ha ha ha!, tamuchungu unanichekesha, eti hakuna daktari anayejisomesha hapa tanzania kwa pesa yake binafsi, kwa kuwa gharama za kusomea udaktari ni kubwa sana, nakuonea huruma, sijui unaishi au umetokea maeneo gani ya tanzania, wapo madaktari wengi tu wanaojisomesha kwa pesa zao binafsi na za wazazi au walezi wao bila kutegemea serikali wala wafadhili, toka food, stationaries, fees, usafiri n.k, na wanaishi maisha mazuri ndani ya chuo sio ya kubangaiza na kujinyima kwa kupiga dash mchana au asubuhi, watu tumetofautiana mheshimiwa, usiseme "twafa" sema "nafwa", watu wamejiandaa vema kutunza familia zao though wengine wanatumia fedha za utapeli, wizi, madawa ya kulevya n.k but wapo wanautumia fedha waliyoipata kihalali pia, kuna watu wana hela bongo hii kama ulikuwa hujui!, mi kuna mtu namfahamu, baba yake kamsomesha urubani marekani kwa fedha yake mwenyewe ya mfukoni, baba yake ni mfanyabiashara, na wala si mtu maarufu, kamgharamia mwanae kila kitu kwenye masomo na maisha yake, kuanzia nauli za kwenda na kurudi, chakula, mavazi, vifaa vya shule, malazi, fedha za matumizi, fedha za matibabu n.k na alikuwa anaishi maisha mazuri tu marekani ila mwenyewe aliamua kutafuta tu kajob ka kizushi, ili asimkamue sana mzee wake ili aweze kuhangaika na ndugu zake wengine home bila hofu ya kuhisi mwanaye atakuwa na shida ndogo ndogo, so kuna watu wana hela ndugu yangu, na ukiwaona wengine wako simple tu
Follow Us Here