuendesha shughuli za mahakama inatolewa kwa wakati kukidhi uhalisia na mahitaji ya hizo mahakama? Au ni kuongeza tuu majaji na mahakimu bila kujali kama kuna majengo au vitendea kazi kuendesha hizo kesi?
swali 1. ni kwa nini utawala wa raisi kikwete umegubikwa na hsutuma za rushwa na ufisadi? na je kwa mtizamo wa zomba ni kweli kikwet kama raisi hana makucha ya kuwadhibiti hawa wala rushwa? kama anayo kwa nini hali iko hivi na kama hana kwa nini asiachie ngazi
swali la 2. raisi kiwkte kwa kiwango kikubwa ameshindwa kuboresha sekta ya afya na kwa kuzingatia mvutano uliopo na na madaktari na hivyo wengi wameamua kuondoa na kwenda nje ya nchi. Nini maoni ya zomba katika hili. ni kweli haiwezekani kuboresha mazingira na malipo ya wafanyakazi wa sekta ya afya?
swali la 3. kwa maoni yako zomba ningependa kujua je demokrasia inakua au inadidimizwa nchini? na vipi kuhusu haki za binadamu je serikali ya kikwete inajali haki za binadamu? jibu swali hili kwa kutumia mifano haiMwali mimi nitaomba uwaulize washiriki kuhusu dhana ya udhaifu wa Kikwete. Je wanakubaliana nayo?
Kama ndiyo ni kwanini kama siyo ni kwanini? Nauliza hivyo kutokana na pamoja kuwa Marais waliopita kuwa na mapungufu mengi lakini haijapata kutokea Taifa kuwa kwenye hali ya mkanganyiko kama sasa, kuanzia sekta ya Afya na mgogoro wa madaktari.
Ukija kwenye Uchumi pia nayo utaona uhujumu uchumi mkubwa unaohusisha viongozi mbalimbali ambapo wanagusa nyanja zote Usafiri, elimu, ujenzi, utalii nakadhalika sasa ukijumuisha yanayotokea kiuhalisia naomba wainyambue hoja ya Udhaifu. AsanteMwali swali langu ni kuwa...Kikwete amefanikiwa vipi kutekeleza kauli mbiu za "ajira milioni moja kwa vijana" "kilimo kwanza" ?Ningetaka kujua toka kwa Zomba yafuatayo:
1. Inflation rate ilikuwa ngapi 2006 na sasa ikoje?
2. Gini Coeefficent ilikuwaje 2006 na sasa mambo yako vipi?
3. Miradi ya barabara iliyokuwa under pipeline 2006
4. Miradi mipya ya barabara iliyoanza (from scrach) tangu 2006
5. GDP growth rate na Inflation kwa hii miaka 1995, 2005 na 212.Asante Mwali pamoja na wageni wetu zomba na Matola,
Mi napata tabu kidogo, ni kweli kwamba wakati wa utawala wa Nyerere ni kweli tulikuwa tuna export sana hasa mazao na tulifikia kuwa tunaongoza kwenye export ya zao la katani Duniani.
Sitaki kwenda mbali sana lakini kwa mtazamo wa sasa inaonekana sio tu kwamba hatuexport tena ila hata chakula tu cha kututosheleza hakipo (Tukumbuke miaka miwili iliyopita) Kwahiyo mkuu zomba je kwa mtazamo wako unataka kunambia leo hali ya kilimo nchini ni mbaya kuliko wakati wa Nyerere?
Mwali sina uhakika kama ulitualika na sisi but kama hukutualika sorrySwali kwa Zomba - Ndugu Kikwete alishawahi kutoa ahadi ya kutengenesha biashara na siasa (wakati wa mdahalo wa urais - 2010) ili kupunguza mgungano wa kimaslahi kwa mtu ambaye ni mfanyabiashara na anataka kuingia kwenye siasa. Aliahidi kuja na sera na sheria ya kutekeleza ahadi hiyo. Swali, unalizungumziaje suala hili? je, huoni hili ni pigo kubwa katika suala zima la uongozi bora na uwajibikaji kwa wanasiasa?!7. Kuimairisha upatikanaji wa haki kwa watu wenye ulemavu na wazee
Maswali kwa Zomba:
- Kukamilika kwa sera ya wazee
Je? Hiyo Sera inatekelezwa? Imewanufaisha wazee wa nchi hii? Toa mifano hai.
- Kukamilisha sera ya watu wenye ulemavu
Je? Hiyo Sera inatekelezwa? Ni kwa nini mauaji ya walemavu wa ngozi yameongezeka kipindi cha Kikwete?
- Kupitishwa kwa sheria ya walemavu 2010
Je? Hiyo sheria inatekelezwa? Ni kwa nini hata shule zenye watoto wenye ulemavu bado hazina mazingira rafiki kwa walemavu?
- Kukarabati nyumba za vyuo vya ufundi kwa watu wenye uelemavu.
Toa mifano hai ukilinganisha na vyuo vya ufundi vilivyopo nchini.
- Kukarabati majengo ya makazi ya wazee
Ni majengo ya wapi hayo yaliyokarabatiwa? Ni mwaka huu tumewaona na kuwasikia wazee wanaoishi katika kambi ya wazee Morogoro wakilalamika kuhusiana na mazingira magumu wanayoishi.
- Kuhamasisha jamii kuhusiana na utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee.
- Kutoa nyenzo (vifaa) za kujimudu kwa watu wenye ulemavu na wazee.
- Kuwajengea uwezo wazee na watu wenye ulemavu kwa kuwapa mitaji midogo midogo.
Naomba utoe mifano hai kwa bullets 3 hapo juu.
