Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 35 of 35
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,153
      Rep Power : 3544
      Likes Received
      3037
      Likes Given
      460

      Default Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?




      Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 11 July 2012

      ULIMBOKA ni neno la Kinyakyusa lenye maana ya Mungu uniponye. Neno hilo ndilo linatumika kama jina na ukoo wa Dk. Steven.

      Mtu akiwa kwenye matatizo, shida, mashaka au mateso huomba huruma ya Mungu amponye. Kwa huruma na upendo, Mwenyezi Mungu ndiye aliwashika wasamaria wema, kwa mkono wake wa miujiza, akawaongoza, bila kujijua kwenda kumwokota na kumfikisha hospitalini Dk. Steven Ulimboka aliyepigwa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande akaachwa afe.


      Mungu aliyewaongoza wasamaria wema kumwokoa na kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI), ndiye amemtia nguvu, anazungumza sasa kwa ‘ufasaha’ alivyopigiwa simu na ofisa wa ikulu, alivyotekwa, alivyoteswa usiku kucha na alivyookotwa.


      Hivi sasa anapata matibabu katika hospitali moja nchini Afrika Kusini, akisubiri ubuponyi yaani uponyaji kamili kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.

      Katika mkanda wa mahojiano maalum akiwa MOI, Dk. Ulimboka haachi chembe ya shaka kwamba mkasa huo ulipangwa na kuratibiwa na kikosi maalum cha ‘mauaji’ ambacho kina maslahi na mgomo wa madaktari ambao umedumu kwa wiki tatu sasa.

      Sehemu ndogo ya maelezo ya Dk. Ulimboka ni kama ifuatavyo….

      …Kazi yao ilikuwa siyo kufanya kazi kama askari, eeh its like they acted under instructions.

      Eeh, yaani unajua, kwa muda kama siku tatu mfululizo, huyu bwana alikuwa anajaribu kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya ratiba yangu ilikuwa haiwezekani kumwona.


      Nilishawahi kumwona zamani, kwenye mgogoro ule mwingine, lakini this time of course alikuwa serious akinitafuta akisema kwamba anataka some hearing ili aweze kushauri. Huyu bwana anafanya kazi ikulu.


      Aah, mimi kwa sababu namfahamu kutokana na incident ya kwanza sikuwa na muda. Lakini jana aka-insist sana na akakaa Hugo pale muda mrefu sana, sisi tulikuwa tumekaa Leaders Club.


      Baadaye nikamwambia Deo kuna jamaa mmoja – ambaye Deo anamkumbuka sana kwa sababu mara zote huwa tunakwenda naye – anataka kutuona. Basi tukawaacha wenzetu wanafanya kazi nyingine, tukaondoka mimi na Deo around saa tano, ilikuwa na robo (5.15).


      Naye akatuarifu kuwa pale Hugo alipokuwa amekaa wanafunga, akawa ameenda kule juu sehemu inaitwa Stereo, akaniambia yupo pale. Mimi nikawasha gari hadi pale, nikaangalia meza ya kwanza pale sikumwona. Tulipoingia pale hatukumwona.

      Nikazunguka sikumwona, nikampigia simu akaniambia, nakuja hapo sasa hivi.


      It took like twenty to thirty minutes tangu aliposema anakuja. Tukaamua kuwasha gari ili kurudi pale Leaders lakini tukaona kama hilo haliwezi kuwepo. tukaishia pale Tunisia Road kuna kontena, tukakaa pale. Sasa akawa anapiga simu akisema anakuja kuna vitu anamalizia; tukawa tunawaza ni vitu gani?


      Basi tukiwa tumekaa, ghafla tukamwona anafika, kwa gari. Akasema uko na Deo, nikasema eeh. Basi tukaanza mazungumzo.


      Kitu ambacho nili-notice, while tukiwa tuna-discuss naye, akitaka kujua namna gani tuweke understanding; matatizo yetu ni yapi, which are the priority areas, eeh kama alivyosema yeye mwenyewe ili aweze ku-advise, kwa sababu wakati mwingine…


      Sisi tukasema mambo yote yanafahamika. Tukaongea naye kwa muda mfupi tu, akawa anaandika kwenye diary yake, kwa hiyo pia alikuwa very bussy communicating, unaona.


