Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

    Report Post
    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast
    Results 41 to 60 of 88
    1. #1
      wakuziba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th June 2012
      Posts : 123
      Rep Power : 580
      Likes Received
      42
      Likes Given
      43

      Default Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      nianze kwa kusema kuwa nakukubali dr slaa kwa kazi nzuri ulioifanya bungeni kipindi cha 2005 - 2010 kabla hujagombea urais. nilikuelewa kama mtu alie makini, mzalendo aso yumbishwa na porojo za kisiasa! siyo siri hicho kipindi ulilitumikia taifa kama mzalendo halisi. hongera kwa hili! lakini baada ya kugombea urais dr umekua ukibadilikabadilika kimsimamo na umekua hueleweki na wafuasi wako. Elewa kuwa ktk uchaguzi wa 2010, uliungwa mkono na watanzania wakikutaka wewe kuwa rais wao. hawakujali itikadi za vyama vyao. walikuona kama mkombozi wao. mambo yafuatayo, nionavyo mimi, yanakutoa kwenye msitari uliyokujengea umaarufu.


      KAULI ZAKO TATA
      wewe ni dokta. una phd (hata kama ni ya mambo ya kidini lkn ni phd). upeo wako wa kuchambua mambo lazima uwe wa hadhi ya phd. kauli hizi zinanitia wasiwasi kuhusu uwezo wako wa kiuchambuzi na kifalsafa!
      "Leo asubuhi Ofisa wa Makao Makuu ya Polisi amenipigia simu kuomba appointment ya kukutanana na polisi kwa mahojiano. nasema sina muda. sisi hatuendi polisi kwa sababu walishatudanganya mara nyingi tu. kama wanataka waje watukamate lkn sisi hatuendi polisi". la kushangaza, jana majira ya saa 4 na dkk 45 asubuhi, dr slaa na lema walikwenda wenyewe makao makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano! walihojiwa kwa saa 2 kisha wakaruhusiwa kuondoka. alipohojiwa na waandishi wa habari nje ya makao makuu ya polisi, slaa alisema "tumehojiwa lkn hatukukubali maelezo yaandikwe. hakuna sehemu ambayo tumetia sahihi maelelezo ya mahojiano".

      namuuliza dr yafuatayo;
      1- ulisema piga, ua, garagaza hutokwenda polisi labda waje kukukamata. la kushangaza ulikwenda mwenyewe!
      2- mahojiano siyo lazima yaandkwe. mahojiano ya kuandikwa kwa teknolojia ya leo hayana mashiko sana. mahojiano mazuri ni yale ya sauti inayosikika. una uhakika hujarekodiwa!?

      Hivi majigambo, ubeberu na ukaidi kwa jeshi la polisi uliouonesha jumatatu ulipoongea na waandishi wa habari vimeishia wapi? hukupima na kuelewa kuwa jeshi la polisi lina nguvu sana!? hukuelewa kuwa wafuasi wako watakushangaa wakiona unakwenda polisi mwenyewe? dr wangu pima kauli zako. nina mifano mingi ya kauli zako tata lkn nazihifadhi hadi siku nyingine.


      Kadhia ya rose kamili na josephine mshumbusi (sp)
      suala hili limekukalia vibaya dr. kwanza ulimpendelea rose ubunge ili akae kimya lkn inaelekea hajaridhika na ofa ya ubunge! ulitaka ufunge ndoa mwezi huu na josephine. umewekewa pingamizi. nakushauri ujitahidi kumalizana na mam rose nje ya mahakama. la sivyo suala hili litakugharimu sana na hadhi yako itaendelea kushuka sana. ss hivi jua kwamba ww siyo slaa aliegombea urais 2010. kosa ulofanya kuzaa ukiwa padri. kosa ulofanya kumtorosha na kujimilikisha mke wa mtu mama josephine, hayatokuacha salama! umeteleza kijamii na kisiasa lkn jitahidi kumalizana na mama rose. mpe hizo 50 m ili mambo yaishe. tunamtaka slaa mwenye uono wa kimantiki kama ule wa 2005-2010 bungeni.


