Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

    Report Post
    Results 1 to 11 of 11
    1. #1
      Kurunzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2009
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 1,956
      Rep Power : 891
      Likes Received
      386
      Likes Given
      147

      Default Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      Na Privatus Karugendo

      KATIKA vyombo vya habari, jana tumesikia CHADEMA wamegundua mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu na hasa ujumbe mfupi wa maneno. Na kwamba mtambo huu umeingizwa nchini kutoka Israel na mtoto wa kiongozi wa CCM; na kwamba mtambo huu umetumika tayari kuingilia mawasiliano ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA, kwenda kwa baadhi ya viongozi wa CCM kwa lengo la kuwatishia maisha.

      Ujumbe unaonekana umetoka kwenye simu za viongozi wa CHADEMA, lakini ukweli ni kwamba ujumbe unakuwa umetengenezwa na mtambo ulionunuliwa Israel na kuupitisha kwenye mtandao wa simu za viongozi wa CHADEMA. Na kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tayari ametangaza nia ya kuwafikisha viongozi wa CHADEMA mahakamani kwa kutumia ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwenye simuzao uliokuwa unawatishia maisha baadhi ya wanachama wa CCM.

      Sikushangazwa na habari hizi na wala sina mashaka kwamba kitu hiki hakiwezekani. Tumeshuhudia “majambazi” wa mtandao wanavyoingilia mtandao wa barua pepe; mtu anaingilia anwani yako na kuwatumia marafiki zako ujumbe kwamba umetekwa, au umeibiwa ukiwa nje ya nchi na unahitaji msaada wa fedha. Hili limewatokea watu wengi. Pia tunajua jinsi watu hawa wabaya wanavyoweza kutuma virusi kwenye kompyuta na wakati mwingine kutumia teknolojia kuiba habari nyeti kutoka kwenye kompyuta za watu; pia tunasikia kila siku jinsi “majambazi” hawa wa mtandao wanavyoingilia akaunti za watu kwenye benki na kuiba fedha. Hivyo na hili la kuingilia ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu za watu linawezekana kabisa.

      Hoja yangu ni kwamba CHADEMA, wamefanya haraka kutangaza jambo hili. Wangefanya subira na kuhakikisha wanamnasa mtu huyu na mtambo wake. Kutangaza kabla ya kumkatamata ni hatari! Wao wametangaza mtu huyu ana fedha nyingi na kwamba ni mtoto wa mtu mkubwa. Hivyo uwezekano wa kuhakikisha mtambo huu unaangamizwa na kupoteza ushahidi ni mkubwa; au mtambo huu kwa miujiza ukageuzwa kuwa ni mali ya CHADEMA ni kitu cha kawaida kabisa; kama Jambazi anaweza kuingia kanisani na kuungama dhambi ya kumteka mtu na kumtesa; Jambazi huyo akakamatwa bila kuonyeshwa sura yake na kufikishwa mahakamani kimya kimya na kutumia tukio hilo kuzima mjadala mzima wa tukio hilo la kinyama la kuteka mtu na kumtesa
      kwa kisingizio cha kesi kuwa mahakamani, kila kitu kinawezekana! Pia, uwezo wa fedha kuingilia uchunguzi wa suala zima la mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu kwa kuziba midomo na akili za wataalamu wa teknolojia nchini ni mkubwa sana. Kwa vile kumekuwepo na shutuma hizi za kutumia teknolojia vibaya kwa muda mrefu, sasa ulikuwa ni wakati muafaka wa kuwakamata watu hawa na kuwafikisha mbele ya sheria.

      Uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ilisikika pia kwamba mtoto wa kiongozi mkubwa alifanya mpango kwa kuwaleta wataalamu wa data na kuhakikisha kura za urais zinavurugwa. Jambo hili lilisikika sana kwenye vyombo vya habari, kufikia hata kutaja sehemu iliyotumika, kompyuta zilizotumika na programu zilizotumika, lakini hakukuwepo na ufuatiliaji. Hili ndilo kosa kubwa tunalolifanya hapa Tanzani. Mambo yanajitokeza na wakati mwingine ni mambo ya uhakika kabisa, lakini ushahidi mzito unakosekana.Tunabaki kwenye maneno mengi na porojo. Huku wenye nia mbaya na uchu wa madaraka wakiendelea kusonga mbele kwa kasi ya kutisha.

      Tumesikia jinsi watu walivyotumia teknolojia na kujitengenezea Luku na kuziuza kinyume na mfumo wa TANESCO. Watu hawa watakuwa wamejitengenezea fedha nyingi wakati TANESCO inaingia kwenye hasara kubwa hadi kufikia hatua za taifa kuingia gizani. Na fedha hizi wanazozitafuta kwa mbinu chafu, inawezekana ni kwa lengo zima la kutafuta madaraka 2015. Pia kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna wajanja wanaotengeneza kadi za muda wa maongezi wa kampuni mbalimbali za simu, na kuwauzia watu.

