
By
Nonda
Mkuu nguruvi3,
Unaionaje hiyo rai ya Mwalimu Nyerere ya kuwa na serikali mbili Tanzanaia? Serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar badala ya serikali ya Tanzania na serikali ya Zanzibar?
Nia ya mjadala/ mijadala hii sio lazima iwe Simba na Yanga. Bali ni kutafuta suluhisho( dawa mjarabu) ya usanii wetu(Muungano wetu). Hii dawa aliyoitoa Mwalimu itatibu matatizo sugu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Itatatua tatizo la kuibebesha mzigo Tanganyika( Tzbara/ bara) na akina sisi tunaotaka kujinasibisha na utanganyika wetu tutatembea na kifua mbele, itamaliza kelele za washirazi(masultani,watwana,wa tumwa,Znz) na itakidhi tunu yetu ya umajumui wa kiafrika(pan-africanism) tuliyonayo; kuwa na nchi kubwa yenye members wengi, Kenya, Uganda, Tanganyika, Zanzibar, Rwanda na Burundi. Yaani nchi yetu itakuwa na wanachama 6. Bila shaka mfumo wake utakuwa mfumo wa shirikisho. Serikali 7, serikali za majimbo 6 na serikali ya shirikisho 1.
Au wewe unataka kubaki na mazingaombwe yaliyodumu kwa miaka 48 ambayo yanazalisha kero tu?
Tazama picha kubwa, usijikite kwenye masimulizi ya Jussa, Seif, Barubaru, Hizbu, ASP, Usultani,mapinduzi daima nk.
Tanabahisho.Litakapoundwa Shirikisho la Afrika Mashariki, utanzania utakufa, utaifa mpya utakuwa Uafrika Mashariki, lakini majina ya maeneo(territories) yatabaki.
Naomba wanajf, tuipokee hii rai, tuifikirie kwa utuo na kama tutaona itatusogeza mbele basi, kampeni ianze mara moja ya Tanzania yenye serikali mbili, ya Tanganyika na ya Zanzibar.
Atakapokuja Warioba na tume/kamati yake tudai, Tanzania yenye serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.
Tunaua dege bili kwa jiwe moja tu.
Soma post #88 hapo juu.
Follow Us Here