Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 37
    1. #1
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,449
      Rep Power : 716
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Wakati watanzania tuko kwenye mchakato wa katiba mpya naamini ni wakati muafaka na wabunge kupitia upya kanuni na taratibu za kuendesha bunge kwani zina mapungufu makubwa na ni janga la kitaifa kwa kuzingatia umuhimu wa bunge.Nitatoa mifano michche ambayo mimi kwangu hainiridhishi:-

      1. Spika,naibu spika na wenyeviti wawe watu huru
      Hii ni kutokana na viongozi hawa kusimamia na kuendesha bunge kwa kuzingatia itikadi za vyama vyao badala ya kufuata kanuni na matokea yake ni mambo kama upendeleo na uonevu ktk maamuzi.

      2. Kanuni juu ya mwongozo na taarifa
      Hii kanuni kwakweli ina upungufu sana kwani inampa spika mamlaka ya kutoa muongozo wakati wowote anaoona unafaa.Nadhani hapa spika anatakiwa awekewe kipengele cha kumbana kwamba ni lazima atoe muongozo ndani ya kipindi fulani na anaposhindwa kufanya hivyo awasilishe sababu bungeni.Vile vile iwe ni lazima kwa spika kupokea muongozo na taarifa kutoka kwa wabunge kwani hivi sasa anaweza kukataa kuruhusu muongozo au taarifa kutolewa.

      3. Taarifa za kamati kutegemea ruhusa ya spika
      Sina uhakika sana na kanuni hii ila kama kweli taarifa ya kamati ya bunge juu ya uchunguzi wa jambo fulani ni lazima kwanza ipate ruhusa ya spika ndio taarifa hiyo iruhusiwe kusomwa bungeni hili nalo ni tatizo kubwa. Nashauri taarifa yeyote ya kamati ya bunge ni shariti isomwe bungeni na spika apewe taarifa tu juu ya uwasilishaji lakini asiwe muamuzi.

      4. Maamuzi yanayohusu mambo mazito kama upitishaji bajeti yawe kwa kura ya siri na sio kwa mtindo wa kuhoji wabunge kwa pamoja.

      5. Wabunge walipwe posho baada ya kusaini mara mbili asubuhi na jioni ili kudhibiti utoro na anaesaini mara moja kwa siku alipwe nusu posho.

      6. Kanuni zipige marufuku mambo kama pongezi za kifamilia na hata mawaziri wasilazimike kuwataja(kuwatambua)wale wote waliochangia ili kuokoa muda na labda anaweza kuwashukuru kwa ujumla tu.

      7. Na kanuni zingine zote ambazo ni kikwazo cha maendeleo kwa taifa letu.

      8. Hoja kwamba jambo lilkishajadiliwa na kufanyiwa maamuzi basi jambo hilo ndio limefungwa rasmi kwa maana ya kwamba halitarudishwa bungeni tena. Kanuni hii ni ya ovyo na inalenga kulea uozo serikalini. Athari ya kanuni hii ni kuhusu mambo kadhaa kwa mfano kashifa ya richmond ambayo kwa sasa imeshafungwa rasmi kujadiliwa bungeni na hata swala la uuzaji wa nyumba za serikali.

      Hapa cha msingi ni kuzingatia nyakati na kama kuna taarifa au ushahidi mpya unaoweza kusaidia jambo fulani kwa wakati wowote jambo husika lilrudishwe bungeni. Pia inawezekana maamuzi ya nyuma yalifanywa kimakosa kutokana na taarifa zilizokuwepo kwa wakati huo na kuna umuhimu wa kuzingatia taarifa mpya au hata mazingira ya wakati wa sasa.
      Last edited by Salary Slip; 16th July 2012 at 10:40.

    2. DNA is offline
      DNA
      #2
      DNA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th June 2012
      Posts : 10
      Rep Power : 354
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      safi i read between the lines nakubaliana na wewe 100%

    3. #3
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,449
      Rep Power : 716
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By DNA View Post
      safi i read between the lines nakubaliana na wewe 100%
      Nashukuru mkuu.

    4. #4
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,825
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1230
      Likes Given
      1193

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Nafikiri kabla kulijadili hili , Mtoa mada ulitakiwa ujue ni nani mwenye mamlaka ya kutunga Kaanun za Bunge. Kumbuka kuwa kaanua hizo za Bunge hazimi kwenye marekebisho au katika katiba mpya mnayokusudia kuiandika hivi karibuni.