      Kwenye simu yake sasa, tukafika kwamba tumemaliza. Ila sisi tulikuwa tuna vinywaji kwa sababu ilikuwa siyo rahisi sana tumwache yeye aondoke sisi tuendelee kubaki. Yeye alikuwa anakunywa maji akasema bwana mi naondoka.


      Kwenye ile line ya yeye kusema anaondoka tu, hapo hapo wakatokea watu kama wanne watano hivi, wakasema, wakaja straight kwenye meza yetu, as if they were directed. Wakasema upo chini ya ulinzi, yaani mimi hapa. Kama mtu hakujui hawezi kuja saa 5 usiku kuja kukukamata.


      They came direct towards me, nikauliza kwani kuna kosa gani? Wakanipiga mtama nikaanguka barabara ya lami. Nilichokifanya kitu cha kwanza ni kutoa simu na kumpa Deo. Sasa they pushed me na kufanikiwa kuchukua simu moja na wallet yangu.


      Nilichowahi ni kuchomoa simu yangu kumpa Deo. Wakaniburuza huku wakini-push again na kuvuka barabara hadi kwenye gari ile, ilikuwa haina namba ile, ni kama Starlet hivi. Nikaamua tu kubaki patient.


      Wakafungua lango la nyuma wakanitupa huko. Wakaja wakanitupa huko. Basi mmoja akaingia upande wangu wa kulia mwingine wa kushoto. Wakaanza kunipiga ngumi, wakanipiga ngumi; mwingine akanipiga vichwa, naona, wengine wana kama dude fulani kama la plastiki hivi, wananipiga kichwani. Wananiambia tulia tutakuua sisi. Kama una ndugu zako aga kabisa kwa sababu leo hurudi.


      Unatuletea usumbufu sana wewe… sasa nikawa najiuliza usumbufu gani? Kwa sababu hata hapo usumbufu, wewe unajua unachokifanya kwa hiyo tunataka kukomesha hiyo tabia. Wakanipiga kwenye gari hiyo huku inakwenda, ilikuwa inaenda mwendo wa kasi sana. Nikafanikiwa kuchungulia hivi nikagundua tuko maeneo ya Victoria…

      …Hata na ile miguu wakafunga sana. Basi wakaendesha gari, wakaendesha this time muda mrefu sana. Sikuwa najua wanaenda wapi. Walipokuja kunishusha, wakaanza kunipiga tena.

      Sasa kwa sababu I was helpless nimefungwa, basi nikawa napigwa nageuka hivi, nikigeuka hivi, nikaona wananipiga kwa sikio la huku, wengine wakawa wananipiga sikio la huku walinipiga sana kama half an hour hivi, and then I think I lost consciousness.


      Unaona na nilikuwa na-bleed sana wakati ule. Kwa hiyo nilichofanya nikawa napata feelings hawa watu they are carrying me somewhere.


      Nikafika mahali nikaona kama vile wamenitupa kwenye shimo hivi. Sijui kama wanataka kunifukia? Unaona, nikawaambia why I are you burring me alive?...

      Katikati ya mateso kama aliyopata Dk. Ulimboka kuna uponyaji. Kwa kuteswa kwake Yesu Kristo binadamu wamepona (biblia).

      Kwa kujichoma moto, mmachinga wa Tunisia baada ya mgambo na polisi kuvuruga biashara yake, nchi nzima iliwaka moto na Watunisia wakapata demokrasia.

      Kutokana na maandamano katika viwanja vya Tahrir na serikali kujibu kwa risasi, Misri iliwaka moto, hatimaye imefanya uchaguzi huru.

      Watu wote wasio na hofu ya Mungu, ndio wanaweza kujisikia raha kuteka watu wasio na hatia na kuwatesa, wakati mwingine, kwa kufurahia vipande vya fedha.


      Yuda Isikarioti alifurahia vipande 30 vya fedha kwa kazi ya kumsaliti Yesu. Aliishia wapi? Kwa kuteswa kwake Dk. Ulimboka, Mungu atawatia adabu walioratibu mpango huo.





    2. FemaTV & Radio

    3. #21
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,609
      Rep Power : 2889
      Likes Received
      3824
      Likes Given
      12196

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By zomba
      Kwi kwi kwi teh teh teh! Ya ngapi?
      Usinitakie ban ya bure ndugu yangu.

