Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Muongozo wa CCM!

    Report Post
    Results 1 to 6 of 6
    1. #1
      vukani's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th December 2009
      Location : Dar and Arusha
      Posts : 241
      Rep Power : 1418
      Likes Received
      146
      Likes Given
      178

      Default Muongozo wa CCM!

      Jana nimekutana na kijitabu kidogo cha kijani kwenye maktaba ya baba yangu. Kitabu hicho kimeandikwa “MUONGOZO WA CCM” ambacho kilichapwa mwaka 1981, na Printpak.

      Wakati nakipitishia macho nikavutiwa sana na vifungu vilivyoandikwa ukurasa wa 77 na wa 80. Naomba ninukuu maneno hayo hapa chini.

      Ukurasa wa 77.

      (6)WIZI WA MALI YA UMMA , HUJUMA ZA KIUCHUMI, MAGENDO NA UJAMBAZI.

      Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu wa aina mbalimbali nchini tangu tupate uhuru. Uhalifu wenye kutia wasiwasi maalum ni uhalifu wa kiuchumi. Wizi wa mali ya umma umeanza kuwa ni jambo la kawaida. Kumekuwa na matukio ya baadhi ya maafisa kuhusika na kuidhinisha mikataba na makampuni ya nchi za nje bila kujali maslahi ya Taifa. Wakati huo huo vipusa, dhahabu na mali mbali mbali a Taifa zinatoroshwa nje ya nchi kwa magendo na kusababisha hasara kubwa kwa Taifa.

      Ujambazi wa kutumia silaha nao umetumika ili kunyang’anya mali na kutisha wananchi.
      Chama kitahakikisha kuwa Serikali inachukuwa hatua kali za kupambana na vitendo hivi vinavyodhoofisha uchumi wa Taifa. Iko haja pia kwa sasa ya kubuni sheria maalum zitakazoelekezwa kwenye vita dhidi ya uhalifu wa kiuchumi unaozidi kuongezeka”

      Mwisho wa kunukuu kipengele hicho.

      Halafu ukurasa wa 80, nao ulikuwa na maneno haya:

      92.
      watu wameanza kuthamini zaidi vitu kuliko utu na tamaa ya kujipatia mali bila kuitolea jasho inaenea, matukio ya wizi wa mali ya umma yameongezeka. Lakini lililo baya zaidi ni kuwa mwizi wa aina hiyo anapogunduliwa, baadhi ya wananchi, badala ya kumfichua au kulaani kitendo chake, humsifu na kumhusudu. Wakati mwingine mvivu na mtegaji kazini hutetewa hata na vyombo vya chama vyenyewe. Wakati huo huo bado kuna mabaki ya tabia ya kupuuza elimu ya shule kwa watoto na badala yake kuna wazazi wanaopendelea watoto wao wachunge mifugo au hata kuolewa badala ya kuendelea na shule...........na blah blah blah blah blah nyingine zinaendelea................... ...........

      Mimi nimesoma tu nikaona ni vyema nikashirikisha wasomaji wa JF kutafakari huo muongozo wa CCM, ulioandikwa hapo mnamo mwaka 1981.
      Ndahani likes this.
      "What I need from you is LOVE"

    2. Miaka 50

    3. #2
      Communist's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Location : Ubungo
      Posts : 2,726
      Rep Power : 2267
      Likes Received
      601
      Likes Given
      783

      Default Re: Muongozo wa CCM!

      Simple life is healthier than egoism.

    4. #3
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Muongozo wa CCM!

      Hivyo vilishachomwa moto Lumumba. Vinatukataza kufanya yale tunayoyafanya kwa nguvu zote
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    5. #4
      WEMBE WENGE's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th March 2011
      Posts : 100
      Rep Power : 440
      Likes Received
      28
      Likes Given
      27

      Default Re: Muongozo wa CCM!

      nAKUSHAURI TOA PHOTOCOPY KITABU CHOTE NA UBAKI NA PHOTOCOPY HALAFY HIYO URIGINO UITUME CCM MAKAO MAKUU KWA ADDRESS IFUATAYO:

      NAPE NAWIE,
      KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI.
      CCM MAKAO MAKUU
      P.O.BOX......
      DAR-ES-SALAAM/DODOMA.

      AKIONE MWENYEKITI NA KATIBU MKUU WA CCM

      Labda atakumbuka vilivyoandikwa na baba yake mzee NNawie. vikapitishwa ma Mlm Nyerere.
      inaweza kuwafanya wajutie ufisadi na kuipenda Tanzania yetu ambayo inaliwa kila kona mpaka CDM watakapoichukua itabaki mashimo na mbuga tuu, madini yoooote hakuna, misitu yooote hakuna.

      halafu tuwaulize yale Matrekata pale JKT Lugalo ndipo kilipo kilimo kwanza???????? kama si ufisadi ni nini?
      CCM hatuwawezi kila mtu ana dili lake, mtu kaanza ooo kilimo kwanza kumbe ana akili yake kandua kuna pesa za matrekta. kwa bidii akaagiza mengiiii akijua kuna mabilioni atavua humo. tukifuatilia kampuni iliyoleta, magumashi, bei yake magumashi, nimesikia bungeni wakisema haa clearing costs pia magumashi,,, eeee makubwa,
      Someni mipango ya wazee wenu muijenge nchi. hta hayo mabilioni yaliyopo uswiss yasingekuwepo badala yake yangenunua vitabu na madawati kwa ajili ya watoto wetu.

