Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 33 of 33
    1. #1
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,394
      Rep Power : 10868
      Likes Received
      3773
      Likes Given
      426

      Post Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

      MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Mwambigija, maarufu kama Mzee wa Upako na Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete, wamekamatwa na kusafirishwa hadi wilayani Chunya kisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kutoa maneno ya uchochezi.

      Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kusema kuwa walikamatwa juzi katika eneo la Inyara, wakiwa ndani ya basi kuelekea Dodoma.

      Alisema kuwa viongozi hao walisafirishwa hadi Chunya ambako waliunganishwa na wenzao wawili kabla ya kupelekwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

      Kamanda Diwani aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Katibu wa CHADEMA Kata ya Makongorosi, Erick Luvanda na Katibu Mwenezi wa kata hiyo, Dominick Chaula.

      Alisema baada ya kusomewa mashtaka yao mahakamani, watuhumiwa walipewa dhamana na kutakiwa kurudi tena mahakamani hapo Agosti 16, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kwa kesi hiyo.

      Hivi karibuni viongozi hao kwa kushirikiana na viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Chunya walifanya mikutano mbalimbali kwa siku 10 wilayani humo ikiwa ni sehemu ya operesheni iliyopewa jina la ‘CHADEMA Twanga Kotekote’ yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kukijenga chama hicho.

      Source:Tanzania Daima
      Mikael P Aweda likes this.

    2. Study Abroad

    3. #21
      Komeo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2011
      Location : Mlangoni
      Posts : 904
      Rep Power : 587
      Likes Received
      338
      Likes Given
      106

      Default Re: Vigogo CHADEMA wafikishwa kortini

      Quote By IDIOS
      MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Mwambigija, maarufu kama Mzee wa Upako na Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete, wamekamatwa na kusafirishwa hadi wilayani Chunya kisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kutoa maneno ya uchochezi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kusema kuwa walikamatwa juzi katika eneo la Inyara, wakiwa ndani ya basi kuelekea Dodoma.
      Hapo kwenye red. Ni nani anayetoa vibali vya kufanya mikutano ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa na Tendwa? Hilo kosa liko kinyume na kifungu kipi cha Katiba au sheria ipi? Ninavyofahamu mimi ni kuwa vyama vya siasa vinaweza lakini havilazimishwi kuitaarifu polisi kwa ajili ya taarifa tu juu ya uwepo wao eneo fulani, na sio kuomba hicho "kibali".
      Kassim Awadh and kibogo like this.
      LIWALO NA LIWE - PINDA.

    4. #22
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,291
      Rep Power : 1195
      Likes Received
      1178
      Likes Given
      1551

      Default Re: Vigogo CHADEMA wafikishwa kortini

      Safi sana, lazime walipie, kupata uongozi ni gharama, wananchi tutawapima kwa uvumilivu wao dhidi ya huu uonevu.Yeyote atakayeshindwa kuvumilia mateso,uonevu,dhiaka,manyanyas o, na hila zote ze serikali ya chama cha Mapinduzi itakuwa ni kwa manufaa ya UMA sababu tutakuwa tumepunguziwa viongozi waoga. Asante CCM na serikali yako kwa kutupitishia watu hawa kwenye tanuru la joto.

    5. #23
      LiverpoolFC's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2011
      Posts : 6,638
      Rep Power : 11269
      Likes Received
      1460
      Likes Given
      570

      Default Re: Vigogo CHADEMA wafikishwa kortini

      Mwanzo wa ukombozi unaonekanaga hv hv!

      Mwanzo mgumu!

    6. #24
      Mende0's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th February 2012
      Location : Magogoni
      Posts : 1,394
      Rep Power : 643
      Likes Received
      397
      Likes Given
      91

      Default Re: Vigogo CHADEMA wafikishwa kortini

      Kamata kamata achia hii ndo inawapa nguvu makamanda na wanazidi kusonga mbele mpaka mkoloni mweusi aachie nchi.
      Bajeti ya maskini tajiri haiwezi

    7. #25
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,550
      Rep Power : 16758
      Likes Received
      2473
      Likes Given
      1841

      Default Re: Vigogo CHADEMA wafikishwa kortini

      Quote By Mwiba
      Mara nyingi huwa wanasamehewa na kuambiwa wasirudie tena.
      Licha ya gharama zote kubwa zilizotumika wanasamehewa kirahisi namna hiyo??