    4. #22
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By Jasusi
      Usinitakie ban ya bure ndugu yangu.
      Umekosa hoja unataka kuanza viroja?
      Jasusi likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    5. #23
      Kigano's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 276
      Rep Power : 414
      Likes Received
      130
      Likes Given
      189

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By zomba
      Vipi hali yake, hajambo> anarudi lini? ataendeleza migomo? vipi huyu alikuwa chadema?

      Nasikia kuna kada wa CCM kauliwa Singida, vipi? mnasemaje kuhusu hilo?
      kumbe mlipteka na kumpiga kwaajli ya migomo ? sasa mbona mnaanza kupeleka wehu mahakamani ? mnaogopa nini kujitokeza na kusema kuwa hamtaki migomo ?

    6. #24
      Makamuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Posts : 1,061
      Rep Power : 597
      Likes Received
      210
      Likes Given
      21

      Default

      Quote By zomba
      Umekosa hoja unataka kuanza viroja?
      Unalipwa sh ngapi ww mtoto wa kike...

    7. #25
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By Makamuzi
      Unalipwa sh ngapi ww mtoto wa kike...
      Kijana naona umekosa adabu mimi ni babu yako kama unabisha kamuulize bibiyo Zomba unamjuwa? atakueleza.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    8. Study Abroad

    9. #26
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By Kigano
      kumbe mlipteka na kumpiga kwaajli ya migomo ? sasa mbona mnaanza kupeleka wehu mahakamani ? mnaogopa nini kujitokeza na kusema kuwa hamtaki migomo ?
      Hujamsikia Kikwete?
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    10. #27
      andrews's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th March 2012
      Posts : 1,683
      Rep Power : 0
      Likes Received
      142
      Likes Given
      76

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      ​kikwete serikali yake inaongoza kuua kuliko marais watatu waliomtangulia sababu ni legelege
      Quote By zomba
      hujamsikia kikwete?

    11. #28
      raha54's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th August 2011
      Posts : 32
      Rep Power : 400
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Ebu someni vizur,

    12. #29
      St. Paka Mweusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2010
      Location : Ukune,
      Posts : 5,289
      Rep Power : 1691
      Likes Received
      1564
      Likes Given
      3289

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By Makamuzi
      Unalipwa sh ngapi ww mtoto wa kike...
      Quote By zomba
      Kijana naona umekosa adabu mimi ni babu yako kama unabisha kamuulize bibiyo Zomba unamjuwa? atakueleza.


      Ndio tatizo la hili jukwaa sasa matusi yantoka wapi tena..?
      UKICHOKA KUFANYA SIRI,FUMANIWA TU YAISHE . By Simon Kitururu.

    13. #30
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      'Hili swala kwa sasa lipo mahakamani' AL-HAJ

    14. #31
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      'Hili swala kwa sasa lipo mahakamani' AL-HAJ

    15. #32
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By MESTOD
      Kikwete mzima?
      Mzima wa afya na leo anapokea wageni wa Taifa, nasikia na Mbowe atakuwepo kwenye mapokezi kama Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    16. #33
      MESTOD's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2010
      Posts : 2,558
      Rep Power : 943
      Likes Received
      677
      Likes Given
      131

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Quote By zomba
      Mzima wa afya na leo anapokea wageni wa Taifa, nasikia na Mbowe atakuwepo kwenye mapokezi kama Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani.

      Kikwete ni mzima?

    17. #34
      Wachovu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th June 2012
      Posts : 222
      Rep Power : 1111
      Likes Received
      44
      Likes Given
      0

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Kwani kupokea wageni kunamwondolea sifa ya kuwa muuaji. Kashindwa kutawala sasa ana genge la wahuni kama Zomba ambao wapo tayari kuua hili kulinda hii tawala dhaifu. Jamani nchi haitawaliwi kwa kuua ni hoja , alete hoja zake tumkubali , yasije yakamkuta ya gadafi na mubaraka

    18. #35
      manucho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Posts : 561
      Rep Power : 469
      Likes Received
      79
      Likes Given
      0

      Default Re: Msaliti wa Dk. Ulimboka yuko ikulu?

      Hakuna kisichokuwa na mwisho, na pale unapojiona wewe ndiyo above te top hapo ndipo unapoanguka kichwa chini miguu juu. Hutaki kamuulize H. Mubarak

    19. Miaka 50
    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...