      USHAURI WA BURE KWA CHADEMA
      chadema ya akina slaa na zitto bungeni ya 2005 - 2010 ilikua chdm yenye mikakakati maridhawa. walikua wachache lkn walitegemea kitu kimoja. KUJENGA HOJA. hiyo ndiyo silaha ilioipa chdm umaarufu. chdm ya 2010 hadi sasa bungeni imekua chdm ya "fungeni milango tupigane" "mwongozo wa spika", "mh spika taarifa", "pigeni wanaonunua viwanja kawe hata kuwaua sawa. nitajibu kama mbunge wenu", "nchemba ulishiriki ktk EPA", "majaji ni wazee na hawana elimu. wanabebwatu" "Rais ni dhaifu" nk........... chdm yenye constructive points and ideologies iko wapi? ccm wamekupandisheni hasira ili kukuyumbisheni kwenye mijadala ya bunge na nyinyi mkaingia mkenge! bado fursa ya kubadilika ipo

      Dr slaa wewe ni jembe. nimeandika haya ili kukushauri kama shabiki wako wa 2005- 2010. sasa hivi nimesimamisha ushabiki kwako hadi nione umebadilika! ni hayo tu!


      Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo!)

    2. Miaka 50

    3. #41
      Neiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2012
      Location : My Profile
      Posts : 606
      Rep Power : 6930
      Likes Received
      453
      Likes Given
      545

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Quote By sweetlady
      Nyie tuacheni na yetu huo ukweli kausemeni kwenye hilo lichama lenu la mabwepande........ya chadema hayawahusu....huko kwenu kuna mengi ya kuwashauri hao wabunge wenu vilaza!.....mnakazana kujenga kwa jirani wakati kwenu kunateketea!....... shame on you chama cha magamba!

      Mkuu sweetlady punguza munkari, hapa inachotakiwa toa hoja, hayo yaliyotolewa ni kweli ama sio kweli? kama sio kweli nini kifanyike watu waache kumfuata fuata Dr. Slaa kwa topic hio hio moja kila siku hasa inapoonekana hakuna shida yoyote? Kufuatiliana kupo katika siasa haza hizi pinzani...
      wakuziba likes this.
      "The past and the future are Irrelevant... When the moment is everything"

    4. #42
      sweetlady's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 24th December 2010
      Location : Tanzania
      Posts : 15,307
      Rep Power : 36527
      Likes Received
      7468
      Likes Given
      4604

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Quote By Neiwa
      Mkuu sweetlady punguza munkari, hapa inachotakiwa toa hoja, hayo yaliyotolewa ni kweli ama sio kweli? kama sio kweli nini kifanyike watu waache kumfuata fuata Dr. Slaa kwa topic hio hio moja kila siku hasa inapoonekana hakuna shida yoyote? Kufuatiliana kupo katika siasa haza hizi pinzani...
      Hawawezi kuacha manake ndio ajira yao ....waache wakale polisi?????......hawa wametumwa so wala hakuna haja ya kujibizana na vilaza!
      Life without problems never make a strong and good person!

    5. #43
      nyabibuye's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th October 2011
      Posts : 43
      Rep Power : 390
      Likes Received
      8
      Likes Given
      0

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Kwa mtoa hoja,

      kwanza sisi wanachama wa CDM tunaheshimu haki ya faragha ya mtu kwa mjibu wa katiba hihi na ubovu wake, kwa maana hii hakuna mwananchama anayeweza kuingilia maisha ya watu binafsi, kama taifa tunahitaji kumtumia Dr kuleta mabadiliko na kurudisha heshima mnayoshusha kwa urafi wa mali na kuigeuza Tz mradi wenu.

      Pili, unawezaje kufunga ndoa na Padri kama unaakili timamu? rejea tarehe ya kufunga ndoa anayo dai huyo Rose na lini Dr aliacha upadri

      Tatu, propaganda kama hizi, mnakosea sehemu ya kuziweka kama ni huku jf hakuna mwanachama anayeweza kuelewa hizi hoja zenu, kwa nini jibu ni lilelile kuwa ni hoja DHAIFU, kama Taifa tunahitaji kujadili umasikini wa Taifa letu na namna tutakavyojiondoa huko, tutatumiaje rasilimali kwa maufaa ya umma na siyo kikundi cha mafisadi kama sasa, tunataka kujua mabilioni yanayofichwa nchi za nje ni ya akina nani na kwanini tusiyapate yakasaidia hata kuboresha huduma za afya.