    8. Miaka 50

    9. #26
      Wambugani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th December 2007
      Posts : 1,239
      Rep Power : 832
      Likes Received
      142
      Likes Given
      169

      Default Re: Vigogo CHADEMA wafikishwa kortini

      Quote By LiverpoolFC
      Mwanzo wa ukombozi unaonekanaga hv hv!

      Mwanzo mgumu!
      Kazi ya polisi siyo usalama wa raia tena. Ndiyo maana Mheshimiwa Deo Haule Filkujombe, Mbunge wa Ludewa alisema kwamba kazi ya virungu vya polisi sasa ni kuwapiga CHADEMA..
      Wars are caused by undefended wealth - Ernest Hemingway, famous American writer

    10. #27
      Kassim Awadh's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Posts : 584
      Rep Power : 478
      Likes Received
      108
      Likes Given
      769

      Default Re: Vigogo CHADEMA wafikishwa kortini

      Quote By Komeo
      Hapo kwenye red. Ni nani anayetoa vibali vya kufanya mikutano ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa na Tendwa? Hilo kosa liko kinyume na kifungu kipi cha Katiba au sheria ipi? Ninavyofahamu mimi ni kuwa vyama vya siasa vinaweza lakini havilazimishwi kuitaarifu polisi kwa ajili ya taarifa tu juu ya uwepo wao eneo fulani, na sio kuomba hicho "kibali".
      Uko sahihi,,cjui ni katiba/shreria ipi,,CPA ama Penal code kifungu gani?pengine ndo maana nyingiwazo zinaishia hewani tu

    11. #28
      Daniel Anderson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2011
      Location : LUPA CHUNYA
      Posts : 826
      Rep Power : 558
      Likes Received
      129
      Likes Given
      348

      Default

      Quote By Sangarara
      Safi sana, lazime walipie, kupata uongozi ni gharama, wananchi tutawapima kwa uvumilivu wao dhidi ya huu uonevu.Yeyote atakayeshindwa kuvumilia mateso,uonevu,dhiaka,manyanyas o, na hila zote ze serikali ya chama cha Mapinduzi itakuwa ni kwa manufaa ya UMA sababu tutakuwa tumepunguziwa viongozi waoga. Asante CCM na serikali yako kwa kutupitishia watu hawa kwenye tanuru la joto.
      nimeipenda hii ila simu haina kitufe cha LIKE. Thanks

    12. #29
      Msolopagazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2010
      Posts : 476
      Rep Power : 525
      Likes Received
      47
      Likes Given
      17

      Default Re: Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

      Mbona Mwigulu,Nape,Lusinde hawakamatwi dawa ni kuwaponda tu

    13. #30
      Pwito's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th March 2012
      Posts : 176
      Rep Power : 395
      Likes Received
      32
      Likes Given
      70

      Default Re: Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

      Embu hawa PoloCCM wajipange kutatua matatizo ya ulinzi na wala sio umaarufu kupitia CDM

    14. #31
      kibogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Location : MBEYA
      Posts : 1,674
      Rep Power : 691
      Likes Received
      418
      Likes Given
      312

      Default Re: Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

      Hawa makamanda wa Polisi katika maeneo mbali mbali hapa nchini naona wameagizwa wafanye kazi ya ziada kuzuia hii M4C na wakifanikiwa watapandishwa vyeo ndoo maana wanakamata tu hata kama makosa yenyewe sio ya msingi lakini mwisho wa ubaya ni AIBU

    15. #32
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,602
      Rep Power : 1103
      Likes Received
      997
      Likes Given
      747

      Default Re: Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

      Soma Historia wakati wa ukoloni viongozi wanana mapinduzi kama akina Mandela, Nyerere, Nkuruma, Lumumba, na wegine wengi sana walifunguliwa kesi za aina hii na wengine waliuawa kama Solomon Mhalangu n.k Ila saa ya ukombozi ilipofika kulikuwa hakuna namna!!CCM wajidanganye kama walivojidanganya wakoloni but time is not their best friend !!!
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    16. #33
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,394
      Rep Power : 10868
      Likes Received
      3773
      Likes Given
      426

      Default Re: Serikali yazidi kuandama CHADEMA:yawafungulia mashtaka madiwani na viongozi wa chama Mbeya

      Mungu akiwa upande wa CDM ni nani atakayesimama?

    17. FemaTV & Radio
    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...