      Ninachoaamini ni kwamba wezi wa kutumia teknolojia ni lazima kuwakamata kwa kutumia teknolojia kama ulivyo msemo wa Kiswahili wa dawa ya moto ni moto. Na hapana shaka kwamba mtu akitumia ujumbe mfupi wa maneno kwenda kwa mtu ni lazima mtu huyu atambuliwe.

      Pamoja na mchakato mzima kwa kuzisajili simu zote; ni lazima mitambo ya makampuni ya simu ya kurushia ujumbe huu mfupi itakuwa na uwezo wa kutunza ujumbe huu na kuweza kutambua unatoka kwenye simu ipi, yenye uwezo upi na iliyotengenezwa na kampuni ipi na mwaka upi. Na kama ujumbe umeingiliwa namtambo mwingine ni lazima mitambo ya makampuni ijue. Na ikitokea ni ukweli kwamba mtambo huu wa kuingilia mawasiliano ya simu upo hapa Tanzania na makampuni ya simu hayajui, basi ni lazima tuwe na mashaka na makampuni haya. Vyovyote vile ni lazima makampuni haya yawajibishwe; kama si kwa kushirikiana na “majambazi” wa mtandao basi yawajibishwe kwa uzembe! Haiwezekani mtambo mwingine uingilie mfumo wao wa mawasiliano na wao wasijue. Kama hili la CHADEMA ni la kweli, basi makampuni ya simu yatakuwa yanafanya kazikwa makubaliano na “Majambazi” wa mtandao.

      ADDITION:
      Tatizo letu hapa Tanzania ni kwamba tunaingiza siasa kwenye mambo yote. Biashara na uwekezaji tumeingiza siasa. Baadhi ya wanasiasa wana hisa kwenye makampuni mbalimbali yanayowekeza kwenye taifa letu. Habari za kuaminika ni kwamba hata makampuni haya ya simu kuna wanasiasa ambao wana hisa kule. Kama hili ni kweli, basi uchunguzi wowote juu ya mawasiliano ya simu (na kama uchunguzi huo unawagusa wanasiasa) ni vigumu kufanikiwa.

      Katika hali ya kwaida, si suala gumu kufuatilia na kujua ni nani amempigia simu nani, siku gani na kwa muda upi, au kufuatilia na kugundua ni mtu gani ametuma ujumbe mfupi kwa nani na kwa wakati gani. Pia si suala gumu kufuatilia na kujua kama haya makampuni ya simu yanatuibia kwa kubinya uwiano wa malipo na muda wa maongezi. Kwa maana kwamba mtu anapolipa elfu moja anaongea kwa muda wenye thamani ya elfu moja. Wanaweza kutoa ofa ya kuongea bure kwa kipindi fulani, au kutoa zawadi mbalimbali, lakini huku wakijua jinsi watakavyotukamua kwenye muda wa maongezi. Hivyo CHADEMA, wangeenda pole pole, kwa uhakika na kwa uchunguzi wa kina, wangeweza kugundua mengi juu ya mfumo mzima wa mawasiliano ya simu. Nao wangeenda Israeli, na kutengeneza mtambo wa kukamata mitambo inayoingilia mawasiliano. Tena wangeenda kwenye kampuni hiyohiyo iliyotengeza mtambo huo wa kuingilia
      mawasiliano ya ujumbe mfupi. Huo ndiyo mchezo wa makampuni makubwa katika mchakato mzima wa ubeberu na unyonyaji. Wanatengeneza virusi vya kushambulia mtandao, na wakati huohuo wanatengeneza silaha za kupambana na virusi hivyo. Kwa njia hii wao wanatengeneza faida kubwa kwa maumivu ya watu wengine.

      Taifa letu sasa hivi linapita katika kipindi kigumu sana. Na kufikia uchaguzi mkuu wa 2015, tutashuhudia mengi. Hivyo ni muhimu CHADEMA na watu wengine wenye nia njema na taifa letu kuvuta subira kwa matukio mbalimbali, ili tuweze kuwafichua majambazi na watu wenye nia mbaya na taifa letu. Mfano hili la kuingilia mawasiliano na kuwachonganisha watu kiasi cha kufikishana mahakamani ni kitendo kibaya kiasi kwamba kinaweza kutufikisha katika umwagaji damu.

      Tutapambana na watu hawa wabaya kwa kupiga hatua za uhakika; na hatua muhimu ni kuwakamata watu hawa wakiwa kazini. Kuwakamata kwenye mazingira ambayo hawawezi kwa namna yoyote ile kukwepa na kuweza kutunga hadithi kama ile ya mtuhumiwa kwenda kutubu Kanisani.