      Tunahitaji kuona mtanzania wa hali ya chini akijikwamua na hataweza kujikwamua kwa sababu mnapoteza mda hapa jf uandika udhaifu huu bali kwa kuwa mnaweza kuachana na udhaifu wenu na kujenga taifa, amini nakwambia ila sikulazimishi kwamba 2015 hata kama watu wote watakuwa wagonjwa vitandani na kushindwa kwenda kupiga kura hakika hata mawe yataenda kupiga kura.
      Kwa sasa hata ukuweka gamba na jiwe hakika jiwe litashinda, inatoshakwa mlichofanya kwa taifa hili, hinyo basi hoja kama hizo za kwenu zinalengo la kutusahaulisha machungu ya taifa na kamwe kama chama hatujaomba msaada wa kuendesha chama chetu, kimefika hapa na kukubalika kwa kuwatumia hawa viongozi na watanzania kwa ummoja wetu kama tulivyokubali kuizika kansa ya magamba ndiyo tutakao amua msitakabali wetu.

      Mwisho ikumbukwe kuwa tuko makini na hoja hizi dhaifu, mkapa aliku na mke wa mramba, kila mtu anajua ya babu seya, kule mbeya kuna wabunge viti maalumu nyumba ndogo za hawa viongozi wenu, viti maalumu Geita ndo usiseme lakini watanzania hatuangali hayo ila ninyi mnajifanya mazuzu kwa hoja nyepesi, WANACHAMA WA CDM na watz wanaopenda mabadiliko liwalo na liwe hapa tulipo ni POINT OF NO RETURN, mkichoka kupiga polojo mtagundua kuwa mlimaliza kuni kwa kuchemsha mawe

    6. #44
      Alexism's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th August 2011
      Location : Iringa Municipal TZ
      Posts : 843
      Rep Power : 564
      Likes Received
      119
      Likes Given
      18

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Hivi mkuu unao uhakika kuwa wanao jibu hivyo ni pro CHADEMA? Nadhani ata wewe umepotea au haujui kwani inawezekana kabisa mtu akawa pro ccm lakini akatoa maneno ambayo yanaashilia kuwa mtu wa CDM. Just read between lines haya yote yaweza kuwa pande mbili avoid kuchukulia mambo kilaisi na kimtazamo chanya.

    7. #45
      laigwenan's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th April 2012
      Posts : 25
      Rep Power : 363
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Ama kweli Nyani haoni Kundule,kabla hujaangalia ma
      baya ya jembe letu Slaa, Jiulize kwanza umeambulia nini kwenye miaka 7 ya jk madarakani!,zaidi ya ufisadi wa kutisha na kubadilisha mawazi.

    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      Hydrobenga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2012
      Posts : 619
      Rep Power : 428
      Likes Received
      55
      Likes Given
      44

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Mkuu umenena vyema....ushauri mwengine wape wana-chadema..wapime habari kwanza kabla ya kuanza kuchangia kwa jazba...utakuta wanamwaga povu humu jamvini na hawataki kukusolewa...wanataka mawazo yao yakubaliwe na kila mtu..hii siyo siasa ni udikteta wa kimawazo

      Kina mijadala mingi imetokea humu..watu wamechangia kwa jazba na matusi ..mwisho wa siku inakuja kujulikana kuwa habari zenyewe ni za uongo....

    10. #47
      masopakyindi's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 5th July 2011
      Posts : 3,706
      Rep Power : 4188
      Likes Received
      987
      Likes Given
      407

      Default

      Quote By Ngarenaro
      Leo ninazidi kujidhihirishia Pro CHADEMA ni watu wanamna gani, yaani hawataki kuambiwa ukweli na wako radhi kukivunja kioo, kikiwaonyesha kwamba wana tongotongo machoni, yaani wenyewe hawataki kukosolewa sababu wanajiona wao wamekamilika na hata malaika kwao anasubiri sababu wao hawana mapungufu kabisa wakati Katibu wao mkuu
      Dr. W. Slaa anawaonyesha kwa vitendo kwamba binadamu hatujakamilika ndio maana yeye alivunja amri ya 6 zaidi ya mara moja kipindi ambacho waliowengi walikua wanajua ni Padri na bado waumini wengi walikua wanakwenda kwake KUUNGAMA, wakati anayewaungamisha nae anatenda Dhambi, tena zaidi hata ya waumini wake kwa kuvunja amri za Mungu ikiwemo Kuzini wakati yeye yupo kwenye kiapo cha Upadri, na hata baada ya kuachana na Upadri bado aliendelea kuzini pasipo kufunga ndoa, kwa ufupi
      Dr. Slaa alikua anaenda sambamba na mtoto wake wakike wa kumzaa kwa kufanya ngono zembe bila kinga kabla ya kufunga ndoa.