    6. MKL
      #5
      MKL's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd March 2012
      Posts : 96
      Rep Power : 542
      Likes Received
      62
      Likes Given
      6

      Default Re: Muongozo wa CCM!

      Quote By WEMBE WENGE
      nAKUSHAURI TOA PHOTOCOPY KITABU CHOTE NA UBAKI NA PHOTOCOPY HALAFY HIYO URIGINO UITUME CCM MAKAO MAKUU KWA ADDRESS IFUATAYO:

      NAPE NAWIE,
      KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI.
      CCM MAKAO MAKUU
      P.O.BOX......
      DAR-ES-SALAAM/DODOMA.

      AKIONE MWENYEKITI NA KATIBU MKUU WA CCM

      Labda atakumbuka vilivyoandikwa na baba yake mzee NNawie. vikapitishwa ma Mlm Nyerere.
      inaweza kuwafanya wajutie ufisadi na kuipenda Tanzania yetu ambayo inaliwa kila kona mpaka CDM watakapoichukua itabaki mashimo na mbuga tuu, madini yoooote hakuna, misitu yooote hakuna.

      halafu tuwaulize yale Matrekata pale JKT Lugalo ndipo kilipo kilimo kwanza???????? kama si ufisadi ni nini?
      CCM hatuwawezi kila mtu ana dili lake, mtu kaanza ooo kilimo kwanza kumbe ana akili yake kandua kuna pesa za matrekta. kwa bidii akaagiza mengiiii akijua kuna mabilioni atavua humo. tukifuatilia kampuni iliyoleta, magumashi, bei yake magumashi, nimesikia bungeni wakisema haa clearing costs pia magumashi,,, eeee makubwa,
      Someni mipango ya wazee wenu muijenge nchi. hta hayo mabilioni yaliyopo uswiss yasingekuwepo badala yake yangenunua vitabu na madawati kwa ajili ya watoto wetu.


      NAPE si mtoto wa Mzee Nnauye hili likukae kichwani kama si rohoni, unakumbuka alipoanza chokochoko za UVCCm mjane wa baba Nnauye alimkana waziwazi? na baada ya hapo uliibuka ukweli? kuanzia leo elewa kuwa Nape si mtoto wa Nnauye na usimshangae kwa roho ya kifisadi aliyonayo ni kuwa hiyto sio Roho ya Mzee Nnauye ni ya Fisadi moja linaumwa kwa sasa.

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Babuu Rogger's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Posts : 234
      Rep Power : 426
      Likes Received
      35
      Likes Given
      2

      Default Re: Muongozo wa CCM!

      Katika kitabu "TANU NA RAIA" kilichoandikwa na JULIUS K. NYERERE cha mwaka 1962 katika kipengele cha uongozi wa tanu aya ya tatu mwalimu anasema 'Asili ya uongozi wetu ni mbili: Ya kwanza ni WATU .Hatukutumwa kutoka katika mwezi kuja kuongoza watu wa nchi hii. Wala sisi si viongozi wa kikoloni kwamba tulitumwa na serikari ya kigeni kuja kuongoza watu wa nchi hii. Uongozi wetu hauna budi utokane na watu wa nchi hii, bila hila, bila rushwa, bila vitisho na ujanja wa aina yoyote, Tunapofika katika uongozi kwa kupitia mlango wa hila, au rushwa, au ujanja wa aina nyingine yoyote, basi hatukutokana na watu wenyewe.
      Asili ya pili ya uongozi wetu ni HAKI. Tuliunda tanu iondoe ukoloni pamoja na maonevu pamoja na dhuluma za aina yoyote zilizoambatana na ukoloni. Lakini HAKI NI HAKI kwa WATU, sio kwa majani au miti. Basi, tukifika katika hali yetu ya uongozi kwa njia yoyote ambayo si ya HAKI, ni wazi kwamba haiwezekani tuwe tumetokana na watu wenyewe. Japo kama uongozi wetu haukutokana na kura za watu, bali niwa kuajiriwa, ni wazi kuwa tumeufikia kwa njia za hila, rushwa, vitisho au ujanja wa aina yoyote, hauwezi ukawa uongozi wa HAKI na hauwezi ukawa uongozi wa WATU. WATU NA HAKI ni misingi ya uongozi ambayo haiachani.
      Nikisema hivyo siyo kwamba kiongozi asiyechaguliwa na WATU hawezi akatenda yaliyo ya HAKI. Anaweza. Maana yangu ni kwamba walinzi wa HAKI za WATU ni watu wenyewe. Kutegemea haki zao zilindwe na viongozi wasiotokana nao ni jambo la kubahatisha.
      THERE AIN'T NO HIDING PLACE FROM THE FATHER OF CREATION.

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...