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      Kurunzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2009
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 1,956
      Rep Power : 891
      Likes Received
      386
      Likes Given
      147

      Default re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      ADDITION:
      Tatizo letu hapa Tanzania ni kwamba tunaingiza
      siasa kwenye mambo yote. Biashara na
      uwekezaji tumeingiza siasa. Baadhi ya
      wanasiasa wana hisa kwenye makampuni
      mbalimbali yanayowekeza kwenye taifa letu.
      Habari za kuaminika ni kwamba hata
      makampuni haya ya simu kuna wanasiasa
      ambao wana hisa kule. Kama hili ni kweli, basi
      uchunguzi wowote juu ya mawasiliano ya simu
      (na kama uchunguzi huo unawagusa wanasiasa)
      ni vigumu kufanikiwa.
      Katika hali ya kwaida, si suala gumu kufuatilia
      na kujua ni nani amempigia simu nani, siku
      gani na kwa muda upi, au kufuatilia na
      kugundua ni mtu gani ametuma ujumbe mfupi
      kwa nani na kwa wakati gani. Pia si suala gumu
      kufuatilia na kujua kama haya makampuni ya
      simu yanatuibia kwa kubinya uwiano wa malipo
      na muda wa maongezi. Kwa maana kwamba
      mtu anapolipa elfu moja anaongea kwa muda
      wenye thamani ya elfu moja. Wanaweza kutoa
      ofa ya kuongea bure kwa kipindi fulani, au kutoa
      zawadi mbalimbali, lakini huku wakijua jinsi
      watakavyotukamua kwenye muda wa maongezi.
      Hivyo CHADEMA, wangeenda pole pole, kwa
      uhakika na kwa uchunguzi wa kina, wangeweza
      kugundua mengi juu ya mfumo mzima wa
      mawasiliano ya simu. Nao wangeenda Israeli,
      na kutengeneza mtambo wa kukamata
      mitambo inayoingilia mawasiliano. Tena
      wangeenda kwenye kampuni hiyohiyo
      iliyotengeza mtambo huo wa kuingilia
      mawasiliano ya ujumbe mfupi. Huo ndiyo
      mchezo wa makampuni makubwa katika
      mchakato mzima wa ubeberu na unyonyaji.
      Wanatengeneza virusi vya kushambulia
      mtandao, na wakati huohuo wanatengeneza
      silaha za kupambana na virusi hivyo. Kwa njia
      hii wao wanatengeneza faida kubwa kwa
      maumivu ya watu wengine.
      Taifa letu sasa hivi linapita katika kipindi
      kigumu sana. Na kufikia uchaguzi mkuu wa
      2015, tutashuhudia mengi. Hivyo ni muhimu
      CHADEMA na watu wengine wenye nia njema
      na taifa letu kuvuta subira kwa matukio
      mbalimbali, ili tuweze kuwafichua majambazi
      na watu wenye nia mbaya na taifa letu. Mfano
      hili la kuingilia mawasiliano na
      kuwachonganisha watu kiasi cha kufikishana
      mahakamani ni kitendo kibaya kiasi kwamba
      kinaweza kutufikisha katika umwagaji damu.
      Tutapambana na watu hawa wabaya kwa kupiga
      hatua za uhakika; na hatua muhimu ni
      kuwakamata watu hawa wakiwa kazini.
      Kuwakamata kwenye mazingira ambayo
      hawawezi kwa namna yoyote ile kukwepa na
      kuweza kutunga hadithi kama ile ya
      mtuhumiwa kwenda kutubu Kanisani.

    4. #3
      markj's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 1,006
      Rep Power : 548
      Likes Received
      164
      Likes Given
      143

      Default re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      wa israel wanachangia kutokomeza amani ya hii dunia kama ni kweli, kwanini watengeneze kitu kama hiki ambacho hakina manufaa yoyote yale kwa upande wowote zaidi ya kuchochea ugomvi! inamaana ntu kama mmarekani anaweza kureceive mawasiliano white house yakiwa kama yametumwa na ikulu ya urusi1 kumbe sio,wamejitumia wao kwa kutumumia aina ya kifaa kama hiki! na vitakuwa viko more advanced tena waweza kuta kikawachapiga hata simu sasa na si sms!