      Mwanye mamlaka ya kutunga kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe ndani ya bunge . Hivyo ni vizuri wabunge hao kwa utashi au kukwazwa kwao na kaanun hizo watachukua nafasi kuomba mwongozo wa kuzitengua na hata kuzifuta na kuweka kaanun muafaka kutokana na wakati husika.

      Kifupi mwenye mamlaka ya kubadilisha kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    5. #5
      makusanya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Posts : 348
      Rep Power : 476
      Likes Received
      44
      Likes Given
      155

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Salary slip View Post
      Wakati watanzania tuko kwenye mchakato wa katiba mpya naamini ni wakati muafaka na wabunge kupitia upya kanuni na taratibu za kuendesha bunge kwani zina mapungufu makubwa na ni janga la kitaifa kwa kuzingatia umuhimu wa bunge.Nitatoa mifano michche ambayo mimi kwangu hainiridhishi:-
      1.Spika,naibu spika na wenyeviti wawe watu huru
      Hii ni kutokana na viongozi hawa kusimamia na kuendesha bunge kwa kuzingatia itikadi za vyama vyao badala ya kufuata kanuni na matokea yake ni mambo kama upendeleo na uonevu ktk maamuzi.
      2.Kanuni juu ya mwongozo na taarifa
      Hii kanuni kwakweli ina upungufu sana kwani inampa spika mamlaka ya kutoa muongozo wakati wowote anaoona unafaa.Nadhani hapa spika anatakiwa awekewe kipengele cha kumbana kwamba ni lazima atoe muongozo ndani ya kipindi fulani na anaposhindwa kufanya hivyo awasilishe sababu bungeni.Vile vile iwe ni lazima kwa spika kupokea muongozo na taarifa kutoka kwa wabunge kwani hivi sasa anaweza kukataa kuruhusu muongozo au taarifa kutolewa.
      3.Taarifa za kamati kutegemea ruhusa ya spika
      Sina uhakika sana na kanuni hii ila kama kweli taarifa ya kamati ya bunge juu ya uchunguzi wa jambo fulani ni lazima kwanza ipate ruhusa ya spika ndio taarifa hiyo iruhusiwe kusomwa bungeni hili nalo ni tatizo kubwa.Nashauri taarifa yeyote ya kamati ya bunge ni shariti isomwe bungeni na spika apewe taarifa tu juu ya uwasilishaji lakini asiwe muamuzi.
      4.Maamuzi yanayohusu mambo mazito kama upitishaji bajeti yawe kwa kura ya
      siri na sio kwa mtindo wa kuhoji wabunge kwa pamoja.
      5.Wabunge walipwe posho baada ya kusaini mara mbili asubuhi na jioni ili kudhibiti utoro na anaesaini mara moja kwa siku alipwe nusu posho.
      6.Kanuni zipige marufuku mambo kama pongezi za kifamilia na hata mawaziri wasilazimike kuwataja(kuwatambua)wale wote waliochangia ili kuokoa muda na labda anaweza kuwashukuru kwa ujumla tu.
      7.Na kanuni zingine zote ambazo ni kikwazo cha maendeleo kwa taifa letu.
      8.Hoja kwamba jambo lilkishajadiliwa na kufanyiwa maamuzi basi jambo hilo ndio limefungwa rasmi kwa maana ya kwamba halitarudishwa bungeni tena.Kanuni hii ni ya ovyo na inalenga kulea uozo serikalini.Athari ya kanuni hii ni kuhusu mambo kadhaa kwa mfano kashifa ya richmond ambayo kwa sasa imeshafungwa rasmi kujadiliwa bungeni na hata swala la uuzaji wa nyumba za serikali.Hapa cha msingi ni kuzingatia nyakati na kama kuna taarifa au ushahidi mpya unaoweza kusaidia jambo fulani kwa wakati wowote jambo husika lilrudishwe bungeni.Pia inawezekana maamuzi ya nyuma yalifanywa kimakosa kutokana na taarifa zilizokuwepo kwa wakati huo na kuna umuhimu wa kuzingatia taarifa mya au hata mazingira ya wakati wa sasa.

      Hapo kwenye red naomba ingeongezwa sentesi hii 'tena saini za waheshimiwa ziwe zinachukuliwa mwishoni na si mwanzo wa sessions ili kuepuka zoezi la kusaini na kuondoka
      OSOKONI and Salary Slip like this.

