SAKATA la ubomoaji majumba ya kifahari yaliyojengwa katika fukwe za Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa kufichua siri ya uhalifu.
Waziri amesema mbali na yeye kutishwa kuuawa, pia Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Manchare ametekwa na watu wasiojulikana wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na kumpiga kisha kumtelekeza eneo ambalo hakulitaja.

Reply With Quote



Follow Us Here