      Sasa kwa kutambua mapungufu hayo wenye mapenzi mema Slaa wanaanzisha mijadala ya kumshauri ili tumshauri kwa pamoja aweze kujirudi na kusafisha nyota yake, cha ajabu wanaojiita wapenzi wa CHADEMA wanapuuza ushauri bila hata kumpa nafasi Dr. Slaa mwenyewe ya ama kukubali ama kukataa ushauri wetu, yaani wanchokifanya wao ni kuendelea kumwambia Dr. Slaa wewe huna tongotongo wala nini endelea kutuongoza kitu ambacho ni kosa kubwa na wanampotosha kwa kiwango kikubwa mwenzao na ndio maana anazidi kufanya makosa yale yale sababu washabiki wake hawataki kumwambia ukweli, bahati mbaya sana yeye Dr. Slaa bado yupo gizani hajajua kua wanaosema wanamkubali Dr. Slaa wa leo sio waliomkubali Dr Slaa wa 2010.

      shame on you Pro CHADEMA
      Asante sana mkuu kwa nasaha iliyotulia.

      Wewe ukikaa mdhabahuni utaaminika kweli

    11. #48
      Anselm's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2010
      Location : Dar-es-salaam
      Posts : 1,460
      Rep Power : 723
      Likes Received
      181
      Likes Given
      138

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Ningeweza kuona dalili nzuri kwa CDM katika uchaguzi unaokuja kama wangekuwa wanapokea ushauri wanaopewa hasa ule wa kukosolewa na kuufanyia kazi,lkn hii dhana ya kutaka kulazimisha kuwa Chama hiki na Viongozi wake ni Malaika hakina/hawana mapungufu hata kidogo ni ya ajabu sana na kwa hakika haiwezi kuifikisha Chama mahali popote
      wakuziba likes this.

    12. #49
      haf2006's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th June 2012
      Posts : 21
      Rep Power : 351
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Quote By wakuziba
      nimeamini jina langu la wakuziba lina uzito wake. kwanza nikishaziba, kuzibua hoja zangu ni shughuli nzito sana. pili lakabu yangu ya "mzee wa maneno yanayochoma nyoyo" ni mujarab na maridhawa kabisa! wengi wanaosoma makala zangu, huumizwa sana na ukweli wa maneno yangu. huwa uwezo wao hauwaruhusu kuzijibu kwa hoja. huishia ama kutukana au kukosa la kuandika! ASANTE MUNGU KWA KUNIPA UWEZO WA KIUCHAMBUZI NA KIMAONO!

      Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo)
      Cha kwanza uwezo wa kiuchambuzi na kimaono hauna, kwa sababu uchambuzi wako umejikita ktk personal and private life ya Mtu(ambayo kwa ufupi ni umbea/mipasho ya taarabu) kwa kuwa haina direct impact na taswira ya Slaa kama kiongozi wa kutegemewa na Jamii ya Watz walio wengi zaidi ya 75%. Refer Jacob Zuma na tuhuma kibao kama hizo unazoeleza za kuwa na mke au wanawake hazikumfanya asionekane kuwa kiongozi anayewafaa watu wa South africa.

      Hivyo hivyo na Slaa unapomshambulia kwa kutumia kigezo cha maisha yake binafsi tena ya unyumba watu wanakushangaa kwa sababu mambo haya ya kuoa mke 1,2,3 au hata 30,40,300 ni utamaduni wa kiafrika na watu hawashangai ,kubwa hapa kuhudumia ndoa na familia. vp baba mwanaasha pale mjengoni anao wangapi? Je ameshaondolewa pale mjengoni kwa sababu tu kaongeza mke mwingine? kama sio utamaduni wa mila na desturi zetu basi utakuwa ni utamaduni wa imani zetu za kidini(unaweza kuwa na kinga hizo mbili unapoamua kuoa).Lakini pia jiulize wewe wakuziba ni wapi imeandikwa kwamba usioe tena baada ya kuwa umeoa. ndo maana watu wanaoa na kufunga ndoa za kidini au kiserikali, baada ya hapo anaoa tena kwa utaratibu wa kimila wa kabila lake, au anatoa talaka kwa mke wa awali kisha anaoa tena, tatizo liko wapi, yote yanawezekana. kadhia ya Rose kamili hapo haipo.