    6. #6
      MNAMBOWA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2011
      Posts : 839
      Rep Power : 555
      Likes Received
      85
      Likes Given
      39

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      mnasumbuliwa udhaifu wa kujenga hoja na ukosefu wa nidhamu2, hakuna ziada

    7. #7
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,449
      Rep Power : 716
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Barubaru View Post
      Nafikiri kabla kulijadili hili , Mtoa mada ulitakiwa ujue ni nani mwenye mamlaka ya kutunga Kaanun za Bunge. Kumbuka kuwa kaanua hizo za Bunge hazimi kwenye marekebisho au katika katiba mpya mnayokusudia kuiandika hivi karibuni. Mwanye mamlaka ya kutunga kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe ndani ya bunge . Hivyo ni vizuri wabunge hao kwa utashi au kukwazwa kwao na kaanun hizo watachukua nafasi kuomba mwongozo wa kuzitengua na hata kuzifuta na kuweka kaanun muafaka kutokana na wakati husika. Kifupi mwenye mamlaka ya kubadilisha kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe.
      Mkuu soma vizuri maelezo yaliyotolewa.Nilichosema ni wabunge wenyewe wabadilishe kanuni za uendeshaji bunge.Swala la katiba limegusiwa tu ili liende sambamba na wabunge kupitia upya kanuni za bunge.

    8. #8
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,931
      Rep Power : 16839
      Likes Received
      2648
      Likes Given
      2033

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By MNAMBOWA View Post
      mnasumbuliwa udhaifu wa kujenga hoja na ukosefu wa nidhamu2, hakuna ziada
      Akina nani wadhaifu??

    9. #9
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,449
      Rep Power : 716
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By MNAMBOWA View Post
      mnasumbuliwa udhaifu wa kujenga hoja na ukosefu wa nidhamu2, hakuna ziada
      Bila shaka wewe ni sehemu ya magamba wanaonufaika na kanuni hizi.
      Hivi hizi kanuni ni msaafa au ni maandiko matakatifu ambayo huwezi kuyabadili?Nipe jibu.

    10. #10
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 4,085
      Rep Power : 1237
      Likes Received
      988
      Likes Given
      247

      Default

      Quote By DNA View Post
      safi i read between the lines nakubaliana na wewe 100%
      unakubaliana na ulipanaji wa posho sio?
      Wabunge hawalitumikii bunge, wanawatumikia wapigakura wao, hivyo basi wasilipwe na ofisi za bunge bali walipwe na waajiri wao kupitia halmashauri zao na mishahara yao ipitishwe na madiwani, iandaliwe kwa mapendekezo ya wapigakura na kujadiliwa na wataalam katika mjadala huru, wabunge waruhusiwe kufanya kazi zao za kitaalamu na kupokea mshahara huko.

      Wabunge wawajibike kwa wapiga kura wao moja kwa moja na si kwa chama wala bunge!

    11. #11
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,825
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1230
      Likes Given
      1193

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Salary slip View Post
      Mkuu soma vizuri maelezo yaliyotolewa.Nilichosema ni wabunge wenyewe wabadilishe kanuni za uendeshaji bunge.Swala la katiba limegusiwa tu ili liende sambamba na wabunge kupitia upya kanuni za bunge.
      Nafikiri nami ukuwa umenielewa.

      Nilichotaka kubainisha mabadiliko ya kaanun za Bunge iwe kwa faida za Bunge lenyewe kwa kurahisisha uendeshaji wake na sio kama wewe ulivyo generalize kusema kwa faida ya taifa. Kwani kuwepo tu kwa kaanun za muhimili huo ni faida kwa Taifa hususan kwa Utawala wa Sharia (Rules of Law).

      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    12. #12
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,912
      Rep Power : 1169
      Likes Received
      1056
      Likes Given
      804

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Barubaru View Post
      Nafikiri kabla kulijadili hili , Mtoa mada ulitakiwa ujue ni nani mwenye mamlaka ya kutunga Kaanun za Bunge. Kumbuka kuwa kaanua hizo za Bunge hazimi kwenye marekebisho au katika katiba mpya mnayokusudia kuiandika hivi karibuni.

      Mwanye mamlaka ya kutunga kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe ndani ya bunge . Hivyo ni vizuri wabunge hao kwa utashi au kukwazwa kwao na kaanun hizo watachukua nafasi kuomba mwongozo wa kuzitengua na hata kuzifuta na kuweka kaanun muafaka kutokana na wakati husika.