    5. #4
      Kigogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,196
      Rep Power : 2095
      Likes Received
      1233
      Likes Given
      313

      Default

      Ccm ni kama mtu anayekata roho...maana wanahangaika kweli..huyo werema ndo mbumbumbu kabisa hata sijui aliupataje huo uanasheria wa serikali

    6. #5
      Nyetk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2012
      Posts : 1,029
      Rep Power : 682
      Likes Received
      574
      Likes Given
      593

      Default re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      [Samahani wakuu, nilikuwa nasaidia ku-edit
      maana mimi binafsi ilikuwa inanitia uvivu kuisoma
      ]

      Nyetk
      Mlitika likes this.

    7. Miaka 50

    8. #6
      ndyoko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 4,505
      Rep Power : 1706
      Likes Received
      1199
      Likes Given
      1916

      Default re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      Mraji and Ridhiwani at work. Shida ya kuendesha kamoeni kifamilia unakuta hata majukumu ya kirais familia nayo inadhani inawajibu wa kuyatekeleza pia!
      “If you can not get what you love, then love what you have”

    9. #7
      Mlitika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2012
      Posts : 411
      Rep Power : 519
      Likes Received
      223
      Likes Given
      319

      Default re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      Quote By Nyetk

      [Samahani wakuu, nilikuwa nasaidia ku-edit

      maana mimi binafsi ilikuwa inanitia uvivu kuisoma]
      Nyetk
      Asante mkuu Nyetk, maana kimchina changu kilishapata moto!
      Nyetk likes this.

    10. #8
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 2,069
      Rep Power : 923
      Likes Received
      837
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By markj
      wa israel wanachangia kutokomeza amani ya hii dunia kama ni kweli, kwanini watengeneze kitu kama hiki ambacho hakina manufaa yoyote yale kwa upande wowote zaidi ya kuchochea ugomvi! inamaana ntu kama mmarekani anaweza kureceive mawasiliano white house yakiwa kama yametumwa na ikulu ya urusi1 kumbe sio,wamejitumia wao kwa kutumumia aina ya kifaa kama hiki! na vitakuwa viko more advanced tena waweza kuta kikawachapiga hata simu sasa na si sms!
      Ukiwa umejifungia kwenye box ndiyo unaweza kuona tecknology ya aina hiyo haina maana yeyote. Lakini kwa Isreal inaweza kuwa na maana sana hasa kwenye masula ya UJASUSI.

      If your memory still serves you well, kumbuka Waisrael walipoingilia mawasiliano ya IKULU ya Uganda enzi za Idd Amin na kwenda kuwakomboa mateka wao walikuwa wamtekwa na kuondoa Entebbe, bila Amini kufahamu.

      Scenerio nyingine, kwa wale tuliokuwa Arusha wakati wa ujio wa Rais Clinton (Sio Bush) wa USA. mawasiliano yote ya simu, internet etc yaliingiliwa na FBI/CIA(?) Arusha nzima ikawa haina mawasiliano kwa masaa kadhaa. Kwa wamarekani walifanya hivyo kwa sababu ya usalaama.
      MIGNON and markj like this.

    11. #9
      wizaga's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th November 2011
      Posts : 69
      Rep Power : 391
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default Re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      nakubaliana kabisa na maneno yako,technogia hizi zipo duniani mfano vita vya waamerika nchini iraqu vyombo vyao vya mawasiliano kutoka iraq kwenda amerika vilikuwa vinaingiliwa na vifaa vya mawasiliano toka urusi lakini wenzetu wajanja waligundua mapema na kutumia tech nyingine pia osama bin laden alikuwa anauwezo wa kuingia kwenye sore au server za white house na kujua walichopanga lakini obama alipoingia madarakani akachenge to victory

    12. #10
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,369
      Rep Power : 1211
      Likes Received
      1214
      Likes Given
      1591

      Default Re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      naona justification zote za matumizi ya hii technologia yamejikita kwenye misingi ya kivita. kwani na sisi tuko vitani?

    13. #11
      Haki Yetu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th April 2011
      Posts : 124
      Rep Power : 433
      Likes Received
      27
      Likes Given
      15

      Default Re: Hili la SMS spoofing, CHADEMA wamefanya haraka!

      Sasa mtoa mada nadhani umesahau kidogo, hivi unakumbuka issue ya mkuu wa wilaya Igunga ilivyokua? Unajua hukumu yake imekuaje?

      Unakumbuka sakata la kukamatwa kwa lori lililojaa masanduku yenye kura jijini Mbeya? Mwisho wake nalo ulikuaje?

      Hilo la hao vijana wa mkuu waliowaleta wenzao kuvuruga kura za urais kwa teknolojia, kwani si hadi mahali wanapofanyia shughuli yao palitajwa, nalo lilikwisha vipi?

      Kutokana na hayo yote walivyosema mapema yote ni sawa kabisa mkuu, utakapomkamata na mtambo huo utashangaa polisi ndo wanaukimbiza na kuuficha na kesi inakurudia wewe!

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...