      Kuhusu Chadema kujenga hoja nadhani hapo hukuwa makini, kwa sababu hoja bado wanajitahidi kujenga sana tena sana ukilinganisha na Mabwepande na ndo maana na wewe unakili kwamba mabwepande kwa kutambua hivyo wanajaribu kuwatoa nje ya mada kwa kutoa maneno yatakayowapandisha hasira na kuwatoa nje ya hoja zao za msingi wanazozisimamia na hilo kila mwananchi amelishuhudia na kuligundua kwa hiyo halijashusha mvuto bali limeongeza mvuto kwa Chadema.

      Fanya utafiti mdogo tu, tembelea eneo lolote palipo na TV kama baa, basi stand nk. ambapo watu wanafuatilia mjadala wa bunge utagundua jinsi watu wanavyochukizwa na uzuzu wa CCM ndani ya bunge kwa kukwepa hoja na kuzua malumbano yasiyo na mantiki bungeni na kuomba ngumi zipigwe kwa sababu ya kushindwa hoja(refer Komba ktk kikao hiki cha nane, sisi ni wengi tukifunga mlango zikapigwa humu mtakufa).kwa hiyo hasira ya chadema bungeni ndiyo hasira ya wananchi wengi wanaokuwa wanatazama bunge, hapo hawajapoteza chochote, ila waachane na janja ya CCM, wajikite kwenye hoja ili wawakamatilie sawasawa. Kuhusu Slaa kwenda Polisi ni jambo la kawaida kwani alipelekewa hati ya kwenda polisi, alichofanya ni kuitika wito na kukataa neno kwa maana ya kutoa maelezo ya kina na ama vielelezo kuhusu kutishiwa kwake, hata kama alirekodiwa jambo la maana ni kama aliyoyaeleza akiwa polisi yana msaada kwao au yanaonyesha msimamo wake wa awali(hapo tumia commonsense yako).

      kimsngi hakuna utata ktk kauli za chadema/slaa, bado ni makini na clarification ziko clear tu na uchambuzi ni wa hali ya juu kabisa na ndo maana CCM hawajiamini mda wote. Na mwisho nikupongeze wewe kama gamba kuikubali Chadema kwamba ni makini na kuwaomba wawe makini zaidi, Shawishi magamba wengine waiunge mkono Chadema kama unavyofanya.

      Pia endelea kutafuta kwa juhudi kubwa sana tena sana Uwezo wa kiuchambuzi na kimaono kwani sasa hivi ni umbea wa saluni tu.

    13. #50
      SURNAME's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th February 2011
      Posts : 80
      Rep Power : 435
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Quote By dedam
      aliyefumaniwa na mke wa kada mwenzie kule igunga anatoka chama gani? alifumuniwa na mke wa askari kule singida anatoka chama gani? anayeongoza kuwa na vimada wengi na watoto wa nje ya ndoa anatoka chama gani?
      Kwa hiyo kama wao walifumaniwa ni sawa na yeye kuiga tabia zao kwa sababu wao walifumaniwa?Cha msingi ni kuangalia wapi tumeanguka au nini tufanye tujisafishe,ugumu wetu CDM ni kama siasa za mpira wa TZ hatutaki kusikia kukosolewa,anayetukosoa ni ADUI yetu mkubwa,CCM wamefika hapa walipo kwa sababu za kutotaka kukosolewa
      wakuziba likes this.

    14. #51
      panadol's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 11th February 2012
      Posts : 352
      Rep Power : 0
      Likes Received
      42
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By wakuziba
      nimeamini jina langu la wakuziba lina uzito wake. kwanza nikishaziba, kuzibua hoja zangu ni shughuli nzito sana. pili lakabu yangu ya "mzee wa maneno yanayochoma nyoyo" ni mujarab na maridhawa kabisa! wengi wanaosoma makala zangu, huumizwa sana na ukweli wa maneno yangu. huwa uwezo wao hauwaruhusu kuzijibu kwa hoja. huishia ama kutukana au kukosa la kuandika! ASANTE MUNGU KWA KUNIPA UWEZO WA KIUCHAMBUZI NA KIMAONO!

      Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo)
      Mkuu hongera sana kwa kuleta hoja nzuri, nzito na yenye mashiko! Ni hoja nzito kilaza yeyote hawezi kuijibu zaidi ya kukukejeli, kukusengenya,kukutukana na kukusemea maneno mengi ya hovyo ch wala usijali mkuu wewe endelea kuelimisha umma juu ya ukweli wa siasa iendeshwayo na CHADEMA ya leo yakina Wenje, Sugu, Lema, Msigwa, Lissu na wengineo mungu atakulipa kwa ukweli wako utatukanwa sana na mashabiki wa CHADEMA na wakati mwingine utasikia wakiwaambia Mods waifute hoja yako na upigwe Ban ukiona hivyo shangilia ujue ujumbe wako umewafikia na umewavuruga hawana huwezo wa kuipangua hoja yako nzito iliyojitosheleza!

    15. #52
      Kaitampunu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2011
      Location : Kwenye Corner
      Posts : 653
      Rep Power : 508
      Likes Received
      137
      Likes Given
      195

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Quote By Bornvilla
      Wakuziba we ni jembe laukweli!tatizo la JF ukisema kweli unakua adui. Kuna watu humu wamekunywa itikadi ya CDM utakalosema bora ya mbuzi anaweza kusikia kuliko hawa wapenzi wa CDM.
      Mleta thread hana tofauti na wabunge wa magamba ambao kwenye mijadala ya bajeti huanza kwa kuunga mkono 100% then kinachofuata hapo ni malalamiko ya hiki na kile. Bandiko hili halina mashiko.

    16. #53
      panadol's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 11th February 2012
      Posts : 352
      Rep Power : 0
      Likes Received
      42
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By SURNAME
      Kwa hiyo kama wao walifumaniwa ni sawa na yeye kuiga tabia zao kwa sababu wao walifumaniwa?Cha msingi ni kuangalia wapi tumeanguka au nini tufanye tujisafishe,ugumu wetu CDM ni kama siasa za mpira wa TZ hatutaki kusikia kukosolewa,anayetukosoa ni ADUI yetu mkubwa,CCM wamefika hapa walipo kwa sababu za kutotaka kukosolewa
      Baelezee, si unajua wengine ni wagumu wa kelewa wala usikate tamaa kwa maneno yao ya kejeli,matusi,masengenyo,mipas ho na wakati mwingine waweza dhalilishwa kwa maneno machafu kabisa wewe sema tu mungu atakulipa kwa mazuri yako!
      wakuziba likes this.

    17. #54
      MKANKULE's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th December 2011
      Posts : 140
      Rep Power : 704
      Likes Received
      20
      Likes Given
      19

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      huu sio uwanja wa siasa kama nyoye ni vidume jitokezeni kwenye ground ya politics tuone kama na nyie hatutaona madhaifu yenu, kuliko hata ya dr. wengine tutakuta mna wanawake kibao au waume kibao.si afadhali hata Dr.AMEJULIKANA NA WAWILI TU.wewe una wangapi au umewahi kutembea na wangapi.

      Mnajifanya watakatifu wakati ndio wachafu kuliko hata Dr.AMEKUWA MKWELI NA kweli huwa inaponya.
      Acheni porojo nyie

    18. #55
      Kigano's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 276
      Rep Power : 414
      Likes Received
      130
      Likes Given
      189

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Mh ! Yetu macho na masikio. Hivi ukweli ni nini ? Ukweli wa mwaka 1987 unaposhuhudiwa leo, tunatakiwa kujiuliza maswali kama great thinkers. Amri ya sita kavunja mwaka 1987 na siku zingine ( hatuzijui). Ufisadi wa fedha za ujio wa Papa Mwaka 1990 ( kama ndivyo inavyoongelewa ), pamoja na wanaosadikiwa kuibiwa kukataa kuwa hawajawahi kuibiwa na huyo mtuhumiwa (sijui kama nawaza sawa). Aliyeibiwa anakataa, sasa inakuwaje ni ukweli ? sasa anayemtuhumu kwa wizi ni nani ? anayeibiwa mke halalamiki mpaka wakati wa uchaguzi ! na mpaka asaidiwe na kundi la itikadi fulani ! ebu tujiulizeni maswali: ni kweli huyu mtu ni mchafu, au anachafuliwa kwa manufaa ya watu fulani ? Mimi nafikiri tuache tuhuma zibaki kuwa tuhuma, mahakama ifanye kazi yake, kwa hili la kuzaa na mwanamke wanaojua ukweli ni wao wenyewe wawili. sisi wengine ni mashabiki tu. Hili la kuiba mke nadhani kila mmoja kati yao atapata nafasi ya kueleza mahakama, na hivyo mahakama itapima na kuona ukweli. Wapo watu waliochafuliwa wakachafuka, wapo watu wachafu ambao mpaka leo hawajulikani na hivyo wanendelea kuheshimika