      Kifupi mwenye mamlaka ya kubadilisha kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe.
      89.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza
      kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa
      kutekeleza shughuli zake.
      (2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii
      zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli
      za Sekretariati ya Bunge na pia utekelezaji wa Shughuli za Bunge
      ndani ya Bunge na zile za Kamati na Kamati ndogo za Bunge

      Katiba inatambua uwepo wa kanuni ila hazijaorodheshwa moja baada ya nyingine, hivo ilivo kwa sheria nyingi hazipo kwenye katiba ila msingi na chimbuko lake ni katiba!
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    13. #13
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,912
      Rep Power : 1169
      Likes Received
      1056
      Likes Given
      804

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By DNA View Post
      safi i read between the lines nakubaliana na wewe 100%
      kanuni nyingi sana zilitungwa wakati wa bunge la chama kimoja na hazikufanyiwa marekebisho ya makubwa ili kulinda chama tawala na serikali!spika anahimiza maswali na majibu kuulizwa au kujibiwa kwa kifupi lakini wakati huohuo anachukua muda mrefu sana ktambulisha wageni sijui wanafunzi,cjui mke wa waziri, sijui wapiga kura, mawaziri nao wanataja wachangiaji mlolongo hauna maana hata kidogo!
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    14. #14
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,842
      Rep Power : 1155
      Likes Received
      194
      Likes Given
      0

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Salary slip View Post
      Wakati watanzania tuko kwenye mchakato wa katiba mpya naamini ni wakati muafaka na wabunge kupitia upya kanuni na taratibu za kuendesha bunge kwani zina mapungufu makubwa na ni janga la kitaifa kwa kuzingatia umuhimu wa bunge.Nitatoa mifano michche ambayo mimi kwangu hainiridhishi:-
      1.Spika,naibu spika na wenyeviti wawe watu huru
      Hii ni kutokana na viongozi hawa kusimamia na kuendesha bunge kwa kuzingatia itikadi za vyama vyao badala ya kufuata kanuni na matokea yake ni mambo kama upendeleo na uonevu ktk maamuzi.
      2.Kanuni juu ya mwongozo na taarifa
      Hii kanuni kwakweli ina upungufu sana kwani inampa spika mamlaka ya kutoa muongozo wakati wowote anaoona unafaa.Nadhani hapa spika anatakiwa awekewe kipengele cha kumbana kwamba ni lazima atoe muongozo ndani ya kipindi fulani na anaposhindwa kufanya hivyo awasilishe sababu bungeni.Vile vile iwe ni lazima kwa spika kupokea muongozo na taarifa kutoka kwa wabunge kwani hivi sasa anaweza kukataa kuruhusu muongozo au taarifa kutolewa.
      3.Taarifa za kamati kutegemea ruhusa ya spika
      Sina uhakika sana na kanuni hii ila kama kweli taarifa ya kamati ya bunge juu ya uchunguzi wa jambo fulani ni lazima kwanza ipate ruhusa ya spika ndio taarifa hiyo iruhusiwe kusomwa bungeni hili nalo ni tatizo kubwa.Nashauri taarifa yeyote ya kamati ya bunge ni shariti isomwe bungeni na spika apewe taarifa tu juu ya uwasilishaji lakini asiwe muamuzi.
      4.Maamuzi yanayohusu mambo mazito kama upitishaji bajeti yawe kwa kura ya
      siri na sio kwa mtindo wa kuhoji wabunge kwa pamoja.
      5.Wabunge walipwe posho baada ya kusaini mara mbili asubuhi na jioni ili kudhibiti utoro na anaesaini mara moja kwa siku alipwe nusu posho.
      6.Kanuni zipige marufuku mambo kama pongezi za kifamilia na hata mawaziri wasilazimike kuwataja(kuwatambua)wale wote waliochangia ili kuokoa muda na labda anaweza kuwashukuru kwa ujumla tu.
      7.Na kanuni zingine zote ambazo ni kikwazo cha maendeleo kwa taifa letu.
      8.Hoja kwamba jambo lilkishajadiliwa na kufanyiwa maamuzi basi jambo hilo ndio limefungwa rasmi kwa maana ya kwamba halitarudishwa bungeni tena.Kanuni hii ni ya ovyo na inalenga kulea uozo serikalini.Athari ya kanuni hii ni kuhusu mambo kadhaa kwa mfano kashifa ya richmond ambayo kwa sasa imeshafungwa rasmi kujadiliwa bungeni na hata swala la uuzaji wa nyumba za serikali.Hapa cha msingi ni kuzingatia nyakati na kama kuna taarifa au ushahidi mpya unaoweza kusaidia jambo fulani kwa wakati wowote jambo husika lilrudishwe bungeni.Pia inawezekana maamuzi ya nyuma yalifanywa kimakosa kutokana na taarifa zilizokuwepo kwa wakati huo na kuna umuhimu wa kuzingatia taarifa mpya au hata mazingira ya wakati wa sasa.