Swali kwa Matola unafikri ni changamoto zipi alizokutana nazo JK ambazo zimekwamisha utekelezaji wa ahadi zake.
Swali kwa zomba ukitilia maanani mabadiliko ya katiba yanayokuja ambayo pengine yakaongeza au kuondoa kikomo cha kugombe urais ......unafikiri JK anastahili kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano? na kwa nini?
Mwali swali langu kwa Matola na zomba tena:
Katika miaka ya karibuni hasa katika kipindi cha JK kumekuwa na mijadala mikali sana ya udini (sio dini) miongoni mwa wanasiasa hata viongozi wenyewe wa dini juu ya mgawanyo wa madaraka na utoaji wa nafasi za elimu na ajira kwa vigezo vya dini ya mtu!
Swali: Mnafikiri ni kwa kiasi gani utawala wa JK umelishughulikia kwa namna ya kutoacha mpasuko katika Taifa?
Nini mchango wa Utawala wake katika mgawanyiko huu?
Naunganisha na maswali yangu ya awali:
Swali kwa Matola unafikri ni changamoto zipi alizokutana nazo JK ambazo zimekwamisha utekelezaji wa ahadi zake.
Swali kwa zomba ukitilia maanani mabadiliko ya katiba yanayokuja ambayo pengine yakaongeza au kuondoa kikomo cha kugombe urais ......unafikiri JK anastahili kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano? na kwa nini?
zomba alitakiwa aongee from his perspectives na ku'compare' na 'international standards'..sasa kuorodhesha asilimia tu pamoja na maelezo mengi hakuleti tija ya mjadala!..
Swali langu..na naomba Mwali ulichukue..ni hivi:
Kwa kuwa tumeamua kuwa na Kauli Mbiu ya Kilimo Kwanza..na kwa kuwa karibu watu wetu 80% wanategemea kilimo..na kwa kuwa Ukiinua Kilimo obviously utakuwa umeinua Uchumi wa Mtanzania..Je? Kwa karibu miaka mitano tangu hii Kauli Mbiu ilipoanzishwa nini Mafaniko yake na nini kiwango cha Utekelezaji wake??Kwenye hoja ya ahadi za rais zomba amesema kuwa ahadi za rais zimetekelezwa. Ningetaka kujua ufafanuzi kwa haya yafuato:
1. Ahadi zote 69 ziligharimu kiasi gani?
2. Bajeti ya ahadi hizo ilipitishwa katiba kikao gani cha bunge?
3. Na hela hizo zilikuwa za ndani (domestic revenue) au misaada/loans? Na kama ni misaada/loans toka wapi?Qn;
Naomba Mkuu zomba kuuliza swali dogo sana.Rais Kikwete ameteua majaji wengi kwa nia ya kukabiliana na mlundikano wa kesi.
Bahati mbaya teuzi hizi haziendani na ongezeko la ujenzi wa mahakama,vitendea kazi vya kisasa kama computer amabazo zingesaidia kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi.Majaji wengi hawana ujuzi wa kutosha na hata hukumu zao tayari zimezua maswali mengi miongoni mwa wataalamu wa sheria.
Qn;
Ujenzi wa UDOM umekomba fedha za NSSF na kusabisha shirika hilo matatizo makubwa ya cash flow na hatimaye sisi wanachama wa NSSF tunalazimika kulipwa fedha zetu tutakapofikisha miaka 60 haijalishi umefukuzwa kazi ukiwa na miaka 20 au 30 !.
[1] Inafahamika wazi ajira za sekta binafsi hazina usalama mtu unafanyakazi miaka yako sita au kumi unatambaa au unakimbizwa.
[2] Umri wa kuishi mTanzania ni chini ya miaka 50 ?
[3] Maamuzi ya ujenzi wa Udom na Daraja la kigamboni wanachama wa NSSF na PPF hawakushirikishwa.
zomba huoni Kikwete na serekali yake wanastahili kushtakiwa kwa kutuweka sisi wanacha wa hiyo mifuko ya hifadhi ya jamii katika hali ya ngumu kwa nia ya kujipatia ujiko wa kisiasa ?.Katiba mpya kipengele cha kumshitaki Rais anayechezea uhai wa wananchi wake kiwekwe.Hili swali liende kwa zomba ,tume shuhudia jk akibadilisha baraza la mawaziri pamoja na mawaziri kwa tuhuma za ufisadi lakini hatuoni hatua yeyote inayo chukuliwa kuwa chukulia hatua za kisheria au kuhakikisha pesa zilizo chukuliwa zinarudishwa.
-Je tuendelee kuona mafisadi wanatamba mtaani na kukimbia na pesa za wananchi?
-Kuna ugumu gani kuwa kamata mafisadi hao na kuwachukulia hatua?Swali langu:
Je kwa kuwa Bunge la Tanzania chini ya RAISI KIkwete na SPIKA Makinda na Majority ya wabunge wa CCM wamekuwa wakipitisha miswada yenye kukandamiza wananchi, Wapinzani wanapojaribu kuhoji kuna kuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa SPIKA. Mafano:-
1. Upandishaji wa Bei ya Mafuta taa huku tukijua kuwa Idadi ya Magari tanznaia hayafiki hata 1 Milioni na watanzania zaidi ya 45 Milioni wakitegemea mafuta taa.
2. Hifadhi ya Jamii, kwamba hakuna tena kuchukua mafao yako pindi unapoacha kazi mpaka hapo utakapo fikisha umri wa miaka 55/60 hata kama umefanya kazi kwa muda mwezi mmoja.
Je ni kwa nini RAISI kikwete amekuwa ni mwepesi kusign hii miswada bila kusikiliza maoni ya wananchi?


Reply With Quote
Follow Us Here