      Quote By Ngarenaro
      Leo ninazidi kujidhihirishia Pro CHADEMA ni watu wanamna gani, yaani hawataki kuambiwa ukweli na wako radhi kukivunja kioo, kikiwaonyesha kwamba wana tongotongo machoni, yaani wenyewe hawataki kukosolewa sababu wanajiona wao wamekamilika na hata malaika kwao anasubiri sababu wao hawana mapungufu kabisa wakati Katibu wao mkuu
      Dr. W. Slaa anawaonyesha kwa vitendo kwamba binadamu hatujakamilika ndio maana yeye alivunja amri ya 6 zaidi ya mara moja kipindi ambacho waliowengi walikua wanajua ni Padri na bado waumini wengi walikua wanakwenda kwake KUUNGAMA, wakati anayewaungamisha nae anatenda Dhambi, tena zaidi hata ya waumini wake kwa kuvunja amri za Mungu ikiwemo Kuzini wakati yeye yupo kwenye kiapo cha Upadri, na hata baada ya kuachana na Upadri bado aliendelea kuzini pasipo kufunga ndoa, kwa ufupi
      Dr. Slaa alikua anaenda sambamba na mtoto wake wakike wa kumzaa kwa kufanya ngono zembe bila kinga kabla ya kufunga ndoa.

      Sasa kwa kutambua mapungufu hayo wenye mapenzi mema Slaa wanaanzisha mijadala ya kumshauri ili tumshauri kwa pamoja aweze kujirudi na kusafisha nyota yake, cha ajabu wanaojiita wapenzi wa CHADEMA wanapuuza ushauri bila hata kumpa nafasi Dr. Slaa mwenyewe ya ama kukubali ama kukataa ushauri wetu, yaani wanchokifanya wao ni kuendelea kumwambia Dr. Slaa wewe huna tongotongo wala nini endelea kutuongoza kitu ambacho ni kosa kubwa na wanampotosha kwa kiwango kikubwa mwenzao na ndio maana anazidi kufanya makosa yale yale sababu washabiki wake hawataki kumwambia ukweli, bahati mbaya sana yeye Dr. Slaa bado yupo gizani hajajua kua wanaosema wanamkubali Dr. Slaa wa leo sio waliomkubali Dr Slaa wa 2010.

      shame on you Pro CHADEMA

    19. #56
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,142
      Rep Power : 3542
      Likes Received
      3034
      Likes Given
      460

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      wakuziba,

      Kwanini Unataka kuingilia PENZI LA MWANASIASA kulifanya ni SIASA? HAYO NI YAKE YA NYUMBANI hakuletei nyumbani

      Kwako, na haimzuii kufanya kazi zake za kisiasa; Penzi lake ni roho yake kupenda... Leo hii wewe pia unaweza

      Kumpenda Dada yule/kaka yule na kesho Dada yule/kaka yule (sijui wewe ni mwanamke au mwanamme)

      kwahiyo tujaribu sana kutokuwaingilia wana siasa wetu mpaka nguoni; Mbona sijaona wa CCM; kuandika haya

      kwa ADAM MALIMA aliposhikwa na MABUNDUKI HOTELINI? Wananchi wake walikaa kimya, Madhahabu na Shaba yaliibiwa

      Hakuna hata mmoja aliyejibwatiza...

      Wanasiasa wetu pia wana Maisha binafsi baada ya Siasa; na Wangependa kuyafanya na kuyatatua bila sisi kuingilia

      Nadhani hatujui kila kitu wewe unachokifanya!!!

      CHAMA CHA CHADEMA bado kina mikakati ILE ILE;

      In life, when we are no longer able to change a situation, we are challenged to change ourselves...