      Nimeshangazwa sana sana na kutojua kanuni za uendeshaji wa mabunge ya nchi za Commonwealth, nenda kazisome then ndipo uje na uzi wenye maana kwetu, kwa hapo umekurupuka sana tu

    15. #15
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,449
      Rep Power : 716
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Dumela Mbegu View Post

      Nimeshangazwa sana sana na kutojua kanuni za uendeshaji wa mabunge ya nchi za Commonwealth, nenda kazisome then ndipo uje na uzi wenye maana kwetu, kwa hapo umekurupuka sana tu
      Kama issue ni commonwealth basi hata ushoga turidhie ili tuende sambamba.
      Inawezekana ulinufaika na hela za richmond zinazolindwa na kanuni hizi mbovu.
      Pia acha kukariri commonwealth kwani hiyo sio sababu.
      Iga kilicho bora na sio kuburuzwa na ujue wenzetu wana nidhamu na wana uzalendo.

    16. #16
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,825
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1230
      Likes Given
      1193

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By OSOKONI View Post
      89.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza
      kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa
      kutekeleza shughuli zake.
      (2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii
      zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli
      za Sekretariati ya Bunge na pia utekelezaji wa Shughuli za Bunge
      ndani ya Bunge na zile za Kamati na Kamati ndogo za Bunge

      Katiba inatambua uwepo wa kanuni ila hazijaorodheshwa moja baada ya nyingine, hivo ilivo kwa sheria nyingi hazipo kwenye katiba ila msingi na chimbuko lake ni katiba!
      Hiyo ulioiweka ni sharia inayotambua kuwepo Kanuni za kudumu za Bunge Sheria namba 14 ya mwaka 1984. Ibara ya 14 kifungu cha 89 (1,2)

      Nazidi kukushauri hebu pitia Sharia ya Mamlaka ya Bunge Sharia namba 15 Ibara ya 2 ya mwaka 1984 na Sharia namba 20 ibara 11 ya mwaka 1992.

      Kwa kupitia hapo utabaini wazi Katiba ya Tanzania imelitambua Bunge na kaanun zake. Lakin mwenye Mamlaka ya kutunga Kaanun hizo ni WABUNGE WENYEWE na sio wananchi.

      Na haiyumkiniki kabisa kuwa mnapofanya au kuandika Katiba Mpya basi ni lazima na Kaanun hizo za Bunge ziandikwe upya. Hilo sio sahihi. Mabadiliko ya Kaanun za bunge yanafanywa na wabunge wenyewe pale wanapoona kuna ulazima wa kufanya hivyo kulingana na matakwa na wakti.

      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    17. #17
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,449
      Rep Power : 716
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Kwa yaliyotokea leo bungeni ni wazi kanuni za bunge hazifa kwani kila kiti ni maamuzi ya spika na ni wazi anaibeba serikali ka manufaa ya chama chake.
      Leo hii kambi rasmi ya upinzani imezuiwa kusoma maoni yake juu ya kipengele cha mauaji yenye sura ya kisiasa kwa kisingizio kesi hizo ziko mahakamani na mojawapo ya mambo yaliyozuiwa ni kuhusu mateso na kipigo cha Dr. Ulimboka.Hii ilikuwa baada ya Lukuvi kuomba muongoza kwamba kipengele hicho kisisomwe bungeni kwani kuna kesi iko mahakamani
      Hotuba ilikuwa ni ya wizara ya mambo ya ndani na upinzani walikuwa wanasoma mapendekezo yao juu ya hotuba ya wizara ya mambo ya ndani.
      Kanuni hizi ni mbovu kwani spika amepewe madaraka makubwa mno.

