Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Tanesco, Robert Mboma amekataa kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari unaotarajia kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, William Mhando.
Uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando unatokana na bifu linalosemekana kuwapo kati ya Mhando na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi; lakini katibu mkuu huyo ametumia udhaifu wa serikali na tanesco kumwadhibu Mhando.
Inasemekana sababu inayotolewa na Katibu Mkuu ni kwamba Mhando alimdharau kwa kutompa taarifa kabla ya Tanesco kutangaza mgawo wa umeme wa hivi karibuni. Kwa mantiki hiyo, akamlima Mhando barua akisema anahujumu shirika. Hata hivyo, wananchi na watumishi wa Tanesco wanajua kuwa anayehujumu Tanesco ni serikali, ambayo inalinyima shirika hilo pesa ilizoahidi kwa ajili ya miradi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme, na kulizuia shirika hilo kuuza umeme kwa faida, kwa sababu za kisiasa.
Inasemekana hatua dhidi ya Mhando inatokana na woga wa waziri na katibu mkuu juu ya mjadala mkali unaotarajiwa kuibuka bungeni wakati wa kujadili bajeti ya wizara yao. Mhando anatolewa kafara kisiasa, lakini taarifa zinasema naye amejibu barua ya katibu mkuu kueleza jinsi asivyohujumu shirika hilo. Habari zaidi baadaye.
source east africa radio breaking news
Breaking news:mkurugenzi mtendaji wa tanesco william mhando asimamishwa kaziBodi ya wakurugenzi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi WILLIAM MHANDO (pichani) ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa dhidi ya Menejimenti ya TANESCO.
Taarifa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo Jenerali Mstaafu ROBERT MBOMA ambapo katika taarifa yake amesema maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha dharura kilichofanyika jana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Taarifa zinasema katika kikao hicho, Bodi iliona tuhuma hizo ni nzito hivyo ni vyema zikafanyiwa uchunguzi huru na wa kina mara moja
KWA HABBARI KAMILI BOFYA HAPA


Reply With Quote


Follow Us Here