    20. #57
      Tukundane's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2012
      Posts : 867
      Rep Power : 803
      Likes Received
      130
      Likes Given
      0

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Hakuna alie kamilika bali tunaishi kwa kukosoana na kuvumiliana hata mungu huwa anakosolewa lakini bado ni mungu tu.

    21. #58
      panadol's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 11th February 2012
      Posts : 352
      Rep Power : 0
      Likes Received
      42
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By MKANKULE
      huu sio uwanja wa siasa kama nyoye ni vidume jitokezeni kwenye ground ya politics tuone kama na nyie hatutaona madhaifu yenu, kuliko hata ya dr. wengine tutakuta mna wanawake kibao au waume kibao.si afadhali hata Dr.AMEJULIKANA NA WAWILI TU.wewe una wangapi au umewahi kutembea na wangapi.

      Mnajifanya watakatifu wakati ndio wachafu kuliko hata Dr.AMEKUWA MKWELI NA kweli huwa inaponya.
      Acheni porojo nyie
      tatizo lipo kwako wewe na kibaraka wa Chadema kwa unatetea upuuzi, Je Baba yako mzazi angeibiwa mama yako mzazi ungeunga mkono?sema ungechukua hatua gani?ushauri , usipende kutetea upuuzi siku moja upuuzi kama huo utakutafuna na wewe pia!

    22. #59
      Kigano's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 276
      Rep Power : 414
      Likes Received
      130
      Likes Given
      189

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      walifumaniwa mwaka 2011/2012, Tuhuma za Slaa ni zamwaka 1987, Sijui kama tunaenda sawa ? Ushauri wako bado ni mzuri

      Kwa hiyo kama wao walifumaniwa ni sawa na yeye kuiga tabia zao kwa sababu wao walifumaniwa?Cha msingi ni kuangalia wapi tumeanguka au nini tufanye tujisafishe,ugumu wetu CDM ni kama siasa za mpira wa TZ hatutaki kusikia kukosolewa,anayetukosoa ni ADUI yetu mkubwa,CCM wamefika hapa walipo kwa sababu za kutotaka kukosolewa[/QUOTE]

    23. #60
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default re: Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

      Quote By Josephine
      CCM bwana,mnajitahidi sana,lakini too late.

      Propaganda hazina nafasi kwa watanzania,watanzania wanataka Tanzania aliyoiota mwl nyerere,ambayo ilitoa Elimu bure,huduma bure za Afya na huduma bora za kijamii bila kuchimba madini ,kusafirisha magogo na kutuibia wanyama wetu.

      Chadema siyo Dr Slaa chadema ni Taasisi,kama taasisi inawashahuri katika nyanja zote,wewe ni nana?

      Ndiyo maana wabunge wa CCM wanashindwa kujadili hoja za maendeleo wanabaki kuhariri hotuba za akina Lissu na Myika unaweza kuona ni kwa namna gani mmepoteza focus na direction.
      Wakuzibwa si mchambuzi ila ni twister na mleta majungu .Slaa alisema hawaendi polisi kutoa taarifa .Na imekuwa hivyo.Nchimbi kakurupuka wamapigia simu akasema no .Wakampelekea barua yeye na Lema , ushauri ukatoka kwenye Chama na wana sheria kwamba nendeni kuitikia wito ila kama ni kuandika lolote jibu ni hapana .Lema na Slaa walienda polisi baada ya kuwa na barua mkononi .Wakafika wakaambiwa sababu za wito wakaombwa kuandika ili wapewe ulinzi pending uchunguzi.Slaa akasema kabla ya kutoa maelezo anataka majibu ya previous chunguzi akiwa Mbunge .Wakawa hawana la kusema wakamwambia nenda na Lema .Sasa ulitaka nini ? Kiburi cha nini ? Chadema ni waungwana na Viongozi wao ni waungwana .Wameondoa sababu za ma CCM kusema mengi na kuwatishia now what are you trying to twist here ? Shame on you .Wewe unachambuliwa wala huchambui lolote
      Nasema : CCM tunadhani adui yetu ni Chadema hapana ni Watendaji wetu katika Serikali ya CCM tukawabane hao - Livingstone Kibajaji Lusinde 2013 25 April at 11:54am.

    24. Study Abroad
    Page 3 of 5 FirstFirst 12345 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...