    18. #18
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,825
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1230
      Likes Given
      1193

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Salary slip View Post
      Kwa yaliyotokea leo bungeni ni wazi kanuni za bunge hazifa kwani kila kiti ni maamuzi ya spika na ni wazi anaibeba serikali ka manufaa ya chama chake.
      Leo hii kambi rasmi ya upinzani imezuiwa kusoma maoni yake juu ya kipengele cha mauaji yenye sura ya kisiasa kwa kisingizio kesi hizo ziko mahakamani na mojawapo ya mambo yaliyozuiwa ni kuhusu mateso na kipigo cha Dr. Ulimboka.Hii ilikuwa baada ya Lukuvi kuomba muongoza kwamba kipengele hicho kisisomwe bungeni kwani kuna kesi iko mahakamani
      Hotuba ilikuwa ni ya wizara ya mambo ya ndani na upinzani walikuwa wanasoma mapendekezo yao juu ya hotuba ya wizara ya mambo ya ndani.
      Kanuni hizi ni mbovu kwani spika amepewe madaraka makubwa mno.

      Nafikiri ahali yangu kama utapunguza ushabiki na kuangalia Katiba yenu hususan pale inapozungumzia separation of power katika Rules of law. Utaona nchi yenu inaongozwa na mihimili Mitatu nayo ni Mahakama, Bunge na Serikali. Na kila kimoja katika hivyo kimepewa mamlaka yake kamili bila kuingiliwa na muhimili mwingine katika utendahi wa Shughuli na kazi zake. Soma Sheria namba Na.15 ib.6 ya 1984, kifungu cha 4 chote.

      Hivyo Bunge wapo sahihi kabisa kisharia kuwa hawaruhusiwi kabisa kujadili kitu chochote au shauri lolote lile kilichopo mahakamani

      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    19. #19
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,449
      Rep Power : 716
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Barubaru View Post
      Nafikiri nami ukuwa umenielewa. Nilichotaka kubainisha mabadiliko ya kaanun za Bunge iwe kwa faida za Bunge lenyewe kwa kurahisisha uendeshaji wake na sio kama wewe ulivyo generalize kusema kwa faida ya taifa. Kwani kuwepo tu kwa kaanun za muhimili huo ni faida kwa Taifa hususan kwa Utawala wa Sharia (Rules of Law).
      Mkuu bunge ni chombo cha uwakilishi kwa umma wote wa watanzania kwani haiwezekani kila mtanzania akaenda pale bungeni na wabunge ni wawakilishi wetu kwahiyo wanayoyafanya si kwa manufaa au faida ya bunge lenyewe kama ulivyodai bali ni kwa faida ya watanzania wote kama taita kwa kupitia bunge hilo. Hivi ni kweli uelewi jambo hili au una ajenda yako binafsi!
      Last edited by Salary Slip; 17th July 2012 at 14:22.

    20. #20
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,825
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1230
      Likes Given
      1193

      Default Re: Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

      Quote By Salary slip View Post
      Mkuu bunge ni chombo cha uwakilishi kwa umma wote wa watanzania kwani haiwezekani kila mtanzania akaenda pale bungeni na wabunge ni wawakilishi wetu kwahiyo wanayoyafanya si kwa manufaa au faida ya bunge lenyewe kama ulivyodai bali ni kwa faida ya watanzania wote kama taita kwa kupitia bunge hilo. Hivi ni kweli uelewi jambo hili au una ajenda yako binafsi!

      Ahali yangu nimekubainishia wazi kama Utapunguza USHABIKI na KULALAMIKA na kutulia kitako kusoma vizuri Katiba yenu utajifunza mengi sana. Kumbuka kuwa katika dhana ya Rules of Law, utaona kila muhimili una kazi zake.

      Kazi za Bunge ni kutunga sharia
      Kazi za Mahakama ni kutafsiri Sharia zinazotungwa na Bunge.
      Kazi za Serikali ni Kusimamia sharia zinazotungwa na Bunge.

      Na hata ukisoma Katiba hiyo hiyo inasema wazi Serikali inawajibika kwa wananchi kwa sababu Serikali ni ya watu. Soma Katiba yya JMTz katika kuona Serikali na watu sharia namba 15 Ibara ya 6 ya mwaka 1984. Imebainisha hivyo.

      Lakin vile vile angalia Sharia hiyo iliyotungwa na Bunge kuhusu separation of Power.
      Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi Sheria namba Na.15 ib.6 ya 1984, kifungu cha 4

      4
      .-
      (1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri

      ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili

      vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka

      ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye

      mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa

      shughuli za umma.

      (2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni

      Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya

      Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki

      vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya

      Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya

      Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na

      kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni

      Bunge na Baraza la Wawakilishi.

      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...